Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live

gardner G habash ndani ya michuzi TV - kaa chonjo


Miss Tabata kupatikana leo Da’ West Park

$
0
0
 Warembo 16 leo watawania taji la Miss Tabata 2014 kwenye shindano ambalo litafanyika katika ukumbi wa Da’ West Park, Tabata.
Mratibu wa shindano hilo Joseph Kapinga amesema kuwa mrembo atakayeshinda atamrithi Dorice Mollel ambaye pia anashikilia taji la Miss Ilala.
Mratibu huyo amesema mshindi huyo atazadiwa 500,000/- wakati mshindi wa pili atapata 300,000/- na watatu 200,000/-. Mshindi wa tatu na wa nne kila moja atapata 150,000/-.
Bali na zawadi ya pesa taslim pia kila mshiriki atapata zawadi ya kujisomea kwa mwaka moja katika chuo cha Data Training College. Thamani ya kila kozi kwa kila mmoja litakuwa ni 800,000/-.
Warembo waliyosalia watazawadiwa 100,000/-  kila mmoja.
Washiriki ni Esther Frank Kiwambo (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22), Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).
Wengine ni Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ambasia Lucy Mally (22), Angle Kashaga (22), Faudhia Hamisi Feka (21), Najma Charles Mareges (19), Lightness Olomi (18), Husna Ibrahim (19), Ramta Mkadara (20) , Marry Henry (22) na Mariam Shwaib Hussein (19).
Mratibu huyo alisema fainali hiyo itasindikizwa na burudani kutoka kwa bendi ya Twanga Pepeta.
Miss Tabata inadhaminiwa na Zanzi, Redds, Fredito Entertainment, CXC Africa, Saluti5 na Nevada Barber Shop.
Miss Tabata inaandaliawa na Bob Entertainment na Keen Arts.

Tanzania yashiriki mkutano wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi mjini Bonn,Ujerumani

$
0
0
Mwenyekiti wa Kundi la Afrika Nagmeldeen Elhassan kutoka Sudan akizungumza wakati wa mkutano wa kundi la Afrika uliokuwa ukitoa taarifa kwa ufupi kwa mawaziri wa mazingira Afrika.kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya makamu wa Rais -Muungano,Mh. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Balozi Ahmed Swaraldhab kutoka Wizara ya Mambo ya Nje nchini Sudan. Waziri Samia anahudhulia Mkutano huo kwa kumuwakilisha Waziri wa Mazingira Tanzania ambae ni mwenyekiti wa Mawaziri wa Mazingira Afrika.
Maafisa kutoka katika serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wakishiriki katika mkutano wa kundi la Afrika kwenye mkutano wa mkataba wa mabadiliko ya tabianchi mjini Bonn Ujerumani Leo.
Waziri wa nchi Ofisi ya makamu wa rais Muungano Mh. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia masuala ya mabadiliko ya Tabia Nchi Bw. Richard Muyungi katika mkutano wa kundi la G77 na China, kwenye mkutano wa Mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Bonn Ujerumani.. (Picha zote na Evelyn Mkokoi wa ofisi ya Makamu wa Rais)

Article 22

ZSTC yastawisha upya zao la karafuu, Zanzibar.

$
0
0

 Zanzibar ni visiwa vinavyosifika kwa uzalishaji wa karafuu bora duniani. Katika miaka 30 ya nyuma pia ilisifika kwa uzalishaji karafuu nyingi, wastani wa tani 8,605 zilikuwa zikizalishwa kwa mwaka.

Jamii ya wakati huo walikuwa wakizijali, wakizithamini na wakizipenda sana karafuu ukilinganisha na kizazi cha sasa. Walihakikisha karafuu zao wakiuza vituoni tena zinakuwa safi, zimekauka vizuri na zinapata daraja la kwanza.

Katika miaka hiyo zao la karafuu lilikuwa ndiyo tegemeo kubwa la pato la kiuchumi katika visiwa vya Zanzibar.  Pato la Serikali lilitegemea sana zao hilo na kuiwezesha kuenedesha mipango yake ya kiuchumi na kijamii bila ya kuyumba. Hali hiyo ilitokana na ukubwa wa soko la dunia na ubora wa kipekee wa karafuu za Zanzibar katika soko hilo.

Lakini kwenye miaka ya 1990, hali ya soko haikuwa nzuri sambamba na kushuga kwa bei na kuongezeka kwa nchi zinazozalisha karafuu duniani na hivyo kuleta ushindani wa kibiashara.

Kushuka kwa bei katika soko la dunia kulipelekea kushuka kwa ari ya  uzalishaji kwa wakulima na kupelekea visiwa vya Zanzibar navyo kupoteza muelekeo wa zao hili. Zao hili lilipoteza hadhi yake ya kuwa zao la uchumi wa nchi.


Wakulima wengi waliacha kulima zao la karafuu na badala yake walijihughulisha na mazao mengine ukiwemo ukulima wa mwani ambapo wakati huo ulionekana kama ungelikuwa mbadala wa zao la karafuu.

Lakini pamoja na kuyumba kwa soko la dunia, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, iliendelea kununua karafuu kutoka kwa wakulima, ingawa si kwa bei ya kiwango cha juu. Serikali ililazimika wakati mwengine kufidia gharama za bei katika kuona mkulima ambaye ni mwananchi anaendelea kujenga imani na kulithamini zao la karafuu.

RAIS KIKWETE AKUTANA NA MJUMBE MAALUM WA RAIS WA AFRIKA KUSINI LEO IKULU DAR ES SALAAM

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Mjumbe Maalumu wa Rais Jacob Zuma wa Afrika kusini ambaye pia ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Mama Maite Nkoana-Mashabane Ikulu jijini Dar es salaam leo Mei 6, 2014.  Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernad Membe alikuwepo pia

PUBLIC LECTURE BY PROFESSOR YASH TANDON

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI AFUNGUA RASMI SEMINA YA WACHIMBAJI WADOGO KIBARA, MKOANI MARA

$
0
0
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akifungua mafunzo ya wachimbaji wadogo yaliyofanyika Kibara, mkoani Mara. Pia semina hiyo ilishirikisha viongozi wa vijiji, vyama pamoja na madiwani lengo likiwa ni kuwapa uelewa wa sheria na kanuni za uchimbaji wa madini. Aliyekaa katikati ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara Mhe. Kangi Lugora. Kushoto ni Kamishna Msaidizi – Uendelezaji wa Uchimbaji Mdogo Mhandisi Fredy Mahobe.
Mtalaamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi akiwasilisha mada wakati wa semina hiyo.
Mtaalamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi akisisitiza jambo wakati wa mafunzo hayo.
Naibu Waziri wa Nishati na Madini anayeshughulikia masuala ya madini Mhe. Stephen Masele akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wachimbaji wadogo mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo.
Sekretarieti ya maandalizi ya semina hiyo ikiwajibika.
Baadhi ya wajumbe wakifuatilia mada iliyokuwa ikiwasilishwa na mwezeshaji kutoka Wizara ya Nishati na Madini Mhandisi Kungulu Kasongi (hayupo pichani)

WIZARA YA UCHUKUZI YAADHIMISHA SIKU YA MAZINGIRA KWA KUFANYA USAFI NA KUPANDA MITI YA KUZUIA MMOMOMYOKO WA ARDHI KWENYE ENEO LA BANDARI YA DAR ES SALAAM LEO

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Rasilimali Watu wizara ya Uchukuzi, Bw. Issa Nchasi, akifanya usafi katika eneo la bandari ya Dar es Salaam kama sehemu ya maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani ambayo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’.
Sehemu ya wafanyakazi wa Wizara ya Uchukuzi na taasisi zake wakiwa kwenye zoezi la usafi wa mazingira katika eneo la Bandari ya Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya siku ya Mazingiza Duniani.
Mkurugenzi wa Idara ya Usalama na Mazingira wa Wizara ya Uchukuzi, Bi, Tumpe Mwaijande (kulia), akipanda mti katika eneo la bandari ya Dar es Salaam leo asubuhi, kama sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Mazingira. Maadhimisho ya Wiki ya Mazingira yanafanyika kitaifa mkoani Mwanza ambapo kwa mwaka huu kauli mbiu ni ‘Tunza mazingira ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi Tanzania’. (Picha na kitengo cha mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

Uzinduzi wa Matangazo ya Televisheni ya Dijitali kwenye Manispaa ya Mji wa Kahama

$
0
0
Muonekano wa mtambo wa kurusha matangazo ya televisheni ya Dijitali uliosimikwa ardhini kwenye mlima wa Igalilimi uliopo mji wa Kahama. Kampeni ya Elimu kwa Umma kwa wakazi wa mji wa Kahama imefanyika na kukamilika kwa kufanya uzinduzi rasmi wa matangazo mwishoni mwa Mwezi Mei, 2014. Picha na taarifa na Prisca Ulomi, Msemaji wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia

Channel ten imeanza kipindi cha DK 45 cha KUELEKEA KOMBE LA DUNIA

$
0
0
 Channel ten imeanza kipindi cha DK 45 cha KUELEKEA KOMBE LA DUNIA ambacho kinatoka kila siku saa 12 jioni na kinarudiwa siku inayofuata saa 6 mchana. Kipindi hicho kinaongozwa na EZEKIEL MWAMBOPO, OREST KAWAW wakishirikiana na DR LIKY katika uchambuzi wa kina kwa kila kundi lenye timu shiriki katika kombe la Dunia mwaka huu nchini Brazil.

Reminder: THE BEAT FESTIVAL TOMORROW 6TH OF JUNE @ TRINITI

$
0
0
THE BEAT FESTIVAL 
FRIDAY 6. June - 20.00-02.00 
Venue: Triniti, Msasani rd. 26, Oysterbay DSM
Entrance: 10.000 tsh only

Lineup:

SWAHILI ALLY – traditional / afrofusion – 21.00
Swahili Ally is a talented Tanzanian singer and songwriter whose talent first appeared in primary school. He was born in 1989 in Tanga region where he grew up in a musical family. He sings in the Digo language mixed with Swahili. The vibrant performance, which fuses Tanzanian traditional music with a unique contemporary edge, delivers a memorable performance and powerful message to audiences every time.

ASHIMBA – Unplugged – afrofusion / traditional – 22.15
Ashimba is one of Tanzania´s most talented singer songwriters. He has a passion for intricate and complex compositions. His sound borrows from the West African griot traditions fused with his own unique style of playing guitar coupled with Swahili, and Sukuma compositions. He has toured in Europe several times and has recently figured in the European World Music Charts.

MZUNGU KICHAA – world / reggae – 23.00
Mzungu Kichaa has not performed at THE BEAT for a while. He will perform a launch concert for his new EP Relax, which will be available in physical format at the venue. The first single “Relax Your Mind” has already made it to number one of the World Music Charts on ethnocloud. The recordings represent his first recordings that he has recorded in the studio with his Tanzanian band Bongo Beat.

ABOUT THE BEAT

The Beat is a monthly festival that takes place on the first Friday of the month, showcasing the best live music from Tanzania and abroad. The festival is hosted by Mzungu Kichaa and is powered by: Caravan Records, Triniti, and Goethe Institut Tanzania. 

Espen Sorensen
- Mzungu Kichaa 
& Caravan Records

congratulatory message to H.M Queen Margrethe II of Denmark on the occasion to celebrate the Constitution Day of Denmark

$
0
0
H.E Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message toH.M Queen Margrethe II of Denmark on the occasion to celebrate the Constitution Day of Denmark on 5th June 2014.


“Your Majesty Queen Margrethe II,

   The Queen of Denmark,

   Copenhagen,

   DENMARK.
It is my pleasure on behalf of the people and the Government of the United Republic of Tanzania to extend to Your Majesty and through you to the people of Denmark my heartfelt congratulations on the occasion to celebrate your Constitution Day.
The celebration of your Constitution Day offers me yet another opportunity to reiterate my personal commitment and that of my Government to working with you and your Government in strengthening further the close and historic relations that happily exist between our two countries and peoples.

Please accept, Your Majesty, my best wishes for your continued good health and peace and prosperity for the people of Denmark. 

Issued by the Ministry of Foreign Affairs and International Cooperation of the United Republic of Tanzania,

Dar es Salaam 

5thJune 2014

YOUTH TRAINING PROGRAMME

Zanzibar itaendelea kuthamini misaada ya Serikali ya Misri - Maalim seif

$
0
0
Na Hassan Hamad, OMKR.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itaendelea kuthamini misaada inayotolewa na Serikali ya Misri katika kuendeleza na kukuza uchumi wa Zanzibar. Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameeleza hayo ofisini kwake Migombani, wakati akizungumza na balozi mdogo wa Misri anayemaliza muda wake balozi Walid Ismail. 
Amesema Serikali ya Misri imekuwa mstari wa mbele kuisaidia Zanzibar katika nyanja mbali mbali za kiuchumi na ustawi wa jamii zikiwemo elimu, afya na kilimo. 
Aidha amesifu mchango wa balozi huyo katika kipindi chake cha utumishi kwa kufanya mambo mengi mazuri yanayohitaji kuendelezwa na mwenzake atachukua nafasi yake hapa nchini. Maalim Seif amesema mbali na balozi huyo kumaliza muda wake wa utumishi hapa nchini, bado anayo fursa na kuchangia maendeleo ya Zanzibar kwa kuwa balozi mzuri wa kuitangaza Zanzibar nje ya nchi, sambamba na kuwahamasisha wawekezaji na watalii kuja kuitembelea Zanzibar. 
Mhe. Maalim Seif pia alitumia fursa hiyo kuipongeza Misri kwa kufanikisha uchaguzi wa Rais kwa amani na utulivu, na kuelezea matumaini yake kuwa wananchi wa nchi hiyo wataendelea kuishi kwa amani na usalama. 
Nae balozi mdogo wa Misri anayemaliza muda wake wa utumishi hapa nchini balozi Walid Ismail, amesifu ushirikiano alioupata kutoka kwa viongozi na wananchi wa Zanzibar katika kutekeleza majukumu yake ya kibalozi. 
Amesema Zanzibar ni kituo kizuri cha kufanyia kazi kutokana na ukarimu wa watu wake, pamoja na kuwepo amani na usalama kwa wakati wote. Balozi Walid Ismail ameahidi kuwa akiwa nje ya Zanzibar ataendelea kuthamini mafanikio aliyoyapata ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa uhusiano kati ya Zanzibar na Misri. 
Akihitimisha mazungumzo yake, balozi Walid alimkabidhi Makamu wa Kwanza wa Rais, zawadi maalum kama ishara ya ushirikiano mwema kati yake na viongozi pamoja na wananchi wa Zanzibar.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiongozana na balozi mdogo wa Misri anayemaliza muda wake balozi Walid Ismail, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani.
 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza na balozi mdogo wa Misri anayemaliza muda wake balozi Walid Ismail, ofisini kwake Migombani.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akipokea zawadi kutoka kwa balozi mdogo wa Misri anayemaliza muda wake balozi Walid Ismail, baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika ofisini kwake Migombani. (Picha na SAlmin Said, OMKR).

kutoka bungeni dodoma leo

$
0
0
Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Wabunge Mhe Zainab  Kawawa wa Viti Maalum (kushoto), Sylivester  Mabumba wa Dole (wapili kushoto), Mhe. Vita Kawawa wa Namtumbo na Mwanaharakati wa Haki za Wanawake na Watoto, Mama Terry Gbemudu (kulia) kwenye viwanja vya Bunge Mjini Dodoma leo

LUPITA NYONG’O NA FAMILIA YAKE KUTUA TAMASHA LA 17 LA ZIFF

$
0
0
*Geneviveve Nnaji na John Dumelo nao ndani
*Habib Koite, Didier Awadi kuburudisha
*Filamu ya Mandela kufungua pazia
DSC_0021
Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando (wa pili kulia) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kuzindua rasmi Tamasha la Filamu la nchi za Majahazi la 17 maarufu kama Zanzibar International Film Festival (ZIFF). Kulia Msaidizi wa Kitengo cha habari ZIFF, Lara Prieston, Kushoto ni Meneja wa Tamasha la ZIFF, Daniel Nyalusi (Dean), Afisa Mawasiliano wa ZIFF, Hassan Musa "Has T" (wa pili kushoto) na Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala (katikati). 
--------------------------------------------------------------------
Na Andrew Chale
DUNIA inatarajia kushuhudia tukio kubwa na la kihistoria ndani ya viunga vya Ngome Kongwe ndani Mji Mkongwe wa Stone Town, Unguja, kwa watu wa mataifa yote watakapoungana na kushuhudia ‘Hatma ya Pamoja’ (A common Destiny) Juni 14 hadi 22, 2014, katika Tamasha la Kimataifa la filamu la Zanzibar (ZIFF).
Tamasha hilo maarufu kama filamu la nchi za Majahazi ZIFF, kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika kwa mara ya 17, tokea kuanzishwa kwake.
Akizungumza mapema leo jijini Dar es Salaam, kwenye halfa maalum ya uzinduzi wa tamasha hilo la 17, kwa wandishi wa habari iliyofanyika Goethe Institut kituo cha utamaduni, Mkurugenzi Mkuu wa tamasha hilo, Profesa Martin Mhando, alisema tamasha hilo msimu wa mwaka huu linatarajiwa kuwa moto kwani linakuja na mambo mbalimbali yenye kuleta mabadiliko ya hali ya juu.
Ni kutokana na mabadiliko hayo, Profesa Mhando anasema tasnia ya filamu kwa Tanzania inahitaji kubadilika ikiwemo wasanii wenyewe kujituma na hata kuingia darasani ili kufanya kazi zenye uhakika.
Akimaanisha kila msanii wa filamu aweze kufikia malengo yake, hana budi kujifunza na kushirikisha wale waliotangulia katika tasnia hiyo.
Anazungumziaje kaulimbiu ya ‘A Common Destiny’
Prof. Mhando amesema kauli mbiu ya mwaka huu yenye kusema Hatma ya pamoja yenye maana ya ‘A common Destiny’, ina lengo la kuwakutanisha watu wa mataifa mbalimbali kuwa kitu kimoja na kufurahia kwa pamoja ikiwemo kubadilishana mawazo kwa pamoja kwa tasnia ya filamu, muziki, kwa mlengo ya kujenga.
“Tukiwa na haja moja, kuishi kwa amani na kuleta mapinduzi ya kiuchumi, kifikira na maendeleo kwa amani, ZIFF kwa kutumia dira hiyo hasa kupitia filamu zetu za ndani zenye mchanganyiko wa utamaduni na asili yetu.
“Wazanzibari na hata wageni watakaoshuhudia filamu hizi wataweza kuchukua utamaduni huo na kuupeleka nje kwa furaha kubwa katika kufikia hatma ya pamoja” amesema Prof. Mhando.
DSC_0082
Music Coordinator wa ZIFF, Edward Lusala akisisitiza jambo wakati wa mkutano na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na wasanii watakaotoa burudani kwenye tamasha hilo.
Lupita-Nyong-o-729-620x349
Lupita Nyong’o, Genevieve ndani ya nyumba
Tukio kubwa ambalo kwa sasa Tanzania hasa kwenye viunga vya Zanzibar  na nchi nyingine duniani katika tamasha hilo la 17, ni ujio wa msanii wa Kenya na Mexico, Lupita Nyong’o, atakayeudhuria utoaji wa tuzo hizo za ZIFF mwaka huu.
Lupita ambaye ametwaa tuzo za Oscar na nyingine nyingi na kupelekea kutikisa Hollywood kwa sasa ni miongoni mwa mastaa watakaokuwa kwenye tamasha hilo huku akitarajiwa kuambatana na wazazi wake wote wawili pamoja na wadogo zake.

Hisia ndani ya Mwanza Jumamosi

$
0
0
This saturday @JB MWANZA Level 9 there will be a performance from @hisiatz along side @zarryedosha from JB Band with an international Tanzanian Comedian @captain_khalid, you dont wanna miss this for only Tsh 5,000 , for tickets and more info contact 0653428787

UBALOZI WA CANADA & BGP INTERNATIONAL TANZANIA LIMITED WAKULETEA MNADA WA HADHARA:

$
0
0
 UNIVERSAL AUCTION CENTRE Kwa idhini waliyopewa na Ubalozi wa Canada & BGP International Tanzania Limitedwatauza kwa mnada wa hadhara  Magari & Fanicha za Ofisi na nyumbani tarehe 7 Juni, 2014 Jumamosi saa 4.00 asubuhi. Mnada utafanyika Golden Resort Sinza,  Lion Street, Dar es salaam.
MALI ZITAKAZOUZWA:Sofa sets, Chest drawer, Recliner, Dressers, Garden chairs, Coffee table, Book shelve, Meza za ofisi/viti, File cabinets, Vitanda ,Magodoro, Fridges, Freezer, Cookers, TV set, Washer, Dryer, Computer set, Photocopy m/c,  A/c split units Etc.

MAGARI YATAKAYOUZWA:

Idadi

Aina

Model

Mwaka

Ushuru

5

Isuzu P/Up Double cabin

 4JB1 Diesel engine, 4 Wheel drive

2006

Bado

1

Toyota Rav4

S/Wagon Petrol engine, 4 Wheel drive

1999

Tayari

1

Toyota mark11

GX81 Petrol engine

1988

Tayari

1

Bajaji Tricycle

TVS 4 stroke

2010

Bado

1

Suzuki Escudo  

Petrol engine, 3 door.

1993

Tayari

Mali zote zinaweza kukaguliwa Golden Resort Sinza,Lion Street tarehe 5 na 6 Juni,  2014 kuanzia saa 4.00. asubuhi mpaka saa 10.00 jioni.

 MASHARTI YA MNADA:
  1. Mnunuzi  wa fanicha atatakiwa kulipa malipo yote pale pale. Na mnunuzi wa Gari atatakiwa kulipa 25% pale pale na salio lilipwe ndani ya siku 7 ukishindwa kulipa kwa muda huo gari litauzwa tena na dhamana haitarudishwa.
  2. Mali zote zitauzwa kama zilivyo.
  3. Mnunuzi atawajibika kulipa ushuru.
  4. Mali yote iliyouzwa itatakiwa kuondolewa siku hiyo hiyo  baada ya kulipia malipo yote pamoja na ushuru

Kwa maelezo zaidi waone:
UNIVERSAL AUCTION CENTRE
NKRUMAH STREET
MKABALA NA CO-CABS

SIMU NA:  0754-284 926, 0757 284 926               Email : universalauction@hotamail.com


DAR ES SALAAM.

Karibu kiwanja cha Via Via jijini Arusha Jumamosi hii

$
0
0
Kwa buku mbili tu za kitanzania Karibu kiwanja cha Via Via jijini Arusha Jumamosi hii tarehe 7 mwezi wa sita mwaka 2014, saa sita mchana hadi moja jioni kujipatia burudani ya muziki toka kwa Vatoloco soldiers, JohnRodgers,Xtra talent, Mafaya Faya, Ima B & Flaxman, BadSpenders, Machiz Flani, Mwaka Mzima, Son, Jambo culture, Mr Right, Son B, Adorabo na wengine kibao powered bywww.vmgafrica.com
Viewing all 110029 articles
Browse latest View live




Latest Images