Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 501 | 502 | (Page 503) | 504 | 505 | .... | 3270 | newer

  0 0

   Na Andrew Chale, Bagamoyo
  CHUO  cha Kilimo na Mifugo Kaole (Kaole College of agriculture (KCA), kesho Jumamosi Julai 12, kinatarajia kufanya mahafali yake ya pili chuoni hapo huku wahitimu  291, wakitarajiwa kutunukiwa vyeti mbalimbali.
  Akizungumza mjini hapa,  principle wa chuo hicho,  Cuthbert Liwa alisema kuwa, tayari maandalizi yamekamilika na mahafali hayo yatafanyika kwenye viwanja vya chuo hiko.
  “Jumla ya wahitimu 291, wanatarajiwa kuhitimu na kutunukiwa  vyeti vyao.   Kati ya hao, wahitimu 179, fani ya Kilimo na  wahitimu 112, kwa fani ya Ufugaji” alisema Liwa.
  Aidha, alisema mgeni rasmi kwenye mahafali hayo, anatarajiwa kuwa Dr. Masuruli wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi.
  Aidha, aliwaomba watu mbalimbali kujumuika kwa pamoja kwenye mahafali hayo, chuoni hapo, Kaole, Bagamoyo. (the college is located in South-East Bagamoyo 3.5 km from Bagamoyo township in the premises of Kaole Secondary school.  The centre is along the showers of the Indian Ocean).


  0 0

   Jaji Chang-ho Chung akimweleza jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule akizungumza na Jaji Chang-ho Chung,  Mgombea wa Nafasi ya Jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kutoka Jamhuri ya Korea ambaye alimtembelea Ofisini kweke tarehe 11 Julai, 2014.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule akizungumza na Jaji Chang-ho Chung,  Mgombea wa Nafasi ya Jaji katika Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) kutoka Jamhuri ya Korea ambaye alimtembelea Ofisini kweke tarehe 11 Julai, 2014. Jaji Chang-ho Chung ambaye kwa sasa ni Jaji wa Kimataifa chini ya Umoja wa Mataifa katika Chemba Maalum za Mahakama nchini Cambodia ni mmoja wa Wagombea wanaowania nafasi sita za Majaji katika Mahakama ya ICC ambao uchaguzi wao utafanyika Mjini New York, Marekani mwezi Desemba 2014 wakati wa Kikao cha 13 cha Nchi Wanachama waliosaini Mkataba wa Rome ulioanzisha ICC. 
  Jaji Chang-ho Chung akizungumza huku akisikilizwa na   Katibu Mkuu na wajumbe wengine akiwemo Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju (wa kwanza kulia) 

  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali ina mpango wa kujenga reli mpya ya kutoka Dar es Salaam hadi Mwanza kupitia mikoa na ya kati na kuelekea Isaka hadi Burundi ambayo ujenzi wake utazinduliwa rasmi Desemba, mwaka huu. 
   Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Julai 10, 2014) wakati akijibu maswali kutoka kwa Watanzania waishio Reading katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Crowne Plaza. Waziri Mkuu ambaye alitumia usafiri wa treni kwenda na kurudi mji wa Reading kutoka London, alisema ni mara yake ya kwanza kufika kwenye mji huo na akaahidi katika siku za usoni kufanya mikutano ya aina hiyo kwa Watanzania waishio kwenye miji mingine ya Uingereza kulingana na ratiba ambayo watu wa ubalozini watakuwa wameipanga. 
   “Kuna mtu ameulizia kuhusu tatizo la usafiri nchini Tanzania, napenda kuwahakikishia kwamba Serikali imeamua kuwekeza kwenye mradi mkubwa wa ujenzi wa reli ya kati. Reli hii itaanzia Dar es Salaam hadi Isaka, Isaka hadi Burundi; itatokea Tabora hadi Kigoma na Tabora hadi Mwanza pamoja na kipande cha Kaliua hadi Mpanda,” alisema. 
   “Mradi huu ni mkubwa ambao ujenzi wake utagharimu dola za marekani bilioni saba, na utatuchukua karibu miaka minne. Kwa hiyo ikiifika Desemba, mwaka huu utafanyika uzinduzi rasmi kwa njia zote hizi za reli,” alisisitiza Waziri Mkuu. 
   Alisema ili kufanikisha ujenzi Serikali imeamua kujenga upya reli ya kati kwa standard gauge hali ambayo haitaathiri usafiri wa treni kwa kutumia njia ya zamani. “Safari hii tumeamua kujenga upya, na siyo kubanduabandua ili wakati reli mpya ikiendelea kujengwa na ile ya zamani inaendelea kutoa huduma kama kawaida,” alisema huku akishangiliwa. 
   Maswali mengine aliyoulizwa Waziri Mkuu yalihusu ujenzi wa barabara ya Lindi-Mtwara, ujenzi wa hospitali ya Kagwa, ujenzi wa uwanja wa ndege wa Musoma, utaratibu wa utoaji wa mizigo bandarini na usumbufu wanaoupata, uraia wa nchi mbili, tatizo la walimu na hali ya elimu nchini ambayo yote aliyajibu na kuahidi kufuatilia masuala mengine akifika nyumbani.
   Kwa ujumal, Waziri Mkuu aliwataka Watanzania waishio nchi za nje (wana Diaspora) kufuatilia kwa makini mikutano ya uwekezaji (Investors’ Forums) ambayo hufanyika kwa kanda au kwa mikoa ili iwasadie kubaini fursa za uwekezaji zilizoko kwenye mikoa wanayotoka.
   “Tumieni fursa hizi, zitawasaidieni kubaini kwa haraka ni maeneo gani mnaweza kuwekeza kwa haraka. Kama Diaspora mnaweza pia kutumia kipengele cha utalii wa Tanzania kutusaidia kuitangaza nchi yetu,” alisema Waziri Mkuu. 
   Waziri Mkuu jioni hii (Jumamosi, Julai 12, 2014) amekutana na Watanzania waishio Uingereza kwenye mkutano uliofanyika kwenye ubalozi wa Tanzania, jijini London.

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akipanda treni kutoka Reading kwenda London Uingereza baada ya kuzungumza na watanzania waishio Reading Julai 10, 2014. 
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu  (kulia) wakiongozana na Madona Pemba (kushoto) , mtanzania aishie Uingereza kuelekea kwenye ukmbi wa mikutano  ili kuzungumza na watanzania waishio Reading Julai 10, 2014.
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu  (kulia) wakisalimiana na baadhi ya watoto na wazazi  waliohudhuria mkutano kati yake na watanzania waishio Reading Uingereza Julai 10, 2014   
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi ya mipira  kutoka kwa watanzania waishio Reading nchini Uingereza  kabla ya kuzungumza nao Julai  10, 2014. Kushoto ni Mwenyekiti wa Umoja wa Watanzania waishio Reading, Hussein Chang'a.  
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0

   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Mgombea Urais kupitia Chama cha Frelimo,nchini Msumbiji Mhe,Filipe Jacinto Nyusi alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo
   Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Mgombea Urais kupitia Chama cha Frelimo,nchini Msumbiji Mhe,filipe Jacinto Nyusi baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ukumbi wa wageni  Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo


  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiagana na Mgombea Urais kupitia Chama cha Frelimo,nchini Msumbiji Mhe,filipe Jacinto Nyusi baada ya mazungumzo yao alipofika Ikulu Mjini Zanzibar akiwa na ujumbe aliofuatana nao leo.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0

   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifungua bomba la maji wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji Bweni wilayani Pangani mkoa wa Tanga leo.
   ais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimtwika ndoo ya maji mmoja wa wakazi wa Bweni Wilayani Pangani wakati wa uzinduzi wa mradi wa maji huko Bweni Wilayani Pangani Mkoa wa Tanga leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na mbunge wa Pangani Mhe.Saleh Pamba wakifunua kitambaa katika jiwe la msingi kuzindua ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari Kipumbwi huko Wilaya ya Pangani Mkoani Tanga leo.
   Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia fukwe za mji wa Pangani wakati akivuka kwenda kata ya Bweni kwa kutumia kivuko kipya M.V.Pangani jana.Mji wa Pangani uko katika hatari ya kumezwa na bahari kutokana na kuongezeka kwa kina cha maji kulikosababishwa na mabadiliko ya tabia nchi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na mwenyeji wake mkuu wa mkoa wa Tanga Mhe.Chiku Galawa wakivuka mto Pangani kwa kutumia kivuko kipya M.V.Pangani kwenda kata ya Bweni ambapo alizindua mradi wa maji,maabara na kuhutubia mkutano wa hadhara. Picha na Freddy Maro.

  0 0

   Na Andrew Chale
  TAASISI ya  Mwangaza wa buradani Zanzibar  (Zanzibar Light Entertainment ) ya mjini Unguja,  Zanzibar, kupitia vyombo vya habari, imemtangaza rasmi , Raisi mstaafu wa  Chama cha Soka  Zanzibar, (Zanzibar Football Association-ZFA) Mzee Ally Fereji Tamim  kuwa mgeni rasmi kwenye michuano maalum ya soka la ufukweni  lijulikanayo kama  (Zanzibar Beach Soccer Championship Bonanza) linalotarajiwa kufanyika Agosti  Mbili mwaka huu katika fukwe za  Nungwi.
  Kwa mujibu wa taarifa yao hiyo  kwa vyombo vya habari, ilieleza kuwa, michuano hiyo ya Zanzibar Beach Soccer inatarajiwa kuzikutanisha timu mbalimbali za Visiwani humo, Bara na nje ya Tanzania ambapo watakutana kwa pamoja na kushiriki kichuano hiyo maalum, kwenye fukwe hizo za Nungwi.
  Mwandaaji wa michezo hiyo, Muslim Nassor ‘Jazzphaa’  alisema  wamejisikia furaha kwa viongozi wa juu na wadau wa soka kuwaunga mkono, kwani inatia moyo katika kuendesha shughuli za kimichezo kama hizo. “Tunapongeza wadau wote, kikubwa  zaidi, ni Mzee wetu,  Ally Fereji Tamim kukubari  kuwa mgeni rasmi, pia milango ipo wazi kwa wadau wengine kujitokeza katika kufanikisha zaidi tukio hili ,muhimu” alisema Muslim  Nassoro ‘Jazzphaa’.
  Aidha, aliendelea kuwaomba  mashirika, makampuni, taasisi za Serikali na za watu binafsi na wadau kujitokeza kwa wingi kudhamini Bonanza hilo la  Zanzibaar Beach Soccer, ilikufikia malengo yaliyokusudiwa katika kuifikia jamii na kuiweka pamoja.
  Muslim  Nassoro ‘Jazzphaa’ aliongeza kuwa, Michezo hiyo yenye lengo ya kuweka watu pamoja, kudumisha utamaduni na kuhimalisha afya ya mwili, pia itakuwa na burudani mbalimbali. Lakini pia alitoa shukrani za dhati kwa uongozi wa beach soccer na kamati yote kwa ujumla katika kufanikisha jambo hilo.
  Kwa upande wake, Rais wa beach Soccer Zanzibar,  Bwana Ally Sheikh Alhabshy  alipongeza Taasisi hiyo kuandaa michuano hiyo ambapo amesisitiza kuwa Wadhamini wasisitite kutoa udhamini wao na kuja kuona mchezo huo unavyochezwa.
  Zanzibar Beach soccer Bonanza kwa  mwaka huu itakuwa ni ya mara ya tatu, kwa taasisi hiyo kuandaa michezo hiyo ya soka la ufukweni.
  Michezo hiyo ya soka la ufukweni imekuwa maalufu katika nchi mbalimbali zenye fukwe, ambapo wananchi na wageni kutoka mataifa mengine ujumuika kwa pamoja.
  Kwa mwaka huu pia kutakuwa na burudani kali na ya aina yake itayaoporomoshwa na dj mkali anayetikisa visiwani humo.


  0 0

   Waziri wa wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh.Eng Christopher Chiza amewataka wanunuzi wa tumbaku kuja na mikakati mipya ili kuwanufaisha na kuimarisha soko la wakulima wa tumbaku. 
  Mhe. Chiza ameyasema hayo leo ofsini kwake alipokutana na Meneja mkuu wa kampuni ya ununuzi wa tumbaku kutoka kampuni ya JTI. 
   Pamoja na mambo mengine waziri amewataka wafanya biashara hao kuaanda mikataba kwa lugha ya Kiswahili na kingereza ili kuwafanya wakulima waelewe masharti na manufaa ambayo yanaweza kupatikana katika mikataba hiyo 
  Akiongea na meneja mkuu wa Kampuni hiyo Bwana Robert Glenn amewataka kuleta mabadiliko chanya kuanzia kwenye hatua ya ulimaji hadi kwenye soko la zao la tumbaku 
  Aidha naye Bwana Robert amesema kuwa Kampuni yake imejipanga kupeleka huduma za ugani kwa wakulima wa tumbaku ili kuongeza ushindani na wafanyabiashara wengine wa ndani na nje.

  Waziri wa  wa Kilimo Chakula na Ushirika Mh.Eng Christopher Chiza akiongea na  meneja mkuu wa Kampuni  ya JTI Bwana Robert Glenn kuhusu ununuzi wa zao la tumbaku.


  0 0  0 0

  The 40Th Edition of  the The Council of East and Central Africa Football Associations, (CECAFA)-KAGAME Club Cup Championship draws took place in Kigali Capital City, Rwanda this Friday with CECAFA, FERWAFA, SUPPERSPORT and Top Government officials witnessing the ceremony.

   The tournament which has attracted a record 14 clubs will now kick off on August 8th and not 9th and end on 24th, one day more from the earlier schedule. A total of 34 matches - all to be shown live by Supersport will be staged at Amahoro and Nyamirambo Stadium.


  President Kagame of Rwanda who is also the patron of CECAFA has already committed USD 60,000 prize money and the Ministry of Sports and other agencies are sponsoring the event.


  Several companies in Rwanda have pledged their total support for the event which will mark 20th anniversary of Rwanda genocide. The fixtures and time schedules will be released next week.  However, the playing Groups are as below:


  Group A                                        Group B                                               Group C

  Rayon Sport [RW]                       APR [RW]                                           Vital’O [BUR]

  Yanga SC [TZ]                               KCC [UG]                                            El-Merreikh [SUD]

  Coffee [ETH]                                 Flambeau De L’est [BUR]               Police [RW]

  Atlbara [S.SUD]                            Gor Mahia [KEN]                             Benadir [SOM]

  KMKM [ZANZ]                               Telcom [DJ]               


  ·         Qualification: A1, A2, A3, B1, B2, B3, C1 and C2

  ·         All clubs to present FA playing Licenses

  ·         Referees Fitness/ Medical tests to be conducted August 5-6

  ·         Latest arrival of teams is August 6th


  Rogers Mulindwa


  Media Manager/Spokesperson


  0 0


  0 0  0 0


  0 0


  0 0

   Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akipokea zawadi kutoka kwa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar.
  Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akizungumza na Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Tanzania ambapo alitumia fursa hiyo kuwaomba wampigie kura kwani amekuja na mikakati mizuri ya kuboresha uchumi ambapo amedhamiria kuiondoa Msumbiji kwenye orodha ya nchi masikini,pia aliahidi kuwawezesha wakina Mama wa Msumbiji.
  Wananchi wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar wakisikiliza sera za Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi kwenye mkutano uliofanyika katika Hotel ya Zanzibar Beach Resort.

  Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia chama cha FRELIMO Mh.Filipe Nyusi akiongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wa Msumbiji wanaoishi Zanzibar Asilia Lunji baada ya kumaliza mkutano wake wa kampeni kwa wapiga kura wanaoishi Zanzibar,Nyusi aliwaambia kuwa amefanya mkutano wa kwanza nchini Tanzania kwa sababu ya mahusiano mazuri baina ya Msumbiji na Tanzania

  0 0

  Askari Polisi wakimtoa nje daktari feki, Karume Habibu (22) kutoka kwenye ofisi ya Mganga Mkuu wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro ambako alihojiwa kabla ya kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi kwa mahojiano zaidi.
  Daktari feki akielekea kwenye gari.
  Daktari feki, Karume Habibu akiingizwa kwenye gari.
  Akificha uso kukwepa kamera za GPL.
  Baadhi ya wafanyakazi wa Hospital ya Rufaa ya 
  Mkoa wa Morogoro wakishuhudia tukio hilo.

  WIMBI la madaktari feki kuingia katika hospitali wakijifanya madaktari na kutoa huduma mbalimbali limeendelea ambapo leo amenaswa mwingine mkoani Morogoro.
  Daktari huyo feki aitwaye Karume Habibu (22)amenaswa katika Hospitiil ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro na kupelekwa Kituo Kikuu cha Polisi mkoani humo kwa mahojiano zaidi.


  PICHA NA DUSTAN SHEKIDELE / GPL, MOROGORO

  0 0

  Filamu Mpya ya Cultural Wars Sasa Yapatikana! Wahi Kujipatia DVD! 

  Ile filamu mliyokuwa mnaisubiri kwa hamu iitwayo “Cultural Wars” iliyoandikwa na kutengenezwa na Deogratius Mhella (Mtanzania anayeishi New York) akishirikiriana na Watanzania na Wamarekani waishio New York, New Jersey Boston na Connecticut sasa imetoka kwa mara ya kwanza na inapatikana kwenye DVD na unaweza kupata “electronic Copy” 

  Filamu hii inazungumzia baadhi ya changamoto za kimapenzi wazipatazo vijana wa Kitanzania hapa Marekani. Na ni ya kwanza iliyochezwa na Watanzania na Wamarekani hapa New York kwa kutumia lugha ya Kiingereza. Baadhi ya “Actors” wa Kitanzania ni Khalifa Siwa aka “Bob”,  Ny Ebra aka “Vijimambo New York”, Akida aka “Mshenga”, Chemi Whitlow aka “Chemponda” na Isaac Kibodya aka “Father”. Wote mliosaidia katika kufanikisha filamu hii ambao hamjatajwa hapo juu, mnapewa shukrani za dhati kabisa. 

  Usikose kujipatia nakala yako kwa
   kuinunua au kuiona kupitia link hapa chini: 

  0 0
 • 07/11/14--16:13: The law school of Tanzania
 • Shule ya Sheria ya Tanzania (The Law School of Tanzania) ambayo iko nyuma na jirani na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Barabara ya Sam Nujoma Road jijini Dar es salaam. Mambo yake yote ukitaka kijua BOFYA HAPA

  0 0
 • 07/11/14--20:00: Naswaha za ramadhan
 • Naswaha za ramadhan

  0 0

   Makamu wa Rais-Utawala wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) William Kallaghe (wapili kushoto) akipokea sehemu ya fedha taslim Tsh milioni 20 zilizotolewa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kusaidia maandalizi ya mashindano ya mwaka huu ya Riadha ya Kitaifa yatakayoanza leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaaam. Kulia ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/ Pan African Power Solutions (PAP), Bw. Joseph Makandege, akifuatiwa na Msaidizi wa kampuni hiyo Rajiv Bhesania na kushoto ni Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui.
   Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui (wapili kushoto) akipokea sehemu ya fedha taslim Tsh milioni 20 zilizotolewa na kampuni ya ufuaji umeme ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) kusaidia maandalizi ya mashindano ya mwaka huu ya Riadha ya Kitaifa yatakayoanza leo katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaaam. Kulia ni Katibu na Mwanasheria Mkuu wa IPTL/ Pan African Power Solutions (PAP), Bw. Joseph Makandege, akifuatiwa na Msaidizi wa kampuni hiyo Rajiv Bhesania na kushoto ni Makamu wa Raisi-Utawala wa RT, William Kallaghe.  0 0

  Mwenyekiti wa CCM Taifa ,Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Mgombea wa Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi katika Ikulu ya Tanga ambapo walifanya mazungumzo.
  Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi akimsalimia Mzee Said Mbaruku wa Tanga wakati alipomtembelea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete akiwa kwenye mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi,Ikulu mjini Tanga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa kwenye mazungumzo na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi pamoja na Mbunge wa Tanga Mjini Mheshimiwa Omar Nundu nje ya Ikulu mjini Tanga.
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Jakaya Mrisho Kikwete na Mgombea wa Urais wa Msumbiji kupitia Chama cha FRELIMO Mheshimiwa Filipe Nyusi wakiwa kwenye picha ya pamoja Ikulu Ndogo mjini Tanga,wengine katika picha ni Komredi Oscar Monteiro,Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Mbunge wa tanga mjini Mh.Omar Nundu ,WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora, Kapteni Mstaafu George Mkuchika na Viongozi wengine kutoka Msumbiji.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

older | 1 | .... | 501 | 502 | (Page 503) | 504 | 505 | .... | 3270 | newer