Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 471 | 472 | (Page 473) | 474 | 475 | .... | 3272 | newer

  0 0

   Hapa ndipo mwili wa Marehemu George Tyson ulipozikwa mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.George Tyson ambaye alikuwa ni mmoja wa Waongozaji filamu mahiri hapa nchini Tanzania,alifarika kwa ajali ya gari wakati akitokea mkoani Dodoma kikazi akirejea jijini Dar.Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi.Amin.
  Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.
  Ndugu na jamaa mbalimbali wakitoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu George Tysombani kwako,katika kijiji cha Siaya nchini Kenya.
  Baadhi ya Ndgu na Jamaa mbalimbali wakiwa kwenye maombolezo ya mwisho ya mazishi ya marehemu George Tyson mapema leo mchana,nyumbani kwao 
  Misa ya mwisho ya kumuombea marehemu George Tyson nyumbani kwao mapema leo mchana katika kijiji cha Siaya,nchini Kenya.
  Mdau Felix akizungumza jambo na kuwashukuru Watanzania wote na wengineo walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kuhakikisha mpendwa wao,ambaye Mwenyezi Mungu kampenda zaida anaenda kuishi kwenye nyumba yake ya milele.
  Watoto wa marehemu George Tyson wakiwa katika picha ya pamoja.
  Nyumba ya milele ya marehemu George Tyson kabla ya kulazwa.Picha kwa hisani kubwa ya Mdau William Mtitu kutoka kijiji cha Siaya,nchini Kenya.

  0 0

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya unawakaribisha wanachama na wananchi wote kwa ujumla katika banda lake kwenye maonesho ya Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kuanzia tarehe 16 hadi 23/06/2014.

  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya utatoa huduma zifuatazo;-
  Elimu kwa Umma juu ya Huduma za NHIF na CHF/TIKA
  Usajili wa wanachama 
  Upimaji wa afya bure kwa wanachama na wananchi wengine na vipimo vitakavyotolewa ni;-
  1.Kisukari,
  2.Shinikizo la damu, 
  3.Hali Lishe
  4.Saratani ya matiti.
  5.Ushauri wa Kitaalam wa namna ya kuepukana na maradhi yasiyoambukiza.
  WOTE MNAKARIBISHWA


  0 0

  Mjumbe wa Kamati kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif akimkabidhi kadi mwanachama mpya wa CCM Shina nambari 23 la Tawi la CCM Fuoni Bibi Faiza Chande Ameir.Kushoto ya Balozi ni Mwenyekiti wa Shina Nambari 23 la Tawi la CCM Fuoni Nd. Daudi Khamis, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Magharibi Nd. Yussuf Mohd Yussuf na Katibu wa CCM Mkoa huo Aziza Ramadhan Mapuri.
  Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Mwanakwerekwe Ndugu Khamis Juma Msonge akimkaguza Mjumbe wa Kamat Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi kuangalia jengo la Ofisi ya Jimbo hilo ambayo iko katika hatua za mwisho za ujenzi wake. Balozi Seif akiwa mlezi wa Mkoa wa Magharibi Kichama alikuwa katika ziara ya kichama ndani ya Wilaya ya Dimani. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba mafanikio ya Uongozi ndani ya Mashina ya Chama cha Mapinduzi ni nguzo pekee inayosaidia uimarishaji wa chama hicho katika ngazi zote.

  Alisema hayo wakati akizungumza na wanachama wa Shina nambari 23 la CCM Tawi la Fuoni baada ya kugawa kadi kwa wanachama wapya 15 wa CCM wa Shina hilo akiwa katika ziara ya kutembelea Wilaya ya Dimani Kichama akiwa mlezi wa Mkoa wa Magharibi.

  Balozi Seif alisema kwa kuwa chama imara ni kile kinachoungwa mkono na watu walio wengi popote pale aliwapongeza Vijana hao wa shina nambari 23 kwa uamuzi wao wa busara wa kujiunga na Chama cha Mapinduzi.

  Alisema nguvu ya Chama ni Vijana ambao pia ni tegemeo kwa Taifa. Hivyo aliwataka waendelee kushikamana pamoja ili kuongeza uzalendo wao katika kulitumikia Taifa lao.

  Katika kuunga mkono juhudi za wanachama hao wa CCM Shina nambari 23 Fuoni Balozi Seif aliahidi kuwapatia seti ya TV Pamoja na King’amuzi chake ili wapate fursa ya kupata habari, burdani pamoja na kuona mashindano ya kombe la dunia yanayoendelea hivi sasa Nchini Brazil.

  Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa akiwa pia ni mlezi wa Mkoa wa Magharibi aliitembelea Ofisi ya CCM Jimbo la Mwanakwerekwe kukagua hatua iliyofikia ya ujenzi jengo lao na kuwapongeza wana CCM hao kwa uamuzi wao wa kujenga Ofisi mpya ya Jimbo hilo inayokwenda na wakati.

  0 0

  JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  OFISI YA RAIS,

  MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA


  RATIBA YA UFUNGUZI WA MAADHIMISHO WIKI YA UTUMISHI WA UMMA, VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM, TAREHE 16 JUNI 2014


  MUDA

  TUKIO

  MHUSIKA

  02.00-03.30

  Burudani

  MC

  03.30-04.00

  Waalikwa Kuingia Uwanjani

  MC/Wageni Waalikwa

  04.00-04.15

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Kuingia Uwanjani

  MC/ Kamati ya Mapokezi

  04.15-04.30

  Mgeni Rasmi Mhe. Waziri wa Nchi, OR MUU Celina O. Kombani (Mb) kuwasili

  Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

  04.30-05.15

  Mgeni Rasmi Kupokea Maandamano

  MC

  05.15-05.30

  Burudani

  MC

  05.30-05.35

  Kumkaribisha Mgeni Rasmi Mhe. Waziri wa Nchi, OR MUU Celina O. Kombani (Mb).

  MC/Katibu Mkuu Utumishi

  05.35-06.00

  Mgeni Rasmi Kufungua Maadhimisho ya Wiki ya Utumishi wa Umma 2014

  MC/ Mhe. Waziri wa Nchi, OR MUU Celina O. Kombani (Mb).

  06.00-06.05

  Kutoa Neno la shukrani kwa Mgeni rasmi

  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma

  06.05-06.20

  Burudani

  MC/Kikundi cha Ngoma

  06.20 na kuendelea

  Mgeni rasmi kutembelea mabanda ya Maonesho

  MC/ Katibu Mkuu Utumishi

  06.20 -06.50

  Burudani

  MC/Kikundi
  0 0

   Hali iko shwari jioni hii katika shopping Mall ya Mlimani City jijini Dar es salaam baada ya wamiliki wapya wa iliyokuwa Shoprite Stores Nakumatt kuamua kufunga seli iliyozua zogo hata ikabidi leo mchana FFU waitwe kutuliza ghasia. Matangazo yanajieleza nini kitaendelea Jumatatu.


  0 0

  Siku ya zoezi la usaili wa nafasi ya Mkaguzi Msaidizi wa Uhamiaji lililofanywa na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi tarehe Ijumaa Juni 13, 2014  katika Uwanja mpya wa Taifa, Dar es Salaam.


  0 0

  .
  DSC_0034
  Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa “Has T” akiwatambulisha wasanii watakaotoa burudani leo kwenye ufunguzi wa Tamasha la 17 la filamu la nchi za Majahazi ZIFF kwenye mkutano mfupi na waandishi wa habari (hawapo pichani).
  DSC_0042
  DJ maarufu Kahlil Jacobs-Fantauzzi kutoka Puerto Rico(kushoto) akiwaeleza waandishi wa habari (hawapo pichani) namna atakavyosugua sahani za muziki usiku wa leo. Wengine ni wanamuziki wa kundi la BODY, MIND & SOUL kutoka Malawi.
  DSC_0075
  Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuwatambulisha wasanii watakaotoa burudani kwenye ufunguzi wa tamasha hilo.

  0 0

   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akipokea ua kutoka kwa Mtoto Mosi Kimosa ,7, anayesoma darasa la pili katika shule ya msingi Msimba iliyoko Kigoma Vijijini na Trisa Luziga,6, anayesoma darasa la kwanza mara baada ya Mama Salma kutua katika uwanja wa ndege wa Kigoma
   Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Mheshimiwa Issa Machibya akimpokea rasmi Mke wa Rais Mama Salma Kikwete mara baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma Mama Salma yuko mkoani humo kuhudhuria maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani Kigoma leo
   Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza ngoma za utamaduni zilizokuwa zikichezwa na akinamama wa Kigoma wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Kigoma kushiriki maadhimisho ya siku ya uchangiaji damu salama duniani inayoadhimishwa kitaifa mkoani humo leo. Picha na John Lukuwi

  0 0

  Na Francis Dande
  MAMIA ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaamna vitongoji vyake, wakiwemo wanamichezo, leo wamejitokeza katika mazishi ya bondia wa zamani wa masumbwi ya kulipwa, Iraq Hudu (49).
  Marehemu Hudu, maarufu kama ‘Kimbunga’, aliyefariki dunia Ijumaa mjini Dar es Salaam, amezikwa leo  majira ya saa 10:00 alasiri katika makaburi ya Kisutu, jijini Dar es Salaam.

  Bondia huyo aliyewahi kutamba vilivyo katika ulingo wa masumbwi, alifariki alfajiri ya Ijumaa katika hospitali ya Hindu Mandal, akisumbuliwa na tatizo la ini na figo kutofanya kazi.
  Hudu alizaliwa mwaka 1965 Ujiji Kigoma, na kupata elimu ya msingi mkoani humo na baadae kuja Dar es Salaam ambako alipata elimu ya sekondari. Baada ya hapo, alijiingiza katika masumbwi katika miaka ya 1990 hadi miaka ya 2000, alipoacha. Marehemu ameacha watoto watatu.
   Mwili wa Iraq Hudu ukishushwa katika gari maalumu wakati wa mazishi yake katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.
  Baadhi wa waombolezaji wakiwa wamebeba jenza lililokuwa na mwili wa bondia wa zamani wa ngumi za kulipwa Iraq Hudu ‘Kimbunga’ wakati wa mazishi yake yaliyofanyika jana katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. 
  Mazishi ya bondia Iraq Hudu yakifanika leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri Mkuu Mizengo Pinda wakiwa katika picha ya pamoja na wasanii mbalimbali wakati wa Tamasha la Uzalendo na uzinduzi wa Video ya Wimbo Maalum wa Mika 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zinazoendelea hivi sasa katika uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma jioni hii. Picha na Freddy Maro
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya wasanii walioshiriki katika tamasha la Uzalendi na uzinduzi wa Video ya wimbo Maalum wa Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Jamhuri mjini dodoma leo jioni.

  0 0

   
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  Covenant  Bi.Sabetha Mwambenja  akitoa mfano wa  beiskali   wakati alipokuwa akiongea na kikundi cha wafugaji Ng’ombe  wa kisasa cha Kata ya Somangila Kigamboni jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mradi huo.Benki hiyo inategemea kutoa  mkopo kwa kikundi hicho ili waweze kuendeleza ufugaji huo. Kulia ni Mratibu wa Wafugaji wa Ng’ombe  wa Kata ya hiyo  Getruda Mpelembe  na katikati ni  mtunza Hazina wa Kikundi hicho Jumanne Hussen na Kushoto ni Mwenyekiti  Taifa Wajasiriamali Dk.Dauda Salmin.
   Mratibu wa kikundi cha wafugaji wa Ng’ombe  wa kisasa Kata ya Somangila  Kigamboni jijini Dar es Salaam, Getruda Mpelembe (kulia) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya  Covenant  Bi,Sabetha Mwambenja,Baada ya kuongea na kikundi hicho kuhusiana na maswala ya mradi wa ufugaji wa ng’ombe wa maziwa  wa kisasa  ambapo kikundi hicho kitanufaika na mkopo kutoka benki ya Covenant kwa ajili ya kuendeleza mradi huo wa ufugaji.   
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya wanawake ya Covenant  Bi,Sabetha Mwambenja  akisisitiza jambo  wakati alipokuwa akiongea na kikundi cha wafugaji wa Ng’ombe wa kisasa cha  Kata ya Somangila kiilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kuhusiana  na mradi wa ufugaji wa kisasa wa  ng’ombe wa maziwa   unaovihusisha vikundi vitatu  vya kata  hiyo ambapo wafugaji hao watapata mkopo wa kuendeleza mradi huo kutoka Covenant  benki.
   
   Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya wanawake ya Covenant Bi. Sabetha Mwambenja  akitoa mfano wa spoko za beiskali kwa kikundi cha wafugaji zaidi ya 45( hawapo pichani)wa Kata ya Somangila kilichopo Kigamboni jijini Dar es Salaam, kuhusiana na mradi wa ufugaji wa Ng’ombe wa kisasa wa Maziwa.Benki hiyo inategemea kutoa mkopo kwa kikundi hicho ilikiweze kuendeleza ufugaji huo. Kulia ni  mtunza Hazina  wa Kikundi hicho Jumanne Hussen.


  0 0
 • 06/15/14--10:32: shukurani
 • Familia ya Prof. Cuthbert Z. M. Kimambo wa Chuo Kikuu cha Dar e Salaam inatoa shukurani za dhati kwa wale wote walioshirikiana nasi kwa kwa maombi, kwa hali na mali, na kutufariji kwa njia moja au nyingine katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na Mtoto wetu Mpendwa Samwel Cuthbert Kimambo kwa ajali ya gari iliyotokea tarehe 1 Juni 2014. 
  Shukurani ziwaendee Uongozi na wafanyakazi wa Benki ya CRDB, Uongozi na wafanyakazi wote wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wanafunzi wa Chuo cha Kampasi cha Uhandisi na Teknolojia - UDSM, Uongozi na wafanyakazi wa Small Entrepreneurs Loan Facility (SELF) Project, Uongozi na washarika wa Kanisa la CCT Chuo Kikuu Dar es Salaam na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Arusha Mjini, Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Kuu ya Jeshi Lugalo, Jeshi la Polisi Idara ya Usalama Barabarani, Ndugu, Jamaa, marafiki na majirani wote wa Dar es Salaam, Arusha, Kilimanjaro, na kwingineko ndani na nje ya nchi.

  Kwa sababu hiyo ninyi nanyi jiwekeni tayari; kwa kuwa katika saa msiyoijua Mwana wa Adamu yuaja.” Mathayo Mtakatifu Sura 24, Mstari wa 44.

  0 0

  Na Allan Ntana, Sikonge 
   MWENYEKITI wa halmashauri ya wilaya ya Sikonge mkoani Tabora Robert Kamoga amepongeza jitihada zinazofanywa na mradi wa PROSPER katika kutokomeza utumikishwaji watoto katika shughuli za kilimo huku akisifu utaratibu wa kurudishwa shule watoto wote waliokosa nafasi hiyo. 
   Kamoga ametoa pongezi hizo alipokuwa akizungumza na mamia ya wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya siku ya kupinga utumikishwaji watoto iliyofanyika kimkoa katika kijiji cha Udongo kata ya Ipole wilaya ya Sikonge mkoani Tabora.
   Alisema mradi huu unastahili kupongezwa kwa sababu mkoa wa Tabora ni miongoni mwa mikoa 5 inayoongoza kwa umaskini hapa nchini na asilimia kubwa ya wananchi wake ni maskini hali inayochangia watoto wengi kutumikishwa katika kazi ngumu kwa ujira mdogo. 
   Mradi huu ni mkombozi kwa watoto wadogo kwa sababu wazazi wengi walikuwa hawawapeleki shule kwa kisingizio cha umaskini na badala yake wanawapeleka shambani wakawasaidie kulima tumbaku au kuchunga ng’ombe, alisema. 
   Kamoga aliongeza kuwa utumikishwaji watoto ni hatari sana katika ustawi wao kwa sababu huwakosesha fursa mbalimbali katika makuzi yao ikiwemo haki ya kupata elimu na malezi bora. "Wataalamu wanasema ukimnyima mtoto haki zake anaathirika kisaikolojia mpaka ukubwani mwake na watoto ndio taifa la leo na kesho, hivyo wanapaswa kulindwa, kutunzwa na kupendwa, kwa kufanya hivyo tutakuwa tunajenga taifa kuanzia ngazi ya familia mpaka taifa, alifafanua. 
   Aidha alisema sheria ya mtoto namba 21 ya mwaka 2009 kifungu cha 78 (1) inakataza mtu yeyote kuajiri au kutumikisha watoto katika shughuli yoyote ile inayowaadhili watoto hao, hivyo kumtumikisha ni kwenda kinyume na sheria za nchi anapaswa kushitakiwa mara moja. 
   Kamoga alisema PROSPER imefanikiwa kuwarudisha shuleni watoto wengi sana waliokosa elimu katika wilaya za Sikonge na Urambo na kuwagharamiwa masomo yao kuanzia darasa la kwanza mpaka la saba huku vikundi mbalimbali vya vijana na akina mama vikipewa mafunzo ya ujasiriamali, kilimo, ufugaji na mikopo kwa lengo la kuwawezesha kiuchumi. 
   Mradi huu umefanya kazi nzuri sana katika vijiji 20 vilivyoko katika wilaya hizo, Mkurugenzi (Bahati Nzunda) naomba uangalie uwezekano wa kupanua huduma hii katika vijiji vingine kwani wapo watoto wengi sana walioathiriwa na utumikishwaji huu, aliongeza. 
   Ili kudhibiti vitendo hivyo, Kamoga aliagiza waalimu wakuu wa shule zote za msingi katika wilaya hiyo kuhakikisha wanafuatilia mahudhurio ya watoto shuleni ili kubaini watoto wasiofika shule ili wazazi wao wakamatwe mara moja na kutozwa faini. 
   Sambamba na hilo aliagiza watendaji wote wa halmashauri kuanzia ngazi ya vijiji na kata kuwachukulia hatua kali watu wote watakaobainika kujihusisha na vitendo vya utumikishwaji watoto katika maeneo yao huku akiomba asasi zingine kuunga mkono jitihada hizo.
   BW.ROBERT KAMOGA (WA KWANZA KULIA) MWENYEKITI WA HALMASHAURI SIKONGE AKIWA NA MKURUGENZI WA MRADI WA PROSPER BAHATI NZUNDA (WA KWANZA KUSHOTO) AKIFUATIWA NA DR MTIBA NA MWENYEKITI HALMASHAURI YA WILAYA URAMBO ADAM MALUNKWI.JPG
  ROBERT KAMOGA AKIHUTUBIA UMATI WA WANANCHI WA VIJIJI VYA UDONGO NA MAKAZI KATIKA KATA YA IPOLE WILAYANI SIKONGE MKOANI TABORA KATIKA MAADHISHO YA SIKU YA KUPINGA UTUMIKISHWAJI WATOTO KATIKA MASHAMBA YA TUMBAKU.JPG

  0 0

  Na Hassan Hamad (OMKR)
  Chama Cha Wananchi CUF kinaendelea na maandalizi yake kwa ajili ya Mkutano Mkuu Taifa utakaoambatana na uchaguzi wa viongozi wakuu wa Kitaifa wa Chama hicho. Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu za Chama hicho Buguruni Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad amesema maandalizi yote ya msingi kwa ajili ya mkutano huo yamekamilika. 
  Maalim Seif amesema katika mkutano huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 23 hadi 27 mwezi huu, wajumbe wa mkutano watapokea taarifa mbali mbali za kazi za chama kuanzia mwaka 2009 hadi 2014 ambapo pia watapata fursa ya kuzijadili. 
  Amebainisha kazi nyengine za mkutano huo kuwa ni pamoja na kuwachagua viongozi wakuu wa kitaifa wa chama hicho ambao ni Mwenyekiti wa Taifa, Makamu Mwenyekiti na Katibu Mkuu. Viongozi wengine watakaochaguliwa katika mkutano huo ni wajumbe wa Baraza Kuu la uongozi taifa pamoja na wajumbe wa viti maalum vya wanawake. 
  Maalim Seif amesema kwa sasa Chama hicho kinaendelea na vikao mbali mbali kikiwemo cha kamati tendaji, ikiwa ni maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mkutano huo ambapo wajumbe wote wa mkutano kutoka Tanzania Bara na Zanzibar watakuwa wamewasili ifikapo tarehe 22/06/2014 kwa ajili ya mkutano huo wa kitaifa. 
  Wakati huo huo Mwenyekiti wa Chama hicho Taifa Prof. Ibrahim Lipumba ameichambua bajeti ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2014/2015, na kusema kuwa ina mapungufu mengi. Prof. Lipumba amewaambia waandishi wa Habari kuwa bajeti ikiwa nyenzo muhimu ya sera za serikali, inapaswa kuandaliwa kwa umakini ili iweze kutekelezwa kwa mujibu wa mahitaji yaliyopo. 
  Amesema ni jambo la kushangaza kuona bajeti inayoidhinishwa katika bunge kila mwaka haitekelezwi kama ilivyopangwa, na badala yake kunakuwa na tofauti kubwa kati ya bajeti inayoaishinishwa na ile inayopatikana kwa matumizi ya mwaka. 
  Amesema baadhi ya Wizara za Serikali zimekuwa zikipata fedha chini ya asilimia 50 ya matumizi yaliyopangwa, na kusababisha miradi mingi ya maendeleo kuzorota kutokana na ukosefu wa fedha. Aidha amesema bajeti hiyo bado inabakia kuwa tegemezi kutokana na mapato ya ndani kuwa madogo ikilinganishwa na matumizi ya kawaida ya serikali. 
  Prof. Lipumba amefahamisha kuwa serikali inapaswa kujipanga ipasavyo, ili kuepuka utegemezi kwa bajeti ya maendeleo ambapo amesema imekuwa ikitegemea zaidi misaada na mikopo kutoka nchi za nje na mashirika ya Kimataifa.
   Ametaja mambo ya msingi yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa utayarishaji wa bajeti kuwa ni pamoja na bajeti kuweza kufikia malengo ya uchumi mpana, ukuaji wa pato la taifa, mfumko wa bei, akiba ya fedha za kigeni pamoja na thamani sarafu. 
  Mambo mengine aliyobainisha ni ni kutaka matumizi yagawiwe kulingana na malengo ya sera ya taifa pamoja na kujenga mazingira ya utekelezaji mzuri wa bajeti. 
  Katika hatua nyingine Prof. Lipumba amesema bado bajeti hiyo haijaweka bayana juu ya ukuwaji wa deni la Taifa ambalo amesema limekuwa likikuwa kwa asilimia 20 kwa mwaka wakati ukuaji wa uchumi ni asilimia 7 kwa mwaka. 
  Amesema deni hilo ni hatari kwa Taifa na linapaswa kuwekewa mikakati imara ili lisiendelee kuongezeka na kudumaza pato la wananchi. Amesema licha ya serikali kusema bajeti imelenga kupunguza gharama za maisha kwa wananchi, lakini wananchi walio wengi bado wanaona kuwa gharama za maisha zinaendelea kupanda kwa kasi kubwa kuliko takwimu zinazotolewa na serikali.
   Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi kuu za Chama hicho Buguruni Dar es Salaam.
   Katibu Mkuu wa CUF Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akitoa taarifa ya Chama kwa waandishi wa habari kuhusiana na mkutano mkuu wa Chama hicho unatarajiwa kuanza rasmi tarehe 23/06/2014. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF Zanzibar, Hamad Massoud Hamad.
  Baadhi ya viongozi wakuu wa CUF wakielekea ukumbi wa mikutano Buguruni Dar es Salaam kwa ajili ya kuzungumza na waandishi wa habari. Picha na Salmin Said, OMKR

  0 0

   Balozi wa Marekani hapa nchini Bw. Mark Childress (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa Helkopta kutoka kwa Taasisi ya Howard G. Foundation inayomilikiwa na mfanyabiashara mashuhuri nchini Marekani Bw. Warren Buffet  (hayupo pichani) kulia ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu.Hafla hiyo imefanyika jana jijini Dar es Salaam.
   Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt.Idd Mfunda (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa Kampuni ya Helkopta Charter (EA) Ltd Bw. Peter Achammer wakitiliana saini katika hati za makabidhiano ya Helkopta moja iliyotolewa kama msaada na Taasisi ya Howard G. Buffet Foundation ya nchini Marekani.Wanaoshuhudia zoezi hilo ni Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyarandu (aliyesimama kushoto) na Balozi wa Marekani hapa nchini Mark Childress
   Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akionyesha ufunguo wa Helkopta mara baada ya kukabidhiwa na Afisa Mtendaji Mkuu & Rubani Mkuu wa Kampuni ya Helcopter Charter (EA), Peter Achammer kwa niaba ya Mfuko wa Howard G. Buffet ambapo ni moja ya utekelezaji wa ahadi za mmiliki wa Mfuko huo alizozitoka kwa Rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara katika Mbuga za wanyama hapa nchini hivi karibuni.Wa pili kulia ni Balozi wa Marekani nchini, Mark Childress naWaziri Kivuli wa Maliasili na Utalii, Mchungaji Peter Msigwa .
   Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa amepanda Helkopta ambayo alikabidhiwa kama msaada kutoka Mfuko wa Howard G. Buffet kwa ajili ya kusaidia juhudi za Serikali katika kupambana na ujangili.
  Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiteta jambo na  Wawakilishi wa Bunge .katika hafla ya makabidhiano ya msaada wa Helkopta kwa ajili kupambana na ujangili nchini Mh. James Lembeli ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Maliasili na Mazingira (katikati) na Mhe. Mch. Peter Msigwa Waziri Kivuli wa Wizara ya Maliasili na Utalii.
   Meneja Mipango na Mikakati wa Howard G. Buffet Foundation Tanzania Chapter Bi. Ellen Mutalemwa akitoa rai wakati wa hafla ya kukabidhi Helkopta moja ambayo ni kati ya ahadi zilizotolewa na Mwenyekiti wa Mfuko huo alipomtembelea Rais Kikwete hivi karibuni. Helkopta hiyo imetolewa ili kusaidi juhudi za Serikali katika kupambana na ujangali katika hifadhi za Taifa.

  0 0

    Mkuu wa Chuo cha Ufundi Arusha,Dk Richard Massika kulia)akiwa na wafanyakazi wenzake kwenye mazoezi ya viungo katika viwanja vya chuo hicho.
  J.Makamu Mkuu wa Chuo,Utawala na Fedha,Dk Erick Mgaya akishangilia baada ya timu yake(Idara ya Umeme)kutwaa ubingwa wa mpira wa miguu dhidi ya AutoMech.


  0 0

   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipokewa na wenyeji wake wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Bolivia juzi Juni 13, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Nchi za G 77 na China, yanayofanyika leo Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Meya wa Jiji la Santa Cruz,  Percy Fernandez, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Bolivia juzi Juni 13, 2014 kwa ajili ya kuhudhuria maadhimisho ya miaka 50 ya Nchi za G 77 na China, yanayofanyika leo Juni 15, 2014, jijini Santa Cruz, Bolivia. Kushoto ni Mama Zakhia Bilal.
   
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Rais wa Bolivia, Evo Morales, walipokutana kabla ya kuhudhuria maadhimisho ya Miaka 50 ya nchi za G77 na China yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia, jana Juni 14, 2014. Katikati ni Mkalimani wa Rais wa Bolivia. Katika mazungumzo hayo Rais Morales aliishukuru Tanzania kushiriki katika maadhimisho haya na akasisitiza kuwa uhusiano wa nchi za G77 unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal akifafanua kuwa Tanzania inatambua na kuheshimu jitihada zinazofanywa na umoja huo na kwamba ni kipindi kizuri kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari kuhusu kutanua fursa za kukuza uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi hizo
   Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na mwenyeji wake Rais wa Bolivia, Evo Morales, baada ya mazungumzo yao yalioyofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia
  Makamu wa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiagana na Mwenyeji wake Rais Evo Morales, Rais wa Bolivia baada ya kufanya mazungumzo saa chache kabla ya kuhudhuria Maadhimisho ya Miaka 50 ya nchi za G77 na China yanayofanyika jijini Santa Cruz, Bolivia. 
  Katika mazungumzo hayo Rais Morales aliishukuru Tanzania kushiriki katika maadhimisho haya na akasisitiza kuwa uhusiano wa nchi za G77 unapaswa kuenziwa huku Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal akifafanua kuwa Tanzania ni inatambua na kuheshimu jitihada zinazofanywa na umoja huo na kwamba ni kipindi kizuri kuadhimisha miaka 50 kwa kutafakari kuhusu kutanua fursa za kukuza uchumi ili kuendeleza wananchi wa nchi hizo. Picha na OMR

  0 0
 • 06/15/14--11:04: Article 17


 • 0 0

   Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akiwasili kwenye ukumbi wa Martin's Crosswinds uliopo Greenbelt, Maryland kwenye usiku wa Wanawake wa Tanzania ulioratibiwa na kikundi cha wakinamama wa tano chenye maskani yao DMV kinachobeba jina la Tano ladies na kuufanya usiku huo kuwa wa aina yake na kuweka historia ya wanawake nchini Marekani kwa kusahau tofauti zao, kuwaacha wapendwa wao nyumbani na kuwa kitu kimoja kwa kujumuika pamoja kuelimishana juu ya kupendana na kuungana mkono kila mwenzao anapofanya jambo jema.  
  Mwenyekiti wa Tano Ladies Asha Hariz akitoa shukurani kwa wanawake wote na kuwashukuru kuwaunga mkono na kukubali wanachofanya.
  Asha Nyang;anyi mmoja wa Tano Ladies akiwashukuru wadhamini.
  Tano Ladies katika picha ya pamoja na Mhe. Balozi  0 0


  Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
  JAMAL Malinzi, rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amesema kwamba kuanzia sasa viingilio vya mechi za timu ya taifa, Taifa Stars kwa maeneo yasiyo ya VIP vitakuwa vya bei nafuu ili kutoa fursa kwa watu wengi kwenda kuishangilia timu hiyo.
  Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mjini Dar es Salaam, Malinzi amesema kwamba wamejifunza hilo kutoka kwa Zimbabwe ambao kwenye mechi za timu ya taifa viingilio vya eneo la mzunguko huwa vya chini mno.

  “Tumeona Zimbabwe, walifanya kiingilio cha mechi yetu na wao dola moja ya Kimarekani, ambayo ni chini ya shilingi 2,000 ya Tanzania, na watu walifurika uwanjani,”alisema.

  Malinzi amesema mashabiki wa soka watarajie viingilio nafuu mno kuanzia sasa katika mechi za timu ya taifa na amewataka wawe wanajitokeza kwa wingi bila kujali mvua wala jua kwenda kuisapoti timu hiyo.
  Taifa Stars inatarajiwa kuondoka nchini wiki ijayo kwenda Botswana kuweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na mchezo dhidi ya Msumbiji kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani Morocco.
  Wachezaji wote wa Taifa Stars waliruhusiwa kurejea makwao jana kwa ajili ya kujiandaa na safari hiyo na watakutana tena kesho.
  Stars inayofundishwa na Mholanzi, Mart Nooij itaondoka nchini Juni 27 kwenda Gaborone, ambako itaweka kambi ya mazoezi hadi Julai 7 itakaporejea nchini.  
  Taifa Stars itamenyana na Msumbiji ‘Mambas’ katika hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco baada ya kuitoa Zimbabwe juzi kwa jumla ya mabao 3-2, ikianza kwa ushindi wa 1-0  nyumbani na kumaliza kwa sare ya 2-2 juzi mjini hapa.
  Mechi yake kwanza itachezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kati ya Julai 19 na 20 mwaka huu, wakati mechi ya marudiano itafanyika Msumbiji kati ya Agosti 2 na 3 mwaka huu. 
  Stars pia inatarajiwa kuwa na mchezo wa kujipima nguvu na Uganda kabla ya kumenyana na Msumbiji.

older | 1 | .... | 471 | 472 | (Page 473) | 474 | 475 | .... | 3272 | newer