Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 475 | 476 | (Page 477) | 478 | 479 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Waziri mkuu mstaafu na mbunge wa Monduli Mh Edward Lowassa akizungumza na sheikh mkuu mkoa wa Dodoma,sheikh Adam Zubeir wakati alipokwenda kumjulia hali nyumbani kwake Kikuyu Flats.Sheikh Zubeir amekuwa akisumbuliwa na maradhi na alipelekwa India kwa matibabu hivi karibuni.

  0 0

  Meneja wa Masoko na Elimu kwa Umma, Anjela Mziray na Ofisa Matekelezo, Geofrey Tumaini wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya wakitoa ufafanuzi kwa wananchi waliotembelea banda la Mfuko katika Maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma.
   Maofisa wa NHIF wakiongozwa na Meneja wa Mkoa wa Temeke, Ellentruda Mbogoro (kushoto) wakichambua na kuhakiki fomu za wanachama waliowasilisha fomu za usajili kwa ajili ya kupatiwa vitambulisho vya matibabu.
  Ofisa Mifumo Habari wa NHIF, Donald Malunda akimhudumia mwanachama kwa kuhakiki taarifa zake katika maonesho hayo.
  Banda la Upimaji Afya bure la NHIF, likiendelea na huduma kwa wananchi waliojitokeza kupima afya zao.
   Upimaji wa urefu na uzito ukiendelea
  Wataalam wakiendelea kutoa ushauri kwa wananchi kulingana na matokeo ya vipimo vyao.

  0 0

  IMG-20140618-WA0007
  Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba akikanusha vikali taarifa za  aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One,Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa
  IMG-20140618-WA0006
  Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa
  IMG-20140618-WA0008
  Waandishi wa habari wakiwa kazini

  Na Pamela Mollel
  Afisa Uhamiaji wa mkoa wa Arusha Daniel Nanomba amekanusha vikali taarifa za  aliyekuwa Meneja Mauzo wa kampuni ya Tanzanite One, Jaques Beytel anayedaiwa kutoroshwa.
  Ameeleza  kuwa mtu huyo  aliamriwa kuondoka nchi Juni 13, mwaka huu na kwamba alisindikizwa hadi mpaka wa Namanga na si uwanja wa KIA kama ilivyoelezwa.
  Kwa mujibu wa Taarifa ya Afisa huyo kwa vyombo vya habari amesema kuwa Maofisa wa Uhamiaji walimkamata Jaques na kumpatia notice ya kuamriwa kuondoka nchini na si kutoroshwa na kufafanua kua uamuzi huo ulizingatia taratibu zote za kisheria.
  Nanomba alisema kuwa Raia huyo ambaye ni mzaliwa wa Afrika kusini  na kuwa alikua mfanyakazi wa kampuni ya Tanzanite One ambao tumewaita na kuwaonya. 
  Afisa huyo amesema kuwa hawamzuii Mwajiri yeyote anayeajiri mtu kutoka nje ya nchi na hivyo kuwataka waajiri wahakikishe kuwa watu hao wana kibali cha kufanya kazi nchi vinginevyo watachuliwa hatua kali na kuongeza kuwa hadi sasa wamewachukulia hatua waajiri watano.
  Ameeleza kuwa kwa kipindi cha Januari mwaka huu hadi sasa tayari wamefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu 35 katika mkoa wa Arusha huku Kenya ikiwa inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji hao nchini.
  Kati ya wahamiaji hao 35 wako raia wa kenya 13,Ethiopia wanne,Kongo 4,Ghana 4,dachi 3,Marekani mmoja na kutoka nchi nyingine
  Pia  wako Watanzania waliochukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kuwaajiri watu kutoka nje wasiokuwa na vibali vya kukaa nchini.  0 0  0 0

  Jeshi la Magereza litafanya Maadhimisho ya Siku ya Magereza Nchini tarehe 20 Juni, 2014 kuanzia saa 2:00 asubuhi katika Viwanja vya Chuo cha Maafisa wa Magereza Ukonga, Dar es Salaam ambapo Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe(MB).

  Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa leo Juni 18, 2014 na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja Maadhimisho haya ni ya pili kufanyika tangu Jeshi la Magereza Tanzania lianzishwe rasmi mwaka 1931. Madhumuni ya Siku ya Magereza ni:-
    a) Kuelimisha jamii juu ya shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza katika
        utekelezaji wa majukumu yake ya uhifadhi na Urekebishaji wa wahalifu kupitia shughuli za
        viwanda Vidogo Vidogo, Ujenzi, Kilimo, Ufugaji na Ufundi katika fani mbalimbali.
    b) Kuelimisha na kuhamasisha jamii juu ya umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika suala zima la
        Urekebishaji wa wahalifu na;
    c) Kutoa elimu kwa umma juu ya huduma na taratibu za Uendeshaji wa Magereza Nchini.  Shughuli zitakazofanyika siku hiyo ni pamoja na ufunguzi wa Duka la Bidhaa zisizolipiwa Kodi (Duty Free Shop) Gereza Keko, kukagua shughuli zinazofanyika kwenye Ofisi za Chama cha Ushirika wa Kuweka na Kukopa kwa Watumishi wa Jeshi la Magereza (TPS SACCOS) eneo la Keko, kufungua Karakana ya Uhunzi Gereza Ukonga, Gwaride Maalum, Onesho kutoka Kikosi Maalum la utayari wa Kutuliza Ghasia Magerezani. Ushuhuda wa Mfungwa  aliyepata Shahada ya Sheria (LLB) akiwa gerezani, Burudani Maalum ya muziki kutoka kwa wafungwa, askari wa kike waliohitimu mafunzo maalum kukabidhiwa vyeti na Mgeni rasmi na maonesho ya kazi mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza.
  Vyombo vya Habari na Wananchi wote wa Mkoa wa Dar es Salaam na Mikoa jirani wanakaribishwa kuja kushiriki katika Maadhimisho haya ili wapate nafasi ya kuona na kujifunzia shughuli mbalimbali zinazofanywa na Jeshi la Magereza.  Imetolewa na;
  Lucas Ambrose Mboje, Mkaguzi wa Magereza,
  Afisa Habari Makao Makuu ya Jeshi la Magereza,
  18 Juni, 2014,
  DAR ES SALAAM.

  0 0

  The ninth edition of Africa’s biggest reality series BIG BROTHER AFRICA kicks off in September. Unlike previous years, this year’s entry process is slightly different as potential housemates are invited to come in their numbers for auditions in their respective country venues.
  “We are very grateful and remain pleasantly surprised by the overwhelming response that the show has been receiving over the years. We look forward to the selection of our potential housemates coming in large numbers to auditions at the specified venues and take that chance at being the next Big Brother star,” says M-Net Africa Regional Director (West Africa) Wangi Wa-Uzoukwu. “The fact that the fans truly adore the show is all the motivation we need to keep it fresh and that is always made possible by the enthusiastic and fun-loving young Africans who will answer to Big Brother. We are rearing to go and we know that this will definitely be another exciting season that is full of quality entertainment!”
  All persons over the age of 21, who are citizens of one of the participating countries and have a valid passport, can enter Big Brother Africa 9. If you are open-minded, bold and adventurous, that’s even better! Previous editions of Big Brother Africa have boasted huge cash prizes for winners and this it is no different as the prize money is USD 300 000.
  Entries are open to the following 14 countries: Botswana, Ethiopia, Ghana, Kenya, Malawi, Namibia, Nigeria, Rwanda, Sierra Leone, South Africa, Tanzania, Uganda, Zambia and Zimbabwe.
  BIG BROTHER AFRICA, beginning on Sunday 7 September, will be screened live 24/7 on DStv and is scheduled to run for 91 days.

  Venues and Dates For Auditions:
  Botswana – Gabarone (Cresta President Hotel):
  4 and 5 July 2014

  Ethiopia – Addis Ababa (Capital Hotel and Spa):
  30 June 2014

  Ghana – Accra (Holiday Inn Hotel Airport):
  5 and 6 July 2014

  Kenya – Nairobi, The Hilton Nairobi:
  3 and 4 July 2014

  Malawi – Lilongwe (The Crossroads Hotel):
  30 June and 1 July 2014

  Namibia – Windhoek (Hilton Hotel):
  8 and 9 July 2014

  Nigeria – Lagos (Protea Hotel Leadway, Ikeja):
  30 June and 1 July 2014

  Rwanda – Kigali (The Lemigo Hotel)
  9 July 2014

  Sierra Leone – Free Town (The Country Lodge Complex):
  9 July 2014

  South Africa – Johannesburg (The Pyramid Venue and Conference Center):
  30 June and 1 July 2014
    
  Tanzania – Dar Es Salaam (New Africa Hotel):
  11 and 12 July 2014

  Uganda – Kampala (Sheraton Hotel):
  7 and 8 July 2014

  Zambia – Lusaka (InterContinental Hotel):
  4 and 5 July 2014

  Zimbabwe – Harare (The Meikles Hotel):
  12 and 13 July 2014

  0 0


  Makamu wa Rais Dk. Mohamed Ghalib Bilal, leo ametembelea mradi mpya wa Dubai Sports City, na kujionea ramani ya mradi huo mkubwa wa kijiji cha michezo Dubai. Kulia kwa Makamu wa Rais, ni Bwana Mohamed Sharif, Mtanzania ambaye ni Mtendaji Mkuu wa Mradi wa Dubai Sports City. Kulia mwa picha ni Balozi Mbarouk, na kushoto mwa picha ni Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai Mhe. Omar Mjenga.

  0 0


   Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania –TRL unasikitika  kuwataarifu wananchi na wateja wake  wa  huduma ya treni ya Jiji kuwa hiyo  imesitishwa kwa muda wa siku 3 kuanzia kesho Juni 19, 2014 hadi  Jumammosi Juni 21, 2014. Aidha huduma hiyo itaanza tena hapo Jumatatu Juni 23, 2014 kwa kufuata ratiba yake ya kawaida.
  Uamuzi huo unatokana na sababu za kiufundi ikiwemo kufanyiwa matengenezo vichwa vyote vya  viwili ambavyo vimekuwa vikihudumia treni hiyo ya Jiji. Vichwa hivyo vinapaswa kufanyiwa ukarabati katika Karakana Kuu ya TRL Morogoro na kwamba vitarejeshwa Jijini Jumapili Juni 22, 2014.

  Uongozi wa TRL inawaomba radhi wananchi na wateja wake wote jijini kwa usumbufu utakaojitokeza.

  -Tamati-

  Imetolewa na Afisi ya Uhusiano ya TRL kwa Niaba ya

  Kaimu Mkurugenzi Mtendaji ,

  Mhandisi  Elias Mshana

  Dar es Salaam,

  Juni 18, 2014.  0 0

  Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Shyrose Bhanji akiwahi uwanja wa ndege kwa Bodaboda baada ya kukwama masaa kadhaa barabarani kutokana na foleni kubwa aliyokutana nayo akiwa mitaa ya Mikocheni jijini Dar es salaam

  0 0

  With salams and jambo from Bukoba
  Please note, the read and blue marking on the head, these are the four points where cancerous boils were removed and he was getting dressing.
  IZAAS bears witness that since ZIDO and these ladies group joined hands with IZAAS they have changed  lives of many children.
  Kindly read see attachment below.
  Mubaarak Abdullah.

  0 0

  Uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia Kidato cha Tano katika shule za Serikali na Vyuo vya Ufundi kwa mwaka 2014 umekamilika. Uchaguzi umefanyika kwa kuzingatia takwimu za matokeo ya watahiniwa waliofanya Mtihani wa Kidato cha Nne Tanzania Bara mwaka 2013. 

  0 0

  Na Abdulaziz ,Lindi 
  Mtandao wa Jamii wa Usimazi wa misitu Tanzania (MJUMITA) wamekuwa wakitoa elimu ya utawala bora katikavijiji 24 vinavyozunguka msitu wa Angai kuanzia mwaka 2011 kwa ufadhili wa Limas (lindi and masasi agribusiness support) Mjumita wamekuwa wakitoa elimu hiyo katika hivyo ikiwemo Uraghabishi ,utawala bora, Usimamizi shirikishi wa misitu,Uongozi na Utawala bora huku Elimu ikitolewa kwa jamiii za vitongoji juu ya uwezeshaji na utunzaji wa misitu kwa manufaa ya jamiii zilizo katika vitongoji na Vijiji wilayani Liwale 
  Akiongea na Globu ya Jamii ,Bw Frank Munuo mwakilishi wa Mjumita wilayani humo alieleza kuwa Vijiji 3 miongoni mwa vijiji 24 vilivyo katika msitu wa Angai wilayani Liwale vitaanza uvunaji mwishoni mwa mwezi huu(June)baada ya kukamilisha michakato yote hatimaye kufikia hatua ya uvunaji 
   Vijiji hivyo ni Mtawatawa, Kitogoro na Litohu vimefikia hatua hiyo baada ya elimu iliyotolewa na ikiwa ni hatua ya kipekee kwa vijiji kuanza kufaidika na misitu ya vijiji kwani kupitia Uvunaji huo asilimia 95% ya mapato yatakuwa ni kwa ajili ya kijiji na asilimia 5% ni kwa Halmashauri ya wilaya kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma pale watakapohitajika kufanya hivyo. 
  Aidha Frank alibainisha pia Kufikia hatua hiyo yaa ya vijiji hivyo 3 kuanza uvunaji ni hatua ya kipekee kwa wanajamii kuanza kunufaika na raslimali hizi za misitu moja kwa moja imetokana na Mafunzo kwa vijiji hivyo 24 mafunzo ambayo yamesaidia utunzaji wa Misitu pamoja na kumaliza migogoro ya Vijiji ikiwemo ya Mipaka na na Utawala Bora 
  Kwa Upande wake,Mkuu wa Wilaya ya Liwale,Ephraim Mmbaga akiongea na waandishi wa habari waliotembelea wilaya hiyo alieleza kuwa Usiri wa jamiii na kuoneana haya ndio changamoto kubwa inayoathiri maendeleo ya wilaya hiyo huku raslimali zikinufaisha wachache 
   Akiongelea mpango unaoendelezwa kwa Usimamizi wa Mjumita na Limas,Mmbaga amesema ameridhishwa na Asasi hizo kwa kusaidia kutoa elimu kwa jamiii kutunza misitu yao ili wanufaike na rasilimali hizo hulu akibainisha uelewa uliopo Vijijini baada ya kupewa mafunzo ya Utawala Bora ambapo kwa sasa vijiji vinakutana kupanga mipango shirikishi ya Maendeleo Ikiwemo kubainisha mapato na matumizi,Usawa wa kijinsia,Huduma za Jamii pamoja na kulinda Misitu baada ya kuelewa manufaa yatakayopatikana
   Mashine inayotumika kukatia magogo ambayo tayari mkoa wa Lindi imepiga Marufuku kutumika kwa mashine hiyo ambayo inachangia kwa kiasi kikubwa Uharibifu wa Misitu
   Wananchi wa kijiji cha Ngunja wilayani Liwale wakiwa katika mkutano mkuu maalum wa kijiji ambao unapokea mrejesho baada ya Mafunzo yaliyotolewa na Mjumita pamoja na Limas
  Picha na Abdulaziz,Lindi

  0 0

  Kwa hisani ya KTN

  0 0

   Majaji wakiwa kazini katika Shindano lililofanyika Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza.Picha na Maktaba.
  Na Josephat Lukaza - Proin Promotions, Dar Es Salaam
  Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) Kwa KAnda ya Pwani limemalizika leo Mkoani Dar Es Salaam mara baada ya washindi watano watakaoiwakilisha Kanda hii katika Fainali kubwa itakayofanyika Mwishoni mwa Mwezi wa nane kupatikana katika Ukumbi wa Makumbusho na hatimaye washindi hao Kukabidhiwa shilingi laki tano taslimu.
  Shindano hili lilianza tarehe 30 Mei 2014 na kusimama kwa Muda kutokana na Msiba wa George Tyson ambae alikuwa ni mzazi mwenza wa jaji Yvonne Cherry au Monalisa. Katika Kuungana nae katika kipindi kigumu alichopitia Timu nzima ya TMT ilibidi kusimamisha Shindao hilo Kwa Muda hadi pale Msiba kumalizika, na Baada ya Msiba kumalizika Shindano hili liliendelea tena mnamo tarehe 15 June 2014 na kufikia tamati leo kwa Washindi watano Kupatikana.
  Kanda ya Pwani inahusisha Mikoa ya Morogoro, Pwani na Dar Es Salaam ambapo takribani washiriki 300 waliweza kujitokeza kwaajili ya kushiriki shindano hili kwa Kanda ya Pwani.
  Washindi watano waliopatikana katika Kanda ya Pwani wataungana na Washindi wengine kutoka Kanda ya Ziwa, Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini ambao walishapatikana kwaajili ya kuingia kambini ambapo wawakilishi hao wa kanda hizo watapewa mafunzo kutoka Kwa Walimu wa Sanaa wa Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam na Kutoka Chuo Cha Sanaa cha Bagamoyo na hatimaye wataendelea na mchujo ambapo Mshindi mmoja ataondoka na Kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania katika fainali kubwa itakayofanyika mwisho wa Mwezi wa nane.
  Vilevile vipindi vya Shindano hili vinarushwa katika kituo cha runinga cha ITV siku ya Jumamosi saa 4 Usiku na Marudio yake ni Saa 10 Jioni siku ya Jumapili na Jumatano ni saa 5 usiku.
  Na Jumamosi ya Wiki kipindi cha Dar Es Salaam kitarushwa muda ule ule wa Saa 4 Usiku siku ya Jumamosi na marudio yake siku ya Jumapili saa 10 Jioni na Jumatano saa 5 usiku.
  Washindi wa Kanda zote wanatarajia kuwasili katika Nyumba ya TMT hivi karibuni kwaajili ya Kuanza kambi kwaajili ya safari ya kuwania Shilingi Milioni 50 katika fainali kubwa itakayofanyika mwishoni mwa Mwezi wa Nane.
  Vilevile katika Fainali hiyo washindi kumi bora watakuwa chini ya Kampuni ya Proin Promotions ambao ni waandaaji na waendeshaji wa Shindano hili na hatimaye wataweza kufanya kazi ya pamoja na hatimaye kunufaika na Kazi hiyo.
  Shindano hili la Tanzania Movie Talents (TMT) lilianza safari zake za kusaka Vipaji katika Kanda ya Ziwa na kuendelea na zoezi hilo kanda ya Kati, Nyanda za Juu Kusini, Kusini na Kaskazini na hatimaye safari hizo zimefikia tamati leo mara baada ya washindi watano kupatikana kutoka Kanda ya Pwani.

  0 0

  IMG-20140618-WA0010
  Mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi ambaye pia ni  mkurugenzi mkuu  wa tume ya mawasiliano nchini Kenya
  IMG-20140618-WA0004
   Mkurugenzi mkuu  wa tume ya  mawasiliano nchini Uganda Patrick Mwesigwa
  IMG-20140618-WA0001
   Mkurugenzi wa  Watumiaji wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema
  IMG-20140618-WA0005
  Balozi Joseph  Bangurambona wa Burundi akiongea juu ya mkutano huo.
  IMG-20140618-WA0012

  Wadau  zaidi ya mia moja kutoka taasisi za mamlaka ya mawasiliano Afrika Mashariki (EACO} wamekutana jijini Arusha ili kuangalia namna ya kuweza kutatua changamoto zilizopo katika sekta hiyo muhimu ya mawasiliano.
   
  Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa umoja huo(EACO) Francis Wangusi  ambaye pia ni  mkurugenzi mkuu  wa tume ya  mawasiliano nchini Kenya alisema kuwa mkutano huo unalenga kujadili  changamoto zilizobainishwa na wadau wa sekta hiyo kuhusu vikwazo ambavyo vinakwamisha mbalimbali  usambazaji wa mawasiliano kwa nchi hizo.
   
  Wangusi alisema kuwa  sekta ya mawasiliano ina vitengo mbalimbali ikiwemo posta,mawasiliano ya simu na utangazaji na mitandao ya kijamii(internet) ambayo bado inakabiliwa na changamoto nyingi  zinazohitaji juhudi za wadau wa sekta hiyo ili kuwafikia watumiaji.
   
  Aidha alibainisha kuwa huduma ya posta bado inakabiliwa na changamoto ya anuani makazi ili kuwawezesha watumiaji  wanaoutumia huduma hiyo iweze kuwafikia kwa haraka kama zilivyo huduma nyingine.
   
  Hata hivyo wangusi aliongeza kuwa changamoto nyingine kubwa ni mawasiliano ya huduma za simu katika nchi za Afrika mashariki ambapo mbali na watoa huduma kupata faida kubwa lakini pia wanawatoza watumiaji gharama kubwa hivyo kupelekea watumiaji kutoka nchi moja hadi nyingine kushindwa kumudu.
   
  Kwa upande wake Mkurugenzi wa  Watumiaji wa Watoa Huduma za Mawasiliano hapa nchini Dkt.Raynold Mfungahema alisema lengo ni kuangalia kuwa mawasiliano yanawafikia watumiaji  na kufaidi huduma hiyo ya simu,internet,utangazaji na maswala ya posta.


  (Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog)

  0 0

  TANGAZO MAALUM  NA MUHIMU
  Ninapenda kuwatumia Watanzania wote habari hii kuhusu hisa za kampuni ya 'Swala Energy' zinazotolewa kwa mara ya kwanza kwa shilingi 500 kwa hisa. 
   Kuna wenye uzoefu wa kufanya shughuli hizi za ununuzi na uuzaji wa hisa lakini kuna wengine ambao wangependa kuanza kufanya kuwekeza kwa njia hiyo. 
   Ni vyema wananchi wawe na habari hizi ili wafanye uamuzi unaofaa badala ya kutokujihusisha na shughuli hii kwa sababu ya kukosa habari au kutokufahamu kinachoendelea. 
   Ninaambatanisha habari. Wasalaam, Dr Casta Tungaraza 
   Tanzania's Tourism Goodwill Ambassador in Australia 
   199 Oxford St, 
  Leederville 6007, 
  Western Australia

  0 0  0 0

  Wajumbe wa Kamati ya Fedha Utawala na Mipango wa Halamashauri ya Wilaya ya Rungwe wakikagua tenki la maji katika kata ya Kyimo
  Jengo la hostel ya wasichana katika shule ya sekondari ya Lupoto, linaendelea kujengwa na Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe


  Wajumbe wa Kamati ya fedha wakiwa pamoja mbele ya jengo la Shule inayojengwa kwa nguvu za wananchi katika kata ya Ikuti.

  Kwa Picha na habari zaidi bofya 

  0 0

  Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Jamal Malinzi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzungumzia ushirikiano wa TFF na Shirika la kutetea haki za watoto la Plan International kwa ajili ya kutetea na kuhamasisha juu ya ulinzi wa haki za mtoto hapa nchini.Hafla hii imefanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa TFF,jijini Dar es Salaam.Wapili Kulia ni Mkurugenzi wa Plan International Tanzania, Jorgen Haldorsen.Picha na Othman Michuzi.
  Mkuu wa Kampeni ya kutetea na kuhamasisha juu ya ulinzi wa haki za mtoto hapa nchini,Bi. Elena Ahmed akielezea namna kampeni hiyo itakavyoendeshwa kupitia Michezo kwa maeneo mbali mbali hapa nchini wakati Mkutano na waandishi wa habari jijini Dar leo.Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Jamal Malinzi.
  Rais wa Shirikisho la Soka Nchini (TFF), Jamal Malinzi (wa pili kushoto) na Mkurugenzi wa Plan International Tanzania, Jorgen Haldorsen wakisaini mkataba wa makubaliano wa Kampeni ya kutetea na kuhamasisha juu ya ulinzi wa haki za mtoto hapa nchini.Wengine pichani ni Golikipa wa timu ya Taifa (Taifa Stars) ambaye pia ni Balozi wa Kameni hiyo,Deogratius Munish (kulia),Ofisa Habari na Mawasiliano wa TFF,Boniface Wambura (katikati) na Mkuu wa Kampeni ya kutetea na kuhamasisha juu ya ulinzi wa haki za mtoto hapa nchini,Bi. Elena Ahmed (kushoto) wakishuhudia.
  Picha ya pamoja mara baada ya kusainishana mikataba ya makubaliano.

  Wakati mamilioni ya Watanzania wakifuatilia Fainali za Kombe la Dunia nchini Brazil, Shirika la kutetea haki za watoto la Plan International limeingia ubia na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kwa ajili ya kutetea na kuhamasisha juu ya ulinzi wa haki za mtoto hapa nchini.

  Kwa lengo hilo, mkataba wa ushirikiano umesainiwa leo katika ofisi za makao makuu ya TFF jijini Dar es Salaam baina ya Mkurugenzi wa Plan International Tanzania, Jorgen Haldorsen na Rais wa TFF, Jamal Malinzi. Ushirikiano huo unalenga kufanya kazi pamoja katika kushughulikia masuala ya ukatili wa kijinsia, ndoa na mimba za utotoni.

  Kwa mujibu wa Haldorsen, mchezo wa mpira ndio unaoongoza nchini na kote duniani kwa kuwa na ushabiki mkubwa na kwamba joto kali juu ya Fainali za Kombe la Dunia linaloendelea Brazil ni ushahidi tosha.

  “Tunatambua uwezo wa mchezo huu wa kuwajumuisha watu. Sasa tunataka tuwajumuishe watu sio tu kwa ajili ya furaha lakini pia kama njia ya kuleta mabadiliko juu ya usawa wa kijinsia kwa kutetea na kuhamasisha juu ya haki za mtoto wa kike,” aliongeza.

  Mkurugenzi huyo alidokeza kuwa ushirikiano na TFF ni sehemu ya kampeni ya kimataifa inayoendeshwa na shirika hilo kote ulimwenguni inayoitwa ‘Because I Am A Girl’-BIAAG au kwa Kiswahili- KWA SABABU MIMI NI MSICHANA ambayo inalenga kuwatoa mamilioni ya wasichana kutoka katika umaskini kupitia uhamasishaji juu ya haki zao, elimu na stadi za maisha.

  “Kwa kupitia ubia huu tutakuwa na uwezo wa kuwafikia mamilioni ya Watanzania na tutawapa wasichana ujumbe kuwa KWA SABABU MIMI NI MSICHANA, lazima nipate fursa sawa na wavulana. KWA SABABU MIMI NI MSICHANA, lazima niwe na uwezo wa kufunga magoli ya kufikia ndoto zangu katika maisha,” Haldorsen alieleza.

  Kwa upande wake, Rais wa TFF, ambaye ni mjumbe katika Kamati ya Huduma kwa Jamii ya Shirikisho   la Mpira wa Miguu Ulimwenguni- FIFA, alisema kuwa ubia huo ni sehemu ya utekelezaji wa sera za huduma kwa jamii ya TFF na kwamba wana furaha kushirikiana na Plan International kwa lengo hili muhimu.

  “Ushirikiano huu ni muhimu sana kwetu kwani unakileta chombo kikubwa kabisa cha michezo hapa nchini pamoja na shirika la Plan International hususan kwa ajili ya haki za mtoto wa kike. Tunategemea kutumia mtandao wetu nchi nzima kuelimisha juu ya usawa wa kijinsia na uhamasishaji wa haki za mtoto wa kike,” alisema Rais Malinzi.

  Kwa pamoja tutashughulikia masuala ya usawa wa kijinsia, hususan kupambana na ndoa za utotoni ambazo zinawazuia mamilioni ya watoto wa kike nchini wasiweze kumaliza shule, kufikia ndoto zao katika maisha, na vile vile kuwaacha waendelee kuteseka katika umaskini,” Rais Malinzi aliongeza.

  0 0

  Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Abdallah Omari Kigoda akiweka sahihi Hati ya Ushirikiano wa Kimaendeleo kati ya Tanzania na Jumuiya ya Ulaya yenye thamani ya Euro 626 milioni zitakazotelewa katika kipindi cha miaka Sita 2014-2020. Hati hii imesainiwa Nairobi Kenya. Anayeshuhudia ni Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala.

older | 1 | .... | 475 | 476 | (Page 477) | 478 | 479 | .... | 3272 | newer