Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 505 | 506 | (Page 507) | 508 | 509 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa GEPF,Bw Aloyce Ntukamazina akiwasilisha mada juu ya uchangiaji wa hiari katika mpango wa VSRS,wakati wa Semina iliyofanyika mwishoni mwa wiki mkoani Mtwara.
  Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa GEPF,Bw Aloyce Ntukamazina akimkabidhi kadi ya uanachama wa hiari,Bi Grace Hokka ambaye ni Mhariri kutoka kampuni ya New Habari huku akifurahia kujiunga rasmi katika mpango wa hiari wa GEPF
  Meneja Masoko na Huduma kwa Wateja wa Mfuko wa GEPF,Bw Aloyce Ntukamazina akimkabidhi na kumkaribisha rasmi Bw Martin Kuhanga kujiunga na wenzake katika Mfuko huku akishuhudiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Bw Absalom Kibanda (kulia).
  Bw Abdalah Majura akipokea rasmi kadi yake ya uanachama baada ya kuelewa umuhimu wa kujiwekea akiba ukiwa bado kazini.
  Katibu Mkuu wa jukwaa la wahariri,Bw Nevile Meena akikabidhiwa kadi ya uanachama baada ya kujiunga rasmi na Mfuko wa GEPF.

  0 0

  Mitumba Bei Rahisi,Jumla na Rejareja Tanzania
  Mwezi mtukufu wa Ramadhan, umebakiza takribani majuma mawili tu. Kwa maana hiyo, maandalizi ya sikukuu ya Eid-El-Fitri tayari yameshaanza. Eid huwa ni wakati wa furaha na mara nyingi huenda sambamba na kujumuika na ndugu,jamaa na marafiki kufurahi na kutukuza yale yote aliyotujalia Mwenyezi Mungu. 

   Palipo na mkusanyiko wa watu, huwa pia pana "mtoko". Kila binadamu hupenda kupendeza. Wenzetu wa jinsia ya kike,hupenda sio tu kupendeza bali pia kusifiwa kwamba "wamependeza". Kupendeza, kwa bahati mbaya, hakutokei kama ajali. Kunahitaji maandalizi. Sharti manunuzi yafanyike. Ili nisije onekana mwenye choyo, napenda kukushirikisha katika hili. 

  Kuna punguzo maalumu kabisa kuelekea sikukuu ya Eid-El-Fitri. Punguzo la nini? Tizama hapa chini. Soma.Usiache kumwambia na mwenzio.

  0 0

  DSC_0008
  Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, (kulia) akisalimiana na Mtendaji wa Kata ya Mnyuzi, Bw. Gosbert Ishengoma mara baada ya kuwasili kwenye ofisi za kata hiyo wilayani Korogwe. Katikati ni Afisa Usafi na Mazingira wa Wilaya ya Korogwe, Bw. Frederick Linga.

  Na Mwandishi wetu, Korogwe
  Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) limezindua mradi wa mamilioni katika eneo la hifadhi Usambara Mashariki, kwa mafunzo kwa wakazi waliomo na wanaozunguka hifadhi ya Usambara Mashariki.

  Mradi huo ambao umelenga kuwainua wanavijiji kiuchumi huku wakitunza mazingira umepata fedha kutoka Shirika la Ushirikiano wa Maendeleo la Kimataifa la Korea ( KOICA).
  Mradi huo unaotekelezwa katika vijiji 19 vinavyozunguka Hifadhi Hai ya usambara mashariki ikiwa ni utekelezaji wa mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai(GEBR).

  Mradi huo utawawezesha wananchi kwenye vijiji hivyo kutumia raslimali zao kwa namna endelevu. Mradi huo unaojulikana kama “Green Economy in Biosphere Reserves (GEBR)”,wenye thamani ya shilingi milioni 700 utapunguza ukataji miti na kulinda hifadhi kwa kutumia raslimali kwa busara zaidi.

  Mradi huo unatarajiwa kuwezesha wananchi wa maeneo hayo kupunguza umaskini kwa kutumia raslimali zilizopo kwa busara na wakati huo huo kuhifadhi mazingira.
  DSC_0012
  Afisa Mradi wa uchumi wa kijani ndani ya hifadhi hai (GEBR) Kitengo cha Sayansi kutoka UNESCO na mwakilishi wa KOICA, Myoung Su Ko, akisaini kitabu cha wageni kwenye ofisi za kata ya Mnyuzi mara baada ya kuwasili wilayani hapo kwa ajili ya kuzindua mradi wa mamilioni katika eneo la hifadhi Usambara Mashariki, na kuendesha mafunzo kwa wakazi waliomo na wanaozunguka hifadhi ya Usambara Mashariki.


  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi  wa Tanzania Nchini  Urusi  Lt.Gen Wynjones Mathew Kisamba alipofika kumuaga Rais leo Ikulu Mjini Zanzibar.(Ramadhan Othman,Ikulu.)


   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na  Balozi  wa Tanzania Nchini  Urusi  Lt.Gen Wynjones Mathew Kisamba alipofika kumuaga Rais Ikulu Mjini Zanzibar leo .(Ramadhan Othman,Ikulu.).

  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Viongozi wa Dini na Viongozi wa Mkoa wa Kigoma wakati alipofanya ziara ya siku moja Mkoani humo leo.
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi na Viongozi wa Mkoa wa kigoma kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma baada ya kukamilisha ziara ya siku moja Mkoani humo leo.(Picha na OMR)
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mkuu wa Mkoa wa kigoma Mhe. Issa Machibya kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma baada ya kukamilisha ziara ya siku moja Mkoani humo leo.  

  0 0

    Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi wa fedha za Serikali ya Baraza la Wawakilishi (PAC), Ofisini kwake Migombani.
   Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi wa fedha za Serikali ya Baraza la Wawakilishi (PAC), Mhe. Omar Ali Shehe, akizungumza wakati kamati yake ilipokutana na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, Ofisini kwake Migombani.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ukaguzi wa fedha za Serikali ya Baraza la Wawakilishi (PAC), pamoja na baadhi ya watendaji wakuu wa ofisi yake, Ofisini kwake Migombani.


  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi balozi Wynjones Kisamba, Ofisini kwake Migombani. (Picha na Salmin Said, OMKR).

   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akisalimiana na balozi mpya wa Tanzania nchini Urusi balozi Wynjones Kisamba, Ofisini kwake Migombani.

  0 0

  Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imezindua kampeni maalum ya kuhamasisha wafanyakazi wake kuhakikisha uendeshaji wa magari na vyombo vingine vya moto unaozingatia usalama ili kulinda afya na usalama wao wawapo barabarani.

  Vodacom ambao ni washindi wa tuzo ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi inayotambuliwa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa Kazi (OSHA) imezindua kampeni hiyo ikiwa ni mwendelezo wa jitihada mbalimbali inazozichukua katika kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake wakati wote wanapokuwa kazini.

  Kampeni iliyozinduliwa ya “Wait to Send Campaign”  inawataka wafanyakazi wa Vodacom wanaotumia magari ya kampauni na wasiotumia kutotumia simu ya mkononi kutuma ama kusoma ujumbe mfupi wa maandishi ili kujiweka katika mazingira salama ya kujikinga na ajali wawapo barabarani. 

  “Tunayofuraha kubwa sana leo kuona tunapiga hatua nyingine moja ya ziada katika kulinda afya na usalama wa wafanyakazi wetu wakati wote. Hili ni jukumu letu tunalolipa kipaumbele cha hali ya juu katika uendeshaji wa shughuli zetu.”Alisema Mkuu wa Idara ya Usalama, Afya na Mazingira wa Vodacom Tanzania Karen Lwakatare.

  “Kila mfanyakazi wetu lazima awe salama na tunapotambua uendeshaji wa majukumu yetu ambao matumizi ya magari na vyombo vingine vya usafiri ni sehemu ya kazi zetu na amsiha yetu ni lazima tukumbushane njia bora za uendeshaji ulio salama kwa faida yao na kwa kampuni pia.”Alisema Lwakatare

  Lwakatare amesema ingawa hakuna ajali nyingi zinazowahusisha wafanyakazi wakiwemo wakandarasi wake lakini jambo hilo haliwezi kuifanya Vodacom kujisahau kwani lengo ni kuhakikisha hata hizo chache zinazojitokeza zinadhibitiwa na kuepukwa.

  Amesema matumizi ya simu za mkononi kwa madereva ni moja ya visababishi vya ajali na hasa kutumia simu ya mkononi kutuma au kusoma ujumbe mfupi wa maadishi na kwamba wanataka kila mfanyakaizi atambue hilo na kujikinga dhidi ya janga analoweza kulipata kwa kutumia simu yake anapoendesha gari.

  Amesema Vodacom inaangalia namna gani wanaweza kushirikiana na Jeshi la Polisi na wadau wengine kuendesha kuihusiha jamii nzima na kampeni hiyo ili kupunguza ajali za barabarani zinazochangiwa na matumizi ya simu za mkononi.

  “Unaweza kuona kama ni kitu cha kushangaza kuwa sisi ndio watoa huduma za simu za mkononi halafu tunakataza matumizi ya simu hizo kwa madereva wawapo barabarani. Kwetu sisi maisha ya mteja wetu na mfanyakazi wetu ni yenye thamani kubwa zaidi kuliko jambo lolote.”

  Vodacom Tanzania ni miongoni mwa makampuni yaliyowekeza vya kutosha katika kuhakikisha afya na usalama wa wafanyakazi wake mahala pa kazi huku kila mfanyakazi akitakiwa kutii amri kuu za usalama na afya wakati wote bila kukosa kwa kisingizio chochote.


  0 0

  KLABU ya yanga imeingia makubaliano ya kununua nyumba kwa ajili ya wachezaji wake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) .

  Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika mkutano maalum na wachezaji hao Mkurugenzi wa uendeshaji NSSF, Crescentius Magori amewaambia wachezaji hao kuwa "kijana mjanja mjini ni yule ambaye ana miliki nyumba ama ardhi kuliko magari" huku akiwahamasisha wachezaji wa Yanga kuchangamkia ununuzi wa nyumba hizo ambazo ziko katika mradi wa makao mapya katika kijiji cha Dege Kigamboni jijini Dar es Salaam.

  “Sisi tuko tayari kuwapa fomu na kwenda kuwaonyesha nyumba hizo ambazo zimejengwa kisasa zaidi hivyo ningependa kuwashauri pindi mnapopata fedha zenu za mikataba mkitoa kiasi ili kuweza kuwa kati ya wamiliki wa nyumba hizo” alisema Magori.

  “Endapo utaweza kumudu na kutoa kiasi cha sh. mil.8 taslimu na kulipa kwa miezi mitatu mfululizo unapewa NSSF wanamupa funguo na kuendelea kulipa kila mwisho wa mwezi hadi kwa miaka 15 unakuwa mmiliki halali wa nyumba hiyo”alisema Magori.

  Aidha aliongeza kwa kuwaambia wachezaji hao kwamba endapo utakufa ndugu anaweza kurithi nyumba hiyo. Huku akiwasisitiza wachezaji ambao bado hawajajiunga na NSSF kufanya hivyo mara moja ili waweze kujivunia matunda ya uchezaji wa mpira hapo baadaye.

  Wakati huohuo Katibu wa Yanga Beno Njovu aliwaambia waandishi wa habari kwamba hayo ni mawazo ya Mwenyekiti wa Yanga Yusuph Manji ambaye alizungumza na Mkurugenzi wa NSSF Ramadhan Dau ambapo wote kwa pamoja wameamua kuwawezesha wachezaji wa timu hiyo ili waweze kuwa na mali zao za kudumu hadi uzeeni.

  Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Crescentius Magori akizungumza na Wachezaji wa Timu ya Yanga wakati wa mkutano wao wa kuzungumzia umuhimu kwa wachezaji hao kumiliki nyumba zao,uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akifafanua jambo mbele ya wachezaji wa timu ya Yanga na viongozi wa timu hiyo (hawapo pichani) wakati wa mkutano huo uliofanyika leo kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.
  Katibu Mkuu wa Timu ya Yanga,Beno Njovu akieleza nia ya Timu yake ya kutaka kuwawezesha wachezaji wao waweze kuwa na Nyumba zao wenyewe.
  Watendaji wakuu wa NSSF
  Sehemu ya Uongozi wa Timu ya Yanga chini ya Kocha Mkuu,Marcio Maximo.
  Wachezaji wa Yanga wakipitia vipeperushi walivyopewa juu mradi wa nyumba za bei nafuu za NSSF.
  Baadhi ya Wachezaji wa Yanga wakifatilia kwa makini maelezo waliyokuwa wakipewa.

  0 0

  Leo majira ya saa kumi alfajiri kumetokea ajali ya maporomoko ya mawe katika eneo la juu la Mlima Kilimanjaro la Hans Meyer na kusababisha kifo kwa mwanafunzi Malata Thomas kutoka Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli .
  Aidha, mwanafunzi mwingine Matenga S.J alivunjika mguu wake na anaendelea na matibabu katika hospitali ya KCMC mjini Moshi.
  Wanajeshi hawa walikuwa pamoja na wenzao 265 walikuwa katika mafunzo yao ya kawaida ya ukakamavu katika Mlima Kilimanjaro.

  Shirika la Hifadhi za Taifa linaendelea na taratibu za kufahamu chanzo cha kutokea kwa ajali hiyo na taarifa kamili itatolewa kwa umma mara baada ya kukamilika.

  Imetolewa na Idara ya Mawasiliano kwa Umma

  HIFADHI ZA TAIFA TANZANIA


  15.07.2014


  0 0


  0 0


  Katika kuelimisha umma wa Watanzania ni nani waliopo kwenye "Cultural Wars" tumeanza kutoa maelezo ya waigizaji ili watu waone kuwa Movie hii ni serious movie. 


  Ili kuwajua BOFYA HAPA

  Jipatie DVD kupitia:

  0 0
 • 07/15/14--13:57: Article 14


 • 0 0

  a.KATIBU mkuu wa umoja wa vijana ccm (UVCCM) Taifa , Sixtus Mapunda wa pili kulia akiwa anatoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari juu ya ziara yake katika mkoa wa Arusha
  b.
  Waandishi wa habari wakiwa kazini

  KATIBU mkuu wa umoja wa vijana ccm (UVCCM) Taifa , Sixtus Mapunda amewataka wazee wa kimila (malwaigwanan), viongozi wa dini pamoja na wazazi kutumia muda wa ziada  kukaa na vijana wao na kukemea kuacha mara moja kutumiwa katika vitendo viovu vinavyoendelea mkoani hapa.

  Alisema kuwa , vijana wengi  wamekuwa wakituhumiwa kufanya  uhalifu  wa  ulipuaji wa mabomu jijini hapa ambapo wengi wao ni vijana kuanzia umri wa miaka 18 hadi 25.

  Aliyasema hayo juzi wakati akizungumza na wananchi pamoja na vijana katika wilaya ya Arusha na Meru wakati alipotembelea  maeneo hayo kwa lengo la kujionea hali halisi ya vijana na kuzungumza nao.

  Alisema kuwa, mkoa  wa Arusha hivi sasa unakabiliwa na wakati mgumu sana kutokana na uvunjifu wa amani unaofanywa na vijana kwa kutumiwa na baadhi ya watu kwa lengo ya kuvuruga amani ya mkoa wa Arusha na kwa nchi kwa ujumla.

  Mapunda alisema kuwa, wazee wa kimila pamoja na viongozi wa dini wana mchango mkubwa sana katika jamii inayowazunguka hivyo wakiweza kuwakutanisha vijana na kuzungumza nao kuhusiana na kutokukubali kutumiwa katika uvunjifu wa amani badala yake wawe walinzi wa nchi yao na kuwa mstari wa mbele kuwafichua wahalifu.

  ‘jamani mkoa wa Arusha una vivutio vingi sana vya watalii ambavyo kwa ujumla vimekuwa vikiingizia mkoa wa Arusha fedha nyingi pamoja na taifa kwa ujumla , na pia kupitia vivutio hivyo vijana wengi wameweza kupata ajira na hata wengine kujiajiri sasa tunapofikia hatua ya kujiingiza kwenye uvunjifu wa amani ,hata uchumi unayumba kwani hakuna atakayependa kutembelea Arusha tena’.alisema Mapunda.

  Alifafanua zaidi kuwa,ni vizuri vijana wakawa mstari wa mbele kuwafichua wale wahalifu wanaovunja amani badala ya kuwakumbatia na kuwapa ushirikiano  hali ambayo inachangia uchumi wa nchi kuyumba kwa ujumla.

  Mapunda  aliwataka wadau mbalimbali nchini kushirikiana na  kuwa walinzi  katika maeneo yao ikiwemo kutoa ushirikiano wa kutosha kwa maeneo husika pale watakapowabaini wahalifu mahali popote ili tuweze kuinusuru nchi yetu badala ya kuachia swala la ulinzi kwa jeshi la polisi peke yake.

  Naye Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha,Robinson Meitinyiku alisema kuwa,kutokana na matukio ya uhalifu wa mabomu yanayoendelea jijini hapa seriakli itaendelea kuchukua wajibu wake na kuhakikisha kuwa amani inadumushwa.

  Alisema kuwa, wao kama uvccm mkoa wa Arusha wamekuwa wakiwaomba wazee wa kimila pamoja na viongozi mbalimbali kukaa na vijana na kuweza kuwasihi kutokubali kutumiwa katika uhalifu huo.(Pamela Mollel wa jamiiblog)

  0 0

  Stuart Page (ICSS Director, Strategy and Policy Development (Anti-Corruption/Transparency)- second from left) and Jake Marsh (Investigator at the ICSS, far right) with the 2014 Street Child World Cup Winners.

  Jake Marsh (Investigator at the ICSS, far right) with young players from the Tanzania Street Children’s Sports Academy and Street Skillz Programme in Mwanza, Tanzania  Stuart Page (ICSS Director, Strategy and Policy Development (Anti-Corruption/Transparency)- left) with the 2014 Street Child World Cup

  Stuart Page (ICSS Director, Strategy and Policy Development (Anti-Corruption/Transparency)delivering a match-fixing education workshop to the Tanzania Under-17 Football Squad

  The ICSS Sport Integrity team with the Tanzania Under-17 Football Squad

     

  0 0  0 0

  Leo Waziri wa Ujenai Dkt. John Pombe Magufuli kama ilivyokuwa kwa  amesisitiza Makandarasi wanaojenga barabara za kwenda Liganga kwenye makaa ya mawe zikamilike ndani ya muda uliopangwa na kuheshimu matakwa ya Mkataba na kwamba kusiwepo na kisingizio cha kuwa wao ni wakandarasi wazalendo. 
  Alisisitiza barabara hizo zinatakiwa zikamilike mapema tayari kwa kupitisha mitambo yenye uzito wa tani 150 itayaosafirishwa kwenda Liganga. 
   Aidha, Dkt.Magufuli akiongea na Wafanyakazi wa TANROADS, TEMESA na TBA wote wa Mkoa wa Njombe alimhakikishia Kaimu RAS wa Mkoa wa Njombe kuwa serikali kupitia Wizara ya Ujenzi mwaka wa fedha 2014/2015 imetenga kiasi cha shilingi bilioni 28 kutoka mfuko wa barabara ambapo shilingi bilioni 17 zitatumika kwenye barabara kuu na za mikoa na shilingi bilioni 11 ni kwa ajili ya kuhudumia barabara zilizo chini ya Halimashauri. 
   Dkt.Magufuli amewahakikishia wananchi wa Njombe ya kuwa mwaka huu wa fedha 2014/2015 serikali imetenga fedha kwa ajili ya kuanza kuzijenga barabara za Njombe kwenda Makete yenye urefu wa kilomita 109.4 na ile ya Itoni kwenda Manda yenye urefu wa kilomita 211 kwa kuanzia kila barabara zitajengwa kwa kiwango cha lami kilomita 50.
  Dkt.Magufuli,Dkt.Wanyancha (M/Kiti Mfuko wa Barabara), Kaimu RAS Njombe,Wafanyakazi wa TANROADS,TEMESA na TBA wote kutoka Mkoa wa Njombe walipokutana kwenye kikao na Waziri wa Ujenzi.


  0 0


  0 0

  Tubingen,Ujerumani,
  Washabiki na wadau wa muziki nchini Ujerumani wanatarajia kujimwaga katika maonyesho ya 5th International African Festival Tubingen 2014, Ujerumani, yanayoanza wiki hii 17 Julai, 2014 hadi 20 Julai, 2014
  ambako bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya Ngoma Africa band inatarajiwa kutumbuiza Usiku wa jumamosi katika maonyesho hayo.
  Bendi hiyo  inayoongozwa na kamanda Ras Makunja, kama ujuavyo ni yenye mazoea ya kuwatia kiwewe washabiki kila wanapotumbuiza.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimkaribisha Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress, ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Waziri Chikawe na Balozi huyo walizungumza masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini.
   Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress (kulia) akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe wakati Balozi huyo alipomtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake, jijini Dar es Salaam leo, kujadili masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Ubalozi wa Marekani na Wizara. 
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kushoto) akizungumza na Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano kati ya Wizara yake na Ofisi ya Balozi huyo nchini. Balozi Childress alimtembelea Waziri Chikawe ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo. Picha na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.


older | 1 | .... | 505 | 506 | (Page 507) | 508 | 509 | .... | 3285 | newer