Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

house for rent at TABATA Changombe in Dar es salaam

$
0
0
 The House is Located at TABATA Changombe in Dar es salaam next to African Schools.
It is fenced with masonry wall fully painted
It has 4 bedrooms i.e. 1master bedroom and 3 normal rooms, Sitting room, dinning room, kitchen and storage room a separate shower and washroom.
In addition is posses an elevated 5,000ltrs water storage tank and 5,000 ground level water stoarge tank.
It has a spacious compound;
For more detail and viewing please contact the following numbers;


Looking for the Idd Crescent and a Comet in July Night Skies over Tanzania

AZANIA BANK LTD TAWI LA MOSHI YAFUTURISHA WATEJA WAKE

$
0
0
Baaadhi ya waalikwa wakipata futari iliyoandaliwa na Benki ya Azania tawi la Moshi.
Mkuu wa wilaya ya Moshi  Mhe Ibrahim Msengi (katikati)akiwa na Shekhe  mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro  Alhaj Shaban Rashid(kulia)
Baadhi ya waalikwa wakipata futari iliyoandaliwa na benki ya Azania Tawi la Moshi.
Meneja wa Azania Bank tawi la Moshi Bi. Hajira Mmambe(shoto)akiteta jambo na mfanyabiasha  Ibrahimu Shayo maarufu kama Ibra line(mwenye kanzu) ,katikati ni mfanyakazi wa taasisi moja ya fedha mjini Moshi.
Afisa Biashara Mwandamizi wa Azania Bank makao makuu ,Othman Jibrea akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata futari ya pamoja iliyoandaliwa na Azania Bank tawi la Moshi.
Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

FFU wa Ngoma Africa Band wawatia wazimu washabiki Tubingen,Ujerumani

$
0
0
Tubingen,Ujerumani,Ilikuwa usiku  jumamosi  19.Julai 2014 bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band aka FFU-Ughaibuni " imefanikiwa tena kuwatia wazimu malefu ya washabiki katika maonyesho makubwa ya International African Festival 2014 mjini Tubingen,Ujerumani. 

Bendi hiyo iliyobatizwa majina mengi ya utani na washabiki wake  imejikuta inaongeza idadi ya maelfu ya washabiki katika maonyesho yake.

Katika hali isiyo ya kawaida usiku wa jumamosi 19 Julai 2014 Ngoma Africa band
imejikuta  ipo ikitingisha jukwaa kwa muziki moto moto ambao mbele ya jukwaa kulikuwa na umati wa washabiki na nyuma ya jukwaa kukiwa na magari maalumu ya Polisi wa kuzuwia ghasia wa kijerumani ambao walikuwa tayari kwa lolote lile!

Maelfu ya washabiki wakiwa wanajirusha bila ya mashaka na muziki wa FFU-ughaibuni aka viumbe wa ajabu Anunnaki Alien ukipenda watoto wa mbwa chini ya uongozi wake mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda Ras Makunja.

Wadau mbali mbali walihojiwa katika maonyesho hayo wameitaja bendi hiyo kila kukicha inazidi kujizolea wingi wa umati wa washabiki kutokana na mvuto na umahili wake. Ngoma Africa band inatajwa ndio bendi pekee ughaibuni inayoongoza kuwa na washabiki wa lika,jinsia na mataifa mbali mbali.
Kamanda wa FFU,Ras Makunja akiongoza mashambulizi.
Binti Komando wa FFU Band akifanya yake.
Mashambulizi yakiendelea.
nyomi uwanjani hapo.

UCHAGUZI DMV: KUKOSA UTOVU WA NIDHAMU DHIDI YA MPIGANIA URAIS HAPA DMV (NDUGU LIBERATUS MWANGOMBE) - SAUTI YA BOARD MEMBA DMV

Globu ya Jamii

BALOZI KAMALA AKUTANA NA MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA UWEKEZAJI NA BIASHARA YA BRUSSELS

$
0
0
Balozi wa Tanzania Belux na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Uwekezaji na Biashara ya Brussels Bi. Benedicte Wilders (kushoto) na Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa wa taasisi hiyo Bwana. Philip Feytons. Balozi Kamala amekutana na viongozi hao leo hii Brussels kuwaomba wahimize makampuni ya Brussels kushiriki ziara ya kibiashara inayoandaliwa kufanyanyika Tanzania mwishoni mwa mwaka huu.

Bweni la shule ya Sekondari Erikisongo Wilayani Monduli lateketea kwa moto leo

$
0
0
Kiasi cha wanafunzi 100 wa shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli wamenusurika kifo baada ya vyumba vitano vya mabweni yao kuteketea na moto leo (Jumatano) asubuhi.

Moto huo ambao inaelezwa chanzo chake ni hitilafu ya umeme ilitokea wakati wanafunzi wote wako darasani.

Hakuna mtu yoyote aliyedhurika lakini mali kadhaa za wanafunzi zimeteketea. Kikosi Cha zimamoto kutoka Arusha kilifika wakati tayari mabweni hayo yameshateketea.

Mbunge wa Jimbo la Monduli Mh Edward Lowassa  ametembelea shule hiyo na kuahidi kuwasafirisha wanafunzi majumbani kwao wakati  utaratibu unafanywa kurejesha katika hali ya kawaida.

Gharama za kuwasafirisha wanafunzi hao ni shilingi laki Saba. Aidha Mh Lowassa amesema kiwanda Cha magodoro Cha Tanform Cha Arusha kimetoa msaada wa magodoro 100 kufuatia kadhia hiyo.
Kikosi Cha zimamoto kikijaribu kupambana na moto ulioteketeza mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo mjini Monduli yaliyoteketea kwa moto, akiongozana na mkuu wa shule hiyo mwalimu Agnes Nyange.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akikagua mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo Monduli mjini yaliyoteketezwa kwa moto.
Mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa afisa elimu wa Monduli mwalimu Shaaban Mgunya wakati alipotembelea mabweni ya shule ya sekondari ya Erikisongo wilayani Monduli yaliyoteketea kwa moto.

WAFANYAKAZI WA VODACOM TANZANIA WAFUTURU KWA PAMOJA NA WATOTO YATIMA WA MWANDALIWA BUNJU JIJINI DAR

$
0
0
Mmoja wa watoto anaelelewa katika kituo cha yatima cha Mwandaliwa Islamic kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam,Asha Ramadhan,akihudumiwa futari na baadhi ya wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakati walipokwenda kufutulisha futari watoto hao wa kituo hicho jana.
Ofisa Mkuu wa Idara ya Huduma kwa wateja wa Vodacom Tanzania Harriet Lwakatare akimmiminia uji Ali Shaban (3) wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo lipokwenda kufuturisha katika kituo cha kulelea watoto yatima cha Mwandaliwa Islamic kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa kitengo cha Uhusiano na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia akiwasaidia kuweka uji kwa baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Mwandaliwa Islamic kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam,Wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo walipotembelea kituo hicho kwa lengo la kujumuika na watoto hao kufuturu kwa pamoja hapo jana.
Mkuu wa kitengo cha kusaidia jamii cha Vodacom"Vodacom Foundation"Yessaya Mwakifulefule akiwagawia futari watoto wanaolelewa katika kituo cha yatima cha Mwandaliwa Islamic kilichopo Bunju jijini Dar es Salaam.Ambapo wafanyakazi wa kampuni hiyo waliwatembelea watoto hao na kujumuika pamoja kwa futari hapo jana.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TBL YATOA MSAADA WA SH. MIL. 45 ZA KISIMA KIJIJI CHA KAMBI YA SIMBA KARATU

$
0
0
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akipeana mkono na Mwenyekiti wa Kijiji cha Kambi ya Simba, Damian John wakati wa makabidhiano ya mfano wa hundi ya Sh. Milioni 45 zilizotolewa kwa ajili ya kuchimba kisima cha maji kijijini hapo mwishoni mwa wiki. Wengine ni Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba (mwenye miwani) na Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Karatu Moses Mabula.
 Ofisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Doris Malulu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kambi ya Simba, Kata ya Mbulumbulu wilayani Karatu, Arusha, wakati wa hafla ya kuwakabidhi mfano wa hundi ya sh. mil. 45 za kugharamia uchimbaji wa kisima cha maji kijijini hapo, mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba na aliyekaa ni Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Karatu, Moses Mabula.
 Wananchi wa kijiji hicho wakishuhudia makabidhiano ya hundi hiyo
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya wilaya ya Karatu, mkoani Arusha, Moses Mabula na Meneja Mauzo TBL Mkoa wa Arusha Richard Temba wakiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Maji ya Kijiji cha Kambi ya Simba pamoja na watalaamu watakaochimba kisima hicho cha maji, baada ya kukabidhiwa mfano wa hundi ya Sh. Milioni 45 na TBL.

TOFAUTI ZA DINI ZISIWAGAWE WATANZANIA - MH. MWINYI

$
0
0
Rais Mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi akiwasili katika viwanja vya Karimjee kuhudhuria Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kushoto) kwa watoto yatima kutoka vituo mbalimbali vya kulelea watoto hao vya jiji la Dar es salaam. Wengine wanaoonekana kutoka kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum.
Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam, Kamishna Suleiman Kova (katikati) akifafanua jambo kwa viongozi wa mkoa wa Dar es salaam Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Bw. Saidi Meck Sadiki (wa pili kutoka kulia), Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi(kulia) na Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema (kushoto) wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa huo katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.
Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Alhadi Mussa Salum (wa kwanza kushoto) na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahmani Kinana wakijumuika katika Futari hiyo.

Na. Aron Msigwa –MAELEZO. 

Rais mstaafu wa awamu ya pili , Ali Hassan Mwinyi ,amewataka watanzania kuwa makini kwa kutoruhusu tofauti za dini zilizopo hapa nchini kuwa chanzo cha mgawanyiko miongoni mwao.

Kauli hiyo ameitoa jana usiku jijini Dar es salaam wakati wa Futari iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki kwa watoto wanaoishi katika vituo vya kulelea watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali iliyofanyika katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es salaam.

Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa Futari hiyo amesema kuwa kila Mtanzania bila kujadili itikadi na dini aliyonayo ana wajibu wa kulinda na kutunza amani iliyopo kwa kuendelea kudumisha upendo na ukarimu kwa wenzake ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo yaliyomo katika vitabu vitakatifu.

“Nawasihi Watanzania wenzangu tuendelee kupendana, tuwe wamoja katika kushirikiana, kamwe tusiruhusu wala kukubali mgawanyiko wa dini wala itikadi zetu” Amesisitiza.

Amewashukuru viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa huo Saidi Meck Sadiki kwa uamuzi walioufanya wa kuandaa Futari iliyowaunganisha watoto yatima, wananchi na viongozi mbalimbali bila kujadili itikadi na dini zao ikiwa ni ishara ya kuonyesha upendo na ukarimu walio nao.

Kwa upande wake Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza wakati wa Futari hiyo aliyowaandalia wageni hao amesema kuwa serikali ya mkoa inaendelea kutekeleza mipango mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ukarabati na ujenzi wa miundombinu iliyoharibiwa vibaya wakati wa msimu wa mvua jijini Dar es salaam.

Bw. Sadiki ameziagiza Halimashauri za Wilaya za Temeke, Ilala na Kinondoni na Wakala wa Barabara (TANROAD) mkoa wa Dar es salaam kuhakikisha kuwa wanarejesha hali ya kupitika kwa barabara iliyokuwepo mwanzo ili kuwaondolea kero ya usafiri wananchi.

Amezitaka mamlaka hizo kutumia fedha za ndani na zile zilizotolewa na Serikali Kuu kukamilisha ukarabati wa miundombinu hiyo yakiwemo madaraja yaliyosombwa na maji kwa muda muafaka ili kuruhusu magari kuweza kufika katika maeneo hayo.

Katika hatua nyingine Bw. Meck Sadiki ametoa wito kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam kushiriki kikamilifu katika suala la usafi na uhifadhi wa mazingira kwa kujenga utaratibu wa kusafisha mazingira ya jiji ili kulinda heshima ya jiji huku akisisitiza kuwa dini zote zinamtaka mwanadamu awe mwadilifu na mwenye kuzingatia usafi.

Amezitaka mamlaka zinazosimamia utekelezaji wa sheria za kuhifadhi mazingira jijini Dar es salaam kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuhakikisha maeneo yote ya jiji yanaendelea kuwa katika hali ya usafi. Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum akuzungumza wakati wa Futari hiyo ameeleza kuwa viongozi wa dini na serikali kote nchini wanalo jukumu kubwa la kuwaongoza wananchi kutenda mema na kuendelea kuvumilia.

MH. PINDA AKUTANA NA VIONGOZI WA MAKAMPUNI YA SOMITO NA CITI BANK

$
0
0
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na viongozi wa Citi Bank ofisini kwake jijini Dar es salaam Julai 23, 2014. Kulia kwake ni Waziri wa Uchukuzi , Dr. Harrison Mwakyembe.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Citi Bank baada ya kuzungumza nao , Ofisini kwake jijini Dar es salaam julai 23, 2014. kushoto ni Waziri wa Uchukuzi aliyemabatana na ujumbe huo na kushoto kwa Waziri Mkuu, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr. Mary Nagu.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa kampuni ya Sumitomo Chemicals ya Japan wanaokusudia kuwekeza kiwanda cha mbolea nchini na katika kilimo cha mpunga. Wapili kushoto ni Waziri wa Kilimo , Chakula na Ushirika, Mhandishi Christopher Chiza. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

HAWZAT IMAM SWADIQ KUONGOZA MAANDAMANO YA KULAANI MAUAJI YA HUKO GAZA

$
0
0
Na Rose Masaka MAELEZO-Dar es Salaam

TAASISI ya  Hawzat Imam Swadiq wameandaa maandamano ya kulaani mashambulizi yanayofanywa na Vikosi vya Israel dhidi ya wananchi wa Palestina wasio na hatia.

Kwa mujibu wa Msemaji wa Taasisi hiyo Profesa Abdul Shariff, maandamano hayo yanalenga kuueleza ulimwengu kuwa wananchi wa Tanzania wanalaani mauaji yanayoendelea huko Gaza Palestina.

Amesema kuwa maandamano hayo  ambayo yatafanyika siku ya Ijumaa  Julai 25 mwaka huu yanatarajia kuanzia Kituo cha Daladala cha Boma na kuishia Kigogo uwanja wa Bibo.

Profesa Shariff ameongeza kuwa wameamua kupaza sauti zao kulaani baada ya kuona Jumuiya mbalimbali za Kimataifa ikiwa imenyamaza huku mamia ya watu wakizi kupoteza maisha yao.

Amesema kuwa inasikitisha kuona hata vyombo vya habari hasa vya Magharibi havitoi nafasi kubwa kwa mauaji hayo ukilinganisha na mauaji yaliyotokea kwa kulipuliwa kwa ndege Malyasia.

Naye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Sheikh Hamed Jalala amesema kuwa wamealika viongozi na Mabalozi wa Nchi mbalimbali ili nao waweze kushiriki katika  kupaza sauti zao pamoja na watanzania kulaani vitendo vinavyofanywa na Israel vya kuua watu wasio na hatia.

Sheikh Jalala amesema kuwa kunyamazia tatizo hilo ni kufanya kosa kwani hakuna hata dini moja inaruhusu mauaji ya binadamu mwingine.

Amesema kuwa maandamano  hayo yatahusisha watu wa dini zote na yamepata Kibali cha Mamlaka husika.

MKUTANO WA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BRN WAFANYIKA LEO JIJINI DAR

$
0
0
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Prof. Benno Ndulu akichangia hoja wakati wa mkutano wa kupitia taarifa ya mwaka mmoja ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa (BRN) uliofanyika leo Jumatano Julai 23, 2014 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji Mhandisi Bashir Mrindoko
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akichangia hoja wakati mkutano huo. Kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Asha- Rose Migiro na (katikati) Mtendaji Mkuu wa Ofisi ya Rais- Usimamizi wa Utekelezaji wa Miradi (PDB), Bw. Omari Issa.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Janet Mbene akichangia hoja wakati mkutano huo. Kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Bw. Jumanne Sagini na kulia ni
 Dk Deodatus Mtasiwa, Naibu Katibu Mkuu, Tamisemi.
Naibu Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Angellah Kairuki (katikati) akichangia hoja wakati mkutano wa kupitia taarifa ya mwaka mmoja ya utekelezaji wa Mpango wa Matokeo Makubwa sasa uliofanyika leo Jumatano Julai 23, 2014 katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Harrison Mwakyembe (kulia) akichangia akichangia hoja wakati mkutano huo. Kutoka kushoto ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mhe. Shukuru Kawambwa, Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Mhe. Mwigulu Nchemba, na Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi.
PICHA NA ISMAIL NGAYONGA- MAELEZO

MIRADI IWE ENDELEVU SIYO KWA MWENGE TU - RACHEL KASANDA

$
0
0
VIONGOZI na watendaji mkoani Pwani wametakiwa kuhakikisha kuwa miradi yote ya maendeleo inayozinduliwa katika kipindi cha mbio za mwenge iwe endelevu ili iwasaidie wananchi na si kwa ajili ya mbio hizo.

Baadhi ya miradi imeonekana kuzinduliwa na viongozi wa mbio za mwenge lakini baada ya muda inakufa jambo ambalo si malengo ya miradi hiyo ambayo imekuwa mkombozi kwa wananchi katika kutatua changamoto za kupata huduma za kijamii.

Hayo yamesemwa na kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Rachel Kasanda kwenye kijiji cha Bungu wakati wa kuweka jiwe la msingi kwenye ujenzi wa stendi ya mabasi ya Ikwiriri wilayani Rufiji mkoani humo.

Kasanda amesema kuwa miradi hiyo inapaswa kuwa endelevu ili jamii iweze kunufaika na si kuwa ya muda kwa ajili ya mwenge kwani hiyo ni michango ya wananchi, wahisani na serikali hivyo lazima iwe na manufaa.

Amesema kuwa Viongozi wanapaswa kuhakikisha kuwa miradi hiyo inafanya kazi baada ya kuzinduliwa kwa kuwa endelevu na kutoa matunda ambayo yanatarajiwa na wananchi kutokana na ujenzi wake.

Amesema kuwa baadhi ya viongozi wamekuwa wakifanya miradi hiyo kwa muda tu ambapo ikishazinduliwa inaachwa hapo hapo pasipo kuendelezwa na kusababisha kufa jambo ambalo halipaswi kuendelea kufumbiwa macho.

Aidha viongozi na watendaji ndiyo watu wa kuwaonyesha njia wananchi kwa hivyo wanapaswa kuhakikisha miradi hiyo inakuwa na mafanikio kwa wananchi ili kuwaondolea changamoto za upatikanaji wa huduma za kijamii.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Rufiji mkoani Pwani Nurdin Babu amesema kuwa yeye kama kiongozi kwa kushirikiana na watendaji, viongozi na wananchi watahakikisha miradi hiyo inakuwa endelevu ili iwe na manufaa kwa wananchi.

Babu amesema kuwa wamejipanga kuhakikisha miradi hiyo inaleta manufaa kwa walengwa ambao ni wananchi kwani wamekuwa na changamoto nyingi ambazo zinatatuliwa hatua kwa hatua kwa kuwashirikisha wadau wa maendeleo. Mbio hizo za mwenge leo zitakuwa wilaya ya Kibaha.

TASO KUTOA ELIMU KWA WANALINDI KUHUSU UBORESHAJI WA KILIMO

$
0
0
Na Rose Masaka - MAELEZO

WANANCHI mkoani Lindi wanatarajiwa kuelimishwa njia bora na za kisasa za uvuvi, ufugaji na ukulima ili waweze kuboresha kipato chao na Taifa kwa ujumla. Kauli hiyo imetolewa leo mjini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wakulima Tanzania(TASO) Engelbert Moyo wakati akiongea na waandishi wa habari.

Amesema kuwa wakati wa maonesho ya nanenane ambayo Kitaifa yanafanyika mkoani Lindi watajitahidi kuhakikisha wananchi wanajifunza teknolojia mpya za kilimo, ufugaji na uvuvi ili waweze kuzalisha mazao yanayokidhi viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

Moyo ameongeza kuwa watawaelimu wavuvi juu ya madhara ya uvuvi haramu na unavyohatarisha mazingira na viumbe wa majini.

Aidha Mwenyekiti huyo amesema kuwa maonesho yatafunguliwa na Rais wa Serikali za Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein na kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.

Amesema kuwa Mawaziri mbalimbali watasaidia kutoa elimu kwa wakazi wa Mkoa huo kuhusu shughuli mbalimbali wanazozifanya katika kuwaletea maendeleo.

Kali TV: Inside DC Modeling Industry

BALOZI KAMALA ASAINI KITABU CHA MAOMBOLEZO YA WALIOFARIKI KATIKA AJALI YA NDEGE YA MALAYSIA

$
0
0
Balozi wa Tanzania BELUX na Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala akisaini Kitabu cha Maombolezo ya waliofariki katika ajali ya ndege ya Malaysia. Kitabu hicho kimefunguliwa leo hii katika Ubalozi wa Malaysia Brussels.

PPF na MSD wasaini makataba wa mpango wa "wekeza"

$
0
0
 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kushoto), na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, wakiweka saini mkataba wa “wekeza” kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD, Keko jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014. Chini ya Mkataba huo, zaidi wa wafanyakazi 400 wa MSD wamejiunga na PPF. 
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, William Erio, (Kushoto), akibadilishana hati na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Bohari ya Dawa, (MSD), Cosmas Mwaifwani, baada ya kusaini mkataba wa mpango wa “Wekeza” kwenye hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya MSD jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014
 Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Malya, (Kushoto), akikabidhi kadi mpya ya uanachama kwa mwanachama mpya ambaye ni mfanyakazi wa MSD, mara baada ya PPF na MSD kusaini makataba wa mpango wa 'Wekeza" kwenye hafla iliyofanyika makao makuu ya MSD, Keko jijini Dar es Salaam, Julai 23, 2014
 Mkurugenzi wa Operesheni wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Asumpta Malya, (Kushoto), akikabidhi kadi mpya ya uanachama kwa mwanachama mpya ambaye ni mfanyakazi wa MSD
 Viongozi wa PPF na wenzao wa MSD, wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutiliana saini mkataba ambapo MSD na PPF zimekubaliana kuanzisha mpango wa "Wekeza" ambapo wafanyakazi wa MSD sasa watakuwa wakichangia kwenye mfuko huo ili kujiwekea akiba na kujipatia mafao mbalimbali
Viongozi wa PPF na wenzao wa MSD, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa MSD waliokabidhiwa kadi za uanachama wa Mfuko huo, mara baada ya kutiliana saini mkataba ambapo MSD na PPF zimekubaliana kuanzisha mpango wa "Wekeza" ambapo wafanyakazi wa MSD sasa watakuwa wakichangia kwenye mfuko huo ili kujiwekea akiba na kujipatia mafao mbalimbali

US-African Diaspora Investment Symposium

$
0
0
Fellow East Africans
The first US-African Diaspora Investment Symposium will be held on 4th August 2014 at theRonald Reagan Building and International Trade Center in Washington DC. 
The event will highlight the tremendous potential for crowd funding and other investment channel for African Diaspora to support economic growth and will allow Homestrings access to investible projects in Sub-Saharan Africa.  
This event is jointly hosted by Homestrings, Developing Market Associates (DMA), the Small Enterprise Fund (SEAF) and the International diaspora Engagement Alliance (IdEA) in partnership with the Eastern Africa Diaspora Business Council (EADBC
 
 
See you there!

Sincerely,
 
EADBC Management
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images