Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 477 | 478 | (Page 479) | 480 | 481 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Na Johary Kachwamba- MAELEZO.

  Maonesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-salaam (38th DITF) yanatarajia kuanza tarehe  28 mwezi huu na kufikia kilele chake tarehe 8 Julai  2014 katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu J.K. Nyerere, barabara ya kilwa, jijini Dar-es-salaam.

  Akitoa taarifa hiyo leo jijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TanTrade Bibi. Jacqueline Mneney Maleko imeeleza kuwa maonesho  ya  mwaka huu yataongozwa na kauli mbiu isemayo “Tunaunganisha Uzalishaji na Masoko”

  Amesema kuwa Kauli Mbiu hiyo imechaguliwa kutumika kuonesha uhusiano uliopo kati ya Uzalishaji na Masoko  na umuhimu wa mnyororo wa uzalishaji ambao ndio chimbuko la upatikanaji wa Bidhaa bora zenye ushindani katika soko. 

  Bibi. Maleko amesema kuwa mwaka huu TanTrade imetenga eneo kubwa zaidi kwa ajili ya Wazalishaji wa ndani ya nchi na kubainisha maeneo yatakayotumiwa na wazalishaji hao kuwa ni jengo namba C.19 na eneo la wazi lililo nyuma ya ofisi za Mkurugenzi wa Utafiti, Mipango na Uwezeshaji kwa ajili ya bidhaa za kilimo na bidhaa zinazotengenezwa Tanzania.

  Kuhusu ushiriki wa mataifa mengine katika maonesho hayo amefafanua kuwa tayari nchi 31 zimethibitisha kushiriki maonesho hayo zikiwemo Afrika Kusini,Czech Republic, China, Ghana, Indonesia, India, Iran, Finland, Ugiriki, Italia, Japan, Jordan, Kenya, Korea ya Kusini, Malaysia, Marekani, Misri, na Ujerumani.

  Nchi zingine ni pamoja na Nigeria, Pakstani, Rwanda, Saudi Arabia, Singapore, Sudani, Syria, Uganda, Uingereza, Burundi, Sweden, Vietnam na Zimbabwe.

  Aidha, amefafanua kuwa makampuni ya nje 490 yamethibitisha kushiriki katika maonesho hayo huku  Wizara na Taasisi za Serikali zilizothibitisha kushiriki maonesho hayo zikifikia 61. 

  Kwa upande wa Mikoa amesema tayari mikoa 10 imethibitisha kushiriki ikiwemo, Mikoa ya Iringa, Ruvuma, Mbeya, Pwani, Kigoma, Kagera, Geita, Mara, Manyara na Ruvuma. Jumla ya Washiriki waliothibitisha kushiriki kutoka ndani ya nchi ni 1700.

  Kuhusu  kiingilio wakati wa maonesho hayo amesema watu wazima walipia Shilingi 2,500 na watoto ni 500 kila siku kwa siku zote za maonesho isipokuwa tarehe 7 Julai,2014 ambapo ada itakuwa Shs. 3,000/= kwa watu wazima  na watoto ni Shs.1000/=

  0 0

   Wafanyakazi wa Kampuni ya Proin Promotions katika Mradi wa Kusaka vipaji vya Kuigiza Nchini TMT (Tanzania Movie Talents) wakishangilia kwa kufungua Mvinyo usio na kilevi mara baada ya kumaliza zoezi la Kuzunguka Katika Kanda Sita nchini kwa kusaka Vipaji vya kuigiza ambapo zoezi hilo lilimalizika katika Kanda ya Pwani, Mkoani Dar Es Salaam ambapo washindi watano kutoka kanda ya Pwani walipatikana na Kupewa zawadi zao za Shilingi laki Tano Kila Mmoja na Kushiriki katika fainali ya Kuwania Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
  Mmoja wa Majaji katika Shindano la TMT Yvonne Cherry au Monalisa akifurahia kufungua Mvinyo huku wafanyakazi wa Proin wakifurahia pia kwa kukinga mvinyo huo mara baada ya kumalizika kwa zoezi la kusaka vipaji vya kuigiza katika Kanda ya Pwani ambapo ndio imefunga zoezi hilo lililoanzia Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini.
  Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin Group of Companies,Bw Johnson Lukaza akiongea na wafanyakazi wa Proin Promotions limited mara baada ya kumaliza vizuri kwa kazi za kutafuta vipaji katika Kanda Sita za Tanzania.Pamoja na kuongea na wafanyakazi hao aliweza kutoa neno la shukrani kwa kila mmoja kwa kutimiza wajibu wake na hatimaye kufanikisha zoezi hilo la hatua ya kwanza kumalizika vyema.
  Na Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar es Salaam.
  Safari ya Kutafuta vipaji katika Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) ilianzia Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza ambapo timu nzima ya TMT ilikuwa katika kanda hiyo kwaajili ya kusaka vipaji kupitia shindano hilo kubwa na la kwanza kufanyika Afrika Mashariki na Kati. 

  Shindano la Tanzania Movie Talents ni shindano ambalo lilizunguka kanda zote sita za Tanzania na hatimaye kilele chake kilimalizika mnamo tarehe 18 Juni 2014 katika Ukumbi  wa Makumbusho ya Taifa Jijini Dar es Salaam katika Ukanda wa Pwani na kupelekea washindi watano kupatikana na kukabidhiwa Shilingi laki tano kila Mmoja.
  Mara baada ya kumalizika kwa hatua ya kwanza ya kutafuta washindi kutoka kanda zote sita sasa ni wakati wa washindi wa kanda hizo kuja jijini Dar es Salaam na Kukaa kambi moja huku wakipatiwa mafunzo kutoka kwa Walimu wa Sanaa kutoka Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Chuo Cha Sanaa Bagamoyo lengo likiwa ni kuwapika kisanaa na kuanza kushindanishwa ili kuweza kupata Mshindi mmoja ambaye ataondoka na kitita cha Shilingi Milioni 50 katika fainali itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane Jijini Dar Es Salaam.
  Mara baada ya Fainali hiyo kumaliza washindi kumi watakaopatikana watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions na wataweza kutengeneza filamu ya Pamoja na hatimaye kuja kunufaika na filamu hiyo.
  Shindano la TMT limekuwa ni shindano kubwa kabisa ambalo halijawahi kufanyika nchini na limekuwa likirusha vipindi vyake katika kituo cha Runinga cha ITV kuanzia mida ya Saa Nne Usiku siku ya Jumamosi na Marudio yake ni Kila Jumapili Saa 10 Jioni na Jumatano Saa 5 usiku huku Jumamosi ya tarehe 21 Juni 2014 kipindi cha Dar Es Salaam kitarushwa kupitia kituo hiko cha runinga na hatimaye Kazi ya Mchujo Kuanza Mara moja mara baada ya washindi wa kanda zote kuwasili Jijini Dar Es Salaam na kuanza kambi huku wananchi watakuwa wakiwapigia kura washiriki ambao wanawaona wenye uwezo.

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni mkuu wa wilaya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu kuanzishwa kwa mfuko wa kuwasaidia wafanyabiashara wa soko la Mchikichini walioathiriwa na janga la moto kwa lengo la kurejesha hali ya maisha waliyokuwa nayo hapo awali.
  Mmoja wa waanzilishi wa mfuko wa kuwasaidia waathirika wa moto soko la Mchikichini ambaye pia ni Meneja wa Vituo vya mizigo vya nchi kavu wa Kampuni ya AZAM Bw. Raymond Adolph akieleza namna walivyoguswa na tukio la moto lililotokea katika soko hilo na kuwaomba watanzania kuunga mkono juhudi hizo.
  Mwenyekiti wa wafanyabiashara wa soko la Mchikichini Bw. Jumanne Kongolo akiongea na waandishi wa habari kuishukuru serikali na wananchi waliojitokeza kufungua mfuko wa kuwasaidia waathirika wa moto katika soko hilo.
  Baadhi ya wafanyabiashara wa soko la Mchikichini walioathiriwa na janga la moto wakifuatilia masuala mbalimbali ofisini kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakati wa uzinduzi wa mfuko wa kuwasaidia wafanyabiashara hao. Picha na Aron Msigwa –MAELEZO.

  Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es salaam wamejitokeza kuanzisha mfuko maaluum wa kuwasaidia wafanyabiashara wapatao 5700  wa soko la Mchikichini walioathiriwa na janga la moto  lililotokea usiku wa kuamkia tarehe 12 mwezi  huu eneo la Karume,jijini Dar es salaam.

  Akaunti hiyo maalum inayojulikana kwa jina la Mkono wa Pole Chinga 2014 imefunguliwa katika Benki ya CRDB Tawi la Lumumba ili kuwawezesha wadau mbalimbali wanaoguswa na tukio hilo kutoa mkono wa pole kupitia akaunti namba 0152270491300.

  Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ambaye pia ni mkuu wa wilaya Ilala Bw. Raymond Mushi akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam amesema kuwa mfuko huo unalenga kurejesha hali ya maisha waliyokuwa nayo wafanyabiashara hao hapo awali kabla ya kuungua kwa vibanda na bidhaa zao.

  Amesema akaunti hiyo itasimamiwa kwa pamoja na wawakilishi kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, wadau waanzilishi na wafanyabishara walioathirika.

  “Tumeanzisha akaunti hii kutokana na wananchi kuguswa na tukio hili kwa kuonesha nia thabiti ya kutaka kutoa mkono wa pole kwa waathirika wa janga hili, nachoweza kusema jambo hili tumeliwekea utaratibu na tutaliendesha kwa uwazi mkubwa kwa kushirikiana na wahusika wa tukio” amesema Bw. Raymond.

  Aidha, amefafanua kuwa serikali kupitia Manispaa ya Ilala ambayo soko hilo liko chini yake itahakikisha inaboresha hali ya miundombinu katika soko hilo zikiwemo barabara za kuwezesha magari na vifaa vya uokoaji kupita wakati wa majanga ya moto huku akiwataka  wafanyabiashara hao kutojenga na kuzuia maeneo ya barabara katika soko hilo.

   Mmoja wa waanzilishi wa mfuko huo ambaye pia ni Meneja wa Vituo vya mizigo vya nchi kavu vya vya Kampuni ya AZAM Raymond Adolph ameeleza kuwa yeye kama mfanyakazi na wafanyakazi wengine wameguswa na tukio la moto lililotokea katika soko hilo na kufafanua kuwa kiasi cha fedha kitakachopatikana kitakabidhiwa kwa walengwa kwa uwazi huku akiwaomba watanzania kuunga mkono juhudi hizo.

  “Akaunti hii tuliyoifungua itakuwa chini ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kiasi tutakachopata tutakikabidhi kwa wahusika kwa uwazi na tunawaomba watanzania wajitokeze ili kwa pamoja tuwasaidie ndugu zetu hawa waliopata matatizo” amesisitiza.

  Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara hao ambaye pia aliathiriwa na moto huo Bw. Jumanne Kongolo ameeleza ameishukuru serikali na wananchi waliojitokeza kufungua mfuko huo kwa lengo la kuwasaidia wafanyabiashara walioathirika na moto huo.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Wazee Mohammed Cheupe (katikati) na Seif Membe (kulia) kutoka Jimbo la Ruangwa ambao walitembela bunge mjini Dodoma Juni 20, 2014, kwa mwaliko wa mbunge wao Kassim Majaliwa ambaye pia ni Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.
  Mbunge wa Rungwe Magharibi, Profesa David Mwakyusa (kushoto) akiteta na Mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim Ahmed, Bungeni mjini Dodoma Juni 20, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Kwa niaba ya uongozi wa Golden bush veterans ambao ni mabingwa wa Tanzania Bara na visiswani yaani Mabingwa wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, napenda kuwapa taarifa kwamba timu kamili ikijumuisha kikosi cha kwanza kama kinavyoonekana katika picha, itaondoka siku ya jumamosi alfajiri kuelekea Makambako kwa ajili ya mechi mbili yaani Makambako Veterans VS Golden Bush na Mafinga Veterans vs Golden Bush.

   Games zote zitapigwa uwanja Makambako Veterans siku ya tarehe 22/06/2014. Kwakutambua umuhimu na ugumu wa game hizo, Golden Bush ametanguliza watu wafuatao kwenda kuweka mambo sawa, Godfrey Chambua a k a Hans Poppe (mwanasheria na mwenyekiti kamati ya ufundi na mambo ya kale), Awilly Mshanga mchezaji mwandamizi kutoka Mbeya na Nico Nyagawa  ambaye ndiye Nahodha msaidizi wa timu yetu.

  Aidha masafara wa wachezaji 28 ni viongozi watu utaondoka siku ya jumamosi. Mkuu wetu wa msafara bwana Waziri Mahadhi “Mandieta” ambaye ndie Mhazini wetu amekamilisha mambo yote ya kiutawala tayari kabisa kwasafari.

  Kwa siku chache zilizobaki tutaweka camp ya muda na kufanya mazoezi ufukweni mwa bahari tayari kabisa kutoa kipigo kwa timu hizo mbili.

  Tunasikitika wapenzi wetu wa Dar es salaam kwamba weekend hii hatutakuwepo kuwapa burudani hadi weekend inayofuata. Nawatakieni maandalizi mema ya mfungo mtukufu wa mwezi wa Ramadhan.

  Asanteni kwa kunisikiliza.

  Onesmo Waziri
  MsEmaji wa timu.

  0 0

   Kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei akionyesha silaha na mavazi ya kijeshi waliyokamatwa nayo Watuhumiwa hao.

  Na John Gagarini, Kibaha

  JESHI la Polisi mkoani Pwani limefanikiwa kuwakamata watu watatu akiwemo mtu Daniel Mtalisi mkazi wa Kisemvule wilaya ya Mkuranga ambaye alipitia mafunzo ya kijeshi kwa tuhuma za kufanya tukio la uhalifu wa kupora silaha na vitu mbalimbali.

  Mtuhumiwa huyo ambayealiwahi kupata mafunzo ya kijeshi kwenye Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kikosi namba 833 Oljoro Arusha na namba yake ni MT. 95150.

  Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa waandishi wa habari mjini Kibaha, kamanda wa Polisi mkoani humo Kamishna Mwandamizi Msaidizi wa Polisi (SACP) Ulrich Matei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 17 mwaka huu majira ya saa 2 usiku huko Kijiji cha Kisemvule kata ya Vikindu kata ya Mkuranga wilaya ya Mkuranga.

  Kamanda Matei alisema kuwa watuhumiwa hao wengine wakiwa ni Khalfan Abas (25) mkazi wa Mwanambaya na Mashaka Masanja (24) mkazi wa Mwongozo Kigamboni Jijini Dar es Salaam walikamatwa baada ya polisi kufanya msako mkali na kumkuta mtuhumiwa huyo akiwa na silaha hiyo ambayo walimpora Musa Kambangwa ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanambaya.

  “Watu hao walimvamia mlalamikaji ambaye alikuwa akirejea nyumbani kutoa kwenye biashara zake walimteka kisha kumpiga na walimwamuru awapeleke nyumbani kwake na kuichukua silaha hiyo bastola yenye namba A 569542 aina ya Browning, Carriber 7.65 mm, magazine 2 na risasi 23, chaja 1 ambavyo alikuwa amehifadhi nyumbani kwake,” alisema Kamanda Matei.

  Aidha Kamanda Matei alisema kuwa kabla ya kukamatwa watuhumiwa hao walifanya tukio hilo Juni 11 mwaka huu huko Kijiji cha Mwanambaya ambapo walimvamia mlalamikaji akiwa na mke wake.
  “Walimjeruhi kwa kutumia silaha mbalimbali za jadi na kumsababishia maumivu makali kisha kumtaka awape funguo ya nyumba yake ili waingie ndani lakini alikataa wakaendelea kumpiga hadi alipopoteza fahamu na kuichukua funguo na kuingia ndani na kuchuakua silaha hiyo na simu 2 aina ya Nokia, Inveta , deki 1 ya Dvd  na viatu pea moja kisha kutoweka na ndipo walipokuja kukamatwa Juni 17,” alisema Kamanda Matei.

  Alisema kuwa baada ya tukio hilo ndipo walipofanya msako na kufanikiwa kuvikuta vitu hivyo ambapo mtuhumiwa wa kwanza alikutwa na sare za Jeshi.

  Alibainisha kuwa mlalamikaji anaendelea vizuri na kuwataka watu kutoa taarifa za uhalifu ili kuzuia matukio hayo ambayo yameanza kuibuka kwa wingi na watuhumiwa hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara upelelezi wa tukio hilo utakapokamilika.

  0 0

  Na. Ally Mataula na Rocky Setembo.

  Wananchi wamehimizwa kutembelea banda la Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.

  Wito huo umetolewa na Afisa wa Maadili Mwandamizi Bw. Bazilio Mwanakatwe wakati akizungumza na Waandishi wa Habari waliotembelea banda la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika maonesho hayo.

  Bw. Mwanakatwe aliendelea kubainisha kuwa lengo kubwa la Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kushiriki maonesho hayo ni kutoa elimu kwa wananchi kuhusu majukumu na mamlaka ya Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma ili nao waweze kufahamu wajibu wao katika jukumu zito la kujenga na kuimarisha Maadili ya Viongozi nchini.

  “Suala la maadili ni mtambuka ambalo linahusisha kila Nyanja katika jamii hivyo usimamizi wake na ukuzaji wake unahitaji ushirikiano wa taasisi zote za umma, sekta binafsi, asasi za kiraia pamoja na jamii kwa jumla. Serikali peke yake haiwezi kufikia lengo lililokusudiwa hivyo inahitaji ushirikiano mkubwa kutoka kwa umma” alifafanua Bw. Mwanakatwe.

  Pamoja na kutoa elimu katika maonesho hayo, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inatoa huduma nyingine kama vile kupokea malalamiko moja kwa moja kutoka kwa wananchi yanayohusu ukiukwaji wa Maadili ya Viongozi Umma.
  Afisa toka Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Bw. Bazilio Mwanakatwe akielezea jambo alipokuwa akihojiwa na Mwandishi wa Habari katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
  Maafisa wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma wakitoa elimu katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayoendelea hivi sasa kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es salaam.
  Aliyekuwa Kamishna wa pili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji (Mst) Steven Ihema, akiuliza swali alipotembelea Banda la Maadili, katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma, yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es saam.

  0 0

  Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Ellentruda Mbogoro akifafanua jambo kuhusiana na huduma zinazotolewa na Mfuko kwa wadau waliofika bandani hapo kwenye maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
  Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma, Grace Michael (kushoto) akihakiki baadhi ya nyaraka zilizowasilishwa kwa ajili ya vitambulisho.
   Meneja wa Masoko na Elimu kwa Umma, Anjela Mziray akitoa ufafanuzi wa jambo kwa wananchj waliofika bandani hapo, wengine ni Luhende Singu na Geofrey Tumaini wakiendelea na huduma.
  Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma, Catherine Kameka (kulia) akielezea namna ya kujisajili kwa watu binafsi katika Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya.
  Baadhi ya wanachama wakipokea vitambulisho vyao baada ya kutimiza vigezo na taratibu zilizowekwa na Mfuko.
  Ofisa Udhibiti Ubora, Dr. Raphael Mwamoto akitoa ufafanuzi wa kitalaam kwa mdau.

  0 0

   Meya Wa Manispaa ya Ilala Mh Jery Silaa Wa Kwanza kulia  akifika eneo la Tabata St Marrys kukagua kipande cha barabara huyo ambacho kimezua mgogoro baina na Manispaa na Shirika la maji safi na salama DAWASA.
   Mwenyekiti wa Serikali za Mitaaa Bwana Hassan Chambuso akimuongoza Mh Meya wa manispaa ya Ilala Jery Silaa kwenda kujionea eneo la kipande cha barabara ya St Marys Tabata ambacho kinaleta shida baina ya Mkandarasi na Dawasa
  Mkandarasi wa barabara ya Tabata-St Mary Bwana  George Lupia wa pili kutoka kushoto akitoa ufafanuzi kwa Meya Wa Ilala Mh Jery Silaa kuhusu kukwama kwake kuendelea na Ujenzi kutokana na Mabomba ya Dawasa kupita Katikati ya barabara Hiyo.
  Pembenini maji yaliyotuama baada ya Bomba la Dawasa kupasuka Hivyo kuleta usumbufu kwa mkandarasi kukamilisha ujenzi wa eneo hilo.
  Akaamua kupanda kwa kasi baaada ya vizuizi kutolewa na yeye mwenyewe.

  Meya wa Manispaaa ya Ilala Mh Jerry Silaa ametembelea eneo la Tabata-St Marys kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo na pia kuweza kuona mabomba ambayo yanaleta mgogoro baina ya mkandarasi na Manispaaa na Dawasa,Akiwa eneo hilo la St Marys Mh Jerry Silaa ameweza kujionea namna mabomba ya Dawasa ambavyo yamepita katikati ya barabara na pembezoni yakiwa katika kima kifupi hivyo kumzuia mkandarasi kuendelea na ujenzi wake.

  Akiongea na vyombo vya habari Mh Meya Amesema kuwa barabara hiyo imetumia gharama za takribani bilioni 1 lakini imeshindwa kumalizika kwa wakati kwa sababu ndogo ya Dawasa kutokushirikiana nao ili kuweza kumpa mkandarasi ramani kamili ya bara bara hiyo,Meya Silaa akaongeza kuwa wameshawasiliana na wenzao wa Dawasa kuhusu tatizo hilo lakina wamekuwa hawapewi majibu kwa wakati na ya kuridhisha.

  Naye mkandarasi wa eneo hilo Bwana George Lupia amesema kuwa alipewa ramani na manispaa ambayo haikuonysha kama kuna mabomba ambayo yamepita hapo,lakini wakati ameanza kuchimba barabara hiyo ndio akakutana na mabomba hayo,Mkandarasi huyo akaongezea kwamba alishawasiliana na Dawasa kitambo sana lakini hapewi majibu ya kuridhisha kuhusu kushirikiana nao kuhamisha bomba hizo. 

  Naye Diwani wa kata Hiyo Bibi  Mtumwa Mohhamed amesema wanainchi wa eneo hilo wanapata tabu sana kwa kuwa magari yao hayawezi kutoka ndani wala kuingia kwa kuwa barabara imechimbwa kwa kina kirefu sana,hivyo amewaahidi wanainchi wa eneo Hilo kwamba wanaendelea kulitatua tatizo hilo na wenzao wa dawasco ili kuweza kuhamisha mabomba ya eneo hilo. 
   PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP. Suzan Kaganda akiongoza mafunzo ya ulinzi shirikishi kwa vijana wa Mkoa huo,yaliyofanyika leo tarehe 20.06.2014 katika shule ya msingi Idudumio iliyopo tarafa ya Nyasa wilaya ya Nzega.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP. Suzan Kaganda akikabidhi zawadi mbali mbali kwa vijana walioshiriki kwenye Mafunzo ya Ulinzi Shirikishi.


  0 0

  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi amewataka makocha wa mpira wa miguu wafanyie kazi kwa vitendo mafunzo wanayopata badala ya kuweka makabatini maarifa waliyopata.

  Akifunga rasmi mafunzo ya wiki mbili ya makocha wa mpira wa miguu ya Leseni B inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) jijini Dar es Salaam leo (Juni 20 mwaka huu), Rais Malinzi amewataka makocha hao kuwapa mafunzo ya awali (basic) walimu wa shule za msingi kwa vile TFF ina mpango wa kuhakikisha kila shule ya msingi nchini inapata mipira kumi kila mwaka.

  “Kila mwaka tutakuwa na mashindano ya kitaifa ya watoto wenye umri chini ya miaka 13 kuanzia mwaka huu. Hivyo ninyi makocha huko mnaporudi muwafundishe walimu wa shule za msingi mafunzo ya awali ya ukocha,” alisema.

  Kozi iliyohudhuriwa na makocha 26 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar ilikuwa chini ya Wakufunzi wa CAF, Honour Janza kutoka Zambia, na Sunday Kayuni na Salum Madadi wa Tanzania. Janza pia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Chama cha Mpira wa Miguu Zambia (FAZ).

  Makocha walioshiriki kozi hiyo ni Abdalla Mohammed Juma (Zanzibar), Abdul Banyai (Temeke), Abdul Nyumba (Temeke), Abdulmutik Haji (Zanzibar), Aley Mohammed (Zanzibar), Ali Vuai Shein (Zanzibar), Dennis Kitambi (Morogoro), Dismas Haonga (Ilala), Emmanuel Massawe (Shinyanga), Fikiri Elias (Arusha), Fulgence Novatus (Mwanza), Hababuu Ali Omar (Zanzibar), Juma Mgunda (Tanga) na Kidao Wilfred (Ilala).

  Wengine ni Maka Mwalwisi (Mbeya), Malale Hamsini Keya (Zanzibar), Mecky Maxime (Morogoro), Mohammed Tajdin (Temeke), Mussa Furutuni (Dodoma), Nassor Salum Mohamed (Zanzibar), Peter Mhina (Ruvuma), Said Mohamed Abdulla (Zanzibar), Salim Makame (Zanzibar), Salum Ali Haji (Zanzibar), Sebastian Nkoma (Ilala) na Wane Mkisi (Dar es Salaam).

  0 0

  Wananchi wengi wamesisimkwa na kufurahishwa na taarifa kwamba Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) inatarijia kuanza zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mapema mwezi Septemba 2014

  Wameseme maandalizi hayo ambayo ni ya kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015 na upigaji wa Kura za Maoni kwa ajili ya mchakato wa Katiba Mpya Hayo yamekuja wakati muafaka.

   Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufaa Damian Lubuva alibainisha mbele ya wahariri wa vyombo vya habari jana kwamba uborehasji wa Daftari la Wapiga kura utakuwa wa mfumo mpya wa Kiteknolojia ujulikanao kama Biometric Voter Registration (BVR) 

  Alisema katika mfumo huo taarifa za mtu za Kibiolojia au tabia ya mwanadamu zitachukuliwa na kuifadhiwa kwenye kanzi data ya Wapiga Kura. Katika mfumo huo wananchi wote wenye sifa za kuwa wapiga kura na wale walio na Kadi za Mpiga Kura watatakiwa kuandikishwa upya ili kupata Daftari sahihi linaloaminika zaidi kwa ajili ya upigaji Kura ya Maoni na Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015. 
  "Uamuzi wa kutumia mfumo huo mpya wa kuandikisha wapiga kura umefikiwa baada ya kubaini kasoro mbalimbali zilizokuwepo kutokana nma kutumia mfumo wa zamani wa Optical Mark Recognition (OMR) hadi kupelekea baadhi ya wadau wa uchaguzi kupigia kelele mfumo huo.
  "Kutumika kwa mfumo wa BRV kutasaidi kuondoa kabisa matatizo yaliyomo kwenye Daftari lililopo ikiwemo kuzuia mtu kujiandikisha zaidi ya mara moja. 
  “Ndugu zangu wahariri ni ukweli ulio dhahiri kwamba matumizi ya OMR yalisababisha kwa kiasi kikubwa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura kuwa na kasoro,zilizopelekea baadhi ya wadau wa uchaguzi kuhoji uhalali wake. Hivyo ni mategemeo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kuwa matumizi ya BVR yatapunguza au kuondoa kabisa matatizo yaliyomo kwenye Daftari lililopo”. Alisema Jaji Lubuva.
   Aidha Jaji Lubuva alitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa Wahariri na Waandishi wa Habari kutoa ushirikiano kwa NEC ilikufanikisha zoezi hili la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura kwa kusaidia kufikisha taarifa sahihi kwa wananchi ili wapate uekewa wa mfumo huu mpya utakaomtumika katika zoezi hilo, na kutoa hamasa wajitokeze katika viotuo vya kujiandikishia.
   Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uchaguzi Julius Malaba amesema kuwa maandalizi ya zoezi la uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura umekamilika kwa asilimia kubwa ikiwa ni pamoja na kufanya uhakiki wa vituo vya kujiandikishia ambapo jumla ya vituo 40,015 vimeainishwa kutoka vituo 24,919 vilivyokuwepo awali. 
  Malaba aliongeza kuwa ongezeko hilo la vituo limetokana na kushusha zoezi la uandikishaji wa Wapiga Kura kutoka ngazi ya Kata, na sasa utafanyika kuanzia ngazi ya Vitongoj,Vijijii na Mitaa ili kuwezesha kuwa karibu zaidi na wananchi.
   Malaba aliongeza kuwa Tume inatarijia kupokea vifaa kwa ajili ya zoezi hilo mapema mwezi Aguosti 2014 kwa aijili ya kuanza rasmi zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura, na kuongeza kuwa vifaa vichache vitawasili mapema mwezi julai kufanikisha mafunzo kwa watendaji watakao husika na zoezi la Uboreshaji wa Daftari la Mpiga Kura.
   Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Mpiga Kura linatarijiwa kuanza mwezi septemba 2014 ambapo kila kituo cha kujiandikisha kinakadiriwa kutumia siku 14 hadi zoezi kukamilika , na jumla ya takribani shilingi Bilioni 293 zinatarajiwa kutumika katika zoezi hilo.
  Jaji Mstaafu Damian Lubuva (kushoto) akifafanua jambo kwa wahariri wa vyombo vya habari (hawapo pichani) wakati wa semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini, kulia ni Mkurugenzi wa uchaguzi toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Julius Mallaba.
  Baadhi ya wahariri wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.

  Baaadhi ya wakuu wa Idara toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.

  Baadhi ya wahariri wakimfuatilia mtoa mada  kwa makini toka Tume ya Taifa ya Uchaguzi Bw. Julius Lubuva (hayupo pichani) mapema hii leo jijini Dar es Salaam wakati akifungua semina kwa wahariri wa vyombo vya habari juu ya maandalizi ya uandikishaji wapiga kura nchini.


  Picha zote na Eliphace Marwa - MAELEZO


  0 0

  Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa shilingi Milioni Nne ikiwa ni nusu malipo ya gharama ya shilingi milioni Nane ilizoahidi kutoa kwa ununuzi wa Mashua kwa ajili ya kufidia chombo cha Wavuvi wa Kijiji cha Kivunge kilichochomwa moto mwezi Januri mwaka huu wa 2014 katika Kisiwa cha Tumbatu.

  Ikasisitiza tena na kuonya kwamba hilo litakuwa ni tukio la mwisho kubebwa na Serikali la kulipa fidia kwa migogoro yoyote itakayosababishwa na wana jamii katika maeneo mbali mbali kutokana na hitilafu wanazoweza kuzikabili wana jamii wenyewe.

  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akikabidhi fedha hizo kwa mdhamini wa ujenzi wa Mashua hiyo Bwana Ali Makame Madaha { Cheupe } hafla iliyofanyika pembezoni mwa bahari ya Nungwi ilipochongwa mashua hiyo Mkoa wa Kaskazini Ungua.

  Akipokea fedha hizo mdhamini wa ujenzi wa chombo hicho cha uvuvi ambae pia ni Katibu wa Kamati Tendaji ya hifadhi ya Mnemba na Chwaka Bwana Ali Makame Madaha { Cheupe } alitahadharisha kwamba ongezeko la wavuvi katika baadhi ya sehemu hapa nchini ndio sababu kuu inayoleta migogoro ya uvuvi kwenye maeneo mbali mbali ya bahari.

  Akikabidhi rasmi chocho hicho kwa wavuvi wa Kijiji cha Kivunge na kushuhudia pia na Uongozi wa Serikali na Vyama vya Siasa wa Mkoa wa kaskazini Unguja Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliendelea kuwaasa Wananchi kwamba Serikali kamwe haitakuwa tayari kubeba dhamana ya kulipa fidia ya mali au vyombo watakavyoharibiana kwenye migogoro wanayoweza kuiepuka.

  Chombo hicho cha uvuvi walichokabidhiwa wavuvi wa kijiji cha kivunge kina uwezo wa kuchukuwa watu kwenda katika shughuli zao za uvuvi kati ya ishirini na ishirini na tano kwa wakati mmoja.
  Balozi Seif akimkabishi rasmi mashua iliyopewa jina Riziki zina Mungu Bwana Dhamiri Makame Juma wa Kijiji cha Kivunge iliyotengenezwa katika Kijiji cha Nungwi.
  Mdhamini wa ujenzi wa Mshua ya Riziki zina Mungu Bwana Ali Makame Madaha { Cheupe } alitia saini hati ya kuuza mashua hiyo akishuhudiwa na Balozi Seif kwa ajili ya kupewa wavuvi wa Kivunge.
  Balozi Seif ahesabu nusu ya fedha zilizoahidiwa kutolewa na serikali Milioni Nne { 4,000,000/- } kulipia fidia kutokana na mashua ya wananchi wa Kivunge kuchomwa moto katika kisiwa cha Tumbatu.
  Mashua ya Riziki zina mola iliyonunuliwa na Serikali kulipwa fidia wavuvi wa Kijiji cha kivunge kufuatiwa mashua yao kuchomwa moto katika kisiwa cha Tumbatu.Picha na Hassan Issa wa – OMPR - ZNZ

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe aliyeketi wa tatu kutoka kushoto , akiwa pamoja na watumishi wa Idara za wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ikiwemo Polisi , Magereza, Uhamiaji, Zimamoto na Uokoaji na Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa baada ya Waziri Chikawe kutembelea mabanda ya wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, aliyeketi wa pili kutoka kushoto ni Msemaji wa wizara Isaac Nantanga.
  Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe akipokea vijitabu vidogo vinavyoelezea masuala ya utendaji wa polisi kutoka kwa afisa wa Jeshi la Polisi Christina Mponji wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Maafisa wa jeshi la Magereza wakifurahia jambo pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yakejana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Mrakibu Msaidizi wa Uhamiaji Mathew E. Ikomba akitoa maelezo ya namna Idara hiyo ilivyofanikiwa kutumia teknolojia mpya ya utoaji wa vibali vya ukaazi kwa mfumo wa kielectroniki na hivyo kuondokana na mfumo wa awali wa kuandika vibali hivyo kwa mkono, mbele ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja.
  Mkaguzi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Laurance Kabigi akimuonesha kifaa cha kuzimia moto Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe wakati Waziri huyo alipotembelea Mabanda ya Wizara yake jana katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Afisa Habari Mkuu na Msemaji wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA) Thomas Willium wa kwanza kushoto akitoa maelezo ya namna Mamlaka hiyo inavyotekeleza zoezi la kuandaa na kutoa vitambulisho vya taifa kwa wananchi wakati Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mh. Mathias Chikawe alipotembelea Mabanda ya Wizara yake katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam jana.

  0 0

  1Wafanyakazi wa Shirika la Madini la Taifa wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda lao.
  ....................................................................................
  Na Mwandishi Wetu
  KAIMU Mkurungenzi Mtendaji mpya wa Shirika la Madini la Taifa, Mhandisi Edwin Ngoyani ameahidi neema kwa wachimbaji wadogo wa madini na vito nchini kwa kuwawezesha kupata masoko ya bidhaa zao pamoja na kuwapatia zana za kisasa za uchimbaji madini.
  "Malengo yangu makuu katika shirika hili ni kuhakikisha wachimbaji wadogo wanawezeshwa kunufaika na rasilimali za nchi yetu pamoja na kuhakikisha kwamba STAMICO linatoa mchango wa mapato katika mfuko mkuu wa hazina kwa kujiendesha kwa faida," Mhandisi Ngonyani alisema katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
  Akizungumza kwa kujiamini, Mhandisi Ngonyani alisema anatarajiwa malengo yake katika STAMICO yataanza kuzaa matunda ndani ya miaka miwili mpaka mitatu ijayo.
  Akizungumzia mkakati kwa wachimbaji wadogo, Ngonyani alisema,ndani ya miaka miwili ijayo, shirika hilo litanunua mitambo miwili ya uchimbaji wa madini ya kisasa (drilling rigs) ambayo itatumiwa na wachimbaji wadogo.
  “Lengo ni kuwafanya wachimbaji wadogo wanufaike na wawe sehemu ya uwekezaji kwenye rasilimali zao, kama ambavyo hao wawekezaji wa nje wanavyowekeza, na sasa watanzania nao watawekeza, ila lazima tuwawezeshe," Ngonyani alisisitiza.
  Alisema lengo la STAMICO kwa wachimbaji wadogo ni kuhakikisha wanawezeshwa kuwekeza na kuchimba kisasa ili pia watoa mitaji ambao ni benki wawe na uhakika wa fedha zao kurejeshwa, na kwamba hata ikibidi, shirika hilo litawawekea dhamana ili wawezeshwe kibenki.
  Alisema hilo litawezekana baada ya mkakati wao wa kuanzisha na kuboresha takwimu za wachimbaji wadogo ambazo zitakuwa na taarifa zao ikiainisha mahali walipo,aina ya madini wanayochimba na mahitaji yao.
  Pia mkakati mwingine ni kubaini vyanzo vya migogoro kwenye maeneo ya wachimbaji na kutafuta suluhu ikiwa ni pamoja na kutenga maeneo yanayofaa kwa uchimbaji mdogo ili kuepusha migogoro isiyo ya lazima.
  Katika hatua nyingine, Ngonyani alizungumzia mradi wa uchimbaji madini kwenye mgodi dhahabu wa Tulawaka ambao hivi sasa umenunuliwa na shirika hilo na kuitwa Biharamulo unaosimaimamiwa na kampuni ya StamiGold.
  Alifafanua kwamba mgodi huo utaanza kazi rasmi Agosti 8, mwaka huu na kwamba baada ya miaka miwili na nusu, wanatarajia kupata faida ya shilingi bilioni saba.
  Awali mgodi huo ulikuwa ukimilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) na mwishoni mwa mwaka jana STAMICO ikaununua kwa dola za Marekani milioni tano.
  ABG iliuza mgodi huo kutokana na kwamba kiasi cha wakia 100,000 kilichopo katika eneo la mradi ni kidogo kwa uchimbaji mkubwa kwa kampuni hiyo kubwa ya madini duniani.
  "Hata hivyo tuna matumaini kwamba katika eneo la kilometa nne kutoka kwenye eneo la mradi kuna uwezekano wa kuwapo mashapo ya kati 150,000 mpaka 200,000. Tutaendelea na utafiti katika eneo hili," Mhandisi Ngonyani alisema.
  Kwa upande wake, Meneja Uchorongaji wa Stamico, Alex Rutagweleka alisema hivi sasa miradi mitano iko kwenye ubia na shirika hilo kwa ajili ya uwekezaji na kuitaja miradi hiyo kuwa ni pamoja na ule wa Itetemia mgodi wa dhahabu ambao Stamiko wameingia ubia na Kampuni ya Madini ya Tancan Ltd.
  Mradi mwingine ni wa Buckreef wa dhahabu ulioko Geita ambao Stamico wameingia ubia na Kampuni tanzu ya TANZAM 2000, ambapo Stamico wana hisa asilimia 45 na 55 iko kwa kampuni hiyo na kwamba wanategemea uzajishaji utaanza Novemba mwama huu.
  Aidha mradi mwingine ni Kiwira ambao unazalisha makaa ya mawe kwa ajili ya kufua umeme utakaounganishwa kwenye gridi ya taifa.
  Akizungumzia mradi huo,Meneja fedha na Utawala wa Stamico, Peter Gembe alisema lengo la mradi huo ni kufua megawati 200 za umeme kwa ajili ya kuunganisha kwenye gridi ya taifa kutoka kwa kiwango cha awali cha megawati 6.
  Stamico ni shirika la umma lililoanzishwa mwaka 1972 kwa lengo la kuongeza mchango wa sekta ya madni katika pato la taifa na kuzalisha nafasi za ajira kwa watanzania.

  0 0

  Jaji mkuu wa Tanzania Ndugu Mohamed Othman Chande leo amewataka mawakili wapya kufanya kazi zao za Uwakili kwa kuzingatia maadili ya taaluma ya uwakili. 
  Jaji Mkuu aliyasema hayo wakati wa Sherehe ya 50 ya kuanzia mwaka 1986 ya kuwakubali na kuwasajili Mawakili wapya,iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es Salaam
   Jaji Mkuu pia amewahimiza Mawakili wapya hao kujiendeleza kitaaluma kwa sababu kuwa wakili sio mwisho wa taaluma, na pia amewataka Mawakili wa zamani kuwapokea Mawakili wapya ili waweze kushirikiana kwa pamoja. 
  Ameongeza kwamba Mawakili wana wajibu wa kulinda siri ya mazungumzo baina ya mteja na Wakili pamoja na kuhakikisha kwamba wana wajibu wa kutokwamisha uharakishaji wa kesi kutokana na mfumo wa sasa ambao unahimiza uharakishwaji wa kesi.
  Picha ya pamoja wakati wa Sherehe ya 50 ya kuanzia mwaka 1986 ya kuwakubali na kuwasajili Mawakili wapya,iliyofanyika leo kwenye Viwanja vya Karimjee,Jijini Dar es Salaam. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0


  0 0
 • 06/20/14--11:39: car wash?

 • Wadau tuwe makini wapi unapeleka kuosha gari lako. Vinginevyo utaishia kuoshewa wese lote kama hivyo...

  0 0

   Na Sultani Kipingo
  Wakiwa wameshinda mara mbili katika michezo yao ya kwanza ya Kombe la Dunia 2014, Costa Rica wamedaka tiketi ya kwenda katika raundi ya mtoano ya 16 huku Brazil.

   Baada ya kufanya maajabu kwa kuifunga Uruguay katika mchezo wao wa fungua dimba, Costa Rica wamaeitungua Italy 1-0 leo katika mchezo mkali wa kundi D katima uwanja wa Pernambuco mjini Recife.
   Goli lao la ushindi limepatikana dakika chache kabla ya mapumziko pale kiungo wao mahiri Bryan Ruiz alipotia ndinga kimiani kwa kichwa kufuatia majalo tamu ya kona ya Junior Diaz.
  Mpira huo baada ya kupigwa kichwa na Ruiz uligonga besela na kudunda ndani ya goli. Teknolojia mpya ya kugundua magoli ilithibitisha hilo ni bao kwani mpira ulishavuka mstari. Matokeo hayo yanaihakikishia Costa Rica nafasi katika raundi ya 16 bora na hapo hapo wanakuwa wameifungashia virago Uingereza.Ushindi huo pia umeongeza kasi ya ushindani baina ya Uruguay na Italy watapokutana Juni 24, ambapo wote walishamchapa Uingereza, na wote wamechabangwa na Costa Rica, na ushindi wowote baina yao utampleka aliyeshinda hatua inayofuata. Ila Italy ndiyo yenye matumaini zaidi kwani ina magoli zaidi.... 


  0 0

   Mwenyekiti wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe Mercy James akikabidhiwa cheti chake. Mafunzo hayo yaliandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Njombe (Njombe Press Club ) yenye lengo la kuwasaidia waandishi hao kuandika habari kwa kufuata weledi wa taaluma hiyo
   Meneja wa kitucha redio Uplands Fm, Novatus Lyaruu akipokea cheti chake kama mshiriki wa mafunzo hayo
  Mwandishi wa habari wa gazeti la Majira na mtandao wa Habari Ludewa Blog NIckson Mahundi akikabidhiwa cheti chake
  Mtangazaji wa Best FM ya Ludewa mkoani Njombe akipewa cheti chake cha ushiriki wa mafunzo hayo
  Mmiliki wa Eddy Blog Edwin Moshi akipokea cheti cha mafunzo hayo ya siku nne yaliyoandaliwa na MCT toka kwa nguli wa habari nchini ambaye pia ni mwalimu wa Ankal Michuzi, Bw. Attilio Tagalile.
   PICHA ZOTE NA EDWIN MOSHI

older | 1 | .... | 477 | 478 | (Page 479) | 480 | 481 | .... | 3272 | newer