Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live

Rais Kikwete atoa changamoto sekta binafsi kujihusisha zaidi na mapambano dhidi ya Ukimwi


SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA,ZAFANA SANA NCHINI OMAN

0
0
Ubalozi wa Tanzania mjini Muscat, Oman chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh, hivi karibuni , uliandaa sherehe iliyofana sana ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano.
Sherehe hii ilifanyika katika ukumbi wa Jibrin kwenye hotel ya kitalii ya Intercontinental  Muscat.

Mgeni rasmi katika sherehe hii alikuwa Mheshimiwa Ahmed  bin Nassor bin Hamad Al Mahrazi,  Waziri wa  Utalii wa Oman aliyeongoza ujumbe mzito wa Serikali ya Oman ambao pia ulijumuisha , Mheshimiwa  Said bin Saleh bin Said  Al Kiyumi, Mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara na wenye viwanda wa Oman  pamoja na wabunge Wabunge la Oman pamoja na wakuu wa Idara na maafisa waandamizi katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman.

Sherehe hii pia ilihudhuriwa na mabalozi mbalimbali wanaoziwakilisha nchi zao nchini  Oman ,  wananchi wa Oman , wafanyabiashara , watanzania waishio Oman , pamoja na waomani wenye asili ya Tanzania

Katika hotuba yake Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh  alieleza kuwa Maadhimisho ya Miaka Hamsini ya Muungano ni tukio muhimu sana katika Historia ya Tanzania, kwani ni kielelezo muhimu kinachoonyesha kwa vitendo nia thabiti ya serikali ya Tanzania kuimarisha umoja na mshikamano miungoni mwa nchi za Afrika, kwani hii ndio ilikuwa azma ya waasisi wa muungano wa Tanganyika na Zanzibar waheshimiwa Mwalimu Julius Nyerere na Mzee Abeid  Amani Karume .

Mheshimiwa Balozi Ali Ahmed Saleh alieleza kuwa katika Miaka Hamsini ya Muungano Tanzania imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika  sekta za uchumi, elimu, biashara, uwekezaji na huduma za jamii kama vile afya na upatikanaji wa maji safi na salama kwa wananchi.

Mbali na maendeleo haya Mheshimiwa Balozi alieleza pia katika kipindi hiki cha miaka 50 Tanzania imekuwamshiriki muhimu katika Jumuiya ya kimataifa  kwa kutoa mchango mkubwa katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika, hifadhi ya wakimbizi toka nchi jirani na kushiriki katika harakati za kulinda amani chini ya umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika katika nchi za Lebanon, DRC, na Darfur .

Mheshimiwa Balozi Ali Saleh alisifu juhudi za serikali za Tanzania na Oman chini ya Uongozi wa Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Muadham Sultan Qaboos bin Said katika kukuza uhusiano baina ya nchi mbili ambo ni wa kihistoria na unazidi kuimarika kadri siku zinavyoenda. Alieleza kuwa Mabadilishano ya ziara za viongozi wa Tanzania na Oman katika ngazi mbalimbali ni kielelezo cha kukuwa na kuimarika kwa uhusiano baina ya Tanzania na Oman.

Alizitaja ziara  hizi kuwa ni ziara ya Waziri wa nishati Na Madini Mhe. Sospeter Muhongo (2012 ) Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud (2013 ), Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali, Zanzibar Mhe. Ali Juma Shamhuna (2014 ) Mkuu wa Majeshi wa Tanzania Jenerali Davis Mwamunyange (2012)  kwa Upande wa Tanzania.

 Upande wa Oman viongozi waliotembelea Tanzania walikuwa Spika wa Bunge la Oman la Majlis Shura (2013), Mwenyekiti wa Chama cha Wafanya Biashara wa Oman Mhe. Khalil Al Khonji .

Mhe. Balozi pia katika hotuba yake alizishukuru kampuni za Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ), Ajib Trading, Safeway LLC, Rahma Business Practices LLC na Hotel ya Intercontinental Muscat kwa michango yao na ushirikiano wao katika kufanikisha shughuli mbalimbali za Ubalozi.
Mheshimiwa Balozi mbali na shukurani hizi alitunuku Tuzo kwa kampuni hizi.

Sherehe hizi zilizofana sana zilipambwa na Kikundi cha Muziki cha Happy Entertainment cha Hapa Oman ambacho kiliimba wimbo Maalum wa Muungano .

Mheshimiwa Balozi na mgeni Rasmi walikata keki ikiwa ni ishara kuitakia mema Tanzania na Oman.
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman (mwenye shati la kitenge) pamoja na Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Ahmed Al Mahrazi, Waziri wa Utalii wa Oman ( wa nne toka kushoto) wakikata keki Maalum huku wageni wa meza kuu wakishangilia katika sherehe za Miaka 50 ya Muungano, zilizofanyika Muscat katika Hotel ya Intercontinental.
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman akitoa hotuba yake katika sherehe za Miaka 50 ya Muungano, zilizofanyika Muscat katika Hotel ya Intercontinental.
Mheshimiwa Ali Ahmed Saleh, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman (mwenye shati la kitenge) pamoja na Mgeni Rasmi, Mheshimiwa Ahmed Al Mahrazi, Waziri wa Utalii wa Oman ( wa pili toka kulia) wakikabidhi tuzo kwa mwakilishi wa Benki ya watu wa Zanzibar (PBZ LTD) katika sherehe za Miaka 50 ya Muungano, zilizofanyika Muscat katika Hotel ya Intercontinental.

MKUTANO WA SIKU MBILI KWA WANAHABARI WAMALIZIKA JIJINI ARUSHA

0
0
Mwenyekiti wa MISA-Tanzania ,Mohamed Tibanyendera akizungumza wakati wa mkutano wa wanahabari pamoja na wadau wao katika siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani,mkutano uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mgeni rasmi katika mkutano huo Mh Jaji Mstaafu Mark Bomani akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa wanahabari pamoja na wadau wao katika siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani,mkutano uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Mwenyekiti wa jukwaa la wahariri Tanzania,TEF,Absalomu Kibanda akitoa hotuba yake wakati wa mkutano wa wanahabari pamoja na wadau wao katika siku ya Uhuru wa vyombo vya habari Duniani,mkutano uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa AICC jijini Arusha.
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakifuatilia kwa karibu hotuba zilizokuwa zikitolewa wakati wa mkutano huo.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

TIMU 16 KUSHIRIKI LIGI KUU MSIMU WA 2015/2016

0
0
Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuanzia msimu wa 2015/2016 itakuwa na timu 16 badala ya 14 za sasa.

Mabadiliko hayo yamepitishwa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana jana (Mei 3 mwaka huu) jijini Dar es Salaam baada ya kupokea mapendekezo ya kuongeza idadi ya timu kutoka kwenye Kamati ya Mashindano.

Uamuzi huo umefanywa kwa lengo la kuongeza ushindani katika ligi hiyo, na kuwezesha wachezaji kupata mechi nyingi zaidi za mashindano. Kwa mabadiliko hayo maana yake ni kuwa Ligi ya msimu wa 2015/2016 itakuwa na mechi 240 wakati kwa sasa ina mechi 182.

Kuhusu idadi ya wachezaji wa kigeni kwenye VPL, Kamati ya Utendaji itafanyia uamuzi mapendekezo katika eneo hilo baada ya kwanza kupata maoni ya klabu za VPL na Ligi Daraja la Kwanza (FDL) ambazo Mei 11 mwaka huu zitakutana na Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Mapendekezo ya Kamati ya Mashindano ni kuwa idadi ya wachezaji wa kigeni iendelee kuwa watano kama ilivyo katika kanuni za sasa za VPL.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

Dkt. Migiro: Nia ya Serikali ni kuongeza uwazi zaidi

0
0
Waziri wa Katiba na Sheria Dr. Asha-Rose Migiro akiwasilisha taarifa ya makadirio ya bajeti ya Wizara yake kwa Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala jana (Jumamosi, Mei 3, 2014). Kulia kwake ni Naibu wake Angellah Kairuki na wa pili kulia ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Wiliam Ngeleja.
Baadhi ya Maofisa wa Wizara ya Katiba na Sheria wakifuatilia mkutano huo. Picha na Wizara ya Katiba na Sheria.

Na Omega Ngole

Serikali imesisitiza nia yake ya kuendesha shughuli zake kwa uwazi na kusema maandalizi ya kutunga sheria ya haki ya kupata taarifa kutoka kwa taasisi za umma yameanza kuongeza uwazi katika uendeshaji wa shughuli za serikali.

Akiwasilisha taarifa ya makadirio ya matumizi kwa mwaka ujao wa fedha kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala jijini Dar es Salaam jana (Jumamosi, Mei 3, 2014), Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Asha-Rose Migiro alisema dhamira hiyo inatokana na matakwa ya Katiba kuhusu haki ya kupata taarifa, Mpango wa Kimataifa wa Uendeshaji wa Serikali kwa Uwazi (OGP) na ahadi ya Rais Kikwete.

Tangazo la Msiba Philadelphia na New York

0
0
Mama Harriette Peace Kagaruki  (pichani) amefariki dunia huko Philadelphia tarehe 28 Apil 2014. Marehemu alikuwa anaishi Tanzania na alikuwa amekuja Marekani kuwasalimia wanawe Erick Kagaruki (Ohio) na Mary Kagaruki (Philadelphia), na ndipo alipougua ghafla na baadae kuaga dunia. 
Marehemu Mama Kagaruki hakuwa mkazi wa Marekani. 

Kwa maana hiyo na kwa sababu msiba huu umetokea ghafla na kwa sababu ni Mtanzania mwenzetu tunaomba tusaidiane ili tuweze kufanikisha shughuli za msiba huu ili aweze kupelekwa Tanzania. 
Kwa vile Marehemu alikuja kutoka Tanzania kutembelea wanawe hana rafiki au watu wa kumsaidia kufanikisha msiba wake hivyo msiba huu ni wetu Watanzania wote waishio Marekani, wewe na mimi. Hivyo tunawaomba muonyeshe ukarimu wenu ili msiba huu uweze kufanikiwa. Kiasi cha dolla 20,000 kinahitajika na tunawaomba mtoe michango ili tuweze kufikisha kiasi hicho. Toeni Kupitia Account Number ifuatayo:
 
Wells Fargo Bank
Routing #: 031000503
Account# 6595913119
 Jina la mwenye akaunti ni la Mtoto wa Marehemu: Mary Kagaruki
 Mwili wa Marehemu kwa sasa uko:
Funeral Home
366 West Lancaster Avenue
Wayne PA 19087
Tel: 610-989-9600 or 610—449-0300
 Kwa taarifa zaidi za msiba huu wasiliana na:
Erick Kagaruki – 937-361-4189
Mary Kagaruki – 267-963-8190
Abbas Babyusha – 914-584-7502
Doris Rweyemamu – 646-379-9135
 
Kwa wale wasioweza kutoka michango kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu mnaweza kufika ubalozi New York na kumkabidhi Ms. Doris Rweyemamu michango yenu na simu yake ni 646-379-9135. Doris atakusanya vile vile michango ya Watu   wa Mount Vernon akisaidiwa na Abbas Byabusha (914-584-7502).
 
Dr. Temba  (347-489-6532) na Raphael Faida (347-869-2230) nao watakuwa wakikusanya michango kutoka kwa Wanajumuiya.
 
Tunawaomba Watanzania wote wa Marekani watusaidie kwa kutoa michango ili tufanikishe shughuli za msiba huu.
 
Kwa niaba ya Familia ya Wafiwa na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania,
 
Deogratius Mhella,
Katibu, New York Tanzanian Community.

Uzinduzi wa Tovuti ya Mhe. Stephen Wasira jijini Dar es salaam leo

0
0
Mhe. Stephen Wasira amezindua tovuti itasaidia umma kupata taarifa zinazohusu shughuli za maendeleo na changamoto katika jimbo la Bunda na nyinginezo. 
Taarifa hizi zinapatikana kwa lugha za Kiswahili na Kiingereza. Unaweza kuzipata kulingana na kifaa (device) ukitumiacho kama desktop/laptop computer (PC), tablet na simu za mkononi. Mbunge wa Serengeti Mhe. Dr. Kebwe alikuwepo pia. 
Muonekano wa tovuti ya Mhe Stephen Wasira wakati wa uzinduzi wake leo
Mhe. Wasira akiangalia tovuti yake baada ya kuizindua leo
Mhe Wasira akiwa na Dkt. Kebwe Stephen KEBWE Mbunge wa Serengeti na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii wakati wa hafla hiyo fupi
Wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa tovuti hiyo

President Kikwete arrives in Arusha to open the 12th IAWJ Biennial conference tomorrow

0
0
 The President of International Association of Women Judges(IAWJ) Hon judge Eusebia Munuo welcomes President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete shortly after he arrived at Kilimanjaro International Airport in Arusha today. The President is expected to officiate the 12th IAWJ Biennial conference to be held Arusha International Conference Centre AICC tomorrow. Looking on third left is the Chief Justice Hon.Mohamed Othman Chande and left is the chairperson of Tanzania Women Judges Association Hon Judge Engera Kileo
President Dr.Jakaya Mrisho Kikwete chats with The President of International Association of Women Judges(IAWJ) Hon judge Eusebia Munuo and  Chief Justice Hon.Mohamed Othman Chande after hi.s arrival in Arusha.
Photos by Freddy Maro

wanahabari lindi washerehekea siku ya uhuru wa habari kwa kupima afya na kutoa misaada hospitali

0
0
WANAHABARI mkoa wa Wa Lindi wakiongozwa na Mwenyekiti wao Bw Abdulaziz Ahmeid wameadhimisha siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani kwa kutoa msaada kwa jamiii baada ya kutoa msaada wa Vifaa mbalimbali katika wodi za wazazi na watoto katika Hospital ya Rufaa ya Sokoine Mkoani Lindi
Wanahabari hapo pia walipimwa afya zao na  Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya mkoani humo ili kila mmoja afanye kazi zake huku akijua Afya yake 
 Akiongea baada ya hafla hizo Bw. Abdulaziz Ahmeid alieleza kuwa katika maadhimisho hayo ambayo kitaifa yamefanyika mkoani Arusha ambayo yana kauli mbiu ya Uhuru wa Habari kwa maendeleo na utawala bora Ambapo wanahabari wameamua kurudi kwa jamii kwa kuona umuhimu wa kusaidia wagonjwa,Wazee na Walemavu 
"Ni Vyema waandishi tukajenga Utayari wa kusaidia Jamii na ndizo zenye Uhitaji wa misaada muhimu na hata kihabari kuliko kujikita na wanasiasa kwa maslahi yao na wakati wao tu Muhimu Tujitambue tutetee haki zetu ikiwemo Kuajiriwa na kufungwa kwa mikataba kuliko ilivyo sasa zaidi ya asilimia 90 HATUJIELEWI.
"Sambamba na hilo Tujikite katika kuandika habari za Uchunguzi na fursa zipo kupitia TMF..Alimalizia Abdulaziz.
Nae Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Mkoa wa Lindi Bi Fortunata Kullaya ambae alikuwa Mgeni Rasmi katika sherehe hizo zilizokutanisha waandishi toka wilaya zote za mkoa wa Lindi aliwataka Waandishi kuandika habari kwa kufuata maadili ili wasijiingize katika matatizo hasa katika kipindi hiki cha mchakato wa katiba na kuelekea katika uchaguzi mkuu hapo mwakani kwa kuwa wanahabari ni watu muhimu katika jamii.
Pia aliwataka kufika vijijini kubaini baadhi ya changamoto ambapo pia aliwahakikishia kuwa Mfuko wa Afya ya Jamii CHF sasa ndio mkombozi wa huduma za afya hivyo pelekeni Ujumbe Jamii Ijiunge na ipate Tiba kwa Unafuu zaidi Nyie ni wadau wakubwa wa NHIF, hivyo mbaini kuwa kalamu zenu zinaweza kujenga au kubomoa hivyo bima ya afya Tawi Lindi 
"Tumeona ni siku muhimu sana kujumuika pamoja kwa kuwapima afya zenu ili mfanye kazi mkijijua Aidha katika maadhimisho hayo pamoja na lutoa msaada kwa Wagonjwa wa hospital ya Rufaa ya Sokoine na kupimwa kwa Afya za Waandishi 
hayo yalifuatiwa na Tafrija Fupi ya Kutakiana heri iliyojumuisha waandishi na Wenza wao pamoja na wadau wengine wa habari iliyofanyika katika Fukwe za Santorin Beach Manispaa ya Lindi
 Mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa Habari Lindi Bw. Abdulaziz Ahmeid akipimwa afya yake na daktari wa NHIF Timoth Mwasajone katika kuadhimisha siku ya Uhuru wa Habari
 Picha ya pamoja ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Mfuko wa NHIF Mara baada ya mfuko huo kujitolea kupima Afya za waandishi wa Lindi
  Mwandishi wa Tbc Lindi Martina Ngulumbi akimbeba  mtoto toka kwa mama alietoka kujifungua siku ya uhuru wa habari
 .Mwenyekiti wa LPC ,Abdulaziz Ahmeid akikabidhi msaada Kwa Muuguzi wa zamu Bi Habiba Chitanda msaada uliotolewa na Wanahabari wa Lindi
Mwenyekiti Abdulaziz akisalimia baadhi ya watoto waliolazwa katika wodi ya watoto katika hospitali ya Sokoine mjini Lindi mara baada ya kukabidhi vifaa mbalimbali katika kusaidia jamii katika siku ya uhuru wa habari

Ole Naiko afungua semina ya mafunzo ya wajasiriamali

0
0

 Mlezi wa  Asasi ya Diana Women Empowerment Organization ambaye pia Balozi wa Heshima wa Botswana nchini Tanzania, Bw. Emanuel Ole Naiko kati akifungua semina ya mafunzo ya wajasiriamali ambao ni wanachama wa asasi hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Kulia ni Mwenyekiti wa taifa wa asasi hiyo, Bi. Farida Khakoo na kushoto ni Katibu wa Taifa wa asasi hiyo, Bi. Joyce Singano.
Mlezi wa  Asasi ya Diana Women Empowerment Organizationambaye pia Balozi wa Heshima wa Botswana nchini Tanzania, Bw. Emanuel Ole Naiko kulia akiangalia kazi za mikono zinazotengenezwa na wajasiriamali ambao ni wanachama wa asasi hiyo  na kushoto ni Mwenyekti wa asasi hiyo taifa, Bi. Farida Khakoo.

VETA MAKETE WATEMBELEA WATOTO YATIMA NA KUTOA MISAADA MBALIMBALI

0
0
 Wafanyakazi wa VETA Makete wakiwa katika picha na watoto yatima wa kituo cha Bulongwa. Kwa habari kamili na picha zaidi

Benki ya NBC yatoa elimu ya kifedha kwa wateja mjini Morogoro na kufundisha watoto kusoma jijini Dar

0
0
Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Amanzi (kushoto) akipokea kitabu chenye mafundisho ya kifedha yanayofuata maadili ya kiiislamu kutoka kwa Meneja Tawi wa Benki ya NBC Morogoro, James Ndimbo wakati wa semina iliyoandaliwa kwa wateja wanaotumia huduma za kibenki zinafuata misingi ya kiislamu (NBC Islamic Banking ), iliyofanyika mjini humo hivi karibuni. Anayeangalia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA) Mkoa wa Morogoro, Bachoo S. Bachoo.
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Industrial, Judith Motta, (kulia) akiwafundisha kusoma baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in the Sun ikiwa ni sehemu ya mpango wa mameneja wa benki hiyo kanda ya Dar es Salaam hivi karibuni kujitolea muda wao kufundisha kwenye vituo mbalimbali vya watoto wanaoishi katika vituo vya watoto wenye mahitaji. Wanafunzi wapatao 27 katika kituo hiki kinachokusanya watoto toka mitaani na kuwalea chini ya uangalizi wenye maadili mzuri na mafunzo ya kazi za mikono hawajui kusoma wala kuandika.
Baadhi ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Child in the Sun kilichopo Mbezi Makabe wakifanya mazoezi ya kusoma na kuandika baada ya kutoka madarasani walikkofundishwa na timu ya Mameneja wa matawi ya NBC yaliyoko Kanda ya Dar Salaam. Tathmini ya wiki ya tatu inaonyesha watoto wote wameshajua kusoma na kuandika na changamoto inayofuata ni kuunganisha maneno na kutunga tungo zenye kuleta maana.

Orodha kamili ya washindi wa Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2014

0
0
Ankal akimkabidhi Tuzo Mtunzi bora wa mwaka bendi Christian Bella.
 Ankal akila selfie na Jose Mara aliyeibuka Mwimbaji Bora wa Bendi wa Kiume
Ankal na DJ Bonny Love na mdau wakiwa na mshindi wa Wimbo bora wa Afrika Mashariki  Jose Chameleone aliyeibuka kidedea kwa kibao chake cha "Tubonge" (BOFYA HAPA uusikie).

1.Wimbo bora wenye vionjo vya asili ya Tanzania ilichukuliwa na wimbo wa Bora Mchawi (Dar Bongo Massive).
2.Msanii Bora chipukizi (Young Killer).
3. Wimbo bora wa Zouk (Yahaya) wa Lady Jay Dee.
4. Wimbo wa Afropop (Number One) na Diamond Platnumz
5. Wimbo bora wa Ragga/Dancehall (Nishai) na Juru ft. Tash.
6. Wimbo bora wa kiswahili (Ushamba Mzigo) na Mashujaa Band.
7. Mwimbaji bora wa kiume taarab (Mzee Yusuph).
8. Mwimbaji bora wa kike Taarabu (Isha "Mashauzi"Ramadhani).
9. Wimbo bora wa Taarab (Wasi wasi wako) na Mzee Yusuph.
10. Wimbo bora wa Reggea imechukuliwa na wimbo wa (Niwe na wewe) na  Dabo.
11. Mtunzi bora wa mwaka Hip hop (Fid Q).
12. Wimbo bora wa kushirikisha/kushirikiana (Muziki Gani) na  Ney wa Mitego ft.Diamond.
13. Msanii bora wa Hip Hop  (Fid Q).
14. Wimbo bora wa Hip Hop (Nje ya Box) na Nikki wa Pili ft.Joh Makini na G Nako.
15. Mwimbaji bora wa kiume kizazi kipya (Diamond Platnumz).
16. Mwimbaji bora wa kiume Bendi  (Jose Mara).
17. Mwimbaji bora wa kike bendi (Luiza Mbutu).
18. Wimbo bora wa R&B (Closer) na Vanessa Mdee.
19. Kikundi bora cha mwaka (Weusi).
20. Mtunzi bora wa mwaka (Diamond Platnumz).
21. Mtunzi bora wa mwaka bendi (Christian Bella).
22. Mtunzi bora wa mwaka taarab (Mzee Yusuph).
23. Wimbo bora wa Afrika Mashariki (Tubonge) na  Jose Chameleone.
24. Wimbo bora wa mwaka (Number One) na Diamond Platnumz.
25.Tuzo ya heshima ya Hall of fame ya Taasisi (Masoud Masoud wa TBC FM).
26.Tuzo ya heshima ya Hall of fame mtu mmoja mmoja  (Hassan Rehan Bitchuka).
27. Mtumbuizaji bora wa kike wa mwaka (Isha  "Mashauzi" Ramadhani.
28. Wimbo bora wa mwaka  (Number One) Diamond Platnumz.
29. Mtayarishaji bora wa nyimbo za kizazi kipya (Man Water).
30. Mtayarishaji bora wa nyimbo wa bendi (Amoroso).
31. Video bora ya Muziki ya Mwaka (Number One) na Diamond Platnumz.
32. Kikundi bora cha mwaka Taarab (Jahaz Modern Taarab).
33. Kikundi bora cha mwaka bendi (Mashujaa).
34. Rapa bora wa bendi wa mwaka (Ferguson)
35. Mtayarishaji bora wa mwaka taarabu (Enrico)
36. Mtumbuizaji bora wa kiume kizazi kipya (Diamond Platnumz).

MKUTANO WA HADHARA WA CCM WAFUNIKA KIBANDA MAITI MJINI UNGUJA LEO

0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,Balozi Seif Ali Idd akiwasalimia wananchi wa Unguja waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa hadhara wa Chama cha Mapinduzi (CCM) uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.
Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Aman Katume,Mama Fatma Karume akiongea kwa msisitizo mkubwa huku akiwataka Wazanzibar kuacha kabisa kuuchezea Muungano kwa kuwafata watu wanaoupotosha.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akimpongeza Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar,Hayati Aman Katume,Mama Fatma Karume mara baada ya kuzungumza na wazanzibar jioni ya leo waliofurika kwa wingi kwenye Uwanja wa Demokrasia ,Kibada Maiti mjini Unguja.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiwaeleza wananchi wa Unguja kuhusu umoja ulioanzishwa wa baadhi ya vyama siasa na malengo ya umoja huo,wakati wa Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar. 
Mbunge wa Viti Maalum CCM,Mh. Ummy Mwalimu akiwahutubiwa wananchi wa Zanzibar kupitia Mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar jioni ya leo.ambapo amewataka Wazanzibari kutohadaishwa na UKAWA kususu swala la muundo wa Serikali katika mchakato wa Katiba.
Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini,Mh. Emmanuel Nchimbi akinukuu sehemu ya maandishi yaliopo kwenye kitabu cha Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Maalim Seif Sharif Hamad wakati wa Mkutano wa hadhara wa CCM uliofanyika jioni ya leo kwenye Uwanja wa Demokrasia uliopo eneo la Kibanda Maiti,Mjini Unguja Zanzibar.

News alert: watatu wapoteza maisha zaidi ya 60 wajeruhiwa kwa mabomu kwenye mabasi ya abiria nairobi leo

0
0
Watu watatu wamepoteza maisha na wengine 62 kujeruhiwa baada ya mabomu mawili kulipuka Jumapili ya leo katika barabara ya Thika, ambayo ni moja ya njia kuu zenye magari mengi jijini Nairobi, Kenya.Majeruhi 20 kati ya hao wako mahututi.


Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi la Kenya Bw. Moses Ombati amenukuliwa akisema kuwa  mabomu hayo yamelipuka kwenye mabasi ya abiria mawili tofauti, ambapo Naibu Mkuu wa kitengo cha kutengua Mabomu, Bw, Eliud Lagat amesema milipuko hiyo imetokana na mabomu yaliyotengenezwa kienyeji.


Milipuko hiyo na maafa hayo yamekuja siku moja baada ya watu wanne kuuwawa kwa mlipuko wa bomu ya kutupwa kwa mkono katika kituo cha mabasi mjini Mombasa. Mlipuko mwingine katika ufukwe wa bahari haukuleta madhara.



Kenya imekumbwa na wimbi la mashambulio ya bunduki na milipuko ya mabomu toka nchi hiyo ilipopeleka majeshi yake kupambana na wanaodaiwa kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi la Al-Shabab mwaka 2011, ambao wameapa kuendeleza mashambulio ya kigaidi kama kulipiza kisasi kwa kuwepo kwa majeshi ya Kenya nchini Somalia.


Airtel yazindua duka la kisasa Mlimani City

0
0
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua rasmi duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia, wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja wa duka Wahida Saleh na Sunil Colaso Mkurugenzi Mkuu Airtel Tanzania.
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet akikata utepe kuzindua duka la Airtel lililopo mlimani city jijini Dar es Saalam.wakishuhidia, wapili ni Andre Beyers Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika akiwa na meneja wa duka Wahida Saleh na Adriana Lyamba Mkurugenzi wa kitengo cha huduma kwa wateja Airtel Tanzania.
Afisa mtendaji Mkuu Airtel Africa Christophe Soulet na Afisa mkuu wa masoko Airtel Afrika Andre Beyers wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Airtel katika duka la mlimani City mara baada ya uzinduzi rasmi wa duka hilo lililofanyiwa matengenezo na kuwa la kisasa zaidi
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania,Beatrice Singano Mallya akipata maelezo ya huduma za Airtel kutoka kwa wafanyakazi wa Airtel katika duka la mlimani City mara baada ya uzinduzi wa duka hilo lililofanyiwa matengenezo na kuwa la kisasa zaidi.
Airtel Tanzania mwishoni mwa wiki hii imezindua duka la Mlimani City baada ya kulifanyiwa  matengenezo na kulipatia sura ya kisasa zaidi. Uzinduzi huu ni kielelezo cha kampuni hiyo  kutoa huduma bora za simu kwa wateja wake

 Akiongea wakati wa uzinduzi Christophe Soulet, Afisa Mtendaji Mkuu Africa alisema” Airtel tunaamini katika kutoa huduma bora za kisasa zinazoendana na mahitaji ya wateja wetu huku tukiwapa uzoefu wa pekee katika huduma zetu.  Mpango huu wa kuboresha maduka yetu unafanyika katika masoko yetu yote yaliyoko barani Afrika na Leo ninayofuraha kuzindua duka hili la kisasa lijulikanalo kama Express shop hapa nchini Tanzania. Duka hili la kisasa linathibitisha  dhamira yetu ya kutoa huduma bora Tanzania na Afrika kwa ujumla

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bwana Sunil Colaso  alisema” duka hilo ni la kwanza kuzinduliwa kwani tunabadilisha maduka yetu yote nchi nzima na kuyafanya yawe na mtazamo mpya na wa kisasa zaidi. Duka hili limetengenezwa na kuhakikisha mteja ataweza kupata huduma kwa haraka , kwa usalama bila usumbufu wowote

Aliongeza kwa kusema Airtel inapenda kuwahakikishia wateja kupata huduma bora wakati wote na pia kupata simu za aina mbalimbali ambazo zitapatikana katika duka hilo jipya la Mlimani City.

Kwa kupitia mtandao wetu mpana ulionea zaidi tunawahakikishia wateja wetu huduma bora za kisasa, za uhakika jijini Dar es salaam

Duka la Mlimani City litaendelea kuuza bidhaa mbalimbali kama vile modem na simu za aina mbalimbali ,  wateja watapata huduma ya Airtel money kwa usalama zaidi , kuunganisha na huduma za simu za malipo ya mwenzi na ya awali , pamoja na huduma za internet na kuunganishwa na mtandao  na kuperuzi kwenye internet , kununua muda wa maongezi pamoja na huduma nyingine nyingi.

Airtel Tanzania inaendele kuboresha huduma zake kwa wateja ambapo inaendele kuboresha maduka yake nchini nzima kwa mwaka huu wa 2014.  Mpango ni kuwafikiwa wateja wengi zaidi na kuboresha huduma zake kupitia maduka yake yote yaliyoko nchi nzima. 

SHERIA GANI INATUMIKA KURUHUSU UHIFADHI TAKA WA AINA HII,KANDO KANDO YA BARABARA KUU??

0
0
 Kamera ya Globu ya Jamii,mchana wa leo imepita kwenye barabara ya Morogoro rodi kuanzia Magomeni mpaka Shekilango na kukuta malundo ya taka ngumu yakiwa yamekusanywa kwa mafungu mafungu namna hii.hapo ndipo swali likanijia,kwamba hivi uhifadhi taka wa namna hii umeruhusiwa kisheria ama ni ndio mambo yetu yake yale kuleana.?? na kama ni Sheria ni ipi inayoruhusu uchafuzi wa mazingira namna hii?? nilijikuta nikikosa majibu na ndipo ilipobidi kuja na mada hii hapa Globu ya Jamii ili tuweze kusea aidia.picha hii imepigwa Magomeni Kagera.
 mbele kidogo ya kituo cha Magomeni Kagera kuna lundo lingine kama lionekanavyo pichani na nyuma ya taka hizo kuna mgahawa wa Mama ntilie ambaye anawauzia watu Chakula. 
Hili lingine liko Manzese karibu kabisa na Kituo cha kwa Bahresa.

MAMA SALMA KIKWETE KATIKA SHEREHE ZA KILELE CHA SIKU YA WAKUNGA DUNIANI

0
0
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akitembelea mabanda mbalimbali yaliyokuwa yakitoa huduma ya afya ya mama na mtoto wakati wa kilele cha cha sherehe za siku ya wakunga duniani iliyoadhimishwa kitaifa mkoani Dar es Salaam tarehe 5.5.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimsalimi mtoto Rahim mwenye umri wa miezi 2 akiwa na baba yake ndugu Amir Adam, 35, na mama yake Hamida (kushoto) walipompeleka kupata chanjo wakati wa sherehe za kilele cha siku ya wakunga duniani iliyoadhimishwa kitaifa katika viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 5.5.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia wakunga na wananchi waliohudhuria sherehe za kilele cha siku ya wakunga duniani iliyofanyika kitaifa hapa nchini kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja tarehe 5.5.2014.

Taarifa ya Msiba Philadelphia na New York

0
0
Mama Harriette Peace Kagaruki amefariki dunia huko Philadelphia tarehe 28 Apil 2014. Marehemu alikuwa anaishi Tanzania na alikuwa amekuja Marekani kuwasalimia wanawe Erick Kagaruki (Ohio) na Mary Kagaruki (Philadelphia), na ndipo alipougua ghafla na baadae kuaga dunia.

Marehemu Mama Kagaruki hakuwa mkazi wa Marekani. Kwa maana hiyo na kwa sababu msiba huu umetokea ghafla na kwa sababu ni Mtanzania mwenzetu tunaomba tusaidiane ili tuweze kufanikisha shughuli za msiba huu ili aweze kupelekwa Tanzania. Kwa vile Marehemu alikuja kutoka Tanzania kutembelea wanawe hana rafiki au watu wa kumsaidia kufanikisha msiba wake hivyo msiba huu ni wetu Watanzania wote waishio Marekani, wewe na mimi. Hivyo tunawaomba muonyeshe ukarimu wenu ili msiba huu uweze kufanikiwa. Kiasi cha dolla 20,000 kinahitajika na tunawaomba mtoe michango ili tuweze kufikisha kiasi hicho. Toeni Kupitia Account Number ifuatayo:

Wells Fargo Bank
Routing #: 031000503
Account# 6595913119

Jina la mwenye akaunti ni la Mtoto wa Marehemu: Mary Kagaruki

Marehemu kwa sasa yuko:
Funeral Home
366 West Lancaster Avenue
Wayne PA 19087
Tel: 610-989-9600 or 610—449-0300

Kwa taarifa zaidi za msiba huu wasiliana na:
Erick Kagaruki – 937-361-4189
Mary Kagaruki – 267-963-8190
Abbas Babyusha – 914-584-7502
Doris Rweyemamu – 646-379-9135

Kwa wale wasioweza kutoka michango kwenye akaunti iliyotajwa hapo juu mnaweza kufika ubalozi New York na kumkabidhi Ms. Doris Rweyemamu michango yenu na simu yake ni 646-379-9135. Doris atakusanya vile vile michango ya Watu   wa Mount Vernon akisaidiwa na Abbas Byabusha (914-584-7502).

Dr. Temba  (347-489-6532) na Raphael Faida (347-869-2230) nao watakuwa wakikusanya michango kutoka kwa Wanajumuiya.

Tunawaomba Watanzania wote wa Marekani watusaidie kwa kutoa michango ili tufanikishe shughuli za msiba huu.

Kwa niaba ya Familia ya Wafiwa na Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania,

Deogratius Mhella,
Katibu, New York Tanzanian Community.

NDUGU HUYU ANATAFUTWA NA NGUGU YAKE WALIEPOTEZANA KWA MUDA MREFU

0
0
MIMI MARIDADI KILONZO KUTOKA MUHEZA, TANGA, TANZANIA NAMTAFUTA NDUGU YANGU  ALIYEKUWA ANAITWA MWANAHAWA KILONZO, AMEZALIWA MWAKA 1986 (06 NOVEMBA) NA AKABADILISHA JINA NA KUITWA ROSE MICHAEL GAVIGAN WAKATI ALIPOCHUKULIWA NA SHANGAZI YETU REHEMA NGAMI (KILONZO MDHAM) NA MUME WAKE MICHAEL GAVIGAN KWENDA KUISHI NAYE UINGEREZA MWAKA 1993. 

TANGU MWAKA HUO HAJARUDI TENA NA HATUNA MAWASILIANO NAYE TENA. SHANGAZI REHEMA ALISHARUDI TANGU MWAKA 1997 NA BAHATI MBAYA AMEFARIKI MWEZI APRIL 2014. 

MAMA NAYE ALISHAFARIKI SIKU NYINGI. KABLA SHANGAZI HAJAFARIKI ALITUACHIA ANUANI HIZI ZIFUATAZO AMBAZO HATUNA UHAKIKA KAMA WAHUSIKA BADO WAKO HAPO KWANI TULIANDIKA BARUA LAKINI HATUJAPATA MAJIBU:- 

MICHAEL GAVIGAN, MRS. R. GAVIGAN,
69 THORNEYWOOD RISE, 10 FREDERICK AVE
THORNEYWOOD, CARLTON,
NOTTINGHAM, NOTTINGHAM,
NG 3 2PE, NG4, IHP,
ENGLAND.ENGLAND. 

KWA HIYO HAKUNA MTU ANAYEFAHAMU HABARI ZAKE TENA. MARA APATAPO UJUMBE HUU TAFADHALI NAOMBA AWASILIANE NAMI KWA NAMBA +255656487459.

HAPA NAAMBATANISHA PICHA ZA ROSE (MWANAHAWA) NILIZOFANIKIWA KUZIPATA.
NASHUKURU SANA.
Viewing all 109593 articles
Browse latest View live




Latest Images