Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live

HONGERA BONGO FC

$
0
0
 (Timu ya watanzania Bongo FC yenye maskani yake Finland.Picha baada ya pambano lake na timu ya Nigeria na kufanikiwa kuzoa ushindi mnene wa mabao 4-2.)
Bongo FC miongoni mwa timu kongwe na kielelezo cha uwakilisha wa Tanzania kwenye ukanda wa nchi za 'scandnavia'.

Bongo FC imefanikiwa kuanza kampeni yake ya msimu wa majira ya kiangazi kwa kucheza michezo miwili.Mchezo wa kwanza waliifunga timu Ethiopia magoli  5-3 na mwishoni mwa juma kuifunga timu ya Nigeria 4-2.

Wafungaji wa magoli akiwa Mwita Chacha , Bakari Salehe, Tonny aka Diego Simeon..Hizi ni salaam kwa ndugu zetu wa Sweden Kilimanjaro FC...

Hongera Bongo FC 

Picha zaidi unaweza tembelea  http://edondaki.blogspot.fi/
Tutafika tu

BINTI SELITIAN NATA,MWENYE UVIMBE ANAOMBA MSAADA WA MATIBABU

$
0
0
Na John Gagarini, Bagamoyo.
 
MSICHANA Selitian Nata (25) mkazi wa Kijiji cha Kisogo kata ya Vigwaza Wilayani Bagamoyo mkoani Pwani yuko kwenye hali mbaya ya kiafya baada ya kuvimba mguu na kuwa kwenye maumivu makali.Ugonjwa huo uvimbe huo ulianza kama kipele kidogo miaka zaidi ya 10  iliyopita lakini kadiri siku zilivyokuwa zikienda ndipo uvimbe huo ulizidi kuongezeka na kufikia usawa wa mbavu.
 
Akizungumza na waandishiw ahabari ambao walimtembelea nyumbani kwao alisema kuwa uvimbe huo una ambatana na maumivu makali pamoja na homa kali hasa nyakati za usiku.
 
“Niko kwenye wakati mgumu kama mnavyoniona napata shida naomba nisaidiwe kwani nimekwenda hospitali toka kipindi hicho lakini sikupata matibabu zaidi ya kupewa vidonge tu ambavyo hupunguza maumivu lakini uvimbe uko pale pale,” alisema Nata.
 
Nata ambaye ana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miaka (2) alisema kuwa wakati tatizo hilo linaanza alikwenda hospitali mbalimbali lakini hakuweza kupatiwa matibabu sahihi na kupelekea uvimbe huo kuongezeka hadi hapo ulipofikia na kumkosesha raha.
 
“Naomba wataalamu mbalimbali pamoja na wafadhili ili niweze kupata matibabu sahihi ambayo yataondoa uvimbe huu ili name niweze kuishi kwa raha kama wengine,” alisema Nata.
 
Kwa upande wa baba yake Nata Mumbi alisema kuwa alimpeleka mwanae kwenye hospitali mbalimbali kwa ajili ya matibabu lakini hakuna mafanikio yoyote.“Tatizo matibabu ambayo wanayompa si ya kina jambo ambalo linasababisha mwanangu asipate nafuu, lakini kupitia vyombo vya habari naomba wasamaria wema wamsaidie mwanangu ili aweze kupata matibabu sahihi,” alisema Mumbi.
 
Aidha alisema kuwa anashangaa kuona kila anapokwenda hospitali mwanae anapewa vidonge tu jambo ambalo linafanya wakate tamaa ya kumpatia matibabu.

NEWS ALERT:AJALI YAUA MTU MMOJA IRINGA

$
0
0
baada ya ajali hiyo, 
Inavyoonekana kwa nyuma
hii ni sehemu ya mbele ya gari hilo
Scania lililogongwa kwa nyuma.
Sehemu ambayo gari hilo dogo liliingia.
AJALI mbaya iliyohusisha gari dogo aina ya Land Rover Freelander lenye namba T368 CVK na roli la mizigo aina ya Scania lenye namba T346 BRF imetokea usiku wa juzi katika eneo la Lugemba, kilomita kadhaa kabla ya kufika mji wa Mafinga.

Taarifa za awali zinaonesha kwamba dereva wa gari hilo jina lake bado halijapatikana alifariki papohapo baada ya gari yake kuingia nyuma ya roli hilo lililokuwa limepaki kandakando ya barabara ya Mafinga Dar es Salaam, akiwa katika mwendo mkali.

Mwanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Tumaini aliyekuwemo katika gari hilo amenusurika kufa; binti huyo ambaye pia jina lake halikupatikana amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Mufindi baada ya kujeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na kukatika mkono.

Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ajali hiyo ilitokea majira ya saa 3 usiku. Na baada ya ajali hiyo wasamalia wema waliukumbiza mwili wa marehemu na majeruhi katika hospitali ya wilaya ya Mufindi.

Jeshi la Polisi limethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na taarifa za awali zinaonesha dereva wa gari hilo alikuwa amelewa wakati akiendesha gari hilo.
HABARI PICHA NA FRANCIS GODWIN-IRINGA

MFUKO WA PSPF WAMALIZA WIKI YA UTUMISHI KWA MAFANIKIO MAKUBWA

$
0
0
Ofisa masoko wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma'PSPF' Bi, Rahma Ngassa kulia akimkaribishakatibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue katika banda la PSPF wakati wa maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyomalizika jumatatu ya wiki hii
Add caption
Ofisa uhendeshaji wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma 'PSPF' Bw, Mohamed Masoud kulia akimpatia mahelezo katibu Mkuu Kiongozi  Balozi Ombeni Sefue alipotembeleabanda la PSPF wakati wa maonesho ya wiki ya utumishi wa Umma yaliyomalizika jumatatu ya wiki hii
Mkurugenzi wa mipango ya uwekezaji wa mfuko wa pesheni kwa watumishi wa umma 'PSPF' Bw, Gabriel Silayo katikati akiwa na baadhi ya maofisa wa PSPF wakati wa maadhimisho ya wiki ya utumishi wa umma
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII,TASAF NA JITIHADA ZA KUPAMBANA NA UMASIKINI NCHINI.

$
0
0
Afisa kutoka TASAF makao makuu Bw. Geodfrey Nyamwihula akisisitiza jambo kwa walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja wakati walengwa wa mpango huo walipopewa mafunzo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP ambayo ni moja ya jitihada za serikali kupitia TASAF kuongeza pato la kaya husika .

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF umeanza zoezi la kuwashirikisha walengwa wa Mpango wa kunusuru kaya masikini kuibua miradi ya Ujenzi PWP ambayo kwa mujibu wa taratibu walengwa watatumia fursa ya kufanya kazi katika miradi watakayoibua kwenye maeneo yao na kisha kulipwa ujira ambao utasaidia kuwaongezea kipato.

Walengwa watafanya kazi hiyo kwa kipindi cha siku 15 katika mwezi na siku 60 kwa mwaka hususani wakati wa kipindi cha hari (kipindi kigumu).Chini ya utaratibu huo asilimia 75 ya fedha zitalipwa kwa walengwa na 25 zitatumika kununua vifaa vitakavyotumika kwenye mradi husika.
Mwezeshaji wa Mpango wa uibuaji miradi ya Ujenzi Issa Jabri akitoa maelezo ya namna ya kuibua miradi ya ujenzi PWP katika shehia ya Bandamaji wilaya ya Kaskazini B Unguja.
 Pichani walengwa wa PWP katika shehia ya Mpapa wakisikiliza maelezo kutoka kwa mwezeshaji (hayupo pichani) juu ya namna ya uibuaji wa miradi kwenye eneo lao.
Mwezeshaji wa PWP katika shehia ya Kipange,huko Unguja Bi. Hidaya Mussa akitoa maelezo ya namna ya kuibua Miradi ya Ujenzi PWP kwa walengwa wa mpango huo .

Rais Kikwete apewa Tuzo Ya Uongozi Bora nchini

$
0
0
 Mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali Bwana Ludovick Utouh akikmabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete Tuzo maalum kwa kutambua mchango wange kwa taasisi simamizi katika kuimarisha Uwazi,Uadilifu na uwajibikaji wakati wa hafla maalum ya chakula cha jioni iliyofanyika katika ukumbi wa  wa kimataifa wa  mikutano Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam leo jioni.

Bwana Utouh alikabidhi Tuzo hiyo kwa niaba ya taasisi sita ambazo niBodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi,TAKUKURU,,Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma,Mamlaka ya udhibiti wa Mifuko ya Hifadhi ya jamii,Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Serikali,na Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa umma (picha na FreddyMaro).

ngoma azipendazo ankal

$
0
0

"I will be right here waiting for you" - Richard Marx

EAC SENSITIZATION WORKSHOP ON VIDEO CONFERENCING PROJECT HELD IN ARUSHA

$
0
0

..As official launching of project set for 30 November
East African Community Secretariat, Arusha, Tanzania,23 June 2014: An East African Community Sensitization Workshop on Video Conferencing (V.C) Project  concluded the EAC headquarters in Arusha, Tanzania

The 19th -20th June workshop aimed at facilitating the establishment and operation of a scalable and extensible Video Conferencing system for interactive Audio Visual communications and virtual meetings among EAC Organs and Institutions, Partner States and other organizations.

The Video Conferencing (V.C) Project  originated from the decisions of the Council of Ministers with regard to strengthening the institutional capacity of EAC to discharge its functions in pursuit to the provisions in the Treaty Establishing the East African Community.

To create awareness of the Project, the Project Implementation team proposed the development of a comprehensive communication strategy to support the project.

Speaking at the opening  ceremony on behalf of the Secretary General, EAC  Acting Director of Finance and Administration, Mr. Juvenal Ndimurirwo, called  upon members at the workshop to identify communication priority components of the project as well as implementation timetables.

Mr. Juvenal Ndimurirwo stated  that while there is a highly technical component to the Project, the underlying motive is to support the management process. It is for this reason that the meeting was tasked with formulating a workplan that will ensure the project is widely known amongst stakeholders at the EAC and Partner States.
The EAC Principal Information and Technology Officer, Mr. Aggrey Nkondola echoed the Director’s statements by adding that sustainability of the project can be achieved if the project is institutionalized to effectively support EAC meetings.

He noted that in addition to the development of appropriate policies and procedures, adequate human and financial resources must be made available to better guarantee sustainability.
.
The workshop was attended by Information Technology and Communication experts from the Partner States as well as I.T experts from TMEA who provided insight into implementing Video Conferencing projects.

The EAC Video Conferencing project has three main components namely: equipment supply, room preparation and bandwidth provision. Equipment for this project is expected to be delivered to all six sites (Arusha and the five Partner States), by end of July, while installation will commence in August 2014.

The official launch of the project is set for 30 November 2014, on the sidelines of the EAC Heads of State Summit. A Project Steering Committee and a Project Implementation team responsible for decision making and operational implementation respectively have been established.

During the end of the workshop, the group developed a communication activity work plan that will address among others awareness creation about the project before, during and after its launch within EAC Organs and Institutions, EAC Ministries, and other stakeholders at large as well as a draft human resource requirements for implementation of the project.

KATIBU MKUU KIONGOZI AELIMISHWA KUHUSU UTHAMINI MADINI YA ALMAS

$
0
0
·        TANESCO  Yaibuka Mtoaji Huduma Bora na Ubunifu
·        Wizara yaingia 10 Bora

Na Asteria Muhozya, Dar es Salaam

Katibu Mkuu Kiongozi,  Balozi Ombeni Sefue ametembelea banda la Wizara ya Nishati na Madini wakati wa kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma na kupata fursa ya kusikiliza maelezo kutoka kwa wataalam wa Wizara kuhusu shughuli mbalimbali zinazofanywa na Wizara ya Nishati na Madini.

Akiwa katika banda la Wizara, Balozi Sefue ameelimishwa namna Kitengo cha Uthamini Madini ya Almas na Vito (TANSORT) kinavyofanya shughuli za Uthamini madini ya Almas na namna kitengo hicho kinavyopata bei za madini katika soko la Kimataifa na namna kinavyowasiliana na wachimbaji kuwafahamisha kuhusu bei hizo katika soko la Kimataifa.

Aidha, Katibu Mkuu Kiongozi amefahamishwa kuhusu namna mashine ya Umeme Tayari (UMETA) “Ready Board” inavyofanya kazi. Akitoa maelezo namna kifaa hicho kinavyofanya kazi, Mhandisi  Mwandamizi  Masoko na Huduma kwa Wateja, Juliana Pallangyo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) ameeleza kuwa, kifaa hicho kinatumika katika maeneo yasiyohitaji ‘wiring’ hasa vijijini na kinatolewa bure vijijini.

Katika hatua nyingine, TANESCO limeibuka na ushindi wa kuwa miongoni  mwa taasisi tatu bora zinazotoa huduma kwa ubunifu katika kilele cha Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, ambapo Wizara ya Nishati na Madini imekuwa miongoni mwa taasisi  10  zenye mabanda bora katika maonesho hayo yaliyofikia kilele leo katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam. 

Akifunga rasmi maonesho hayo, mgeni rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue amesisitiza watumishi wa umma kuwatumikia wananchi kwa uadilifu, ukarimu, upendo, weledi na kwa wakati. 
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akimsikiliza Mtaalamu wa madini ya Vito vya Rangi na Almas Bibi Teddy Goliama kutoka Kitengo cha Uthamini Madini ya Almas na Vito (TANSORT), Wizara ya Nishati na Madini, akimweleza namna Idara hiyo inavyofanya shughuli za Uthamini wa Madini ya Almas. Kushoto kwa Katibu Mkuu Kiongozi ni Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Bw. Eliakim Maswi na anayefuatia ni mmoja wa wateja waliofika bandani hapo.
 Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini  Bw. Eliakim Maswi  (kushoto)akimweleza jambo mgeni aliyefika katika Banda la Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) aliyetaka kufahamu kuhusu Mradi wa Umeme Vijijini unaosimamiwa na Wakala wa Umeme Vijijini (REA). Wa pili kulia anayesikiliza na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Ngosi Mwihava na katikati ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikali Wizara ya Nishati na Madini Bibi Badra Masoud.
  Baadhi ya Watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini na Taasisi zake wakiwa katika picha ya pamoja baada ya TANESCO kupata kombe la Ushindi katika kipengele cha Taasisi iliyotoa huduma Bora na Ubunifu wakati wa Maonesho hayo.
Mhandisi Mwandamizi Masoko na Huduma kwa Wateja, Juliana Pallangyo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) akimweleza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue namna mashine ya Umeme Tayari (UMETA) “Ready Board” inavyofanya kazi. Anaesikiliza ni Katibu Mkuu Bw. Eliakim Maswi wa pili kushoto kwa Katibu Mkuu Kiongozi na anayefuatia ni mgeni aliyefika banda la Wizara.

  

JUMUIYA YA WATANZANIA NCHINI KOREA KUSINI YAIPEPERUSHA VYEMA BENDERA YA TANZANIA

Serikali ya Ujerumani Yaahidi Kutoa Msaada wa Euro Milioni Moja Kusaidia uhifadhi wa pori la akiba selous

George W Bush, Tony Blair and ISIS

umbea wa nathan mpangala

DILI LA kutafsiri Video za mkutano wa TED kwenda Kiswahili

$
0
0
Habari zenu wadau,

Kwa wale ambao hawalifahamu hili ni kwamba kuna mkutano ambao umekuwa maarufu sana duniani unaitwa TED(TED: Ideas worth spreading), mkutano huu unakusanya wataalamu wa kada mbalimbali kujadiliana kuhusu jinsi ya kutatua na kukabiliana na changamoto mbalimbali za maisha. 
mijadala hii inarekodiwa katika video ambazo mtu yeyote anaweza kuziangalia, lakini mara nyingi lugha inayotumika katika mijadala hii ni kiingereza ,ili kuweza pia kuwafikia watu wengine duniani ambao kiingereza sio lugha yao, TED imeanzisha mpango wa kujitolea wa mtu yeyote kutafsiri video hizi kwenda katika lugha yake. 
Kwa upande wa kiswahili mwamko umekuwa mdogo mno, ukizingatia kutafsiri ni rahisi sana kwa mtu yeyote ambaye ana nia hiyo. kuna fursa mbalimbali ambazo TED wanazitoa kwa watu wanaojitolea kama kupewa nafasi za kuangalia mikutano ya TED live wakati inafanyika popote pale duniani. Kwa yule atapenda kufanya hivyo, tafadhali tembelea hapa , Translate | Participate | TED . jisajili na fuata maelekezo mafupi ili uweze kuanza kutafsiri.

Asanteni
MDAU WA TED

SHULE YA JAMII YA WAMAASAI WILAYANI HAI YAPIGA MAENDELEO YA KASI

$
0
0
 Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga akihutubia wazazi,wanafunzi na wageni waalikwa katika siku ya shule ya The O'Brien School for the Maasai.
Siku maalumu ya shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza kwa watoto wa jamii ya Kimaasai iliyopo katika kijiji cha Sanya Stesheni wilayani Hai ya The O'Brien School for the Maasai
  Sehemu ya wageni kutoka nchini Marekani waliohudhuria sherehe za siku ya shule ya msingi ya mchepuo wa kiingereza ya O'Brien ya Hai
 Diwani wa kata ya Kia,Sinyoki Ole Nairuki akiwatambulisha wageni mbalimbali katika sherehe za siku ya shule ya O'Brien.
 Mkuu wa wilaya ya Hai,Novatus Makunga na mfadhili Bibi Kellie O.Brien wakishuhudia shughuli mbalimbali za siku ya shule ya msingi ya O'Brien.
 Wanafunzi wa shule ya O'Brien wakitoa burudani
  Sehemu ya akinamama wa Kimaasai waliohudhuria shule ya siku ya shule ya The O'Brien School for the Maasai
Buruduni mbalimbali za ngomba za asili zikiendelea.

CHINA NA TANZANIA ZAZINDUA UJENZI WA JENGO LA TAASISI YA MWALIMU NYERERE JIJINI DSM

$
0
0
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (kushoto) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (kulia) kwa pamoja wakizindua jiwe la msingi katika eneo litakapojengwa jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao (katikati) na Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda (wa pili kulia) kwa pamoja wakimwaga mchanga kuashiria kuanza kwa ujenzi jengo la Taasisi ya  Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania Lu Youqing.
 Makamu wa Rais wa China Li Yuanchao ( kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda, Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli Edward Lowassa akisalimiana na Rais mstaafu wa awamu ya pili Ali Hassan Mwinyi (Kulia) na Mama Maria Nyerere wakati wa hafla ya uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere.
Viongozi mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa jengo la Taasisi ya Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam. Kutoka kushoto ni Mama Maria Nyerere, Rais Mstaafu wa Wawamu ya tatu, Benjamini Mkapa,Waziri Mkuu mstaafu Cleopa Msuya na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Warioba.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

DAR LIVE INAKULETEA FUNGA KAZI, JUMAMOSI JUNE 28, 2014

Mama Kikwete apewa Zawadi ya Kinyago

$
0
0
 Mkrugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Mifuko ya Hifadhi za jamii(SSRA) Bibi Irene Kisaka akimkabidhi zawadi ya kinyago cha mpingo Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwa kutambua mchango wake katika kumsaidia Mh.Rais katika jitihada zake za kujenga utawala bora nchini katika hafla iliyofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa kimataifa wa Julius Nyerere(JNICC) jijini Dar es Salaam jana usiku(picha na Freddy Maro).

WADAU WAKUTANA LEO KUJADILI UTAYARI WA TANZANIA KATIKA KUPOKEA NA KUTUMIA FEDHA ZA KUPAMBANA NA MABADILIKO YA TABIANCHI

$
0
0
 Meneja Mradi wa Mazingira UNDP, Helene Gichenje akifafanua jambo kwa wadau wa mazingira wakati wa mkutano wa kujadili ripoti ya awali juu utayari wa Tanzania katika kupokea na kutumia fedha za misaada za kupambana na mabadiliko ya tabianchi
Msimamizi wa masuala ya mabadiliko ya tabinachi wa UNDP, Abbas Kitogo akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mkutano wa kujadili ripoti ya awali juu utayari wa Tanzania katika kupokea na kutumia fedha za misaada za kupambana na mabadiliko ya tabianchi
Baadhi ya wadau wa mazingira waliohudhuria mkutano wa kujadili ripoti ya awali juu utayari wa Tanzania katika kupokea na kutumia fedha za misaada za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.
PICHA ZAIDI BOFYA HPA

MAKAMU MWENYEKITI WA CCM (BARA) PHILIP MANGULA AKUTANA NA MAKAMU WA RAIS WA CHINA LI YUANCHAO

$
0
0
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Philip Mangula akimkabidhi zawadi Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa  China Li Yuanchao mara baada ya kumaliza mkutano .
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa  China Li Yuanchao akionyesha zawadi aliyopewa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula mara baada ya kumaliza mkutano baina ya viongozi wawili.
 Viongozi wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Watu wa  China Li Yuanchao(hayupo pichani) kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Balozi wa China Nchini Tanzania Lu Youqing akifafanua jambo wakati wa Semina ya Ujamaa iliyohusisha CCM na CPC kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
 Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Ndugu Philip Mangula akizungumza wakati wa Semina inayohusu Umuhimu wa Ujamaa na Kukua kwa Uchumi,wengine pichani(kushoto) ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Abdala Bulembo ,Mwakamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM Mboni Mhita ,Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana CCM Ndugu Sixtus Mapunda ,Profesa Max Muya ,na Makwaia wa Kuhenga.
 Mr Ma Zhongji kutoka Ubalozi wa China akisaidia kutafsiri wakati wa Semina ya Ujamaa iliyohusisha CCM na CPC iliyofanyika kwenye Hotel ya Serena jijini Dar es Salaam.
Viewing all 109921 articles
Browse latest View live




Latest Images