Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live

Vijana wa Babati wapata Mafunzo kuhusu upatikanaji wa Mikopo kutoka Mfuko wa Maendeleo ya Vijana

$
0
0
Na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini - WHVUM

Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati waaswa kuzingatia Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana ya Mwaka 2007 ili kuweza kuleta maendeleo katika Halmashauri ya Mji wa Babati na hivyo kuwa chachu ya maendeleo nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerose Mtenga wakati wa Mafunzo kwa Vijana kuhusu upatikanaji wa Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana yaliyofanyika leo Mjini Babati.

Akitoa mada kuhusu Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana Bibi Mtenga amewataka vijana kujitambua na kujua kuwa wao ni rasilimali muhimu na mchango mkubwa kwa maendeleo ya kiuchumi na Kijamii hivyo kuithamini Sera ya Vijana inayomtambua kijana kuwa ni mtu mwenye umri kuanzia miaka 15 hadi 35 na kutumia fursa hiyo kupata haki zao kama vijana.

Aidha Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga amewataka Vijana wa Babati kuweka jitihada katika uandikaji wa miradi yao kwa kuzingatia muongozo wa utoaji fedha za mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana na kubuni, kuanzisha na kutekeleza miradi endelevu ambayo itakuwa na sifa za kupata mikopo hiyo kupitia SACCOS ya vijana ya Halmashauri hiyo.

Kwa upande Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole amewataka Vijana wa Babati kutumia fursa hiyo ya kipekee ya kutembelewa na maofisa kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na kupewa mafunzo ya kuwajengea uwezo mzuri wa kuendesha shughuli zao za uzalishaji mali kwa ufanisi kwani huu ni muda muafaka kwa Vijana kuendeleza vikundi vyao na kuweza kuimarisha SACCOS ya vijana kwa maendeleo yao na Mji wa Babati.

Nao vijana walioshiriki mafunzo hayo wameitaka Serikali kupitia Idara ya Vijana kuhakikisha kuwa mafunzo hayo yanakuwa endelevu na yanawafikia vijana nchini kote ili kuwawezesha vijana kufahamu umuhimu wa Mfuko huo, upatikanaji wa fedha, pamoja na sifa za upatikanaji wa fedha kutoka mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerose Mtenga akisalimiana na Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole alipomtembelea ofisini kwake wakati wa ziara ya Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati.
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerose Mtenga akizungumza na Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole ofisini kwake kabla ya kukutana na Vijana kwa ajili ya Mafunzo yanayohusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati.
Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Venerose Mtenga akitoa mada kwa wanamafunzo (hawapo pichani) wakati wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kulia ni Mkurugenzi wa Mji wa Babati Bw. Omari M. Mkombole na katikati ni Afisa Maendeleo ya Vijana Bi. Amina Sanga.
Bw. Petro Benedict kutoka Kikundi cha Ebenezer Group akichangia mada wakati wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati yaliyoandaliwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Amina Sanga akitoa mada wakati wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati (hawapo pichani) kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati.
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Godfrey Nyaisa akitoa mada wakati wa Mafunzo ya Vijana wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati (hawapo pichani) kuhusu Mikopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana leo Mjini Babati. (Picha na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini – WHVUM)

President Uhuru Kenyatta Speech on Mpeketoni Attack

Blue Leaf Mabingwa Safari Pool mkoa wa Lindi

$
0
0
KLABU ya mchezo wa Pool ya Blue Leaf Mkoani Lindi imemefanikiwa kutwaa Ubingwa wa fainali za mashindano ya mchezo huo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition 2014” uliomalizikamwishoni mwa wiki Mkoani humo na kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Lindi kwenye fainali za zinazotarajiwa kufanyika Mkoani Kilimanjaro.

Nafasi ya pili ilichukuliwa na Bwalo la Polisi Pool Klabu na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya tatu ni Fisi Pool Klabu ambao walijinyakulia fedha taslimu Shilingi 250,000/=

Upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaumeHassan Salum alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= na nafasi ya pili ilichukuliwa na Pius Abubakari ambaye alizawadiwa Shilingi 250,000/= 

Mchezaji mmoja mmoja Wanawake, Mwajuma Othman alifanikiwa kutwaa ubingwa huo na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi300,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za kitaifa upande wa wanawake.Nafasi ya pili ilichukuliwa na Mariam Hassan ambaye alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=.

Fainali za kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni Tabora,Shinyanga,DodomaMbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,
Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
Bingwa wa mchezo wa Pool Afrika upande wa mcvhezaji mmoja mmoja Wanaume(Singles), Patrick Nyangusi (kushoto) na Salum Ally wakishindana kucheza(Lag) wakati wa fainali za mchezo huo upande wa mchezaji mmoja mmoja wanaume uliochezwa katika klabu ya Jambo Lee Kawe jijini Dara es Salam mwishoni mwa wiki.Partick Nyangusi alishinda mchezo huo.
Mchezaji wa Klabu Pool ya Jaba, Kinondoni Dar es Salaam, Mayaula Muhagama akicheza wakati wa fainali zamchezo huo za mashindano yajulikanayo kama ‘Safari National Pool Competition 2014” ngazi ya Mkoa,yaliyofanyika katika Klabu ya Jambo Lee Kawe Dar es Salaam.Kulia ni Mwamuzi wa mchezo huo, Peter Majani.  

TASWIRA MBALIMBALI ZA KUTOKA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

$
0
0
 Naibu waziri wa Fedha Mhe. Mwingulu Nchemba akizungumza na Madiwani wa Kongwa,Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Wilaya (Kongwa) ambo wamefanya Ziara ya kimafunzo leo kujionea uendeshaji wa Shughuli za Bunge.
 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Kazi Maalum Mhe.Marck Mwandosya akiwapungia mkono ishara ya kuwasalimia  Madiwani wa Kongwa,Wenyeviti wa Serikali za Mitaa na Wilaya Kongwa ambao wamefanya Ziara ya kimafunzo leo kujionea uendeshaji wa Shughuli za Bunge leo
 Mhe.Vicky Paschal Kamata kushoto akibadilishana mawazo na wabunge wenzake kutoka kushoto kwake,Mhe.Anna Abdallah,Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa ,Mhe.Gaudentia Kabaka(Waziri wa Kazi na Ajira) na Mhe.Rosemary Kasimbi Kirigini.

 Balozi wa Tanzania Ujerumani Mhe.Philip Marmo katikati akijadiliana jambo kutoka kulia Mwanasheria Mkuu,Mhe.Jaji Frederick Werema,Mhe.Vita Kawawa,Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa na Mhe.Beatrice Shelukindo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA


NAIBU KATIBU MKUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI ATEMBELEA MABANDA MAONYESHO UTUMISHI WA UMMA DAR

$
0
0
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu akimkaribishaNaibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wapili kulia) katika Banda la Nida kujifunza masuala mbalimbali ya kiutendaji yanayofanywa na Mamlaka hiyo iliyopo Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari wa Wizara hiyo, Christina Mwangosi.
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kulia) akimsikiliza kwa makini Afisa Tawala Mwandamizi wa Idara ya Wakimbizi, Jenita Ndone wakati alipokuwa anaeleza majukumu ya Idara hiyo ambayo inasimamia masuala ya wakimbizi nchini, wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Manzi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
 
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) akimuuliza maswali Afisa wa Idara ya Uhamiaji, Mathew Ikomba kuhusu matatizo mbalimbali likiwemo baadhi ya wananchi wanailalamikia Idara hiyo kuhusu uombwaji wa rushwa wakati wanapoomba kupatiwa Hati ya Kusafiria (pasipoti). Malemi aliitaka idara hiyo ifuate haki wakati wananchi wanapoomba pasipoti. Wizara na Idara zake inashiriki katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam
 Koplo wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Loyce Abeid, akimuonyeshaNaibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (kushoto) kifaa kinachotumika kwa ajili ya uokozi wa magari yanapopata ajali hasa magari ya tenki. Malemi alitetembelea Banda la Wizara na Taasisi zake katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam.
 
 Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwamini Malemi (wapili kushoto aliyekaa kwenye kiti) akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Wizara yake ambao wapo katika Maonyesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam. Kushoto aliyekaa kwenye kiti ni Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida), Dickson Maimu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 





"WOMEN WITH ATTITUDE" SINEMA YENYE LADHA YA SHUGHULI KUONYESHWA NGOME KONGWE LEO

$
0
0
DSC_0166
Mtanzania mmoja kati ya wawili walioshirikishwa katika filamu ya "Woman with Altitude" iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Ashura Kayupayupa (kulia), akizungumza na waandishi wa habari leo mchana kwenye hoteli ya Doubletree by Hilton Zanzibar. Kushoto ni Mratibu wa Majaji wa tuzo za ZIFF 2014, Fabrizio Colombo na Katikati ni Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo.(Picha na Zainul Mzige wa MOblog).
Na Mwandishi wetu, Zanzibar
UNAWEZA kudhani kamba kila aliyefanikiwa amezaliwa na kijiko cha fedha, yaani amezaliwa katika eneo lenye hali shwari na kitanda chake ni mayai ya dhahabu, kumbe sivyo kabisa.
Hili linajadliwa kwa undani katika sinema iliyoandaliwa na Shirika la Mpango wa chakula duniani (WFP), Women with Atitude.
Sinema hii ambayo inaoneshwa katika ukumbi wa wazi wa Ngome Kongwe imetengenezwa na watanzania kwa ajili ya kuhamasisha Watanzania kutambua kwamba maisha ni mkusanyiko wa utatuzi wa migogoro inayowakuta na kwa kupitia elimu.
Women with Altitude inazunguka katika vitu vingi, lakini cha maana ni wanawake wanaojiamini.
Baada ya kufanikiwa kupanda mlima Everest mwaka 2008, wanawake saba wa Nepal waliamua kupanda milima mingine nmirefu katika mabara mbalimbali wakiwa na lengo la kutoa ushawishi kwa wanawake na wasichana duniani kote kufuatilia mambo ambayo yanaonekana ni magumu na hayawezekani.
DSC_0162 
Afisa Habari wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Mpango wa Chakula Duniani (WFP), Fizza Moloo akizungumzia kuhusiana na documentary iliyopewa jina la “Women with Altitude” ambapo ndani yake wameshirikishwa wasichana wa kitanzania wawili na imefadhiliwa na shirika hilo itakayooyeshwa leo jioni ndani ya viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar linakoendelea tamasha la 17 la ZIFF 2014.
Machi 2013,wanawake hao walipata ushosti kutoka kwa wanawake wa Kiafrika wane akiwemo muigizaji wa Afrika kusini Hlubi Mboya,ambaye anatambulika sana kwa kuigiza nafasi ya mtu anayeishi na VVU kama Nandipha kwenye Isidingo kupanda mlima mlima mkubwa wa bara la Afrika, Mlima Kilimanjaro.
Tofauti ya utamaduni na mazingira kwa wanawake wote 11 ilikuwa pia ni ishara ya matatizo waliyokumbana nayo katika maisha yao.
Filamu hii ya Women with attitude inaonesha matatizo ya wanawake hao 11 waliokuwa wakikumbana nayo katika maisha yao yote, na nafasi ya elimu katika kuwasaidia kufika pale walipo kwa leo.
Wanawake hawa wanaonekana wakikabiliana na Mlima Kilimanjaro, wakiangalia maisha ya wenzao na kuwashawishi katika kutokata tama na badala yake kutumia changamoto kuleta maisha yenye hadhi ya aina yake.
Ofisa habari wa WFP, Fizza Moloo akizungumza katika mahojiano alisema kwamba taarifa iliyomo ndani ya sinema hiyo ni ujumbe tosha kwa vijana na wanawake kuhusu ukweli wa maisha na namna ya kuyabadili.
  DSC_0098
Baadhi ya wasanii na waigizaji filamu wanaohudhuria tamasha la ZIFF 2014 linaloendelea kutimua vumbi kwenye viunga vya Ngome Kongwe visiwani Zanzibar.

DIAMOND, WEMA WANOGESHA KILI MUSIC TOUR SONGEA

$
0
0
 Diamond akiburudisha wakaazi wa Songea katika uwanja wa Majimaji
 Diamond akimuimbia Wema wimbo wa "You are my Number One"
Wakaazi wa Songea wakishuhudia burudani toka kwa wakali wa muziki nchini katika tamasha la Kili Music Tour kwenye Uwanja wa Majimaji Songea.

Shoti ya Umeme yasababisha Kukosekana Umeme Baadhi ya Maeneo Zanzibar leo

$
0
0
                     Hii ndio breaker liyoungua na kusabibisha maeneo ya mjini Ubguja kukosa umeme leo


 Mafundi kutoka ZECO wakiwa katika harakati za kutengeneza panel iliyoleta hitilafu za umeme na kupelekea maeneo yote ya mji wa Unguja kukosa umeme


Baada ya kukamilika kwa matengenezo


Kuamkia alfajiri ya leo ya tarehe 17/06/2014 maeneo yate ya mji wa Unguja na maeneo jirani ya mji wa Unguja yalikumbwa na ukosefu wa umeme uliotokea kuanzia majira ya saa 11 asubuhi hadi saa 7 mchana kulikosababishwa na hitilafu zilizotokea katika moja ya panel zake na kuungua kwa breaker katika kituo cha kusambazia umeme Mtoni mjini Unguja.

Katika kipindi hicho chote njia (laini)  za maeneo ya mji wa Unguja zinazopokea umeme wa  mkondo wa 11kV yalikosa umeme.  Njia (laini) hizo ni njia ya Mtoni-Mpendae, Cotex, Saateni 5 na Saateni 6.

Miongoni mwa maeneo yaliyokosa umeme ni:

Laini ya Saateni 5: Saateni, Mkele, Muungano, Jang’ombe, Mpendae, Kidongochekundu, Kilimani, Kikwajuni.

Laini ya Saateni 6: Mlandege, Darajani, Malindi, Kiponda, Forodhani, Mkunazini, Gongoni, Mwembetanga, Shangani, Hospitali ya Mnazi Mmoja.

Laini ya Cotex: Mwembemakumbi, Kwaalamsha, Kariakoo, Mwembeshauri, Misufini, Maruhubi, Mabanda ya Ng’ombe, Mtoni, Beit el Ras, Kibweni, Bububu, Mwanyanya, Dole, Kizimbani, Kinumoshi.

Laini ya Mtoni-Mpendae: Chumbuni, Makadara, Darajabovu, Kilimahewa, Sebleni, Nyerere, Magogoni, Magomeni, Mwanakwerekwe, Melinne Uzi, Kijitoupele, Kwarara, Nyarugusu, Fuoni, Chunga, Welezo, Kinuni, Masingini, Kianga, Meli sita, Mwera, Koani, Kidimni, Dunga, Mgenihaji, Uzini, Bambi, Pagali.

Tahadhari kwa wateja ni kwamba wakati wowote ule umeme unapozimika ni vyema kuzima vifaa vya umeme vilivyowazi ili kuepuka athari ya kuunguza vifaa vyao wakati umeme utakaporudi.

Wakaazi wa Mpeketoni wameanza kuhama makwao baada ya watu tisa wengine kuuawa Lamu, Kenya

kombe la chandimu tandika

$
0
0
Gado-kwa-gado katika mechi hii ya mchangani huko Tandika, Dar es salaam. Baada ya viwanja vingi kuvamiwa jiji limebakiwa na vichache vya kukuza vipaji kama ilivyokuwa zamani.

KIOTA KIPYA CHA MARAHA CHAIBUKA KATIKATI YA JIJI LA DAR, UFUNGUZI RASMI JUMAMOSI

$
0
0
 Haya sasa wakazi wa Dar es Salaam, Shughuli imewadia kushudia club ya aina yake hapa nchini. Iko katika jingo jipya la IT PLAZA mtaa wa Ohio Street, inatazamana na PPF TOWERS. Club hii mpya inajulikana kwa jina la HIGH SPIRIT LOUNGE ambayo iko ghorofa ya 11. Parking za kumwaga mpaka underground na ulinzi wa kutosha. Fika ujionee mwenye ufunguzi rasmi Tarehe 21/6/2014 kuanzia saa tano usiku. Ma- DJ watakao kupatia burudani tosha. SOUND MPYAAAAA. Pia Kombe la Dunia utaliona katika luninga ya kisasa na surround sound. USIKOSE.

Article 4

NEWS ALERT: MUME WA FROLA MBASHA APANDISHWA KIZIMBANI kWA KESI YA UBAKAJI

$
0
0
 Na Mwene Said 


MSANII Emmanuel Mbasha (32) na mume wa Mwimbaji wa Injili, Flora Mbasha (pichani wakiwa, amefikishwa katika Maha kwenye shughuli zao siku za nyuma) kama ya Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na mashitaka mawili ikiwemo ya ubakaji.

Mshtakiwa huyo ambaye ni mfanyabiashara na mwimbaji alisomewa mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Wilberforce Luago.

Wakili wa Serikali Nassoro Katuga alidai kuwa mshtakiwa alitenda makosa hayo mawili maeneo ya Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam.

Katuga alidai katika shitaka la kwanza kuwa, Mei 23, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, Wilaya ya Ilala, jijini Dar es Salaam,  kinyume cha sheria huku akijua ni kosa alimuingilia kwa nguvu msichana anayedaiwa kuwa shemeji yake (jina limehifadhiwa).

Katika shtaka la pili, ilidaiwa kuwa Mei 25, mwaka huu eneo la Tabata Kimanga, jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria, mshtakiwa aliumuingilia kwa nguvu  mfanyakazi wake (jina limehifadhiwa).

 Hata hivyo, mshtakiwa alikana mashitaka hayo .


Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi la dhamana.

Hakimu Luago alitaja masharti ya dhamana kwa mshtakiwa kuwa na wadhamini wawili, mmoja awe mtumishi wa serikali na mwingine kutoka taasisi inayotambulika watakaosaini hati ya dhamana ya Sh. milioni 5.

Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana hivyo alipelekwa rumande na kesi iliahirishwa hadi Juni 19, mwaka huu itakapotajwa.

Mbasha akiwa chini ya ulinzi wa askari polisi alisindikizwa katika basi la Jeshi la Magereza kwa ajili ya kwenda kuanza maisha mapya mahabusu ya Keko, jijini Dar es Salaam.


kipute cha leo cha kombe la dunia Brazil kupitia superSport

TAARIFA YA MH. JERRY SILAA BAADA YA KUIBIWA AKAUNTI ZAKE ZA FACEBOOK NA TWITTER

$
0
0
TAHADHARI 
Hii ni taarifa kwa umma kwa ujumla kwamba mtu au kikundi cha watu wasiojulikana na wasiokuwa waaminifu wametengeneza au kuingia kwa jinai kwenye anuani yangu ya facebook na Twiter (TWITA) kuanzia tarehe 6 Juni 2014 kupelekea mimi kushindwa kufanya chochote ikiwamo kuandika au kuposti kitu chochote tokea tarehe 7 Juni 2014. Kwa taarifa hii ijulikane kuwa posti zote toka tarehe 7 June 2014 sio zangu au sihusiki nazo.
Kwamba watu hao wanaojifanya ni mimi wanatumia maneno au jina "Jerry Silaa" na kujifanya kusapoti harakati za VIKOBA na wanaalika watu kujiunga na VIKOBA kwenye au kwa njia ya mtandao wa simu na intaneti . 

Mimi sihusiki na madai hayo ya kitapeli na ya uongo kwa namna yoyote  na wala sijamualika mtu yoyote kujiunga na VIKOBA kwenye mtandao kama inavyoenezwa na hao matapeli  ieleweke kuwa vikoba kama jumuia za kijamii zina taratibu zake za kujiunga na ofisi zilizosajiliwa na taasisi husika na zinazoeleweka hivyo ye yote atakaye kujiunga na VIKOBA lazima kufanya hivyo kwa kufuata taratibu zilizowekwa ambapo ni pamoja na kutembelea ofisi rasmi ili kusajiliwa na sio kwenye mtandao.
Wasalaam,
Jerry Silaa
================

KWA KIMOMBO 

Announcement
This is to inform the General Public that some unscrupulous person or persons have created an account for facebook that bear the words or name “Jerry Silaa” or the same person or persons have hacked my facebook account and proceeded to post an invitation or solicitation or promotion of “VICOBA” online.
I am disassociating myself with this malicious claims and solicitation and I have not invited anyone on line to join any VICOBA as advertised and therefore all people should beware of this malicious spread of news and whoever wishes to join a VICOBA should do so by following a laid out procedures which includes visiting the official registered offices.
Regards,
Jerry Silaa


WARSHA YA TASAF ILIVYOZINDULIWA LEO NA WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA PILI WA RAIS,MH.MOHAMMED ABOUD,ZANZIBAR

$
0
0
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akifunguwa Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania, ilioandaliwa na TASAF Taifa. Iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Mkurugenzi Uratibu wa Shughuliza Serekali Zanzibar, Ndg Issa Ibrahim Mahmoud, akitiwa maelezo ya Ufunguzi wa Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania unaotekelezwa na TASAF, uliofanyika katika ukumbi mdogo wa Baraza la Wawakilishi Chukwani. Kushoto kwake Mkurugenzi wa Program wa TASAF Ndg Amadius Kamngenge akifuatiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais Mhe Mohammed Aboud. Mohammed.

Baadhi ya Washiriki wa Warsha ya  Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Zanzibar wakimsikiliza Mkurugenzi wa Program wa Tasaf Ndg. Amadius  Kamangenge, akitowa maelezo ya Mradi TASAF.wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo. Yaliofanyika katika ukumbi mdogo wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
 Mkurugenzi wa Program wa TASAF Ndg Amadius Kamagenge, akitowa maelezo ya Utekelezaji wa miradi ya maendeleo ya Ujenzi  ambayo pia itawanufaisha walengwa  wa mpango wa kunusuru kaya masikini Tanzania.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania, ilioandaliwa na TASAF Taifa. Iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Mohammed Aboud Mohammed, akiwa katika picha na Maofisa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii Tanzania (TASAF) baada ya ufunguzi wa  Warsha ya Kuwajengea Uelewa wa Utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi (PWP) katika mpango wa Taifa wa Kunusuru Kaya Masikini Tanzania, ilioandaliwa na TASAF Taifa. Iliofanyika katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar.

M-Pesa yarejea hewani,Vodacoma yawaomba radhi wateja wake kwa tatizo lililojitokeza

$
0
0
Wateja wa huduma ya M-pesa wamehakikishiwa usalama wa fedha zao wakati ambapo huduma hiyo ikiwa imerejea kwa asilimia mia moja baada ya kukosekana kufuatia tatizo la kiufundi lililojitokeza mwishoni mwa wiki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza amewaambia waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo kuwa huduma hiyo kwa sasa iko imara na kuchukua nafasi hiyo kuwoamba radhi wateja kwa usumbufu walioupata wakati huduma hiyo ilipokosekana.

“Napenda kuwaomba radhi wateja wetu ambao wamekuwa na wakati mgumu kupata huduma ya M-pesa katika siku chache zilizopita. Tunatambua umuhimu wa huduma hii kwao. Hali iliyojitokeza ilikuwa nje ya uwezo wetu na kamwe hatukulitarajia.”Alisema Meza

Meza amesema kilichotokea kwenye mfumo wa M-pesa ni changamoto ambayo mfumo wowote unaotumia teknolojia unaweza kukumbana nayo bila kutarajia lakini jambo la muhimu ni kwa jinsi gani mtoa huduma anavyoweza kujipanga kuitatua kwa uharaka kudhibiti madhara makubwa zaidi kwa wateja.

“Unapokuwa katika suala la teknolojia chochote kinaweza kutokea ni kama vile inavyoweza kutokea kompyuta kukataa kuwaka lakini cha msingi ni kwa uharaka gani unaweza kudhibiti tatizo na kufikia ufumbuzi, hilo ndilo tulilolifanya na kwa sasa tunayo furaha kwamba wateja wetu wanaendelea kupata huduma.”Aliongeza

Kuhusu usalama wa fedha Meza amewahakikishia wateja wa Vodacom na wabia wake wote wanaoutumia huduma hiyo kwamba fedha zote zipo salama na zinalindwa kwani kilichotokea ni wateja kushindwa kuipata huduma hiyo kwenye menyu za simu zao  za mkononi na sio tatizo kwenye mfumo mzima wa M-pesa.

‘Fedha zote zipo salama na zinalindwa. Kama wakati tatizo lilipotokea mteja alikuwa na Sh 1/- au Sh 100/- ,Milioni basi ni kiwango hichohicho atakuwa amekikuta kwenye akaanti yake ya M-pesa au hata ya M-pawa mara baada ya huduma kurejea.”Alifafanua Meza

Meza amewashukuru wateja wa M-pesa kwa uvumilivu na ustahamilivu wao wakati timu ya watalaamu wa ndani na nje ya nchi walipokuwa katika juhudi  za kutafuta uvumbuzi wa tatizo lililojitokeza.

“Wateja wetu wamekuwa wavumilivu na wameendelea kuitumia kupitia mawakala zaidi ya 70,000 walioko nchi nzima. Hili unaweza ukaliona kupitia namna ambavyo wateja walivyoendelea kuitumia M-pesa mara baada ya kurejea, tunawashukuru sana na tunaendelea kuwaahidi huduma bora.”Aliongeza

“Hakuna madhara ya kibiashara kwetu, ila kutokana na M-pesa kuwa tegemezi kwa mamilioni ya watanzania katika maisha yao ya kila siku ikiwa ndio huduma kinara ya fedha kwa njia ya simu za mkononi, ni wazi kwamba imeleta usumbufu mkubwa kwa watumiaji.”

SEMINA YA KUJITAMBUA, KUBADILI FIKRA NA MBINU ZA KUONGEZA KIPATO

Washindi Promosheni Shinda Ki-Brazil na Mwanaspoti wazawadiwa

$
0
0
Washindi wa bahatinasibu ya Shinda Ki-Brazili na Mwanaspoti,Issa Rashid (wapili kushoto) na Michael Msumba (wapili kulia) wakipokea zawazi zao kutoka kwa Afisa Uhusiano wa Mult Choice ( Dstv ) Barbara Kambogi (kulia) na Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi,Edward Uisso.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi,Edward Uisso (wapili kushoto) akiongea na Mshindi wa promosheni ya Shinda Ki-Brazili na Mwanaspoti,wakati wa kuchezesha droo ya wiki ya pili, kulia ni Afisa Uhusiano wa Mult Choice (Dstv ) Barbara Kambogi.

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited kupitia gazetilake la michezo la Mwanaspoti kwa kushirikiana na DSTV wamekabidhi zawadi za washindi wa kwanza wa ptomosheni ya Shinda Ki-Brazil iliyozinduliwa wiki iliyopita.

Washindi walizawadiwa ni Michael Namenga, Issa Ndingo na Christopher Chengulla ambao walizawadiwa ving'amuzi na vifurushi vyake huku Jackson Fredrick wa Mwanza akikabidhiwa jozi ya jezi yenye jezi 16.

Mbali ya kukabidhi zawadi hizo, promisheni hiyo pia iliendesha droo na kupata washindi wapya. Washindi wa vingamuzi vya DSTV pamoja na kifurushi kizima cha malipo kwa mwezi mmoja (Compact Plus) waliopatikana ni Sharifu Migui (34) ambaye ni Fundi Magari, John Kilalago (39) ambaye ni Mlinzi, Mahmud Salum (54) ambaye ni Mtaalamu wa Takwimu wakati mshindi wa jozi moja ya jezi(ina jezi 16) ni Bariki Massawe(38) ambaye kazi yake ni mfanyabiashara.

Migui ambaye ni mkazi wa Mikumi Morogoro alisema, " Ninafuraha kushinda kwenye shindano hilo. Ni kitu rahisi kupata kama mtu unashiriki kwani unakuwa umejijengea nafasi ya kutosha endapo ninashiriki na mimi nimeshiriki mara nyingi ."

Massawe ambaye ni mkazi wa Tabata Kinyerezi alisema," Nimefurahi kushinda jezi baada ya kushiriki kwenye promosheni bomba ya Mwanaspoti. Jezi hizo nitatoa zawadi kwa timu yangu ya maveterani inayoitwa Kinyerezi Veteran FC."

Afisa Masoko wa Kampuni ya MCL, Edward Uisso, amesema kuwa bado kuna zawadi nyingi zimebaki kwa wasomaji ambazo ni runinga tatu zenye ukubwa wa inchi 32, dekoda 24 za DSTV zilizounganishwa na kifurushi cha Compact Plus kwa muda wa mwezi mmoja, seti nne za jezi pamoja na fedha taslimu zinazotolewa kila siku mpaka shindano litakapomalizika.

Promosheni hiyo ambayo ilifunguliwa Juni 2 itafungwa Julai 13 siku ya mwisho ya fainali hizo.Ili kuendelea kushiriki, wasomaji wa Mwanaspoti watatakiwa kutuma namba zitakazopatikana kwenye ukurasa huu wa tatu wa gazeti la Mwanaspoti kwenda namba 15551.

Kwa mujibu wa vigezo na masharti ya promosheni hiyo, kila nakala ya gazeti la Mwanaspoti itakuwa na namba mbili za ushiriki zenye tarakimu nane kila moja.

Mshiriki ana hiari ya kutuma namba yoyote kati ya hizo kushinda aina moja ya zawadi, au akipenda anaweza kutuma namba zote mbili ili kujishindia aina zote mbili za zawadi.

Namba moja imetambulishwa kwa herufi B na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za binafsi. Namba ya pili imetambulishwa kwa herufi T na itamwezesha mshiriki kuingia kwenye droo ya zawadi za timu.

LILY NA DERICK WAMEREMEKA BAADA YA KUPATA KUMUNIO YA KWANZA

$
0
0
 Derick Edward (kushoto), na Lily Charles wakijiandaa kukata keki.
 Derick Edward na Lily Charles wakikata keki wakati wa sherehe za kuwapongeza baada ya kupata Komunio ya Kwanza. Kushoto ni John Charles akishuhudia.

BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Viewing all 110025 articles
Browse latest View live




Latest Images