Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 486 | 487 | (Page 488) | 489 | 490 | .... | 3272 | newer

  0 0


  0 0

   Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), akiwa katika picha ya pamoja na Mgeni Rasmi Mhe. Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na Ulaya katika ukumbi wa Kenyata International Convention Centre hivi karibuni jijini Nairobi, Kenya. Kushoto kwa Rais Kenyata ni Rais wa Baraza la Mawaziri wa Umoja wa Nchi za Ulaya (EU), Mheshimiwa Kyriakos Gerentopoulos. Ujumbe wa Tanzania ulishirikisha pia Mhe. Janet Mbene (Mb), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara (aliyevaa gauni la kijani).

   Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), Waziri wa Viwanda na Biashara akimshukuru Mhe. Uhuru Kenyata, Rais wa Jamhuri ya Kenya mara baada ya kufungua rasmi Mkutano wa 39 wa Pamoja Kati ya nchi za ACP na Ulaya katika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre jijini Nairobi, Kenya.  Waziri wa Viwanda na Biashara Mheshimiwa Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), na Rais wa Baraza la Mawaziri wa Nchi za Afrika, Carribean na Pacific akiongoza Mkutano wa 99 wa Baraza hilo la Mawaziri. Kushoto kwake ni Mheshimiwa Adan Abdulla Mohamed, Waziri wa Viwanda wa Jamhuri ya Kenya akifuatilia mkutano huo uliofanyika ukumbi wa Kenyatta International Conference Centre, Nairobi Kenya.

  0 0

  Maharusi wakifurahia kuanza kwa historia mpya katika maisha yao.
  Bi Harusi mtarajiwa Mebo Malakasuka (shoto)akitabasamu kwa mbaaali wakati wa sherehe ya kumuaga(Send Off)iliyofanyika katika ukumbi wa Green View jijini Dar es salaam.
  Ndugu wa karibu wa Bw Harusi Peter Steven John wakiwa katika picha ya pamoja.
  Bi Harusi mtarajiwa akasindikizwa kwenda kupumzika.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini aliyeko jijini Dar es salaam.

  0 0

   Mkurugenzi Msaidizi  Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  Bw. Robert Kibona akitoa mada wakati wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini wakifatilia mada mjini Dodoma leo.
  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu nchini imepanga  kuwachukulia hatua waajiri wote nchini kwa kushindwa kuwasilisha taarifa  za wahitimu wa elimu ya juu wanaodaiwa na Bodi hiyo.

  Hayo yalisemwa na Mkurugenzi Msaidizi  Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu  Bw. Robert Kibona alipokuwa akitoa mada kuhusu urejeshwaji wa mikopo ya elimu ya juu kwenye mkutano mkuu wa mwaka wa Wakurugenzi wa Utawala na Rasilimaliwatu Serikalini mjini Dodoma leo.
  “Mpaka sasa tumewachukulia hatua jumla ya waajiri watano ambao wameshindwa kuwasilisha taarifa za watumishi wao  wanaodaiwa na Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu” alisema Bw.Robert.

  Alisema, mwajiri atakayeshindwa kutoa taarifa za wahitimu wa elimu ya juu katika Bodi kwa wakati atatakiwa kulipa faini ya shilingi milioni saba au kutumikia kifungo kisichopungua miezi 12 au vyote kwa pamoja. Aidha,Bw. Robert alisema kuwa mpaka sasa takribani waajiriwa 18 wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kushindwa kurejesha mikopo hiyo.

  Bw.Robert alifafanua kuwa ili kufanikisha zoezi la urejeshaji  mikopo kutoka kwa wadaiwa,  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu inatunga sheria na mifumo  mbalimbali ya kuwadhibiti wadaiwa hao. “Tunatengeneza sheria ambazo zitawazuia wadaiwa wa mikopo ya elimu ya juu kupata hati ya kusafiria nje ya nchi au kibali cha kusafiri hadi atakapowasiliana na Bodi.”

  Pia,alisema mhitimu atakayeshindwa kulipa mkopo taarifa zake zitatangazwa kwenye vyombo vya habari na kwenye taasisi za mikopo ili asipate huduma yoyote ya kifedha.

  Naye, Msaidizi wa Mkurugenzi Mtendaji Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu Dk. Veronica Nyahende amewataka wahitimu wa elimu ya juu nchini kutumia elimu waliyonayo kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri kuajiriwa. Alisema changamoto ya kurejesha mikopo  ni kubwa kwa upande wa wahitimu wa elimu ya juu ambao hawana kazi ama hawajajiajiri.

  “Changamoto iliyopo ni wahitimu kushindwa kulipa mikopo hiyo kutokana na kuwa na kipato cha chini ama kukosa ajira.” Alisema Bodi imeingia mkataba na kampuni zitakazokusanya mikopo kwa walionufaika na mikopo hiyo na kushindwa kuilipa .

  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu iko katika mchakato wa kuelimisha umma na watendaji wakuu Serikalini ili kuhakikisha wanawasilisha taarifa za watumishi wao wanaodaiwa mikopo hiyo.

  0 0  0 0

  United States Ambassador to Tanzania Mark B. Childress (left) and Tanzania’s Minister for Natural Resources and Tourism Lazaro Nyalandu toast the 238th anniversary of American Independence and the bonds of friendship between the two countries.  Minister Nyalandu joined scores of Tanzanians, members of the diplomatic corps, and other distinguished guests at a colorful Independence Day reception at the U.S. Embassy in Dar es Salaam on June 26, 2014. (Photo courtesy of the American Embassy).
  In celebration of the 238th anniversary of American Independence, United States Ambassador to Tanzania Mark Childress hosted a colorful reception at the U.S. Embassy grounds on June 26 in Dar es Salaam.  The event focused on four iconic cities in the U.S.: Boston, Los Angeles, Chicago and New Orleans, and finished off with a fireworks display.  The guest of honor from the Government of Tanzania was Hon. Lazaro Nyalandu, Minister for Natural Resources and Tourism. 
  Addressing an audience of approximately 500 guests, Ambassador Childress remarked that both the United States and Tanzania stand for liberty, justice and prosperity.  At his first Independence Day celebration as the U.S. Ambassador to Tanzania, Ambassador Childress pledged to further strengthen the friendship between the two nations.  More specifically, Ambassador Childress said he will work closely with the Government and People of Tanzania to address the problem of wildlife trafficking.
  In his remarks, Hon. Lazaro Nyalandu congratulated the American people on the occasion of their Independence Day, and remarked on the birth of the relationship between the U.S. and Tanzania with the close friendship between the late Mwalimu Julius Nyerere and the late President John F. Kennedy.  Minister Nyalandu also commended Ambassador Childress for his commitment to wildlife conservation, and pledged to ensure Tanzania does all that is within its powers to combat the problem of elephant poaching.
  The United States’ Independence Day, commonly referred to as Fourth of July, is celebrated to commemorate the adoption of the Declaration of Independence on July 4, 1776, announcing the separation of America from Great Britain.
   


  0 0

   Mtaalam wa Maswala ya Uchunguzi wa Uhalifu (Crime and Investigation) kutona nchini Uingereza,Steven Gaskin (kulia) akizungumza wakati wa kutoa mafunzo kwa waandini wa habari (hawapo pichani) kutoka nchi mbali mbali barani Afrika ya namna ya kuweza kuchunguza na kuweza kubaini mwalifu katika tukio lolote,katika mafunzo yaliyofanyika jana kwenye ufukwe wa hoteli ya Trou Aux Biches,Mauritius.Mafunzo hayo yametolewa ikiwa ni sehemu kujionea kazi mbali mbali zinachoonyeshwa kwenye DSTV na GOTV kutoka MultiChoice Afrika.kushoto ni MC wa Kimataifa ambaye pia ni Muongozaji wa Mashindano ya Big Brother Africa, IK Osakioduwa
   Mtaalam wa Maswala ya Uchunguzi wa Uhalifu (Crime and Investigation) kutona nchini Uingereza,Steven Gaskin akinyesha kifaa maalum cha kuweza kumbaini muhalifu kwa kupitia nywele.

  Sehemu ya wanahabari hao wakiwa kwenye zoezi la mafunzo na kumbaini muhalifu kwa kupitia alama za vidole.

  0 0

  Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika, Eng. Christopher Chiza akiwa na ujumbe wa Wizara yake, kulia ni Mkurugenzi wa Usalama wa Chakula, Bwana Karim Mtambo na kushoto ni Bi. Margaret Ndaba, Waziri huyo na ujumbe wake, wapo Jijini Malabo, Equatorial Guinea kuhudhuria Mkutano wa Wakuu wa nchi za Umoja wa Afrika (Picha kwa Hisani ya WKCU)


  0 0
 • 06/28/14--00:35: UCHOKOZI WA KIJAST BIKOZ LEO


 • 0 0

  Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa na usalama katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kulia ni Meneja bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Moses Krom.
  Meneja bidhaa na Maendeleo ya M-Pesa wa Vodacom Tanzania, Moses Krom akizungumza na waandishi wa habari (Hawapo pichani) kuhusiana na kulipia viingilio kwa njia ya M-Pesa katika maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba)Dar es Salaam yatakayo anza rasmi kesho na kumalizika julai 8 mwaka huu. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa TanTrade, Anna Bulando.

  Mamlaka ya maendeleo ya biashara Tanzania ( TanTrade) imetangaza viingilio vipya vya watu na magari katika maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam, (DITF) yatakayo anza tarehe 28 ya mwezi juni hadi tarehe 8 mwezi julai.

  Akizungumza na waandishi wa habari, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tantrade Bi. Anna Florence Bulondo amesema viingilio vya mwaka huu havina tofauti na vya mwaka jana lakini sasa yamefanyika maboresho ikiwa ni pamoja na ukataji wa tiketi kwa njia ya Kielectroniki na kwa njia ya M -pesa.

  “Viingilio vya mwaka huu ni Shilingi elfu 2500 kwa watu mzima na shillingi 500 kwa watoto kila siku isipokuwa siku maalum ya tarehe 7 ambapo viingiio vitakuwa shilingi 3000 kwa watu wazima na watoto shilingi 1000.” Alisema Bulondo.

  “Kwa watakao hudhuria maonyesho hayo na magari madogo watatakiwa kununua tiketi kwa shilingi 4000, kama ambavyo mchanganuo wa malipo unavyobainisha malipo ya huduma nyingine zikiwemo za kupaki magari kama malori na magari makubwa pamoja na huduma nyingine.”

  Aidha, Kaimu Mkurugenzi Mkuu huyo aliongeza kuwa, katika maonesho ya Mwaka huu, Usalama umeimarishwa kwa kiasi kikubwa na kutakuwa na Ulinzi wa Uhakika pamoja na Camera maalum zitakazo wekwa katika mageti na sehemu mbalimbali kuzunguka maeneo yote ya maonesho.

  Kwa Upande wake, Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa, amesema kwa mwaka wa pili sasa wameendelea kuwawezesha watu, kufanya malipo ya tiketi kwa njia ya M pesa.

  “M pesa inaendelea kurahisisha maisha ya Watanzania na mwaka huu, watu wote watakao kuja katika maonesho haya tumewawezesha kulipa viingilio kupitia M pesa na pia kufanya manunuzi na kulipa kwa M pesa katika banda letu la Vodacom.” Alisema Twissa.
  Malipo ya ada binafsi.

  1.      Kwa siku - watu wazima (siku za kawaida) – 2,500/-
  2.      Kwa siku- watoto (siku za kawaida) – 500/-
  3.      Kwa siku – watu wazima (siku ya SabaSaba) – 3,000/-
  4.      kwa siku – Watoto (siku ya SabaSaba) – 1,000/-
  5.      malipo kwa kipindi chote cha maonyesho - Beji kwa wahusika wa maonyesho   - 20,000/-
  6.      Beji kwa wahusika wa maonyesho (maeneo) – 3,000/- 

  Tiketi za uegeshaji magari.

  1.      Kwa siku (magari madogo)  - 4,000/-
  2.      kwa kipindi chote cha maonyesho – 30,000/-
  3.      Malipo kwa pamoja – 200,000/-
  4.      Tiketi za maegesho maalum – 400,000/-
  5.      Maroli na magari makubwa – 500,000/-
  6.      Malipo ya kuegesha magari nje ya viwanja vya saba saba – 1,500/-

  Maonesho ya kimataifa ya Dar es salaam ni maonesho pekee yanayoongoza katika huduma za masoko Tanzania, maonesho hayo yanayodumu kwa siku kumi, huvutia watazamaji zaidi ya laki tatu na nusu na kutoa fursa kwa makampuni kuonyesha bidhaa zao na wanaohudhuria kununua vitu mbalimbali kwa gharama nafuu na kupata fursa ya kuuliza maswali na kulinganisha ubora wa bidhaaa kadha wa kadha.

  0 0
 • 06/28/14--13:30: RATIBA YA KOMBE LA DUNIA LEO


 • 0 0

   Mkuu wa kituo cha polisi Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ASP Lwitiko Norman Kibanda, akizungumza jana na madereva wa pikipiki za kubeba abiria ambao waliandamana hadi kwenye kituo hicho wakipinga kutozwa fedha sh22,000 na maofisa biashara wa wilaya hiyo, waliodai kuwa tozo hizo ni amri ya Mamlaka ya Usafirishari wa vyombo vya usafiri wa majini na nchi kavu (Sumatra)


  0 0

   The EAC Regional Programme for Sensitization of Border Communities commenced 24 June 2014, at Rusumo town which sits at the border of Rwanda and Tanzania.
  The programme’s overall objective is to raise awareness among cross-border communities within the EAC region, with particular focus on small scale traders to enhance their understanding of the EAC integration agenda, as well as identify the stakes and opportunities of the EAC integration.

  Speaking during the official opening on behalf of the EAC Principal Public Relations Officer, the EAC/GIZ Media Expert; Mr. Sukhdev Chhatbar emphasized the importance of empowering the common ‘mwananchi’ at the grass-root level to enhance their involvement and active participation towards building a stronger and solid foundation for a people-centred EAC integration process. This is said noting that the people of East Africa are the key beneficiaries of the integration course.
  “There is need to ensure that the citizens of EAC Partner States are well equipped with the necessary tools and skills to actively participate in the regional integration process and therefore contribute to the overall development of the region", he added.
  Simplified and audience-tailored presentations were delivered by Microjustice Rwanda (MJR) on the Customs Union and Common Market opportunities, benefits, requirements, processes and procedures for acquiring legal documents for free movement of goods, services, labour and capital at the border posts.Participants of the programmes raised concerns on various issues assumed to affect the smooth undertaking of business across the border points, including non-adherence to the rules and regulations stipulated in the EAC Treaty as well as corruption within the customs and immigration departments.  The queries and concerns were subsequently addressed by representatives from the Ministries of East African Community Affairs from Rwanda and Tanzania, also present at the workshop.
  The programme is expected to adequately familiarize stakeholders with the benefits and opportunities of the EAC integration process, particularly the Customs Union, the Common Market and the rights and freedoms established under these protocols to achieve the EAC mission which is to widen and deepen economic, political, social and cultural integration. The EAC integration agenda aims at improving the quality of life of the people of East Africa through increased competitiveness, value added production, trade and investments.To achieve the objective of the sensitization programme, a training session was also conducted by EAC Youth Ambassadors to inspire the youth into spearheading the EAC integration agenda in their communities.The next sensitization workshop is set to be carried out at Manyovu and Mugina towns in Tanzania and Burundi respectively next week.

  0 0  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Alhaj Dk.Ali Mohamed Shein akitoa salamu za Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa   Wananchi  wa Zanzibar na Tanzania kwa Ujumla. Pia aliwatakia mfungo mwema  wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kwa kufanya ibada mbali mbali. Picha na Ramadhan Othman,  Ikulu

  0 0
 • 06/28/14--03:50: KUTOKA BUNGENI DODOMA.
 •   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akiteta na Mbunge wa Mbinga Magharibi Cpt. John Komba, Bungeni Mjini Dodoma Juni 27, 2014.
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wabunge Samuel Sita wa Urambo Masharikiambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki (katikati) na  Mbunge wa Tabora mjini Aden Rage kwenye viwanja vya Bunge mjini  Dodoma Juni 27, 2014.
   Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akitambulishwa na Mbunge wa  Hanang na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Ukezaji na Uwezeshaji, Dr. Mary (kulia) kwa Wananchi kutoka jimbo hilo waliotembelea Bunge mjini Dodoma Junu 27 kwa mwaliko wa mbunge wao.
    Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda  akizungumza na wabunge  kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma juni 27, 2014. Kutoka kushoto ni Martha Mlata wa Viti Maalum,Tundu Lissu wa Singida Masharikina na Felister Bura wa Viti Maalum. (Picha na Ofisi yaWaziri Mkuu).

  0 0

  Balozi Seif akizungumza na waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kijiji cha Kiboje Mamboleo mara baada kuufungua msikiti wao wa Ijumaa uliofanyiwa matengenezo makubwa.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

   Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Moh’d Raza Hassanali akielezea mikakati ya kamati ya ujenzi wa misikiti, Madrasa na maskuli nchini ilivyopania kuendeleza malengo yake.  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi amezikumbusha Kamati za Misikiti hapa  nchini kuendelea kuwa imara kwa kutowaruhusu watu wanaopenda kujipenyeza ndani ya kamati hizo kwa nia ya kuanza kutoa madarasa ya uchochezi na kuwagawa waumini kimadhehebu.

  Alisema uimara huo ndio njia sahihi itakayoilinda misikiti hiyo na wimbi la vurugu na migogoro ambayo hatiae husababisha mmong’onyoko mkubwa wa  ukosefu wa maadili  katika jamii za kiislamu.

  Akiufungua msikiti mpya wa Ijumaa uliofanyiwa matengenezo makubwa katika Kijiji cha Kiboje Mambo leo Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alisema msikiti ni taasisi yenye mchango mkubwa wa kuutangaza ukweli dhidi ya unafiki pamoja na mambo ya kheri kwa jamii ya Kiislamu. 

  Balozi Seif alisema katika kuihuisha nyumba ya Mwenyezi Muungu  Msikiti ni vyema kwa waumini hao mbali ya kutekeleza vipindi vya sala lakini pia ni vyema wakaendeleza madarasa hasa kipindi hichi kinachokaribia cha  mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa kujifunza masuala ya dini yao.

  Akisoma risala ya waumini na wananchi hao wa Kiboje Mamboleo Ustadhi Juma Abdulla alisema wana jamii hao wameelezea faraja yao kutokana na kumalizika kwa ujenzi wa msikiti huo,lakini hata hivyo bado zipo baadhi ya changa moto zinazoendelea kuwakabili wana jamii hao wa Kiboje Mambo leo ambazo zimekuwa zikiwapa wakati mgumu kwao na kizazi chao.

  Mapema Mwenyekiti wa Kamati ya usimamizi wa ujenzi wa Misikiti, madrasa na majengo ya skuli hapa Zanzibar ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Uzini Mh. Moh’d Raza Hassanali alisema kamati hiyo iliyo chini ya mwenyekiti wake Rais Mstaafu wa Tanzania Alhajj Ali Hassan Mwinyi itaendelea kuongeza nguvu zake kwenye ujenzi wa majengo ya taasisi hizo yenye upungufu hapa Nchini.


  Othman Khamis Ame
  Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
  27/6/2014.

  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Dr Ally Olot, mtafiti wa chanjo ya malaria na kiongozi wa watafiti wa Ifakara Health Institute (IH) I Malabo, Equatorial Guinea) walipomtembelea kwenye makazi yake mjini Malabo ambako Rais alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika. Wengine ni Dr. Mwajuma Chemba ambaye ni Mtalaamu mratibu wa tafiti za chanjo ya malaria, na Elizabeth Nyakarungu, Mtaalamu wa maabara, utambuzi wadudu wa malaria).
    Dr Ally Olot, mtafiti wa chanjo ya malaria na kiongozi wa watafiti wa Ifakara Health Institute (IH) I Malabo, Equatorial Guinea) akifafanunua jambo kwa Rais Kikwete walipomtembelea kwenye makazi yake mjini Malabo ambako, Rais Kikwete alikuwa anahudhuria mkutano wa kawaida wa Umoja wa Afrika. Wengine ni Dr. Mwajuma Chemba ambaye ni Mtalaamu mratibu wa tafiti za chanjo ya malaria, na Elizabeth Nyakarungu, Mtaalamu wa maabara, utambuzi wadudu wa malaria).
  Picha ya pamoja.Picha na Ikulu

  Rais Kikwete aliwapongeza sana watafiti hao pamoja na taasisi ya IHI kwa kuiletea sifa Tanzania katika fani ya utafiti nje ya nchi.Watafiti hao wako Equatorial Guinea (EG) kwa mwaliko wa serikali ya nchi hiyo kwa ajili ya kutoa msaada wa kitaalamu katika utekelezaji wa mradi wa utafiti wa chanjo ya malaria iitwayo PfSPZ na kuwafunza wenzetu kuhusu maarifa ya fani hii ya utafiti wa chanjo ya malaria.

   IHI ni shirika la utafiti lenye kufanya tafiti za afya nchini Tanzania lenye uzoefu wa miaka zaidi ya miaka hamsini. Mfano mmoja wa mafanikio yake ni utafiti uliopelekea vyandarua vyenye dawa kutumika kama moja wapo ya njia za kujikinga na malaria nchini Tanzania. Tunafanya kazi pamoja madaktari na wataalamu kutoka Wizara ya Afya ya EG, shirika lisilo la kiserikali la Marekani liitwalo MCDI (Medical Care Development International) na Sanaria ambao ndio watengenezaji wa chanjo hiyo ya malaria.

  Mradi huu wa utafiti  unagharamiwa na serikali ya EG pamoja na sekta binafsi za mafuta. Mradi huu wa miaka mitano una lengo la kuchunguza kuhusu uwezo wa chanjo hiyo kukinga dhidi ya ugonjwa wa malaria. Ushirikano huu ni mmoja ya mfano wa mashirikano kati ya sekta ya umma na sekta binafsi ili kutafuta njia bora za kukinga maradhi katika jamii. Vilevile ni moja ya kielelezo kizuri cha jinsi gani nchi za kusini zinaweza kushirikiana katika taaluma mbali mbali (south south corporation).

  Tumepata fursa ya kukutana na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshima Jakaya Mrisho Kikwete Malabo na kumueleza kuhusu kazi tunayofanya na changamoto mbalimbali zinazotukuta pamoja na kutoa ombi kwa mheshimiwa Rais kusahilisha mashirikano kati ya nchi mbili za Tanzania na Equatorial Guinea kupitia Wizara za Afya na Tume za Sayansi na technologia za nchi hizi mbili. Hili litafanya utelekelezaji wa mashirikiano hayo kuwa bora zaidi kwa lengo la kunufaisha nchi zote mbili.

  Mashirikiano haya ni fursa ya watanzania kuwafunza wenzao pamoja na wao kujifunza kutokana na mashirikiano hayo. Utafiti huo pia utasaidia juhudi za kutokomeza ugonjwa wa malaria kwa kufanya tafiti zenye lengo la kutafuta chanjo bora ya malaria pamoja na njia bora za kusambaza chanjo hiyo kwa nchi zote mbili kama itakuwa ni yenye mafanikio.

  0 0

   Mgombea wa nafasi ya urais Evans Aveva, akiwa na Mlinzi wake 'Board Guard' (nyuma) akijinadi kwa wanachama, wakati wa mkutano wake wa kampeni za mwisho na waandishi wa habari kuelekea uchaguzi mkuu wa Klabu hiyo kesho, kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kuiongoza Klabu ya Simba kwa kipindi kijacho cha miaka minne. Hitimisho hilo la kampeni zake limefanyika leo kwenye Hoteli ya Hyatt Kilimanjaro, jijini Dar es Salaam. 
   Mwenyekiti wa zamani wa Simba, Hassan Dalali, akimnadi mgombea Urais Evans Aveva.
   Sehemu ya waandishi wa habari waliohudhuria mkutano huo.
   Baadhi ya wanachama wa Simba waliohudhuria mkutano huo.
  HABARI ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

   Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk Goodluck Mlimbila akijaribu kusukuma moja kati ya viti 33 vilivyotolewa na asasi ya MUVIMA kwa ajili ya hospitali ya wilaya ya Mufindi. Anayefurahi katikati ni mkurugenzi mwenza wa MUVIMA, Albert Chalamila akipongezwa na Katibu wa Afya wa Wilaya hiyo, Atupekisye Mwakifamba
  Albert Chalamila na baadhi ya wanahabari wakiangalia hali ilivyo ndani ya wodi ya wazazi ya hospitali hiyo; hapa wanaonekana baadhi ya wajawazito wanaolala chini kutokana na ukosefu wa vitanda.

  0 0
 • 06/28/14--05:04: UJUMBE WA WIKEND HUO...!


older | 1 | .... | 486 | 487 | (Page 488) | 489 | 490 | .... | 3272 | newer