Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 446 | 447 | (Page 448) | 449 | 450 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Na Mwandishi Maalum

  Touch Foundation , Taasisi isiyo ya kiserikali na yenye makao yake nchini Marekani, mwishoni mwa wiki (Mei 8), imeadhimisha miaka kumi ya kazi zake na kuahidi kuendelea kushirikiana na serikali ya Tanzania na Taasisi nyingine katika uboreshaji na uimarishaji wa sekta ya afya nchi.

  Katika hafla iliyojulikana kama Asante Supper 2014, ilihusisha pia utoaji wa tuzo kwa wadau mbalimbali ambao wamekuwa nguzo muhimu ya Taasisi hiyo. Asante Supper ilihusisha pia harambee ya uchangishaji wa fedha kwaajili ya kusaidia sekta hiyo ya afya. Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi wa Morgan Library Museum, Jijini New York.

  Akiwakaribisha wageni waalikwa, Rais wa Touch Foundation, Lowell Bryan pamoja na kuelezea mafanikio ya taasisi yake iliyoanzishwa mwaka 2004 katika uboreshaji wa sekta ya afya nchini Tanzania, amewataka wafadhili mbalimbali kuendelea kujitolea na kuchangia zaidi ili sekta ya afya nchini Tanzania iweze kuimarika na hatimaye kumaliza au kupunguza changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta hiyo.

  Akasema utashi wa kisiasa na wa kiuongozi ambao Mh. Rais Jakaya Mrisho Kikwete ameonyesha katika, si tu kutambua na kuthamini mchango wa Touch Foundation na Taasisi nyigine kama hiyo, bali pia amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha kwamba sekta ya afya inaimarika nchini Tanzania na huduma za afya zinawafikia wananchi kule walipo.

  Naye Padre Dkt. Peter le Jacq ambaye naye amekuwa na mchango mkubwa wa uimarishaji wa sekta ya afya nchini kupitia Hopistali ya Buganda ana ambaye haswa ni chimbuko la Touch Foundation, hakusita kutoa shukrani zake kwa Rais Kikwete na kumuelezea kama kiongozi anayejituma, kujitolea na mwenye ushirikiano mzuri za sekta binafsi.

  Katika Miaka kumi ya uhai wake Touch Foundation imekuwa ikishirikiana na kufanya kazi kwa Karibu na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, na hususani Chuo Kikuu cha Kikatoliki cha Afya na Sayansi Mwambata cha Bugando (CUHAS). Ushirikiano huo unahusisha katika maeneo mbalimbali mtambuka yakiwamo mafunzo ya madaktari na wataalam wa fani mbalimbali kupitia CUHAS na hivyo kuchagia ongezeko la madaktari na wataalam.

  Mbali ya watendaji wakuu wa Touch Foundation, wakiongonzwa na Rais wake, Bw. Lowell Bryan, pamoja na wafadhili.Asante Supper 2014 ilihudhuriwa pia na wageni maalum kutoka Tanzania na ujumbe huo ulihusisha Muhashamu Thaddaeus Ruwa’ichi Askofu Mkuu wa Mwanza na Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa,Balozi Tuvako Manongi alikuwa miongoni wa wageni waaalikwa.

  Wengine kutoka CUHAS walikuwa ni Askofu Augustine Shao, Makamu Mkuu wa CUHAS ,Profesa Jacob Mtabaji, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine, Padre Dkt. Charles Kitima, Profesa Paschalis Rugarabamu, Dkt, Isidor Nyahomela, Dkt. Frederick Kigadye, Dkt. Charles Majinge, Dkt. Manage Manyama, Dkt. Stella Mongella, Dkt. Godwin, Godfrey Sharau na Sister Marie- Jose Voeten kutoka hospitali Teule ya Sengerema.

  Baadhi ya Madaktari hao kutoka Bugando na hasa wale walionufaika na ufadhili wa Touch Foundation walielezea walivyonufaika na ufadhili huo ambao umewawezesha kusoma, kujipatia ujuzi na hivyo kupata fursa ya kuwahudumia watanzania wenzao.
  Rais wa Touch Foundation, Bw. Lowell Bryan akiwa katika picha ya pamoja na Balozi Tuvako Manongi, Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania Umoja wa Mataifa na Mke wa Balozi, Bibi Upendo Manongi wakati wa Hafla ya Asante Supper 2014 iliyofanyika mwishoni mwa wiki, hafla hiyo ilikuwa ni kuadhimisha miaka 10 ya Taasisi hiyo iliyokwenda sambamba na harambee ya kuchangia uimarishaji wa sekta ya Afya nchini Tanzania. Touch Foundation inafanya kazi kwa karibu na Serikali ya Tanzania na Chuo Kikuu cha Kanisa Katoliki cha Afya na Sayansi Mwambata ( CUHAS) Bugando Tanzania. Katika hafla hiyo, ambayo ilihudhuriwa na Viongozi wa CUHAS wakiongozwa na Mhashamu Askofu Mkuu, Yuda Thaddaaeus Ruwa'ichi, Bw. Bryan alisifu na kupongeza utashi wa Kisiasa na Uongozi wa Mhe. Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika kuhakikisha huduma za afya zinawafikia wananchi , ushirikiano wake na kutambua kwake mchango wa sekta binafsi katika eneo hilo.
  Balozi Manongi na Upendo Manongi wakiwa na Padre Dkt. Peter Le Jacq wa Shirika la Maryknoll ambaye alianza kufanya kazi na Bugando Medical Center katika miaka ya 80 ambaye kwa kushirikiana kwa karibu na Marehemu Mhashamu Askofu Aloysius Balina walianza juhudi za kuyatafutia ufumbuzi matatizo ya sekta ya afya hasa upungufu wa Madaktari. Padre Dkt. Jacq pamoja na rafiki zake alikuwa chumbuko la Kamati ya Touching Tanzania katika miaka hiyo ya 80 na hatimaye kuzaliwa kwa Touch Foundation mwaka 2004. Dkt. Jacq naye kwa upande wake amesifu na kutambua mchango wa Mhe. Rais Jakaya Kikwete na kujituma kwake kuimarisha sekta ya afya kwa kushirikiana na wadau wengine.
  Makamu Mkuu wa CUHAS Professa Jacob Mtabaji kushoto kwa Balozi Manongi na Professa Paschalis Rugarabamu ambao walikuwa sehemu ya Ujumbe uliohudhuria Asante Supper 2014 wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa.

  0 0
 • 05/10/14--23:59: KUMBUKUMBU

 • 0 0

  Na Dixon Busagaga,Hai. 


  WANANDOA wawili wameuawa kinyama baada ya mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Yusuf Njau (32),  anayeaminika kuwa ni mtoto wa wanandoa hao, kuwacharanga kwa shoka kisha kuchoma moto nyumba  yao na kutokomea kusiko julikana.
    
  Tukio hilo la kusikitisha na la aina yake limetokea juzi majira ya saa 12:30 jioni katika kijiji cha Masama-Roo,  Kata ya Machame Mashariki,
  wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro baada ya kijana huyo kuchukua uamuzi huo ambao unadhaniwa ni sababu za ugomvi wa kifamilia. 

  Waliouawa wametambulika kwa majina ya Shahidu Njau(60) ambaye  ni baba yake mzazi wa mtoto huyo na  Minae Swai (57) ambaye ni mama mzazi wa mtoto huyo ambao kwa pamoja waliuawa baada ya kupigwa na shoka katika maeneo mbalimbali ya mwili. 

  Kwa mujibu wa Taarifa kutoka kwa Mwenyekiti wa kijiji hicho, Halfani Swai alisema walipofika katika eneo la tukio baada ya kusikia ukunga, walikuta watu wakizima moto huku mwili wa Mama yake muuaji uliocharangwa na mapanga kila mahali ukiwa chini. 

  Alisema kuwa wakati kijana huyo akiendelea kutenda unyama huo, alitokea baba yake mzazi, Mzee Shaidu  aliyekuja kuingilia kati ugomvi wa Mama na mwanae lakini naye alikatwa kichwani. 

  Swali alisema Mwili wa Baba ulikutwa ukiwa pembeni wa mwili wa Mama ukiwa umekatwa kichwani na ubongo kufumuliwa lakini hata hivyo alikuwa bado hajafa. 

  Alisema walimchukua kwa nia ya kuokoa uhai wake lakini muda mfupi baada ya kutoka kwenye eneo la tukio wakiwa katika kituo cha mafuta maeneo ya kwa Sadala Shaidu alipoteza maisha. 

  "Tulikuta mwili wa Baba ukiwa pembeni nao ukiwa umejeruhiwa vibaya kichwani, ubongo ulikuwa pembeni, tulimchukua kumpeleka Hospitali lakini tulipofika kwa Sadala alipoteza maisha," alisema Swai.
   
  Taarifa kutoka katika kijiji hicho zilisema muuaji, Yusuf Njau, ambaye amewahi kujifunza ngumi akiwa Dar es salaam amewahi kuwatishia Uhai baadhi ya ndugu zake zaidi ya mara mbili. 

  Akizungumzia hali hiyo, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Halfani Swai alisema kuwa kijana huyo ambaye ni morofi sana aliwahi kutishia kuwaua Shangazi na Baba mdogo.  "Muuaji aliwahi kuwatishia shangazi yake na Baba mdogo,amewahi kujifunza Ngumi na ni mkorofi sana kijijini kwake," alisema Swai.  Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Robert Boaz alithibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo alisema mtuhumiwa huyo katika tukio la kutishia kuuwa shangazi na Baba Mdogo alikatwa na kuachiwa. 

  Alisema kuwa miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya wilaya ya Hai ambapo juhudi za kumsaka Muuaji anayedaiwa kuonekana akiranda
  kijijini hapo zinaendelea. 
   


  Kwa upande mkuu wa wilaya ya Hai Novatus Makunga alisema tukio hilo ni kinyama na kuwataka wananchi kuwa na subira huku akitahadharisha raia kuchukua hatua mikononi. Makunga aliwataka Wananchi kuwaachia watu wa usalama kuchukua hatua huku akitahadharisha kuhusu jaribio la wananchi kuchukua hatua mikononi kuwa inaweza kuleta madhara zaidi. 

  Wakati huo miili ya marehemu imezikwa jana mchana majira ya saa 7, kwenye makaburi ya Nyumbani, katika kijiji cha Masama Roo, Tarafa ya Masama, |Kata ya Machame Mashariki, wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro.

  0 0
 • 05/11/14--00:38: BARUA YA MAOMBI YA KAZI


 • 0 0

  Sehemu ya foleni ya malori ikielekwa kubeba mzigo katika kiwanda  cha Saruji cha Dangote  kilichopo katika eneo la Obajana,  Jimbo la Kogi, kilomita 400 Kaskazini Mashariki mwa mji maarufu wa kibiashara wa Nigeria, Lagos. 
  Kwa sasa Kiwanda hicho  kinazalisha tani za kimetriki milioni 10.25 kwa mwaka na hivyo kukifanya kiwanda hicho kuwa kiwanda kikubwa zaidi cha saruji duniani kilichoko katika eneo moja. 
  Baada ya upanuzi unaoendelea kufanywa kwenye kiwanda hicho, uwezo wake wa uzalishaji utaongezeka na kufikia tani za kimetriki 13.0 kwa mwaka. Kiwanda hicho kilicho kwenye eneo la kilomita za mraba saba kitakuwa kimegharimu kiasi cha dola za Marekani bilioni 2.5 wakati upanuzi wake utakapokamilika mwakani. Kwa sasa kiwanda hicho kina biashara ya dola za Marekani bilioni mbili kwa mwaka. 
  Kiwanda hiki , kilichoanza kujengwa mwaka 2003 na kukamilishwa mwaka 2006,  na hatimaye awamu zake za kwanza na za pili kuzinduliwa rasmi na Rais Olusegun Obasanjo Mei 12, mwaka 2007, wiki mbili kabla ya kustaafu Urais wa Nigeria, kinaajiri watu 800 kwa wakati mmoja na hivyo kuwa miongoni mwa waajiri wakubwa zaidi katika Nigeria.
   Sehemu ya malori yakiwa katika foleni ya kusubiri zamu kuelekea kiwandani kupakia mzigo

   Malori zaidi
  Uwanja wa ndege binafsi wa kiwanda cha saruji cha Dangote.

  0 0


  0 0

  Serikali imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Balozi wa Malawi hapa nchini Hayati Mhe. Flossie Gomile Chidyaonga kilichotokea juzi Ijumaa tarehe 09 Mei, 2014. Balozi Chidyaonga alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali ya Aga Khan ya hapa Dar es Salaam.

  Balozi Flossie Chidyaonga alizaliwa tarehe 16 Juni, 1960 huko Blantyre nchini Malawi. Balozi Chidyaonga aliitumikia Serikali ya Malawi katika nyadhifa mbalimbali. Kati ya mwaka 2006 hadi 2010 alikuwa Naibu Balozi wa Malawi nchini Uingereza na baadaye Kaimu Balozi hadi alipoteuliwa kuwa Balozi wa Malawi hapa Tanzanaia.

  Siku ya Jumatatu, tarehe 05 Mei, 2014, Balozi Flossie Chidyaonga alishinda vizuri na kufanya shughuli zake kama kawaida. Hata hivyo, ilipofika usiku, alijisikia vibaya na kupelekwa hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam ambapo alipatiwa Matibabu na kuwekwa mapunziko kuanzia saa 6 usiku hadi saa 12 asubuhi aliporuhusiwa na kupewa dawa za kutumia nyumbani. Balozi Chidyaonga aliendelea kutumia dawa hizo na hali kuonekana kuimarika hadi siku hiyo ya ijumaa, tarehe 09 Mei, 2014.

  Siku hiyo, aliamka vizuri hadi ilipofika majira ya saa 6 mchana, hali yake ilipobadilika na kukimbizwa tena hospitali ya Aga Khan ambapo alipokelewa Daktari alisema amekwishafariki. Sasa hivi, Mwili wa Marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Uchunguzi wa madaktari umeonesha kuwa marehemu amefariki kutokana na Mshipa Mkuu wa AORTA kuvimba na kupasuka kulikosababisha damu kukusanyika kwenye mfuko wa moyo na hivyo kufanya moyo ushindwe kufanya kazi yake.

  Kesho tarehe 12 Mei, 2014 mwili wa Marehemu utachukuliwa kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kupelekwa kwenye Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere ambapo kutafanyika misa ya kumuombea Marehemu na kutoa heshima za mwisho kuanzia saa 4 asubuhi. Mwili wa Marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda Blantyre, Malawi siku ya Jumanne tarehe 13 Mei, 2014 na mazishi yanatarajiwa kufanyika siku ya Jumatano tarehe 14 Mei 2014 huko Blantyer, Malawi.

  Katika kipindi chote alichokuwa mwakilishi wa Malawi hapa nchini, Balozi Chidyaonga alifanya kazi yake ya kukuza na kuendeleza ushirikiano kati ya nchi zetu mbili kwa umahiri wa hali ya juu. Siku zote alikuwa mstari wa mbele kutoa ushirikiano kwa Serikali na Mabalozi wenzake wanaowakilisha nchi zao hapa Tanzania.

  Mungu aiweke roho ya marehemu Balozi Flossie Chidyaonga, mahali pema peponi.

  AMEN
  Imetolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
  Dar Es Salaam, Tarehe 11 Mei, 2014
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa John M. Haule akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) Juu ya Kifo cha aliyekuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania Hayati Mhe. Flossie Chidyaonga kilichotokea kwenye Hospitali ya Aga Khan Jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa Tarehe 09 Mei 2014.

  Bwa. John M. Haule akiendelea kuzungumza huku Mkurugenzi wa Idara ya Afrika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Balozi Vicent Kibwana (kushoto) akiyafuatilia kwa makini mazungumzo hayo na waandishi wa Habari (hawapo pichani)
  Mazungumzo yakiendelea kati ya waandishi wa habari na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.Picha na Reginald Philip.

  0 0

  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Kiongozi wa Shirika la Maendeleo la wa Mataifa (UNDP Adminostrator) na Waziri Mkuu wa zamani wa Newzealand, Helen Clark wakati alipofungua mkutano kuhusu Tembo barani Afrika (The African Elephant Conference) kwenye hoteli ya Hyatt Regency mjini Dar es salaam May 10, 2014.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).


  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea kwa masikitiko kifo cha Balozi wa Malawi nchini, Flossie Gomile-Chidyaonga kilichotokea juzi (Mei 9 mwaka huu) jijini Dar es Salaam.

  Balozi Gomile-Chidyaonga ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Malawi nchini Tanzania mwaka 2011, alikuwa Naibu Balozi wa nchi hiyo Uingereza alifikwa na mauti baada ya kuugua kwa muda mfupi.

  Msiba huo ni mkubwa katika fani ya mpira wa miguu nchini kwani, Balozi Gomile-Chidyaonga ndiye aliyefanikisha ujio wa timu ya Taifa ya Malawi (The Flames) ambayo Mei 4 mwaka huu ilicheza mechi ya kirafiki na Taifa Stars jijini Mbeya.

  TFF tunatoa pole kwa familia ya marehemu Balozi Gomile-Chidyaonga, Ubalozi wa Malawi nchini na Chama cha Mpira wa Miguu Malawi (FAM), na kuwataka kuwa na subira na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu cha msiba huo mzito.

  Bwana alitoa, Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. Amina.

  BONIFACE WAMBURA
  OFISA HABARI NA MAWASILIANO
  SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0
 • 05/11/14--05:46: KUMBUKUMBU
 • Marehemu Mama Victoria T. Kiama
  (22/06/195
  1-11/05/2013)
  Ni mwaka mmoja tayari umepita tangu ulipotwaliwa mpendwa mama yetu Victoria. 

  Ni Roho Mtakatifu pekee anayetufariji kila mara majonzi na huzuni vinapotuzidi lakini tunaamini kuwa umepumzika katika utukufu wake Mungu. 

  Unakumbukwa sana na mumeo Thomas Kiama, wanao Evelyn, Grace, Mary, Agnes, Esther na Stella,wakwe zako Wilfred, Noel na Richard, wajukuu zako Clifford, Ian, William, Eleon, Mainda, Kandi, Agnes, Mboni na Lincoln. 

  Upendo, ucheshi,tabasamu na mafundisho yako yatabaki mioyoni mwetu siku zote. 

  Tunamshukuru sana Mungu kwa maisha aliyokupa hapa duniani.Mama tulikupenda sana lakini Mungu Mwenyezi alikupenda zaidi. Umepumzika kwa amani!

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia watoto mapacha waliokuwa wanasubiri kupata matibabu katika Hospitali ya Ngaliema iliyopo jijini Kinshasa jana.Rais Kikwete alikwenda hospitalini hapo kumjulia hali balozi wa Tanzania nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mh.,Antony Ngereza Cheche anayetibiwa hospitalini hapo(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Ndugu Wanajumuiya wa Minnesota/New York,
  Sisi watoto na familia ya Mama Lulu Mwaluko, tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati kwa jumuiya za watanzania za Minnesota na New York, kwa msaada mkubwa wa hali na mali, na mapenzi mliyotuonyesha katika kipindi kifupi cha kumuuguza, mpaka mauti ya mama yetu mpendwa, Lulu J.M. Mwaluko aliyefariki March 7, 2014 katika hospitali ya Calvary huko Bronx, New York.

  Kwa kweli hakuna maneno yanayoweza kuelezea jinsi tulivyofarijika kwa uwepo wenu kati yetu katika kipindi chote cha msiba, ila tunaomba mpokee salamu hizi kama ishara ya shukrani zetu kwenu nyote:
  • Wanajumuiya wa New York, mlituonyesha ushirikiano mkubwa haswa katika maandalizi ya kumuaga marehemu kule Mount Vernon, NY; na pia katika kukamilisha mipango ya kumsafirisha mama yetu kuelekea Moshi, Kilimanjaro ambako marehemu sasa amepumzika katika mji aliozaliwa.
  • Wanajumuiya wa Minnesota ambao ingawa hamkuwa nasi jimboni New York, tunashukuru kwa kuwa nasi kiroho, na misaada ya hali na mali.
  • Bila kuwasahau Ubalozi wa Tanzania-NY ambao walikuwa nasi bega kwa bega katika kukamilisha zoezi zima la kumpeleka mama yetu kwenye pumziko lake la milele.
  • Mwisho tunapenda kuwashukuru ndugu, jamaa na marafiki wengine wote popote pale walipo, ambao pia walikuwa pamoja nasi kwa karibu sana, na kwa hali na mali katika kipindi hiki kigumu.
  Mungu andelee kuwabariki sana, na kuwa pamoja nanyi nyote ili muendeleze ushirikiano na upendano kama mlivyotuonyesha.

  Wenu,
  Emma Kasiga
  Mwanajumuiya wa Minnesota,
  K.N.Y. Watoto na Familia nzima ya Marehemu Mama Lulu Mwaluko.

  0 0

  Mlezi wa chama cha wake wa viongozi Mama Tunu Pinda akipokea vitabu vyenye thamani ya shilngi milioni 35 kutoka kwa Meneja Mkuu wa kituo cha kuendeleza vipaji kwa vijana THT Bwana Mwita Mwaikenda na anaye shuhudia ni Mwenyekiti wa chama cha wake wa viongozi Germina Lukuvi msaada huo wa vitatabu ni kwaajili ya kusaidia Elimu kwa watoto na vijana wenye ulemavu wa ngozi (ALIBINO) sherehe hiyo ya makabidhiano imefanyika katika makazi ya waziri mkuu jijini Dar es salaam.Picha na Chris Mfinanga.


  0 0

  Na Mwandishi Wetu

  Serikali ya Tanzania imeendelea kuweka misingi imara ya kufanyiakazi maoni ya wananchi kuhusu hali ya utawala bora nchini kama yalivyobainishwa kupitia Ripoti ya Hali ya Utawala Bora iliyoandaliwa na Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

  Itakumbukwa kuwa, Tanzania ni miongoni mwa nchi 34 kati ya 54 za AU zilizokwishajiunga na Mpango wa APRM. Tanzania ilijiunga na mchakato huu mwaka 2004 na Bunge kuridhia mnamo tarehe 1 Februari 2005.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam leo Jumapili, Mei 11, 2014 na APRM Tawi la Tanzania, imeeleza kuwa tayari Wizara mbalimbali zilizoguswa na Ripoti hiyo zimekwishakuelekezwa kufanyiakazi changamoto zilizobainishwa na kutoa taarifa.

  “Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuiwasilkisha Ripoti ya Tanzania mbele ya Wakuu Wenza wa Nchi za APRM mwaka jana, Serikali ilitakiwa kuanza kufanyiakazi changamoto za kiutawala bora zilizobainishwa.

  “Utekelezaji huo unaendelea vyema. Masuala mengi ya kikatiba yameingizwa kwenye rasimu inayojadiliwa. Masuala ya kisera na kitaasisi tayari yamefikishwa katika taasisi husika kwa ajili ya kufanyiwakazi,” ilisema taarifa hiyo.

  APRM ni nyenzo mojawapo ya kutathmini mafanikio na changamoto za utekelezaji wa shughuli za maendeleo na ujenzi wa utawala bora kote Barani Afrika ikiwemo Tanzania katika ili kutafakari kwa pamoja namna bora Zaidi ya kuziendeleza juhudi hizo.

  “Mpango huu wa kujithamini Kiutawala Bora ni muhimu kwetu na unaakisi Sera zetu na za Waasisi wa Taifa hili juu ya Kujikosoa na Kujisahihisha. Aidha, unahusisha Viongozi wa Afrika na unatoa fursa kwa wananchi kutathmini hali ya utawala bora katika nchi zao na kuendeleza dhamira ya serikali ya uwazi na ujenzi wa pamoja wa utawala bora nchini kwa kuwashirikisha Wananchi wake,” imesisitiza sehemu ya taarifa hiyo.

  Ripoti ya APRM Tanzania ambayo itatumika kama rejea muhimu, imeeleza kwa kina juhudi za Tanzania katika kulinda amani. kuimarisha utawala bora na wa sheria na jitihada katika kulinda haki za binadamu.

  Hata hivyo Ripoti hiyo pia imegusia changamoto zinazopaswa kufanyiwakazi ambazo ni suala la kushughulikia kero za Muungano, kuimarisha usimamizi wa utekelezaji wa mipango ya maendeleo, kuimarisha zaidi juhudi za kuondoa umaskini na kuilinda amani ya nchi na ujenzi wa utawala bora.

  Kuhusu mchakato wa sasa wa Katiba unaendelea taarifa hiyo imesisitiza: “Tumeaswa kuutumia vyema mchakato wa sasa wa Mabadiliko ya Katiba kuijenga Tanzania bora zaidi katika miaka mingine mingi ijayo.”

  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, wakati wa mwendelezo wa ziara hiyo ndani ya  Mkoa wa Tabora.Kinana amemaliza ziara yake katika Wilaya ya Igunga na Nzega na kesho kuhamia wilayani Uyui,katika suala zima la kuimarisha chama,kutekeleza na kuhimiza maendeleo ya Ilani ya Uchaguzi ya mwaka 2010,sambamban a kusikiliza matatizo ya wananchi na kuyapatia ufumbuni kwa namna moja ama nyingine,zira hiyo itakuwa ni ya siku kumi ndani ya mkoa wa Tabora.
  Baadhi ya wakazi wa jimbo la Bukene wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,kata ya  Bukene, wilayani Nzega leo. 
  Wanachama wapya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wakila kiapo cha utii wa chama hicho, baada ya kukabidhiwa kadi na Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Kinana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa katika Kata ya Bukene, wilayani Nzega leo. 
  Katibu wa NEC,Itikadi,Siasa na Uenezi,Ndugu Nape Nnayue akiwahutubia wakazi wa Bukene,kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa Kata ya Bukene, wilayani Nzega, mkoani Tabora.
  Baadhi ya wakazi wa jimbo la Bukene wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Taifa,kata ya  Bukene, wilayani Nzega leo.
  Kinana akishiriki kufyatua tofali ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi wa matofali wa akina mama wa CCM Wilaya ya Nzega. Mradi huo umefadhiliwa na Mbunge wa Viti MaalumMkoa wa Tabora, Munde Tambwe (pichani kushoto), katika eneo la Ofisi za CCM Wilaya ya Nzega leo.Nyuma ni Mbunge wa jimbo la Nzenga,Dkt.Hamis Kingwangallah.
   Kinana akishuka kwenye tanki  alipokuwa akikagua mradi wa maji wa Kijiji cha Itobo, Jimbo la Bukene, wilayani Nzega leo.
  Kinana akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Mamlaka ya Maji Safi na Taka Nzega, Samweli Buyigi alipokuwa akikagua chujio la maji mjini Nzega leo.
  PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

  0 0  0 0


  NA MIRIAM MOSSES
  MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imetupilia mbali pingamizi la awali la upande wa utetezi kuhusu kusitisha kusikiliza kesi  inayomkabili  Mbunge Omary Badwel  (pichani) ya kuomba na kupokea rushwa kutokana na kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na mshtakiwa huyo kutokuwa na uhusiano na tuhuma za jina zinazomkabili.

  Uamuzi huo ulitolewa jana na Hakimu Mkazi Mkuu, Mhe. Hellen Riwa, kwamba kesi ya jinai inayomkabili Badwel haina uhusiano na kesi ya Kikatiba aliyofungua katika Mahakama Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam.

  Hakimu Riwa alisema kesi inayomkabili mshtakiwa iliyopo mbele yake itaendelea kusikilizwa kutokana na kesi hizo mbili kutokuwa na uhusiano.

  "Mahakama imekataa pingamizi la awali la utetezi na itaendelea kusikiliza kesi hii ya jinai haina uhusiano na kesi ya Kikatiba aliyofungua mshtakiwa Mahakama Kuu... "alisema Hakimu Riwa.

  Alisema ushahidi wa upande wa Jamhuri utasikilizwa Juni 12, mwaka huu.

  Mapema mahakamani hapo, wakili wa utetezi Mpale Mpoki, alidai kuwa wamefungua kesi ya Kikatiba Mahakama Kuu Tanzania kwa hiyo kesi hiyo isiendelee kusikilizwa Mahakama ya Kisutu, hadi ile ya Kikatiba itakapotolewa uamuzi.

  Alidai kesi hiyo ya Kikatiba ilifunguliwa Desemba 5, mwaka jana na kusajiliwa kwa namba 48/2013, wanaiomba Mahakama Kuu, kutengua sheria namba 25 ya mwaka 2002 iliyofanyiwa marekebisho sheria namba 372 kifungu kidogo cha cha (2) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa Jinai (CPA).

  Alisema sheria hiyo inakataza mtu yoyote kupinga uamuzi unaotolewa ndani ya usikilizwaji wa kesi na kwamba sheria hiyo inakinzana na Ibara ya 136 (a) ya Katiba inayosema mtu yoyote ana haki ya kukata rufaa ya aina hiyo.

  Hata hivyo, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Lizy Kiwia alidai kuwa kesi ya Kikatiba haihusiani na kesi ya tuhuma za rushwa inayoendelea kusikilizwa dhidi ya mbunge huyo hivyo mahakama itupilie mbali ombi la utetezi.

  Katika kesi ya msingi, ilidaiwa kuwa  mshtakiwa akiwa kama Mbunge wa Jimbo hilo, Mjumbe LAAC na mtumishi wa umma, alitenda kosa hilo kati ya Mei 30 hadi Juni 2, mwaka 2012 jijini Dar es Salaam.

  Ilidaiwa kuwa,  kinyume na Sheria ya Kupambana na Kuzuia Rushwa, Mbunge huyo alishawishi kutolewa kwa  rushwa ya Shilingi milioni nane kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, Sipora Liana, ili awashawishi  wajumbe wa kamati hiyo wakati wa kupitia ripoti ya bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka 2011/12.

  Ilidaiwa katika shitaka la pili kuwa, Juni 2, mwaka 2012, katika Hotel ya Peacock, jijini Dar es Salaam, mshitakiwa alipokea rushwa ya Shilingi milioni moja kutoka kwa Liana kwa ajili ya kuwashawishi wajumbe wa LAAC kupitisha ripoti ya bajeti ya halmashauri hiyo ya mwaka 2011/12 bila vikwazo.

  Hata hivyo, Mbunge huyo alikana mashtaka dhidi yake na yuko nje kwa dhamana.

  0 0

   Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo UNDP Mhe.Hellen Clark (kushoto) akikaribishwa na Spika wa Bunge Mhe.Anne Makinda mjini Dodoma baada ya kukutana na chama cha wabunge wanawake katika ukumbi wa Spika.
   Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo UNDP Mhe.Hellen Clark akisaini kitabu cha wageni
   Mhe.Hellen Clark (katikati) akizungumza na chama cha wabunge wanawake,kushoto kwake ni mwakilishi wa UNDP hapa nchini Ndugu Philippe Poinsot na kulia kwake Ana Havhannesyan(UNDP Technical Advisor))
  Mwenyekiti wa chama cha Wabunge wanawake Mhe.Anna Abdallah (kulia) akishirikiana na Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa kumvalisha vazi la kanga walilomzawadia Mhe.Hellen Clark. Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Maendeleo UNDP, mjini Dodoma leo.
  Picha na Deusdedit Moshi

  0 0

  Mechi ya kwanza ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itafanyika Jumapili (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

  Awali mechi hiyo tulipanga ichezwe Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa nia ya kuhakikisha mikoa yote ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mechi za kimataifa.

  Ili Uwanja wa Sokoine uweze kuchezwa mechi za kimataifa za mashindano, Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) lilituma Mkaguzi (inspector) wake kwenye uwanja huo Jumamosi (Mei 10 mwaka huu) ambapo imeamua kuwa marekebisho yanayofanyika hayatamalizika katika muda stahili, hivyo mchezo huo kutochezwa Sokoine.

  Tunatoa mwito kwa wamiliki wote wa viwanja kuwasiliana na TFF ili Idara ya Ufundi iwaelekeze maboresho ya kufanya ili viwanja vingi iwezekanavyo viweze kukidhi viwango vinavyotakiwa na CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).

  Taifa Stars ambayo ilikuwa kambini mkoani Mbeya itarejea Dar es Salaam keshokutwa (Mei 14 mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.

  BONIFACE WAMBURA
  OFISA HABARI NA MAWASILIANO
  SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)  0 0


older | 1 | .... | 446 | 447 | (Page 448) | 449 | 450 | .... | 3270 | newer