Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 512 | 513 | (Page 514) | 515 | 516 | .... | 3283 | newer

  0 0  0 0

   Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili akizungumza mbele ya wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya Azania,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

  Bwa.Singili alisema kuwa Benki ya Azania ni kama sehemu ya jamii, watajitahidi kutoa msaada kwa jamii katika Nyanja za elimu,afya na kusaidia yatima kila nafasi na uwezo unaporuhusu.Benki ya Azania pia iliwaalika Watoto waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House Foundation.

  Mkurugenzi huyo alisema kuwa  benki ya Azania imekuwa sasa na kufikia matawi 15 ikilinganishwa na matawi matatu waliyokuwa  nayo mwaka 2007,alisema kwa Dar es salaam pekee wana jumla ya matawi 05. ''tunawashukuru wateja wetu,kwani bila uwepo wao tuingefika hapa,tunapenda kuwahakikishia kuwa tunaendelea na juhudi zetu za nia ya kutaka kuwa na teknolojia ilio sahihi'',alisema MKurugenzi huyo.
   Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili (kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wageni wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri ukumbi humo pamoja na waalikwa wengine kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar.
   Afisa mkuu maendeleo ya biashara kutoka benki ya Azania,Bwa.Othman Jibrea akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kupata ftari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar Es Salaam.
   Watoto waishio katika mazingira magumu kutoka kituo cha Mitindo House Foundation wakipata futari ya pamoja iliyoandaliwa na Benki ya Azania sambamba na wadau wengine wa benki hiyo,hafla hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar Es Salaam.
  Sheikh Abdulrahman Ali Issa akitoa shukurani za dhati (kwa niaba ya sheikh wa Mkoa Dar Es Salaam),kwa uongozi wa benki ya Azania kwa kutoa mwaliko wa futari kwa wageni waalikwa mbalimbali wakiwemo watoto yatima kutoka kituo cha Mitindo House Foundation..
    Mkurugenzi Mtendaji wa Azania Bank Limited,Bwa.Charles Singili (kwanza kulia) akiwa na baadhi ya wageni wakipakua ftari ya pamoja iliyoandaliwa na benki hiyo,mwishoni mwa wiki kwenye moja ya ukumbi  uliopo ndani ya jengo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA),jijini Dar.

  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Uongozi na Wafanyakazi wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki unatoa pole kwa Katibu Mkuu wake Bi. Joyce K.G. Mapunjo kufuatia kifo cha Mume wake Profesa Zakaria Mmbwambo (58) kilichotokea Jumamosi tarehe 19 Julai 2014, Dar es Salaam.

  Wizara inaungana na ndugu, jamaa na marafiki katika kuipa mkono wa pole familia ya Profesa Mmbwambo katika kipindi hiki kigumu.

  Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi. Bwana ametoa, Bwana ametwaa Jina la Bwana lihimidiwe.

  Ratiba ya Maombolezo na Mazishi ni kama ifuatavyo:
  1: LEO JUMATATU JULAI 21, MWILI WA MAREHEMU UTAAGWA MUHIMBILI NA WAFANYAKAZI WENZAKE SAA 6 MCHANA KWA MAANDAMANO YA WANATAALUMA NA HESHIMA ZA MWISHO ZITATOLEWA SAA 7 MCHANA MUHAS. BAADA YA HAPO MWILI UTAPELEKWA NYUMBANI KWAKE OYSTERBAY NA KUTOLEWA RAMBIRAMBI SAA 8 MCHANA. SAA 11 JIONI  MWILI UTAPELEKWA KIMARA STOP-OVER NYUMBANI KWAKE PIA.

  2: KESHO JUMANNE JULAI 22, MWILI UTAKUWEPO NYUMBANI KWAKE KIMARA NA MAOMBOLEZO NA RAMBIRAMBI ZITAANZA SAA 4 ASUBUHI NYUMBANI KWA MAREHEMU, SAA 7 MCHANA MWILI UTAPELEKWA KANISANI KIMARA LUTHERAN CHURCH KWA AJILI YA SALA SALAMU ZA MWISHO. SAA 10 JIONI MWILI UTAPELEKWA NYUMBANI KIMARA KWA MAZISHI.

  0 0

  Barua ya Wazi kwa Uongozi wa CCT juu ya Tamko la Mapatano ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 48 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania la tarehe 3 Julai, 2014.


  •   Sio la Kiponyaji, linatonesha Madonda
  •   Watu wa Mungu hawategemewi Kupotosha, Labda Wamepotoshwa


  Na John Nkhundi
   Si kawaida yangu kulumbana na viongozi wa dini kwa sababu ya heshima waliyonayo katika jamii na matumaini ya waumini wao kwao.  
  Hata hivyo, leo nimelazimika kuandika baada ya kusoma tamko la Jumuiya ya Kikristo Tanzania (CCT) lililotolewa na Mkutano wa Halmashauri Kuu iliyokutana tarehe 3 Julai, 2014 ambalo maudhui yake ni ya kisiasa na limesheni mambo ya dunia.
  Tamko hilo lililopewa jina la "Tamko la Mapatano ya Mkutano wa Halmashauri Kuu ya 48 ya Jumuiya ya Kikristo Tanzania wa Julai 2-3, 2014" limenistua kwa mambo makubwa matatu. Mosi, tamko hili limetolewa Julai 3, 2014 lakini likatolewa magazetini tarehe 15 Julai,2014 tena katika gazeti moja tu la Mwananchi. 
  Mtiririko huu wa matukio yaani muda wa Tamko lilipotolewa na muda lilipochapishwa kunatia mashaka ikiwa ni jambo la kimkakati au nasibu tu. 
  Zaidi, upana huu wa muda kati ya lilipotolewa na kuchapishwa kunaleta pia wasiwasi kuhusu uhalisia wa tamko lenyewe. Maana, kwa kawaida matamko ya aina hii hutolewa mara tu Mkutano unapoisha, tena kwa kusomwa mbele ya waandishi wa habari.

  0 0

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nachingwea, Mathias Chikawe akizungumza na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Kata ya Namikango, Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi leo. 
  Waziri Chikawe aliwataka viongozi hao kuwa na umoja ili kukipa nguvu chama chao hasa katika kipindi hiki wanapoelekea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa, ambapo kila mwanachama wa chama hicho alisisitizwa kuchukua fomu wakati muda utakapofika wa kuchukua fomu hizo. 
  Uchaguzi wa Serikali za Mitaa unatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mwaka huu ambapo wananchi watachagua Viongozi wa Mamlaka za Wilaya, Mamlaka za Miji midogo, Mamlaka za Miji na Halmashauri za Vijiji na Vitongoji. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nachingwea, Albert Mnali. Picha na Felix Mwagara wa WMNN.


  0 0


  VIONGOZI wa Benki ya Posta Tanzania (TPB) wakimsikiliza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mhe. Balozi Seif Ali Idd(hayupo pichani) wakati wa uzinduzi wa Mikopo ya Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na TPB, uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliyopo Kilimani mjini Zanzibar.
   WAFANYAKAZI wa Benki Posta Tanzania (TPB) wakiwa katika uzinduzi wa Mikopo ya Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kupitia Benki hiyo uliozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar , Mhe. Balozi Seif Ali Idd katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani

   MENEJA Mahusiano wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Ndg. Noves Moses akiwatambulisha viongozi wa Benki hiyo waliohudhuria katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki hiyo. Uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliyopo Kilimani
   OFISA Uhusiano wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF), Ndg. Khatib Idd akiutambulisha uongozi wa Mfuko huo uliohudhuria hafla ya uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa ZSSF kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania.
   OFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Ndg. Sabasaba Moshingi akitoa maelezo ya benki hiyo wakati wa uzinduzi wa Mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View
   OFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Ndg. Sabasaba Moshingi akitoa maelezo ya benki hiyo wakati wa uzinduzi wa Mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki hiyo uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View
   BAADHI ya Wastaafu wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) wakiwa katika uzinduzi wa Mikopo ya Wastaafu wa mfuko huo kwa mashirikiano na Benki ya Posta Tanzania (TPB) uliozinduliwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani Mjini Zanzibar.(


   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akiwa  Meza kuu  na WAZIRI wa Fedha Zanzibar, Mhe. Omar Yussuf Mzee (kulia)  OFISA Mtendaji Mkuu wa Benki ya Posta Tanzania (TPB), Ndg. Sabasaba Moshingi (kushoto)
   WAZIRI wa Fedha Zanzibar, Mhe. Omar Yussuf Mzee akizungumza katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanizbar (ZSSF) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani mjini Zanzibar

   WAZIRI wa Fedha Zanzibar, Mhe. Omar Yussuf Mzee akizungumza katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanizbar (ZSSF) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani mjini Zanzibar
   WAALIKWA mbali mbali wakiwa katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania (TPB), uzinduzi huo ulifanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani
   MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akizindua mfuko wa Mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania (TPB) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani mjini Zanzibar
   WAALIKWA mbali mbali wakiwa katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania (TPB), uzinduzi huo
   
   MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Balozi Seif Ali Idd akizindua mfuko wa Mikopo kwa wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa kushirikiana na Benki ya Posta Tanzania (TPB) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani mjini Zanzibar
   MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharib , Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akitoa shukrani katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa mashirikiano na Benki ya Posta Tanzania (TPB) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani mjini Zanzibar
  MKUU wa Mkoa wa Mjini Magharib , Mhe. Abdalla Mwinyi Khamis akitoa shukrani katika uzinduzi wa Mikopo kwa Wastaafu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) kwa mashirikiano na Benki ya Posta Tanzania (TPB) uliofanyika katika Hoteli ya Zanzibar Ocean View iliopo Kilimani mjini Zanzibar. Picha zote na Haroub Hussein

  0 0


  0 0
  0 0

  Courtesy of KTN

  0 0

  Mkwezi akiwa kazini kama alivyokutwa na mdau Salehe Ngayonga 
   wa Kibiti,Rufiji, Mkoa wa Pwani  kwa niaba Globu  ya Jamii 

  0 0

    BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA MHE GRACE MUJUMA (KATIKATI) AKIWA NA UONGOZI WA WAISLAM WAISHIO ZAMBIA WAKATI WA FUTARI ALIYOANDAA KWA WATANZANIA WAISHIO ZAMBIA NYUMBANI KWAKE JIJINI LUSAKA LEO
   BALOZI WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA MHE GRACE MUJUMA (KATIKATI) AKIWA NA UONGOZI WA WAISLAM WAISHIO ZAMBIA. KUTOKEA KUSHOTO JUMA NURU MWAKILISHI WA LAKE PETROLEUM, HUDDY KIANGI AFISA WA UBALOZI, SHEIKH ALI MOHAMED ALLIY KAIMU MUFTI, MHE GRACE MUJUMA BALOZI, SHEIKH ASSADULLAH MWALE GRAND MUFTI NA MUUMINI ALIYEFUATANA NA MUFTI.
   WAALIKWA WAKIPAKUA FUTARI
  MHE BALLZI GRACE MUJUMA AKIWA KATIKA PICHA YA PAMOJA NA BAADHI YA WAALIKWA WA FUTARI ILIYOFANYIKA NYUMBA KWA MHE BALOZI

  0 0

  Mwili wa Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS) , marehemu, Profesa Zakaria Mbwambo , ambaye ni mume wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi . Joyce Mapunjo ukiwasili leo kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam. Pembeni ni baadhi ya maprofesa wenzao wakiusindikiza.
  Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS) Profesa Ephata Kaaya akiuaga mwili wa Mhadhiri wa wa chuo hicho , marehemu, Profesa Zakaria Mbwambo , ambaye ni mume wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi . Joyce Mapunjo leo kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya maprofesa wa Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili, (MUHAS), wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Profesa mwenzao , marehemu, Profesa Zakaria Mbwambo , ambaye ni mume wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi . Joyce Mapunjo leo kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.

  baadhi ya waombezaji waiombeleza wakiwa katika hali ya huzuni wakati wa kuuaga mwili wa marehemu, Profesa Zakaria Mbwambo , ambaye ni mume wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki, Bi . Joyce Mapunjo leo kwenye viwanja vya chuo hicho jijini Dar es Salaam.Picha zote na Magreth Kinabo - Maelezo

  0 0

   Gari likiwa limebeba mifuko yenye viuongo hivyo, ambapo Jeshi la Polisi wilaya ya Kinondoni limesema kuwa limeanza uchunguzi wa kina baada ya kukakamata viungo mbalimbali vinavyodhaniwa kuwa ni vya binadamu katika  mifuko ya plastiki katika machimbo ya kokoto sehemu za Mbweni Mpiji, Magohe, nje kidogo ya jiji la Dar es salaam. 
  Habari zinasema  kwamba  hayo ni masalia ya viungo vya binadamu vilivyotupwa maeneo ya kutoka  chuo kimoja cha udaktari (jina kapuni kwa sasa)  baada ya wanafunzi kumaliza kutumia kwa mazoezi. Viungo hivi vilitupwa baada ya kukosa pesa za kuteketeza kwenye tanuri maalum. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam Suleiman Kova anatarajiwa kuzungumza mchana huu juu ya sakata hilo.
   Sehemu ya mifuko ya plastiki iliyokutwa na viungo hivyo ambavyo inasemekana ni pamoja na mikono, miguu, ngozi na sehemu nyingine za miili


  0 0

  Ndugu WanaDMV, kwa heshima na taadhima nachukua nafasi hii kujitambulisha kwenu rasmi kama Mgombea wa Nafasi ya Makamu wa Raisi wa Jumuiya ya Watanzania DMV.
  HARRIET SHANGARAI

  Nikiwa na mapenzi ya dhati kwa jamii,nimekuwa mtetezi wa haki za watoto yatima toka utotoni mwangu. Binafsi, nilijitoa kwa kidogo nilichokuwanacho na pia, nimekuwa muhamasishaji wa misaada ya elimu,chakula mavazi na malazi kwa watoto yatima. Kwa ufupi  nimeona mafanikio ya kina, japo bado wahitaji ni wengi.
  Vile vile, nilikuwa mstari wa mbele katika uanzishwaji wa Kikundi cha Wanawake cha Kupambana na Ukimwi “KIWAKUKI”.Chombo hiki kimedumu takribani miaka 25 na  kinaendelea kusaidia wengi nchini Tanzania kikishirikina na mashirika mbali mbali duniani.
  Nikiwa Mwanadiaspora nimepitia changamoto nyingi za afya na huduma zake. Jambo ambalo lilinishawishi kuingia taaluma ya afya ili niweze kuwa msaada kwa jamii. Jitihada hizi zimenipelekea kuanzisha blog yenye kutoa elimu afya kwa jamii kwa lugha ya kiswahili “NesiWanguBlogspot.com”. Nia ni kuleta mwamko katika uwanja wa afya na huduma zake.
  Zaidi, nimejihusisha na zoezi  la utafutaji wa Maangalizi ya Afya kwa wanaDMV.  Zoezi hilo lilikuwa  jaribio la ufumbuzi wa matatizo ya fya kwa Wanadiaspora. Nashukuru kwa mchango wa kila mmoja wenu na ninaomba Wanadiaspora wa vitengo vya afya kuwa mstari wa mbele katika kujali afya za jamii yetu. 

  0 0

   
  Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, Mhe Omar Mjenga leo ametembelea kampuni ya Nyumba ya NAKHEEL, ambayo ndio kampuni kubwa ya Serikali Dubai, kwa lengo la kujionea miradi mikubwa iliyotekelezwa na kampuni hiyo.

  Baadhi ya miradi iliyosimamiwa na kampuni hiyo ni pamoja na The Palm Dubai (the largest island Palm City in the World), Nakheel Mall, Dragon Mart na baadhi ya hotel za nyota tano Jijini Dubai.

  Kufuatia mazungumzo kati ya Mhe. Mjenga na Bw. Rashid Lootah, mwenyekiti wa NAKHEEL, wamekubaliana kwa pamoja kuwa mwenyekiti huyo na ujumbe wa washauri na wataalam wake kufanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania, tarehe 10 hadi 13 Agosti, 2014.

  Wakiongozana na Mhe. Balozi Mdogo Mjenga, watakutana na taasisi mbali mbali zikiwamo NHC, Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), TTB, TANAPA na zingine nyingi. Aidha, watapata fursa ya kuongea na Mawaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Viwanda na Biashara, Ardhi, 
  Nyumba na Maendeleo ya Makazi. 

  Kampuni hii ina nia ya kuwekeza katika hotel za nyota tano, nyumba za makazi na biashara pamoja na maduka makubwa(shopping malls).
   Mifano ya majengo ya kampuni hiyo
   Balozi Mdogo wa Tanzania, Dubai, alipotembelea kampuni ya Nyumba ya NAKHEEL
   The Palm Dubai (the largest island Palm City in the World


  0 0

  MWANAMKE mkazi wa kijiji cha Ikandamoyo, wilayani Katavi, Veronica Saleh ‘Mama Kaela’ (50), amefanya uamuzi adimu wa kuolewa na wanaume wawili ambao anaishi nao kijijini hapo.
  Kijiji hicho kipo umbali wa takribani kilometa 30 kutoka mjini hapa katika Jimbo la Katavi linalowakilishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda.
  Pamoja na ndoa hiyo iliyowezeshwa na mume mkubwa kukubali kuishi na mume mdogo, imeelezwa kuwa mwanamke huyo ndiye ‘aliyewaoa’ wanaume hao kwa zaidi ya miaka saba sasa, huku akiwa na amri kuu katika nyumba, kama ilivyo katika ndoa za kawaida.
  Wanaume hao ni Paulo Sabuni ‘Baba Kaela’ (60) ambaye ndiye mume mkubwa na Arcado Mlele (45) ambaye ni mume mdogo.
  Taarifa za kuwapo kwa ndoa hiyo ya aina yake, ziliifikia Globu ya Jamii na kufanyiwa uchunguzi kwa zaidi ya wiki tatu, na hatimaye katikati ya wiki hii, wahusika walikubali wao wenyewe kuzungumzia suala hilo. Kwa mujibu wa maelezo ya mwanamke huyo ambaye alionekana kuwa msemaji wa familia hiyo, yeye na mumewe mkubwa, walifika kijijini hapo miaka 24 iliyopita, wakitoka kijiji cha Usumbwa mpakani mwa Chunya, Mbeya na Tabora.

  0 0


  0 0


   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimwagilia maji mti wa kumbukumbu aliupanda muda mfupi baada ya kuzindua barabara ya Songea hadi Namtumbo yenye urefu wa kilomita 71.4 katika hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo leo. Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli, Watatu ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt.Servacius Likwelile, Wanne ni Mkurugenzi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Tanzania Bwana Bernard Mchomvu,Wapili kulia ni mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa na kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za Milenia Bwana Karl Fickenscher.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Balozi Mdogo wa Japan Bwana Kazuyoshi Matsunaga(katikati) na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika(African Development Bank) ADB Bibi Tonia Kondiero kulia wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua rasmi ujenzi wa Barabara ya Lami ya Namtumbo- Matemanga  yenye urefu wa kilomita 128.9 uliofanyika katika kijiji cha Migelegele .Wapili kushoto ni Waziri wa Ujenzi Dkt.John Pombe Magufuli na watatu kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete.Barabara hiyo inajengwa na serikali ya Tanzania ikisaidiwa na fedha kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika na serikali ya Japan kupitia shirika lake la misaada la JICA.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na mbunge wa Namtumbo Vita Kawawa wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa hospitali mpya ya wilaya ya Namtumbo Mkoani Ruvuma uliofanyika jana.Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Saidi Mwambungu.D92A7678
   Dkt.Jakaya Kikwete na Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge Corporation Bwana Karl Fickensher wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi Kuzindua Barabara ya Lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa msaada wa Watu wa Marekani kupitia mfuko huo wakati wa hafla iliyofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo leo.
  D92A7684 
  Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Mkurugenzi Mkazi wa Mfuko wa Changamoto za millennia(Millenium Challenge Corporation Bwana Karl Fickensher wakati wa uzinduzi wa Barabara ya lami ya Songea-Namtumbo yenye urefu wa kilometa 71.4 iliyojengwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na msaada kutoka kwa watu wa Marekani kupitia mfuko huo katika sherhe zilizofanyika katika kijiji cha Migelegele wilayani Namtumbo Mkoani Ruvuma leo. Picha na Freddy Maro

  0 0

  Mdau Ruger  Kahwa ambaye ni mkuu wa ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia  uratibu wa majanga na misaada ya kibinadamu  nchini Papua New Guinea  akitia saini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa Malyasia  nchini Papua New Guinea kufuatia kutunguliwa  ndege ya nchi hiyo na kuua abiria wote nchini Ukraine.  

older | 1 | .... | 512 | 513 | (Page 514) | 515 | 516 | .... | 3283 | newer