Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaanza leo jijini Dar

0
0
Brass Band ya Jeshi la Polisi ikiongoza maandamano ya Maadhimishi ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Watumishi kutoka Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wakipita mbele ya meza Kuu wakati wa Maandamano Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Menejiment ya Utumishi wa Umma Hab Mkwizu akizungumza wakati akimkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Mgeni Rasmi kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utawala Bora Kapteni Mstaafu George Mkuchika akizungumza kuzindua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Baadhi ya watumishi wa Umma wakifuatilia Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Afisa Habari wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Robi Bwiru akimueleza jambo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la Wizara hiyo wakati wa Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma iliyoanza leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salam.
Baadhi ya wananchi wakipata maelezo kuhusu shughuli zinazofanywa na Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki , wakati walipotembelea banda la Wizara hiyo. Picha na Hussein Makame-MAELEZO

MUSOMA VETERANI MABINGWA CASTLE LAGER PERFECT SIX KANDA YA ZIWA

0
0
Afisa Mauzo wa Kampuni ya Bia Tanzania mkoani Mwanza Liston Chale (kulia), Meneja Matukio, TBL Mwanza Eric Mwayela, na Meneja wa Bia ya Castle Lager, Kabula Nshimo wakimkabidhi Kapteni wa timu ya Musoma Veterani, Ramadhani Magoe (kushoto) kombe baada ya kutawazwa mabingwa wa fainali za Castle Lager Perfect Six kanda ya Ziwa jana baada ya timu yake kuwafunga Milango Kumi FC ya Kahama mabao 3-2 katika mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana. Mabingwa hao wataiwakilisha Kanda ya Ziwa kwenye fainali za taifa.
Wachezaji wa Timu ya Musoma Veterani, wakishangilia na kombe lao walolipata baada ya timu hiyo kuifunga timu ya Milango Kumi FC ya Kahama magoli 3-2 na kuibuka mabingwa wa Castle Lager Perfect Six kanda ya Ziwa katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Furahisha jijini Mwanza jana.

EAC CONFERENCE ON PERSONS WITH DISABILITIES SET FOR 19-20 JUNE IN NAIROBI,KENYA

0
0
 cid:image001.png@01CF865E.938D6A00
East African Community

East African Community Secretariat, Arusha, Tanzania, 16  June 2014: A Regional Conference on Persons with Disabilities themed  Empowerment: The disability concern in the EAC regional Integration Agenda is  slated for 19-20 June 2014 at the Intercontinental Hotel in Nairobi, Kenya.

The Conference will bring together a selection of persons with disabilities, representatives of people with disabilities, policy makers from the EAC region, Members of the East African Legislative Assembly (EALA) and officials from the EAC Secretariat. 
The overall objective of the conference is to ensure that disability concerns are mainstreamed in laws and policies at both the national and regional level. In addition, the conference will review progress made by the EAC Partner States in the attainment of Millennium Development Goals in relation to People with disability" and their participation the Post 2015 agenda. 
The conference will be addressed by key EAC policy makers as well as renowned personalities regarding the main theme “Empowerment: the Disability Concern”. In addition presentations on measures undertaken by the EAC Partner States towards empowering the disability concern will be made by each Partner State.
 Some of the issues  expected  as outputs of the PWDS Conference include resolutions and recommendations that will guide mainstreaming of disability concern in National and Regional Laws and Policies; increased awareness on the rights of PWDs among all stakeholders as well as the development of an East African Declaration on Disability mainstreaming. 
According to the tentative programme released by the EAC Secretariat, the conference will be attended by Technical Experts from the relevant Ministries responsible for Persons with Disabilities, EAC Affairs, Labour as well as  Technical Experts representing Umbrella Trade Union and National Employer Association/Federation.
 Others include representatives of the National Council of Persons with Disabilities, Persons with Disabilities (Representing categories of PWDs),Interpreter/Sign Language Experts, Aides to the PWDs, Experts (Equal Opportunities) drawn from the office of the Ombudsma and Members of the National Parliaments of the EAC Partner States.
 All the EAC Partners states have policy measures that are put in place to mainstream the disability concern at both the national and regional level, the EAC and the East African Legislative Assembly (EALA), both recognize the need to empower Persons with Disabilities. 
This is also in line with the Post 2015 UN Agenda on Permanent Forum on Indigenous Issues where the main priority areas include prioritizing of the special conditions and needs of indigenous women, children, youths and indigenous persons with disabilities.
 The interests of the PWDS have also been taken into consideration:  national, Regional and International level by the International Disability Alliance (IDA) which plays an important role together with Inclusion International to advance the human rights of persons with Disabilities: - 

-          There are one billion persons with disabilities worldwide, 80% of whom live in developing countries
-          A number of high-level commitments have been made, both at the global and regional levels, to promote equality and inclusion of persons with disabilities in development, and recognition of the United Nations Convention on the Rights of Persons with Disabilities (UN CRPD) as both a human rights and development instrument

 It is for this reason that the EAC Conference on Persons with Disabilities has been organized with a definitive purpose to determine how best the current provisions of the EAC Treaty can be used as a basis for developing a comprehensive regional policy governing persons with disabilities as well as proposing the adoption of a legally binding protocol or enactment of a regional law.
The second regional  conference on persons with disabilities builds on the first EAC conference that was held from 19-20 February  2010, at the Sheraton Hotel, Kampala, Uganda, whose theme was “Towards a policy and law to address challenges facing persons with disabilities in the EAC region.

KITOKOLOLO RAPA WA FM ACADEMIA AHAMIA BENDI YA MASHUJAA

0
0
1b
3b
…………………………………………………………………….
BENDI ya Mashujaa imemchukua rapa, Kalidjo Kitokololo ‘Kuku’ kutoka bendi ya  FM Academia na kusaini naye  Mkataba wa miaka miwili.
Akizungumza kwenye ukumbi wa Milenium Business  Park leo , Kijitonyama, Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mawasiliano wa bendi hiyo, Maximillian Luhanga amesema  kupatikana kwa  Chitokololo ni furaha kubwa kwao.
“Kalidjo anakuwa rapa wa tatu katika bendi ya Mashujaa , baada ya Saulo John maaurufu  Ferguson na Sauti ya Radi, ambao wote ni wakali, kwa marapa hao wote tunaamini bendi yetu itakuwa inatisha sana,”amesema Luhanga.  
Maxmilian Luhanga  amesema Kitokololo anaanza kazi mara moja baada ya kusaini mkataba mpya.
Kwa upande wake, Kitokololo mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amesema  amekuja Tanzania kutafuta maisha na Mashujaa imempa ofa nzuri ndiyo maana amejiunga na bendi hiyo.
Amesema ameondoka vizuri FM Academia akiwa amewaaga vizuri wenzake ambao wameridhia kuondoka kwake.
  Kitokololo amesema kwamba amejiunga na Mashujaa akimfuata  King Dodo  ambaye kimuziki ni baba yake , King Dodoo  ndiye aliyemleta nchini kwa mara ya kwanza mwaka 2004.
Mashujaa itamtambulisha rasmi mwanamuziki huyo katika onyesho maalum litakalofanyika ukumbi wa Letasi Lounge Ijumaa wiki hii.
Mashujaa pia wanatarajiwa kuwa na ratiba ndefu mara baada ya mfungo mtukufu wa ramadhani ambapo Maximillian Luhanga amewaambia mashabiki wa bendi hiyo nchini kote kukaa mkao wa kula, Kwakuwa bendi hiyo itakuwa na ziara karibu mikoa yote ya Tanzania ili kutoa burudani kwa mashabiki wao.

askari wawili wapoteza maisha katika ajali chalinze leo

0
0

Na John Gagarini, Kibaha 

WATU wawili wamefariki dunia huku mmoja akijeruhiwa baada ya magari waliyokuwa wakisafiria kugongana uso kwa uso.
 Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa Polisi mkoani Pwani, kamishna Msaidizi mwandamizi wa polisi (SACP) Ulrich Matei  (pichani) amesema kuwa ajali hiyo ilihusisha lori na gari dogo. 
Kamanda Matei alisema kuwa ajali hiyo ilitokea Juni 16 mwaka huu majira saa 1:15 usiku eneo la Chamakweza kata ya Pera tarafa ya Chalinze wilayani Bagamoyo. 

Alisema ajali hiyo ilihusisha lori aina ya Scania lenye namba za usajili T 164 AUS na tela namba T 498 AZ likiendeshwa na Hassan Shaban mkazi wa Dar es Salaam ambaye aligongana na gari aina ya Isuzu Carry lenye namba za usajili Z 190 DR likitokea mkoani Morogoro. 
“Waliokufa ni dereva wa gari dogo Meja Edward Mosi ambaye ni ofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) kikosi cha Kinonko na mkaguzi Msaidizi wa Polisi wa wilaya ya Korogwe mkoani Tanga Johnson Zakaria,” alisema Matei. 
Aidha alisema katika ajali hiyo mtu mmoja alijeruhiwa na kukimbizwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Pwani Tumbi kwa ajili ya matibabu huku miili hiyo nayo ikiwa hospitalini hapo kusubiri ndugu kwa ajili ya mazishi. 
“Kutokana na ajali hiyo jeshi la polisi linamtafuta dereva wa lori ambaye alikimbia mara baada ya tukio hilo, ili aweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria,” alisema Matei.

MKUU WA WILAYA YA MAKETE ATOA RAI KWA JAMII YA MAKETE KUSAIDIA WATOTO YATIMA NA WAISHIO KWENYE MAZINGIRA HATARISHI

0
0
 Mkuu wa wilaya ya Makete mwenye suti nyeusi (aliyesuka nywele) Mh. Josephine Matiro, mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helen Kijo Bisimba (kulia kwa mkuu wa wilaya) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto walioshiriki maadhimisho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro(wa tatu kushoto walioketi) na Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu Helen Kijo Bisimba (wa pili walioketi kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa shirika la wasaidizi wa kisheria Makete
 Katika picha ya pamoja na wanafunzi wa sekondari ya Iwawa Makete ambao nao walishiriki
 Wanafunzi wa shule ya msingi Ndulamo wakiwa katika picha ya pamoja.(Picha/habari na Edwin Moshi na Conrad Mpila, Makete.)
Imeelezwa kuwa ni jukumu la kila mmoja kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, na si kuiachia serikali ama mashirika yasiyo ya kiserikali peke yao kufanya kazi hiyo
 
Kauli hiyo imetolewa leo hii Juni 16 na mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika yaliyofanyika kitaifa (kwa asasi zisizo za kiserikali) katika viwanja vya mabehewani kata ya Iwawa wilayani Makete mkoani Njombe.
Hata hivyo mkuu wa wilaya hiyo amekiri kuwepo kwa changamoto ya watoto walio wengi Wilayani Makete ambao ni Yatima na waishio katika mazingira magumu ambao wanahitaji msaada wa kila mmoja

"Ni kweli wilaya ya Makete ina watoto ambao ni yatima na wanaoishi katika mazingira hatarishi, wengine wanalelewa katika vituo maalum vilivyopo wilayani mwetu, hivyo ni jukumu letu kuwasaidia kila mtu kwa kadri ya uwezo wake, mwenye sabuni, kalamu, fedha ama chochote anaweza kufanya hivyo kwa wakati wake" amesema Matiro

Katika risala iliyosomwa na mwanafunzi Gaudencia Malangalila wa Shule ya msingi Ndulamo kwa niaba ya wanafunzi wenzake amesema Kuwa watoto walio wengi wanakabiliwa na unyanyasaji kwa kufanyishwa Kazi ngumu na hatarishi,kutopata haki katika huduma za matibabu,walezi kunyang'anya misaada wanayopewa na wadau mbalimbali

Naye Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) Bi. Helen Kijo Bisimba amesema Kuwa kwa Tafiti alizofanya amebaini Kuwa kuna watoto ambao waliondoka kwenda nje ya Makete kwa kufanya Kazi na hawarudi tena huku wazazi hawajui Kama wapo hai au la,kwani hata mawasiliano na wazazi ama walezi wao bado ni magumu.
Hivyo amewasihi wazazi/walezi Kuwa makini na watoto wao pindi wanapoitwa kwenda kufanya Kazi maeneo ya mbali kwani mara nyingi huko wanakokwenda wanakutana na mambo ambayo ni kinyume na walioyatarajia.
Katika maadhimisho hayo kikundi cha wazazi kutoka Kijiji cha Isapulano na Ndulamo Maarufu Kama mama mkubwa wamesema Kuwa vikundi hivyo vitaendelea Kulinda haki za watoto na kutoa ujumbe kwa jamii kwa njia ya sanaa  na kufanya uchunguzi dhidi ya watoto wanaofanyiwa unyanyasaji na watatoa taarifa katika ngazi husika na wakigundulikaa wahusika wachukuliwe hatua za kisheria
 Kauli mbiu ya mwaka huu ni "kila mtoto ana haki ya elimu bora bila vikwazo" 

appreciation note from the family of the late George Tyson

0
0
The family of Mr and Mrs Okumu would like to thank you  all who came out in kind to assist in the funeral of the late Art Director George Tyson.
To you all in Tanzania and here in Kenya we say ASANTE SANA, MUNGU NA AWALIPE KWA YOTE
We buried the late George Tyson last weekend and  it went on well.
May the Almighty God bless you  all and  may the soul of our late brother rest in eternal peace - Amen
Yours 
Benson Okumu
Brother to the Deceased.

TAARIFA YA KAMATI YA BUNGE YA BAJETI KUHUSU HALI YA UCHUMI WA TAIFA KWA MWAKA 2013 NA MPANGO WA MAENDELEO WA TAIFA KWA MWAKA 2014/15 PAMOJA NA TATHMINI YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA 2013/14 NA MAPENDEKEZO YA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2014/15.


Je wajua kuwa wakongwe wa Brazil walihusishwa kuandaa kombe la dunia 2014?

0
0

Na Sultani Kipingo

Kamati ya maandalizi ya Kombe la Dunia 2014 ilikuwa na nyota watano wa zamani wa Brazil (pichani wakiwa na maafisa wa chama cha soka cha Brazil) waliowahi kuwika katika michuano hiyo tokea mwaka 1958 ilipofanyika nchini Sweden. Kamati hiyo, iliyoundwa January 2013 inaundwa na wachezaji wakongwe kina kutoka kushoto juu:

Amarildo Tavares da Silva (wa tatu toka kulia) , José Roberto Gama de Oliveira (Bebeto), Carlos Alberto Torres, Marta Vieira da Silva, Ronaldo Luis Nazario de Lima (wa pili kulia) na  Mário Jorge Lobo Zagallo (kushoto).

Watano kati ya wanakamati hao ambao wamepewa Ubalozi wa FIFA waliwahi kuchezea Brazil wakati nchi hiyo ilipofanikiwa kunyakuwa kombe hilo la dunia. Nao ni Mário Zagallo (mwaka  1958 nchini  Sweden), Amarildo (waka 1962 nchini Chile), Carlos Alberto (mwaka  1970  nchini Mexico), Bebeto (waka  1994 nchini Marekani), na Ronaldo (mwaka  2002 nchini Korea ya kusini na Japan).

Balozi mwingine ni mwanamama Marta Vieira da Silva ambaye ni mshindi mara 5 wa tuzo ya Mchezaji Bora wa FIFA kwa wanawake katika miaka ya  2006, 2007, 2008, 2009 and 2010.

Ronaldo alisema baada ya kuteuliwa: “Ni muhimu tukawa makini maana mbele yetu tuna kazi ya kuangalia maendeleo ya ujenzi wa viwanja, kuchagua mahali ambapo timu ya Taifa itapiga kambi na viwanja mahususi vya mazoezi, na pia kufikia maamuzi muhimu ya kihistoria kama vile kuzindua kauli mbiu ya michuano na Mwanasesera wa Kombe la Dunia la FIFA.”



ratiba ya kombe la dunia 2014 huko brazil leo

Introducing Kiba Square's new hit single "PITA MBELE"

Mhe. Vicky Kamata aibuka na wimbo mpya wa "Moyo wa mtu kichaka" baada ya mikasa yake ya kuugua ghafla kabla ya ndoa yake

0
0
Mh. Vicky Kamata aliwasili Bungeni Dodoma na kama ilivyo ada alipokewa vizuri na kila mbunge aliyekutana nae. 
Wabunge wengi walimpa pole baada ya kuugua siku chache kabla ya ndoa yake na kumtakia kila la kheri, huku wengi wakiamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kua Ndoa yake ipo na itakuwepo siku yoyote Mungu akiamua kulitimiza kusudi lake juu ya Mh. Vicky Kamata.. 
 Wakati wabunge wengi wakimuhurumia na kudhani kua kutofungwa kwa ndoa yake kungemgharimu siku nyingi kurudi katika hali ya kawaida, 
lakini  ilikua ni tofauti kabisa kwa upande wa Mh. Vicky Kamata kwani muda wote alikua na amani na kwamba hakujiskia vibaya kama wengi walivyodhani na ndio maana ilichukua muda mfupi sana na aliweza fika Bungeni na kazi ya kuwatumikia wananchi wake wa Geita na Tanzania kwa ujumla ilianza mara moja na kwamba bado anaamini kilichotokea ni mpango wa Mungu na kwamba Mungu hakosei na anamini Muda si mrefu atafunga ndoa na kila mtu atashuhudia na mkono wa Mungu utasiamama juu ya ndoa yake.
Na anabainisha yote hayo katika wimbo wake mpya "Moyo wa mtu Kichaka" hapo chini. (Picha kwa hisani ya Vicky Kamata blog)

ujerumani leo yaigaragaza Ureno ya Cristian Ronaldo 4-0 kama wamesimama vile.....

0
0
 Na Sultani Kipingo
Ushindi kwa Ujerumani ulitegemewa, ukizingatia Ureno  ni kama kwamba timu ya mtu mmoja – Ronaldo. Lakini ukweli ni kwamba isingekuwa hivyo baada ya Pepe kuoneshwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza. Ila mechi hii haikuwa ni juu ya Pepe, na wala haikuwa ya Miroslav Klose, na hata haikuwa juu ya Cristiano Ronaldo. Mechi yote hii ilikuwa juu ya Thomas Muller.
 Mshambuliaji huyu wa Ujerumani tayari ameshaanza mbio kuelekea kwenye mstari wa mwisho wa mfungaji bora wa michuano, baada ya kupiga mabao matatu (hat trick), na kuendelea kuinyanyasa Ureno na Ronaldo wao muda wote wa mchezo.

Hakika michuano hii ya Kombe la Dunia huko Brazil imekuwa ni ya kuvutia hadi sasa. Na mechi ya Ujerumani na Ureno ilisemwa kuwa mtanange wa mwaka. Na Ilikuwa hivyo kwa Ujerumani kuondoka na ushindi wa mabao 4-0

ANGALIA MECHI ZA KOMBE LA DUNIA LIVE SASA - GHANA VS USA

SUMATRA YAWATAKA ASKARI WA USALAMA BARABARANI KUKAMATA MABASI YANAYOSIMAMA KUCHIMBA DAWA OVYO PORINI

0
0
          Mwanasheria mkuu  wa  SUMATRA Bi Leticia Mutaki
 Bw  Mpina wa Sumatra  makao  makuu  akifafanua  jambo wakati wa semina elekezi  kwa askari wa usalama barabarani
Watenda kazi  wa Sumatra  Iringa  wakiwa na mwanahabari wa TBC Taifa  Iren Mwakalinga  kulia  wakifuatilia  semina  hiyo.

.....................................................
ASKARI  wa usalama barabarani  nchini  wamepewa  rungu  la kuwakamata  madereva  wa mabasi ya abiria na magari mengine  ambayo yatapatikana yakivunja  sheria ya  uchafuzi wa mazingira ya kusimamisha mabasi ili  abiria  waweze kuchimba  dawa porini kinyume na taratibu.
Agizo  hilo  limetolewa  leo wakati  wa  semina  elekezi ya mikakati ya kuthibitia  ajali na uboreshaji wa  huduma ya  usafiri  iliyoandaliwa na Mamlaka ya Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu( SUMATRA)makao  makuu kwa askari wa usalama barabarani  mkoa  wa Iringa.

Mwanasheria mkuu  wa  SUMATRA Bi Leticia Mutaki  alisema  kuwa kisheria  kuchimba  dawa  ovyo ni kosa na  hivyo lazima  askari  wa  usalama barabarani kote  nchini kuhakikisha  wanasimamia  sheria  hiyo  ikiwa ni  pamoja na  kuwakamata  wale  wote  wanao vunja  sheria  hiyo.

Alisema  kuwa  tarayi  SUMATRA  ilitangaza  vituo  vya uchimbaji  dawa kwa barabara zote  nchini na wamili  wa mabasi  hayo  wamepewa nakala  yake  hivyo ni lazima  kuzingatia  sheria  hiyo na kusimamisha basi  eneo   husika ambao wametengewa.
Huku  kwa upande  wake mkuu wa uparesheni barabarani kutoka  Sumatra Person Mpina  alisema  kuwa mbali ya  askari  hao  kuwabana  madereva  ambao  wanavunja  sheria kwa  kuchimba dawa  popote bado askari  hao  wanapaswa kuchukua  hatua kwa madereva wa mabasi ya nje ya nchi ambao  wamekuwa  wakikiuka sheria kwa  kufanya biashara  ya  kupakia abiria  wakiwa ndani ya nchi .

Alisema  kisheria ni  kuwa  mabasi  yaliyosajiliwa kwa namba za usajili za Kenya ,Kampala ,Zambia  na nchi  nyingine wanapaswa  kupatika  abiria wanapoingia katika nchi  husika  na sio  kupakia abiria ndani ya nchi.Kuhusu mabasi ya masafa marefu yaendayo mikoani kuingia ama kutoingia katika  stendi ya  wilaya  alisema kuwa si lazima kwa mabasi ya mikoai kuingia katika  stendi  za wilaya  na kuwa mabasi hayo  yanaruhusiwa  kuingia stendi  za mikoa pekee na si vinginevyo .

"Suala  ambalo  tunaliangalia  hapa na tutalitolea majibu ni  juu ya stendi ya ipi  ya mkoa kati ya Ipogolo na ile ya Iringa mjini ....kwani  kumekuwepo na mkanganyiko mkubwa  wa stendi ya  mkoa katika mkoa  wa Iringa ambapo  wengi  wao  wanatumia stendi zote  mbili ya Ipogolo na Miyomboni kama stendi  kuu"
Japo  alisema abiria anayohaki ya  kushushwa katika stendi ya  mkoa na si vinginevyo na  kuwa kitendo cha madereva wa mabasi  ya mikoani kuwashusha abiria  Ipogolo na  kuwafanya  kukodi Taxi kuja mjini Iringa ni kosa kubwa na iwapo abiria ataamua  kuchukua hatua  za  kisheria lazima dereva  achukuliwe hatua.  

marekani yaifunga Ghana 2-1 kulipiza kisasi cha kutolewa nayo mapema mwaka 2010 afrika kusini

0
0
 Kocha wa Marekani ambaye ni mshambuliaji nyota wa zamani wa Ujerumani Jurgen Klinsmann na wachezaji wake wakishangilia bao la kwanza lililofungwa sekunde ya kwanza na Clint Dempsey pichani chini
Goli la dakika ya kwanza lililowekwa kimiani na Clint Dempsey na lingine la dakika za lala salama la rizevu John Brooks katika mchezo  uliopigwa usiku uliopita mjini Natal, Brazil,  ni magoli ambayo yameiwezesha Marekani kulipiza kisasi dhidi ya Ghana waliowafunga 2-1 na kuwafungasha virago mapema katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 Afrika ya Kusini

Ushindi huo unaiweka Marekani  katika nafasi ya pili ya kundi G nyuma ya Ujerumani. Marekani inafundishwa na mshambuliaji nyota wa zamani wa Ujerumani Jurgen Klinsmann. Ghana na Ureno ya Cristian Ronaldo wanachechemea kwa kila mmoja kutokuwa na pointi hadi sasa.

Likiwekwa kimiani katika sekunde 29 tu za mchezo, bao la Dempsey lilikuwa la tano kwa kufungwa mapema katika historia ya kombe la dunia, katika orodha ya mabao inayoongozwa na Hakan Sukur wa Uturuki aliyefunga dakika ya 11 dhidi ya Korea mwaka 2002.

Wakionekana kupagawa kwa goli hilo la mapema, Ghana walijitahidi kujiweka sawa, lakini kipa Tim Howard wa Marekani alikuwa makini.

Kukiwa kumesalia dakika nane mpira kumalizika, Andrea Ayew alisawazisha kwa bao tamu, pale alipopokea pasi ya nyuma toka kwa Asamoah Gyan, kabla ya kumtungua Howard kwa shuti la nje ya mguu.

Hata hivyo Marekani hawakukatishwa tama, pamoja na kuchezewa nusu uwanja kwa muda mwingi dakika za lala salama, Brooks aliyeingia kipindi cha pili alitingisha nyavu kwa kichwa baada ya majalo tamu ya kona toka kwa Graham Zuzi.
Angalia Hakan Sukur wa Uturuki akiweka mpira kimiani dakika ya 11 na kuweka rekodi ya bao la haraka katika Kombe la Dunia dhidi ya Korea mwaka 2002.

kikao cha Baraza la Mawaziri la Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) jijini nairobi

0
0

Mhe. Dr. Abdalah Kigoda (wa nne kutoka kushoto) akiongoza kikao cha Baraza la Mawaziri wa nchi za ACP. Kikao hicho kimeanza leo Nairobi, Kenya.
Mhe. Janet Mbene Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara (wa pili kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na  Balozi wa Tanzania Kenya Dr. Batilda Burian (wa pili kutoka kushoto) na Balozi wa Tanzania Ubelgiji (wa kwanza kulia). Mhe. Mbene yupo Kenya akihudhuria kikao cha Baraza la Mawaziri la Afrika, Karibiani na Pacific (ACP).
>

Balozi Seif akagua shughuli za uwekezaji na hifadhi ya mazingira katika visiwa vya Bawe na Changuu

0
0
Msimamizi wa mradi wa uhifadhi wa Makobe katika kisiwa cha Changuu Nd.Suleiman Mnemo akitoa maelezo ya uhifadhi wa viumbe hao adimu duniani kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyetembelea kisiwa cha Changuu.
Balozi Seif akikagua baadhi ya majengo ya Hoteli zilizomo ndani ya kisiwa cha Changuu wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uwekezaji katika sekta ya Utalii . Kulia ya Balozi ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Leisure Hoteli inayoendesha mradi wa hoteli Bawe na Changuu Bwana Freddy Tenga na Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh. Said Ali Mbarouk.
Balozi Seif akikagua moja ya vyumba mardadi vilivyopo katika majengo ya Hoteli ya Leisure iliyopo Kisiwa cha Changuu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Kushoto akiwa pamoja na Waziri wa anayesimamia Utalii Mh. Said Ali Mbarouk wakiangalia mazingira ya kuvutia ndani ya eneo la Kisiwa cha Changuu.
Balozi Seif akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Leisure Hoteli na watendaji wa taasisi mbali mbali za Serikali aliyofuatana nao wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za utalii katika Visiwa vya Bawe na Changuu.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akifanya ziara maalum ya kukitembelea Kisiwa cha Bawe kilichopo Magharibi ya Mji wa Zanzibar kuona shughuli za uwekezaji katika sekta ya Utalii. Kulia ya Balozi Seif ni:- Waziri wa Habari Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar Mh. Said Ali Mbarouk.Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

WENGI WALIVYOJITOKEZA KWENYE SEMINA MAALUM YA UONGOZI BORA ILIYOANDALIWA NA MIKONO SPEAKERS

0
0
Nguli wa Maswala ya Uongozi na Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Kimataifa ya Brian Tracy kutoka nchini Marekani,Brian Tracy akikiongoza semina maalum ya uongozi bora iliyoandaliwa na Mikono Speakers,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,Jijini Dar es Salaam.Nguli mwingine alietoa mada kwenye Semina hiyo ni Azim Jamal ambaye ni Mwanzilishi na Mkurugenzi wa Corporate Sufi Worldwide Inc. kampuni inayojihusisha na kusaidia wadau na makampuni kupata muhimili stahiki katika kazi zao.
Sehemu ya Wadau kutoka nyanja mbali mbali wakiwa wamejitokeza kwa wingi kwenye Semina hiyo iliyoongozwa na Manguli wa Maswala ya Uongozi Duniani, Brian Tracy na Azim Jamal,iliyofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya Wadau wakifatilia kwa makini Mada mbali mbali kwenye semina hiyo.

USHAHIDI WA SHAHIDI WA MRAMBA WAFUTWA MAHAKAMANI LEO

0
0
Na Mwene Said, 
wa Globu ya Jamii Mahakamani

MAWAKILI wa utetezi wa Waziri wa Fedha wa zamani, Basil Mramba, wameondoa mahakamani ushahidi wa Kamishna wa zamani wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Felician Busigara, baada ya kuzua mvutano kati ya mawakili wa pande  zote mbili kwamba ushahidi wa shahidi huo ulikuwa wa kitaalamu na siyo dhidi ya mashitaka yaliyopo mahakamani.
Mbali na Mramba, washtakiwa wengine ni Waziri wa Zamani, Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja, wote kwa pamoja wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabara ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7.
Wakili wa utetezi, Peter Swai, alitoa maombi hayo jana mbele ya jopo la mahakimu watatu, likiongozwa na Mwenyekiti, Jaji John Utamwa akisaidiana na Jaji Sam Rumanyika(walioanza kusikiliza kesi hiyo kabla ya kupanda vyeo) na Msajili Saul Kinemela wanaosikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam.
Awali, Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro, alidai shauri linakuja kwa ajili ya kutolewa uamuzi wa mahakama kuhusu ushahidi wa shahidi huyo na kuendelea na utetezi.
Hata hivyo, Swai aliomba kumuondoa shahidi huyo na ushahidi wake aliuotoa na aliomba mahakama kupanga tarehe nyingine ya kusikiliza ushahidi wa utetezi kwa kuwa hawakuwa na shahidi.  Upande wa Jamhuri haukuwa na pingamizi kuhusu maombi hayo ya upande wa utetezi.
Jaji Utamwa alisema shahidi huyo wa pili wa utetezi ushahidi wake unaondolewa na kwamba ombi la kuahirishwa linakubaliwa.
Kesi hiyo iliahirishwa hadi Julai 17 na Agosti 15, mwaka huu itakapotajwa na itaendelea kusikilizwa ushahidi wa utetezi Agosti 21, mwaka huu.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images