Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110152 articles
Browse latest View live

WAZIRI WA UJENZI MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI (Mb) KUZURU MIKOA YA MWANZA NA MARA

$
0
0
Wizara ya Ujenzi napenda kutoa taarifa ka umma kuwa Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (Mb) anatarajia kufanya ziara ya kukagua miradi  mbaimbali ya Maendeleo katika  mkoa wa Mwanza na Mara.
Mheshimiwa Waziri Magufuli ataanza ziara yake Mkoani Mwanza tarehe 06 Julai ambapo atakagua mradi wa Ujenzi wa barabara ya Usagara – Kisesa (by pass) yenye urefu wa km. 16.7 inayojenga kwa kiwango cha lami.

Siku inayofata tarehe 07 Julai, Mheshimiwa Waziri ataelekea mkoani Mara kukagua  mradi wa barabara ya Makutano – Natta – Mugumu (sehemu ya Makutano – Sanzate km 50).

Siku hiyo hiyo mchana Dkt. Magufuli  atazindua rasmi kivuko cha MV. Mara kitakachotoa huduma kati ya Iramba na Majita.

Aidha, baada ya uzinduzi huo  Mheshimiwa  Waziri wa Ujenzi atafanya  mkutano wa hadhara na kuongea na wananchi wa eneo la Mwibara ikiwa ni sehemu ya ukaguzi wa mradi wa Barabara ya  Nyamuswa – Bunda – Kisorya – Nansio (sehemu ya Bulamba – Kisorya km 51).

Mheshimiwa Magufuli ataendelea na ziara yake tarehe 09 Julai Mkoani Mwanza ambapo atazindua kivuko cha MV. Temesa katika eneo la Nyegezi(Sweya).

Kivuko hicho kimefungwa mitambo ya kukiwezesha kusafiri kwa mwendo wa kasi ili kukiwezesha kutoa huduma katika mwambao huo wa ziwa Victoria. Aidha, Kivuko hicho chenye uwezo wa kubeba Tani 65 ambazo ni sawa na abiria 80 na magari madogo matano kwa wakati mmoja.

Kivuko hicho kitakuwa kinafanya kazi kutoka Luchelele kupitia Sweya, Butimba, Mkuyuni, Igogo hadi Kirumba ikiwa ni mkakati wa kupunguza foleni katika jiji la Mwanza.


NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI WIZARA YA UJENZI


05/07/2014


JK Atembelea Banda la Mambo ya Nje, Sabasaba

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Kikwete akiwasili kwenye Banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwenye viwanja vya Sabasaba
Rais Dkt. Kikwete akiweka saini kwenye kitabu cha wageni katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje
Rais Kikwete (Mwenye Koti la Blue) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Taasisi zake.
Mtumishi Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mbwana Msingwa akiweka saini katika kitabu cha wageni alipokuja na familia yake kwenye banda la Mambo ya nje lililopo kwenye viwanja vya sabasaba
Ankal akisalimiana na Afisa Mawasiliano Ally kondo, alitembelea Banda la Mambo ya Nje katika Viwanja vya Sabasaba. Picha na Reginald Philip

Maalim Seif atembelea masoko ya manispaa ya Zanzibar.

$
0
0
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea kuridhishwa kwake na uwepo wa vyakula na matunda yenye viwango kwa ajili ya mwezi mtuku wa Ramadhani. Hata hivyo amesema bei zake bado ziko juu ikilinganishwa na kipato cha wananchi, na kwamba wananchi walio wengi wanashindwa kumudu kununua bidhaa hizo. 
Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya kutembelea masoko mbali mbali ya manispaa ya mji wa Zanzibar, kuangalia hali ya upatikanaji wa bidhaa na matunda, ambayo hutumika sana katika mwezi wa Ramadhan. 
Amewashauri wakulima na wafanyabiashara kuzingatia hali za maisha ya wananchi, na kuangalia uwezekano wa kupunguza bei, ili wananchi waweze kumudu kununua bidhaa hizo. 
“Sitaki niwambie kuwa wauze kwa hasara, lakini wapunguze kuingiza faida nyingi ili kila mwananchi aweze kumudu kununua, na wakifanya hivyo inaweza kuwa sadaka nzuri kwao katika mwezi huu wa Ramadhan”, alisisitiza Maalim Seif na kuongeza, “Nashkuru katika bidhaa nilizoziona ziko katika kiwango cha kuridhisha, na sijaona dalili ya ndizi au matunda mengine yaliyochomwa moto”, alisema. 
Amesema Serikali imetoa fursa ya soko huria kwa wafanyabiashara, na kwamba upandaji wa bei kwa bidhaa hizo unayokana na wakulima na wafanyabiashara wenyewe. Akizungumzia kuhusu upatikanaji wa vitoweyo, Maalim Seif amesema hali hairidhishi, kwa vile samaki waliopo ni wachache, na hivyo kuuzwa kwa bei ya juu. 
Kuhusu uvumi wa kuwepo kampuni inayotaka kuingiza samaki kutoka nje ya Tanzania na kuuzwa kwa bei nafuu, na kuwepo madai kuwa kampuni hiyo imezuiwa na Serikali, Maalim Seif amesema yeye hana taarifa hiyo, lakini ikiwa kuna ukweli wowote inawezekana kuwepo sababu za msingi kwa Wizara inayohusika kufanya hivyo.
 Aidha Maalim Seif ameelezea kuridhishwa na maendeleo ya soko la Mombasa ambalo linaendelea kufanyiwa matengenezo makubwa ambayo yatasaidia kutunza hadhi ya soko hilo la matunda. Hata hivyo ameelezea kutoridhishwa na hali ya usafi katika soko la samaki Malindi, na kuliagiza Baraza la Manispaa kuweka utaratibu mzuri wa kulitunza eneo hilo la kuuzia samaki, ili liwe katika hali ya usafi wakati wote. Baadhi ya wafanyabiashara wameiomba serikali kuwawekea mazingira bora ya kufanya biashara zao, sambamba na kulalamikia baadhi ya wafanyabiashara waliorejea soko la Mwanakwerekwe baada ya kuhamishiwa katika soko la Mombasa. 
Katika ziara hiyo Maalim Seif ametembelea soko la matunda Mombasa, soko Kuu la Mwanakwerekwe, Kituo cha biashara Saateni na Soko Kuu la Darajani. Wakati huo huo Mhe. Maalim Seif amewatembelea na kuwafariji watoto yatima wanaolelewa na jumuiya ya Muzdalifat katika eneo la Amani mjini Zanzibar. Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdallah Hadhir Abdallah ameishukuru serikali kwa mashirikiano waliyonayo kwa jumuiya hiyo, na kuiomba kuongeza misaada yake ili kuwaendeleza watoto yatima wanaolelewa katika vituo mbali mbali vya Zanzibar.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiulizia bei ya samaki na pweza katika soko la Darajani, akiwa katika ziara yake ya kutembelea masoko ya manispaa ya Zanzibar.
 Mfanyabiashara wa muhogo na majimbi, akitoa bei ya bidhaa hizo wakati Maalim Seif alipofanya zaira ya kutembelea soko la Mwanakwerekwe.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia biashara ya mitumba katika kituo cha biashara Saateni, akiwa katika ziara yake ya kutembelea masoko ya manispaa ya Zanzibar.
 Mfanyabiashara wa soko la matunda Mombasa, akimkabidhi boga Maalim Seif kwa ajili ya futari, wakati alipotembelea soko hilo.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiulizia bei ya samaki, akiwa katika ziara yake ya kutembelea masoko ya manispaa ya Zanzibar. Picha na Salmin Said, OMKR

HOSPITALI YA MOUNT MERU ARUSHA YAPIGWA JEKI NA BENKI YA KCB TANZANIA

$
0
0
 Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount Meru wakiwa kwenye picha ya  pamoja na wafanyakazi wa benki ya KCB Tanzania tawi la Arusha baada ya kupokea msaada wa kitanda maalumu chenye thamani ya shilingi Milioni 11 kwa ajili ya akina  mama kutumia wakati wa kujifungua  na vifaa tiba mbalimbali, msaada huo ulitolewa na tawi la benki hiyo mkoani arusha.
 Daktari wa kitengo maalum cha wakina mama katika hospitali ya Mount Meru ya jijini Arusha,Mathew Kasumuni(Kushoto) akiwa tayari kupokea msaada wa  kitanda na vifaa tiba mbalimbali kutoka kwa Meneja  benki ya KCB Tanzania tawi la arusha Judith Lubuva kwa ajili ya akina mama wenye matatizo ya uzazi wanaotibiwa katika hospitali hiyo.Benki hiyo pia ilitoa msaada wa kitanda kwaajili ya kinamama wakati wa kujifungulia chenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 11 kwa ubora wake kitatumika kwa zaidi ya miaka 30.

Daktari wa kitengo maalum cha wakina mama katika hospitali ya Mount Meru ya jijini Arusha,Mathew Kasumuni(Kushoto) akipokea msaada wa  kitanda na vifaa tiba mbalimbali kutoka kwa Meneja  benki ya KCB Tanzania tawi la arusha Judith Lubuva kwa ajili ya akina mama wenye matatizo ya uzazi wanaotibiwa katika hospitali hiyo.Benki hiyo pia ilitoa msaada wa kitanda kwaajili ya kinamama wakati wa kujifungulia chenye thamani ya zaidi ya shilingi Milioni 11 kwa ubora wake kitatumika kwa zaidi ya miaka 30.

Balozi seif ali Iddi atembelea Kijiji cha Kilombero

$
0
0
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar { ZECO } Nd. Hassan Ali Hassan alisema shirika lake linakusudia kutumia rasilmali ilizonazo katika kuhakikisha huduma za umeme zinapatikana kwenye kisima cha maji cha Kijiji cha Kilombero ili kuwaondoshea usumbufu wa huduma za maji safi  kwa Wananchi wa Kijiji hicho. 
Alisema kazi hiyo itakayoanza wakati wowote kuanzia sasa inatarajiwa kukamilika sambamba na ulazwaji wa mabomba ya maji utakaofanya na wahandisi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } kutoka kwenye kisima hicho hadi maeneo ya wakaazi wa Kijiji hicho. 
Nd. Hassan Ali Hassan alitoa kauli hiyo mara baada ya kupokea hundi ya shilingi Milioni 14,000,000/- zilizotolewa na Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi kupitia mfuko wa Jimbo ili kuanza kazi za kukipatia umeme kisima hicho kilichopo ndani ya shamba la ASP mashariki mwa Kijiji cha Kilombero. Alisema licha ya gharama halisi zinazohitajika katika mradi huo wa umeme zinayokadiriwa kufikia zaidi ya shilingi Milioni 60,000,000/- ikijumuisha nguzo, waya pamoja na transfoma lakini shirika litajitahidi katika kuona mradi huo unafanikiwa ili umeme upatikane katika kisima hicho. 
Mapema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Garu alisema kisima hicho tayari kimeshakamilika kwa muda mrefu sasa, lakini kilichobakia ni kusambazwa kwa mabomba kazi itakayochukuwa muda kidogo. 
Akizungumza na wananchi wa kijiji hicho cha Kilombero Mbunge wa Jimbo la Kitope ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwapongeza wanakiji hao kwa ustahamilivu wao mkubwa wa kukosa huduma za maji safi na salama kwa muda mrefu. Zaidi ya shilingi Milioni 20,000,000/- zilizotolewa na Mbunge wa jimbo la Kitope Balozi Seif zimetumika kugharamia ujenzi wa kibanda cha kisima hicho kilichochimbwa na Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA }.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maji Zanzibar { ZAWA } Dr. Mustafa Garu akitoa ufafanuzi kwa wananachi wa Kijiji cha Kilombero Wilaya ya Kaskazini “ B “ juu ya hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa kisima cha maji safi na salama cha kijiji hicho.
Ufafanuzi huo aliutoa wakati wa hafla fupi ya Mbunge wa Jimbo la Kitope Balozi Seif Ali Iddi kukabidhi  hundi  ya shilingi milioni 14,000,000/- kwa ajili ya uwekwaji wa huduma za umeme katika Kisima hicho.
 Mbunge wa Jimbo la Kitop[e ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwapongeza wananchi wa Kijiji cha kirombero kwa ustahamilivu wao wa muda mrefu kutokana na ukosefu wa huduma ya maji safi yanayotarajiwa kupatikana muda si mrefu kijijini hapo.
Balozi Seif akimkabidhi Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar Nd. Hassan Ali Hassan Hundi ya shilingi Milioni 14,000,000,/- kwa ajili ya uwekwaji wa huduma za umeme kwenye kisima cha maji cha kijiji cha Kilombero.
Aliyepo kati kati yao ni Mkuu wa Wilaya ya Kaskazini “B “ Nd. Khamis Jabir Makame. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

The United Nations Population Fund (UNPF) has a new Country Representative in Tanzania

$
0
0
The United Nations Population Fund has a new Country Representative - Dr. Natalia Kanem. She presented her credentials to the Minister of Foreign Affairs, Bernard Membe, on Friday 4th of July 2014. at the Minister's office in Dar es salaam.
Dr. Natalia Kanem. She presents  her credentials to the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Hon. Bernard Membe
Dr. Natalia Kanem smiles as  the Minister for Foreign Affairs and International Cooperation Hon. Bernard Membe holds a small gift she has presented to him.

BRIEF BIO
Dr. Natalia Kanem is a women and children’s health advocate with over two decades of leadership roles in international philanthropy. In her early medical career she focused on maternal and pediatric HIV and AIDS research and clinical practice.
Dr. Kanem most recently was a senior associate at the Lloyd Best Institute of the West Indies, based in Trinidad and Tobago. From 2005-2011, she served as founding president of the ELMA Philanthropies, a major donor group promoting health and education for African children and youth. 
During thirteen years at the Ford Foundation, Dr. Kanem served as their Representative for West Africa based in Nigeria, and in New York headquarters as head of international grants administration and Deputy Vice President for global peace and social justice programs. 
She also convened the Council on Foundations-European Foundation Center’s task force on accountability in philanthropy. 
Earlier she had co-founded the Harlem Center for Health Promotion, during her joint appointment at Columbia University’s schools of medicine and public health. This led to her involvement as a researcher with the first successful drug trials for maternal and pediatric HIV treatment. 
 A magna cum laude history and science graduate of Harvard, Dr. Kanem received her medical MD degree from Columbia University and her Masters in Public Health in epidemiology and preventive medicine from the University of Washington. 
She has been honored by organizations such as the American Medical Association, the University of Washington, the Asia-Pacific Islanders Community Health Agency (New York) and the African Women's Development Fund.


Rose Muhando kupeleka Pindo la Yesu Mwanza

$
0
0

MWIMBAJI mahiri nchini, Rose Muhando anatarajia kutambulisha kwa mashabiki wake albamu ya Kamanda Pindo la Yesu Agosti 10 mwaka huu Uwanja wa CCM Kirumba Mwanza.

Albamu hiyo itazinduliwa Agosti 3 mwaka huu ukumbi wa Diamond, Jubilee Dar es Salaam na baada ya hapo itatambulishwa katika mikoa kadhaa nchini.

Taarifa ya mwimbaji huyo kwa vyombo vya habari jana, ilieleza kuwa tayari mkoa wa Mwanza umekuwa chaguo lake la kwanza baada ya uzinduzi wa Dar es Salaam.“Nitazindua Diamond Jubilee Agosti 3, baada ya hapo nitaenda Mwanza Agosti 10 Uwanja wa CCM Kirumba, naomba mashabiki wangu wajiandae kupata vitu vizuri sana.“Nimejipanga kuhakikisha nawapa burudani ya nguvu, najua nini wanakitaka, pia najua waimbaji gani wanawapenda, nipo katika utaratibu wa kuhakikisha wanafurahi,” alisema Muhando.

Kwa mujibu wa Muhando, nyimbo zilizopo katika albamu yake ya Kamata Pindo la Yesu ni Bwana Niongoze, Wewe Waweza, Usiniache, Nibariki, Muongo, Kwema, Kamata Pindo la Yesu na Facebook.

Hivi sasa Muhando anatamba na albamu yake ya Utamu wa Yesu yenye nyimbo saba, ambazo ni Utamu wa Yesu, Raha Tupu, Tamalaki, Ndivyo Ulivyo, Woga Wako, Imbeni na Kusifu na Achia.

Mbali na Utamu wa Yesu, Rose Muhando pia amewahi kutamba na albamu za Uwe Macho, Nyota ya Ajabu (Zawadi ya Krismasi) na Jipange Sawasawa, Kitimutimu, Mungu Anacheka, Wololo.Pia amepata kung’ara katika wimbo wa Vua Kiatu, alioshirikiana na Anastazia Mukabwa wa Kenya.

WAKAAZI WA MTO WA MBU NA WAFANYAKAZI WA HIFADHI YA ZIWA MANYARA WASHIRIKI KUTUNZA MAZINGIRA

$
0
0
Wakaazi wa kata ya Mto wa Mbu waliwapongeza wafanyakazi hao kwa kujitolea na kuacha shughuli zao kwenda kuhimiza usafi wa mazingira ya mji wao huku wakiwataka wenzao kujali usafi wa mazingira ilikuepuka magonjwa ya milipuko 
 Kwa upande wake kaimu mhifadhi wa hifadhi ya ziwa manyara Ibrahimu Yamola alisema kuwa wakazi hao ambao ni jirani na mbuga hiyo wnapaswa kuyajali mazingira wanamo ishi kwa kyaweka katika hali ya kuvutia kwani mji wao unapokea wageni mbalimbali kutoka mataifa mbalimbali wanaokuja kutembelea mbuga hizo 
 Aktanabaisha kuwa siku ya uhifadhi duniani inasherehekewa duniani kote na hapa nchini imekuwa ikisherehekewa kwa kufanya shughuli mbalimbali za ujirani mwema kama tulivyofanya leo kufanya usafi wa mazingira kuzunguka kata ya mto wa mbu
 Baadhi ya wananchi wa kata ya mto wa mbu wakiwa na wafanyakazi wa hifadhi ya ziwa Manyara wakishiriki kufanya usafi wa mazingira kwenye mji wa Mto wa Mbu ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya uhifadhi duniani
Usafi ukiendelea
Bango likihamsasisha usafi na utunzaji wa mazingira
Kila mtu bize
Bajaji likipakiwa takataka
Picha ya pamoja baada ya kusafisha kata ya Mto wa Mbu

WIZARA YA NISHATI NA MADINI YAENDELEA KUNG'ARA KWENYE MAONESHO YA SABASABA

$
0
0
 Baadhi ya washiriki kutoka Shirika la Umeme Nchini (TANESCO) na kampuni ya Max- Malipo wakiwa katika picha ya pamoja kabla ya  kuanza kwa maonesho.
 Mtaalamu kutoka  Tanzania Gemmological Centre (TGC) Bw. Prosper Tingo akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda la TANSORT
Mjiolojia kutoka Idara ya Nishati Bw. Habass Ng’ulilapi akielezea sera ya nishati kwa wananchi waliotembelea banda la Wizara.

JK ATEMBELEA BANDA LA JESHI LA MAGEREZA KATIKA MAONESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA, LEO JIJINI DAR ES SALAAM

$
0
0
 Kamishna wa Fedha na Utawala wa Jeshi la Magereza, Gaston Sanga akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza lililopo katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa, leo Julai 5, 2014 Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia Mbogamboga aina ya Kabeji ilivyostaawi katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.  
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia kiatu aina ya Buti ambacho kimetengenezwa katika Kiwanda cha Gereza Karanga Moshi, Kiwanda hicho kinamilikiwa na Jeshi la Magereza. Rais Kikwete ametembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014  katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea Jijini, Dar es Salaam.
 Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini Kitabu cha Wageni alipotembelea Banda la Jeshi la Magereza leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayofanyika katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere uliopo Jijini Dar es Salaam(wa pili kulia) ni Kamishna wa Fedha na Utawala, Gaston Sanga(wa kwanza kulia) ni Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza, Sania Kigwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akitoka katika Banda la Jeshi la Magereza alipotembelea Banda hilo leo Julai 5, 2014 katika Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea  Jijini, Dar es Salaam(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

KONGAMANO LA TATHMINI YA MIAKA 13 YA UTEKELEZAJI WA SERA MPYA YA MAMBO YA NJE LAFANYIKA DAR ES SALAAM

$
0
0
 Waziri wa Ardhi na Makazi Profesa Anna Tibaijuka akitoa mchango wake katika Mada ya Ushirikiano wa Vijana katika vyama vya Siasa Kimataifa wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.
 Mwakilishi wa Mgeni Mualikwa Balozi Joseph Sokoine akizungumza na Vijana waliohudhuria Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto,upande wake wa kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ndugu Ramadhani Madabida na kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM Tawi la Chuo cha Diplomasia Dk.Telephory Kyaruzi,Kongamano hilo lilifanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.(Balozi Joseph Sokoine alimuwakilisha Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Bernard Membe ambaye alikuwa na hudhuru)
 Wadau wakifuatilia kwa makini michango ya Mada zinazotolewa wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.
 
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam akizungumzia suala la kukuza na kuendeleza Umoja wa Afrika na kukuza Umoja wa Kiuchumi ikiwa pamoja na kuunga mkono sera ya kutofungamana na upande wowote na kuwataka Vijana wasomi kusimamia na kuchangia maoni yao katika upatikanaji wa Itikadi ya nchi.
 Mtumishi wa Mungu Askofu Isaya Joseph akifuatilia kwa makini Mada mbali mbali wakati wa Kongamano la Tathmini ya Miaka 13 ya Utekelezaji wa Sera Mpya ya Mambo ya Nje -Diplomasia ya Uchumi , Mafanikio na Changamoto lililofanyika kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dar es salaam,Julai 5.2014.

Argentina yasonga nusu fainali kwa kuibanjua Ubelgiji bao 1-0

$
0
0
Na Sultani Kipingo
Bao la dakika ya nane lililowekwa kimiani na mshambuliaji wa Napoli Gonzalo Higuain lilitosha kuipeleka Argentina kwenye nusu fainali za Kombe la Dunia walipocheza dhidi ya Ubelgiji ambayo ilishindwa kabisa kuonesha cheche zake leo jijini Brasilia.
Higuain alitumia vyema kosa la kizembe la nahodha wa Ubelgiji Vincent Kompany kuipaisha Argentina kwa jaribio lao la kwanza kwenye goli la adui.

Kompany aliupoteza mpira na Lionel Messi akauzima kabla ya kumtilia pande Angel Di Maria upande wa kulia, na nyota huyo wa Real Madrid alibahatika pale pasi yake ilipomgonga beki wa Ubelgiji Jan Vertonghen, na mpira ukajipeleka mbele ya Higuain ambaye hakufanya makosa. Pichani  Di Maria na Higuian wakimshukuru Messi ambaye pande lake lilizaa goli lao.




UZINDUZI WA MASHINE ZA ATM ZA SELCOM WAFANA KATIKA VIWANJA VYA SABASABA

$
0
0
Meneja miradi wa kampuni ya Selcom Wireless, Gallus Runyela kulia akiwaelekeza kina mama waliotembelea kutoa pesa wakati wa uzinduzi wa mashine ya ATM ya kampuni hiyo ambazo zinatoa  pesa kwa kutumia mitandao mbalimbali ya simu kama M-pesa, Tigo pesa, Airtel Money, walipo tembelea katika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere  kushoto ni Ester Kariwa na Joyce Mtema 
Mmoja ya wateja waliotembelea banda la kampuni ya Selcom Wireless, Bi,Joriet Benjamin akichukuwa fedha zake katika ATM mashine mpya za kampuni hiyo wakati wa maonesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyerere
Wafanyakazi wa Selcom kampuni ya Wireless, wakiwa katika banda lao wakati wa maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam, kwenye viwanja vya Mwalimu JK Nyererekutoka kushoto ni Juma Mgori Meneja ukuzaji biashara na masoko,Ofisa Mauzo Ally Mbaga na Meneja miradi wa kampuni hiyo Gallus Runyela.

WADAU WA TANZANIA DIASPORA WAKO NDANI YA MAONYESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA YA SABASBA.

$
0
0
Sehemu ya muonekano wa banda hilo ndani ya viwanja vya Mwalimu JK Nyerere kunakofanyuika maonyesho ya 38 ya biashara ya kimataifa ya saba saba.
  Wadau mbalimbali wakipita kwenye banda hilo kujipatia maelezo ya hapa na pale.
"Wageni wote wanakaribishwa kwenye banda la Diaspora..."anasema Bi Lucy Naivasha, ambaye ni meneja wa Tanzanite Account ya CRDB ambayo imeboreshwa kuhudumia vyema walio ughaibuni na hata wa hapa nyumbani. Banda lao lipo ndani ya banda kuu la Tanzania

tangazo kwa umma: barabara za kawawa na morocco kufungwa Jumapili na jumatatu kupisha ujenzi


Wakiwezeshwa wanawake wanaweza: Msikilize Sauda Mwilima wa Radio Free Africa, Kiss FM na Star TV akitangaza soka

$
0
0
Ni kijana mdogo lakini maarufu sana katika Star TV,  hususan katika kipindi chake cha "Bongo Beat". Pia husikika katika Radio Free Africa na Kiss FM. Akifuata nyayo za dada yake Saida Mwilima aliyekuwa mtangazaji wa TBC kabla ya kuhamia Uingereza, Sauda hivi sasa anasikika pia akitangaza mpira (Bofya mshale mwekundu umsikie). Hongera sana mdogo wetu kwa juhudi zako na kazi nzuri. Hakika unaweza kabisa kuziba pengo aliloacha marehemu Halima Mchuka, mwanamke wa kwanza kutangaza soka nchini akiwa na RTD wakati huo ambayo sasa ni TBC Taifa - Ankal

KANISA LA TAG (TANZANIA ASSEMBLIES OF GOD) LAKABIDHI MSAADA WA VYANDARUA 1300 KWA HOSPITALI NA VITUO VYA AFYA MKOANI RUKWA

$
0
0
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji Nestory Watua akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka vyandarua 1300 vya kukinga mbu waenezao Malaria kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya tarehe 04/07/2014. Msaada huo ni sehemu ya vyandarua 8550 vitakavyotolea na Kanisa hilo kwa Mikoa ya Mbeya, Njombe na Rukwa katika kuadhimisha  Jubilee ya miaka 75 ya Kanisa hilo nchini. Pamoja na zoezi la ugawaji vyandarua hivyo maadhimisho hayo yataenda sambamba na zoezi la uchangiaji damu na huduma mbalimbali za kiroho.
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Methew Sedoyyeka akizungumza katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano ambapo amelishukuru kanisa hilo kwa mchango walioutoa wa kuunga mkono juhudi za Serikali katika mapambano dhidi ya malaria. Ameziomba taasisi zingine binafsi kuiga mfano huo kwa kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuleta maendeleo hapa nchini. Katika hatua nyingine amepiga marufuku matumizi mabaya ya vyandarua ikiwemo tabia ya kuzungushia kwenye bustani za mbogamboga ambapo amezitaka mamlaka husika kuwakamata watu wa aina hiyo na kuwachukulia hatua kali kutokomeza tabia hiyo.
Muwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya katika hafla hiyo fupi ya makabidhiano Ndugu Methew Sedoyyeka ambae ni Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga akizungumza katika hafla hiyo ambapo amewataka viongozi wa Serikali na wananchi kuhamasishana kwenye shughuli za usafi na uhifadhi wa mazingira ili kutokomeza mazalia ya mbu waenezao Malaria na ugonjwa hatari wa Dengue. 
Askofu wa Kanisa la Tanzania Assemblies of God (TAG) Jimbo la Rukwa Mchungaji Nestory Watua akizungumza katika hafla hiyo muda mfupi kabla ya kukabidhi vyandarua 1300 kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa tarehe 04/07/2014. Alisema kuwa Kanisa la TAG lilizaliwa Igale Mkoani Mbeya mwaka 1939 na sasa  linaadhimisha Jubilee ya miaka 75 ambapo kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni "Mungu anajali roho yako na mwili wako, jenga mahusiano nae"
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dkt. Mtika akifanya utambulisho wa wenyeji katika hafla hiyo.
Vyandarua 1300 vilivyokabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa na Kanisa la TAG, vyandarua hivyo vitagawiwa katika hospitali, vituo vya afya na zahanati zilizoainishwa Mkoani Rukwa. 
Picha ya pamoja.

JK atembelea banda la NSSF, avutiwa na mradi wa ujenzi wa mji wa kisasa wa Dege Eco Village, kigamboni

$
0
0
 Banda la NSSF linavyoonekana kwa nje.
 Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika banda la Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF)
 Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na watoto wa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Dk. Ramadhani Dau wakati alipotembelea banda la NSSF. Kutoka kushoto ni Abeid, Zhulkifir na Thamrat Dau. 
Rais Jakaya Kikwete  akipata maelezo kutoka kwa Mhandisi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Julius Nyamuhokya kuhusu mradi mkubwa wa ujenzi wa  mji wa kisasa unaojulikana kwa jina laDege Eco Village utakaokuwa na nyumba za kuishi 7000 katika eneo la Dege Kigamboni jijini Dar es Salaam, mradi huo unatekelezwa kati ya NSSF kwa ushirikiano na kampuni ya Azimio. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NSSF,Abubakar Rajabu na wa pilikushoto ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt Abdallah Kigoda. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

lengo la swaum

IJUE HISTORIA YA GLOBU YA JAMII (CHANGAMOTO)

$
0
0
Mahojiano na Vijimambo Agosti 2011
Viewing all 110152 articles
Browse latest View live




Latest Images