Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109597 articles
Browse latest View live

Waziri mkuu Pinda ahudhuria mkutano wa benki ya dunia,awataka wajasiriamali walioko katika sekta isiyo rasmi kurasimisha biashara zao.

0
0
 Waziri Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda akizungumza na waandishi wa habari  nje ya Hotel ya Serena ambapo alihudhuria Mkutano wa Tano unaohusu masuala ya Uchumi,kulia kwake ni mkurugenzi wa benki ya Dunia nchini Ndugu Philippe Dongier
 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Mwandishi wa Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo aliwaeleza waandishi hao Tanzania ina nafasi kubwa ya kupanua wigo wa ajira kwa kutengeneza mazingira ya kufanyia kazi yenye ubora hasa kwenye  miji inayokuwa kwa kasi hii itasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa Vijana na Wanawake.
 Mkurugenzi wa Benki ya Dunia nchini Tanzania Philippe Dongier akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa kivukoni Serena Hotel jijini Dar es Salaam, akiwa pamoja na Mwandishi wa Mada Ndugu Jacques Morisset ambapo alikiri pamoja na kukua kwa uchumi lakini bado uchumi haujafungua au kutengeneza ajira kwa wananchi .
 
Na Benedict Liwenga-MAELEZO. 

WAZIRI Mkuu wa Tanzania Mheshimiwa Mizengo Pinda amesema kuwa wakati umefika wajasiriamali nchini wanaoendesha shughuli zao katika sekta isiyo rasmi kuboresha shughuli zao ili waweze kuzirasimisha kwa ajili kuboresha maisha yao na Taifa kwa ujumla.

Mheshimiwa Pinda amesema hayo jana (leo) jijini Dar es salaam wakati wa Uzinduzi wa taarifa ya Hali ya Uchumi wa Tanzania-Toleo la Tano iliyoandaliwa na Benki Kuu ya Dunia.

Taarifa hiyo inalenga kutoa Sera na hatua za kuchukua kuwezesha kupanuka kwa biashara katika miji na majiji nchini kwa ajili ya kuongeza ajira zaidi kwa wananchi na hasa vijana.
Aidha, Mheshimiwa Pinda alitoa wito kwa vijana nchini kujiajiri katika sekta mbalimbali kama vile kilimo na kukiendesha katika mfumo ulio rasmi ili kiweze kuwakomboa katika maisha yao na kuwasaidia kupata ajira.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania, Burundi na Uganda Bwana Philip Dongier ametoa wito kwa watunga Sera nchini kuweka msisitizo katika kuendeleza ukuaji wa viwanda ili kutengeneza idadi kubwa ya ajira mpya na zenye tija kwa wananchi.

Bwana Dongier aliongeongeza kuwa changamoto nyingi zinazowakabili wajasiriamali wadogo katika kusaka ajira ni fursa zinazotokana na mchakato wa kupanuka kwa haraka kwa miji huku makisio ya hivi karibuni yakionesha kwamba ifikapo mwaka 2030 watanzania wengi watakuwa wakiishi mijini kuliko vijijini.

Taarifa ya Hali ya Uchumi ambayo huchapishwa mara mbili kwa mwaka na Benki ya Dunia inaeleza kwamba kuna uwezekano wa uchumi wa Tanzania kuendelea kukua asilimia 7 kwa mwaka.
 
 

Waziri wa fedha Mhe.Saada Mkuya Kujibu Hoja za Wabunge jioni ya Leo

0
0
 
 Naibu Waziri wa Fedha Mhe.Mwingulu Nchemba kulia akijadiliana na Maofisa wa Wizara ya Fedha,wakati wakitoka kwenye Ukumbi wa Msekwa walikokuwa na kikao cha kuandaa majibu ya Hoja za Wabunge kwa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2014-2015.Baada ya mjadala uliochukuwa takribani wiki nzima.Bajeti ya Serikali Ilisomwa na waziri wa Fedha Alhamisi iliyo[pita na Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya nakufuatiwa na uchangiwaji na mjadala kwa kuchangiwa na Wabunge mbalambali.
  Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya (aliyevalia Hijabu )akitoka katika Ukumbi wa Msekwa kuandaa majibu kwa Hoja za Wabunge kwa Bajeti ya Mwaka 2015-2015 kwa kushirikiana na wataalamu wa Wizara ya Fedha.

Jioni hii Waziri wa Fedha atajibu Hoja za Wabunge na Kufuatiwa na upigaji kura wa Mbunge mmoja mmoja ili kuwena kupitisha Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2014-2015. Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Photyo Solutions wawakilishi wa Michuzi Blog Kanda ya Kati


Sera za Libe Mgombeya wa Jumuiya ya waTanzania DMV

0
0
Kutakuwa na Mkutano wa Sera za Mkombea wa Jumuiya ya waTanzania DMV
Bwna Liberatus Mwang'ombe
Atakachoongea katika mkutano wake ni
 Kuhusu Elimun Diversity visa Lotterry/ YOUNG African Leaders Initiatives
Jumiaya na Afya, Baraza la ushauri, Darasa la Kiswahili. Ushirikiano na umoja, Jumuiya na wajasiriamali, Jumuia na vyanzo vya mapato, Jumuiya na mrejesho wa ubalozi, "Power of attorney" , Mkutano huo utafanyika Siku ya Jumamosi, June 28, 2014 kuanzia saa 10 Alasiri (4pm) Meadowbrook Park
7901 Meadowbrook Lane
Chevy Chase, MD 20815Kutakua na vinywaji pamoja na uchomaji wanyama chomaNyote Mnakaribishwa**********

RAIS KIKWETE ATAJA MISINGI MIKUU MITANO YA UTHIBITISHO WA KUSHAMIRI KWA UTAWALA BORA NCHINI

0
0


THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone:255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ametaja misingi mikuu mitano ambayo utekelekezaji wake unathibitisha kushamiri kwa utawala bora nchini.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa pamoja na kwamba utawala bora unaendelea kushamiri nchini, bado taasisi za usimamizi wa masuala ya utawala bora zina nafasi ya kuboresha kazi yao na kupanua kwa kiasi kikubwa zaidi utawala bora.

Rais Kikwete aliyasema hayo usiku wa jana, Jumatatu, Juni 23, 2014, wakati alipozungumza baada ya kuwa ametunukiwa Tuzo ya Kutambua Mchango Wake wa Kuimarisha Utawala Bora nchini ambayo imetolewa na taasisi nane za usimamizi nchini.

Taasisi hizo ni Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA), Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (PCB), Mamlaka ya Manunuzi ya Umma (PPRA), Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Jamii (SSRA), Ofisi ya Mhasibu Mkuu wa Serikali (ACCGen-D), Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Serikali (IAG-D) na Sekretarieti ya Tume ya Maadili.

Hiyo ni mara ya kwanza kwa Tuzo hiyo kutolewa nchini na ilikabidhiwa kwa Rais Kikwete wakati wa chakula cha usiku kilichoandaliwa kwa ajili ya wajumbe wa Mkutano wa Mwaka wa Wakaguzi wa Hesabu za Serikali kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNICC) mjini Dar Es salaam.

Mkutano huo wa mwaka pia unahudhuriwa na wajumbe waalikwa kutoka nchi za Ujerumani, Afrika Kusini, Uganda, Sweden, Sierra Leone, Nigeria, Niger, Ghana, Kenya, Zambia, Rwanda, Burundi na Ethiopia. Akizungumza baada ya kukabidhiwa Tuzo hiyo na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) Bwana Ludovick Utoh, Rais Kikwete alisema kuwa Tanzania ina utawala bora kwa sababu inadumisha misingi yote mikuu ya utawala bora.

Aliitaja misingi hiyo kuwa ni kushamiri wa demokrasia, uhuru wa kutoa maoni na wa vyombo vya habari, haki ya kila Mtanzania kuishi, utawala wa sheria, kutoingiliana kwa mihimili mitatu ya Serikali.

Rais Kikwete ambaye amesema kuwa amepokea Tuzo hiyo kwa niaba ya viongozi wenzake katika Serikali – Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, Mawaziri, Wakuu wa Mikoa, Katibu Mkuu Kiongozi, Makatibu Wakuu na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama – amesema kuwa utawala bora ni jambo muhimu na halina mbadala wake.

“Tanzania tumeruhusu uhuru mkubwa kwa wananchi wetu kushiriki katika shughuli zao. Serikali yetu haitishi watu wake. Hatufanyi hivyo. Ziko nchi zinaishi kwa kutisha raia wake na nyie mnazijua, “alisema Rais Kikwete.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM
24 Juni, 2014

Germany contributes 24 Million Euros to EAC to support Media relations and Water sector development

0
0

East African Community Secretariat, Arusha, Tanzania, 24 June 2014;The Federal Republic of Germany today signed an intergovernmental agreement with the East African Community (EAC) in order to support higher education and training for future journalists and media professionals.

Germany makes available a financial contribution of 14 million Euros in support of the Graduate School of Media and Communications (GSMC) of the Aga Khan University, a recently established Centre of Excellence for media education in East Africa.
 
The education and training programmes of the GSMC will have a strong regional focus and will foster a diverse array of media leaders, enterprises and institutions that will be distinguished by high standards of competence, ethics, professionalism and social responsibility.

 The GSMC will closely cooperate with the Deutsche Welle Akademie (DWA), which is the media development division of Germany's well known international broadcaster Deutsche Welle (DW).

Furthermore, the Federal Republic of Germany announced a new commitment to the East African Community in the water and sanitation sector. The EAC and Germany believe that coordinated transboundary investment approaches are needed to cope with the growing demand for safe water, to fight increasing pollution of water systems and to deal with climate-related challenges.

In this regard, Germany committed a first tranche of 10 million Euros to the 'Trans boundary Water Supply and Sanitation Programme' in order to contribute to improved water and sanitation infrastructure in selected EAC border towns. The programme will be implemented with the Lake Victoria Basin Organisation (LVBC) of the EAC as Project Executing Agency.

Dr. Richard Sezibera, Secretary-General of the EAC and Member of the GAVI Board said “I am happy with the way things are moving in regard to EAC-Germany relations. The Agreement we have signed shows that Germany is indeed our valuable partner”.

Hans Koeppel, Chargé d´Affaires at the German Embassy in Tanzania, said: "The new commitments underline that Germany continues to be a strong partner for the EAC, contributing to an integration process that puts the people in the centre".

Since as early as 1998, Germany's development cooperation, on behalf of the German Federal Ministry for Economic Cooperation and Development (BMZ), contributes to the capacity development of the Secretariat of the EAC and the regional integration in East Africa through a variety of programmes and projects. Germany's funding for Technical and Financial Cooperation with the EAC amounts to a total of 125.9 million Euros. Germany also provides substantial support for the water and governance sectors in selected EAC member states.

MANISPAA YA ILALA YASAINI MKATABA WA BILIONI 2.1 KWA AJILI YA UJENZI WA MRADI WA MAJI KATA ZA KIVULE NA KIPUNGUNI

0
0
 Meya Wa manispaa ya Ilala Mh Jery Silaa akikabidhiana Mikataba na Mkandarasi kwa Ajili ya mradi wa maji kwa kata za Kipunguni B na Kivule.
 Mkandarasi kutoka Kika Construction Mbaraka Kihawe wa pili kutoka kushoto akitia sahihi mkataba wa ujenzi wa mradi wa Maji kata za Kipunguni B na Kivule na Manispaa ya Ilala,Meya Wa Manispaa ya Ilala(mwenye miwani)akishuhudia Mwanasheria wa Manispaa Kulia akitia sahihi Mikataba Hiyo.


Wanainchi wa kata Za Kivule na Kipunguni B wakifuatilia utiaji sahihi wa mikataba hiyo kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa Maji.PICHA ZOTE NA DJ SEK BLOG.PICHA ZAIDI INGIA HAPA

RAIS KIKWETE ATUA MALABO, EQUTORIAL GUINEA, KUHUDHURIA MKUTANO WA 23 WA UMOJA WA AFRIKA

0
0
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewasili mji mkuu wa Equatorial Guinea wa Malabo leo Juni 24, 2014 kuhudhuria Mkutano wa Umoja wa Africa –African Union (AU).

Akiwa Malabo, Mheshimiwa Rais Kikwete pia atakuwa Mwenyekiti wa kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa AU kitakachojadili mazingira. Rais Kikwete na ujumbe wake anatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Waziri Mkuu wa Equatorial Guinea Mhe Vicente Ehate Tomi alipowasili  katika katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, leo Juni 24, 2014
PICHA NA IKULU
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa katika uwanja wa ndege wa Malabo, Equatorial Guinea, leo Juni 24, 2014

Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
IKULU
DAR ES SALAAM.

Cameroon: From Indomitable Lions (Italia 90) To Disgraced Alley Cats (Brazil 2014)


MultChoice Africa yakutana na wadau wake nchini Mauritius

0
0
Mtendaji Mkuu wa MultChoice Afrika,Nico Meyer akitoa hotuba yake wakati wa tafrija ya ufunguzi wa Mult Choice Africa Extravaganza uliofanyika leo kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Trou Aux Biches,Morisi ndani ya Kisiwa cha Mauritius.Hafla hiyo imekusanya wadau mbali mbali wa MultChoice barani Afrika,ambapo Kampini hiyo itakuwa ikinyesha mambo mbali mbali wanayojihusisha nayo kwenye vipindi mbali mbali vya Televisheni zao za DStV na GoTV.Picha zote na Othman Michuzi.
Meneja wa MultChoice kwa Ukanda wa Afrika Magharibi,Bi. Wangi Mba-Uzoukwu nae alipata wasaa wa kuzungumza machache wakati wa tafrija hiyo ya ufunguzi wa Mult Choice Africa Extravaganza uliofanyika leo kwenye Ufukwe wa Hoteli ya Trou Aux Biches,Morisi ndani ya Kisiwa cha Mauritius.
Watangazaji wa Kipindi cha JARA kinachorushwa na DStV, Uti Nwachukwu na Juliet Ibrahim wakiongoza kipindi chao Live ukumbini hapo.
Meneja Mahusiano wa MultChoice Tanzania,Barbara Kambogi (kulia) na Mdau Sidi Mgumia (kushoto) wakiwa kwenye picha ya pamoja na Watangazaji wa Kipindi cha JARA,Uti Nwachukwu na Juliet Ibrahim. 
Team Tanzania wakiwa ndani ya Mauritius.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

FIRST CRESCENT IN JUNE SKIES IN TANZANIA

0
0
The Moon will make it into the news this month following its New Moon phase 27th June.  The beginning of the holy month of Ramadhan can be expected on 29th following observation of the first crescent at sunset on June 28.  Each day, the Moon shifts significantly in the sky, (nearly 12 degrees per day = 1/30 a full cycle).  Hence it will have grown in size and risen high enough to be observable on 28th, a day following the New Moon.  The first crescent will be easy to locate soon after sunset low in the western horizon just below the trio of bright planet Jupiter, and the two bright stars Procyon and Pollux. 

The weather has been unstable for the past month oscillating between heavy clouds and crispy clear skies.  Is this a sign of climate-change being upon us? Possibly, but we hope not.  The skies clear up by night time so the delights of the night skies remain open for our eyes to feast on.

For city folks the skies may not show its full glory due to light pollution.  Hence just as city kids go off for school trips to the national parks we can join them in the depths of darkness in the parks where the stars light up the sky.  Astro-tourism is a novel activity that you can take up easily when you escape the hustle and bustle of city life to visit your grandparents and family in the village. Tourists from outside Tanzania can enjoy the Tanzanian night skies even more since life in their modern, highly lighted cities remove all the darkness of their night skies.

Among the delights this month for the eyes are several planets, the Moon, and several stars forming distinctive constellations. The line up of the planets continues from last month to the end of June.  Jupiter, Mars, Saturn and Moon appear along the east west line across the sky.  Giant Jupiter is close to the western horizon so will be the first to leave the skies towards the end of June.  A modest telescope shows the four main moons of Jupiter as tiny starry points, while the planet will be seen as a disk with larger telescopes able to show parallel cloud belts across its middle.

Mars shines brightly red overhead and on its way back towards its normal eastward movement after about two month of retrograde (reverse, westward) movement.  It also continues to recede from earth making it shine less brightly as days go by.  Through a modest telescope it is seen as a red disk without features.

Saturn is the jewel of the skies though it appears as a tiny steadily shining star half way up towards the east.  A telescope shows its beauty of a flat ring system surrounding a the planet disk.  Currently the ring system is well suited for viewing and appears as though you are watching it off center from above.

A crescent Moon will be seen close and below Venus before dawn (before sunrise) on 24th June while on the morning of 25th it will be seen above Venus.  In its next cycle the Moon will be close to Mars in the evening skies of 5th July and close to Saturn on 7thand 8th July, all the time being within the line forming perfect planet lineup of the past few weeks. Follow the progress of the planets, Moon and stars on www.astronomyintanzania.or.tz.

The sky this month shows 18 constellations and asterisms, though you will need to take an astro-tour away from light polluted towns and cities and travel to villages or parks to see them all.  Marked alphabetically from A to R these are, from south to north, then east to west: A – Sagittarius the archer, B – Scorpius,  C –  Ara the alter, D – Triangulum Australe, the southern triangle, and E – the famous Southern Cross continuously pointing south.  F – is the False Cross, G – is Vela, the sail, H – is the zodiacal constellation of Libra the scales of justice and I – is the long Hydra the snake.  J is Virgo the virgin while K – is Leo the Lion.  L - is Cancer the crab while M – is Hercules, N – is Bootes the herdsman and O – is the famous Big Dipper pointing north. P – is Ursa Major, the big bear while Q – is Draco the dragon. R – is the Little Dipper in Ursa Minor whose end star is the North Star but which we never see as it is below the horizon.

Among the bright stars marked ‘m’ to ‘s’ on the map are:  ‘m’ – Alpha Centauri the closest star at a distance of 4.3 light years and ‘n’ – is Beta Centauri. ‘o’ - is red star Antares in the neck of Scorpius, ‘p’ – is Spica in Virgo while ‘q’ is the third brightest star Aructurus (the first and second brightest stars are respectively Sirius and Canopus will have set in the south west by 8 pm). ‘r’ – is Regulus in Leo while ‘s’ – is Procyon.

The full glory of the dense concentration of stars and dust can be seen in the Milky Way which stretches across the southern skies from southwest to southeast containing the constellations or asterisms C, D, E, F and G.  It runs parallel to the zodiacal constellations A, B, H, J, K, L.  

June 21 is the Solstice day this year, when the Sun starts its journey back towards the Equator from its northernmost position of 23.5 degrees at the Tropic of Cancer.  This day marks the beginning of northern summers and southern winters.

Dr. N. T. Jiwaji
ntjiwaji@yahoo.com. 

AFRICA SPORTS DAY IN COVENTRY -WEST MIDLANDS-ENGLAND

0
0

 Dear all please kindly join us at The Africa sports Day in coventry-West midlands on the 28th hue 2014 from 2PM .The Tanzania Cubs ,a football team based in Coventry will be participating .Come and cheer them up and also have a good family day out. Karibu sana

DKT BILAL AZINDUA SHEREHE ZA KIJADI ZA WASUKUMA WILAWANI MAGU MKOA WA MWANZA

0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikabidhiwa Usinga na wazee wa kijiji cha kisesa wilayani Magu baada ya kusimikwa kuwa kiongozi wa kabila la wasukuma na, wakati wa Sherehe za kijadi na maadhimisho ya siku ya ngoma na nyimbo za kabila la kisukuma zilizofanyika Wilayani magu mkoani Mwanza jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipiga  Ngoma  kuashiria uzinduzi wa Mashindano ya Ngoma na Nyimbo katika Maadhimisho ya Tamasha la Jadi la Wasukuma  kwenye Uwanja wa Kisesa Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimsalimia Mtoto  fredrik  Emmanuel  Mara Baada ya Kumalizika kwa Sherehe za Uzinduzi wa tamasha la Ngoma na Nyimbo za Kabila la wasukuma zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kisesa Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza jana
 Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha kisesa mkoani mwanza, Wakimsikiliza Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  Mohammed Gharib Bilal,  alipokua akiwahutubia  kwenye Uzinduzi wa Mashindano ya Ngoma na Nyimbo za kabila la kisukuma zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kisesa Wilaya ya Magu Mkoa wa Mwanza jana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Ngoma ya Kabila la Wasukuma wakati wa Tamasha la siku ya Bulabo  zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kisesa Wilayani Magu Mkoa wa Mwanza jana. 
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.  Mohammed Gharib Bilal, akiagana na wananchi  wa kijiji cha kisesa baada ya kuzindua  Mashindano ya Ngoma na Nyimbo za kabila la Wasukuma zilizofanyika kwenye Uwanja wa Kisesa Wilayani  Magu Mkoni Mwanza jana .(Picha na OMR)

FILAMU MPYA YA KISWAHILI ILIYOCHEZWA NCHINI UHOLANZI KUINGIA MTAANI HIVI KARIBUNI

0
0
Filamu mpya ya kiswahili iliyochezwa nchini Uholanzi chini ya Director mpya Hija Salehe.Filamu yenye mafunzo,ucheshi na vingi vihoja ndani ya wasanii wapya wenye mvuto na ujuzi mwingi ndani yake.tazama kibwagizo tu kidogo uhondo unakuja hivi karibu.Jina la filamu ni NIMPENDE NANI Kutana na wasanii wenye makeke kama Omary Abbas,Khatib Mustapha,Nicolas Gabino,Mrembo anayekubalika Sonia Kasuka,Shamim Sudi,na wengine kibao ambao ni gumzo katika filamu hii mpya ya kiswahili.

Article 2

0
0
Yassini A Kapuya's all his e-book and hard copy are available online at:  Amazon.com.And to find out date and place of his on site seminar go to his face book account

Hotuba ya Boss Mkuu wa MultChoice Afrika katika event iliyofanyika jana usiku nchini Mauritius


Bunge lapitisha Bajeti ya Serikali kwa kura za ndiyo

0
0


 Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya akijibu Hoja za Wabunge kabla ya Bunge kukaa na kupiga kura kuamua Bajeti ya serikali  kwa Mwaka 2014-015.
  Wabunge wakimsikiliza Waziri wa fedha Mhe Saada wakati akijibu hoja za waheshimiwa Wabunge kabla ya zoezi la kupiga kura kwa ajili ya kupitisha Bajeti ya serikali kwa mwaka 2014-2015.
 Spika wa Bunge akiendesha kikao cha Bunge la Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2014-2015 akisaidiwa na Makatibu wa Bunge mbele yake wakati waziri wa Fedha akijibu hoja za wabunge.
 Waziri wa Fedha Mhe.Saada Mkuya (aliye vaa kilemba) akitoka katika ukumdi wa Bunge akiongozana na Naibu waziri, mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya Serikali kwea mwaka 2014-2015 kwa zaidi ya kura miambili.
 Maofisa wa wizara ya Fedha wakiwapongeza Mawaziri wa Wizara yao mara baada ya Bunge kupitisha Bajeti ya mwaka Serikali  kwa Mwaka wa fedha 2014-2015.Na Deusdedit Moshi Mtendaji Mkuu wa Phpoto Solutions wawa kilishi wa Nichuzi Blog kanda ya Kati.

MAPENDEKEZO YA MAREKEBISHO YA KATIBA YA CUF YAPITISHWA

0
0
Na Hassan Hamad (OMKR). Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF Taifa wamepitisha mapendekezo mbali mbali yaliyowasilishwa na Baraza Kuu la uongozi la chama hicho kuhusu marekebisho ya baadhi ya vipengele vya katiba ya chama hicho. Katika mkutano mkuu wa chama hicho unaoendelea kwa siku ya tatu katika ukumbi wa Ubungo Plaza Dar es Salaam, wajumbe hao pamoja na mambo mengine wamekubaliana kuwa mkutano mkuu wa chama hicho ufanyike mara moja katika kipindi cha miaka mitano badala ya miaka miwili na nusu kama ilivyopitishwa na mkutano mkuu mwaka 2009. 
Katibu Mkuu wa chama hicho Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kuona kuwa mapendekezo yaliyopitishwa mwaka 2009 hayatekelezeki kutokana na ukosefu wa fedha unaokikabili chama hicho. 
Hata hivyo amesema kwa mujibu wa sheria hiyo mkutano mkuu taifa unaweza kufanyika kwa dharura wakati wowote utakapohitajika. Wajumbe wa mkutano huo pia wamekubali mapendekezo ya kuongezwa ngazi ya uongozi ya Jimbo kwa upande wa Tanzania Bara ambapo kabla ya hapo hawakuwa na ngazi hiyo. Mapendekezo mengine yaliyopitishwa ni kwa Mwenyekiti wa chama hicho kupewa uwezo wa kuongeza wigo wa uteuzi kwa wajumbe wa kamati tendaji taifa, nje ya wajumbe wa baraza kuu na mkutano mkuu kwa kadri anavyoona inafaa kwa maslahi ya chama. 
Aidha wajumbe hao wamekubaliana kuwepo kamati ya nidhamu na maadili kikatiba katika ngazi zote za uongozi kuanzia ngazi ya tawi hadi taifa, sambamba na mambo ya uchaguzi kuondolea kwenye katiba na badala yake yabakie kwenye kanuni. 
Kwa upande mwengine wajumbe wa mkutano huo wamekataa pendekezo la kuwepo uongozi katika ngazi ya Mkoa kwa upande wa Tanzania Bara, na kutaka ngazi za uongozi ziendelee kama kawaida kwa kuwepo ngazi ya Wilaya ikifuatiwa na ngazi ya Taifa. 
Wajumbe hao wamekataa pendekezo hilo kwa madai kuwa ngazi hiyo itaongeza utitiri wa viongozi wasiokuwa na ulazima kwa maendeleo ya chama. 
Pendekezo jengine walilolikataa ni uteuzi wa makatibu wa Wilaya ambapo wamekubaliana kuwa makatibu wa ngazi hiyo waendelee kuchaguliwa na wajumbe wa mkutano mkuu wa Wilaya. Marekebisho ya katiba hiyo yakayoingizwa kwenye “Katiba ya CUF ya mwaka 1992 toleo la 2014”, yataanza kutumika kuanzia tarehe 22/08/2014.
 Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akiunga mkono moja ya hoja za marekebisho ya katiba ya CUF yaliyofanywa katika ukumbi la Ubungo Plaza Dar es Salaam.
 Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba, akiunga mkono moja ya hoja za marekebisho ya katiba ya CUF yaliyofanywa katika ukumbi la Ubungo Plaza Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF Taifa wakiunga mkono moja ya hoja za marekebisho ya katiba ya CUF yaliyofanywa katika ukumbi la Ubungo Plaza Dar es Salaam.
 Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF Taifa wakiunga mkono moja ya hoja za marekebisho ya katiba ya CUF yaliyofanywa katika ukumbi la Ubungo Plaza Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad akitoa ufafanuzi juu ya hoja ya marekebisho ya katiba ya CUF yaliyofanywa katika ukumbi la Ubungo Plaza Dar es Salaam. (Picha na Salmin Said, OMKR)

TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUHAKIKISHA INAWEKA MIUNDOMBINU MIZURI KWA WALEMAVU.

0
0

Na John Gagarini, Kibaha.

TUME ya Taifa ya Uchaguzi Nchini (NEC) imesema kuwa itahakikisha kuwa inaweka miundombinu mizuri kwa watu wenye ulemavu wakati wa uboreshaji wa zoezi la Daftari la Kudumu la Wapiga Kura litakalofanyika hivi karibuni.

Kutokana na umuhimu wa zoezi hilo Tume imejipanga kuhakikisha kila kundi ndani ya jamii ikiwemo ile ya walemavu wanashiriki kikamilifu zoezi hilo ambalo litaambatana na utoaji wa vitambulisho vipya vya wapiga kura vitakavyotumika kwenye wakati wa uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Hayo yalisemwa mjini Kibaha na makamu mwenyekiti wa (NEC) Jaji Mstaafu Hamid Mahmoud Hamid, wakati wa mkutano wa Tume na waandishi wa habari wa mkoa wa Pwani juu ya uboreshaji wa Daftari hilo la wa Wapiga Kura. “Tumejipanga kuhakikisha hata watu wenye ulemavu wakiwemo, wasioona, walemavu wa viungo, viziwi na ulemavu wa aina yoyote ile kwani nao wanahaki ya kupiga kura kuchagua viongozi wanaowataka,” alisema Jaji Hamid.

Aidha alisema kuwa kwa wale wasio na viungo vya mikono (vidole) watatambulika kwa sura kupitia picha lakini kwa wale wasio na tatizo watachukuliwa alama za vidole 10 vya mikono, sahihi na picha. “Zoezi hilo litatumia teknolojia mpya ya Biometric Voter Registration (BVR) ambayo itachukua taarifa za mtu za kibaiolojia au tabia ya mwanadamu na kuzihifadhi katika kanzi data (Database) kw ajili ya utambuzi ambapo mfumo huu utasaidia kuwa na daftari sahihi na linaloaminika zaidi kwa ajili ya upigaji kura za maoni na uchaguzi mkuu wa 2015,” alisema Jaji Hamid.

Jaji Hamid alisema kuwa kwa zoezi hilo vituo vitasogezwa na kuwa vingi zaidi ili kurahisisha walengwa kupata huduma karibu zaidi badala ya kutembea umbali mrefu. Kwa upande wake mkurugenzi wa sera na mipango wa NEC Orgenia Mpanduji alisema kuwa waandishi ni kiungo muhimu cha kuhamasisha wananchi kushiriki zoezi hilo ambalo litakuwa la siku 14.

Mpanduji alisema kuwa endapo wananchi watshindwa kutumia kipindi hicho kuboresha taarifa zao watakuwa hawawezi kupiga kura hivyo ni vema wakatumia fursa hiyo ili kufanikisha zoezi hilo litakalowapatia vitambulisho ambavyo vitatumika kwenye zoezi la upigaji kura tu pekee.

MSHINDI WA ‘CHEMSHA BONGO YA BRAZIL’ AKABIDHIWA CHAKE

0
0
MSHINDI wa Chemsha Bongo ya Brazil inayoendeshwa na gazeti la Championi, Afande Jamila Omari Mkele, leo amekabidhiwa king'amuzi na dishi kutoka Azam TV pamoja na televisheni ya kisasa (flat screen) kutoka kampuni ya Sony baada ya kushinda shindano hilo.

Makabidhiano hayo yamefanyika leo katika ofisi za Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Uwazi, Amani, Risasi,  Ijumaa,  Championi na Ijumaa Wikienda.
Afisa Masoko wa Azam TV, Shah Mrisho (kulia) akimkabidhi zawadi zake Afande Jamila.
Afande Jamila baada ya kukabidhiwa zawadi zake.
Afisa Masoko wa Global Publishers, wachezashaji wa Bahati Nasibu hiyo, Innocent Mafuru, akiongea na wanahabari baada ya mshindi kukabidhiwa chake.
Afisa Masoko wa Azam TV, Shah Mrisho, akiwaeleza jambo wanahabari (hawapo pichani).
PICHA : RICHARD BUKOS / GPL     

msaada.

0
0
Msaidizi wa waziri wa maliasili na utalii,Helen Mtalemwa,akimkabidhimsaada wa shilingi 10 milioni  katibu wa ofisi ya Qadhi mkoa wa Singida,Alhaj Burhan Mlau kwa ajili ya kupunguza makali ya uendeshaji wa mahakama hiyo mjini hapa. 
 Mkuu wa wilaya ya Singida, Queen Mlozi, akizungumza muda mfupi kabla msaidizi wa Waziri wa Maliasili na Utalii,Helen Mtalemwa (wa pili kulia) kukabidhi shilingi milioni kumi kwa ajili ya kuipunguzia makali ya uendeshaji ofisi ya Qadhi mkoa wa Singida.

Viewing all 109597 articles
Browse latest View live




Latest Images