Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 514 | 515 | (Page 516) | 517 | 518 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Baada ya kuridhishwa na matumizi mazuri na mafanikio makubwa ya Maktaba yao ya kwanza waliyoifungua mwaka 2009 katika kijiji cha Ngongongare Mkoani Arusha,  Taasisis isiyo ya kiserikali ya The Crawford Smith Foundation yenye makazi yake nchini Marekani na ambayo ndiyo inayosimamia mradi wa uanzishwa na uendeshaji wa Maktaba hususani katika maeneo ya vijijini, sasa inakusudia kujenga maktaba nyingine sita katika maeneo mbalimbali nchini Tanzania.
   Maktaba hiyo ya kwanza na ya aina yake na ambayo imepewa jina la Jifundishe Free Library, si tu inatoa huduma za vitabu vya kiada na ziada kwa watumiaji ambao ni kuanzia wale wa shule za awali, msingi, sekondari na hata vyuo vikuu, bali pia imekuwa kituo ambacho kinawasaidia wanawake na vijana kujifunza stadi mbalimbali zikiwamo za ujasiliamali, vyama ya kuweka na kukopa, huduma za kinga ya afya, huduma za internet na mafunzo ya ziada ambayo yamekuwa yakitolewa na wataalamu wa kujitolea kutoka nje na ndani ya Tanzania. 
   Hayo yameelezwa na Viongozi wakuu wa Taasisi hiyo ya The Crasford Smith Foundation wakati walipofika na kufanya Mazungumzo na Balozi Tuvako Manongi Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa. 
   Kwa mujibu wa maelezo ya Bw. Steven Smith aliyekuwa amefuatana na Mke wake Bibi. Judithi Smith amesema kuwa mwitikio mkubwa na matumizi sahihi na endelevu vya Jifundishe Free Library na matokeo mazuri ya wanafunzi katika mitihani yao, kumewafanya watambue ni kwa kiasi gani huduma hiyo muhimu inahitaji kusambazwa katika maeneo mengine hasa ya vijijini. Lengo likiwa ni kuwafikia na kuwapatia huduma hiyo wasio kuwa na uwezo wa kuipata kwa urahisi. 
   Mradi huo wa Maktaba licha ya kutoa huduma mbalimbali, lakini umekwenda mbali zaidi kwa kutoa ufadhili wa masomo ya Chuo Kikuu kwa wanafunzi wanne hadi sasa. baadhi ya wanafunzi hao wamerudi na kutoa mchango wao katika Maktaba hiyo na jumuiya inayoizunguka. 
   Baadhi ya maeneo ambako wanakusudia kupelea huduma hiyo muhimu ya maktaba ni Kisarawe , Chunya , Iringa, Morogoro na Kilimanjaro. 
   Aidha wakuu hao wameeleza kuridhidhwa kwao na Ushirikiano wanaoupata kutoka kwa viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, baadhi ya Makampuni ambayo yameonyesha nia ya kushirikia na Taasisi hiyo katika utoaji wa huduma hiyo, na vilevile mwamko na moyo wakujitolea wa watanzania katika maeneo wanayokusudia kuanzisha maktaba hizo. 
  Kwa upande wake, Mhe. Balozi Balozi Manongi aliishukuru Taasisi hiyo kwa mchango wake mkubwa na ambao umeonyesha mafanikio na mabadiliko makubwa kwa jamii inayohudumiwa. 
  Akasema Tanzania inatambua umuhimu wa maktaba katika mustakabali mzima wa elimu na mafunzo na kwamba mchango wa taasisi zisizo za kiserikali unakaribishwa sana.
   Kutoka kushoto ni  Bw. Steven Smith,  Bi Ann Hanin, Mhe.  Balozi   Tuvako Manongi na Bibi Judith Smith


  0 0

  Kijana aliyetambulika kwa jina la Musa Mbeko(24) anayedaiwa kuwa ni mwandishi wa habari mkoani Tabora akiwa mikononi mwa Jeshi la Polisi mkoani humo baada ya kujifanya kuwa ni afisa kutoka idara ya usalama wa taifa (TISS). Kijana huyo inadaiwa aliwahi kufanya kazi kituo cha radio cha Voice of Tabora (VOT) kinachomilikiwa na mbunge wa Jimbo la Tabora mjini, Mhe. Ismail Aden Rage. Hata hivyo Uongozi wa VOT umekana kijana huyo kuwa ni mwandishi wao na kwamba ulikwisha mfukuza kazi kutokana na makosa mbalimbali yakiwemo ya tuhuma za utapeli
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzan Kaganda akiwaonesha waandishi wa habari kitambulisho kilichokuwa kikitumiwa na Mussa Mbeko akijifanya ni Afisa Usalama wa Taifa.
   . 
  Kitambulisho alichokuwa akitumia kijana Musa Mbeko.
  Kijana Musa Mbeko akiwa mbele ya kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Suzana Kaganda.

  Kijana Musa Mbeko akiwa chini ya Ulinzi 

  0 0


  0 0
 • 07/23/14--13:22: ESAMI - SUZA Short Courses


 • 0 0

  Basically Massawe has no meaning, but represent the society of pastoralists, traditional healers, agriculturalists etc. There are different sources, some information explains that Massawe were the legal specialists to Mangi (Chief) and they were experts in environments, particularly on rainfalls.

   As opposed to other developed nations, Tanzania has more that 100 tribes, reflecting an average of the same number of Mother Languages throughout the nation. However, with the influence of Mwalimu Nyerere, Kiswahili was therefore promoted to unite people from their different tongue as formal medium of communication along with English Language. Massawe are Chagga people; and it is a name of one of the clans in Tanzania, found in the northern part of the country and on the slopes of Mountain Kilimanjaro in the Kilimanjaro region of the country.
  Massawe people are now days located in different parts of the country and even in the outside world searching for better lives, serving other people, communities and organizations. 
  It is believed that, their emigration is due to land tenure system of which small peaces of land they inherit from their parents throughout generations made it difficult for them to remain in their motherland due to land scarcity. 
  This scenario also affects other clans like Munishi, Chami, Mushi, and Makishe, located in the Kilimanjaro region. It is also believed that when it was raining, and when snows felled on the grounds they were termed as “Massaawe”, reflecting a huge sound developed while snows were felling down.On the same note, as the said community of people were very prosperous, famous and very strong in trade, warfare, intellectuals, animal keepers, and traditional healers; as such, the head of the area (the Mangi) named them Massaawe, reflecting on the powerful voice of snows when felled down!
  To date, the term has been shorten from “Massaawe” to “Massawe”, may be because of pronunciation problems or other reasons; studies does not indicate anything on its reality. In the present time, some people whom have happened to like the name, have decided to name their children Massawe, knowing or unknowingly that it was meant to be one of the Clans’ names from northern parts of Tanzania.

  For more on the Chagga Tribe of Kilimanjaro
   Region visit Alex George Massawe's blog: CLICK HERE


  0 0

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi  amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu Nchini kuendelea  kushikamana kwa lengo la kutekeleza maamrisho ya dini yao  kama inavyoagiza wakati wote. 
  Balozi Seif alitoa himizo hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada  ya futari ya Pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete kwa ajili  ya Wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba hapo katika Majengo ya  Ikulu ya Mjini Wete,  Pemba
   Balozi Seif alisema njia ya kusimamisha mshikamano kwa  waislam hupatikana katika mjumuisho wa makundi ya ibada, akiyataja kuwa ni pamoja na madrsasa, sala pamoja na  mikusanyiko ya kufutari kwa pamoja. 
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema  kitendo cha Rais Kikwete cha kukutanisha waumini na baadhi  ya wananchi katika maeneo tofauti Nchini kwa ajili ya futari ya pamoja ni moja ya njia ya kuwajengea waumini hao  ushirikiano utakaoongeza mapenzi baina yao. 
   Balozi Seif aliwatakia funga njema pamoja na kusherehekea  kwa amani na upendo siku kuu ya Idd el fitri waumini wote wa  Zanzibar.
  Akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa mikoa miwili ya  Pemba Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi  alimshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr.  Jakaya Mrisho Kikwete kwa moyo wake wa kutekeleza ibada  hiyo.
  Mh. Dadi alisema mpango huo wa Rais Kikwete ambao pia  hufanywa ba baadhi ya Viongozi wa wengine wa juu hapa  nchini, wakiwemo pia wale wa Taasisi za umma na binafsi  hutoa faraja kwa waumini ambao hali yao ya kipato ni duni  katika kujipatia futari.
  Wananchi wa Mikoa miwili ya Pemba  wakifutari pamoja hapo ikulu ya Wete futari iliyoandaliwa na  Rais wa Jamhuri ya Mauungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho  Kikwete ambaye aliwakilishwa na  Makamu wa Pili wa Rais wa  Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi. 
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa  Rais wa Zanzibar Mhe Mohamed Aboud Mohamed (katikati)  akiwa pamoja  na Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Dadi Faki Dadi kulia yake na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mzee Mberwa Hamad Mberwa wakijumuika na wananachi wa mikoa miwili ya Pemba kwenye futari iliyoandaliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi  Seif akitoa shukrani kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri ya  Muungano wa Tanzania Dr. Kikwete mara baada ya futari ya pamoja kwa wananchi wa mikoa miwili ya Pemba.
   Balozi Seif akiwaaga na baadhi ya wananchi wa mikoa miwili ya pemba waliohudhuria futari ya pamoja iliyoandaliwa na Rais Kikwete hapo Ikulu ya Wete Pemba.
  Balozi Seif akibadilishana mawazo na  mmoja wa watoto walioshiriki futari ya pamoja iliyoandaliwa  na Rais Dr. Mrisho Kikwete hapo Ikulu ya Wete,  Pemba. Habari na picha na Hassan Issa wa OMPR.

  0 0

  Sweet Escape Tz is an event planning consultancy with a focus on social events, while still maintaining a presence in the corporate event world.

  If you are looking for a fresh perspective and want to bring some sizzle to your corporate or social event, contact us to find out how we will wow your stakeholder,friends and family to generate results.

  We put love and dedication into every single one of our events and deliver the highest degree of customized service.
  There is no small event for us....
  We are here to jazz up your event in every special way.

  Your Dream our Reality !!!

  0 0

  Video imepigwa na Dixon Busagaga wa 
  Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini .

  0 0

  Mhe. Balozi Tuvako Manongi, Muwakilishi wa Kudumu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, jana Jumatano ameungana na Mabalozi wengine wanaoziwakilishi Nchi zao katika Umoja wa Mataifa, kutia saini kitabu cha maombolezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa Udachi ( Netherlandes) katika Umoja wa Mataifa kuwakumbuka watu 298 waliopoteza maisha baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria ya MH17 inayomilikiwa la Shirika la Ndege la Malaysia kuangushwa katika eneo la Mashariki ya Ukraine wiki iliyopita. Idadi kubwa ya abiria hao walikuwa ni raia wa Udachi.

   Balozi Tuvako  Manongi,akiandika katika kitabu  cha maombolezo kilichofunguliwa katika Uwakilishi wa Kudumu wa  Udachi ( Nertherlands) kuomboleza familia 298   ambazo maisha yao yamekatishwa baada ya ndege waliyokuwa wakisafiria MH17 kuangushwa nchini Ukraine wiki iliyopita.
   Balozi Manongi akiwaombea marehemu
   Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,  Balozi Tuvako Manongi, akizungumza machache na  Muwakilishi wa Kudumu wa   Udachi katika Umoja wa Mataifa,  Balozi  Karel van Oosterom mara baada ya Balozi Manongi  kusaini kitabu cha maombolezo.
   "Asante sana kwa kuja  kutufariji katika kipindi hiki kigumu, asante sana, natambua vema ushirikiano  mzuri uliopo baina ya  serikali zetu".  ndivyo aliyosikika akisema  Muwakilishi wa Kudumu wa Udachi Balozi  Karel van Oosterom

  0 0

   Jina la Tanzania linameremeta wakati wanamichezo wetu walipopita katika maandamano ya ufunguzi wa Michezo ya Jumuiya ya Madola kwenye sherehe kabambe za ufunguzi katika Uwanja wa Celtic Park jijini Glasgow, Scotland, uliobeba watazamaji 40,000 huku watu bilioni 1 wakiangalia live sherehe hizo kupitia katika TV zao. Takriban  mashabiki 100,000, na wanamichezo 4,000 kutoka katika nchi 71 zitakazoshindana wapo hapo kwa michezo hiyo ambapo hii ni mara ya 20 kufanyika toka ianzishwe.
   Sehemu ya wanamichezo wa Tanzania kwenye sherehe hizo za ufunguzi. Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada za Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand
   Tanzania Oyeeeee....!!!!
   Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha nchini Suleiman Mjaya Nyambui (T-shirt ya njano) akihamasisha vijana wake
  Nahodha na bondia wa Tanzania Seleman Salum Kidunda akipeperusha juu bendera ya Taifa wakati akiongoza wenzake kwenye maandamano hayo ya ufunguzi

  0 0

  Na Rose Masaka-MAELEZO-Dar es Salaam.

  Serikali imewataka  wananchi       kujihadhari na wizi ambao hufanywa na Taasisi za Fedha hewa ambazo zimekuwa zikidai kutoa mikopo kwa njia ya simu.

  Tahadhari hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari(MAELEZO) Assah Mwambene wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.

  Amesema kuwa Taasisi hizo zimekuwa zikitumia  mitandao ya simu za mkononi kutapeli wananchi kwa kuwaraghai kuwa watawapatia mikopo.

  Mwambene ameongeza kuwa Taasisi hizo zimekuwa zikitumia majina ya viongozi wakubwa mbalimbali wa vyama na Serikali kuwatapeli wananchi kwa kuwachukulia fedha zao.

  Amesema kuwa baadhi ya taasisi hizo zinatumia namba za uongo za Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuwaibia wananchi.

  Mkurugenzi huyo amezitaja baadhi ya Taasisi hizo kuwa ni pamoja na Social credit Loans ambayo inadai  imesajiliwa na TRA kwa namba Reg.No.33/SCC/REG/7894 na namba ya utambulisho wa mlipa kodi ni TIN:203-344-6789.

  Taasisi nyingine ni Saving Foundation na Quicken Loan ambazo zote hizo zimekuwa zinawatapeli wananchi.

  Amesema kuwa baada ya kuwasiliana Mamlaka ya Mapato Tanzania, imebainika kuwa hakuna taarifa yoyote kuhusu Taasisi hizo. 

  Mwambene amesema kuwa Serikali inaendelea kufanyia uchunguzi ili wahusika waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua.

  Aidha , Mkurugenzi huyo amewakumbusha wananchi kutokubali maombi ya fedha, fadhila au maelekezo yanayodaiwa kutolewa na uongozi wa juu bila kupata uthibitisho kutoka mamlaka husika.

  0 0

  Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa(katikati)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na uzinduzi wa huduma mpya itakayokuwa inatumiwa na wateja wanaotumia mtandao wa simu za mkononi wa vodacom kupata habari za punde (Breaking News)za kitaifa na kimataifa kupitia magazeti ya Nipashe na The Guardian, mahali popote na muda wowote. Ili kujiunga mteja anatakiawa kuandika neno Nipashe au The Guardian kwenda namba 15501. Kushoto ni Meneja Uendeshaji Premier Mobile Solution Lulu Ramole na kulia ni Meneja Masoko wa kampuni ya The Guardian Simon Marwa.
  Meneja Masoko wa kampuni ya The Guardian na Nipashe, Simon Marwa akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusiana na uzinduzi wa huduma mpya itakayokuwa inatumiwa na wateja wanaotumia mtandao wa simu za mkononi wa vodacom kupata habari za punde (Breaking News)za kitaifa na kimataifa kupitia magazeti ya Nipashe na The Guardian, mahali popote na muda wowote. Ili kujiunga mteja anatakiawa kuandika neno Nipashe au The Guardian kwenda namba 15501. Kushoto ni Meneja Uendeshaji Premier Mobile Solution Lulu Ramole na katikati ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa.

  Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania na The Guardian Limited wachapishaji wa magazeti ya The Guardian na Nipashe imezindua huduma mpya ya kufikisha habari za punde (Breaking News) kwa jamii, kuanzia leo.

  Ujio wa huduma hiyo ni utekelezaji wa azima ya makampuni yote mawili ya kutaka kuona wananchi wakiwa na njia bora na ya uhakika ya kupata taarifa mbalimbali mara tu zinapotokea.

  Huduma hii mpya itakayojulikana Kama'GUARDIAN SMS na NIPASHE SMS ni huduma iliyobuniwa kuhakikisha mamilioni ya watanzania wanaotumia mtandao mkubwa wa kampuni ya Vodacom wanapata habari kwa haraka na za motomoto kupitia simu zao za kiganjani. 

  Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Kelvin Twissa amesema kuwa Vodacom inafurahi kuungana na magazeti ya The Guardian na Nipashe kuanzisha huduma hiyo chini ya kampuni ya Premier Mobile Solution.

  Twissa amesema huduma hiyo itakayo wahusisha wateja wa Vodacom itasaidia kuwawezesha wateja hao kupokea taarifa mbalimbali kupitia simu zao za mkononi kwa gharama nafuu ya Sh 100 kwa siku.

  "Mteja wa Vodacom ataunganishwa na huduma hii kwa kupeleka ujumbe wenye neno GUARDIAN au NIPASHE kwenda namba 15501, kwa gharama nafuu kabisa ya Sh100 kwa siku, na baada ya hapo atakuwa akipokea taarifa mbalimbali kutoka vyumba vya habari vya magazeti ya The Guradian na Nipashe"

  Naye Meneja Masoko wa kampuni ya The Guardian Simon Marwa ameitaja huduma hiyo kuwa itawawezesha wasomaji wa magazeti ya hayo ambao ni wateja wa mtandao unaoongoza nchini wa Vodacom kupata habari za punde kirahisi. "Huduma hii ni muhimu kwetu na kwa vodacom kwani wasomaji wa magazeti haya sasa watakuwa na uwezo wa kupata habari za punde za kitaifa na kimataifa kiurahisi kupitia simu za viganjani."Alisema Marwa

  "Vodacom imeenea nchi nzima hivyo ubunifu huu wa upashanaji habari wananchi wa njia ya kisasa ni wazi utawanufaisha walio wengi na kutaleta utofauti kwa jamii."Alisema Marwa.

  Kwa upande wake Meneja Uendeshaji wa kampuni ya Premier Mobile Solution Lulu Ramole amesema huduma ya Nipashe SMS na The Guardia SMS imebuniwa wakati muafaka ambapo jamii ina mwamko wa kupata taarifa mbalimbali.

  "Ni furaha kubwa kwetu kuona tunasimamia huduma inayowaleta pamoja makampuni mawili makubwa katika nyaja ya Mawasiliano na Habari.Tumejipanga kuiwezesha huduma hii kuwa bora zaidi"Alisema Lulu

  Ameongeza kuwa mteja ana uhuru wa kujiunga na kujiondoa wakati wote atakapojisikia kufanya hivyo kwa kutuma neno STOP au ONDOA kwenda namba 15501 kutoka simu yake ya mkononi. Aliongeza kwamba huduma hii itatolewa kwa saa 24

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein akipata maelezo kutoka Naibu katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Nd,Juma Ali Juma wakati alipotembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia Mradi wa SAEMAUL UDONG.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein na Balozi wa Korea Bw.IL Chung (katikati) wakiangalia embe zilizokaushwa zikiwa katika Mpango maalum wa kuhifadhiwa wakati alipotembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia Mradi wa SAEMAUL UDONG.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bw.IL Chung (katikati) wakiangalia embe zilizokaushwa zikiwa katika Mpango maalum wa kuhifadhiwa wakati alipotembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia Mradi wa SAEMAUL UDONG.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein(katikati) na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bw.IL Chung wakipata maelezo kutoka Naibu katibu Mkuu Wizara ya Kilimo na Maliasili Nd,Juma Ali Juma (kulia) wakati alipotembelea mitambo katika kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia Mradi SAEMAUL UDONG.
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK.ALi Mohamed Shein akibadilishana mawazo na na Balozi wa Korea Nchini Tanzania Bw.IL Chung mara baada ya kutembelea kituo cha kukausha Embe Dodo katika Kijiji cha Cheju kibonde maji leo kilichojengwa na Shirika la misaada la Koika nchini Korea kupitia Mradi SAEMAUL UDONG .[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Ally CHangwila akimkabidhi msaada wa Madaftari na vyakula mbalimbali Samson Ali (12) ambaye ni mmoja wa watoto waishio katika mazingira magumu ambao hivi sasa wanalelewa katika Kituo cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam kituo hicho kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki.watoto hao wanapatikana kwa kukusanywa mitaani.
  Mwalimu wa Kituo cha Kulea watoto waishio katika mazingira Magumu cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, Martin Modest akipokea Msaada wa Vyakula na Vifaa vya Shule yakiwemo Madaftari kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Ally Changwila ,Watoto hao wanapatika kwa kukusanywa kutoka mitaani na kulelewa hapo ambapo wanapatiwa ushauri kabla ya kuanzishwa shule.
  Watoto wanaolelewa katika kituo cha kuleya watoto waishio katika mazingira magumu cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, wakifurahia madaftari waliyokabidhiwa msaada na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)Ally CHangwila ambaye ndiye aliyekabidhi msaada huo.
  Watoto wanaoishi katika Mazingira magumu ambao wanalelewa katika kituo cha Child In The Sun kilichopo Manzese Dar es Salaam, kikiwa chini ya Kanisa Katoliki wakibeba mizigo ya vyakula mbalimbali na vifaa vya shule baada ya kukabidhiwa msaada na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Kwa ajili ya kusherehekea sikukuu ya Idd.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wajumbe wa Chama cha Wabunge kutoka nchi za Jumuiya ya Madola (CPA) katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini Arusha. Mheshimiwa Makamu wa Rais alifungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Mkutano huo sambamba na masuala mengine pia unajadili juu ya wajibu wa mabunge na mchango wao katika kusimamia utawala bora pamoja na kusaidia serikali za Afrika kubuni mipango ya maendeleo inayolenga vizazi vya sasa kwa lengo la kuijenga Afrika ijayo.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Makamu wa Rais wa CPA na Spika wa Ufalme wa Lethoto, Enoch Sephir Motanyane, wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, jijini Arusha kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na baadhi ya Wabunge wakati akiondoka nje ya ukumbi wa AICC jijini Arusha baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Spika wa Bunge la Jamhuri, Anne Makinda na Mwenyekiti wa CPA Tawi la Tanzania, Azan Zungu, wakifurahia ngoma ya asili wakati walipokuwa wakiwasili kwenye ukumbi wa AICC, jijini Arusha kufungua mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wabunge baada ya kufungua rasmi mkutano wa 45 wa CPA unaozikutanisha nchi za Afrika unaofanyika nchini Tanzania, kuanzia leo Julai 24 hadi Julai 27, 2014. Picha na OMR

  0 0

  Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy akisoma hotuba kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernad K. Membe (Mb.) kwa ajili ya kumuaga Balozi wa Norway nchini, Mhe. Ingunn Klepsvik ambaye amemaliza muda wake wa kazi. Hafla hiyo fupi ya chakula cha mchana ilifanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Dar es Salaam.
  Balozi Mushy akimkabidhi Balozi Klepsvik zawadi ya picha ya kuchora ya Twiga  kama ukumbusho wake kwa Tanzania
  Balozi Klepsvik naye akizungumza machache wakati wa hafla hiyo.
  Mkuu wa Mabalozi  ambaye pia ni Balozi wa DRC hapa nchini, Mhe. Juma Halfan Mpango (kushoto) pamoja na Balozi Mushy na Balozi Klepsvik wakati wa hafla hiyo.
  Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya na Amerika, Bibi Victoria Mwakasege akiwakaribisha wageni waalikwa wakati wa hafla ya kumuaga Balozi Klepsvik.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitia saini tamko la Mkutano Maalum wa Nchi za Maziwa Makuu (ICGLR) kuhusu mikakati ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana kupitia Uendelezaji Miundombinu na uwekezaji, uliofanyika kwenye hoteli ya Kempinski jijini Nairobi Julai 24, 2014. Kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Batilda Burian na wapili kushoto ni Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Wakuu wa shule za serikali zilizofanya vibaya kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha sita mwaka huu  pamoja na Maofisa elimu wa Mikoa wamepewa muda wa mwezi mmoja ili kubaini chanzo cha  shule zao kuwa na ufaulu hafifu.
   Baada ya kubaini chanzo hicho cha ufaulu hafifu wanatakiwa kutoa taarifa kwa katibu mkuu Tawala za mikoa na serikali za mitaa-TAMISEMI.
   Miongoni mwa shule ambazo wakuu wake wametakiwa kujieleza ni pamoja na shule ya Tambaza iliyopo jijini Dar es salaam na shule ya Iyunga ya Mkoani Mbeya, ambapo muda huo wa mwezi mmoja umeanza  leo.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam,  katibu Mkuu Tamisemi Jumanne Sagini amesema, kushuka kwa ufaulu kwa shule hizo kumewashtua  watu wengi, kwani shule hizo zimejengewa uwezo mzuri wa vifaa pamoja na miundombinu.
   
  Hata hivyo Sagini amesema, idadi ya wanafunzi 22,685 waliofaulu masomo ya sayansi kwa mwaka  huu wa 2014  ni kubwa kwa  zaidi ya wanafunzi 3,939 ikilinganishwa na wanafunzi 18,746  waliofaulu masomo hayo mwaka jana.
   
  Amesema kuwa ufaulu huo umeipa changamoto Serikali na imekuwa ikifanya kila jitihada kuhakikisha kuwa kila mwanafunzi ambae amefaulu na kupata alama stahiki  katika masomo aliyoyachagua anapata shule.
   
  Aidha amewataka wazazi wa wanafunzi waliokuwa wamepangiwa kusoma masomo ya sanaa ilihali ufaulu wao ni katika masomo ya sayansi, kutokuwa na wasiwasi kwani serikali imebaini changamoto hiyo na kuifanyia kazi.

  0 0

   MECHI kati ya timu Israeli ya Maccabi dhidi ya Lille ya Ufaransa iliahirishwa baada ya waandamanaji wanaoiunga mkono Palestina kuvamiwa uwanja.
  Waandamanaji hao walioripotiwa kuwa na asili ya Uturuki waliingia katika uwanja wa Austrian ambapo mchezo ulikuwa unaendelea na kuwavamia wachezaji wa Maccabi na kuzua vurugu.
  Mmoja wa wachezaji alionekana akizozana na shabiki kabla ya kuanza kurushiana makonde mazito. Hata hivyo wachezaji wa Maccabi walifanikiwa kutoka uwanjani bila kujeruhiwa. Tukio hili limekuja wakati huu ambao majeshi ya Israel yamevamia na kufanya uhalifu dhidi ya majeshi ya Hamas huko Gaza.  0 0older | 1 | .... | 514 | 515 | (Page 516) | 517 | 518 | .... | 3270 | newer