Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 508 | 509 | (Page 510) | 511 | 512 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0


  Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Julai 17, 2014 kuelezea msimamo wa JUKWAA LA KATIBA juu ya mwenendo uliopita wa bunge hilo. Picha na Cathert Kajuna wa Kajunason Blog

  Kiongozi wa Shule Kuu ya Sheria nchini Kenya, Profesa Patrick Lumumba alisisitiza suala la wanasiasa kurudi bungeni na kuhakikisha katiba mpya inapatikana.

  Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano huo.

  Wajumbe wa JUKWAA LA KATIBA wakisisitiza jambo.
  Na Hellen Kwavava, Dar es Salaam.
  Ushauri Umetolewa kwa Wajumbe wa Bunge Maalum la katiba kuwa na Mtazamo mpya utakaoiletea nchi maslahi pindi watakaporudi bungeni katika mchakato wakutafuta katiba mpya unaotarajiwa kuanza mapema mwezi ujao.
  Hata hivyo kundi la Umoja wa katiba ya wananchi (UKAWA) limezidi kushauri wakirudi bungeni na kuendelea na majadiliano kwa msingi wa rasimu ya katiba.
  Hayo yamesemwa jijini Dar es Salaam leo Julai 17, 2014 na mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba, Bw. Deus Kibamba ambapo ameeleza kwamba wabunge wanatakiwa kuachana na mtazamo wa kisiasa pamoja na lugha zisizo na staa kwenye bunge hilo kwani wanatakiwa kuzingatia uzalendo kwanza.
  Aidha Bw. Kibamba amesema kwamba licha ya muda kuwa mfupi kuelekea katika uchaguzi wa mwaka 2015 wao wanapendekeza juhudi zaidi zifanyike ili kukamilisha upatikanaji wa katiba hiyo.
  Naye Kiongozi wa shule kuu ya Sheria nchini Kenya Profesa Patrick Lumumba amewasihi wanasiasa wa nchini kuhakikisha katiba inapatikana kutokana na matakwa ya wananchi kwani nchini jirani zimekuwa zikiiga mambo mengi kutoka huku.
  Bunge Maalum la katiba linatajiwa kuanza tena Agosti 5, 2014 mwaka huu.


  0 0

  Hongera sana Mr. President ‘Jakaya M. KIKWETE’ 

  “I am Moved”, sababu nikirudi nyuma kidogo katika historia ya nchi ya Tanzania mwanzoni mwa miaka ya 90 wakati sanaa ya muziki wa kizazi kipya ilipoanza kuchipuka ikifuatiwa na vita kubwa dhidi ya kukemea kijana kuwa msanii waHIP HOP nchini na sanaa hii kupewa majina ya kutisha kama muziki wa “kufoka foka, kihuni”na sanaa hii haikukubalika kabisa katika jamii ya kitanzania.
  Binafsi naweza nikasema kipindi cha awamu ya 4 ya uongozi wa serikali ya Tanzania kupitia Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ‘Dk. Jakaya Mrisho Kikwete’ ndio wakati pekee ambapo wasanii na sanaa ya kitanzania inaweza kujivunia sana. 
  Kwanza kabisa naweza kudiliki kusema ndio wakati pekee wasanii wa nchini wameweza kutembelea IKULU ya Tanzania kuliko vipindi vyote vilivyopita na pia kuwa ni kiongozi ambae amekua na ukaribu wa hali ya juu na wasanii wa nchini. Hata mimi binafsi ambae sijawahi kupata nafasi ya kuingia IKULU, natamani ningekua msanii kipindi hichi ili niweze kupata nafasi ya kuwa na ukaribu na Rais wa nchi yangu na naamini inaleta msukumo mkubwa sana kwa vijana ambao wanafanya sanaa nchini Tanzania kwa sasa.

  0 0


  0 0

   KATIKA KUELEKEA MSIMU WA SIKUKUU YA EID EL FITR NA KUHAKIKISHA KWAMBA WATU WANATOKA NA PAMBA KALI NA ZA KISAWASA,DUKA LAKO PENDWA LENYE VIWALO VYA NGUVU NA VYA KISASA JIJI LA DAR ES SALAAM LINALOFAHAMIKA KAMA J&M VIRGO,LIMESHUSHA MALI MPYA NA ZA UHAKIKA KABISA KWAKO WEWE MTANZANIA.

  HIVYO FIKA DUKANI KWAO PALE MIKOCHENI KWA WARIOBA,JENGO LA C&G PLAZA GHOROFA YA KWANZA ILI UWEZE KUJIPATIA VITUZZ NA VIWALO VYA KIJANJA,POCHI BABKUBWA,MOKA ZA KISASA NA MICHUCHUMIO YA HAJA KWA KINA DADA.

  KWA TAARIFA ZAIDI TEMBELEA LIBENEKE LAO

   KIVAZI CHA KINA DADA
   KOBAZI MATATA KABISA KWA KINA BABA
   MTOKO WA KIOFISINI.
  MOKA YA NGOZI YA CHATU NA MKANDA WAKE.

  0 0

  IMG_3297
   Mkurugenzi wa Tan Communication Media  inayo miliki kituo cha  Radio 5 chenye makao yake makuu jijini Arusha  Bw Robert Francis wakati akiwa na wageni wake waalikwa mbalimbali wakipata iftari ya pamoja kwenye hafla hiyo,hafla iliyofanyika katika studio za redio hiyo zilizopo Njiro jijiniArusha iliyohudhuriwa na Viongozi wa dini na wadau wengine.IMG_3270
  Sheikh Mkuu wa Bakwata mkoa wa Arusha,Shaaban Juma aliyekuwa mgeni rasmi katika halfa hiyo iliyoandaliwa na kampuni ya Tan Communication Media.IMG_3278
  Mbunge wa Arusha Godbless Lema  wa pili kutoka  kushoto naye alihudhuria halfa hiyo.IMG_3325
  Mchekeshaji  kutoka nchini kenya Peter Sankale maarufu kama “Olexander Jospat”katika igizo la VIOJA MAHAKAMANI akitoa burudani baada ya Futari.PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

  0 0

  Na Mwandishi Maalum, New York
   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Bw. Said Djinnit wa Algeria kuwa Mjumbe wake maalum atakaye shughulikia Eneo la Maziwa Makuu. 
  Bwana Djinnit anachukua nafasi ya Bi. Mary Robinson wa Ireland, ambaye mapema wiki alimtangaza kumteua kuwa Mjumbe wake Maalum kuhusu mabadiliko ya tabia nchi ( Climate Change) 
   Akitangaza uteuzi huo Ban Ki Moon, amemuelezea Bw, Djinnit kama mtu mwenye uzoefu mkubwa na ambaye amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya Umoja wa Mataifa na katika Umoja wa Afrika. Na kwamba kutokana na uzoefu wake anamtarajia kutoa mchango mkubwa katika mchakato wa utafutaji wa Amani ya kudumu katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. 
  Kuanzia mwaka 2008 hadi hivi karibuni, Bwana Djinnit amekuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Msimamizi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi. Pia amehudumu kama Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Katibu Mkuu nchini Nigeria,akisaidia juhudi za kupambana na Boko Haram. 
  Djinnit ana uzeofu mkubwa katika masuala ya diplomasia, akiwa amewahi kuhudumu kama Kamishna wa kwanza wa Organi ya Usalama na Amani ya Umoja wa Afrika ( AU) na kabla ya kuzaliwa upya kwa AU, aliwahi Katibu Mkuu Msaidizi wa Masuala ya Siasa katika OAU ( Organization of African Union) 
  Wakati huo huo Katibu Mkuu pia amewateua Bw. Staffan de Mistura kuwa Mwakilishi wake Mpya kuhusu Syria atasaidiana na pia amemteua Bw. Ramzy Ezzeldin Ramzy kama makamu wake. 
   Bw. Staffan de Mistura anachukua nafasi ya Mwanadilomasia mzoefu na anayeheshimika Bw. Lakhder Brahimi aliyejiuzuru mwezi mei mwaka huu. Bw, Staffad de Mistura anakuwa Mwakilishi wa tatu kuteuliwa kushughulikia mgogoro wa Syria, wa kwanza alikuwa ni aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Kofi Annan ambaye naye alijiuzuru.
    Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  Ban Ki Moon akiwa  Bw. Said Djinnit wa Algeriaambaye amemtangaza kuwa  Mjumbe wake Maalum   atakayeshughulikia Eneo la Maziwa Makuu. Bw. Djinnit anachuka  nafasi ya  Bi. Mary Robinson wa Ireland ambaye hivi karibuni   Katibu Mkuu amemteua kuwa mjumbe wake katika masuala ya mabadiliko ya Tabia nchi
  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa  akiwa  katika picha ya pamoja wa Wawakilishi wake ambao amewateua kushughulikia mgogoro wa Syria kushoto kwa  Katibu Mkuu ni  Bw.   Staffan de Mistura   na kulia kwa Katibu Mkuu ni  Bw. Ramzy Ezzeldin Ramzy  ambaye  ni  Makamu wa Bw. Mistura. Bw. Staffan de Mistura anachukua nafasi iliyoachwa na Bw.  Lakhder Brahimi aliyejiuzuru mwezi  Mei

  0 0

   Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, akifungua mkutano wa siku moja wa  Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa ambapo siku nzima ya Alhamisi liLIjadili  ajenda ya uwekezaji kwa Afrika  na  mchango wake kwa Maendeleo endelevu. Katika hotuba yake,  Ban Ki Moon alisema  Afrika isiridhike na ukuaji  wa jumla wa uchumi wake ambao umekuwa ni mzuri bali inahitaji kuwekeza zaidi  ili uwekezaji huo uweze kuchangia katika kuleta maendeleo endelevu,  kuwaondolea  watu wake umaskini, kukuza ajira na kipato na  kwamba Afrika ilihitaji kuwekeza zaidi katika miundombinu,  kilimo na nishati endelevu pamoja na mambo mengine.

  Muwakilishi wa Kudumu wa  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Tuvako  Manongi akizungumza wakati wa mkutano kuhusu uwekezaji katika Afrika.  Katika mchango wake, alisisitiza kuwa  pamoja na Afrika kuchagizwa kuvutia uwekezaji zaidi pamoja na ukusanyaji wa mapato ya  ndani   Jumuiya ya kimataifa  inatakiwa kutoa ushirikiano  usio na shaka katika udhibiti wa ukwepaji mkubwa wa kodi, utoroshwaji  na biashara harafu ya fedha  na ambayo  inazinyima nchi za Afrika mapato ambayo yangeweza kutumika katika  utekelezaji wa miradi mbalimbali  ya maendeleo na hivyo kuwaondoelea  wananchi wake  umaskini  uliokithiri.

  0 0

  1A
  Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza na uongozi wa polisi Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kipolisi ya Chalinze pamoja na wananchi waliojitokeza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwa jeshi hilo zikiwemo kompyuta, mifuko ya Saruji pamoja na fedha vilivyotolewa na mbunge huyo, Kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya ulizni na usalama wa raia na mali zao. Pamoja na kukabidhi kompyuta hizo zitakazosaidia katika utunzaji wa kumbukumbu pia mbunge huyo ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi vya Mbwewe na Kiwangwa ambavyo thamani inafikia zaidi ya shilingi milioni 11, Kushoto kwake ni Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jana kwenye kituo kikuu cha polisi Chalinze.
  1
  Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Kamanda ACP Ulrich Onesphory Matei zilizokabidhiwa na mbunge huyo kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo jimbo la Chalinze katikati ni Mkuu wa kituo cha polisi Chalinze Afande J. S. Magomi.
  2
  Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua ili kuonyesha kompyuta hizo huku viongozi wa jeshi hilo mkoani Pwani na jimbo la Chalinze wakishiriki shghuli hiyo.
  3
  Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimuonyesha moja ya kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei.

  0 0


  0 0

   Timu ya Tanzania kwenye Michezo ya Jumuiya ya Madola imewasili katika  uwanja wa ndege wa Kimataifa Glasgow, Scotland jana usiku wa kuamkia leo kwa ndege ya Shirika la ndege la Falme za Kiarabu (Emirates).

   Jumla ya wanamichezo 42 waliwasili Uwanjani hapo na kupokelewa  na Afisa Ubalozi wa Tanzania London Bw. Amos Msanjila. Pamoja na mapokezi na shamrashamra za wenyeji, baadhi ya Watanzania waishio Glasgow walikuwepo Uwanjani hapo wakipeperusha bendera za Tanzania kuwahamasisha wanamichezo hao.

   Bw. Msanjila akimlaki  Nahodha wa Timu hiyo Selemani Kidunda. Katikati ni Kiongozi wa Msafara Bw. Muharami Mchume 

   Bw. Msanjila akimkabidhi bendera ya Tanzania Nahodha wa Timu hiyo Selemani Kidunda. 

  Baadhi ya Watanzania na marafiki zao waishio Glasgow walikuwepo Uwanjani hapo wakipeperusha bendera za Tanzania kuwahamasisha wanamichezo hao. 

  Michezo ya Jumuiya ya Madola inayotarajiwa kufunguliwa rasmi Jumatano (23 Julai 2014) na Malkia Elizabeth wa Pili itajumuisha nchi na Himaya 70. Michezo hiyo itafungwa tarehe 3 Agosti 2014.     


  0 0

   Balozi wa heshima Mhe. Ahmed Issa akifanya mazungumuzo na Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Lazaro Nyalandu Beverly Hills California mapama leo mazungumuzo yaliyohusu kutangaza Utalii wa Tanzana nchini Marekani pia Waziri Nyalandu alimpongeza Balozi wa Heshima kwa kuendelea kutangaza utalii wa Tanzania kwenye magari yake ya mizigo.

  0 0

  MHESHIMIWA BALOZI  WA TANZANIA NCHINI ZAMBIA MHE GRACE MUJUNA (KATI)  NA MAAFISA WAKE WAKIWA KWENYE MKUTANO WA MAANDALIZI YA MAONESHO YA TANZANIA WEEK. KUTOKEA KUSHOTO HUDDY KIANGIA (AFISA FEDHA WA UBALOZI), MR. MUNATTA (AFISA MAWASILIANO WA UBALOZI), MHE GRACE MUJUMA (BALOZI), JUSTA NYANGE (MKUU WA UTAWALA WA UBALOZI) NA RICHARD LUPEMBE (COUNSELOR WA UBALOZI)

  0 0

  Oliver Benson Israel ambaye ni mwanakwaya na sololist wa kwaya ya uinjilisti KKKT kijitonyama kwa kushirikiana na kwaya ya uinjilisti kijtonyama  anatarajia kuzindua CD yake jumapili tarehe 20/07/2014 katika kanisa la lutheran kijitonyama,dada huyu ndiye aliyeimba wimbo wa hakuna mwanaume kama yesu na nyingine nyingi, baada ya uzinduzi ibadani mchana kutakuwa na tamasha kubwa la kumwimbia mungu karibuni sana!

  0 0

  Tranforming the art of ICT, Telecom and Electrical Engineering


  iVoice Technologies Company Limited is pleased to invite participants to its technical seminar on effective Earthing, Lightning and Surge protection which is scheduled to be conducted on 14thand 15th of August 2014 at Protea Hotel  Dar es Salaam, Tanzania.

  As different researches on earthing perpetuate worldwide, an exploration for the standard, sustainable and everlasting mechanism to achieve the desirable earthing resistance value has been a challenging process. Though embraced by Tanzania and Africa as whole, the widely practiced traditional method of lowering the earthing resistance by treating the soil with salt, charcoal and water is only beneficial for short duration of time. Furthermore the corrosive nature of salt can corrode the bonding joints and ultimately increase resistance value around the area.

  In contrast to earthing, the concern in Lightning and surge protection is mainly on methodology rather than standardisation.  In Tanzania majority of Engineers use normal insulated cable to transfer lighting effect to the ground. While the insulated cable can with stand a maximum of 600 Volts before becoming a conductor, a single strike can generate thousands and hundred thousands of volts. This is evident that, the normal insulated cable can never be sufficient to be used as a down conductor.

  iVoice Technologies Company Limited envisages to bring world class technical skills to Tanzania and East African region by bringing world class experts around the world on board. We research and understand the current technical problems facing our country and through training and seminars we can build the capacity of our Engineers and technical personnel.

  This seminar will be presented by Carlos Alberto Paganini, a USA senior Facility protection expert and an experienced Electrical Engineer who has trained on lighting, earthing and surge protection in over 30 countries worldwide.  This seminar is intended to both senior and junior Electrical Engineers in Government institutions, Telecoms, Power generation, Mining, Oil/ Gas industry, Electrical Consultants and Contractors.

  The fee is US$ 450 per person. The fee covers all educational presentations, lunch and the experience-sharing seminar sessions. All other expenses such as travel, accommodation, and incidentals are the responsibility of each individual participant. Once we receive confirmation and payment, we will reserve space for the staff and provide a full programme package.                                         
  We are extremely delighted to welcome you and hoping to learn much from you as you will from us. For registration and payment details please contact number 0719903900 or email on ivoicetechltd@gmail.com.

  0 0

                                   ASSALAM  ALAIKUM

  Madrasatul  Aqsaa  Coventry  UK inapenda  kuwajulisha kuwa  tumeandaa chakula cha  pamoja siku  ya  Eid Mosi kama  ifuatavyo:

  Kiwango £6 kwa  watu  wazima na £4 kwa  watoto

  Pahala: Muslim Resource  centre

                 Red Lane, Coventry CV6 5EE

  Tunapokea  majina  na  mwisho  ni Jumatatu  Tareh 21/7/2014

  Kumbukeni  kwamba  tutaswali  sala ya  Eid  pale  pale  Muslim  Resource  Center.Darasa zentu  zinaendelea  LIVE  kama  kawaida  www.madrasatulaqsa.com.

  Halikadhalika Karibu  Mihadhara  yetu  kila  juma  pili kuanzia  Saa moja jioni.Tunaomba  kila  mmoja  aje  na  Iftaar ili  apate  fadhila  za  kumfuturisha Muislam mwengine.

  Kwa Taarifa  Zaidi wasilian  na :

  Simu :07767241499,07717724094

  www.madrasatulaqsa.com


  Wabillah  Tawfiq


  0 0


  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo pinda akizungumza na Balozi wa Tanzania nchini Russia, Luteni Jenerali Wynjones Mathew Kisamba ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam leo  Julai 18, 2014 kuaga. 
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

  0 0

   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (mwenye shati la drafti) akipiga picha maji yanayopita kwenye mto Kibandu kutoka kiwanda cha NIDA Textile Mills Ltd.Kulia ni Diwani wa Kata ya Kigogo Richard Chengula.
   Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.  Binilith Mahenge (kulia) akipiga picha bomba linalotiririsha maji machafu kutoka kiwanda cha NIDA kilichopo Kigogo Mkuyuni jijini Dar es Salaam, 
   Bomba linalotiririsha maji machafu kutoka kiwanda cha NIDA kilichopo Kigogo Mkuyuni jijini Dar es Salaam, 
  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (katikati) akiongozwa na Meneja Mkuu wa NIDA Textile Mills Ltd Imran Lohya kupanda kwenye tenki la maji yanayutumika na kiwanda hicho.

  0 0

   Mkuu wa mkoa wa Mtwara Mhe Joseph Simbakalia akimkaribisha Waziri wa Nishati na Madini pamoja na ujumbe alioambatana nao akiwemo balozi wa China nchini Bw…. Mara baada ya kufika ofisini kwake kuelezea uwepo wapo katika mkoa huo

   Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mhe John Simbakalia  akimweleza Waziri wa Nishati na Madini jambo linalohusu sekta ya umeme ambapo Prof. Muhongo anaisimamia ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
   Mkandarasi anayehusika na usambazaji wa umeme vijijini Bwana  Luta (mwenye shati nyeupe), mara baada ya kusimamishwa na Waziri wa Nishati na Madini Prof Muhongo ili kuelezea maendeleo aliyoyafikia katika kukamilisha mradi huo kulia kwake ni Mkurugenziwa Huduma za Ufundi (REA) Injinia Bengiel H. Msofe.

   Prof Muhongo na balozi wa China wakikgua mtambo wa kuchujia maji uliopo katika maeneo ya makazi ya watumishi ambao utawasaidia wananchi wanaozunguka eneo hilo kupata huduma ya maji safi na salama. 
   Waziri wa Nishati na Madini na ujumbe wake wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba za kuishi watumishi wa mtambo wa kufua gesi lililopo katika eneo la Madimba Mkoani Mtwara
  Baadhi ya nyumba zitakazotumika kwa kuishi watumishi wa eneo la kuchakata gesi Madimba ni nyumba za kisasa zilizojegwa kwa ubora mkubwa sana kama zinavyoonekana.
  --------------------------
  Waziri wa Nishati na Madini Prof Sospeter Muhongo akiambatana na Balozi wa China nchini Dk. Lu Youging wamefanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi linalotarajiwa kuleta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kwa watanzania na hivyo kuchangia kuiingiza nchi kati ya nchi zenye uchumi wa kati ifikapo 2025.

  Akizungumza na waandishi wa habari balozi alisema ziara za kukagua bomba la gesi zinalenga katika kuhakikisha kazi inayofanyika ni bora na ipo katika viwango vinavyotakiwa na kuifanya nchi yake kuwa sehemu ya mradi na maendeleo ya nchi.

  Kwa upande wake Prof. Muhongo amefurahishwa na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo na kukiri kuwa kila mara afanyapo ziara kwenye miradi hiyo anakuta mabadiliko makubwa yanayomfanya kufurahia juhudi ya wakandarasi itakayopelekea mradi kukamilika kwa wakati uliopagwa mezi desemba 2014.

  “Jamani ni nani walikuwepo tulipokuwa tukikabidhiwa eneo hili kwa ajili ya kuanza mradi? Eneo hili lilijaa mikorosho tu, lakini sasa tunaona kazi kubwa ya ujenzi iliyofanywa na wakandarasi hawa.

  Aidha Muhongo alipotakiwa kueleza manufaa watakayoyapata wananchi wa Lindi na Mtwara alishangaa kuona kuwa bado watu hawaoni manufaa hayo na kuwaeleza waandishi wa habari kutosubiri yeye ndio aseme wakati wao wenyewe wanashuhudia wananchi wakipata ajira, huduma za jamii zikiboreka, wakipewa kipaumbele katika masuala ya elimu.

  Hata hivyo Muhongo amewaeleza wanamtwara kuwa wasitegemee manufaa ya kuwepo kwa rasilimali ya gesi ni kuwagawia pesa aidha wanatakiwa kujiendeleza kielimu na kutumia fursa zinazojitokeza ikiwa ni pamoja na ufadhili wa masomo vilivyo ili waweze kujikwamua kimaisha na kushiriki katika kunufaika na gesi iliyogunduliwa katika eneo lao.

  Akizungumzia suala la kukamilika kwa mradi huo msimamizi wa ujenzi wa bomba hilo Injinia Balthazar Mrosso alisema limekamilika kwa asilimia 70 na maeneo yaliyosalia ni yale yanayohitaji umakini mkubwa ikiwa ni pamoja na maeneo yanayoathiriwa na mafuriko pembezoni mwa mto wa Ruvu ambako kazi ya kuchimba mashimo ili kufukia mabomba hayo inaendelea, maeneo yenye miinuko na madaraja.

  Akielezea suala la kukamilika kwa miradi ya kusambaza umeme vijijini Prof. Muhongo amesema miradi yote nchini inatakiwa kukamilika ifikapo juni 2015 na kuagiza mkandarasi asiye na uwezo wa kufanya hivyo kurudisha mradi huo apewe mtu mwenye uwezo.


  Muhongo alimtaka mkandarasi Luta kuelezea hatua aliyofikia katika kusambaza umeme huo katika mkoa wa Mtwara ambapo alieleza kuwa suala la kusafisha mkuza limekamilika pamoja na kusambazwa na kusimikwa kwa nguzo kwa eneo Fulani. Aidha Mkandarasi Luta alimhakikishia Profesa Muhongo kuwa mradi huo utakamilika kwa wakati.

  Akitanabaisha nia ya dhati ya kuhakikisha miradi inakamilika kwa wakati Muhongo alisema kuanzia mwezi huu hadi mwezi Oktoba atakagua miradi yote ya REA II na kwa wakandarasi watakaoonesha kutoridhisha kupokonywa miradi. “Hatutasubiri kufika mwezi juni ndipo tuanze kufukuzana na kukamilika kwa miradi mpaka desemba wakandarasi watakaoonesha kuzubaa watapokonywa na kupewa mtu mwingine awe mzawa au mgeni” alisisitiza Muhongo.


  Tangia kuanza kutekelezwa kwa mradi huo mkubwa wa Bomba la gesi hii ni mara ya tatu kwa profesa Muhongo kuzungukia maeneo hayo kujionea jinsi kazi inavyofanyika na kukiri kufurahishwa na kasi ya wakandarasi hao.older | 1 | .... | 508 | 509 | (Page 510) | 511 | 512 | .... | 3272 | newer