Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live

Vodacom yatoa vitanda vya wagonjwa Kituo cha Afya Chipanga Chapokea Wilayani Bahi

$
0
0
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Mkoani Dodoma Betty Mkwassa (wa ttau kushoto) akipokea moja ya vitanda 9 kutoka kwa Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati Mruta Hamisi vilivyotolewa na mfuko wa kampuni hiyo wa kusaidia jamii (Vodacom Foundation) kwa ajili ya wodi ya wanawake katika kituo cha afya cha kijiji cha Chipanga.Kampuni ya Vodacom imejikita katika kusaidia uboreshaji wa huduma za afya hasa kwa wanawake na watoto chini ya mpango wake wa uwajibikaji kwa jamii.
Mama mjamzito Vailet Petro (katikati) mkazi wa kijiji cha Chipanga, Wilaya ya Bahi Dodoma akimwaga chozi la furaha mbele ya Mkuu wa Wilaya hiyo Betty Mkwassa (kushoto) na Mkuu wa Vodacom Kanda ya Kati (kulia) baada ya kushuhudia kituo cha afya cha kijini hapo kikipokea vitanda tisa kutoka Vodacom Foundation kwa ajili ya wodi ya wanawake. . Msaada huo umewaondolea adha akina mama ambao walikuwa wakilala sakafuni kutokana na uhaba mkubwa wa vitanda uliokuwa ukikikabili kituo hicho.
Baadhi ya Wananchi wa kijiji cha Chipanga wakisaidia kubeba vitanda vya msaada vilivyotolewa na Vodacom Foundation kuvipeleka katika wodi ya akinamama tayari kwa ajili ya matumizi.Vitanda hivyo vilikuwa na thamani ya Sh 10 Milioni .
Mkuu wa Wilaya ya Bahi Betty Mkwassa (katikati) akiteta na Mkuu wa Vodacom kanda ya kati Mruta Hamisi wakati walipokuwa wakimjulia hali mzazi aliyejifungua katika kituo cha afya Cha Chipanga wilayani Bahi.Kituo hicho huhudumia wakazi wa Bahi mka wa Dodoma na Manyoni mkoani Singida. Vodacom Foundation imekabidhi vitanda 9 vya wagojwa kwa ajili ya wodi ya wanawake yenye uhaba mkubwa wa vitanda.
Mkuu wa Wilaya ya Bahi, Mkoani Dodoma Betty Mkwasa, akiongea na Wananchi wa kijiji cha Chipanga kabla ya kupokea msaada wa vitanda kwa ajili ya zahanai ya kijijini hapo vilivyotolewa na Vodacom Foundation kuboresha huduma za afya kwa mama na mtoto.

TASWIRA ZA JIJI LA DAR KUTOKEA BAHARI YA HINDI

NAPE ALIPOHUTUBIA KIBANDA MAITI ZANZIBAR

Nyota anayechipukia Young Killer a.k.a Msodoki akiwa live kwenye show ndani ya Maisha club may 4, 2014

JUST IN: UPOTOSHWAJI WA TAHADHARI YA HALI YA HEWA KUHUSIANA NA MVUA ZINAZOENDELEA KUNYESHA

$
0
0
Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini inapenda kukanusha kuhusiana na taarifa ya ujumbe mfupi wa simu na katika mitandao ya kijamii wenye maneno yafuatayo :‘TMA warning heavy rains of strong easterly winds 100km an hour expected to hit Dar coast from Somalia, Heavy rains 120mm above sea level expected today and tommorrow. People must avoid Sea and areas near to Sea should be alert cautioned. Tanzania Meteorological Agency  www.tma.gov.tz’  

Mamlaka inapenda kuutaarifu umma kuwa taarifa hiyo siyo ya kweli  na ina  lengo la kupotosha umma na wala haijatolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania.


Mamlaka ina kuwakumbusha wananchi wote kuendelea kufuatilia taarifa zetu kupitia vyanzo husika vya Mamlaka vikiwemo utabiri wa kila siku utolewao kupitia radio, televisheni na tovuti ya Mamlaka (www.meteo.go.tz).

 Taarifa sahihi za mwenendo wa mvua na tahadhari za hali mbaya ya hewa zinatolewa  na zinapatikana kupitia njia rasmi za utoaji taarifa maalum za kiofisi (official weather statement). 
Hivyo taarifa kuhusiana na mvua zinazoendelea imekuwa ikitolewa katika utabiri wa kila siku kupitia vyombo vya habari, mtandao wa kijamii  wa Mamlaka na tovuti ya Mamlaka.


Tunawatakia shughuli njema 
katika ujenzi wa Taifa letu.

 IMETOLEWA NA MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA

CHATO WAASWA KUJITOKEZA KUWAPELEKA WATOTO KUPATA CHANJO

$
0
0
 Jamii wilayani Chato imeaswa kutambua umuhimu na kuwapeleka watoto kupata chanjo kwenye hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati kwa muda muafaka. 
Wito huo umetolewa hivi karibuni na Mwenyekiti wa bodi ya Afya Wilayani Chato Bw. Edward Buhile ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa ufunguzi wa wiki ya Chanjo iliyofanyika hivi karibuni katika hospitali ya Wilaya ya Chato. 
Bw. Buhile amesema kumekuwa na tabia ya wazazi kutokuwapeleka watoto kupata chanjo kitendo ambacho si kizuri kwani chanjo hutolewa bure na serikali kupitia hospitali, vituo vya afya na zahanati.
"Ninawaombeni mulete watoto wenu wapate chanjo, tena ni bure kabisa ili tuweze kuwaepusha na magonjwa hatari na Hatimaye kupoteza maisha ya watoto wetu” alisistiza Bw. Buhile.
 Katika uzinduzi huo pia Mkuu wa kliniki ya watoto Wilayani Chato Bibi Mary Basiga amewaasa wanaume kuambatana na wake zao pindi wanapohudhuria kliniki ili waweze kujua maendeleo ya mtoto na kumsaidia mama wakati akiwa kliniki ambapo jukumu la kupeleka watoto hivi sasa limeachwa kwa akina mama pekee. 
Walengwa wa chanjo ni watoto wenye umri chini ya miaka miwili ambao hawakupata au hawajakalisha chanjo . 
Magonjwa ambayo yanakingwa na chanjo nchini Tanzania kwa sasa ni ni kifua kikuu, Dondakoo, Kifaduro, Pilio, Surua, Pepopunda, Homa ya ini, homa ya uti wa mgongo, kichomi na kuhara. 
Kwa mwaka 2013 jumla ya watoto 77,824 walipata chanjo mbalimbali wilayani Chato na mwaka huu zaidi ya watoto 80,000 wanategemewa kupatiwa chanjo hizo.
 Mwenyekiti wa bodi ya Afya Wilaya ya Chato bw. Edward Buhile akiongea na wananchi wa Chato mjini waliohuhudhuria  kwenye uzinduzi wa wiki ya Chanjo Wilayani Chato
 Mwenyekiti wa bodi ya Afya Wilaya ya Chato bw. Edward Buhile (kulia)akimpa mtoto chanjo ya kuzuia ugonjwa wa Polio  kuashiria uzinduzi wa Chanjo Wilayani Chato
 Mwenyekiti wa bodi ya Afya Wilaya ya Chato bw. Edward Buhile akifurahia jambo na mtoto aliyepewa chanjo

 Baadhi ya wakazi wa Chato mjini waliohudhuria kwenye uzinduzi wa wiki ya Chanjo Wilayani Chato
Mkuu wa Kliniki ya Watoto Bibi. Mary Basiga akifafanua jambo kwa wananchi kuhusu umuhimu wa Chanjo. 
Habari na picha na Richard Kagembe

INTRODUCING NEW VIDEO FROM TID Feat. Julio “Check Me”

RAKESH RAJANI ON CNN'S AFRICA VOICES PROGRAMME

$
0
0
Rakesh Rajani is a Tanzanian civil society leader of Indian descent. He has led many key social projects in the evolution of education in Tanzania and East Africa throughout the last decade including HakiElimu, familiar to many people in Tanzania, especially as a vocal advocate for young people through education and recently, with Twaweza, technology and ICT. He is also a thought leader for much International Development work in Tanzania who consults with Hivos, the World Bank and the Center for Global Development. He recently was interviewed by the CNN

mradi wa mabasi yaendayo haraka jijini dar es salaam kuanza kutoa huduma mapema mwakani

$
0
0
Na Frank Mvungi- Maelezo 
Serikali inatarajia kuanza kutoa huduma za awali (interim services) katika mradi wa Mabasi yaendayo Haraka (DART) Kutoka Kimara mwisho hadi Kivukoni jijini Dar es salaam mwaka 2015 baada ya miundombinu yake kukamilika. 
 Hayo yamesemwa na Meneja Uhusiano wa Wakala wa mabasi yaendayo haraka (DART) Bw.William Gatambi wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam. 
Bw. Gatambi alisema kuwa mara baada ya kukamilika kwa miundo mbinu ya mradi huo awamu ya kwanza mwishoni mwa mwaka 2014 itasadia kufanikisha usafiri wenye tija kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam na vitongoji vyake. 
Miundombinu hiyo, inajumuisha barabara ya kilomita 20.9 kuanzia Kimara Mwisho hadi Kivukoni,Barabara ya Kawawa kutoka Morocco hadi Magomeni na Barabara ya Msimbazi hadi eneo la Gerezani Kariakoo.
 Aliongeza kuwa ina vituo vidogo 27,vituo vikuu vitano, vituo mlisho vine na karakana mbili. 
Pia inajumuisha njia za waenda kwa miguu na baiskeli. Akifafanua Gatambi alisema mradi wa majaribio utaanza na mabasi 20 yatakayokuwa na uwezo wa kuchukua abiria kati ya 145 hadi 160 kwa wakati mmoja hali itakayosaidia kuondoa kabisa kadhia ya usafiri kwa wakazi wa jiji la Dar es salaam. 
Aidha, katika mradi huo wa majaribio Gatambi amesema kutakuwa na mabasi mengine 10 yenye uwezo wa kuchukua abiria kati ya 50 na 60 ambayo yatatumika kuchukua abiria kutoka pembezoni mwa jiji la Dar es salaam kuja katika vituo vikuu vya mabasi yaendayo Haraka. 
Kwa upande wake Meneja Usimamizi wa Barabara wa DART Mhandisi Mohamed Kuganda amesema mradi huo utasaidia kuondoa tatizo la foleni Jijini Dar es salaam na kuwafanya wananchi kupata huduma ya usafiri yenye kukidhi viwango vya Kimataifa. 
Pia Kuganda alisema DART kwa kushirikiana na Halmashauri za Jiji la Dar es salaam inafanya maandalizi ya kuboresha barabara mlisho (feeder roads) katika maeneo yatakayotumiwa na mabasi mlisho. Katika mradi wa mabasi yaendayo haraka kutakuwa na Vituo Vikuu (terminals) vitano 5 katika, maeneo ya Kimara, Ubungo, Morocco, Kariakoo na Kivukoni ambapo vituo hivi ndiko mabasi yatakapokuwa yanaanzia na kumalizia safari kubadilishana abiria kati ya njia kuu na njia mlisho (feeder roads) ambapo vituo hivyo vikubwa vinatoa nafasi ya kuweza kuanzishwa kwa huduma muhimu kwenye vituo hivyo kama maeneo ya kukatia tiketi na vyoo. Mwisho

BALOZI LIBERATA MULAMULA AHUDHURIA ONYESHO LA PICHA ZA KUCHORA LA JAMBO, TANZANIA

$
0
0

Mariam Osher Mmarekani mchoraji aliyetembelea mbuga za wanyama Tanzania na kubuni uchoraji wa wanyama aliowaona huko Tanzania na kutumia michoro hiyo kuitangaza Tanzania kwa Wamarekani na raia wengine ambao wajawahifika Tanzania kwenye maonesho ya picha zake yaliyofanyika leo Silver Spring, Maryland kwenye ukumbi wa WPG uliopo 8230 Georgia Ave.

Mhe. Liberata Mulamula , Balozi wa Tanzania nchini Marekani (wapili toka kulia) akiwa pamoja na Afisa wa Ubalozi kitengo cha Utalii Bi. Immaculata Diyamett wakifuatilia maelezo ya Marian Osher.

Balozi Liberata Mulamula pamoja na Afisa Immaculata Diyamett wakifuatilia maelezo ya Marian Osher
Juu na chini ni watu mbalimbali waliofika kwenye onesho hilo la Marian Osher.


Mhe. Balozi Liberata Mulamula akitoa shukurani zake kwa Marian Osher huku akiongea na watu waliofika kwenye onesho hilo kuwaelezea vivutio vilivyopo kwenye mbuga zetu za wanyama.

TAARIFA KUTOKA JESHI LA POLISI MKOA WA TABORA LEO MEI 5, 2014

Breaking Nyuzzzzz: wananchi Kibaigwa wafunga barabara usiku huu

$
0
0
Wananchi wa kijiji cha kibaigwa wamefunga Barabara kuu ya Morogoro kwenda Dodoma usiku huu, kwa madai ya kutaka kupunguzwa Kwa ushuru wa mazao na kuamua kufunga barabara hiyo ili waweze kuonana na uongozi wa juu wa Serikali ili kusikilizwa mahitaji yao ambayo wanadai hayajawahi fanyiwa kazi na viongozi wa Kijiji. 

Kinachoendelea hivi sasa ni Jeshi la Polisi likijaribu kuwatawanya wananchi hao kwa kutumia mabomu ya machozi.

Wananchi hao wamejikusanya kuwatawanya kwa wingi katika eneo hilo huku wakiwa wamewasha moto mkubwa ambao umepelekea kuwaka kwa gari moja lililopo kwenye eneo hilo kutokana na kuzuiliwa na wananchi hao huku wakisema hapiti mtu leo hapa. 

Magari ya kwenda na kurudi kutoka mikoa ya dodoma na mingine ya kanda ya ziwa yamekwama pande zote mbili za barabara kwa zaidi ya saa sasa .Gari moja LA serikali limeharibiwa na wananchi hao.

Globu ya Jamii inaendelea kufuatilia tukio hilo kwa ukaribu kabisa na tutaendelea kuwapa taarifa kadri zinavyotufikia

shimo hatari barabara ya Ali hassan Mwinyi jijini Dar es salaam

$
0
0
Shimo hatari lililopo katika Barabara ya Ali Hassan Mwinyi jirani na Kituo cha ITV, Mwenge jijini Dar ambalo limekuwa kero kwa watumiaji wa barabara hiyo! Ungana na Global TV Online kushuhudia tukio hilo!

Article 6

Rais Kikwete afungua mkutano wa Majaji Wanawake jijini Arusha leo

$
0
0
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete,Waziri wa Katiba na Sheria Dkt.Asha Rose Migiro,Jaji Mkuu Mohamed Othman Chande,pamoja na Rais wa Chama Cha Kimataifa cha Majaji Wanawake wakiimbaq wimbo wa taifa wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa 12 wa chama hicho uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa Arusha AICC.Mkutano huo ulifunguliwa na Rais Kikwete.
Baadhi ya majaji wanawake wanaoshiriki Mkutano wa 12 wa Chama Cha Kimataifa cha Majaji wanawake unaofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano mjini Arusha(picha na Freddy Maro).
Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Washiriki wa Mkutano wa Majaji Wanawake Duniani, walitoka nchini,Mara baada ya kupungua mkutano huo rasmi.
Mkutano huo umeshirikisha takribani  wajumbe 600 kutoka nchi mbalimbali duniani. (Wa tatu kutoka kushoto ni Mhe. Mohamed Chnade Othman, Jaji Mkuu wa Tanzania, wa pili kutoka kushoto ni, Mhe. Asha-Rose Migiro, Waziri wa Katiba na Sheria, wa kwanza kushoto ni Jaji Mkuu wa Nigeria, Mhe. Aloma Mariam Mukhtar, wa pili kutoka kulia Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani (T), ambaye pia ni Rais wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani, Mhe. Eusebia Munuo, wa kwanza kulia ni Mhe. Jaji Engera Kileo, Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Tanzania. (TAWJA).

Meza Kuu ikiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa Mkutano huo kutoka Latin America.

SHIRIKA LA NELICO NA MABARAZA YA WATOTO WILAYA YA GEITA WAFANYA ZIARA YA KIMAFUNZO KATIKA SHIRIKA LA KIVULINI

$
0
0
Mkurugenzi wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake na Wasichana la KIVULINI akitoa historia ya shirika la KIVULINI kwa wawakilishi wa mabaraza ya watoto mara baada ya kutembelea ofisi za shirika hilo hapo jana. KIVULINI ni shirika lisolo la kiserikali linalofanya shughuli za kupinga na kutetea Haki za Wanawake na Wasichana katika mikoa yote ya kanda ya ziwa pamoja na mkoa wa Singida tangu mwaka 1999.
Afisa Utetezi na Mitandao ya Kijamii toka Shirika la KIVULINI Bi. Khadija Liganga akifafanua jinsi KIVULINI ilivyoweza kuliinua Shirika la Mtandao la Watoto la Jijini Mwanza (Mwanza Youth and Chidren Network) na kuweza kusimamia na kutetea Haki za Watoto katika jiji la Mwanza. 
Picha ya Pamoja ya Maafisa wa Shirika la KIVULINI, Mkurugenzi na Afisa Mradi wa NELICO, Afisa Maendeleo jamii wa wilaya ya Geita, Muwakilishi wa Plan International pamoja na Wawakilishi wa Mabaraza ya watoto wilayani Geita mara baada ya kumaliza ziara ya Kimafunzo katika ofisi za shirika la KIVULINI.
----------------------------
Shirika la watoto la New Light Children Center Organization (NELICO) la mkoani Geita kwa kushirikiana na Idara ya Maendeleo ya jamii Geita, limeambatana na wawakilishi 20 toka Mabaraza ya watoto ya kata kumi na moja (11) za wilaya ya Geita kwa ziara ya kimafunzo katika shirika la kutetea Haki za Wanawake na wasichana, KIVULINI la mkoani Mwanza.


Ziara hiyo ya kimafunzo katika shirika la KIVULINI imefanyika hapo jana ikiwa na lengo la kujifunza namna KIVULINI ilivyosaidia Baraza la watoto Mwanza kuweza kuratibu na kutekeleza shughuli zake kikamilifu na kuwa imara zaidi.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mkurugenzi wa NELICO Bi. Paulina Alex alisema kwamba ziara hiyo imelenga kutoa mafunzo kwa mabaraza ya watoto wilayani Geita juu ya mbinu za kuratibu na kutekeleza miradi mbalimbali lakini pia kujua mafanikio na changamoto za shirika la KIVULINI katika kupiga vita ukatili dhidi ya wanawake na wasichana katika mikoa ya kanda ya ziwa.
“Mabaraza ya watoto ya  Geita bado ni machanga sana na hivyo kufanya safari hii ya mafunzo kuwa ya muhimu sana. Katika safari hii wawakilishi wa mabaraza ya watoto wameweza kupata elimu kubwa kutoka KIVULINI na Baraza la watoto la Mwanza (Mwanza Youth and Children Network) ambalo ni zao la KIVULINI” alisema Bi. Paulina.

Ziara hiyo pia ilikuwa na Bw. Maximillian Kitigwa amabe ni mwakilishi toka shirika la Plan International ambao ni wadau wakubwa wa watoto kwa mkoa wa Geita pamoja na Afisa Maendeleo ya jamii wa wilaya ya Geita Bi. Emma Busanji. Watoto hao pia watafanya ziara katika Mkoa wa Arusha kujionea juhudi za  wadau wa maendeleo katika mkoa huo katika kuwaokoa watoto dhidi ya kufanyishwa kazi hatarishi hasa katika sekta ya madini.

Kivulini ni shirika lisilo la kiserikali la kutetea na kulinda Haki za Wanawake na Wasichana. Shirika la Kivulini linahamasisha jamii (Wanawake, Wanaume na Vijana) kulinda, kutetea Haki za Wanawake na Wasichana kwa kupinga vitendo vyote vya ukatili wa kijinsia. Makao makuu ya shirika yapo jijini Mwanza, Wilaya ya Ilemela, Tanzania. 

mambo ya Ligi Kuu Uingereza ndani ya DSTV wiki hii

pata mambo ya globu ya jamii katika simu yako ya mkononi

IMPORTANT NOTICE: power outage at UNIGLOBE SKYLINK TRAVEL & TOURS LIMITED at AMANI Place in DAR ES SALAAM

$
0
0
Dear all,  
We are having serious power outage at our Corporate Office at AMANI Place and our Exchange Server has shut down.
 

For all your urgent bookings, please telephone our Julius Nyerere International Airport on Telephone nos.+255 22 2842739  /+255 782 540881 / +255 713 540 881 
Or Email us on dia@skylinkonline.com for immediate assistance

We have been advised by the building Management that the power outage will be resolved by the evening tomorrow , Tuesday, 6th May,2014.

Our Management Team can be reached on their individual mobile telephones for further guidance and assistance.

We apologise for any inconveniences caused and count on your patience.


MANAGEMENT - UNIGLOBE SKYLINK TRAVEL & TOURS LIMITED

NMB YAZINDUA KAMPENI MPYA YA JIHUDUMIE

$
0
0
Benki ya NMB imezindua kampeni mpya ya Jihudumie yenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa haraka wa huduma mbalimbali za benki hiyo. Akizindua kampeni hiyo jijini Dar es Salaam Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Bw. Mark Wiessing alisema mbali ya upatikanaji wa huduma haraka, kampeni hiyo itawezesha huduma kupatikana muda wowote na mahali popote.

Sasa wateja wa NMB wanaweza kupata huduma bila kwenda katika tawi la NMB. “Tunapenda kuwafahamisha wateja wetu kwamba sasa wanaweza kupata huduma za kibenki kupitia simu za mkononi na njia nyingine mbadala kama mashine za ATM, huduma za benki kwa njia ya intaneti, PesaFasta na Akaunti ya Chap Chap,” alisema Wiessing.

kupitia kampeni hiyo, NMB imeweza kuzingatia mahitaji ya msingi ya wateja wake, ikiwemo uhakika wa huduma za kibenki na uwezo wa kuzipata wakati wowote na mahala popote.

“Kwa kubonyeza tu kitufe cha simu, fedha itaweza kutoka kwenye akaunti yako ya NMB kwenda mahala pengine popote kama vile kwenye malipo ya LUKU, kulipia muda wa maongezi wa simu na hata kuweza kutoa kiasi kinachofikia shilingi milioni moja kupitia mashine za ATM,” alisema.

Baada ya uzinduzi huo mwendelezo ulifanywa kwa matawi yote ya benki hiyo jijini Dar es Salaam, wateja wa benki hiyo walisifia kampeni hiyo, wakisema imelenga kuwapunguzia adha, usumbufu na kuokoa muda wa kupata huduma za kibenki.
Afisa Mkuu wa Fedha wa benki ya NMB Bw. Waziri Barnabas (kushoto) akimpa maelekezo ya kutumia huduma ya kifedha ya Jihudumie Frances Mbena katika tawi la Kariakoo Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Afisa Mkuu wa Huduma kwa Wateja Wakubwa wa NMB Bw. Richard Makungwa akiwapa maelezo wateja kuhusu huduma wa Jihudumie katika tawi la NMB Magomeni.
Afisa Mkuu Operesheni na Mawasiliano wa NMB Bw. Pete Novat (kulia) akimwelekeza mteja katika tawi la NMB Temeke jinsi ya kujisajili na huduma ya NMB mobile kupitia mashine ya ATM.
Afisa Mkuu wa Ukaguzi wa ndani wa benki ya NMB Bw. Augustino Mbogella (Kulia) akielimisha wateja katika tawi la NMB Sinza kuhusu huduma za jihudumie ambazo ni, NMB mobile, PesaFasta, NMB ATM, NMB ChapChap account, POS, NMB Tigo Pesa, NMB M-Pesa na NMB inakubalika hapa.
Viewing all 110016 articles
Browse latest View live


Latest Images