Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live

cheka unenepe


Mualiko wa Kongamano la 6 la Kukaribisha Mwezi mtukufu wa Ramadhan kufanyika juni 22, 2014

$
0
0
TAMPRO inayofuraha kwa heshima na taadhima kukuarifu kufanyika kwa Kungamano la Sita la Kukaribisha Mwezi wa Ramadhan 1435H, Siku ya Jumapili Juni 22, 2014 Katika ukumbi wa Julias Nyerere International Convention Centre (JNICC) – Shaaban Robert Street,Dar es Salaam kuanzia saa 02:30 Asubuhi Mpaka Saa 10:30 Alasiri.

TAMPRO ni Taasisi ya wanataaluma wa Kiislamu katika fani mbali mbali iliyosajiriwa Mwaka 1997 kwa lengo la kuwaleta pamoja wanataaluma wa kiislamu kulitumikia taifa huku wakiendelea kuimarisha misingi na thamani za matendo bora ya kiislamu.

Wanachama wake hutokea katika taaluma mbali mbali zikiwemo za Afya, Uchumi, Uhandisi, Elimu, Sheria, Usimamizi wa Biashara pamoja na nyanja mbali mbali za Uongozi na sayansi za jamii.
Kwa Miaka Sita Mfululizo, TAMPRO imejenga utamaduni wa kuwaalika Waislam Mbali mbali kujumuika pamoja katika Jumapili ya Mwisho ya Mwezi wa Shaaban katika kongamano la kuwaandaa na kukaribisha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan “Welcoming Ramadhan Conference” ili kufahamiana, kudumisha udugu, Kuwa Karibu na Wanazuoni wa Kiislam na kuonyesha uwepo wao katika Jamii.
Katika Kongamano la Mwaka huu “The 6th Welcoming Ramadhan Conference 1434H” Anwani ya Mkutano itakuwa ni “Vijana Wetu, Hazina Yetu” ambapo mambo kadhaa yatajadiliwa ikiwa ni pamoja na Mafanikio na changamoto zinazowakabili Vijana katika jamii.

1. Sheikh, Mwanasayansi, Profesa Mohammed Badamana kutoka Chuo Kikuu Cha Nairobi atazungumza kuhusu “Changamoto za kuwalea vijana wa kiislam katika dunia ya sasa inayobadilika kwa haraka”
2. Sheikh Mh. Amir Mussa Kundecha, Kutoka Baraka Kuu la Jumuia na Taasisi za Kiislam ambaye pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba atazungumza kuhusu “Qur an Tukufu, Katiba mpya ya nchi yetu na Mustakbali wa Vijana wa Kiislam”
3. Ndugu Ali Masoud Maarufu Kama Masoud Kipanya atazungumza kuhusu “Vijana, Vyombo vya Habari na Utandawazi”
Karibu Ujumuike na Waislamu Wanaataluma mbali mbali zaidi ya 600katika kusukuma mbele Uislamu kwa kujuana na kuongeza Mshikamano wa Wanazuoni Wetu Mbali Mbali. Mchango wa ushiriki na Maandalizi ya Kongamano ni TZS 30,000 kwa Mtu na TZS 50,000 kwa Mke na Mume. Mume mwenye Mke Zaidi ya Mmoja atapewa upendeleo Maalum.
Tuna matumaini makubwa na kupata uwakilishi wako katika shughuli hii pamoja na kuwafikishia taarifa hii wanataaluma wengine watakaoweza kufika na kujumuika Pamoja.

Kadi za Ushiriki zinapatikana Ofisi za TAMPRO Makao Makuu Magomeni Usalama karibu na Ofisi za Manispaa ya Kinondoni, Dar es salaam au Piga Simu namba hizi ili kuletewa au kuwekewa kadi yako:0688 130828.   0714151532 .   0767 151532
In sha Allah Mwenyezi Mungu atufikishe salama na atufanyie wepesi kujumuika na kutimiza malengo ya mjumuiko huu.

Maassalaam

Mohamed,
Mwenyekiti, Kamati ya Maandalizi
+255787670714 or 0767565560.

Michuzi TV - You'll love it!

kutoka maktaba: ikarus kumbakumba we miss you... post back by popular demand

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZINGIRA YATOA MSISITIZO WA USIMAMIZI WA SHERIA ZA UHIFADHI WA MAZINGIRA

$
0
0
Mkuu wa wilaya ya Temeke Bi. Sophia Mjema ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Meck Sadiki (katikati) akipokea maandamano ya wadau mbalimbali wakati wa maadhimisho ya kilele cha wiki ya mazingira jijini Dar es salaam.Kulia ni Meya wa Manispaa ya Ilala Mh. Jerry Silaa. 
Baadhi ya wananchi na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa kwenye maandamano huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa kilele cha wiki ya mazingira duiniani leo.
Baadhi ya wananchi na wanafunzi kutoka shule mbalimbali za jiji la Dar es salaam wakiwa kwenye maandamano huku wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe mbalimbali wakati wa kilele cha wiki ya mazingira duiniani leo.
Kikundi cha ngoma za asili kutoka shule ya msingi Umoja kikitoa burudani wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika katika uwanja wa Mnazimmoja jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wafanyakazi na wadau wanaojihusisha na shughuli za usafi na usimamizi wa mazingira jijini Dar es salaam wakiwa na zana zao za kazi wakati wa maadhimisho ya wiki ya Mazingira yaliyofanyika katika uwanja wa Mnazimmoja jijini Dar es salaam.

WAZIRI MWANDAMIZI WA MAMBO YA NJE NA NDANI WA SINGAPORE ZIARANI NCHINI

$
0
0
Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yake na Waziri Mwandamizi anayeshughulikia Mambo ya Nje na Ndani wa Jamhuri ya Singapore, Mhe. Masagos Zulkifli ambaye yupo nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tano. Katika mazungumzo yao walisisitiza kuimarisha ushirikiano katika masuala mbalimbali ikiwemo utalii, uchukuzi  na uwekezaji.
Mhe. Zulkifli naye akizungumza wakati wa mkutano wake na Mhe. Dkt. Maalim.

Balozi wa Tanzania nchini India anayewakilisha pia nchini Singapore, Mhe. John Kijazi (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. Nathaniel Kaaya wakifuatilia mazungumzo kati ya Mhe. Maalim na Mhe. Zulkifli (hawapo pichani)
Bw. Adam Isara (kushoto), Katibu wa Naibu Waziri na Bw. Khatib Makenga, Afisa Mambo ya Nje wakifuatilia mazungumzo
Mhe. Dkt. Maalim akimsindikiza Mhe. Zulkifli na ujumbe wake mara baada ya mazungumzo yao
Mhe. Dkt. Maalim akiagana na Mhe. Zulkifli.

Golden Bush kupeleka Makali yake Makambako

$
0
0
Tunapenda kutoa taarifa kwamba ile timu tishio upande wa veterans hapa nchini yaani Golden bush veterans ambao ndio mabingwa wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yaani Bara na visiwani watakuwa Makamboko siku ya tarehe 22 June 2014 kwa mualiko wa Makambako Veterans wakishirikiana na Serengeti Breweries.

 Mwaliko huu umetokana na historia ndefu ya timu yetu ambayo imejijengea heshima ya kuwa na ushirikiano wa karibu na timu nyingi za veterans wakiwemo Makambako Veterans ambao ndio watakuwa wenyeji wetu siku ya tarehe 22. Aidha tunapenda kutumia nafasi hii kama sehemu mojawapo ya kutengeneza urafiki wa karibu Zaidi na timu za nyanda za juu kusini.

Maandalizi yamekamilika kwa asimia 95 ambapo mkuu wetu wa msafara bwana Waziri Mahadhi Mandieta akishirikiana na mwenyekiti wa kamati ya ufundi bwana Yahaya Issa wanakamilisha baadhi ya mambo madogo madogo tayari kwa safari ya kuelekea mkoani Njombe.

Kesho tutakuwa na mechi ya kirafika na Wizara ya afya ikiwa na sehemu mahususi kabisa ya kupasha misuli kabla ya kuanza safari ndefu kabisa ya kuelekea Makambako. Karibuni sana, game ya kesho itapigwa katika uwanja wa Kinesi ali maarufu kama St James’ park kuanzia saa saa mbili kamili asubuhi.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.

Onesmo Waziri “Man of the match” “Ticotico” “player Maker” Msemaji wa timu na Mchezaji Mwandamizi.

Wizara ya Mambo ya Nje yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akipanda mti katika kuashiria kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani katika eneo la Kituo wa Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC) kilichopo jijini Dar es Salaam. Siku hiyo iliadhimishwa duniani kote tarehe 05 Juni, 2014.  
Afisa Mambo ya Nje, Bi. Naomi Zegezege akipanda mti kwa niaba ya Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani.
Bw. John Haule akiongozana na Mkurugenzi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere  Bw. Deus Kulwa (kulia) baada ya kupanda miti katika kuadhimisha siku ya mazingira duniani. Kushoto ni Bi Naomi Zegezege, Afisa Mambo ya Nje
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule akizungumza na Wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje pamoja na Wafanyakazi wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani.
Baadhi Wafanyakazi wa Wizara  ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakimsikiliza Katibu Mkuu  (hayupo pichani)
Katibu Mkuu, Bw. John Haule na Mkurugenzi wa JNICC, Bw. Kulwa katika picha ya pamoja.
Katibu Mkuu akiwa katika picha ya pamoja na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa baada ya Wizara kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani kwa kupanda miti.
Bw. John Haule akizungumza na waandishi wa habari


Picha na Habari na Reginald Philip

Wizara ya Mambo ya Nje yaadhimisha Siku ya Mazingira Duniani

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bw. John Haule, amewataka wafanyakazi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa na watanzania wote kwa ujumla kutumia nishati endelevu badala ya kuni na mkaa, kuunga mkono juhudi za serikali za kunusuru mazingira.

Akiongea katika maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani yaliyoandaliwa na wizara kwenye ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam leo, Bw. Haule alisema hatua nyingine za kutunza mazingira ni kupanda miti; kutolima kwenye miteremko ya milima; kupunguza matumizi makubwa ya mbolea na kuachana na matumizi ya mifuko ya plastiki isiyiteketezeka kwa urahisi.
Wawekezaji katika viwanda watumie teknolojia ya kisasa isiyoongeza gesi joto, alishauri.

Katika maadhimisho hayo chini ya kauli mbiu isemayo  “Sayari ya dunia ni kisiwa chetu wote kwa hivyo tuunganishe nguvu zetu kulinda kisiwa hiki,” Bw. Haule alipanda mti kuanzisha mpango wa wizara wa kupanda miti kutunza mazingira. Miti saba ilipandwa nje ya ukumbi wa Julius Nyerere leo kwa kuanzia.


Maadhimisho hayo pia yalishirikisha wafanyakazi wa AICC na ukumbi wa Julius Nyerere.

MWENYEKITI CCM TAWI LA MOSCOW URUSI ATOA MSIMAMO WAKE JUU YA MCHAKATO WA KATIBA, ASEMA SERIKALI MBILI NDIO SULUHISHO

$
0
0
MWENYEKITI TAWI LA CCM MOSCOW URUSI, NDG SALIM MFUNGAHEMA: 

 Mwenyekiti tawi la CCM Moscow Ndg Mfungahema Salim amesema muundo wa muungano wa serikali Mbili ndio suluhisho pekee la watanzania, Akizungumza katika kikao cha kamati ya siasa ya tawi kilichofanyika 05.06.2014, bwana Mfungahema alisema muungano wa serikali mbili ndio umetufikisha hapa tulipo na kuna mafanikio makubwa TULIYOYAPATA, pamoja na changamoto chache zinazojitokeza lakini zinarekebishika.

 Bwana Mfungahema aliwataka vijana wa CCM kuendelea kuungamkono muungano wa serikali mbili kwani ndio muungano wenye tija kwa taifa. Bwana Mfungahema alisema serikali tatu ni mzigo kwa taifa na hivyo hatunabudi kuendelea na mfumo wa serikali mbili na ikibidi tuelekee kwenye serikali moja kwani ni muungano sahihi na utaleta tija na mshikamano zaidi kwa watanzania. Pia mwenyekiti alimshukuru Mh Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete kwa jitiada zake za kuwaletea maendeleo watanzania na kuboresha utawala bora Tanzania na Afrika kwa ujumla.

 Mh mwenyekiti Ndg SalimMfungahema alitumia fursa hiyo pia kumpongeza Mh Rais Kikwete kwa kupata tunzo la kuwa kiongozi bora barani Afrika mwenye mchango mkubwa wa kuleta maendeleo, amani na utawala bora, bwana Mfungahema alisema Rais Kikwete ametupatia heshima kubwa watanzania kote duniani.

   Kuhusu uchaguzi wa mwaka 2015, bwana Mfungahema alisema CCM inatarajia kupata ushindi mkubwa na wa kishindo mwaka 2015 kwa sababu CCM imetekeleza ilani yake ya uchaguzi vizuri na kwa wakati, na hivyo kuwafanya wananchi wawe na imani kubwa na CCM.

   Mwenyekiti pia alimpongeza katibu mkuu wa CCM MH Abdulrahmani Kinana kwa mchango wake mkuwa na kuimalisha chama, na kukipa cha uhai mkubwa na kurudisha imani ya wananchi kwa CCM, alisema jukumu la kuimalisha chama ni la kila mwana CCM na sio viongozi pekee, hivyo alitoa wito kwa vijana wanaporudi nyumbani Tanzania kutoa ushirikiano wa kuimarisha chama katika maeneo yao, ikiwa ni pamoja na kuelezea jinsi ilani inavyotekelezeka.

                                KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
                               IMETOLEWA NA KATIBU WA TAWI
                              NDG HASSANI KAPILIMA, CCM MOSCOW.

TFF YATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA MSIBA WA GEBO PETER

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha mchezaji wa zamani wa timu ya Simba na Taifa Stars, Gebo Peter kilichotokea usiku wa kuamkia leo (Juni 6 mwaka huu) katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Gebo aliyezaliwa mwaka 1961, pia aliwahi kuchezea timu za Sigara ya Dar es Salaam, CDA ya Dodoma na kombaini ya Mkoa wa Dar es Salaam (Mzizima United). Hadi mauti yanamkuta alikuwa akijishughulisha na biashara, kubwa ikiwa ya vifaa vya michezo.

Msiba huo ni mkubwa katika familia ya mpira wa miguu nchini kwani, Gebo enzi za uhai wake alitoa mchango mkubwa akiwa mchezaji na baadaye kiongozi katika timu ya Manyema ya jijini Dar es Salaam.

TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Gebo Peter, klabu ya Manyema na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

Msiba upo nyumbani kwao Vingunguti karibu na Kanisa Katoliki ambapo taratibu za mazishi zinaendelea kufanywa na familia.

Marehemu ambaye ameacha mjane na watoto watatu anatarajiwa kuzikwa kesho (Juni 7 mwaka huu) nyumbani kwao Kigurunyembe, mjini Morogoro.

Bwana alitoa, na Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Utambulisho wa video mpya ya Chereko Chereko - CPwaa

$
0
0
Uzinduzi wa Video mpya ya CPwaa "Chereko Chereko" utafanyika Jumapili hii (8/6/2014) ndani ya New Maisha Club Club. sambamba na uzinduzi huo kundi la wasanii wa kizazi kipya "Wadananda" litatambulisha wimbo wao mpya uitwao "Kidaluse". Watakaosindikiza usiku huo ni pamoja na: Dullayo, Spince Senseme,Wakazi,Dknob,Country Boy,Young Suma,Msami,Gnex, The B est of Kino na The chocolate Dancers.

President Kikwete has sent a congratulatory message to His Majesty, King Carl XVI Gustav of Sweden

$
0
0
H.E Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to His Majesty, King Carl XVI Gustav of Sweden on the occasion to celebrate the Swedish National Day on 6th June, 2014.

 “Your Majesty King Carl XVI Gustav,
   The King of Sweden,
   Stockholm,
   SWEDEN.

It is my pleasure on behalf of the people and the Government of the United Republic of Tanzania to extend to Your Majesty and through you to the people of Sweden my heartfelt congratulations on the occasion to celebrate the Swedish National Day. 

The celebration of your National Day offers us yet another opportunity to reaffirm our commitment to continue working closely together in enhancing the existing bilateral ties between our two countries. I am confident that the bonds of friendship, co-operation and partnership that our two countries enjoy will continue to grow in greater heights for our mutual benefit.

Please accept, Your Majesty, my best wishes for your continued good health and peace and prosperity for the people of Sweden”. 

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation of the United Republic of Tanzania, 

Dar es Salaam.

SERIKALI YASHAURI WADAU WA MICHEZO KUJITOKEZA KUSAIDIA MICHEZO NCHINI

$
0
0
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kupokea msaada wa hundi ya milioni kumi kutoka Zantel kwa ajili ya Chama cha Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT) leo jijini Dar es Salaaam, kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara (kulia), Afisa Mtendaji Mkuu Zantel Bw. Pratap Ghose (kushoto) pamoja na viongozi kutoka Chama cha Ngumi Tanzania (BFT) wakiunganisha mikono kwa pamoja kuonyesha ushirikiano wakati wa makabidhiano ya hundi ya shilingi Milioni kumi kama msaada kutoka Zantel kwa Chama cha Ngumi Tanzania (BFT).
Rais wa Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Mutta Rwakatare akitoa shukrani kwa Zantel baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni kumi kuinua mchezo wa ngumi, kushoto ni Katibu Chama cha Ngumi Tanzania Bw. Makole Mashaga na kulia ni Mjumbe wa Maendeleo ya Wanawake Bi. Aisha George Voniatis. Picha na Genofeva Matemu.

Mafunzo kwa Maafisa Mawasiliano Serikalini kuhusu Itifaki na Huduma kwa Mteja

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa Elisante Ole Gabriel (aliyevaa tai) akiwa kwenye Picha ya pamoja na Maafisa Mawasiliano Serikalini wa kutoka kwenye Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali. Mafunzo hayo yamefunguliwa na Bibi. Sihaba Mkinga, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo. Prof. Gabriel mbali na Kuwa Naibu Katibu Mkuu, pia ni Mwalimu ambapo alitoa mada kwa Maafisa hao namna ya kuwahudumia vizuri wateja wao mahali pa kazi.

Maendeleo ya Msiba wa Gebbo Peter nyumbani kwake Vingunguti,jijini Dar

$
0
0
Msemaji wa familia ya Marehemu Gebo Peter, Peter Tino ambae pia ni kaka wa marehemu (wa kwanza aliesimama) akiwa pamoja na baadhi ya wachezaji wa zamani kulia kwake ni Aboubakar Kombo aliekaa kuanzia kulia ni Idi Pazi ambae ni kocha wa makipa wa Simba akifuatiwa na Khamis Kondo na David Mwakalebela wakiwa nyumbani kwa marehemu Vingunguti.(Picha na Evance Ng'ingo).


KUMBUKUMBU

$
0
0
MAREHEMU MWASHABAN A. LIGANJA

Mpendwa Mama,

Mama unatimiza miaka saba (7) sasa. Tunamshukuru Mungu kwa muda wote uliokuwa nasi, si tu kuwa Mama bali ulikuwa mtu wa pekee miongoni mwetu Mama. Ulibarikiwa mambo mengi ambayo tukianza kuyaorodhesha hapa tunaweza kujaza kitabu ila kwa ufupi UPENDO usiokuwa na kipimo.
Mama DAIMA utakumbukwa na Mumeo Mpendwa George Mapango, wanao Mariam (Chuma), Eva (Hawa), Jackson (Kibabu), Patrick (Said), Richard na watoto wote kwa upande wa Dada zako na kaka zako. Mkweo Deogratius Sakawa, Wajukuu zako Precious (P), Pricilla na Jasmine. Wadogo zako, Ndugu, Jamaa, Marafiki zako, Majirani na Wafanyakazi Wenzako.

Tutaendelea kufuata ushauri wako na mema mengi uliyotufundisha. Kwa upendo wako unatuunganisha familia na tutaendelea kukumbuka busara zako na hekima daima. KISOMO KITAFANYIKA KESHO TAREHE 07 JUNI, 2014 SAA 04.00 ASUBUHI.


INNA LILAH WAINA LILAH RAJIUUN

Article 13

Mh. Lowassa azindua bwawa kubwa la maji Monduli

$
0
0
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akifungua kibambaa kuashiria uzinduzi wa bwawa kubwa la maji la Leken katika kata ya Seleli wilayani Monduli leo Ijumaa Juni 06,2014.Bwawa hilo ambalo limegharimu kiasi Cha shilingi bilioni moja unusu, lina ukubwa wa kilomita tatu.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa akizungumza mara baada ya kufungua Bwawa hilo.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli,Mh. Edward Lowassa na Mkewe Mama Regina Lowassa akikagua eneo la bwawa hilo huku akiongozana na viongozi wa wilaya hiyo.

Serikali yapiga marufuku ajira za watoto kwenye migodi

$
0
0
Na Greyson  Mwase, Tarime

Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia madini Stephen Masele amekemea vikali tabia ya wamiliki wa migodi  kuajiri watoto wenye umri wa chini ya miaka 18  kwani inarudisha maendeleo ya watoto hao na kwa jamii kwa ujumla inayowategemea

Waziri Masele ameyasema hayo kwenye ufunguzi wa semina iliyoshirikisha wachimbaji wadogo, madiwani, viongozi wa vijiji, wilaya, madiwani pamoja na viongozi wa vyama  vya siasa inayoendelea katika jimbo la Mwibara wilaya ya Bunda mkoani Mara.

Waziri Masele alisema kuwa kumekuwepo na tabia ya wamiliki wa migodi, ikiwa ni pamoja na wazazi wenye watoto wenye umri chini ya miaka 18 kuruhusu watoto hao kufanya kazi kwenye migodi badala ya kuwahimiza kwenda shule na kupata elimu itakayowasaidia kutoka kwenye giza.

BALOZI KAMALA ABAINISHA MTAZAMO MPYA WA USHIRIKIANO KATI YA AFRIKA, KARIBIANI, PASIFIKI NA JUMUIYA YA ULAYA

$
0
0
Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala akihutubia wadau wa ushirikiano kati ya nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya. Balozi Kamala alisisitiza umuhimu wa nchi za ACP na Jumuiya ya Ulaya kushirikiana katika kujenga uchumi, kukuza na kutumia teknolojia kuharakisha maendeleo na kuweka mazingira mazuri ya kufanya biashara yenye kunufaisha pande zote. Wadau wa ushirikiano wa ACP na Jumuiya ya Ulaya wamekutana leo Brussels kutafakari miaka 39 ya ushirikiano.
Viewing all 110170 articles
Browse latest View live




Latest Images