Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109592 articles
Browse latest View live

SHIRIKA LA UNDER THE SAME SUN LATOA PONGEZI KWA UONGOZI WA MKOA WA RUKWA KWA KUFANIKIWA KUWAKAMATA WATUHUMIWA WALIOMKATA MKONO MLEMAVU WA NGOZI (ALBINO) NA KIZIBITI HICHO

0
0

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella Manyanya (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wa shirika linalotetea haki za watu wenye ulemavu wa ngozi nchini (Albino) Vicky Mketema kulia na wajumbe wenzake wa shirika hilo watatu waliosimama nyuma. Kulia waliosimama ni katibu wa Mkuu huyo wa Mkoa Frank Mateni na kushoto aliyekaa ni Afsa maendeleo ya jamii Mkoa wa Rukwa Deonisya Njuyui.
 
Mama Maria Chambanenge mlemavu wa ngozi anayenyonyesha mtoto wa miezi mitano alikatwa mkono na watuhumiwa ambao wameshatiwa nguvuni na jeshi la polisi Mkoa wa Rukwa na Mkono wake uliokatwa umeshapatikana. Upelelezi bado unaendelea kuwapata watuhumiwa zaidi wanaohusika na vitendo hivyo. 
 
Mkurugenzi wa shirika la under the same sun Vicky Mketema ametoa pongezi za dhati kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa kwa kushughulikia tatizo hilo kikamilifu na kwa haraka na kufanikiwa kupata kiungo hicho na watuhumiwa waliohusika kwa muda wa siku mbili. Alisema endapo mikoa yote ingekuwa inashughulikia matatizo kama hayo kwa muda mfupi kama huo basi uhalifu na namna hii ungekuwa umeshatoweka nchini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Rukwa ametoa onyo kali kwa wale wote watakaohusika na vitendo vya uvunjifu wa amani Mkoani humo ambapo amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kwa vyombo vya ulinzi pale wanapowashuku wahalifu wa vitendo hivyo. Amewato hofu wananchi kwani vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwa ajili yo.

Muathirika huyo anaendelea kupata huduma za matibabu katika Hospitali Kuu ya Mkoa wa Rukwa na hali yake inaendelea vizuri.Picha Na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa 

Rais Kikwete na Maaskofu wa KKKT jijini Arusha

0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Maaskofu wa Kanisa la kiinjilki la Kilutheri Tanzania (KKKT) muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya Mazishi ya Marehemu Askofu Dkt.Thomas Laizer ilkiyofanyika katika usharika wa mjini Kati jana jioni.(picha na Freddy Maro).

ZIARA YA MAMA SALMA KIKWETE yaendelea leo mkoani lindi

0
0
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na wananchi wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo, Feb 16, 2013.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimiana na watoto wa kijiji cha Narunyu, Kata ya Tandangongoro, alipokwenda kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji hicho leo, Feb 16, 2013.
 Mkazi wa Kijiji cha Ng'apa wilaya ya Lindi mjini, akionyesha kadi yake ya matibabu ya Huduma ya Kadi ulkiopo chini ya Bima ya Afya, wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika kijiji hicho, leo Feb 16, 2013. Mama Salma Kikwete alimpatia fursa ya kuzungumza wakati akihimiza umuhimu wa wananchi kujiunga na mpango huo wa matibabu.
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwa amegoma kushuka katika gari lake, kukataa kwenda kwenye mkutano wa ndani wa Chama Kata ya Tandangongoro, uliokuwa umepangwa na viongozi wa kata hiyo kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya msingi ya kijiji cha Ng'apa, mkoani Lindi, leo Februari 16, 2013. Hatua hiyo iliwalazimu viongozi kutafuta ukumbi mwingine wa dharura. Mama Salma alisema si sahihi mkutano wa ndani wa Chama cha siasa kufanyika katika chumba cha darasa la shule ya serikali
Umati wa wananchi wa Kijiji cha Ng'apa wakimsiliza Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akilipowahutubia mkutano wa hadhara leo, Feb 16, 2013. PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO).

Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki Meets with tourism stakeholders in Arusha

0
0
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (with mic) addressing tourism stakeholders in Arusha.
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (with mic) addressing tourism stakeholders in Arusha.
TANAPA representatives at the stakeholders meeting.
Tourism Stakeholders in the country listening attentively to the Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki

Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (left) greets the former government minister Basil Mramba during the meeting.
Minister for Natural Resources and Tourism Hon. Ambassador Khamis Kagasheki (left) greets the former government minister Basil Mramba during the meeting.Director of Tanzania Tourist Board Dr. Aloyce Nzuki (right) paying attention to some of the tourism stakeholders during the meeting.
Director of Tanzania Tourist Board Dr. Aloyce Nzuki (right) paying attention to some of the tourism stakeholders during the meeting
Former Minister Basil Mramba talking to TANAPA officials Dr. Ezekiel Dembe, Acting Director of Touris_ (second left)_ Johnson Manase, Tourism Manager and Alphonce Akarrow, CIA(1)
Former Minister Basil Mramba talking to TANAPA officials Dr. Ezekiel Dembe, Acting Director of Touris; (second left); Johnson Manase, Tourism Manager and Alphonce Akarrow, CIA
Minister for Natural Resources Hon. Ambassador Khamis Kagasheki in a jovial mood with the CEO of Leopard Tours Mr. Fazal
Minister for Natural Resources Hon. Ambassador Khamis Kagasheki in a jovial mood with the CEO of Leopard Tours Mr. Fazal.
NCAA Public Relations Manager Adam Akyoo (right) talking to Paul Srakikya (middle) who is the Assistant Director of Ant poaching in the Ministry.
NCAA Public Relations Manager Adam Akyoo (right) talking to Paul Srakikya (middle) who is the Assistant Director of Ant poaching in the MinistryTTB Managing Director Dr. Aloyce Nzuki and Kibo Palace Hotel Marketing Manager Charity Githinji were also there to attend Tourism Stakeholders meeting.
TTB Managing Director Dr. Aloyce Nzuki and Kibo Palace Hotel Marketing Manager Charity Githinji were also there to attend Tourism Stakeholders meeting.

gado leo

ITIFAKI YA AMANI NA USALAMA YA EAC YASAINIWA

0
0
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akiweka saini Itifaki ya Amani na Usalama ya Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Uwekaji saini huo ulifanyika katika Hoteli ya New Africa, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Membe (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wenzake wa nchi za EAC wakiwa wameshikilia Itifaki hiyo mara baada ya kusainiwa
Mhe. Membe akipitia Itifaki hiyo kabla ya kusainiwa huku Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa akishuhudia.
Mhe. Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wake Bw. Haule. Mwingine katika picha ni Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.
Picha nyingine ya Mhe. Membe na Katibu Mkuu wake Bw. Haule na wajumbe wengine waliohudhuria mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt. Richard Sezibera (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi wa Uganda.
Mhe. Membe akifanya mahojiano na Waandishi wa Habari baada ya shughuli ya utiaji saini kukamilika.
Picha zaidi za mahojiano kati ya Mhe. Membe na Waandishi wa Habari.

sakata la uchaguzi TFF sasa lafika patamu,Rais Tenga asema hana uwezo wa kuingilia maamuzi ya kamati

0
0
Rais wa TFF, Leodegar Tenga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo juu ya sakata la uchaguzi mkuu wa TFF,kwenye ukumbi wa mikutano uwanja wa taifa.

SAKATA la uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limefika patamu baada ya rais wa TFF, Leodegar Tenga kudai kuwa yupo tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali kwa walioenguliwa kuomba upya marejeo (review) ya rufaa zao.

Tenga ambae juzi alikuwa na kikao kizito na kamati zake za uchaguzi kabla ya leo asubuhi kuwa na kikao kingine Wizarani,alisema binafsi hana uwezo wa kutengua maauzi ya kamati zake kwa kuwa ni huru lakini yupo tayari kutoa muongozo kwa atakayetaka ili aweze kufanikiwa kupata haki yake.

Akizungumza na Wanahabari jijini Dar es Salaam leo, Tenga alisema kuwa kwa mujibu wa katiba yua TFF kamati ya rufaa ndiyo ya mwisho katika maamuzi lakini mlalamikaji anaweza kuomba marejeo ili kutafuta haki yake.

"Jambo la kwanza mtu kama hajaridhika na uamuzi anaweza kuomba review(Marejeo) katika kamati ya rufaa, majibu yatakayopata kama hajaridhishwa tena anaweza pia kupeleka malalamiko yake Shirikisho la Soka la Dunia (fifa) na tatu ni kwenda CAS (mahakama ya usuluhishi).

"Jambo hili linazungumza kinazi zaidi watu hawaangalii katiba inasemaje, lugha za kejeli zimekuwa zikitumika kiasi kwamba maamuzi yaliyofanywa tunaonekana kana kwamba sisi wote ni wapumbavu, watu wanaotaka kutusaidia kukuza mpira wetu (wadhamani) hawawezi kuja kama kuna migogoro.

"Nipo tayari kufanya kila njia kuhakikisha tunatoa msaada kwa kila anayetaka kamati ya rufaa itakaa kesho kupitia review (marejeo) ya watu wawili ambao wameomba.

Tenga aliwataja walioomba marejeo ya rufaa hizo kuwa ni Jamali Malinzi ambaye alienguliwa kwa kigezo cha kukosa uzoefu wa miaka mitano kwenye masuala ya soka ikiwa ni pamoja na kupinga mabadiliko ya katiba ya TFF na Hamad Yahaya ambaye alienguliwa kuwania nafasi ya mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Kuu.

"Sisi tupo tayari kutoa msaada kwa ambaye hajaridhishwa na uamuzi wa kamati ya rufaa kwa kuwaelekeza taratibu zinazotakiwa kufuata katika kutafuta haki zao wanatakiwa kujenga nguvu ya hoja na si hoja ya nguvu,".alisema Rais huyo.

Kauli ya Tenga imekuja ikiwa ni siku chache baada ya kamati ya rufaa chini ya mwenyekiti wake Idd Mtiginjola kumuengua kwenye kinyang'anyiro cha urais katibu mkuu wa zamani wa Yanga Jamali Malinzi ambaye pia amepinga kuenguliwa kwake na tayari ameshawasilisha ombi lake la kutaka marejeo ya rufaa yake sambamba na mwenyekiti wa Mtibwa Sugar Hamad Yahaya ambaye naye alienguliwa kwenye kinyang'anyiro hicho ambacho alikuwa akiwania nafasi ya mwenyekiti wa bodi ya Ligi Kuu.

Wakati huo huo,Tenga alipangua hoja ya Katibu Mkuu wa zamani wa Fat sasa TFF Michael Wambura ambaye alidai katiba imesiginwa kwa TFF kuikiuka katika mchakato mzima wa kuifanyia mabadiliko.

Mapema wiki hii Wambura alitoa siku tatu kwa TFF kuhakikisha inaangalia upya suala la kuenguliwa kwa Jamali Malinzi na hadi Jumatatu kama rais Tenga angekuwa hajatoa kauli yoyote angeenda kufungua kesi mahakamani ili haki itendeke.

Alisema pia TFF ilikiuka katiba yao kwa kufanya marekebisho kwa njia ya waraka na pia kumdanganya msajili wa vyama vya michezo kuwa mkutano mkuu ulikaa Desemba 15 kitu ambacho si cha kweli huku kanuni za uchaguzi zikianza kutumika Januari 7 wakati katiba imepigwa muhuri wa msajili Januari 12 na kuiita katiba hiyo ni batili na mchakato mzima wa uchaguzi.

Akizungumzia suala hilo Tenga alisema "Kikao sio lazima tukae sasa hivi dunia imebadilika hata kwa njia ya mtandao watu mnafanya kikao tulitoa waraka kwa kupiga kura wanachama 70 walisema ndio na 33 wakasema hapana.

"Kamati yetu ya utendaji ndio ilipokea majibu ya waraka Desemba 15 na haraka ikaanza kutumika, hatukudanganya na barua tuliyopeleka Wizarani na taarifa za kikao zilisema hivyo.

Kuhusu kupigwa stop kwa uchaguzi wa TFF baada ya aliyekuwa mgombea wa nafasi ya urais Richard Rukambura kwenda mahakamani kwa kupinga kuenguliwa kwake Tenga alisema "Mpaka sasa mimi sijaona samsa ya mahakamani kwa hiyo siwezi kuzungumza lolote kwa sasa."

Azam yafanya kweli taifa leo,yaichapa el Nasir ya Sudan ya Kusini bao 3-1

0
0

 Kikosi cha el Nasir ya Sudan ya Kusini
 Kikosi cha Azam FC.
Kiungo wa timu ya Azam FC, Bolou Kipre (kushoto) akitafuta mbinu za kumtoka mshambuliaji wa El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Abdallmelik Sebit, wakati wa mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo Azam, imeibuka na ushindi wa mabao 3-1. Mabao ya Azam yamefungwa na Abdi Kassim, katika kipindi cha kwanza, na mabao 2 yamefungwa na Kipre Tchetche katika kipindi cha pili.
 Wachezaji wa Azam FC wakishangilia bao la pili la timu yao lililofungwa na Kipre Tchetche (katikati) wakati ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya El -Nasir ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. 
Kipre Tchetche (kushoto) akichuana kuwania mpira na beki wa Al-Nasri.
 Jabir Aziz akitafuta mbinu za kuwatoka mabeki wa El Nasir FC ya Sudan ya Kusini katika mchezo wa Kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
 Mshambuliaji wa Azam FC, Brian Umomy akiwatoka walinzi wa timu ya El-Nasir FC ya Sudan ya Kusini, Jacob Osuru na Abdallmelik Sebit katika mchezo wa kombe la Shirikisho uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa Azam, wakishangilia. Picha Zote na Dande JR

MKURUGENZI MKUU WA TAASISI YA ELIMU NCHINI ABWAGA MANYANGA

0
0
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania, Dk Paul Mushi (pichani) amejiuzulu wadhifa wake huo Kufuatia sakata kuwa Serikali haina mitaala rasmi ya kufundishia shuleni na Nafasi yake imechukuliwa na Mkurugenzi wa Idara ya kubuni na kuendeleza Vifaa vya Elimu, Dk. Leonard Akwilapo.

Akihojiwa na Mwandishi wetu kwa njia ya simu jana jijini Dar es Salaam, Dk. Mushi alithibitisha kujiuzulu na kusema alichukua hatua hiyo kwa hiari yake bila kushinikizwa na mtu.

"Hakuna aliyenishinikiza nimeamua mwenyewe kuandika barua ya kujiuzulu," alisema Dk. Mushi

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Dk. Akwilapo alipohojiwa juu ya mtangulizi wake aliyeachia ngazi , Alhamisi wiki hii, alisema aliondoka kwa maamuzi yake mwenyewe bila shinikizo kama alivyoeleza.

"Sio siri ni kweli amejiuzulu na aliniambia ni maamuzi yake aliyoyafanya ya kujivua madaraka ya Mkurugenzi Mkuu bila ya kugombana na mtu na juzi ndio alipewa barua yake na mimi kupatiwa barua ya kuwa kaimu," alisema Dk Akwilapo.

Katika mkutano wa Bunge la mwezi huu, Mbunge wa kuteuliwa na Rais James Mbatia (NCCR-Mageuzi), aliwasilisha bungeni hoja binafsi kuhusu udhaifu uliopo katika sekta ya elimu hapa nchini.

Katika hoja hiyo, aliibua sakata la kutokuwapo kwa mitaala inayoongoza ufundishaji wa masomo shuleni hali inayosababisha kudorora kwa elimu.

Kadhalika aliibua tuhuma za uchapishwaji wa vitabu ambavyo maudhui yake hayana viwango pia waliopewa kazi ya kuchapisha ndiyo hao waliokuwa wahariri na waandishi .

Pia alihoji sababu za uchapishaji wa vitabu hivyo kufanyika nje ya Tanzania hali ambayo inasababisha kuwapo kwa matumizi mabaya ya fedha .

Katika kujibu hoja hizo, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alilithibitishia Bunge kuwa serikali ina mitaala na nakala zake ziliwasilishwa bungeni na hoja hiyo ikazimwa.

Baada ya kuwasilishwa kwa mitaala hiyo, bunge iliunda kamati ya kujiridhisha kama ni kweli mitaala hiyo ni sahihi ambapo ilikuja na majibu ya kujiridhisha kuwa ni ya kweli.

Hata hivyo, kwa upande wa James Mbatia alisema bado kuna utata katika mitaala hiyo licha ya kamati hiyo kujiridhisha kuwa mitaala ipo sahihi.

CHANZO: NIPASHE

Waziri Mkuu Mizengo Pinda Alipokutana na Viongozi wa dini za Kikristo na Dini ya Kiislamu na kujadili mgogoro wa uchinjaji

0
0

 Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akijadili jambo na Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Ahmed  Ali (kushoto) na Sheikh wa msikiti wa Buswelu, Athumani Ali  katika kikao cha kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kati ya Waziri Mkuu na viongozi wa dini za Kikristo na Kiislamu kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013.
 Mkurugenzi wa Radio ya Kikristo ya jijini Mwanza ya Kwaneema, Askofu Mpemba akichangia katika kikao kati ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Viongozi wa dini za Kikristo na Dini ya Kiislamu cha kujadili mgogoro wa uchinjaji  wanyama kilichofanyika kwenye ukumbi wa Benki Kuu  jijini Mwanza Februari 16,2013.
 Sheikh Hasani Kabeke wa Mwanza  akichangia katika kikao cha klutatafuta muafaka kati ya Waislamu na Wakristo kuhusu uchanjaji wanyama kilichoitishwa na Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwenye ukumbi wa Banki  Kuu jijini Mwanza Februari 16, 2013
 Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kikristo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013.
 Viongozi wa madhehebu ya Dini ya Kiislam wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  wakati alipozungumza na Viongozi wa Dini ya Kiislam na Kikristo kujadili mgogoro wa uchinjaji wanyama kwenye ukumbi wa Benki Kuu jijini Mwanza Februari 16,2013.Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

RAIS KIKWETE ALIPOKWENDA ZIFARIJI FAMILIA ZA WALIOKUFA KATIKA AJALI YA GARI UBENA ZOMOZI

changamkieni punguo la gharama za umeme - Mama Kikwete

0
0
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akihutubia mkutano wa hadhara kijiji cha Mingoyo mkoani Lindi leo wakati akiwa katika ziara yake ya kukagua na kuimarisha uhai wa chama,Mkoani humo.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo.Picha na Bashir Nkoromo.

Na Anna Nkinda – Maelezo , Lindi

Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) taifa (NEC) Mama Salma Kikwete amewataka wakazi wa kijiji cha Kitumbikwela na Mingoyo wilayani Lindi mjini kuchangamkia punguzo la kuingiza umeme katika nyumba zao na kuepukana na gharama za mafuta ya taa ambazo zinapanda mara kwa mara.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mke wa Rais aliyasema hayo jana wakati akiongea kwa nyakati tofauti na wananchi hao katika ziara yake ya kichama ya kuwashukuru wanachama wa CCM kwa kumchagua kuwa mjumbe wa NEC kutoka wilaya ya Lindi mjini.

Alisema kuwa miaka ya nyuma gharama za kuweka umeme majumbani zilikuwa kubwa na kufikia shilingi milioni mbili na nusu lakini hivi sasa zimeshuka hadi shilingi laki nne na arobaini elfu fedha ambazo hata mwananchi wa kawaida anaweza akajiwekea akiba na kuzipata.

Mama Kikwete alisema, “Kuweka umeme katika nyumba yako si utajiri kwani gharama za uwekaji zimepungua ukilinganisha na miaka ya nyuma jambo la muhimu ni nyumba iwe imeezekwa vizuri na kuwekwa nyaya za kuingiza umeme ndani ya nyumba (wire ring).

Hata kama hauna hela unaweza kuweka akiba yako kidogokidogo kila mwaka pale unapouza mazao na baada ya miaka michache utakuwa umepata fedha yote, nawasihi wananchi wenzangu hakikisheni kuwa umeme utakapofika kijijini mnautumia kwani wenzenu wanatamani kuwa na umeme lakini bado haujawafikia”.

Aidha Mama Kikwete pia aliwashimiza wanawake wajitokeze kwa wingi katika miradi ya kukopa mbuzi lipa mbuzi na kopa ng’ombe lipa ng’ombe kwani wakipata fedha kidogo pamoja na za waume zao pato la familia litaongezeka na hivyo kujikwamua kimaendeleo.

Akiwa katika kijiji cha Mingoyo aliwasihi wazazi kuwalea vijana wao katika maadili mema na kuwaelekeza pale ambapo wanapokosea kwani utandawazi unawaharibu vijana wengi na kujikuta wanajiingiza katika matendo yasiyofaa ikiwa ni pamoja na utumiaji wa madawa ya kulevya na uvutaji wa bangi.

“Baadhi ya vijana wanaona fahari kuwa na wapenzi wengi jambo ambalo ni la hatari kwa kuwa unajiandalia mazingira ya kupata kirahisi maambukizi ya virusi vya Ukimwi na takwimu zinaonyesha kuwa kwa kila watanzania mia moja sita wanamaambukizi. Muache tabia hiyo na kufuata vitabu vitakatifu vya dini vinavyosema kwani ugonjwa huu hauna dawa zaidi ya dawa za kupunguza makali tu”, alisema Mjumbe huyo wa NEC .

Kwa upande wake diwani wa kata ya Mingoyo Jamridi Mandowa alisema kuwa tangu Serikali ilipotangaza kuanza kwa mradi wa kusambaza umeme vijijini, kupunguza gharama za ufungaji wa umeme majumbani na kusogeza muda wa kupokea maombi wananchi wamejitokeza kwa wingi kutuma maombi lakini kasi ya usambazaji ni ndogo hawaelewi tatizo ni kitu gani.

Naye Diwani wa Kata ya Msinjahili ambaye ni Meya wa Lindi Mjini Frank Magali alisema kuwa kata yake inamradi wa kopa ng’ombe lipa ng’ombe na kopa mbuzi lipa mbuzi ambapo kwa upande wa ng’ombe walipata majike nane na dume mmoja na kuwakopesha wananchi ambao kwa kiasi kikubwa wamenufaika na mradi huo.

Mama Kikwete alifanya mikutano ya hadhara na kujibu maswali ya wananchi wa kata za Msinjahili, Mingoyo na Mitandi na kuwakabidhi kadi wanachama wapya wa CCM 37, Umoja wa vijana 37, Umoja wa Wanawake 92 na Jumuia ya Wazazi 73.

Montage Charity ball 2013

Vodacom,HPSS zazindua mfumo mpya wa menejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF Iliyoboreshwa) kwa Mkoa wa Dodoma

0
0

  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala Za Mikoa na Serikali za Mitaa Aggrey Mwanri akihutubia hafla ya uzinduzi wa mfumo mpya wa menejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya Mfuko wa Afya ya Jamii ulioboreshwa (CHF Iliyoboreshwa) mjini Dodoma mwishoni mwa wiki. Kushoto ni Meneja wa Mradi wa HSPP Madfred Stroemer watekelezaji wa mfumo huo mpya kwa ufadhili mkuu wa Serikali ya Uswisi na Vodacom(katika mawasiliano).
  Naibu Waziri Mwanri akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dk. Rehema Nchimbi kadi ya uanachama wa mfuko wa Afya ya Jamii Ulioboreshwa - CHF muda mfupi baada ya kuzindua mfumo mpya wa nmenejimenti ya taarifa za bima kwa ajili ya mfuko huo utakaowezesha uandikishaji, ukusanyaji  na uwasilihaji madai ya malipo kwa wato huduma na ufuatiliaji wa taarifa za wanachama kwa njia rahisi ya kielekrtoniki kutumia mtandao wa Vodacom mjini Dodoma mwishoni mwa wiki.

WATU WATATU WASHIkiLIWA NA POLISI KUFUATIA MAUAJI YA PADRI EVARIST MUSHI-ZANZIBAR


wasanii wa Epiq BSS waifunika Dodoma

0
0

Mmoja wa Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search pichani shoto,Walter akionesha umahiri wake wa kuimba akiwa sambamba na msanii mwingine wa bongofleva ajulikanae kwa jina la Ben Paul,kwenye onesho lao la pamoja lililofanyika mwishoni mwa wiki  katika ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma.
 Mmoja wa Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search pichani shoto,Wababa akipongezwa na mmoja wa mashabiki waliofika kushuhudia onesho lao la pamoja lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma. 
 Mmoja wa Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya walioshiriki shindano la kuimba la Epiq Bongo Star Search pichani,Husna akiwapagawaisha mashabiki (hawapo pichani),kwenye onesho lao la pamoja lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma. 
 Mmoja wa wasanii mahiri wa bongofleva,Barnaba akiwaimbisha mashabiki wake( hawapo pichani) waliofika kushuhudia wakali wa Epiq Bongo Star Search walipofanya onesho lao  la pamoja lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma. 
Pichani ni baadhi ya mashabiki wakifurahia burudani nzuri iliyokuwa ikitolewa na wasanii walioshriki shindano la Epiq Bongo Star Search,lililofanyika mwishoni mwa wiki  kwenye ukumbi wa Club Maisha  mkoani Dodoma.

News alert: Balozi Mwanaidi Sinare Maajar ateuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia

0
0
Flashback: Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mh. Mwanaidi Maajar akiwa katika picha ya pamoja na Rais wa Marekani Barack Obama mara baada ya kukabidhi hati ya utambulisho wa Balozi wetu huyo nchini humo tarehe 16.09.2010


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Balozi Mwanaidi Sinare Maajar kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR) kilichopo Kurasini Jijini Dar es Salaam.


Aidha, kufuatia uteuzi huo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard Kamillius Membe (Mb.) amewateua Wajumbe wa Bodi hiyo kuwa ni:-


1.           Bw. Dushhood M. K. Mndeme

2.           Mhe. Balozi Abdi Mshangama

3.           Mhe. Dkt. Leonidas Mushokolwa

4.           Mhe. Dkt. Harold Utouh

5.           Mhe. Saidi Mtanda (Mb.)

6.           Mhe. Betty Machangu (Mb.)

7.           Bw. Affan Othman Maalim

8.           Bw. Abdurahaman Abdallah


Uteuzi wa Mwenyekiti na Wajumbe hao ni kwa kipindi cha miaka mitatu (3) kuanzia tarehe 22 Januari, 2013 hadi tarehe 21 Januari, 2016.

  
IMETOLEWA NA: WIZARA YA MAMBO YA NJE NA


USHIRIKIANO WA KIMATAIFA, DAR ES SALAAM


15 FEBRUARI, 2013







mrisho mpoto apania kurejesha msisimko wa maigizo ya jukwaani

0
0
 Mrisho Mpoto akiigiza kama FALSTAFF na kulia ni Bw Ogutu Mulaya, alie tafasiri mchezo huu kwa Kiswahili, akicheza kama Bi Quickly. 

 Mrisho Mpoto akiwa na waigizaji wenzake kutoka Kenya ambao waliigiza kama WANAWAKE WA HERI WA WINSA  wakionesha umahiri wao katika Ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.


Kulia kabisa ni Bw Ogutu Mulaya, alie tafasiri mchezo huo kwa Kiswahili, akiigiza na wenzake huku akiwa kwenye husika nyingine.



Mrisho Mpoto ni moja kati ya wasanii wakubwa wa Muziki na Maigizo ya Jukwani hapa nchini. Michezo hii ya jukwaani ambayo ni adimu na adhimu sana hapa nchini kutokana na umakini na utaalaam mkubwa unao hitajika katika uandishi, uongozaji na hata uchezaji jukwaani.


Hapa nchini kuna wasanii wachache wenye uwezo wa kutimiza hatua zote za maandalizi ya mchezo wa jukwaani. Tumekuwa tukishuhudia  wataalam walio pikwa kutoka Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo na wale wa Chuo kikuu cha Mlimani katika Idara ya Sanaa na Maonesho na Chuo kikuu Huria wakishughulika sana na tasnia hii.


Baada ya kuona Tasnia hii inasua sua, Bwana Mrisho Mpoto aliamua kwa dhati kurudisha heshima ya michezo hiyo kwa kuishawishi kampuni inayo jishughulisha na Maonesho ya Jukwaani ya nchini Kenya Kuuleta mchezo ulio jipatia umaarufu mkubwa kwenye nchi mbali mbali ulimwenguni na hata kupata heshima ya nyota tano nchini Uingereza ambapo Mrisho yeye mwenyewe akiucheza mchezo huo kama mhusika mkuu.


TAARIFA YA HITMA

DEBATE ON DEMOCRACY: Where Are We Planning To Go, Who Is To Lead Us There?

0
0

By Mdau Tuntufye
A true democracy will come from our people; if our people will value every single vote, we can move forward.  If every single individual will value a vote more than a precious stone, and consider it as, as valuable as an investing asset, our society can dismantle the vicious cycle of poverty. What if our people value a vote for only TZS 10,000, or for exchange of some token things? I'm afraid to say that majority of our people do not know whether there is a better life outside of what they live now, that is why, may be, they are easily ensnared by greedy culprit political aspirants. 

This is a fundamental problem. You can’t make a concerted effort for something you don’t aspire. Our aspirations drive and motivate us not only to work hard in anyhow but to stick to well- thought strategies, policies and plans. Our people should understand themselves that they are poor, therefore, should aspire for a better future and be determined to move out of the current condition. Here is where the power of vote or people’s power comes in, well informed people can decide about their own destiny.  

Outside of this, it is a deception and a self destructive means towards a true democracy. "People power" refers to the peaceful social revolution. Otherwise it is a manipulation of people’s mind by taking advantage of their ignorance and problems facing them.


A true change can’t be brought by mobilizing underprivileged groups to rally in the streets, yes it can be, but not a plausible solution. Let’s start with a very crucial things here, let’s educate our people how to exercise the true power, the power of the vote.  

It is really  absurd to see some media posting names of the so called presidential candidates for 2015 without telling us what exactly are they going to do. Let’s go back to the Mwalimu’s suggestions, let’s discuss problems that are most binding constraints to our societies before we discuss names of candidates. What are the critical problems that face Tanzania so far, then who are the suitable candidates to take us through those problems facing us? Here is where we can exercise our power. Mwalimu suggests that everyone should be honest and be convinced in his/her conscience about the true candidate to solve our problems, otherwise no one to blame, and if we will be still poor, it’s because we made that choice.


The fate of better life is in our votes, we are responsible for success and failure through our votes. It is real very sad to see most Tanzanian media never discussing about major issues, like what are the current economic, social and political status, then who, do we think can mobilize us together with our resources to make a move forward. Surprisingly, our media never discuss about strength and weakness of who in their perspective they think are the candidates for presidential election 2015. What you happen to see in newspapers, is only nicely painted names without any critical analysis of why do they think those candidates are suitable. 

Wake up guys, stop painting names, help Tanzanians to get a true partisan and son of Tanzania, who is free from, and not entangled in any enslavement, be it religious, ethnic, political, hatred or “mtandao.” At once, Mwalimu said, we need a person who knows that State House is not a place for doing business, neither a place for celebrity nor show off.  Rather, it is a place for carrying Tanzanians’ burdens, a place for someone striving to relieve Tanzanians from these burdens. We need a person who is globally competent and his/her first priority is Tanzania’s interest.


 It’s your role, you media people to help Tanzanians to identify who is that candidate, so that our people would have informed decision to exercise people’s power in their honesty through voting. Expose to us the strengths and weaknesses of people you paint on newspapers and other media and match with our problems whether these people are capable of solving them, then we can decide.



Viewing all 109592 articles
Browse latest View live




Latest Images