Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 437 | 438 | (Page 439) | 440 | 441 | .... | 3286 | newer

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi hundi ya jumla ya Shilingi Milioni miamoja na Hamsini 150m/- kwa wawakilishi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Moyo wa Huruma kilichopo mkoa wa Geita.

  Fedha hizo si sehemu ya shilingi milioni mia saba(700m/-) alizokabidhi Rais Kikwete jana usiku kwa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na mapambano dhidi ya ukimwi Tanzania.Fedha hizo zinatokana na kampeni ya kukusanya fedha kwa njia ya kupanda mlima Kilimanjaro kila mwaka ambapo wafadhili mbalimbali huchangia watoto na watu wengine.Pichani watoto wawili watakaopanda mlima Kilimanjaro Jacob Musa(watatu kushoto) na Julitha Sylvester(wapili kulia) wanaofadhiliwa na kituo cha Moyo wa huruma wakipokea hundi ya kituo chao.

  Wengine katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr.Florence Turuka,Mkurugenzi Mkuu wa TACAIDS Bi Fatma Mrisho,Mkurugenzi Mtendaji wa Geita Gold Mines Bwana Michael Van Anen(watano kushoto),Naibu Waziri wa Afya Dr.Steven Kebwe, na kulia ni msimamizi wa kituo cha kulelea watot yatima cha Moyo wa Huruma Sista Adalbera Mukure.
  Katika hafla ya jana ya kuchangia kampeni hiyo iliyofanyika katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro jijini Dar es Salaam zaidi ya shilingi milioni mia tisa 900m/- zilikusanywa(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Postamasta mkuu na afisa mtendaji mkuu wa shirika la posta Tanzania Ndugu Deos Khamisi Mndeme(mwenye koti kushoto) akikabidhi cheti na hundi kwa mfanyakazi bora kitaifa kutoka wafanyakazi wasimamizi, Ndugu Michael Mhagama (kulia).
  Ndugu Deos Khamisi Mndeme akikabidhi cheti na hundi kwa mfanyakazi bora kutoka wafanyakazi watendaji Ndugu Joseph Kakokele.

  Mfanyakazi bora kutoka Divisheni ya Rasimali za Shirika, Fredrick Makundi, akipokea cheti na tuzo kutoka kwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati wa hafla hiyo.
  Mfanyakazi bora kutoka Divisheni ya Rasimali za Shirika, Abdallah Waziri, akipokea cheti na tuzo kutoka kwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati wa hafla hiyo.
  Mfanyakazi bora kutoka Ofisi ya Postamasta Mkuu, Mashala Lifunga, akipokea cheti na tuzo kutoka kwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakati wa hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
  Mfanyakazi bora kutoka  Ofisi ya Postamasta Mkuu, Christopher Mjema, akipokea cheti na tuzo kutoka kwa Postamasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), kwenye hafla hiyo.
   

  0 0


  Vikwangua anga vinavyoendelea kuibuka kwa kasi katika eneo la Chake Chake,Kusini Pemba

  Chai Maharage bado ndio usafiri unaoaminika kwa kusafirishia abiria katika maeneo mbali mbali huku visiwani Zanzibar.

  Chake Chake,Pemba.  0 0

  Katibu  wa chama  cha waandishi wa habari  mkoa wa Iringa (IPC) Francis Godwin wa pili  kulia  akiongoza  wanahabari na wananchi wa kata ya Ilala kwenda kufanya usafi wa mazingira   leo  wakati wa maadhimisho ya siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani.
  Wanahabari  mkoa wa Iringa  wakiadhimisha siku ya uhuru wa  vyombo vya habari kwa kufanya usafi.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akifungua kongamano la siku mbili la Kitaifa la Ajira kwa Vijana katika ukumbi Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja leo.
  Baadhi ya washiriki katika Kongamano la Kitaifa la Ajira kwa Vijana wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akitoa hutuba yake ya ufunguzi leo katika ukumbi wa Salama Bwawani Hotel Mjini Unguja.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.

  0 0

  Mhe. Naimi Aziz, Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia na mwakilishi wa kudumu katika Umoja wa Afrika akiongoza mkutano wa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika uliofanyika tarehe 2 Mei 2014 mjini Addis Ababa, Makao Makuu ya Umoja huo. Tanzania itakuwa mwenyekiti wa chombo hicho muhimu kinachoshughulikia Amani na Usalama barani Afrika kwa kipindi cha Mwezi Mei 2014. Katika kipindi cha Uwenyekiti wake, Tanzania pamoja na mambo mengine itaongoza Baraza hilo katika kujadili na kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa migogoro inayoendelea huko mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Sudani ya Kusini,, Afrika ya Kati, Mali na ukanda wa Sahel, pamoja na Darfur, Sudan. Aidha, Tanzania itaongoza mjadala wa wazi (open session) kuhusu hali ya watoto katika migogoro barani Afrika ( Children in Armed Conflicts in Africa). Tanzania itaongoza pia mkutano wa pamoja wa majadiliano ( joint consultative meeting) kati ya Baraza la Amani na Usalama la Afrika na Baraza la Amani na Usalama la Ulaya utakaofanyika Brussels, Ubelgiji. Wakati wa kusherehekea miaka 10 ya kuanzishwa kwa Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika tarehe 25 Mei 2014, Tanzania itaongoza mjadala kuhusu "Miaka 10 ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika mafanikio, changamoto zilizopo na namna ya kusonga mbele".
  Bw. Samwel Shelukindo, Afisa Mambo ya Nje Mkuu wa Ubalozi wa Tanzania Addis Ababa akiwa katika kikao cha Baraza la Amani na Usalama la Afrika kilichokuwa kinaongozwa na Mhe. Balozi Naimi Aziz wa Tanzania.

  0 0

  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akishiriki katika Mkutano wa tano wa wa Nchi za Jumui ya Afrika Mashariki wa tano wa ushirikiano wa miradi ya maendeleo ya ukanda wa kaskzin (5th Summit of the Northern Corridor Intergration Projects)Uliofanyika kwenye hoteli ya Safari Park mjini Nairobi Mai 2, 2014.Viongozi waliohudhria mkutano huo ni Makamu wa Rais wa Kenya William Ruto, Makamu wa Rais wa Burundi, Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na viongozi Wakuu wa Nchi za Afrika ya Mashariki katika mkutano wao wa tano wa ushirikiano wa Maendeleo wa miradi ya maendeleo wa ukanda wa Kaskazini (5th Summit of the Northern Corridor Intergration Projects) uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Safari Park, Nairobi May 2/2014. Alimwakilisha Rais Jakya Kikwete katika mkutano huo. Viongozi hao kutoka kushoto ni Makamu wa Rais wa Kenya William Samoei Ruto, Makamu wa Rais wa Burundi, Rais wa Rwanda Paul Kagame, Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta na Rais wa Uganda Yoweri Museveni.
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Rais wa Kenya ,Uhuru Kenyatta katika mkutano wao wa tano wa ushirikiano wa Maendeleo wa miradi ya maendeleo wa ukanda wa Kaskazini (5th Summit of the Northern Corridor Intergration Projects) uliofanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Safari Park, Nairobi May 2/2014. Alimwakilisha Rais Jakya Kikwete katika mkutano huo.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Rais wa Shirika la Simu la China Bwana Yang Jie ikulu jijini Dar es Salaam leo. Bw. Yang na ujumbe wake walimtembelea Rais Kikwete ikulu na kufanya naye mazungumzo yaliyohusu uboreshwaji wa miundo mbinu ya mawasiliano nchini

  0 0

  Na Woinde Shizza, Arusha 
  Jaji mstaafu Mark Bomani leo amezindua rasmi video ya wimbo wa waandishi wa habari ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu pamoja na albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani jijini Arusha. 
  Uhuru wangu uko wapi mwanahabari mie,kalamu yangu,sauti yangu kamera yangu leo ndio kaburi langu mie Huo ndio wimbo wa kundi la Mrisho Mpoto Band ambalo ulikuwa ukiwaburudisha wanahabari katika uzinduzi wa albamu Mrisho Mpoto Band,unaoelezea mambo mbalimbali wanayokumbana nayo wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari. 
  Akighani mashairi ya wimbo huo katika uzinduzialisema poleni sana misa Tanzania,TMF,MOAT,UTPC ,TCRA kama mtu ile timu ya watu watano tuyioituma Ujerumani ,Norway,Sweden ipo wapi ripoti yake 
  kiongea wakati wa uzinduzi wa albamu hiyo pamoja na wimbo huo wa wanahabari msanii mrisho mpoto alisema kuwa yeye alifarijika sana pale alivyofatwa na wanahabari na kumuomba awatungie wimbo ambao unawahusu wanahabari pamoja mambo ambayo yanawakabili. 
   Alisema kuwa wamekaa wakashauriana na timu yake na bendi yake kuwa watu wasanii wengi wamekuwa wakizindua albamu kwa kuweka viingilio vikubwa kualika watu wengi lakini yeye binafsi ameamua kuzindua albamu hii katika siku hii ya waandishi wa habari kwa kuwa wamemtoa mbali na ana kitu cha kuwapa zaidi ya kuwapa zawadi hii ya kuzindua albamu yake mbele yao. Alibainisha kuwa mbali nakuzindua albamu hiyo pia kwa kuwa waandishi wamempa hadhi ya kuwatungia wimbo pia anajitolea kuweka wimbo huu wa waandishi wa habari ndani ya albamu yake ili kila mtanzania na mshabiki wake ambaye atanunua albamu yake aukute wimbo ndani ya albamu yake. 
  "Hii albamu yangu itakuwa na nyimbo zangu zote ikiwa na wimbo wa nikipata nauli adi nyimbo zake zote ambazo zinajulikana na kiukweli najisikia kulia sana kupewa heshima hii nzito ya kuzindua albamu yangu na ata jana nilivyokuwa nakuja uku nilikuwa na zunguma na mh bomani kuwa hii kwangu itakuwa ni historia katika maisha yake"alisema mpoto 
  Katika wakati wimbo huu ukiendelea wanahabari walionekana wakitoa machozi kwa kuuzunishwa na tenzi zilizopo katika wimbo huu kwani msanii huu ameuimba kiualisiazaidi.

  Jaji mstaafu Mark Bomani akiongea wakati wa kuzindua rasmi video ya wimbo wa waandishi wa habari ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu pamoja na albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani jijini Arusha. 
  Jaji mstaafu Mark Bomani akizindua rasmi video ya wimbo wa waandishi wa habari ujulikanayo kwa jina la Uhuru wangu pamoja na albamu mpya ya msanii wa mziki wa nyimbo za asili Mrisho Mpoto ijulikanayo kwa jina la Waite katika kilele cha maathimisho ya uhuru wa vyombo vya habari duniani jijini Arusha. Chini Mrisho Mpoto akielezea wimbo wake.
  Picha na Woinde Shizza wa Globu ya Jamii, Arusha

  Video na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Moshi.

  0 0

   Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba, akifungua kikao cha siku tatu cha Baraza Kuu la Uongozi CUF Taifa, katika ofisi kuu za Chama hicho, Buguruni Dar es Salaam.
    Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba, akiongozana na Katibu Mkuu wa Chama hicho Maalim Seif Sharif Hamad, kuelekea ukumbi wa mikutano katika ofisi kuu za Chama hicho, Buguruni Dar es Salaam.
  Baadhi ya wajumbe wa Baraza Kuu la Uongozi CUF Taifa, wakifuatilia kikao hicho kinachofanyika Ofisi Kuu za CUF Buguruni Dar es Salaam. (Picha na Salmin Said, OMKR)

  0 0


  0 0

   Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.Katika hobuba yake,Ndg. Kinana amewataka Wananchi wa Kisiwani humo,kutohadaika na Wanasiasa wanapita kila mahali kwa lengo la kulipotosha Taifa,hasa juu ya swala la Muundo wa Serikali katika Mchakato wa Katiba Mpya.
   Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,Ndg. Vuai Ali Vuai akizungumza na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
   Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akiwapa somo wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.
  Makamu Mwenyekiti UWT,Bi. Asha Bakari Makame akizungumza kwa msisitizo mkubwa na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

  Naibu Katibu Mkuu UVCCM Zanzibar,Ndg. Shaka Hamdu Shaka akizungumza machache na wananchi wa Mikoa miwili ya Kisiwani Pemba waliofurika kwa wingi kwenye Mkutano wa Hadhara wa Chama cha Mapinduzi,uliofanyika jioni ya leo kwenye Viwanja vya Gombani ya Kale,Kisiwani Pemba.

  Vijana wa CCM, Fatma Juma Ramadhan (kushoto) na Halima Juma Hajj wakighani mashairi mazuri ya kumkaribisha Katibu Mkuu wa CCM,Ndg. Abdulrahman Kinana (hayupo pichani).


  0 0

  Mwanamuziki Mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platinum,akiwapagawisha mashabiki wake wa mkoa wa mtwara waliofurika katika Tamasha la Ties & Heels lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika kwenye ukumbi wa Makonde beach Mkoani Mtwara jana.
  Mwanamuziki Mahiri wa muziki wa kizazi kipya nchini Diamond Platinum,akicheza na madansa wake wakati wa Tamasha la Ties & Heels lililodhaminiwa na Vodacom Tanzania na kufanyika kwenye ukumbi wa Makonde beach Mkoani Mtwara jana.

  Mwanamuziki Mahiri wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini Diamond Platinum ameahidi kuwatendea haki wakazi wa mikoa ya kusini kila mwaka kwa kile anachodai mafanikio makubwa ya ndoto yake ya kuwa mwanamuzi bora hapa nchini imeanzia mkoa wa Mtwara.

  Mwanamuziki huyo  aliambatana na  kipenzi chake, Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu – ‘Beautiful Onyinye’ au Madame kama mashabiki wake walivyokuwa wakimuita amethibitisha kauli hiyo  kwa mashabiki wake waliofurika katika tamasha maalumu la Ties & Heels lililofanyika katika ukumbi wa makonde  beach Mkoani Mtwara na kudhaminiwa na kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania.

  Amesema tangu kuanza kwake kujiingiza kuwa mwanamuzi wa muziki wa kizazi kipya alianza kwa shoo yake mkoani mtwara ambapo ilionyesha kuwakuna wapenzi wengi na aliendelea kujulikana maeneo mengi hapa nchini kutokana na wapenzi walivyoanza kukumkubali, na ndipo aliwaahidi wapenzi hao kuwa ataendelea kuwasili mkoani humo kila mwaka kwa kulipa fadhila kwa mafanikio anayoyapata.

  Akizungumzia juu ya shoo hiyo iliyokuwa ya kukata na shoka kwa wakazi wa mkoa wa Mtwara, Mkuu wa Kanda ya kusini wa Vodacom Tanzania, Henry Tzamburakis amebainisha kuwa tukio hili limeandaliwa ikiwa ni sehemu ya burudani kwa wateja wetu, kufurahi kwa pamoja na kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutumia huduma zetu.

  “Hakuna kitu ambacho tunajali na kukithamini kama wateja wetu, haijalishi wawe kona gani ya Tanzania, walipo popote tutawafikia. Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza kwa mawasiliano nchini.” Alisema Tzamburakis.

  Kwa kuongezea Tzamburakis amewashukuru  wakazi na mashabiki wote wa Diamond na wapenzi wa muziki wa Bongo Flava kujitokeza kwa wingi kwani mbali na burudani wamenufaika na baadhi ya huduma na bidhaa mbali mbali za Vodacom.

  Nae Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu alieambatana na mpenzi wake alisema hakuona shida kumsindikiza asali wake wa moyo mtwara yote haya kwaajili ya mashabiki wao. Kwa tafsiri nyingine mashabiki wa Mtwara wanabahati kubwa ya kutembelewa nasi na tutadumisha utamaduni huu kila mwaka.

  0 0

  http://www.kililager.com/KTMA

  0 0

  Meneja wa kilaji cha Kilimanjaro Lager wa TBL Bw. George Kavishe azungumzia maandalizi ya Tuzo za Kili Music Awards zitazotolewa leo May 3, 2014 kuanzia saa tatu usiku katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam

  0 0


  Ufunguzi wa Shoo katika Tuzo za Kilimanjaro Tanzania Music umengozwa na msanii wa Bongo Fleva,Hamis Mwinjuma a.k.a MwanaFA akiwa ameambata na Wamasai kawa waonekanavyo pichani.
  Selfie ya Ankal na Anti ndani ya Ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es Salaam hivi sasa,wakiwa kwenye hafya ya utoaji tuzo za Kili Music Awards.


  0 0
 • 05/03/14--20:00: ngoma azipendazo ankal
 • Chameleone anakupa "Kipepeo"

  0 0  Mwimbaji Mahiri wa muziki wa nyimbo za Kiroho a.k.a Injili,Rose Muhando akiimba wimbo wake mpya wa Facebook na Twitter mbele ya mashabiki wake,katika uwanja wa Kambarage mapema jioni ya leo mkoani Shinyanga,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa tamasha la Pasaka.Tamasha hilo linaloandaliwa na Msama Promotions Ltd  kesho jumapili linaendelea katika uwanja wa CCM Kirumba jijiini Mwanza,ambapo Nyota wa Nyimbo za Injili kutoka nchini Afrika Kusini,Rebecca Malope atawatumbuiza wakazi wa jiji hilo sambamba na waimbaji wengine..
   Mwimbaji wa nyimbo za Injili,Upendo Kilahiro akiimba mbele ya wapenzi wa muziki wa injili ndani ya uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga.
    Sehemu ya wapenzi wa muziki wa injili wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri uwanjani hapo.
   Upendo Nkone,ambaye amejizolea sifa kubwa kwa kuimba nyimbo za kusifu na kuabudu,akiwaimbisha mashabiki ba wapenzi wa muziki wa injili ndani ya uwanja wa kambarage jioni ya leo.


  0 0

   Tingatinga la Mamraka ya ustawishaji makao makuu [CDA] likibomoa moja ya nyumba zilizopo katika hifadhi ya Barabara inayotarajiwa kuanza kujengwa havi karibuni, ambapo zaidi ya nyumba 65 zilibomolewa katika eneo hilo la mlamwa kusini.

   Wanawake wa mtaa wa Mlimwa wakimsaidia Mwenzao aliyezirai baada ya Tingatinga la CDA kufika kwa ajili ya kubomoa nyumba yake kwa ajili ya kupisha ujenzi wa Barabara, zoezi hilo lilifanyika Jana ambapo nyumba zaidi ya 65 zilibomolewa na kuacha familia zaidi ya 150 zikikosa makazi.
   Mwenyekiti wa mtaa huo Zubeda Haji akielekeza jambo wakati wa ubomoaji huo.
   Wananchi wa Mlimwa waking'oa mabati muda mfupi kabla ya Tinga tinga la CDA kufika na kuibomoa nyumba hiyo ili kupisha hifadhi ya Barabara
    Bibi huyu mkazi wa Mlimwa Kusini ambaye hakufahamika jina lake akiwa hajui la kufanya baada ya nyumba yake aliyokuwa akiishi iliyojengwa kwa mtindo wa Tembe huku akiachwa na vyombo vyake alivyoweka kwenye shamba la mahindi baada ya CDA kufanya uvunjaji huo kwa nyumba zote zilizopo katika hifadhi ya Barabara.
  Wananchi wa Mlimwa kusini wakiwa katika hekaheka ya kuhamisha mizigo yao na kukimbia nyumba zao baada ya kupata taarifa za ujio wa Tinga tinga la CDA kwa ajili ya kubomoa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa barabara.PICHA NA JOHN BANDA WA PAMOJA BLOG

  0 0

  Ofisa Mkuu wa Idara ya Sheria na Udhibiti, wa Vodacom Tanzania, Akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Mawasiliano wa Vodacom wakati walipofanya kongamano na Mkurugenzi wa Benki ya NBC Mizinga Melu, ikiwa ni sehemu ya kubadilisha uzoefu na kujengeana uwezo. Kongamano hilo lilifanyika katika makao makuu ya kampuni Mlimani City jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu, akisikiliza swali kutoka kwa mfanyakazi wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, …… wakati wa kongamano la kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo, lililofanyika katika Makao makuu ya Kampuni hiyo. Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuthamini mchango wa Mwanamke wa Kitanzania ndani ya jamii.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu, akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, wakati wa kongamano la kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo, lililofanyika katika Makao makuu ya Kampuni hiyo. Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuthamini mchango wa Mwanamke wa Kitanzania ndani ya jamii.
  Mfanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Anni Ngondo, akichangia mada wakati wa kongamano la kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo, lililofanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuthamini mchango wa Mwanamke wa Kitanzania ndani ya jamii.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu, akiwa katika picha ya Pamoja na baadhi ya wafanyakazi wanawake wa kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania mara baada ya kumalizika kwa kongamano la kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo, lililofanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuthamini mchango wa Mwanamke wa Kitanzania ndani ya jamii.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu, akizungumza na Mfanyakazi wa Kampuni ya Mawasiliano ya Vodacom Tanzania, Menbib Jemadari mara baada ya ya Vodacom Tanzania baada ya kumalizika kwa kongamano la kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo, lililofanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuthamini mchango wa Mwanamke wa Kitanzania ndani ya jamii.
  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Mizinga Melu, akifurahia jambo na Mkuu wa Idara ya Huduma kwa Wateja wa Vodacom Tanzania,, Menbib Jemadari mara baada ya ya Vodacom Tanzania baada ya kumalizika kwa kongamano la kubadilishana uzoefu na kujengeana uwezo, lililofanyika katika makao makuu ya Kampuni hiyo Mlimani City jijini Dar es Salaam. Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa jamii ya Watanzania kuendelea kuthamini mchango wa Mwanamke wa Kitanzania ndani ya jamii.

older | 1 | .... | 437 | 438 | (Page 439) | 440 | 441 | .... | 3286 | newer