Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

REMEMBRANCE

$
0
0


Mom, it has been eight years now since God and His angels called you away from us. We still feel the sorrow and sadness due to your absence, but we believe you are in Heaven, praying for us and guiding us in your daily lives.

You are sadly missed by your beloved husband- Joshua Daniel Minja, your children- Andrew, David, Alfred and Peter, your daughters-in-law- Dr. Irine and Ngianasia and your lovely grandchildren Danielle, Esther, Gabriella, Joshua and Robert without forgetting all other members of the family, relatives and friends who loved you whole heartedly.


You will forever lives in our hearts and ask God to give you a peaceful rest. 
In time we shall join you in Heaven.

Amen.


ngoma azipendazo ankal - kizazi kipya

$
0
0
Hakika mshumaa umezimika wakati bado mapema. Marehemu Sharo Milionea akimshikirisha Dully Sykes katika ngoma yake ya 'Chuki Bure' unathibitisha hilo. Rip Sharo Milionea. We gonna miss U forever!

Heineken rewards best performing employees

$
0
0
 Heineken Tanzania Team in a group photo
 from Right: Uche Unigwe – Country Manager Tanzania, Elizabeth Buitendijk – PA to the Country Manager and Koen Morshuis – General Manager East Africa. 

from left to right: Uche Unigwe-Tanzania Country Manager, Fey Gwendolene Bananuka – Hassan – Trade Marketing Consultant Tanzania and Koen Morshuis-General Manager East Africa.

CHRISTIAN BELLA LIVE IN HELSINKI AT CLUB VENUE 30.12.2012

Unique Model 2012 kupatikana leo Maisha Club jijini Dar

$
0
0
Ile siku iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na watanzania wengi kutaka kujua nani ataibuka mshindi wa shindano la kumsaka mwanamitindo wa mwaka mwenye sifa za pekee nchini Tanzania (Unique Model 2012) sasa imewadia.

Homa ya shindano imezidi kupanda ikiwa usiku wa leo atajulikana nani atavishwa taji la unque model of the year 2012 taji lenye heshima katika tasnia ya mitindo nchini Tanzania.

Jumla ya washiriki kumi na mbili wanapanda jukwaani kuwania taji hilo kwenye fainali zake zitakazofanyika katika ukumbi wa maraha wa New Maisha club uliopo Oysterbay jijini Dar usiku wa leo.

Washiriki wanaowania taji hilo ni Vestina Jax,Judith sangu,Amina Ayoub,Catherine Masumbigana,Elizabeth Pertty,Elizabeth Boniface,Vivian Gilbert ,Darline Mmari , Zeenath Habibb,Sandra Suleiman,Cecilia Emmanuel,Magreth Msafiri.

Mratibu wa shindano hili Bwana Methusela Magese amewaomba watanzania wajitokeze kwa wingi siku ya leo kwani kuna mambo mazuri ya kufurahisha ikiwemo burudani ya muziki wa bendi toka kwa mashujaa,ngoma za asili na bongo flava kwa kiingilio cha Tshs 15,000/= tu.

Shindano hili limedhaminiwa na Giraffe ocean view hotel,Kitwe general Traders,sophanaa investment ltd,dtv,88.4 clouds fm,Gazeti la Tanzania Daima,Gazeti la Kiu,mashujaa investment ltd,Michuzi blog,jiachie blog,Lmada Apartments & Hotel,mtaa kwa mtaa blog,Fabak fashins,Genessis health center na Yung don Records,Paka wear,Mtoko Design,Dina ismail blog na Unique Entertainment Blog. 

Wananchi wa Mtwara Mjini wafanya maandamano makubwa kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar

$
0
0

Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Mtwara Mjini wakiwa kwenye maandamano makubwa waliyoyafanya kupinga gesi kusafirishwa kwenda Dar!
Wakazi hao wakiwa na mabango yao yenye jumbe mbalimbali kama uonavyo pichani.
Waandamanaji wakiwa wamekusanyika kwenye moja ya uwanja mjni Mtwara wakipinga gesi kusafirishwa kwenda jijini Dar!
Mmoja wa wakazi wa mji wa Mtwara mjini akiwa amebeba bango lake.
Baadhi ya askari wakiwa kwenye gari yao wakiangalia usalama wa hapa na pale kufuati maandamano makubwa yaliyofanywa na wakazi wa Mkoa wa Mtwara,wakipinga gesi kusafirishwa kwenda jijini Dar!

I AM SINGLE AND READY TO MINGLE! - SPORAH SHOW

Libeneke jipya la malumbano ya hoja

$
0
0

Tunaukaribisha mwaka 2013 kwa kuwaletea ubao mpya wa malumbano ya hoja:

Filosofa Forum (http://www.filosofaforum.com/)

Katika fani hii ya mawasiliano, iwe kwa blog za jamii, barua pepe, magazeti, tovuti na aina nyingine nyingi, jambo moja ambalo baadhi yetu wadau wa malumbano ya hoja tungependa kuweka juhudi kulibadilisha katika mwaka huu mpya 2013, ni jukwaa la habari, mipasho (malumbano) ya kisiasa, kimichezo, na utani wa kikabila, wenye ustaarabu na maadili yaliyopevuka bila kudhihaki jinsia, dini, maumbile au kabila la mtanzania yeyote. 

Awe mtoto, kijana, mzee, mvulana, msichana, mwanaume au mwanamke, Filosofa Forum inaamini sisi sote ni matokeo ya uumbaji wa mwenyezi mungu.

Hivyo basi  kama unaamini kwa dhati kuwa huu ndo mwelekeo unaostahili katika malumbano ya hoja bila vioja, hapa ndio mahali muafaka ambapo mijadala ya aina zote itazingatia maadili , uwazi, na kuheshimu tofauti za kiitikadi, dini , na tamaduni zote za mtanzania.

KARIBUNI SANA UELIMIKE NA KUELIMISHA WENGINE

Happy New Year 2013
By Filosofa Forum team.

Last Pool And Beach Party Of the Year at Azura Beach

$
0
0
So grab your swimsuits and come get WeTT @ thE Last " HOT & WET POOL & BeACH Xperience @ the most beautiful AZURA Beach (next 2 kawe bridge) From 11:30am-8pm!

Entry: 10,000 inclusive of Water! Barbecue, 2$ Cocktails, Music by Dj SuMMeR, HOTT People Getting WETT all day by the Pool or at the beach! Grab a friend n Come enjoy the Xperience! Oh yea..U can Bring UR Own BottLes! Can't Beat That!

HaPPy New Year!
DONT MISSSSSS!!!!

DEATH ANNOUNCEMENT

$
0
0

The family of Mama Joyce Kibaja with heartfelt sadness, Announce the death of their beloved Father Dr.Julius Vincent Kibaja who passed away on 22/12/2012 at Muhimbili Hospital, His memorial ceremony will take place on 28/12/2012 at his home Mlalakuwa survey at 9:00 am and then at St. Nicholaus church ilala at 12:00 pm, His body will be laid to rest on 29/12/2012 to his home town Kwemhosi kigunga village Muheza.

May almighty father rest his soul in peace, 

Amen…..John 11;25.

MAKACHERO KUTOKA DAR WATUA ZANZIBAR KUCHUNGUZA SHAMBULIO LA PAROKO

$
0
0
Na Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi Zanzibar

Makao Makuu ya Jeshi la Polisi Dar es Salaam, imetuma timu ya Makachero kuja Zanzibar kuungana na wenzao wengine wa Polisi Zanzibar katika Upelelezi wa tukio la kushambuliwa kwa Paroko wa Parokia ya Mpendae Amrose Nkenda (pichani).

Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Zanzibar ACP Yusuf Ilembo, amesema kuwa timu hiyo ambayo inaongozwa na Afisa mmoja wa ngazi ya juu (hakumtaja jina) ina jumla ya Makachero watano waliobobea katika masuala ya upelelezi hapa nchini.

Amesema kuwa nia ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini Inspekta Jenerali Saidi Mwema, kuituma timu hiyo kuja hapa Zanzibar, ni kutaka kuengeza nguvu katika tukio hili ambalo linatazamwa kwa aina tofauti hasa ikizingatiwa kuwa aliyeshambuliwa ni Kiongozi mkubwa wa dini na limetokea katika kipindi cha siku kuu ya Krismas.

Amesema Jeshi la Polisi limeamua tukio hili kupelelezwa kwa pamoja kati ya wenzao wa makao makuu ya Polisi Dar es salaam na wa hapa Zanzibar ili kuhakikisha kuwa wale wote waliohusika katika kumshambulia Paroko huyo wanakamatwa.

Hata hivyo kamanda Ilembo amesema kuwabado Polisi wanaendelea na Upelelezi wa kubaini sababu za kushambuliwa kwa Paroko huyo bila ya kuibwa kwa kitu chochote kutoka kwa mshambuliwa.

Amesema kuna uwezekana kuwa watuhumiwa wameshindwa kuchukua kitu chochote baada ya kubaini kuwa eneo la tukio lisingekuwa salama kwao kwa vile kulikuwa na walinzi na ni eneo ambalo ni karibu kabisa na makazi ya viongozi wengine wa dhehebu hilo.

Akizungumzia siku kuu ya mwisho wa mwaka 2012 na mwanzoni mwa mwaka 2013, Kamanda Ilembo amewahimiza wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa pale wanapobaini kuwepo kwa wahalifu ili wachukuliwe hatua.

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Mjini Magharibi Zanzibar ACP Aziz Juma Mohammed, amewatahadharisha wazazi na walezi kutowaruhusu watoto wadogo kuranda barabarani ama kwenda katika fukwe za bahari kuogelea pasipo uangalizi wa watu wazima.

Kamanda Aziz amesema kuwa uzoefu unaonyesha kuwa watoto wengi wamekuwa wakigongwa na magari ama kuzama na kufa maji katika siku hizi za siku kuu za mwisho wa mwaka kwa kukosa uwangalizi wa watu wazima.

Aidha amewataka wananchi kutoziacha nyumba zao wazi ama bila ya kuwa na uwangalizi wa kutosha ili kutowapa nafasi kwa wahalifu kupata fursa ya kuwaiba.

HOJA YA MDAU : Heshima ya Taifa Inadharauliwa

$
0
0
Mpendwa,

Katika kuzingatia misingi ya nchi yangu popote pale nitakapokuwa katika ulimwengu huu; kuheshimu na kuthamini mchango wa mapambano ya mashujaa wetu katika kujikomboa kutoka makucha ya wakoloni,sina budi kusimamia kwa kadri ya uwezo wangu heshima kubwa tuliyonayo. 

Kuna mambo kadha wa kadha ambayo nawajibika nayo, ila mojawapo ni kuona taifa langu halihujumiwi na linaheshimiwa kwa kadri ile ile ambayo naweza kuipigania.

Siku chache zilizopita nilizunguka katika Supermarket moja hapa jijini changchun china, ambako nimekua kwa kadri ya mwaka sasa nikifanya masomo ya elimu ya juu. 

Kwa hakika kuna mazuri mengi ambayo najifunza hapa, na pia yale ambayo waswahili wanasema 'ukishangaa ya musa utayaona ya firauni", kwa yumkini yote ni sehemu ya kujifunza kwangu.


Aidha katika pitapita hiyo sokoni hapo, nikaona bidhaa moja ambayo iliniuma sana, ila nikaona niweke wazi ili nipate kujua ukweli kwa wadau na wazalendo wengine huko nyumbani. Suala lenyewe ni matumizi ya nembo ya taifa ambayo ikiwa imechakachuliwa kidogo ikitumika kama alama (logo) ya mvinyo mmoja hapa china.


Nilinunua mvinyo huo ambao kiukweli una majina haya "DongaDa Wine" " Tonghuadongda wine", "Red Wine" ili nipate kuweka kumbukumbu za digitali kama ushahidi ambao unaonyesha maelezo zaidi ya mvinyo huo ambao unatumia nembo ya taifa langu.


Kwa hakika nilijiuliza maswali mengi sana ila machache ni haya; (i) Je ni kweli nyuma ya nembo hii kuna kampuni lolote la Tanzania ambalo linaebndesha biashara ya bidhaa hii hapa china? (ii) Je kuna haki au uhalali wowote wa kuchakachua nembo ya taifa kwa maslahi binafsi aidha kwa mtu mmoja mmoja ndani na nje ya Tanzania? (iii) Je inapotokea hali hii ima kwa muhusika kutoka Tanzania au nje ya Tanzania, ni hatua gani zinatakiwa kuchukuliwa?


Kwa hakika najua habari hii yaweza kuwa na mitazamo mingi na mawazo mnyumbuko, ila swali la msingi je hii ni heshima kwa Taifa letu? Napenda kugawana picha za bidhaa hii ya DongDa Wine ili watanzania wajionee wenyewe tunavyochakachuliwa.

Nipo tayari kutoa ushirikiano zaidi wa habari hii kwa maswali yatakayojitokeza

Patriotspy.

Warsha kwa Maafisa wa Mipakani yafanyika Mwanza

$
0
0
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua Warsha kwa maafisa wa mipakani kuhusu usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na Bioteknolojia ya kisasa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Julius Ningu na kushoto ni Afisa Mazingira Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Esta Makwaia. Warsha hii imefanyika leo kwenye Hotel ya La kairo jijini Mwanza.
Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya Usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa wakimsikiliza Mgeni Rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava [pichani hayupo] kwenje Hoteli ya La kairo Jiji Mwanza.
Washiriki wa Warsha ya Usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na bioteknolojia ya kisasa wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi (katikati) Mara baada ya kufungua warsha hiyo kwenye Hoteli ya La kairo Jiji Mwanza.
Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Ngosi Mwihava akifungua Warsha kwa maafisa wa mipakani kuhusu usimamizi wa mazao na bidhaa zitokanazo na Bioteknolojia ya kisasa. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira Dkt. Julius Ningu na kushoto ni Afisa Mazingira Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Esta Makwaia. Warsha hii imefanyika leo kwenye Hotel ya La kairo jijini Mwanza.

Zuku Adds Clouds Media Group

$
0
0

Zuku Pay TV, the leading Pay TV provider in Tanzania, has today announced that it has added Clouds TV and Clouds FM to its local channels to its bouquet of TV channels and radio channels respectively. Clouds TV is now found on Channel 27 while Clouds FM is now available on the audio channels of Zuku. The local channels now available include TBC, Chanel 10 and Clouds TV.


Fadhili Mwasyeba, Country Manager Zuku said, “We are excited that Clouds Media Group has partnered with us and now Tanzanians can enjoy their products from our Pay TV platform.” He added, “We are committed to adding local content on our Zuku platform and are looking forward to making more strategic partnerships here in Tanzania.”

In addition Zuku Pay TV has over 3,000 subscription agents across the country following their partnership agreements with MaxMalipo and Selcom. This is in addition to the existing payment options with Vodacom and Tigo.

Currently, the Zuku is running the customer reward programme “Zuku Tunakuthamini – Pata TV Bure” which seeks to reward their customers for their service and loyalty to the programme. Customers are guaranteed of winning 22 inch and 44 Inch Flat Screen TV for introducing five (5) or (10) customers respectively.
Zuku Pay TV offers a wide selection of entertainment channels covering news, sports, movies, documentaries and music. These include various 3rd party channels such as BBC, MTV Base, Setanta Sports, MGM Movies and E to name but a few.

The provider also offers many of its own tailor-made channels such as Zuku Africa airing African content, Zuku Life airing documentaries, Zuku Sports as well as a number of themed movie channels. The service is available via satellite throughout Tanzania.

KUMBUKUMBU

$
0
0
Ni miaka 10 imepita tangu ulipotutoka mpendwa wetu Leutenant Colonel Jonathan Nassoro Kambi.Hatutasahau,upendo,ucheshi na busara zako daima. 

Unakumbukwa sana ma Mke wako Ndumiakunda,Wanao Baraka,Wema,Michael na Emmanuel.Nduguzo; Godfrey,Hadija,Pili na Haeshi,Wajukuu zako: 

Salome,Jerry,Ray,Deborah,Junior,Joshua,Lightness na Baby, ndugu, jamaa na marafiki. UJUMBE:Tunakumbuka Ujasiri wako,mwanga wa milele ukuangazie,upumzike kwa amani.

-amina.

MSANII RICH MAVOCAL AWASHUKURU WADAU WA MUZIKI

$
0
0
Msanii Richard Lusinga (a.k.a - Richie Mavoko) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), wakati akitoa shukrani kwa niaba ya Kampuni yake ya Aljazerra Entertaiment, katika shukurani zake amesema," kama msanii wa kizazi kipya amewomba radhi kwa wote aliowakosea na yeye pia amewasemehe" Pamoja na Kushukuru kampuni ya Aljazerra Entertaiment, waandishi wa habari na wadau wote wa muziki nchini, kwani ndio waliomfikisha hapo alipofikia na kuahihidi atazidi kuboresha na kuwaletea nyimbo kali zaidi washabiki wake katika mwaka wa 2013.Richie Mavoko anatamba na nyimbo zake kama Mbona silai,Folo folo me,one time na Mery me . (kushoto ) Ni Msanii Mwanaisha Nyange (a.k.a DYANA).
Msanii wa kike anaechipukia na kung"ara katika fani ya muziki nchini Tanzania, Mwanaisha Nyange (a.k.a- Dyana) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani), ametoa shukranii zake kwa Aljazerra Entertaiment kwa kumsaidia kumtoa msanii huyo kimuziki , bila ya kuwasahau, wadau mbalimbali wote wa muziki nchini ambao amesema ndio waliomsaidia kumfikisha hapo alipo sasa katika sanaa hii ya muziki huu wa kizazi kipya , kwani bila ya kupata ushirikiano wao asingeweza kufikia hapa alipo. . (kushoto) ni Msemaji wa Aljazerra Entertaiment Simon John .

Naibu Waziri apokea Hati za Utambulisho za Mwakilishi mpya wa UNHCR nchini

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akipokea Hati za Utambulisho kutoka kwa Bibi Joyce Mends-Cole, Mwakilishi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) hapa nchini. Hafla hiyo fupi ilifanyika leo Wizarani.
Mhe. Mahadhi akizungumza na Bibi Mends-Cole mara baada ya kupokea Hati za Utambulisho.
Bibi Mends-Cole akifafanua jambo kwa Mhe. Maalim wakati wa mazungumzo yao.
Maafisa kutoka Ofisi za UNHCR hapa nchini waliofutana na Bibi Mends-Cole (hayupo pichani) alipofika Wizarani kuwasilisha Hati za Utambulisho. Kushoto ni Bi. Linmei Li  na Bi. Janet Sato-Prima.
Maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Ali J. Mwadini na Bi. Ramla Khamis wakinukuu masuala mbalimbali wakati wa mazungumzo kati ya Mhe. Maalim na Bibi Mends-Cole (hawapo pichani).
Mhe. Maalim akiagana na Bibi Mends-Cole mara baada ya mazungumzo yao.

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI TOKA TFF LEO

$
0
0

KLABU ZASUBIRI FEDHA ZAO TRA ZICHEZE LIGI KUU
Klabu 14 ambazo timu zao zinashiriki Ligi Kuu ya Vodacom zimesema hazitacheza hatua ya pili ya Ligi hiyo inayotarajiwa kuanza Januari 26 mwakani hadi zitakaporejeshewa fedha zao zilizochukuliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kutoka kwenye moja ya akaunti za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

Novemba 23 mwaka huu, TRA kwa uwezo ilionao kisheria iliielekeza benki ya NMB kuilipa fedha hizo (sh. 157,407,968) kutoka kwenye moja ya akaunti za TFF ikiwa ni Kodi ya Lipa Kama Unavyopata (PAYE) kutoka kwenye mishahara ya waliokuwa makocha wa timu za Taifa.

Serikali ndiyo inayolipa mishahara ya makocha hao moja kwa moja kwenye akaunti zao, lakini ilikuwa haikati PAYE kutoka kwenye mishahara hiyo, hivyo malimbikizo kufikia sh. 157,407,968.

TFF bado inaendelea na mazungumzo na pande husika (Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa upande mmoja na TRA kwa upande mwingine) ili fedha hizo zirejeshwe kwani zilitolewa na mdhamini wa Ligi Kuu (kampuni ya Vodacom) kwa ajili ya maandalizi ya timu hizo tayari kwa mzunguko wa pili wa Ligi hiyo.

OFISA WA CAF KUTUA MWAKANI KUKAGUA VIWANJA
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) litamtuma nchini ofisa wake Abbas Sendyowa kukagua viwanja na hoteli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa utaratibu wa klabu kupata leseni zitakazoziwezesha kushiriki michuano inayoandaliwa na Shirikisho hilo.

Ofisa huyo kutoka Uganda atawasili nchini Januari 7 mwakani ambapo anatarajiwa kukamilisha kazi hiyo Januari 14 mwakani na baadaye kupeleka ripoti yake CAF.

Utekelezaji wa kazi yake nchini utahusisha mwakilishi kutoka TFF, mwakilishi kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, mameneja wa viwanja husika na Ofisa Usalama wa TFF.

NAZARIUS KILUNGEJA AONDOLEWA UCHAGUZI RUREFA
Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imekubaliana na uamuzi wa Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Rukwa (RUREFA) kumuondoa Nazarius Kilungeja kugombea uenyekiti katika uchaguzi wa chama hicho.

Kutokana na uamuzi huo, Kamati ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA kuendelea na mchakato wa uchaguzi huo kama ilivyopangwa awali.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

PROF. BRUNO J. NDUNGURU TO BE LAID TO REST SATURDAY IN DAR ES SALAAM

$
0
0
PROF. BRUNO J. NDUNGURU


THE FAMILY OF PROF. BRUNO J. NDUNGURU REGRET TO ANNOUNCE THE SAD DEATH OF THEIR BELOVED, PROF. BRUNO J. NDUNGURU WHO PASSED AWAY ON WEDNESDAY 26TH DECEMBER AT AMI HOSPITAL IN DAR ES SALAAM.

THE WAKE WILL BE HELD AT HIS RESIDENCE AT  BOKO IN DAR ES SALAAM.

HIS BURIAL WILL TAKE PLACE  ON SATURDAY 29TH DECEMBER 2012 AT THE KINONDONI CEMETERY IN DAR ES SALAAM.

WHAT GOD GIVES, GOD TAKES. MAY HIS SOUL REST IN ETERNAL PEACE.

FOR MORE INFORMATION CALL:  0754 300408  - COLLETA

Mhe Makala akutana na viongozi wa tasnia ya filamu

$
0
0
Naibu Waziri wa  Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mheshimiwa Amos Makala akiongea na Viongozi wa Mashirikisho ya tasnia ya Filamu na Muziki Jijini Dar es Slaam leo juu ya Urasimishaji wa Tasnia hiyo.(Picha na Benjamin Sawe wa WHVUM)
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live


Latest Images