Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 476 | 477 | (Page 478) | 479 | 480 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Warembo wanaowania taji la mkoa wa Tanga, Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakijiaandaa kufanya usafi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ikiwa ni moja ya kampeni ya kuendelea kulifanya jiji hilo liwe safi muda wote.
  Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakitupa takataka katika gari maalum la kubeba taka. Mshindi wa kwanza katika shindano hilo atapata zawadi ya gari dogo aina ya Toyota Vitz.
  Zoezi la usafi limepamba moto na kuliacha eneo hilo safi kabisa. Mgeni rasmi katika shindano hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Chiki Gallawa.


  0 0

  H.E Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to her Majesty Queen Elizabeth II on the occasion of her 88th birthday.

  The message reads as follows:-
  “Your Majesty Queen Elizabeth II,
  Buckingham Palace,
  London,
  UNITED KINGDOM.

  On behalf of the people and the Government of the United Republic of Tanzania, I extend sincere congratulations on the occasion of your 88th birthday.

  As you celebrate your birthday allow me to take this opportunity to express my appreciation on the good relations that exist between our two countries and peoples.

  The celebration of your birthday offers us yet another opportunity to reaffirm our commitment to continue working closely together in strengthening further the relations between our two countries.

  Please accept, Your Majesty, my best wishes for your continued good health and peace and prosperity for the people of the United Kingdom.”

  Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation, Dar es Salaam

  18th June 2014

  0 0


  Mkurugenzi mtendaji wa kituo cha Baba watoto Center Bw.Mgunga Mwamnyenyelwa kilichopo mburahati kwa jongo wilaya ya kinondoni Dar es salaam, akizungumzia juu ya kituo hicho kinavyo fanya kazi na sababu za kuwakusanya watoto hao katika kituo hicho ikiwa ni pamoja na kuwajengea uelewa zaidi na kuwafundisha vitu mbalimbali kama Ngoma, Sarakasi, ushonaji ili baadae waweze kuja kujitegemea wenyewe.

  Meneja mradi wa Fit For Life Habiba Issa akielezea kwa kina juu ya Mradi huo pamoja na malengo yake.
  Kikundi cha ngoma ndani ya kituo cha Baba watoto pamoja na wanafuzi waki achia burudani ya muziki aina ya Samba Rege.
  Vijana wakifanya mafunzo ya serekasi katika kituo cha Baba watoto center.

  BOFYA HAPA KWA HABARI KAMILI

  0 0

  LAKE GAS LTD - One of Tanzania’s fastest growing Marketing company, engaged in the importation and distribution of Liquefied Petroleum Gas (LPG), launched an innovative product – “COMPOSITE CYLINDERS” - the first of its kind in Tanzania.

  In Tanzania, the usage of Metal cylinders has been the most prevalent up to now; henceforth a discerning consumer shall have a choice as to what type of cylinder best suits their family.

  “This composite cylinder have very unique features, they are non explosive, non corrosive, light in weight and is translucent. These four properties will reassure consumer of its safety and usability other than the fact that it’s aesthetically pleasing” stated CEO of Lake Gas Ltd Mr. Ally Edha Awadh.

  The first Lake Gas composite cylinder was handed over to the Guest of Honour representing on behalf of Minister of Energy and Minerals, Prof Sospeter Muhongo -, Asst Commissioner for Energy Eng Nobert Kahyoza by Mr. Ally Edha Awadh, thus marking the beginning of commercial usage of this state of art cylinders.

  “Lake Gas Ltd has led the way, by launching such new and innovative products, we as the Ministry loud such efforts by the Private sector. Not only does it spur competition but creates employments and most importantly provides revenue for the government” stated Eng Kahyoza

  Lake Gas Composite cylinders are made by one of the leading Manufacturer of Composite cylinders in India and are now available with all Lake Gas Super Dealerships in Dar es Salaam as well as up country locations across Tanzania.

  Lake Gas Ltd is part of the Lake Group of companies, a prestigious conglomerate of companies originated from Tanzania. This is again the brainchild of Mr. Ally Edha Awadh who spotted the huge potential for LPG product in a country starved for cooking fuel. With the strong investments made in the sector, now the company is looking at expansion to surrounding countries and also into allied sectors like cylinder manufacturing.

  Lake Gas Ltd's import terminal facilities are located at Kigamboni. The 750MT(1,600,000 Liters) Liquefied Petroleum Gas (LPG) storage capacity terminal is capable of receiving the product directly from ships through a 3,500meters long pipeline from the oil jetty at Dar es Salaam port. The company aims to increase its storage capacity to more than 3000MT in near future with the new Depot coming up at Tanga. Currently, Lake Gas Ltd is operating a LPG cylinder filling plant in Mikocheni, Dar es Salaam which has capacity to store about 30MT LPG and fill more than 2MT LPG or about 1200 cylinders in a single calendar day

  Right from the importation stage of LPG up to the supply to the end user, the Company conforms to the highest HSE standards. Lake Gas Limited aims to make a significant contribution to the social development of its consumers and communities at large in Tanzania.
  Ally Awadh addressing the invited guest yesterday.
  celebrity radio Prsenter Babbie Kabaye hostiing the Lake Gas Composite cylinder launch.
  Owner of lake Oil group handing over the first composite cylinder to asst commissioner of Energyy Eng Norbert Kahyoza.
  Sensational songstress Shaa performing during the Lake Gas Composite cylinders launch.

  0 0


  0 0

  Wanafunzi wa shule ya sekondari Mnazi Mmoja wakiangalia moja ya mfano wa ndege wakati walipotembelea katika banda la Mamalaka ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA, Katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
  Afisa Utwala Baraza la Ushauri la Watumiaji wa Huduma ya Usafiri wa Anga Tanzania TCAA,Catherine Morarya akiwaonyesha Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mnazi Mmoja ya jijini Dar es Salaam redio ya upepo inayotumika kwa mawasiliano ya anga, wakati walipofika kujifunza maswala ya anga katika banda la Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania kwenye maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea hapa nchini.
  Afisa Habari wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania *TCAA* Faustine Ngongo akiwaelezea baadhi ya wananchi waliofika katika banda hilo lililopo kwenye Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam.

  0 0

  Watu waliofika katika banda la Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), wakimsikiliza Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko huo, Rahim Mwanga wakati wa Maonesho ya wiki ya Utumishi wa Umma.

  Ofisa Mafuzo wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Hilder Lyimo akitoa maelezo kwa baadhi ya watu waliohudhuria Monesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma katika viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo.
  Elimu kuhusu mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji ilitolewa kwa watu waliofika katika banda la UTT.
  Nadhani umeelewa.......Ofisa Masoko na Uhusiano wa Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Rahim Mwanga akitoa ufafanuzi kwa watu waliofika katika banda lao.
  Ofisa Masoko Mwandamizi na Uhusiano Mfuko wa Dhamana ya Uwekezaji Tanzania (UTT), Martha Mashiku akizungumza na waandishi wa habari wakati wa Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma. 

  0 0

  Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI akifungua Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma 2014 katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere mapema leo. Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI akifungua Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma 2014 katika Kituo cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere mapema leo.
  Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu akiongea kabla ya ufunguzi rasmi wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere mapema leo. Kongamano hilo ni sehemu ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2014.
  Katibu Mkuu mstaafu Bi. Ruth H. Mollel akiwasilisha mada wakati wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Julius Nyerere (JNICC). Anayeonekana kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu, ambaye ni Mwenyekiti wa Kongamano hilo.
  Sekretarieti ikichukua michango wakati wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerer (JNICC) uliopo jijini Dar es Salaam mapema leo.

  Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI (wa tatu kutoka kulia) akiwa na wageni waalikwa wa Kongamano la Miaka 50 ya Muungano katika Utumishi wa Umma.Kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Bw.Phillemon Luhanjo akifuatiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Prof.Sifuni Mchome.Kulia kwa mgeni Rasmi ni Kaimu Katibu Mkuu Utumishi Bw.HAB Mkwizu.

  0 0

  Tarehe 20 Juni ya kila mwaka ni siku ya Wakimbizi duniani na kwa Tanzania siku hiyo itaadhimishwa kitaifa hapa Dar es Salaam katika Hotel ya Sea Cliff, ambapo mgeni rasmi katika halfa hiyo atakuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe.

  Kufuatana na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “Familia moja kusambaratika na vita ni wengi mno” au kwa Kiingereza “1 family torn apart by war is too many”.

  Taarifa hiyo inaongeza kuwa kiasi cha watu 43 milioni duniani kote wamelazimika kuyahama makazi yao kwa sababu ya vita, machafuko au majanga ya asili, na kati yao kiasi cha milioni 10 wanahudumiwa na Shirika hilo.

  Kwa upande wa Tanzania, kiasi cha wakimbizi wapya wanaoomba hifadhi imepungua ilikinganishwa na miaka ya nyuma ambapo kuna wakati idadi yao ilikaribia kufikia milioni moja. Kupungua huku ni ishara ya kuimarika kwa hali ya usalama ndani ya nchi walizotoka wakimbizi hao, hususan nchi za eneo la Maziwa Makuu. Hata hivyo, bado hali si shwari sana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), hali inayosababisha baadhi ya raia wa nchi hiyo kuikimbia na kwenda kuomba hifadhi ya ukimbizi katika nchi nyingine ikiwemo Tanzania.

  Mfano wa mafanikio yaliyopatikana hapa nchini kuhusiana na suala la Wakimbizi ni kufungwa kwa kambi za wakimbizi zaidi ya kumi na mbili ambapo kambi ya mwisho kufungwa ya Mtabila iliyokuwa wilayani Kasulu mkoani Kigoma iliyokuwa na raia zaidi ya 35,000 toka Burundi ilifungwa mwishoni mwa Desemba, 2012. Sasa hivi Tanzania imebakiwa na kambi moja tu ya Nyarugusu, wilayani Kasulu mkoani Kigoma ambayo ina wakimbizi takribani 65,084, wengi wao wakiwa ni kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

  Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi na Jumuiya ya Kimataifa linaamini suluhisho la kudumu kwa tatizo la wakimbizi ni kwa wakimbizi kupata nafasi ya kurejea kwao kwa hiari, mara baada ya mazingira yaliyowafanya kuzikimbia nchi zao kutoweka.

  Jambo hili litafanyika na kufanikiwa pale Serikali za nchi na Jumuiya ya Kimataifa zitakapochukua hatua za makusudi kuhakikisha kuwa sababu zinazowafanya raia wa nchi mbalimbali kuzikimbia nchi zao zinatafutiwa ufumbuzi. Hii ni pamoja na kuwa na Serikali zinazozingatia sheria, utawala bora na haki za binadamu.

  Imendaliwa na: Isaac J. Nantanga – Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
  19 Juni, 2014

  0 0

  Na Mwene Said wa Globu ya Jamii
  MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam, imeambiwa kwamba upelelezi wa kesi ya ubakaji inayomkabili Msanii Emmanuel Mbasha (32) - pichani - na mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha, umekamilika.
   Hatua hiyo imefikiwa leo mbele ya Hakimu Mkazi Mh. Wilberforce Luago aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo. 
  Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa kesi hiyo ilipangwa kutajwa jana na kwamba upelelezi wake umekamilika.
  “Mheshimiwa kwa kuwa upelelezi wa kesi hii umekamilika tunaomba tarehe ya kumsomea mshtakiwa maelezo ya awali…” alidai Katuga. 
  Hakimu Luago alisema mshtakiwa atasomewa maelezo ya awali Julai 17, mwaka huu.  Kabla ya kuahirishwa kesi hiyo mshtakiwa alitimiza masharti ya mahakama na yuko nje kwa dhamana.
  Katika kesi ya msingi, ilidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam,  kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).
  Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu  mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa). 
  Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .
  Awali, mahakama hiyo ilimtaka msanii huyo kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.

  0 0

  Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeikataa rufani ya  Michael Richard Wambura (pichani) kupinga kuenguliwa kugombea urais katika uchaguzi wa klabu ya Simba unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.


  Wambura aliwasilisha rufani yake mbele ya Kamati hiyo iliyokutana leo (Juni 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam chini ya Kaimu Mwenyekiti Wakili Mwita Waissaka kupinga uamuzi wa kumwengua katika kinyang’anyiro hicho uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya Simba kwa kufanya kampeni kabla ya muda uliopangwa.

  Baada ya kupitia vielelezo, kanuni na sheria, Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF imeridhika kuwa mrufani (Michael Wambura) alifanya kampeni kabla ya muda kinyume na Ibara ya 6(1)(a) na (g), Ibara ya 6(1)(l) pamoja na Ibara ya 14(3) ya Kanuni za Uchaguzi za TFF toleo la 2013.

  Kwa mujibu wa ibara hizo, Kamati ya Uchaguzi ya Simba inayo mamlaka ya kumwengua (disqualify) mgombea anayefanya kampeni ama kukiuka maagizo halali ya Kamati ya Uchaguzi.

  Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF imeziagiza kamati zote za uchaguzi za wanachama wa TFF kufuata kanuni za uchaguzi kama zilivyoainishwa katika Katiba zao ili kuepusha rufani za mara kwa mara.


  Uamuzi wa Kamati ya Rufani ya Uchaguzi ya TFF umezingatia Katiba ya TFF pamoja na kanuni zake, na pia Katiba ya Simba.

  0 0

  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk. Sarah Maongezi(mwenyesuti ya bluu), akikata utepe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa Kliniki mpya ya watu waishio na seli mundu wakati wa maadhimisho ya Siku ya Seli Mundu Duniani, Muhimbili Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Tiba na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Profesa Eligius Lyamuya na Mkurugenzi wa Tiba Muhimbili,  Dk. Hedinga Swai na kutoka kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Damu, Dk. Alex Magesa na Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto na Mkuu wa Idara Muhimbili, Dk. Mary Charles.
  Picha ya pamoja na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) na wafadhili.
  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk. Sarah Maongezi,katika picha ya pamoja na watoto wenye Siko Seli
  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo (WAMA), Dk. Sarah Maongezi, katika picha ya pamoja na watoto wenye Siko Seli pamoja na Madaktari Bingwa wa Hospitali ya Taifa Muhimbili(MNH) Dar es Salaam leo katika Maadhimisho ya Siko Seli Duniani.

  0 0


  Bw. Anic Kashasha, Mwenyekiti Mtendaji wa shirika lisilo la kiserikali Tanzania Creative Industries Network (TACIN) ya Dar es Salaam, nilikuwa ninahutubia mkutano wa waandishi wahabari kwenye ukumbi wa Safari Lounge, mjini Mtwara, juu ya kuanzisha Mtwara Festival, utakaofanyika tarehe 16 - 17 Agosti, 2014 kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona,Mtwara.

  Mtwara Festival imeandaliwa kwa kushirikiana na washirika wakuu na wadhamini wa TACIN, Shirika la maendeleo ya Petroli  Tanzania (TPDC). Huu ni mkakati endelevu wa mawasiliano ili kuwahasisha wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi, kuzitambua, kujiandaa na kuzichangamkia fursa zinazotokana na uiwekezaji mkubwa unaendelea katika mikoa hiyo.

  Mtwara Festival itakuwa ni tukio la kila mwaka kwa malengo ya kuitangaza mikoa ya Mtwara na Lindi kama mikoa yenye vivutio vingi vya utalii wa utamaduni ikiwa ni pamoja na uchongaji wa vinyago vya na ngoma mbalimbali zenye mvuto Mkubwa. Bodi ya Utalii (TTB) ni Wadau katka mpango huu na watautangaza kupitia njia zake zote yaani mtandaoni, DVD, na majarida yatumikayo kuitangaza Tanzania kwenye Masoko mbalimbali duniani kote. Aidha, TTB wataiweka Mtwara Festival kwenye kalenda ya matukio ya ki- utalii ya Tanzania.

  Wenyeji wa Mtwara Featival ni Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mtwara, Mkurugenzi wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara (V). Chama cha Wafanyaniashara, Wenye Viwanda na Wakulima (TCCIA) tawi la Mtwara nao ni washirika wa mpango huu.

  0 0

  ADDRESS YETU MPYA NI;
  UNIT 16D TILBURY INDUSTRIAL COMPLEX
  TILBURY FREEPORT
  ESSEX
  RM18 7HB
  KUANZIA SASA MZIGO WA NDEGE NI SIX DAYS GUARANTEE
  SALOON CARS TO DAR NOW £680
  4 X 4 CARS TO DAR  NOW £770
  UKISHIP MAGARI ZAIDI YA MOJA UNAPATA BIG DISCOUNT!
  AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
  KAMA UNA MZIGO WA MSAADA TUNASAFIRISHA BURE
  FREE STORAGE IN OUR OFFICE
  FREE COLLECTION FROM EAST LONDON 
  £50 COLLECTION FROM ANYWHERE IN UK
  COLLECTION POINT IS
  ILALA MTAA WA BUKOBA
  CONTACT; TORNADO +255713607116
  SIMPLY THE BEST IN BUSINESS
  JUST DROP YOUR CAR AT OUR OFFICES AND WE WILL TAKE CARE OF IT
  WE WILL GET IT INSPECTED AND LOAD IT TO THE SHIP FOR YOU!
  BEI ZETU HAZINA WASHINDANI NDIO MAANA TUMEZIANIKA WATU WAJUE
  THE DIFFERENCE IS CLEAR!
  WE ARE NOW OPEN ON SATURDAYS
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  Tupigie kwa namba hizo hapo Chini au  tutumie email tafadhali
  SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243
                 HQ -  UNIT 16D TILBURY INDUSTRIAL COMPLEX, TILBURY FREEPORT, ESSEX                    RM18 7HB

  0 0  0 0

   Semi-Trela likiwa limebeba kontena likiwa limeanguka baada ya kulielemea  kwa uzito na kulivunja daraja la chuma katika barabara ya Banana-Kinyerezi maeneo ya Tabata jijini Dar es salaam leo. Haikuweza kufahamika mara moja lilikuwa limebeba mzigo gani na kama dereva alikuwa anajua daraja hilo ni kwa magari yenye uzito wa wastani  wa tani 7 tu au ni kiburi tu.  Hakika Waziri wa Ujenzi Dkt John Pombe Magufuli  na jeshi lake wana kazi ya ziada kuhakikisha uzembe kama huu hautokei na haujirudii. 
  0 0

   Mkuu wa Divishen ya Elimu Zanzibar Maalim. Ahmed Abdul-majid ambae ni Mgeni rasmin siku ya Kichocho Zanzibar, akihutibia wananchi na wanafunzi waliofika katika hafla hiyo huko Skuli ya Mwera Wilaya ya Kati Unguja ambapo kunasadikiwa kuwa na wingi wa Koa wambukizao Kichocho
   Wanafunzi wakionyesha picha jinsi ya maambukizi ya Kichocho yanavyopatikana.
   Sehemu ya wanafunzi  waliofika katika sherehe ya siku ya Kichocho inayoadhimishwa kila mwaka hapa Zanzibar.
   Aina za Konokono wanaoambukiza Kichocho na wale wasio ambukiza.
   Sehemu wanaopenda kukaa Konokono wanaoambukiza Kichocho. Mto wa Mwera Wilaya ya Kati Unguja. Picha na Makame Mshenga Maelezo Zanziba

  0 0

  Mdau akisherehekea ushindi wa Chile dhidi ya Spain na mashabiki wa timu hiyo Brazil. 

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI


  Wasailiwa 1,281 kati ya 6,115 waliofanya usaili wa kwanza tarehe 13 Juni, 2014 jijini Dar es Salam kuomba nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji (Assistant Inspector of Immigration) wanatarajiwa kuingia duru ya pili na ya mwisho ya usaili huo baada ya kufanikiwa kufaulu usaili wa kwanza.
  Usaili huu ambao utafanyika kwa awamu utaanza tarehe 23 Juni hadi 03 Julai, 2014 na utafanyikia katika Bwalo la Maafisa Magereza, Ukonga jijini Dar es Salaam kuanzia saa 1.30 asubuhi.
  Tofauti na usaili wa kwanza ambao ulikuwa wa kuandika na ulihusisha maswali ya hesabu na ufahamu wa jumla, usaili wa awamu ya pili utakuwa wa maswali ya ana kwa ana ambao utahusisha kupima uwezo wa msailiwa kujieleza na kufafanua mambo.
  Kuchaguliwa kwa wasailiwa hawa kulifanyika baada ya kusahihisha majibu yao na majina kuingizwa katika mfumo wa kimtandao ambao ulisaidia kuchagua wasailiwa waliopata alama hamsini na kuendelea.

  Majina ya wasailiwa hawa yanapatikana katika Tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, www.moha.go.tz  na ya Idara ya Uhamiaji, www.uhamiaji.go.tzna watatakiwa kuja na vyeti vyao halisi vya kuzaliwa, vya shule na picha mbili za pasipoti.
  BOFYA LINK HIYO HAPO CHINI KUSOMA MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI
  http://www.moha.go.tz/phocadownload/Kuitwa%20Kwenye%20Usaili_Uhamiaji.pdf
  http://www.moha.go.tz/phocadownload/Kuitwa%20Kwenye%20Usaili_Uhamiaji.pdf

  Awali, kiasi cha wasailiwa 10,801 waliitwa kwa ajili ya usaili wa kwanza
  baada ya kupokea maombi yao, lakini waliohudhuria ni 6,115 na kati yao ndio walipatikana 1,281 ambao watasailiwa ili kupata watakaojaza nafasi sabini (70) za Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji katika Idara ya Uhamiaji.

  Sgn Isaac J. Nantanga

  MSEMAJI,
  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

  0 0
 • 06/19/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • New Edition - "Cool It Now"

older | 1 | .... | 476 | 477 | (Page 478) | 479 | 480 | .... | 3286 | newer