Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 440 | 441 | (Page 442) | 443 | 444 | .... | 3284 | newer

  0 0


  0 0

  Rais wa Jamhuri ya Muungano  wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Dkt Laurent M. Shirima kuwa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma (PPRA).

  Dkt. Shirima ni Mkurugenzi wa kujenga Uwezo wa Huduma za Ushauri (Capacity Building and Advisory Service-PPRA) na pia ndiye anaye kaimu nafasi ya Mtendaji Mkuu wa PPRA.

  Kulingana na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue, Uteuzi huu umeanza tarehe 2 Mei, 2014.

  Imetolewa na;

  Premi Kibanga,
  Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
  Ikulu-Dodoma
  Tanzania.

  6 Mei, 2014

  0 0

  Kaimu Mkuu wa Chuo cha Uandishi wa Habari Zanzibar (ZJMMC) Rashid Omar akimkaribisha Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk katika mkutano na Wanafunzi wa chuo hicho ngazi ya Diploma na Sataficate katika Ukumbi wa Sanaa rahaleo studio Zanzibar.
  Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari (ZJMMC)wakimsikiliza Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk hayupo pichani wakati akitoahotuba kwa wanafunzi haokatika Ukumbi wa Sanaa rahaleo studio Zanzibar.
  Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk akiwahutubia Wanafunzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari (ZJMMC) katika ukumbi wa Sanaa rahaleo studio Zanzibar.
  Mwanafunzi Mwajuma Ali Kombo wa chuo cha Uandishi wa Habari (ZJMMC)akiuliza maswali kwa Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alipokutana na Wanafunzi hao na kuwataka kuelezea matatizo yao katika Ukumbi wa Sanaa rahaleo studio Zanzibar.
  Mwanafunzi Mwita Abdalla wa chuo cha Uandishi wa Habari (ZJMMC)akiuliza maswali kwa Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk alipokutana na Wanafunzi hao na kuwataka kuelezea matatizo yao katika Ukumbi wa Sanaa rahaleo studio Zanzibar. PICHA NA YUSSUF SIMAI -MAELEZO ZANZIBAR

  0 0

  Na Demetrius Njimbwi - Jeshi la Polisi

  Mkuu wa Dawati la Jinsia Nchini Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Adolfina Chialo, amewataka askari wote nchini hususan wale waliopo katika dawati la jinsia kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi ili kukomesha vitendo vya ukatili na unyanyasaji wa kijinsia dhidi ya wanawake na watoto.

  Hayo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo ya siku tano yanayotolewa kwa Maafisa na askari wa Jeshi la Polisi katika mkoa wa Dar es salaam, ambapo washiriki hao watapatiwa mafunzo ya namna ya kukabiliana na makosa ya ukatili wa kijinsia.

  Kamishna Chialo, alisema kuwa, ili kutokomeza makosa yatokanayo na ukatili wa kijinsia na unyanyasaji kwa watoto, ameihasa jamii kutofumbia macho uovu au aina yeyote ya ukatili na badala yake kuripoti jambo hilo mahala husika au  katika madawati ya jinsia ya Polisi katika kituo chochote cha Polisi  ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa ambapo kwa sasa jumla ya madawati ya jinsia 417 yameanzishwa hapa nchini.

  Kwa upande wake mgeni rasmi wa semina hiyo ambaye pia ni Afisa Ustawi wa Jamii, Bi. Eva Mbilinyi, alisema Kuwa, lengo kuu la mafunzo haya ni kuwasaidia askari Polisi kwa kuwajengea uwezo katika utendaji wao wa kazi na namna sahihi ya kuwahudumia waathirika wa ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto.

  Bi. Eva Mbilinyi, aliongeza kuwa, bila ulinzi, malezi na makuzi sahihi kwa watoto ni wazi kuwa, taifa haliwezi kupiga hatua katika maendeleo hivyo jamii inatakiwa kuhakikisha kuwa, inamlinda mtoto dhidi ya ukatili wa aina zote za unyanyasaji alisema.

  0 0

  Na Mwandishi wetu, Lubumbashi

  Wafanyabiashara wa Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo (DRC) wamesema wana matumaini makubwa na hatua ya Tanzania kufungua ofisi ndogo ya mawasiliano ya Mamlaka ya Bandari (TPA) mjini Lubumbashi, jimbo la Katanga nchini humo.
  Wakiongea kwa niaba ya wenzao baada ya kuzinduliwa kwa ofisi hiyo hivi karibuni, wafanyabiashara hao wanaopitisha mizigo yao katika bandari ya Dar es Salaam, wamesema kuanzishwa kwa ofisi hiyo kumekuja wakati muafaka na kuwa itawarahisishia biashara yao.

  Sasa wafanyabiashara hao wataweza kufanya malipo ya bandari wakiwa Lubumbashi na kuepuka hatari ya kusafiri na kiwango kikubwa cha pesa na kuibiwa.

  Mmoja wa wafanyabishara hao, Bw. Mubanzo Fils anayeendesha kampuni ya ETS Mubanzo alisema jumuiya ya wafanyabiashara Lubumbashi imefurahia sana kupata ofisi hiyo wanayotarajia kurahisisha kazi zao na kukuza biashara baina ya nchi hizo mbili.

  “Tuna furaha kubwa sana kwa hatua hii muhimu,” alisema.

  Inatarajiwa kwamba tatizo lililokuwa linawakabili wafanyabiashara hao la kukabiliana na wakala wa kupakia na kupakua mizigo wasio waaminifu, sasa litakuwa historia kwa kuwa ofisi ya Lubumbashi itakuwa na orodha ya wakala wanaokubalika na waaminifu.

  Pia mienendo ya taarifa za mizigo itafanyika mjini humo na hivyo kuharakisha taratibu za mizigo bandarini hapo.

  Kwa upande wake, Bw. Lumbu Useni wa kampuni ya Luwang SPRL alitoa wito kwa wafanyakazi kwenye ofisi hiyo ili kutimiza lengo lilikusudiwa.

  “Wafanye kazi kwa bidii na akili zao zote ili lengo lililokusudiwa na nchi hizi lifikiwe na sisi tuweze kufaidika,” alifafanua.

  Mizigo ya DRC inayopita katika bandari ya Dar es Salaam imekuwa ikiongezeka kwa asilimia takribani 24 kwa mwaka tangu mwaka 2004 ikiongezeka toka tani 155,611 hadi tani 1,117,249 mwaka 2013.

  Nchi hiyo ni ya pili kwa kupitisha mizigo mingi katika bandari ya Dar es Salaam.  kwa mujibu wa takwimu zilizopo, mizigo ya DRC inachukua asilimia 25 ya mizigo yote ya nchi jirani inayopita katika bandari hiyo.

  Mfanyabiashara mwingine, Bw. Mohamed Hassan Hammy, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Drill Tek ya mjini humo alisema Kongo ni soko kubwa hivyo Tanzania imefanya busara kubwa kufungua ofisi hiyo.

  Bw. Hammy ambaye ni mtanzania alisema pamoja na kwamba kufungua ofisi hiyo ya TPA ni hatua kubwa, jumuiya ya wafanyabiashara mjini hapo wanaomba serikali kufungua ofisi ndogo ya ubalozi wa Tanzania Lubumbashi ili kuwasaidia katika mambo yao mbalimbali.

  “Tunaipongeza serikali kufungua ofisi hii ya TPA lakini pia tunaiomba ifungue ubalozi mdogo hapa Lubumbashi ili kutusaidia sisi watanzania tunaoishi hapa,” alisema, na kuongeza kuwa kwa sasa wanalazimika kusafiri umbali wa kilometa 2,000 hadi mjini Kinshasa wanapohitaji huduma za ubalozi wa Tanzania.

  “Kinshasa ni mbali sana na ni gharama kubwa,” alifafanua.

  Awali, Waziri ya Uchukuzi wa jimbo la Katanga, Bw. Kahozi Sumba alisema ufunguzi wa ofisi hiyo sio tu utarahisisha na kuleta ufanisi katika kusafirisha mizigo ya wafanyabiashara wa Kongo wanaotumia bandari ya Dar es Salaam, bali pia utasaidia kuboresha maisha yao.

  “Kurahisisha biashara ina maana ya kupata maendeleo na kuboresha maisha yetu, tunaishukuru sana serikali ya Tanzania kwa uamuzi huu,” alisema baada uzinduzi huo uliofanywa na Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe.

  Aliihimiza jumuia ya wafanyabiashara wa nchi hiyo kuthibitisha kuwa kweli walikuwa wanaihitaji ofisi hiyo kwa kuitumia kutatua matatizo yao.


  “Thibitisheni kwa vitendo kuwa kweli mlikuwa mnaihitaji ofisi hii,” aliwaambia baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa katika tukio hilo la uzinduzi.   
   Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (katikati) akisaini kitabu cha wageni katika ofisi mpya ndogo ya mawasiliano ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mjini Lubumbashi, jimbo la Katanga hivi karibuni.  Wanaoshuhudia ni Waziri wa Uchukuzi wa Jimbo la Katanga, Bw. Kahozi Sumba (kushoto) na mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Bi. Zarina Madabida (kulia).

   Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe (wa pili kushoto) na Waziri wa Uchukuzi wa Jimbo la Katanga, Bw. Kahozi Sumba wakifuatilia jambo wakati wa uzinduzi wa ofisi ofisi ndogo ya mawasiliano ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mjini Lubumbashi katika jimbo hilo hivi karibuni.  Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, Bw. Peter Serukamba (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Eng. Madeni Kipande (kulia).

   Sehemu ya wafanyabiashara wa DRC Congo waliohudhuria uzinduzi wa ofisi ndogo ya mawasiliano ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mjini Lubumbashi, jimbo la Katanga hivi karibuni.  Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Harrison Mwakyembe kusaidia wafanyabiashara wa nchi hiyo wanaotumia bandari ya Dar es Salaam.

   Sehemu ya wafanyabiashara wa DRC Congo waliohudhuria uzinduzi wa ofisi ndogo ya mawasiliano ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mjini Lubumbashi, jimbo la Katanga hivi karibuni.  Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Harrison Mwakyembe kusaidia wafanyabiashara wa nchi hiyo wanaotumia bandari ya Dar es Salaam.


  Sehemu ya wafanyabiashara wa DRC Congo waliohudhuria uzinduzi wa ofisi ndogo ya mawasiliano ya Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) mjini Lubumbashi

  0 0

  DSC_0083
  Mshehereshaji ambaye ni Mwanakamati ya maandilizi ya maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014, Usia Nkhoma Ledama akiwatambulisha baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (hawapo pichani) kwa mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani.
  (Picha zote na Zainul Mzige).

  Na Mwandishi wetu
  Jaji Mstaafu Mark Bomani amesema lengo la mchakato wa Katiba ni kuhakikisha kwamba Tanzania inapata Katiba ambayo ni bora zaidi kuliko zote itakayoshughulikia changamoto na kuweka mazingira ambayo yatamrahisishia maendeleo mwananchi kwa haraka.
  Akitoa risala katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani leo katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa AICC jijini Arusha, Jaji Mstaafu Mark Bomani, amesema jukumu la mwanahabari ni kuwaelimisha baadhi ya wabunge wa Bunge Maalum la Katiba ambao hawana uelewa mkubwa na mchakato wa Katiba hawajui maana halisi ya Katiba mambo ambayo yanasababisha kujadili Katiba hiyo kwa maneno mabaya, kutishiana, matusi na kejeli.
  DSC_0171
  Baadhi ya waandishi wa habari wakongwe (Ma-veterans) wakimsalimia mgeni rasmi.
  “Zoezi la mchakato wa Katiba ni kubwa na wabunge wengi wa Bunge Maalum la Katiba hawaelewi wajibu wao katika kuijadili Katiba hiyo matokeo yake ndio hayo wanayoshuhudia Watanzania”.
  Mara nyingi Watanzania wameshuhudia mijadala ya kejeli, malumbano, matusi, kudharauliana pale hoja zinapojengwa na upande ambao haukubaliki na upande mwingine jambo ambalo limewavunja moyo Watanzania na kutokuwa na imani ya kupata Katiba inayolenga kumlinda mwananchi.
  Jukumu la wanahabari ni kutoa elimu ya kutosha kuhusu yaliyomo katika Katiba Mpya na kuandika habari za maendeleo ili majadiliano yatokanayo yawe endelevu yamtendee haki mwananchi wa kawaida kwa lengo la kuboresha maisha yao.
  DSC_0077
  Meza Kuu, kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Elimu, Sayansi na Mawasiliano ya Umoja wa Mataifa (UNESCO) Bw. Abdul Wahab Coulibaly, Mkurugenzi wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF) Bw. Ernest Sungura, Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Bw. John Mongela, Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Bw. Mohamed Tibanyendera, Rais wa Umoja wa Vilabu vya Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) Bw. Kenneth Simbaya na Meneja Utafiti na Ushapishaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. John Mirenyi.
  “Inasikitisha kuona kuwa hali ya Mtanzania inazidi kudidimia au kubaki pale pale katika sehemu nyingi hasa vijijini katika kipindi cha miaka 40 iliyopita kwa kukosa fursa muhimu za maendeleo na viongozi hawalioni hilo”, amesema Jaji Mstaafu Mark Bomani.
  Wakati huo huo mgeni huyo rasmi amekemea tabia ya kuandika habari za kuwasifu viongozi na kupokea Rushwa hali iliyojitokeza katika miaka ya hivi karibuni na kusema kwamba ni fedhea kwa tasnia ya habari kutofuata maadili ya uandishi.
  Amesema kwamba nchi itaendeshwa kwa kusimamia haki na ukweli na kuwataka wanahabari wasichoke kuisimamia haki na uhuru wa nchi yao bila woga kwani bila kufanya hivyo nchi itaongozwa kiimla.
  DSC_0348
  Mgeni rasmi Jaji Mstaafu Mark Bomani, akitoa risala wakati wa maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani 2014 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa AICC jijini Arusha mwishoni mwa juma.
  “Kuna tabia ya vyombo vya habari ya vyombo vya habari kununuliwa ili visiandike au kufichua maovu ni fedhea kwani vyombo vya habari ni kioo cha jamii”.
  Akizungumzia kuhusu sheria za habari za mwaka 2007 na 2008, Jaji Mstaafu amesema ni aibu kuona mswaada wa sheria ya habari umekwama kwa zaidi ya miaka 10 kwa sababu ambazo hadi leo hazijaeleweka.
  Amewataka waandishi wa habari wasikate tamaa na badala yake waendelea na kupambana kuhakikisha kwamba harakati za kupata Sheria ya Haki ya Kujua inafanikiwa ili kupunguza matukio ya manyanyaso, kupigwa, kuteswa, kufungwa kwa vyombo vya habari na kuuwawa.
  “Haki haiyombwi simamieni Haki zenu na songeni mbele”, ameongeza Jaji Bomani. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Kamera yetu leo inakuletea Taswira hii ya kikwangua anga kinachoibuka kwa kasi kando kando ya mto unaokatiza bonde la Jangwani na barabara ya Morogoro rodi,jijini Dar.


  0 0  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akizungumza na Uongozi wa Ungozi wa Ofisi ya Rais tawala za Mikoa na idara Maalum za SMZ katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi wa robo tatu ya mwaka kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.
  Baadhi ya Wakuu wa Mikoa na Wilaya za Zanzibar pamoja na Maafisa Tawala wakiwa katika kikao cha utekelezaji wa mpamgo wa kazi wa robo tatu ya mwaka kutoka Julai -Machi 2013/2014,katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) [Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

  0 0


  0 0

  Spika wa Bunge,Mh. Anne Makinda na watendaji wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya shughuli za Bunge kuanza leo mei 6, 2014.
  Mbunge Mpya wa Jimbo la Kalenga,Mh. Godfrey Mgimwa akisindikizwa na wabunge wa CCM kuingia Bungeni mjini Dodoma leo Mei 2014.
  Mbunge Mpya wa Jimbo la Kalenga,Mh. Godfrey Mgimwa akila kiapo Bungeni mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
  Mbunge Mpya wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akisindikizwa na wabunge wa CCM kuingia kwenye Ukumbu wa Bunge Mjini Dodoma, leo Mei 6, 2014
  Mbunge Mpya wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete akila kiapo Bungeni Mjini Dodoma,leo Mei 6, 2014.
  Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akimpongeza Mbunge Mpya wa Chalinze,Ridhiwani Kikwete baada ya kuapishwa, Bungeni Mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
  Waziri wa Nchi,Sera na Uratibu wa Bunge,Mh. William Lukuvi akimpongeza Mbunge Mpya wa Chalinze,Ridhiwani Kikwete baada ya kuapishwa, Bungeni Mjini Dodoma leo Mei 6, 2014.
  Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akiwa Bungeni Mjini Dodoma Mei 6,2014 wakati mwanae,Ridhiwani Kikwete alipoapishwa . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dr. Rehema nchimbi.
  Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete na familia wakiwa Bungeni Mjini Dodoma leo Mei 6,2014 wakati mwanae,Ridhiwani Kikwete alipoapishwa . Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Dr. Rehema Nchimbi.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Asia Hamisi akiwa amezirai mahakamani
  baada ya kuhukumiwa miaka mitano jela

  Watu wawili wa familia moja Frank Charles na mkewe Asia Khamis wamehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela au kulipa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja kwa kosa la kukutwa na madawa ya kulevya aina ya bangi.
  Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Mbeya Maria Batulaine amewatia hatiani wanandoa hao baada ya  kuridhishwa na ushahidi usio shaka wa mashahidi wanne wa upande wa mashitaka.
  Imedaiwa na Mwendesha mashitaka wa Serikali Juliana William amesema kuwa washitakiwa hao walikutwa na kete 100 za bangi Novemba 19 mwaka jana eneo la Makunguru Jijini Mbeya baada ya upekuzi wa Polisi.
  Baada ya kusikiliza pande zote mbili aliwapa washitakiwa nafasi ya kujitetea ambapo walisema kuwa wana watoto wawili mmoja akiwa darasa la nne na mwingine akiwa kidato cha tatu hivyo kuiomba mahakama kuwaangalia kwa jicho la huruma kwa kuwa hilo ni kosa lao la kwanza.
  Wakati Hakimu Batulaine akitafakari adhabu kwa washitakiwa hao mshitakia wa pili Asia Khamis alianguka ghafla kizimbani na kuzirai na kumwacha Hakimu akiwa kimya kwa muda kabla ya kutoa hukumu.
  Mwendesha mashitaka Juliana William aliiomba mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya kuvuta na kuuza madawa ya kulevya.
  Hakimu Maria Batulaine aliwahukumu kwenda jela miaka mitano jela au kulipa faini ya shilingi milioni moja kila mmoja na mshitakiwa wa kwanza alikuwa akihaha kutafuta fedha hizo na baadhi ya wasamaria walikuwa wakitoa huduma kwa mkewe baada ya kudondoka kizimbani na  kuzirai.
  Na Mbeya yetu

  0 0

  Madaktari wakianza kumfanyia Operesheni ya tumbo kwa ajili ya kuondoa mfuko wa nyongo, mmoja wa wagonjwa waliolazwa katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es Salaam kwa kutumia vifaa vya kisasa ambapo mgonjwa hufanyiwa upasuaji kwa njia ya matobo.
  Madaktari wakiendelea na upasuaji.
  Dokta Muganyizi Kairuki akifanya upasuaji huku akiangalia kwa kutumia kamera maalum wakati wa kufanya operesheni.

  0 0

   Mhe. Jaji Sanji Monageng ambaye ni Makamu wa Rais wa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa (ICC) Botswana akitoa mada katika Mkutano wa Majaji Wanawake unaoendelea kufanyika katika UKUMBI wa (AICC) mkoani Arusha.
   Mhe. Jaji Mstaafu Eusebia Munuo, Rais wa Chama cha Majaji Duniani (IAWJ) pamoja na wenzake wakifuatilia Mada katika Mkutano huo.
   Wajumbe wa Mkutano huo wakifuatilia mada katika Mkutano huo mapema leo.
   Wajumbe wa Mkutano huo wakifuatilia mada katika Mkutano huo mapema leo.
  Baadhi ya Majaji na Mahakimu Wanawake  kutoka Tanzania na nchi nyinginezo wakifuatilia mada katika Mkutano huo, moja ya mada zilizojadiliwa ni pamoja na Unyanyasaji wa Jinsia unaohusishwa na Matumizi ya Ngono n.k Picha na Mary Gwera, Mahakama ya Tanzania

  0 0

  Kamati ya Miundombinu ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mapema wiki hii ilikutana na Watendaji wa Wizara ya Ujenzi kwa ajili ya kupitia maepndekezo ya bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2014/15. 
   Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli awali kabla ya kuwasilisha mapendekezo hayo kwanza alianza kwa kutoa tarifa ya utekelezaji kwa mwaka wa fedha wa 2013/14 ambapo Wizara ya Ujenzi ilitengewa Shilingi 381,205,760,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Hadi kufikia mwezi Aprili 2014 jumla ya Shilingi 372,088,829,186.73 zilikuwa tayari zimetolewa na HAZINA. Kiasi hicho ni sawa na asilimia 97.61 ya kiasi kilichokuwa kimepangwa. Akizungumzia fedha za Mfuko wa Barabara (Road Fund), Waziri wa Ujenzi alibainisha kuwa katika mwaka wa fedha wa 2013/2014 Mfuko huo ulipangiwa kukusanya Shilingi 504,306,000,000 kwa ajili ya Wizara ya Ujenzi, TANROADS na TAMISEMI. 
   Hadi kufikia mwezi Aprili, 2014 fedha zote zilizokusanywa zilikuwa zimefikia Shilingi bilioni 496.220 sawa na asilimia 98.4 ya malengo ya mwaka huu wa 2013/14. Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. Magufuli akiwasilisha mapendekezo ya bajeti kwa mwaka ujao wa 2014/15 alifafanua kuwa ili Wizara ya Ujenzi ili iweze kutekeleza majukumu na malengo yake itahitaji kiasi cha Shilingi trilioni moja, bilioni mia mbili kumi na tisa, milioni mia saba kumi na saba, mia tano tisini na mbili elfu (1,219,717,592,000.00). 
  Fedha hizo zimeelezewa kuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida pamoja na miradi ya maendeleo. Kamati hiyo ya Bunge baada ya kupitia vipengele vyote ilihitimisha kikao hicho kwa kupitisha mapendekezo hayo ya Wizara ya Ujenzi ili yaweze kuwasilishwa rasmi katika Mkutano unaoendelea wa Bunge la Bajeti. 
   Hata hivyo katika hatua nyingine, Kamati hiyo iliitaka Wizara hiyo ya Ujenzi kuhakikisha inasimamia ipasavyo sheria na taratibi zilizowekwa kwa lengo la kulinda miundombinu mbali mbali inayosimamiwa na wizara hiyo. 
   Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Serukamba alisisitiza kuwa kuwepo kwa matuta barabarani pamoja na kutosimamia ipasavyo udhibiti wa uzito wa magari hasa makubwa katika barabara zetu huathiri kwa kiasi kikubwa miundombinu hiyo
   Naibu Waziri wa Ujenzi Mhe. Eng. Gerson Lwenge akifafanua jambo wakati wa kikao cha Kamati ya Miundombinu kujadili bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2014/15. Wengine ni Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Magufuli (katikati) na Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Mhe. Peter Serukamba (kulia)
   Baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Ujenzi wakiwa katika kikao cha kujadili bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2014/15.
   Baadhi ya Wabunge (mstari wa mbele) ambao ni Wajumbe wa Kamati ya Miundombinu wakiwa katika kikao cha kujadili bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2014/15.

   Baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Ujenzi wakiwa katika kikao cha kujadili bajeti ya wizara hiyo kwa mwaka 2014/15.
   Baadhi ya Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Wizara ya Ujenzi

  0 0
 • 05/06/14--07:54: Miss Tabata kufanyika Juni 6
 • Washiriki wa Miss Tabata 2014 wakiwa kwenye pozi.

  Shindano la kumtafuta Redds Miss Tanzania Tabata 2014 limepangwa kufanyika Juni 6 katika ukumbi wa Da’ West Park.

  Mratibu wa Miss Tabata Joseph Kapinga alisema kuwa warembo 24 watachuana vikali kutaka kumrithi Dorice Mollel ambaye anashikilia taji hilo.

  Dorice pia ndiye anayeshikilia taji la Redds Miss Ilala.

  Kapinga alisema kuwa warembo hao wanaendelea kujifua katika ukumbi wa Da’ West kila siku kuanzia saa nane mchana chini ya waalimu wawili, Neema Mchaki na Pasilida Mandali.

  Mratibu huyo alisema fainali hiyo itasindikizwa na aina mbali mbali ya burudani ikiwemo wasanii kutoka nje ya nchi.

  Warembo wanaendelea na mazoezi kila siku ni Esther Frank Kiwambo (20), Badra S. Karuta (20), Mercy Mathias Kazula (19), Lydia Charles (22),  Nuru Omary Athumani (19) na Happyclarrice Wilson Mbahi (19).

  Wenine ni Evodia Peter (22), Fatma Hussein Ismail (20),  Ambasia Lucy Mally (22), Faudhia Hamisi (21), Najma Charles Mareges (19), Lightnes Olomi (18), Husna Ibrahim (19), Ramta Mkadara (20) na Mariam Shwaib Hussein.

  Warembo watano kutoka Tabata watashiriki kwenye shindano la kanda ya Ilala, Redds Miss Ilala baadaye mwaka huu.

  Miss Tabata inaandaliwa na Keen Arts na Bob Entertainment.

  0 0

  Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania imeshinda tuzo ya nafasi ya kwanza ya Usalama na Afya Mahala pa kazi kwa mwaka 2014 kwa upande wa sekta ya mawasilinao ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo kushinda tuzo hiyo tangu ilipoanzishwa mwaka 2000.

  Tuzo hiyo inayotolewa na Mamlaka ya Usalama na Afya Mahala pa kazi Nchini (OSHA) imetolewa wakati wa maadhimisho ya kilele cha siku ya Usalama na Afya Mahala pa kazi Duniani ambapo kitaifa ilifanyika jijini Dar es salaam wiki iliyopita.

  Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Rene Meza amesema ushindi wa tuzo hiyo iliyokabidhiwa kwa Vodacom na Makamu Wa Rais Dk. Mohamed Gharib Bilal ni matokeo ya juhudi za makusudi ambazo Vodacom imekuwa ikiziweka katika kulinda,kuhamasiha na kuimarisha usalama na faya za wafanyakazi wake.

  Amesema kwa Vodacom sula la usalama na afya ya mfanyakazi ni jambo lisilokuwa na mbadala na kwamba mkazo mkubwa unawekwa katika eneo hilo kwa wafanyakazi pamoja na wakandarasi na watoa huduma wengine wa Vodacom.

  “Tunawashukuru sana wafanyakazi wetu na pia wadau wetu kwa kuunga mkono sera, mikakati na miongozo yetu inayolenga kuhimizana na kukumbushana miongoni mwetu umuhimu wa kuzingatia bila shuruti usalama na afya ya kila mmoja wetu wakati tunapotimiza majumuku yetu, bila yao tuzo hii isingekuwa rahisi kwetu kuipata.”Alisema Meza

  “Unaweza kuona jinsi watu walivyo salama katikakati ya shughuli zetu zinazohusisha kandarasi za ujenzi wa minara, wafanyakazi wetu wetu wanatumia vyombo vya usafiri katika kutekeleza majukumu yao n.k hivyo ni jambo lenye kufurahisha kuona kwamba yote hayo yanafanyika pasi na kuhatarisha usalama na afya zao ni kutufikisha kushinda tuzo “Aliongea Meza

  Amesema kwa kushinda tuzo hiyo, OSHA imetambua mchango wa Vodacom katika kutoa mchango wake wa kuhakikisha kunakuwepo na utekelezaji wa miongozo yenye kulinda usalama na afya ya mfanyakazi wakati wote anapotimiza majukumu yake kwa mwajiri.

  Meza amesema kampuni ya Vodacom inatoa kipaumbele na mkazo mkubwa katika eneo la usalama na afya mahala pa kazi kwa wafanyakazi ikiamini kuwa kwa kufanya hivyo kunachangia pia kuongeza ufanisi kwa wafanyakazi huku wakijilinda na kwa faida zao na familia zao.

  “Kila wakati tunawaeleza na kuwakumbusha wafanyakazi wetu kwamba usalama na afya zao kwanza kwa kuwa kampuni inawahitaji na familia zao zinawategemea, kampuni inafanya kila lililo ndani ya uwezo wake na wao kwa upande wao wanapokea na kutii yale tunayokumbushana. Hii ndio siri ya ushindi wetu.”Amesema

  Hii ni tuzo ya nne ya kitaifa kwa kampuni ya Vodacom katika kipindi cha nusu mwaka. Tuzo nyengine ambazo Vodacom imeshinda hivi karibuni ni Tuzo ya mwajiri bora wa mwaka iliyotolewa na TEA, Tuzo ya mlipa kodi mkubwa wa mwaka katika sekta ya mawasiliano kutoka TRA pamoja na tuzo ya mlipa kodi mkuu wa tatu kitaifa pia kutoka TRA,

  Kuhusu mipango katika miezi michache ijayo, Meza amesema mbali na kutimiza wajibu wake kwa wadau wote wa ndani na nje wakiwemo wateja na wafanyakazi, Vodacom itaendelea kuwa mwezeshaji mkuu wa huduma za mawasiliano ya simu za mkononi  nchini kupitia teknolojia bora.

  Kwa sasa Vodacom inawafikia watanzania zaidi ya 90% huku ikiongeza mtandao wake wa teknolojia ya 3G kuwezesha watanzania wengi zaidi kuwa na huduma za Intaneti na pia kuwezesha huduma mtandao katika biashara, elimu, kilimo, afya na huduma nyengine mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

  0 0

  Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma.

  Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu 34 wakazi wa Mji mdogo wa Kibaigwa Kata ya Kibaigwa Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma kwa makosa ya kufanya fujo na kuharibu mali tukio lililotokea tarehe 05/05/2014 majira ya saa 13:30Hrs.

  Kamanada wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema Vijana wanaokadiriwa kuwa zaidi ya miatatu wakishirikiana na Wabeba mizigo wa Soko Kuu la Mazao la Kibaigwa, walifanya maandamano bila kibali na kung’oa bango la Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa lenya tangazo la kutoruhusu wafanyabiashara kuingiza mazao sokoni bila kulipa ushuru uliowekwa kwa mujibu wa sheria. 

  Viwango vya ushuru vinavyotozwa vilipanda tangu tarehe 01.07.2013 ambapo gunia la Kg. 100 za karanga zilipanda kutoka Tshs. 1000/= hadi Tshs 3000/=, guina la mahindi lilipanda kutoka Tshs. 500/= hadi Tshs. 1000/=, dumu la mafuta ya alizeti lilianza kutozwa Tshs. 500/=, gunia la mashudu lilianza kutozwa Tshs. 1000/=, gunia la alizeti lilianza kutozwa Tshs. 1000/= ushuru ambao unapingwa na wabeba mizigo.

  Vijana  hao wabeba mizigo walifanya fujo kwa kufunga barabara kuu ya Dodoma – Morogoro kwa mawe na kuchoma mataili, pia walivamia maduka na bar za jirani na kupora vinywaji na kuvunja majokofu.


  0 0


  0 0
 • 05/06/14--13:25: Article 4
 • SERENGETI FREIGHT FORWARDERS LTD
  WAZEE WA KAZI

  TUMEHAMIA NDANI YA TILBURY PORT
  ADDRESS YETU MPYA NI;
  UNIT 16D TILBURY INDUSTRIAL COMPLEX
  TILBURY FREEPORT
  ESSEX
  RM18 7HB

  20' CONTAINER TO DAR /MOMBASA NOW £1,200 
  40' CONTAINER TO DAR MOMBASA NOW £1,700 
  SALOON CARS TO DAR NOW £680
  4 X 4 CARS TO DAR  NOW £780
  AIR CARGO TO DAR £3.80 INCLUSIVE CLEARANCE
  KAMA UNA MZIGO WA MSAADA TUNASAFIRISHA BURE
  FREE STORAGE IN OUR OFFICE
  FREE COLLECTION FROM EAST LONDON 
  £50 COLLECTION FROM ANYWHERE IN UK
  COLLECTION POINT IS
  ILALA MTAA WA BUKOBA
  CONTACT; TORNADO +255713607116
  SIMPLY THE BEST IN BUSINESS
  JUST DROP YOUR CAR AT OUR OFFICES AND WE WILL TAKE CARE OF IT
  WE WILL GET IT INSPECTED AND LOAD IT TO THE SHIP FOR YOU!

  BEI ZETU HAZINA WASHINDANI NDIO MAANA TUMEZIANIKA WATU WAJUE
  THE DIFFERENCE IS CLEAR!
  WE ARE NOW OPEN ON SATURDAYS
  WE PROMISED, WE DID IT AND WE ARE MAKING IT EVEN BETTER!
  Tupigie kwa namba hizo hapo Chini au  tutumie email tafadhali
  SIMON  LOUIS +44 (0) 79 506 89 243
                 HQ -  UNIT 16D TILBURY INDUSTRIAL COMPLEX, TILBURY FREEPORT, ESSEX                    RM18 7HB

older | 1 | .... | 440 | 441 | (Page 442) | 443 | 444 | .... | 3284 | newer