Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 500 | 501 | (Page 502) | 503 | 504 | .... | 3286 | newer

  0 0


  0 0

  Mchezaji wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Ally Mayay Tembele (pichani) anawaarifu ndugu, jamaa na marafiki pamoja na jamii ya Tanzania kwa jumla kwamba email address yake ya maya@yahoo.comimeibwa na matapeli na kuanza kutumika vibaya (phishing) kwa kudai kuwa yeye yupo Ukraine na amekumbwa  na matatizo hivyo anaomba msaada wa pesa haraka.


  Mbaya zaidi, katika email yake hiyo Ally Mayay Tembele aliwahi kuambatanisha nyaraka nyeti kadhaa ikiwemo pasipoti ambazo wezi hao wanazitumia kama alama ya uthibitisho kuwa wao ni yeye. Hao jamaa ni wezi na waongo wakubwa. Msiwape ushirikiano kabisa.  Ukweli ni kwamba Ally Mayay Tembele yupo Dar es salaam na wala hajasafiri kwenda nje ya nchi hivi karibuni. Hivyo anaomba yeyoye anayeletewa email hiyo ya mayayt@yahoo.comaidharau na wala asitoe ushirikiano wowote na hao watumaji. Ni wezi na matapeli.

  0 0

   Waziri wa Ujenzi Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli leo amefungua Mradi wa Taa za kuongozea Magari katika mji wa Dodoma.Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng.Musa Ibrahim Iyombe Mradi huo ambao umefanywa na wakandarasi Wazawa umegarimu shilingi Milioni 384.Mataa yaliyozinduliwa leo ni yaliyopo ANJIA PANDA ya Barabara ya Nyerere na Mpwapwa na yale yaliyopo njia panda ya Barabara ya Area D na barabara  ya kuelekea Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Dkt.Rehema Nchimbi kulia akimkaribisha  Waziri wa Ujenzi,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli Kufungua Mradi wa Taa za kuongozea Magari Mjini Dodoma.
   Waziri wa Ujenzi,Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria ufunguzi wa Mradi wa Taa za kuongozea Magari Mjini Dodoma.
   WAZIRI WA UJENZI DKT.JOHN MAGUFULI KATIKATI AKIKATA UTEPE KUASHIRIA KUZINDUA UJENZI WA BARABARA YA MANYONI MJINI YENYE UREFU WA KILOMITA NNE

   WAZIRI WA UJENZI DKT. JOHN MAGUFULI AKIWA PAMOJA NA MKUU WA MKOA WA SINGIDA DKT.PARASEKO KONE, MBUNGE WA MANYONI JOHN CHILIGATI PAMOJA NA MWENYEKITI WA WENYEVITI WA CCM MGANA MSINDAI WAKIFUNGUA JIWE LA MSINGI KUASHIRIA UJENZI WA BARABARA HIYO. PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0  THE GRADUATING CLASS OF NECTA 2014 (BOYS)
  THE GRADUATING CLASS OF CIE 2014 (BOYS)
  THE GRADUATING CLASS OF NECTA 2014 (GIRLS)

  THE GRADUATING CLASS OF CIE 2014 (GIRLS)
  FOR MORE CLICK HERE

  0 0

  The popular Ngoma Africa band will be among many acts expected to thrill fans at the 5th International African Festival in Tübingen, Germany. The extravanganza will take place from July 17-20.
  Ngoma Africa, based in Germany, founded 1993 by bandleader Ebrahim Makunja also known as Kamanda Ras Makunja, is home to a number of talented musicians, including soloist Christian Bakotessa aka Chris-B. Others are Jo Souza, Matondo Benda, Aj Nbongo, Flora William, Jessicha Ouyah, Groly Mundeke, Gailo Proof and others.
  The band, followed by millions worldwide, is famous for driving audience crazy with “Extraordinary Rhythm” Bongo dance from East Africa.
  Ngoma Africa has released numbers of CDs, including latest “BONGO TAMBARARE”  which you can listen to at www.ngoma-africa.com 

  0 0

  • Ni ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme 
  •Kujenga mtambo wa kusindika gesi ya LPG, na kuuzwa kwenye mitungi. 
  • Sekta ya madini pia yaguswa 

   Habari na picha 
  na Asteria Muhozya 
  Tanzania na Algeria zinakamilisha majadiliano ya kuanzisha kampuni ya Ubia itakayohusika na ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme na Kampuni ya Ubia ya kujenga mtambo wa kusindika gesi ya “Liquefied Petroleum Gas” (LPG) na kuiuza gesi kwa wananchi kwa kutumia mitungi. 

  Makubaliano hayo yamefikiwa katika ziara ya kikazi ya Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo na ujumbe wake nchini Algeria, ambayo inalenga kufuatilia utekelezaji wa makubaliano ya awali ya kushirikiana katika kubadilishana uzoefu kwenye masuala yanayohusu sekta za Nishati na Madini kufuatia Mkataba wa Makubaliano ya ushirikiano wa nchi hizo uliosainiwa tarehe 2 Disemba, 2013 nchini Algeria.

   Kwa mujibu wa makubaliano ya mkutano baina ya Mawaziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria Mhe. Youcef Yousfi, mawaziri hao wameyaagiza mashirika ya Umeme ya Tanzania (TANESCO) na Shirika la Umeme la Algeria (KAHRIF) kukamilisha majadiliano ya kuanzisha kampuni ya ubia ya ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme. 

  Mkutano huo wa mawaziri, ulitanguliwa na kikao cha awali cha wataalamu wa nchi zote mbili, ambacho kiliongozwa na Kamishna Msaidizi anayeshughulikia masuala ya Umeme , Wizara ya Nishati na Madini, Mhandisi Innocent Luoga, ambacho kilijadili maeneo ya ushirikiano yanayohusu umeme, mafuta, gesi na madini. 

  Katika hatua nyingine, Mawaziri hao wameziagiza kampuni za mafuta na gesi likiwemo Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) na kampuni za mafuta na gesi za Algeria za NAFTAL na SONATRAC kukamilisha majadiliano ya kuanzisha kampuni ya ubia ya kujenga mtambo wa LPG na kuuza gesi hiyo kwa wananchi kwa kutumia mitungi, ambapo kampuni zote za ubia zimetakiwa kuanza kazi ifikapo Januari, 2015. 

  Wakati huo huo, Waziri Muhongo amekutana na Waziri wa Viwanda na Migodi wa Algeria Mhe. Abdessalem BOUCHOAREB ili kujadili maeneo ya ushirikiano katika sekta ya Madini ambapo wamezielekeza taasisi zinazohusika na madini za nchi hizo, kuandaa mpango wa utekelezaji wa ushirikiano katika kuwajengea uwezo wataalamu wa madini kubadilishana uzoefu na teknolojia, utafutaji na uendelezaji wa madini ya dhahabu, chuma, almasi, phosphates na utunzaji wa taarifa za jiolojia na madini (Management of geological and mining database). 

  Katika ziara hiyo, Waziri Muhongo na ujumbe wake wamepata nafasi ya kutembelea Mtambo wa kufua umeme wa kutumia gesi asilia wa HAMMA ambao unamilikiwa na serikali ya nchi hiyo kwa asilimia 100 na una uwezo wa kuzalisha megawati za umeme 418, na uwezo wa kutumia mafuta ya dizeli na gesi kwa nyakati tofauti. 

  Vilevile, ujumbe huo wa Tanzania umepata fursa ya kuona mashine za kuzalisha umeme zinazotembea (mobile generators) ambazo hufungwa kwa dharura sehemu inapohitajika na kuhamishiwa sehemu nyingine, ambapo mashine moja ina uwezo wa kuzalisha megawati za umeme 20. 

  Katika ziara hiyo, Mhe. Muhongo ameongozana na Kamishna Msaidizi wa Nishati anayeshughulikia masuala ya umeme, Mhandisi Innocent Luoga na wataalamu kutoka Wakala wa Jiolojia Tanzania (GST), TPDC na TANESCO. Mkataba wa Makubaliano (MoU) ya ushirikiano wa Tanzania na Algeria, ulisainiwa na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo kwa upande wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Mhe. Youcef Yousfi.
  Ujumbe wa Tanzania (kushoto) ukiongozwa na Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo (wa nne kutoka kushoto) wakiwa katika mkutano wa majadiliano ya kuanzisha kampuni za Ubia za ujenzi wa miundombinu ya kusambaza umeme na ujenzi wa Mtambo wa kusindika gesi ya “Liquefied Petroleum Gas’ (LPG) ambayo itauzwa kwa wananchi kwa kutumia mitungi. Walio upande wa kulia ni Waziri wa Nishati na Migodi wa Algeria, Mhe. Youcef Yousfi, Algeria (wanne kutoka kulia) na ujumbe wake.

  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Profesa Muhongo  Wa kwanza kulia), akiongea  jambo  na wataalamu wa masuala ya gesi na umeme wa Algeria wakati walipokwenda  kutembelea Mtambo wa kufua umeme kwa kutumia gesi asilia wa HAMMA ,Mtambo huo wenye uwezo wa kuzalisha mewagati za umeme  418 unamilikiwa na Serikali ya Algeria  kwa asilimia 100.

  Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Sospeter Muhongo (Kushoto), akiongea na Waziri wa Viwanda na Migodi wa Algeria, Mhe. Abdessalem BOUCHOAREB.(Kulia)  Mawaziri ambapo wamejadili maeneo ya ushirikiano katika sekta ya Madini. Katikakati ni mkalimani.


  0 0  0 0

  Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa rais Mazingira Dkt Binilith Mahenge amewataka wananchi kupuuza taarifa zozote zinazotolewa kwa jina lake kupitia mtandao wa facebook kwa kuwa yeye hatumii mtandao huo. 

  Waziri Mahenge ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Makete mkoani Njombe ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na mwandishi wetu wilayani hapo na kusema kumekuwa na baadhi ya watu wanaoitumia mitandao hiyo vibaya kwa kufungua akaunti yenye jina lake ilihali yeye hajawahi kujiunga na facebook na hana mpango huo. 

  Amesema kwa kuwa yeye ni kiongozi mkubwa wa serikali wapo watu wanaoziamini taarifa mbalimbali zinazotolewa kupitia mtandao huo wakidhani zimetolewa na yeye lakini imekuwa tofauti na kuwataka wananchi kuzipuuza taarifa hizo kwa kuwa zinatolewa na mtu ama watu fulani na si yeye.

   "Ukiangalia pale pana picha yangu kweli, lakini taarifa zingine ni uongo mtupu, kwa mfano tarehe yangu ya kuzaliwa iliyoandikwa hapo sia ya kweli, hii inaashiria wanavyoviweka ni vya uongo" amesema Waziri Mahenge.

   Aidha ametoa rai watu kuitumia vizuri mitandao hiyo kwa kuisaidia jamii huku akiwataka waliofungua akaunti hiyo kuifunga na kuacha kuwapotosha watu kwa kutumia jina lake kwani ni kinyume cha sheria na atakayebainika sheria iko wazi dhidi yake. 

  Hivi karibuni kumekuwa na watu fulani kufungua akaunti kwnye mitandao ya kijamii kwa kutumia majina ya viongozi mbalimbali kwa lengo la kuwahadaa watu na kuwapa taarigfa ambazo si sahihi

  Habari/Picha Na Edwin Moshi, Makete

  0 0

  WINGU JEUSI LATANDA MSIBA WA SISTA ANNA, DAYOSISI YA KUSINI KATI YATANGAZA KUENDELEA KUENZI KAZI ZA MAREHEMU

  Sista Anna Enzi za uhai wake.

  Msiba wa sista Anna Peterson umeibua simanzi si kwa familia yake tu bali kwa wananchi wa wilaya ya Makete mkoani Njombe alipokuwa akifanya kazi za kijamii tangu 
  ujana wake. 

  Hayo yamebainika wakati wa ibaada maalum ya kumkumbuka iliyofanyika hii leo katika kanisa la KKKT usharika wa Amani Bulongwa, ibaada iliyoongozwa na baba askofu wa dayosisi ya kusini kati Levis Sanga, Askofu Mstaafu Dkt. Solomon Swallo na Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa pamoja na msaidizi wa askofu Philemon kahuka. 
  Akihubiri katika ibaada hiyo maalum Askofu Mstaafu Shadrack Manyiewa amesema marehemu alikuwa akifanya kazi zake kwa mkono wa dayosisi ya kusini kati tangu enzi za ujana wake bila ubaguzi ingawa yeye alikuwa mzaliwa wa nchi ya Sweden. 

  0 0


  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa nchi za ACP Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) akishukuru Benki ya Maendeleo ya Ulaya (EIB) kwa kutoa  mikopo ya gharama nafuu na kusaidia Maendeleo ya nchi za ACP. Balozi Kamala ameitaka Benki hiyo kuongeza kiwango cha mikopo inayotoa katika nchi za ACP kutoka asilimia 10 ya mikopo inayotoa sasa hadi asilimia 20. 

  Kamati ya Mabalozi wa nchi za ACP leo imekutana na Uongozi wa Benki ya Maendeleo ya Ulaya, Luxembourg kubadilishana mawazo jinsi ya kuboresha utendaji wa Benki na kuweka vipaumbele vya maendeleo na ushirikiano kati ya nchi za ACP na Benki ya Maendeleo ya Afrika.

  0 0

     Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere akizungumza machache wakati wa hafla aliyowakaribisha chakula cha jioni wasanii wa Filamu na wadau mbalimbali wa filamu Bongo ikiwa ni kuungana na wenzao waliokatika mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. Hafla hiyo ilifanyika ndani ya Great Wall Restaurant iliyopo Osterbay jijini Dar esa Salaam.

   Wageni waalikwa wakisikiliza kwa makini maneno yaliyokuwa yakitolewa na Rais wa Bongo Movie, Steve Nyerere.
   Wasanii wakipata maakuli...
   Wolper na Kajala wakila chakula wakati wa hafla hiyo.
  PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

    Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na wajumbe wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi  na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) iliyofanyika katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
   Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi Dkt. Fatma Mrisho akizungumza na wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa majumuisho ya hali ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam mara baada ya kukamilisha ziara ya siku nne mkoani Dar es salaam. Dkt. Fatma ameeleza kuwa maabukizi yameendelea kupungua kutokana na juhudi kubwa inayofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
   Naibu Meya wa Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge akitoa mchango wake kuhusu namna viongozi wanavyoweza kusaidia kupunguza vitendo hatarishi vinavyochangia maabukizi mapya ya VVU katika maeneo wanayoyaongoza, wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara ya siku nne ya viongozi  na watendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) jijini Dar es salaam.
  Wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa majumuisho ya ziara ya watendaji wa TACAIDS katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam kuangalia hatua iliyofikiwa katika mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU katika jiji la Dar es salaam. 

  0 0

   Aisha Sururu Foundation inawataarifu fainali ya mashindano ya kuhifadhi Qur'an takatifu ya Taifa ya mwaka 2014 yatafanyika Jumamosi hii ya tarehe 12/07/2014 katika ukumbi wa Diamond Jubilee Hall ambapo vijana wanawake na waume walioshiriki katika mashindano hayo watapigania nafasi zao za kwanza mbele ya umma na wageni waalikwa katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhan.

  Mwaka huu Aisha Sururu Foundation imeshirikisha mikoa 9 ya Tanzania ikiwemo visiwa vya Zanzibar na Pemba ambapo vijana watakaoshiriki kutoka visiwa vya Pemba ni vijana walemavu wa macho, walemavu wa viungo na kadhalika. 
  Njoo uje ushuhudie kwa uwezo wa Allah (Mwenyezi Mungu) vipi walemavu wa macho na vijana wengineo walivyojiwezesha kufika kwenye jukwaa la mashindano ya kuhifadhi Qur'an ya taifa ya mwaka 2014.

  Uongozi wa Aisha Sururu Foundation unawaalika Watanzania wote waje pamoja kushuhudia mashindano haya na kuwashajiisha vijana wote walioshiriki katika mashindano haya ya taifa ya mwaka 2014.

  Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall
  Tarehe 12/07/2014, Jumamosi
  Kuanzia saa tatu asubuhi (9am) mpaka saa nane mchana (2pm)

  Wabillahi tawfeeq,
  Ramadhan Mubaarak,


  0 0

  mwenyekit
  Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida, Iddy Mnyampanda akizungumza shule ya sekondari Kinyeto.

  Na Hillary Shoo, SINGIDA.
  Mbunge wa Jimbo la Singida Kaskazini Mkoani Singida, Lazaro Nyalandu ametoa mchango wa mabati 420 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 10 kwa shule mbili za sekondari za Kata za Mtinko na Kinyeto.
  Mchango huo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi zake kwa wananchi wa Jimbo hilo kuchangia katika ujenzi wa maabara mbalimbali kwenye shule za sekondari za Jimbo hilo.

  Akikabidhi msaada huo kwa Niaba ya Nyalandu ambaye pia ni Waziri wa Maliasili na Utalii, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Singida Narumba Hanje aliwataka wananchi kuheshimu michango ya Mbunge wao na kuachana na porojo za siasa za mitaani.
  kinyeto
  Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akizungumza kwenye shule ya sekondari Kinyeto wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya mabati 200.
  “Nataka niwaulize swali hivi ni wananchi ndio wenye matatizo au ni sisi viongozi, jibu ni rahisi ni sisi viongozi ndio wenye matatizo, haiwezekani Mbunge anatoa msaada mkubwa namna hii halafu watu wanajipitishapitisha wakitukana.” Alisema Hanje kwa hasira.

  Aidha alisema wapo watu wanaompaka matope Waziri Nyalandu, lakini matunda yake yanaonekana na anaendelea kutekeleza ahadi zake.
  “Mimi inanishangaza sana kuna watu wameanza kujipitisha pitisha huko na wengine wanatukana kisa eti ni kaligi sijuji Mpombo Cup, fanya vitu vionekane sio maneno maneno kaka, na mimi ndiye mtekelezaji mkuu wa Ilani ya Chama Willaya hii.” Alisema Hanje kwa kujiamini.
  diwani
  Diwani wa Kata ya Kinyeto, Francisco Ng’eni akipokea msaada wa mabati 200 kutoka kwa Mwenyekiti Hanje kwa niaba wa Mbunge wa Jimbo hilo Mhe, Lazaro Nyalandu.

  0 0


  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Nagu katika hotuba yake,amesema atawasimamia Makatibu hao na kuhakikisha wanaanzisha Benki yao ambayo itawawezesha kuweka abiba zao na kukopeshana pia.

  Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania na Mshauri wa Mambo ya Kisheria wa TAPSEA,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake katika ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Kairuki amewahimiza Makatibu Muhtasi hao kuhakikisha wanaudumisha na kuulinda umoja walionao,kwani umoja ndio msingi wa maendeo.
  Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akisoma hotuba yake kwenye ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 kwenye hoteli ya Malaika,jijini Mwanza.
  Washiriki wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania kutoka maeneo mbali mbali wakifatilia mada mbali mbali.


  0 0

   Mgombea Urais wa Msumbiji kwa tiketi ya chama cha Ukombozi cha FRELIMO Filipe Nyusi akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, Ikulu Ndogo mjini Tanga, mgombea huyo alipokwenda kumsalimia na kuwa na mazungumzo na Rais leo.
  Rais Kikwete na Mkewe Mama Salma, wakiwa katika picha ya kumbukumbu na mgombea huyo kwa tiketi ya FRELIMO Filipe Nyusi, Ikulu Ndogo mjini Tanga. Kushoto ni Mwenyeji wa Mgomba huyo, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana. Picha na Adam Mzee wa CCM Blog.

  0 0

  Mkurugenzi wa Sekretarieti ya Dunia ya Nishati Bwana. Steivan Defilla (kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala (katikati) baada ya kumaliza kikao ofisini kwake. Kulia ni Bwana. Nodal Tayel Mratibu wa Taasisi hiyo. Ujumbe huo ulifika Ubalozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya, Brussels kueleza faida za nchi kuwa mwanachama wa Taasisi ya Nishati Duniani.

  0 0  0 0


  African Voices highlights Africa's most engaging personalities. This week on African Voices, we talk to filmmaker Martin Mhando.  Showtimes: (all times GMT
  Friday: 0730 - 11/07
  Saturday: 1430 - 12/07
  Sunday: 0230, 0800, 1730 - 13/07
  Monday: 0930, 1430 - 14/07
  Tuesday: 0430- 15/07


  Cheers
  Zanzibar International FilmFestival

older | 1 | .... | 500 | 501 | (Page 502) | 503 | 504 | .... | 3286 | newer