Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 507 | 508 | (Page 509) | 510 | 511 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Jumuia ya watanzania Sweden inawakaribisha WaTanzania wote waishio nchini Sweden na nchi za skandinavia kuhudhuria kwenye Sherehe za TANZANIA DAY 2014 .

  Sherehe itafanyika Stockholm  tarehe 27th Sept 2014 kufanyika katika Ukumbi utakua wa Bergshamra: Adress ni Bergshamra Skola, Hjortstigen 1, Bergshamra, Solna.
  Kuanzia saa 15:00 jioni mpaka saa 03:00 Usiku. Kutakuwa na Nyama choma itayoambatana na viburudishi mbalimbali kuanzia 15:00 jioni mpaka saa 20:00 usiku.

  Saa 20:00 mpaka 03:00 usiku Dj atatumbuiza kwa miondoko ya Bongo flava RNB ,Ragga ,Hip Hop na vionjo vingine vingi vya mziki unaotamba kwa sasa Duniani.

  Lengo ni kuimarisha jumuia yetu ya yenye makao Makuu kwenye jiji la Stockholm .
  Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi

  0 0

  Mimi Reppyson Ishababaki na mke wangu Elida Fundi. Tunapenda kutoa taarifa ya kupotea kwa mtoto wetu kipenzi Meryline Reppyson. Ameibiwa jana jioni na mtu tusiyemfahamu na hatujampata mpaka sasa hivi.

   Tunawaomba Watanzania na watu wote mtusaidie kumtafuta mtoto wetu. Maneno yanayosemwa kwamba kachukuliwa na baba yake si ya kweli kwani mimi ndiye baba yake mzazi na tunaishi pamoja na mke wangu. 

  Asanteni sana kwa msaada wenu na Mungu awabariki.

  0 0

  VITABU VIMEZINDULIWA ZANZIBAR TAREHE 14.7.2014.  NI VITABU VYAKE VYA KWANZA KUVITUNGA,KITABU CHA "MAMU NA MUNA" (KWA WATOTO) NA "MBONA KINYUME" (KWA WATU WAZIMA). MTUNZI NI BI.  MWANAMKAA ABDULRAHAMAN AMBAYE NI MWANASHERIA NA MRAJIS WA ARDHI ZANZIBAR
   Mwalimu mkuu chuo cha kiislamu Zanzibar shekh Muhidin Ahmed ambae ni mgeni rasmi akizindua vitabu hivyo
  Bi. Mwanamkaa Abdulrahman akielezea muhtasari kuhusu vitabu vyake
  Mwalimu mkuu chuo cha kiislamu Zanzibar shekh Muhidin Ahmed akisifia vitabu hivyo
  Wananchi wakinunuwa vitabu hivyo.

  0 0

   Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania akibadilishana mawazo na Viongozi wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Uganda mapema Leo a alipotembelea ofisini kwa Mhe. Jaji Mkuu, wa pili kulia ni Mhe. Jaji James Ogoola, Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wa Uganda, wa tatu kulia ni Mhe. Jaji Dk. Esther Kisaakye ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Uganda, wa kwanza kushoto ni Mhe. Jaji Edward Rutakangwa, Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Tanzania.
   Wajumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Uganda pamoja na Tanzania wakibadilishana uzoefu jinsi ya kufanya kazi mapema Leo
  Mhe. Mohamed Chande Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama ya Tanzania (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe ya Tume ya Utumishi ya Mahakama ya Tanzania na Uganda mapema Leo baada ya kubadilishana uzoefu juu ya utendaji kazi wa Tume hizi. Ujumbe wa Tume ya Utumishi wa Mahakama wa Uganda upo nchini kwa Siku mbili lengo likiwa ni kuja kupata uzoefu jinsi gani Tume ya Utumishi wa Mahakama inafanya kazi. Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania

  0 0  0 0

   Jaji Mfawidhi  Mhe. SS Kihiyo (mwenye suti ya kijivu)  na ujumbe wake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukagua Magereza ya Mkuza, Kibaha, akiwa  katika ziara yake mkoa wa pwani .
  Jaji mfawidhi Mhe. SS Kihiyo na ujumbe wake wakiwa mbele ya jengo la Mahakama ya Mwanzo Kibaha Maili Moja ambako ametoa agizo kuwa shughuli za mahakama zitahamia mahakama yenye nafasi  kwani jengo hilo halifai kwa matumizi.
  Jaji Mfawidhi  Mhe. SS Kihiyo akiongea na watumishi katika ziara yake Mkoa wa Pwani.

  0 0


  0 0


  0 0


  0 0

  Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akizungumza wakati wa mdahalo wa viongozi wadogo wanaoshiriki programu ya rais Obama kwa viongozi wadogo wanaoonyesha dira .Mdahalo huo umefanyika katika chuo kikuu cha Arkansas ambacho Rais Mstaafu wa Marekani  Bill Clinton na mkewe Hillary walianzia kazi ya kufundisha Sheria.
  Baadhi ya washiriki katika mdahalo huo ambamo miongoni mwa waalikwa walikuwa ni watanzania waishio Arkansas.
  Mkurugenzi wa program ya Rais Obama ya "Young African Leaders initiative "(YALI) Dr, Leyah akizungumza katika mdahalo huo uliobeba kichwa cha "BRINGNG THE GAP BETWEEN THE DIASPORA AND OUR HOME COUNTRIES".
  Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akizungumza muda mfupi baada ya kutembelea makao makuu ya shirika la Heifer International ambalo limetoa ahadi ya kuendelea kusaidia jamii hususani katika elimu na mitaji huku likitoa mradi wa Ng'ombe wa maziwa kutoka kwa jimbo la Arumeru Masharik


  Mbunge jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nssari akila pozi la picha na mratibu wa kijiji cha Heifer ,Bi Hellen Brown .
  Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari pia alipata nafasi ya kushiriki mahojiano juu "vijana na mustakabali wa Afrika"katika kituo cha Luninga cha Umma kinachojulikana kama Fayetteville Public  Access Television.shoto ni mwandishi wa kituo hicho Dan,Prof Mitiku toka chuo kikuu cha Makelle nchini Ethiopia,wote hawa wanashiriki program ya Rais Obama ya viongozi wadogo wa kiafrika katika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani.
  Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari akiwa na mshiriki mwenzake katika programu ya rais Obama ya viongozi wadogo wa kiafrika inayofanyika katika chuo kikuu cha Arkansas nchini Marekani ,Bi Clara toka nchini Nigeria ambaye pia ni balozi wa UN Charter nchini Nigeria.

  0 0
  0 0

  Watch below posts for samples.
  Interested?  Email us via issamichuzi@gmail.com

  0 0

  Na Sultani Kipingo
  Kocha mpya wa Manchester United Louis van Gaal ameongea na wanahabari kwa mara ya kwanza leo, akisema kuwa klabu hicho cha Old Trafford ni kikubwa duniani isipokuwa inabidi wajipeleleze upya kufuatia kuboronga katika msimu uliopita.

  "Msimu uliopita mmemaliza ligi mkiwa nafasi ya saba kwa hiyo nyie sio klabu kubwa duniani. Mnahitaji kujidhihirisha wenyewe, ingawa dunia nzima wanazungumzia Manchester United - hiyo ndio tofauti", alisema.

  "Hii ni changamoto kubwa na ndio maana nikachagua klabu hii. Nimefundisha Barcelona, Ajax na Bayern Munich ambazo zote ni namba moja nchini kwao. Sasa niko Manchester United ambayo ni namba Moja England.
  "Sijawahi kufanya kazi katika ligi kuu ya England na hilo ni changamoto nene. Nilipofanya kazi Barcelona, ilikuwa ligi bora. Nilipofanuya kazi Germany,nako ilikuwa ligi bora. Sasa nafanya kazi hapa penginepo hii ndiyo ligi bora.


  0 0

  It makes it easy for everyone to quickly search and find what they are looking for - all in one place.
  Our mission is to connect people, provide information, creating a community of equal members, which can transfer ideas, use different channels to advertise their small and big businesses, offer their services or products and search for anything they want.

  Tupomoja is super easy to use! We have many different channels to bring people together and interact with them directly and offer personal service:
  Website, SMS, Tupomoja Magazine, email and facebook.

  Regarding the 38th DITF and Mr. Costa Siboka 
  Our Team was present at the Saba Saba Fair to offer our services personally to the customers, visitors and exhibitors of the event. 
  We had many official and popular visitors, one of them Mr. Costa Siboka (pictured above right) who created a Listing of his music group on the Tupomoja website: 
  Listings are the basic entries on our website, where people can describe what they offer or look for and where pictures are displayed. 
  Other visitors at our stall were the 2nd Vice President of Zanzibar, the First Lady and the President of Tanzania, Mr. Kikwete.  
  Regarding the Tupomoja Magazine: 
  Every issue of the Tupomoja Magazine will bring you the latest listings to connect you with other people in our community quickly and easily. We will present you inspiring business ideas. We will talk about problems, difficulties but also solutions in people’s everyday life. We will discuss meaningful topics from health and relationships to politics and education.   0 0


  0 0

  Baadhi ya watuhumiwa wanaodaiwa kujihusisha na vitendo vya ugaidi katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakisindikizwa na askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kuingia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Julai 17,2014 kusomewa mashitaka yao. Watuhumiwa 16 walisomewa mashitaka.PICHA NA PHILEMON SOLOMON  
  Askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakiimarisha ulinzi.
  Watuhumiwa wakiingia ndani Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
  Watuhumiwa wakipelekwa maabusu baada yakusomewa mashitaka yao.


  Na Mwene Said wa Blogu ya Jamii 
   WAKAZI wa jijini Dar es Salaam 16 leo wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na kesi mbili tofauti ikiwemo ikiwemo kula njama na kusaidia wenzao kufanya ugaidi sehemu mbalimbali Tanzania na kutumia mtandao wa Fesibuku kupata mbinu za kutengeza mabomu ya kwenda kufanya ugaidi nchini Kenya. 
  Katika kesi ya kwanza washtakiwa hao ni, Nassor Abdallah, Hassan Suleimani, Anthari Ahmed, Mohamed Yusuph, Abdallah Hassan maarufu kama Jibaba, Hussein Ally, Juma Juma, Said Ally, Hamis Salum, Said Salum, Abubakar Mngodo, Salum Salum, Salum Amour, Alawi Amir, Rashid Nyange ama Mapala na Amir Juma. 
  Mashtaka hayo yalisomwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa wa mahakama hiyo. Upande wa Jamhuri uliongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Prosper Mwangamila akisaidiana na Mawakili wa Serikali, George Barasa, Mwanaamina Kombakono na Brenda Nick. 
  Barasa alidai kuwa katika tarehe tofauti kati ya mwaka 2013 na mwaka huu sehemu mbalimbali nchini Tanzania, washtakiwa walikula njama ya kutenda kosa la kusaidia kufanyika ugaidi. Ilidaiwa katika shitaka la pili, kati ya Januari mwaka 2013 na June mwaka huu sehemu mbalimbali Tanzania, washtakiwa wote kwa pamoja waliwasaidia Sadick Absaloum na Farah Omary kufanya ugaidi kinyume cha sheria. 
  Hakimu Riwa alisema kesi hiyo itatajwa Julai 23, mwaka huu na washtakiwa wataendelea kukaa mahabusu. Katika kesi ya pili, mshtakiwa ni, Jihad Swalehe anakabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo kula njama na kufanya mawasiliano kupitia mtandao wa kijamii Facebook ya kupata mbinu za kufanya ugaidi nchini Kenya. Nick alidai kuwa siku na mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alikuwa na njama ya kutenda kosa la kigaidi. 
  Upande huo wa Jamhuri ulidai kuwa kati ya Machi 21, mwaka 2013 na Juni 2, mwaka huu mahali pasipofahamika kupitia mtandao wa Facebook, mshtakiwa alifanya mawasiliano na Nero Saraiva na wengine kumsaidia namna ya kutega mabomu nchini Kenya kwa lengo la kuwasababishia kupoteza maisha na majeraha wananchi wa nchi hiyo. 
  Washtakiwa wote kwa nyakati tofauti hawakutakiwa kujibu chochote kutokana na mahakama hiyo kutokuwa na mamlaka ya kusikiliza kesi hizo hadi upelelezi utakapokamilika itahamishiwa Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam. 
   Mapema leo katika viunga vya Mahakama ya Kisutu, washtakiwa hao walifikishwa wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari kanzu wenye bunduki na Kikosi Maalum cha kutuliza ghasia (FFU) waliokuwa na silaha pamoja na mabomu. 
  Hali ilikuwa tulivu huku askari hao wakiimarisha ulinzi kila kona ya viunga hivyo jana saa 6:05 mchana mara tu baada ya washtakiwa hao kufikishwa mahakamani hapo. mwisho

  0 0


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi nyumba zilizojengwa na Shirika la Nyumba la Taifa NHC huko Mkuzo, wilayani Songea mjini mkoani Ruvuma leo. Kutoka kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete, Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi Prof.Anna Tibaijuka, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa Bwana David Misonge Shambwe, na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Bwana Said Mwambungu.
  Ris Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunua jiwe la msingi wakati wa ufunguzi wa nyumba zilizojengwa kwa gharama nafuu na Shirika la Nyumba la Taifa(NHC) huko Mkuzo wilayani Songea mjini Mkoani Ruvuma leo.Kushoto ni kaimu Mkurugenzi wa NHC Bwana David Misonge Shambwe na wwapili kushoto ni Waziri wa Ardhi Nyumba na makazi Prof.Anna Tibaijuka.
  Picha na Freddy Maro. Picha zaidi BOFYA HAPA
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akipanda mti wa kumbukumbu wakati wa ufunguzi  rasmi wa ofisi za taasisi ya kuzuia rushwa TAKUKURU mkoa mjini Songea leo.Kushoto ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete na kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU Bibi Mary Mosha.

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jingo la ofisi ya TAKUKURU mkoa wa Ruvuma leo mjini Songea.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na kaimu Mkurugenzi mkuu wa TAKUKURU Bibi Mary Mosha wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi wakati wa ufunguzi wa jingo la ofisi za TAKUKURU Mkoa wa Ruvuma leo.Rais Kikwete yupo katika ziara ya kikazi  ya wiki moja mkoani Ruvuma 


  0 0

   The video was done in South Africa by Director Kyle White,It also features Tanzanian model Daxx, Tandi model from South Africa and Lexi who participated in the Big brother South Africa.
  Lexi ,Feza and Tandi on Location -Northcliff JB
  Feza being made up on Location JAB GYM, Johannesburg
  South African Police at the airport they are just Fans

  0 0


older | 1 | .... | 507 | 508 | (Page 509) | 510 | 511 | .... | 3285 | newer