Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live

Dkt. Shein afungua Madrasa Qamaria Matemwe,Mkoa wa Kaskazini Unguja

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein (kushoto) akisalimiana na Sheikh Yakob Mfadhili wa Madrasa Qamaria wakati alipowasili katika Kijiji cha Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja leo kuifungua rasmin Madrasa hiyo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein,akifungua pazia kuashiri ufunguzi wa Madrasa Qamaria katika kijiji cha Kijini Matemwe Kaskazini Unguja leo,madrasa hito iliyojengwa na Jumuiya ya ALFATAH ambapo itawanufaisha watoto wa kijiji hicho kujipatia Elimu ya Qurani na hadith mbali mbali,(wa kwanza kulia) mwenyekiti wa CCM Mkoa Kaskazini Mhe,Haji Juma Haji na Mkuu wa Mkoa huo Mhe, Pembe Juma Pembe .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein,akipata maelezo kutoka kwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Alfatah Rashid Salim,ambayo imejenga madrasa Qamaria katika kijiji cha Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakati alipotembelea vyumba vya Madrsa hiyo baada ya kuifungua rasmin leo
Baadhi ya wanafunzi wa Madrasa Qamaria ya Kijiji cha Kijini Matemwe Mkoa wa Kaskazini Unguja,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa nasaha zake kwa wananchi na wanafunzi hao ,katika suala zima la Elimu ya Quran,baada ya kuifungua rasmi madrasa Qamaria iliyojengwa kwa usimamizi wa Jumuiya ya ALFATAH,ufunguzi huo ulifanyika leo.
Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Kabi,alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein (kushoto) kuzungumza na wananchi na wanafunzi wa madrasa Qamaria ya Kijiji cha Kijini Matemwe Mkoa wa kaskazini Unguja baada ya kuifungua leo,(kutoka kulia) Mfadhili wa Ujenzi Sheikh Yakub ,Katibu wa Mufti Sheikh Fadhil Suleiman Soraga na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Unguja Mhe,Haji Juma Haji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt .Ali Mohamed Shein (wa tatu kushoto) pamoja na Viongozi wengine na Mfadhili ujenzi wa Madrasa Qamaria Sheikh Yakub (kulia) wakiitikia Dua iliyoombwa baada ya kumalizika kwa hafla ya ufunguzi wa madrasa Qamaria katika Kijiji cha Kijini Matemwe Mkoa wa kaskazini Unguja leo.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]

WATOTO WALIVYOJITOA KUKIPIGA SOP SOP KITUO CHA DALADALA CHA UBUNGO JIJINI DAR

0
0
Children who are housed at the SOS Children’s Villages at Dar es Salaam tie refuse bags after participated of cleaning the Ubungo Commuter buses shelter located along Morogoro Road in Dar es Salaam on Saturday last week as part of their program to educate the community on the environment cleaning awareness.

SPIKA MAKINDA AFUNGUA GYM YA MAZOEZI YA BUNGE KWA AJILI YA WABUNGE

0
0
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Gym ya Mazoezi katika Viwanja vya Bunge. Gym hiyo itatumiwa na Wabunge , Wafanyakazi pamoja na Wananchi wa Nje watakaopenda kufanya mazoezi kwa lengo la kuboresha afya zao za Miili yao. Pembeni ni Mkurugenzi wa Gym hiyo Ndg. Omar Ige.
Muonekano wa Jengo litakalo na GYM ya Bunge kwa nje katika viawanja vya Bunge.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiangalia baadhi ya wananchi waliofika kufanya mazoezi katika GYM ya Bunge baada ya kuizindua rasmi katika viawanja vya Bunge. Kulia ni mfanyakazi wa GYM hiyo Ndg. Ekarist Liheta akitoa maelezo kwa Mhe. Spika.
pika akipima uzito kabla ya kujisajiri katika GYM hiyo.
Mkurugenzi wa GYM hiyo Ndg. Omar Ige akimkabidhi Mhe. Spika vifaa vya mazoezi tayari kwa kuanza mazoezi.
Meneja wa GYM hiyo Bi. Suzan akitoa neno la Shukrani kwa uongozi wa Bunge pamoja na Spika baada ya Ufunguzi rasmi. Picha kwa hisani ya Bunge

PROF. MAGHEMBE AKUTANA NA UJUMBE WA SERIKALI YA SINGAPORE

0
0
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe leo mchana amekutana na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Singapore, Masagos Zulkifli kuzungumzia Maendeleo ya Sekta ya Maji nchini ofisini kwake Ubungo Maji Dar es Salaam.

“Tunatekeleza miradi mikubwa mitatu Nchini, mmojawapo ni ujenzi wa Bwawa kubwa la Kidunda, mkoani Morogoro ambalo litasaidia kuongeza upatikanaji wa maji jijini Dar es Salaam kwa miaka 20 ijayo,” alisema Waziri Maghembe.

“Hivyo, tunahitaji Ushirikiano wa Taasisi za Kibinafsi na Kiserikali kwa Maendeleo ya Kiuchumi Nchini (PPP) katika kuhakikisha tunatekeleza miradi ya maji na kuinua sekta hii, maana kutegemea bajeti ya Serikali pekee haitoshelezi kufikia malengo makubwa tuliyojiwekea kama Wizara.” alisisitiza Prof. Maghembe.

Pia, Waziri Maghembe alizungumzia changamoto tatu kubwa zinazoikabili Wizara yake katika kuhakikisha maji yanafika katika kila nyumba kwa wakazi karibu milioni 3.3 wa Dar es Salaam, ujenzi wa miundombinu ya majitaka na upotevu wa maji na kusisitiza ni jambo la kupatiwa ufumbuzi haraka iwezekanavyo.

Katika mazungumzo hayo, Waziri Maghembe alimuomba mgeni wake kuhakikisha nchi yake inawekeza katika Sekta ya Maji ambayo ni muhimu katika nchi hii, na ikizingatiwa eneo la Kusini mwa Tanzania linategemea kushamiri kwa viwanda na wingi wa watu baada ya kugundulika gesi na hivyo uhitaji wa maji utaongezeka kwa kasi.

Aidha, Waziri wa Singapore, Masagos Zulkifli alisema watahakikisha wanawekeza na kuleta maendeleo katika sekta ya maji na kutumia wataalamu na uzoefu walionao kutoka nchi yao. Huku akisisitiza kufanikisha zoezi la uunganishaji mabomba kwa kila nyumba, kujenga miundombinu ya majitaka nchi nzima na upotevu wa maji.

Waziri huyo wa Singapore aliambatana na ujumbe mkubwa uliojumuisha wataalamu mbalimbali wa sekta tofauti nchini humo, ambao wapo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe akiwa na mgeni wake, Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Singapore, Masagos Zulkifli wakielekea kwenye chumba cha mkutano.
Baadhi ya wataalam waliombatana na ugeni kutoka Singapore uliomtembelea Prof. Maghembe.
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe (katikati) akiwa na, Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Singapore, Masagos Zulkifli (kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Inj. Bashir Mrindoko (kulia).
Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Singapore, Masagos Zulkifli, wakibadilishana zawadi.

ZANZIBAR PETROLEUM LTD BINGWA KOMBE LA MAZINGIRA ZANZIBAR

0
0
Meneja wa Zanzibar Petroleum LTD Altaf Jiwan akiwapongeza wachezaji wake kwa kuchukua ubingwa wa Kombe la Mazingira lililoandaliwa na Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais Zanzibar, kwa kuifunga tim ya Wizara ya Fedha kwa mikwaju ya penanti 4 kwa 3.Sherehe hizo ilifanyika Ofisini kwao Mtoni Zanzibar.
Kocha wa Tim ya Zanzibar Petroleum LTD Ali Hakiba Hassan alieshika kombe na kikosi kamili cha Zanzibar Petroleum kilicho twaa ubingwa wa Kombe la Mazingira kwaka 2014/2015.
Wachezaji wa Tim ya Zanzibar Petroleum LTD na wafanyakazi wa Kampuni hiyo katika picha ya pamoja.(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

WANANCHI KATA YA NZIHI JIMBO LA KALENGA WAMPONGEZA MBUNGE MGIMWA

0
0
Wazee kijiji cha Nyamihuu wakimpa baraka na kumpongeza mbunge  Mgimwa  kwa uchapa kazi wake 
Na Francis Godwin Blog
MBUNGE  wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amesema atahakikisha anafanya kazi na  vyama  vyote vya  siasa na  kuwa kuwataka  wananchi wa  jimbo la Kalenga kuachana na makundi  ya vyama vya siasa na kuunagana  pamoja  ili  kufanikisha  jimbo hilo kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo.

Mbali ya  kuwataka kuachana na makundi  ya kisiasa  pia amewataka  waliokuwa  wagombea  wa nafasi za ubunge katika uchaguzi mdogo  kupitia  CCM kuacha  kujipitisha  kwa  sasa kwa  wananchi na badala yake kusubiri uchaguzi mkuu mwaka 2015.

Akizungumza kwa nyakati  tofauti katika  mikutano yake ya hadhara  kwa lengo la kuwashukuru wananchi kwa  kumchagua na leo katika kata ya Nzihi ,mbunge huyo  alisema kuwa amelazimika  kuomba ruhusa bungeni kwa  spika  ili kurudi  kuwashukuru  wananchi hao hasa  kutokana na upendo mkubwa ambao  wananchi wa jimbo hilo  walionyesha kwake.

"Ndugu  zangu nilianza  kuzunguka katika baadhi ya maeneo  na kutekeleza ahadi  mbali mbali hata kabla ya  kuapishwa  rasmi  bungeni ......na nitajitahidi kulingana na uwezo wangu  ili kuona natimiza wajibu  wangu kwenu na kamwe  sitawaangusha ndani ya bunge na nje ya  bunge"

Hivyo  aliwataka  wananchi  kwa umoja  wao kuendelea  kumuombea afya  njema  ili kufanikisha  kutimiza ndoto  yake ya  kufikisha maendeleo  katika  jimbo hilo ikiwa ni pamoja na kutimiza sehemu kubwa ya ahadi ambazo zilitolewa na marehemu Dr Wiliam Mgimwa aliyekuwa  mbunge  wa  jimbo  hilo.

Kuhusu  suala la kuyawezesha makundi mbali mbali Mbunge Mgimwa  aliwataka  wananchi  kujiunga na vikundi  vya VICOBA ili  kuviwezesha  vikundi  hivyo  kiuchumi zaidi badala ya  kuwa mtu mmoja mmoja na kuwataka  wazee  pia  kuanzisha umoja  wao na  kupeleka mahitaji yao katika  ofisi  yake.

"Kuna  vikundi  vya VICOBA ambavyo tayari  vimeanzishwa na   moja kati ya  vikundi  hivyo  tayari  nimechangia kiasi  cha Tsh 500,000 na nitaendelea  kuchangia na kuna eneo ambalo marehemu mbunge wetu aliyepita aliahidi kuchangia milioni 1 katika  kikundi cha VICOBA Magubike nasema  fedha  hizo  nitazitoa  mimi "

Alisema  kuwa tayari ameanza  kupigania  suala la umeme na maji katika  vijiji  vya jimbo la Kalenga  bungeni na kuwa  mawaziri wa  wizara  hizo  wameahidi  kulifanyia kazi na kuendelea kusaidia miradi hiyo mikubwa ambazo ndizo ahadi  kubwa  zaidi.

Awali  wananchi  wa kijiji cha Magubike  walimpongeza mbunge  huyo na  kuwa katika historia ya  jimbo la Kalenga  hawajapata kuwa na mbunge mkweli na mchakakazi kama  huyo na kurudi mapema zaidi kwa wananchi kuwashukuru na hivyo kumhakikishia  kuwa hawana mpango wa kumchagua mbunge mwingine mwaka 2015 na kukiomba chama cha mapinduzi kumbariki kuendelea  kuongoza jimbo hilo .

Kwa  upande  wake katibu mwenezi wa CCM wilaya ya Iringa Denis Lupala alisema  kuwa utendaji kazi mzuri wa mbunge  huo ndio ambao unakishawishi  chama kuendelea  kumpa ushirikiano zaidi na kuwa wananchi hawana sababu ya kubabaishwa na wapinzani ambao  wameanza kujipitisha katika  jimbo hilo.

SERIKALI YAWAPA VYETI VYA URAIA WATANZANIA WENYE ASILI YA KISOMALI 1,514

0
0
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (kulia) akimpa cheti cha uraia wa Tanzania, Mkimbizi wa Kisomali mwenye asili ya Kibantu, Ramadhani Haji katika hafla iliyofanyika katika Kijiji cha Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo ambao waliomba kupewa uraia kwa mujibu wa Sheria ya Tanzania. Kulia kwa Waziri ni Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi nchini, Harrison Mseke.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe akizungumza na mamia ya wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu (hawapo pichani), baada ya kutoa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi hao ambao sasa ni raia halali wa Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani. Kulia (Meza Kuu) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Chima. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mathias Chikawe (watatu kulia waliokaa), Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Wakimbizi, Harrison Mseke (kulia), Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Salum Chima (wapili kulia) na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR), Joyce Mends-Cole wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu baada ya kupewa vyeti vya uraia wa Tanzania.Waziri Chikawe alitoa vyeti vya uraia kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika Makazi ya Chogo, Wilaya ya Handeni mkoani Tanga. Katika hotuba yake, Waziri Chikawe aliwataka Wakimbizi hao ambao sasa ni raia halali wa Tanzania kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani.
Sehemu ya Wakimbizi wa Kisomali wenye asili ya Kibantu wanaoishi katika Makazi ya Chogo, Handeni mkoani Tanga wakimshangilia Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (hayupo pichani) alipofika katika makazi yao ili kuwapa vyeti vya uraia wa Tanzania kwa wakimbizi 1,514 waliopo katika makazi hayo baada ya kuomba uraia kwa mujibu wa sheria ya Tanzania. Waziri Chikawe alitoa vyeti kwa wakimbizi hao na kuwataka kudumisha amani kwa kufuata sheria za nchi ili waweze kuishi kwa amani. Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

MEM II NEWS Bulletion 19


ngoma azipendazo ankal

0
0

Saida Karoli - Ndombolo ya solo

MBUNGE JOSHUA NASSARI KUFANYA HARUSI YA HALAIKI LEO JIMBONI KWAKE

0
0
Askofu Mkuu wa Dayosisi ya Meru Dr Paul Akyoo akifanya maombi kwa Bw Joshua Nassari ,Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki na Bi Anande Nnko wanaotarajia kufunga ndoa Jumamosi hii.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akimwimbia mchumba wake Bi Anande Nnko wakati wa sherehe ya Send off iliyofanyika nyumbani kwao na Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru.
Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassari akiwa amekumbatiana na Mchumba wake Bi Anande Nnko muda mfupi baada ya kumtafuta kwa muda katika sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwa Bi Harusi Mtarajiwa ,Meru.
Bi ,Harusi Mtarajiwa Anande Nnko akimpatia zawadi ya T-Shirt Mumewe Mtarajiwa Bw Joshua Nassari wakati wa sherehe ya Send Off iliyofanyika nyumbani kwao Meru.
Na Dixon Busagaga wa Globu 
ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa Jimbo la Arumeru Mashariki ,Mh Joshua Nassari kesho anatarajia kufunga ndoa na Bi Anande Nko katika kanisa la Pentekoste, Kilinga lililoko wilaya ya Meru ambako Mh Nassari alianzia masuala ya Kiimani ikifuatiwa na Sherehe kubwa ya Harusi itakayo fanyika katika viwanja vya Usa-River Academy jirani na Hotel ya Ngurdoto.

Kwa Mujibu wa Mh Nassari ,sherehe hizo zitakazoanza majira ya saa saba mchana  watu wote wamealikwa wakiwemo ndugu, marafiki, Jamaa na wananchi jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tukio hilo na kamba hakuna kadi.

"Nichukue tena fursa hii kuwakaribisha ndg, marafiki, Jamaa na zaidi sana wananchi wangu wa jimbo la Arumeru Mashariki kwenye tendo hadhimu la kusherekea harusi yangu , Jumamosi Juni 7, Usa-River academy grounds kuanzia saa saba mchana. Kwa Pamoja Tulianza na Mungu, Tutamaliza na Mungu Pamoja. ...No cards on entrance!"alisema Nassari.
Nassari amesema watu zaidi ya 8000 wanatazamiwa kushiriki katika sherehe hiyo ya aina yake wakiwemo viongozi mbalimbali na wabunge kutoka maeneo mbalimbali .

christian bella na bendi yake ya malaika wateka mji wa tabora

0
0
 Mpiga kinanda na stage manager wa Malaika Band akiwa kazini usiku wa kuamkia leo katika ukumbi wa Bwalo la Maafisa wa Polisi mjini Tabora wakati bendi hiyo inayokuja juu kwa kasi chini ya uongozi wa mtunzi na mwimbaji mahiri na mtunzi bora wa mwaka wa Kili Music Awards Christian Bella ilipotumbuiza mamia ya wapenzi wao katika ukumbi huo mkongwe
 Safu ya ushambuliaji ya Malaika band wakiwa jukwaani
 Mandhari ya ukumbi
 Wanenguaji wa Malaika band wakiwajibika
Kiongozi, mtunzi na mwimbaji mahiri ambaye ni mtunzi bora wa mwaka wa Kili Music Awards Christian Bella akikonga nyoyo za mamia ya wapenzi wao katika ukumbi huo mkongwe.
Picha na Sultani Kipindo wa Globu ya Jamii

Mahojiano kuhusu mchakato wa Katiba katika kipindi cha Tuambie TBC1

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA NISHATI KWA NCHI ZA AFRIKA

0
0
 Waziri wa Nishati  na Madini Profesa Sospeter Muhongo akiongea wakati wa mkutano wa Mawaziri wanaohusika na  masuala ya   Nishati ambapo aliwatangazia wajumbe hao kwamba Tanzania itakuwa mwenyeji wa Mkutano wa  Bara la Afrika  kuhusu  Nishati Endelevu katika muda utaopangwa na Umoja wa Mataifa.
 Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa siku tatu wa Nishati Endelevu kwa Wote ( SE4ALL)  ulioandaliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa.  Eng. Yahya  Samamba Katibu wa Waziri na  Eng. Styden Rwebangila
Watanzania wengine ambao ni sehumu ya Ujumbe wa Tanzania.  Kutoka  kushoto ni  Bi. Venosa Ngow ( TPDC) Eng. Leonard Masanja kutoka Wizara ya  Nishati na Madini na  Eng Jones fredrick Olutu kutoka  Wakala wa Nishati  Vijijini ( REA)
---------------------------------
Na  Mwandishi Maalum,  New  York

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  imeelezea utayari wake wa  kuwa mwenyeji wa mkutano wa Bara la Afrika kuhushu Nishati Endelevu kwa wote.

Ahadi hiyo imetolewa  siku ya Ijumaa,  na Waziri wa Nishati na Madini ,  Profesa Sospeter Muhongo ( Mb) mwishoni wa mkutano  wa siku tatu , uliojadili kwa kina upatikanaji wa nishati endelevu kwa wote. Mkutano huu  uliojumuisha wadau wa kada mbalimbali uliandaliwa na  katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,  ambapo pia  palifanyika    uzinduzi wa mwongo wa nishati endelevu kwa wote unaoanza 2014 hadi 2024.

“  Ninapenda kutaarifu kwamba,  nimezungumza na   Rais wangu, Tanzania iko tayari kuwa mwenyejiji  wa mkutano wa nchi za Afrika kuhusu nishati endelevu. Tutakuwa  wenyeji wa mkutano huo pale Umoja wa Mataifa utakapokuwa tayari”. akasema  Waziri Muhongo. Kauli iliyopokelewa vema na waandaji wa mkutano huo.

Waziri Muhongo ambaye ameshiriki  kikamilifu mijadala mbalimbali tangu mwanzo wa mkutano hadi mwisho, alisema Tanzania na kama  ilivyo kwa nchi nyingine nyingi hasa za Afrika,  Nishati Endelevu ni muhimu  katika utekelezaji na ufanikishaji wa  Maendeleo  Endelevu  badaa ya  mwaka 2015.

Akasisitiza kuwa katika utekelezaji wa mpango wa  nishati mbadala kwa wote,  Afrika  inapashwa kupewa kipaumbele cha pekee.

Katika siku hii ya tatu na ya mwisho ya mkutano huu,  Mawaziri walioziwakilisha nchi zao, walipata fursa ya kubadilishana mawazo,  kuelezea uzoefu wao,  kutoa maoni yao na  halikadhalika kupendekeza nini  cha kufanya ili hatimaye watu wengi zaidi hususani katika nchi zinazoendelea  waweze kupata huduma hii ya nishati endelevu.

Inakadiriwa kwamba  zaidi ya  watu 1.3 bilioni duniani kote hawana huduma ya umeme na zaidi wa 2.6 bilioni wanatumia nishati asilia kwa  kupikia na  kupata joto. Matumizi ya  nishati asilia yanasababisha    watu  4.3 milioni kufariki kila mwaka  kabla ya wakati  wao  huku wengi  kati yao wakiwa ni   wanawake na watoto  kutokana na uvutaji wa  moshi.

Waziri Muhongo ambaye ameongoza  ujumbe wa  Tanzania katika mkutano huu  akiwamo  Muhandisi kutoka  Wakala wa Nishati  Vijijini. Amesisitiza pia  uhusiamo kati ya   nishati na elimu   kwa kile alichosema ili mwanafunzi aweze kujiandaa au kujisomea vizuri anahitaji nishati ambayo ni endelevu na yenye  uhakikia.

 “ Hii itakuwa mara yangu ya nne  kutoa maoni na mchango wangu na  kwa sababu hiyo  nisingepeda kutumia muda  mwingi na  pengine kurudia  kile ambacho nimeshakisema huko nyuma. Nisisitize kwamba tunapozungumzia mpango wa  nishati endelevu kwa wote basin chi za afrika  zinatakuwa kupewa kipaumbele cha pekee,  vile vile  suala  la uwepo wa nishati endelevu lina uhusiano mkubwa na utekelezaji wa maendeleo endelevu baada ya  2015.

Akasisitiza kuwa Tanzania  imejipanga vema katika kuhakikisha kwamba  wananchi wake wanapatiwa huduma  hiyo muhimu kwa maendeleo yao na  nchi kwa ujumla.

Akinukuu wanafalsafa mbalimbali,  Waziri Muhongo amebainisha kwamba  dhana hiyo ya kumpatia  huduma ya nishati endelevu  kila mtu inawezekana   ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake pamoja na ushirikiano.

Baadhi ya wazungumzaji katika mkutano huo wa  Mawaziri walieleza kwamba  inawezekana kabisa kutumia mifano  ya huduma za  usambazaji  wa simu za mkononi huduma ambayo imewafikia watu wengi ikatumika katika usambazaji wa  nishati  endelevu.

Wengine walisisitiza umuhimu wa nishati mbadala kama vile wa matumizi ya nguvu za jua na upepo kama moja wa  eneo muhimu la kuwafikia watu wengi. Huku baadhi wakisisitiza  umuhimu wakuwatumia wataalamu waliopo pamoja na tafiti ambazo zimekwisha kufanyika kuhusu suala zima la nishati. 






kutoka maktaba: basi la uda miaka ya 1980

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI MWANDAMIZI WA MAMBO YA NDANI NA NJE WA SINGAPORE

0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Wa pili kutoka kulia mstari wa mbele ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Rajabu Gamaha, na kushoto kwake ni Balozi wa Tanzania nchini India anayewakilisha pia nchini Singapore, Mhe. John Kijazi.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli, Ikulu jijini Dar es salaam Mei 6, 2014. Waziri huyo na ujumbe wake yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano.PICHA NA IKULU

JUST IN: AMBASIA MALIY ATWAA TAJI LA MISS TABATA 2014

0
0
Miss Tabata 2014, Ambasia Maliy akitabasamu baada ya kutangazwa  rasmi kuwa Mrembo wa Kitongoji cha Tabata.
Miss Tabata 2014, Ambasia Maliy akipunga mkono kwa mashabiki wake muda mfupi baada ya kutawazwa rasmi kuwa Mrembo wa Kitongoji cha Tabata, Shindano hilo lilifanyika kwenye Ukumbi wa Da'west Park,Tabata jijini Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo Jumamosi. Wengine pichani ni Mshindi wa Pili wa shindano hilo,  Faudhia Feka (kulia) pamoja na Mshindi wa Tatu, Ramta Mkadara .
 
Miss Tabata aliemaliza muda wake, Doris Molel (alieketi) akisuburi kutangazwa kwa mrithi wake. Kwa mapicha zaidi BOFYA HAPA

Mkazi wa Sinza kuona Kombe la Dunia kupitia promosheni ya Kwea Pipa na TBC

0
0
Na Mwandishi Wetu

Promosheni ya Kwea Pipa na televisheni ya Taifa ya TBC  kwa kushirikiana na kampuni ya Push Mobile Media Limited imezidi kupamba moto baada ya mshindi mmoja zaidi kupatikana.

Deocary Mkenda ambaye ni mkazi wa Sinza ameungana na wenzake wawili ambao wamekwisha zawadiwa tiketi zao na sasa kampuni ya Push Mobile Media Limited inawatafutia pasipoti kwa ajili ya kusafri na kuona mechi ya Brazil na Cameroon Juni 23 mjini Rio de Janeiro.

Mkenda (35) ambaye ni Mhasibu katika kampuni ya Ernst & Young ya jijini anaungana na Donald Milinde Shija (34) mkazi wa Mabibo jijini ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya Davis and Shirtliff na mshindi mwingine ni Shaban Athumani Saidi (22) mkazi wa Banana-Kitunda.

Meneja kampeni wa promosheni hiyo ya Semu Bandora alisema kuwa bado tiketi mbili kwa ajili ya mashabiki wa soka nchini ili kujishindia tiketi kwa ajili ya kuona kombe hilo.

Bandora alisema kuwa droo nyingine itafanyika wiki ijayo na lengo ni kuona mashabiki wanapata fursa hiyo ya kuona mashindano hayo makubwa kabisa ya soka duniani.

“Tunawaomba mashabiki wa soka kuendelea kushiriki katika promosheni hii ili kupata nafasi ya kuwaona mastaa wa dunia kama akina Benoit Assou-Ekotto, Alex Song na Samuel Eto’o na yule wa  Brazil kama vile Neymar da Silva Santos Júnior, Thiago Silva, Dan Alves na wengine wengi,” alisema Bandora.

Alisema kuwa mbali ya tiketi za kombe la dunia, pia kuna zawadi za ving’amuzi zaidi ya 250, televisheni za flat screen sita na fedha taslimu ambazo zote zimeandaliwa kwa ajili ya kuwazawadia mashabiki wa soka.

Mwili wa Marehemu Gebbo Peter waagwa leo nyumbani kwake Vingunguti,Kuzikwa kijijini kwao Kigurunyembe mkoani Morogoro

0
0
Sehemu ya wachezaji mpira wa sasa na wazamani wakiwa wamesimama pembeni ya Jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa Mchezaji wa Timu ya Simba miaka ya nyuma,Marehemu Gebbo Peter aliefariki jana kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam.hapa wakiwa nyumbani kwake Vingunguti tayari kwa safari ya kwenda kwenye maziko yake Kigurunyembe mkoani Morogoro (Picha na Evance Ng'ingo)

Wadau mbali mbali wa soka wakiwemo viongozi wa soka wakipita kutoa heshima zao za mwisho kwa mwili wa Marehemu Gebbo Peter,Nyumbani kwake Vingunguti,jijini Dar es Salaam kabla ya kuanza safari ya kuelekea Kigurunyembe mkoani Morogoro kwa mazishi.
Ibada ikifanyika.
Mbunge wa Jimbo la Ilala,Mh. Mussa Azzan Zungu akitoa heshima za Mwisho.

Mwili ukiwasili nyumbani.

HIGH PERFORMANCE LEADERSHIP SEMINAR

RAIS KIKWETE AONGOZA WAOMBOLEZAJI KUAGA MWILI WA MFANYAKAZI WA IKULU MAREHEMU ERNESTI B. NGEREZA

0
0
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakitoa heshima zao za mwisho katika Kanisa la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Ernesti B. Ngereza, aliyekuwa mfanyakazi wa Ikulu aliyefariki dunia Mei 5, 2014, kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu Lushoto, Mkoani Tanga Ijumaa Mei 6, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete wakijumuika na waombolezaji wengine katika Kanisa la Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam wakati wa kuaga mwili wa Marehemu Ernesti B. Ngereza, aliyekuwa mfanyakazi wa Ikulu aliyefariki dunia Mei 5, 2014, kabla ya mwili huo kusafirishwa kwenda nyumbani kwa marehemu Lushoto, Mkoani Tanga Ijumaa Mei 6, 2014.
Viewing all 109587 articles
Browse latest View live




Latest Images