Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

NCHI ZIMILIKI MAGEUZI YA SEKTA ZA USALAMA - TANZANIA

$
0
0
Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza katika Chemba ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa siku moja wa Baraza hilo uliofanyika juzi ( jumatatu) mkutano huo ulihusu mageuzi ya sekta za usalama, ambapo kwa mara ya kwanza Baraza Kuu la Usalama lilipitisha Azimio linalojitegemea kuhusu mageuzi katika sekta za usalama. Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi 42 zilizochangia majadiliano hayo yaliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ambapo hoja iliyozungumzwa na wengi ni umuhimu wa nchi kumiliki mchakato wa mageuzi ya sekta za usalama. Nyuma ya Balozi, ni Lt. Kanali Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi katika Uwakilishi wa Kudumu.

NEW SONG : STEVE RNB - SHE DANCE

Misokoto ya bangi 2,676 yakamatwa Manyara; watuhumiwa waendelea kupeta mtaani!

$
0
0
 JESHI la Polisi hapa nchini, limeshindwa kuwafikisha mahakamani watuhumiwa wa madawa ya kulevya katika mkoa wa Manyara, ambapo kwa sasa Polisi wamekamata misokoto ya bangi 2,676 na mirungi bunda 70 katika mkoa huo, huku likishindwa kakabiliana na hali hiyo kutokana na Askari wake kushiriki vitendo hivyo katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Bangi1
Aidha kumbukumbu zinaonyesha kuwa katika kipindi cha Machi, mwaka 2012, Jeshi hilo mkoani Kilimanjaro lilimshikilia Askari wake (G 842, Konstebo Deogratius), ambaye alikamatwa na misokoto mine ya bangi akiwa katika ukumbi wa disko wa Albeto uliopo mjijni Moshi, huku akifanya vurugu katika ukumbi huo ambapo pamoja na Jeshi la Polisi mkoani humo kuthibitisha tukio hilo, mtuhumiwa huyo akisukwa rumande pamoja na Askari mwingine ambaye aliingia katika ukumbi huo akiwa na bunduki aina ya SMG na kufanyia watu fujo.

Mbali na matukio hayo Jeshi hilo, lilitoa taarifa ya kukamata kwa watuhumiwa 45 wakihusishwa na matukio ya utumiaji wa bangi, mirungi na gongo katika msako wa kuimarisha doria katika maeneo mbalimbali mkoani humo, msako ambao hadi leo Polisi mkoani humo wameshindwa kuwafikisha makahamani watuhumiwa wakidai bado uchunguzi haujakamilika Globu ya Jamii imebaini.

Upigaji Kura Kili Music Awards Mwisho Leo

TAARIFA YA MABADILIKO YA ANUANI YA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA

$
0
0
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma inapenda kuwafahamisha wadau wake kuwa anuani yake imebadilika hivyo kuanzia sasa mawasiliano yafanyike kwa kutumia anuani ifuatayo;

OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA
UTUMISHI HOUSE
8 BARABARA YA KIVUKONI
11404 DAR ES SALAAM
au
PRESIDENT’S OFFICE, PUBLIC SERVICE MANAGEMENT
UTUMISHI HOUSE
8 KIVUKONI ROAD
11404 DAR ES SALAAM

Anuani hii inachukua nafasi ya Sanduku la Posta 2483, Dar es salaam. Hivyo, mawasiliano yote yazingatie anuani mpya. 

Limetolewa na
Katibu Mkuu
Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma
Barua pepe; permsec@utumishi.go.tz

Airtel yatoa msaada wa vifaa vya ofisi kwa shule ya Msingi Chau Chalinze

$
0
0
Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani William Mrocky akikabithi kwa mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau Bwana Elvin Msangi msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu wa shule ya msingi ya chau iliyoko Chalinze Mkoani Pwani.

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel kwa kupitia shughuli zake za huduma kwa jamii imetoa msaada vifaa kwa ajili ya ofisi ya  walimu kwa shule ya msingi ya Chau iliyoko Chalinze mkoani Pwani.

Akiongea kwa niaba ya Airtel Afisa mauzo wa kanda ya Pwani  William Mrocky alisema” leo tunayofuraha kutoa msaada wa viti na meza kwaajili ya ofisi ya walimu shuleni hapa, msaada huu unalenga katika kuboresha mazingira ya ofisi  na kuwawezesha walimu kufanya kazi zao kwa ufanisi zaidi.

Huu ni mwendelezo wetu wa huduma kwa jamii hususani katika sekta ya elimu ambapo kupitia mradi wetu wa “shule yetu” tumeziwezesha shule mbalimbali za sekondari kupata vitabu vya ada na kiada na kukabili changamoto za uhaba wa vitabu mashuleni. Sambamba na vitabu pia tunatoa msaada wa madawati na vifaa vya ofisi kama tunavyofanya leo katika shule hii ya msingi Chau
”Tunaamini msaada huu utaleta tija na kuboresha utendaji wa kazi kwa walimu shuleni hapa” aliongeza Mrocky.

Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Chau bwana Elvin Msangi alisema” nashukuru sana Airtel kwa kutufikia shuleni hapa, hii ni mara yakwanza kupokea msada kama huu shuleni hapa hivyo tunajisikia faraja kuona kampuni kama ya Airtel inafanya kazi kubwa katika kusaidia sekta ya elimu. Tunayo mahitaji mengi hapa shuleni, Tunategemea huu ni mwanzo hivyo mtatumkumbuka katika program zetu itakayokuja  siku za usoni.

Msaada huu utawawezesha walimu kuwa na ofisi nzuri na kuwaboreshea mazingira yao ya kazi kuwa bora zaidi.
Airtel kupitia mradi wake wa shule yetu unaziwezesha shule mbalimbali nchini kufaidia na vitabu, zaidi ya shule 900 nchini zimefaidika na mradi huu mpaka sasa.

JK ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI SINGIDA

BASI LA SUMRY LAUA WATU 19 WAKATI WAKISITIRI MWILI WA MTU ALIYEGONWA NA GARI SINGIDA.

$
0
0

WATU 19 wakiwemo askari Polisi wanne wamepota maisha katika ajali ya barabarani, wakati basi linalomilikiwa na Kampuni ya Sumry, lilipopamia watu hao wakati wakimsitiri mtembea kwa miguu, aliyekufa kwa kugongwa na gari lisilofahamika. Ajali hiyo ilitokea usiku wa kuamkia jana katika Kijiji cha Utaho, kilometa 20 nje ya Mji wa Singida katika Barabara Kuu ya Singida Dodoma. 



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Singida, Kamishina Msaidizi Mwandamizi, Geofrey Kamwela, alisema jana kuwa mbali na askari hao, wengine waliokufa papo hapo ni viongozi watatu wa kijiji hicho na wananchi wanaowaongoza na wengine wanne ambao hawajatambulika. 
Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, askari waliokufa katika ajali hiyo ni Koplo Boniface Magubika, PC Jumanne Mwakihaba, PC Novatus Tarimo na PC Michael Mwakihaba na wote wanatoka katika kituo kimoja cha kazi. 
Viongozi wa Kitongoji na Kijiji cha Utaho waliokufa ni Ramadhan Mjengi, ambaye ni Ofisa Mtendaji wa Kijiji, Paul Hamis, ambaye ni Mwenyekiti wa Kijiji na Ernest Salanga ambaye ni Mwenyekiti Kitongoji. 


Wananchi wanaowaongoza katika kijiji hicho waliokufa ni Saidi Rajabu, Ushirika Itambu, Chima Mughenyi, Salim Juma, Abeid Ramadhan, Mwinyi Hamis na Issaha Hussein. 
Kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, miili ya watu wengine wanne haikuwa rahisi kutambulika mara moja na wote wamehifadhiwa katika Hospitali ya Mkoa mjini Singida. 

Kamanda Kamwela alisema ajali hiyo ilisababishwa na basi la abiria lenye usajili namba T.799 BET aina ya Nissan, mali ya Kampuni hiyo ya Sumry, inayomilikiwa na Mohamed Abdallah wa Sumbawanga, lililokuwa likienda jijini Dar es Salaam likitokea Kigoma. 

Alisema kuwa basi hilo lililokuwa likiendeshwa na Paul Njilo, mkazi wa Dar es Salaam, liliwagonga waenda kwa miguu hao waliokuwa wamekusanyika kando ya barabara wakisaidiana na askari Polisi kuondoa mwili wa marehemu Gerald Zephania, aliyekuwa amegongwa na lori lisilofahamika juzi saa moja usiku. 

Katika ajali hiyo kwa mujibu wa Kamanda Kamwela, watu wengine wanane walijeruhiwa na wamelazwa katika Hospitali ya Misheni Puma ya mjini Singida. 

Habari kutoka eneo la tukio zinasema kilichosababisha ajali hiyo huenda ni kuegeshwa vibaya kwa gari la Polisi, wakati likipakia mwili wa marehemu Gerald, aliyekuwa amegongwa na lori mapema kabla ya basi hilo kufika hapo. 

Akizungumzia ajali hiyo katika Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam jana, Kamishna Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Paul Chagonja, alitoa pole kwa wananchi wote waliofiwa na ndugu zao na kuwaombea majeruhi kupona haraka. 

Alisema Askari wa Usalama Barabarani hawatakuwa na muhali na dereva yeyote atakayekwenda kinyume na Sheria ya Usalama Barabarani. Kutokana na hilo, ametoa mwito kwa madereva kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za usalama barabarni, ili kuepusha ajali zinazoweza kuzuilika. 

“Polisi iko imara kuchukua hatua zozote za kisheria, kwani kuna baadhi ya watoa huduma wa usafiri hugoma pale wanapotaka kuchukuliwa hatua kwa sababu mbalimbali matokeo yake ni uvunjaji wa sheria kwa makusudi,” alisema. 

Alisema Jeshi la Polisi limeanzisha msako mkali wa dereva wa basi hilo ambaye alitoroka ili kufikishwa mahakamani, na kuwaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu wa aina yeyote ile, ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani. 

Chanzo:HabariLeo

MABWENI YA WASICHANA YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA VITANDA

$
0
0
 Mwalimu mkuu shule ya sekondari Mwembetogwa Kelvin Mlengule akitoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita kuhusiana na mabweni ya wasichana wa shule hiyo.
 Baadhi ya wahitimu wa shule ya sekondari Mwembetogwa
 Mwalimu mkuu shule ya sekondari Mwembetogwa Kelvin Mlengule akitoa taarifa ya shule kwa wazazi na wanafunzi wa shule ya sekondari Mwembetogwa katika mahafali ya 18 ya shule hiyo.
Mkuu wa wilaya ya Kilolo Gerald Guninita akichangisha fedha kwa wazazi kwa ajili ya ununuzi wa vitanda vya mabweni ya wasichana wa shule ya sekondari Mwembetogwa. (picha zote na Denis Mlowe)

Na Denis Mlowe,Iringa

SHULE ya Sekondari ya Mwembetogwa iliyoko katika halmashauri ya Manispaa Iringa inakabiliwa na upungufu mkubwa wa vitanda 160 kwa wanafunzi wa kike wanaotakiwa kuishi katika mabweni yaliyokamilika katika shule hiyo.

Akizungumza katika mahafali ya 18 ya kidato cha sita na harambee ya kuchangia ununuzi wa vitanda iliyofanyika jana katika ukumbi wa shule hiyo Mkuu wa shule,Kelvin Mlengule alisema upungufu wa madawati umesababisha wanafunzi wa kike wanaotakiwa kuishi shuleni hapo kulazimika kupanga katika nyumba za watu binafsi na kuwasababisha wengi wao kujiunga katika makundi hatarishi na kupata ujauzito.

Mlengule alisema kwa sasa wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanapata vitanda kwa ajili ya mabweni ya wasichana ambayo tayari yamekwishamilika huku wakiendelea na mpango wa kujenga mabweni mengine ya wavulana wa kidato cha tano na sita shuleni hapo.

Alisema harambee iliyofanyika katika mahafali hayo wamepata mchango wa zaidi ya shilingi milioni 10 zikiwemo ahadi kutoka kwa wadau mbalimbali kati ya shilingi milioni 15 zinazohitajika kukamilisha upungufu wa vitanda na milango katika mabweni hayo.

Kwa upande wake mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa Dk Christene Ishengoma (Mb), Mkuu wa wilaya ya Kilolo,Gerald Guninita amewataka wanafunzi wanaotarajia kufanya mitihani ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita nchini kutumia muda uliobaki kwa ajili ya maandalizi ya mtihani wa kumaliza masomo yao kikamilifu.

“Vijana wangu ni vyema mkatumia muda huu mchache ulibaki kwa ajili ya kujiandaa zaidi katika kukabiliana na mtihani wenu mnaotarajia kuanza kuufanya Mei 5nkwa  kuweza kufanya vizuri na kuepuka tabia hatarishi ambazo zinaweza kuwakosesha maisha mazuri hapo mbeleni “ alisema Guninita

Guninita alisema maadili waliyofundishwa shuleni hapo ni vema wakayatumie vizuri kwa kuwa mabalozi katika jamii wanayoishi na kuepuka vishawishi na tama za kutaka vizuri kuliko uwezo wao na kuwataka kudumisha suala la nidhamu na kukataa kutumiwa na wanasiasa hususani katika suala hili linalo endelea sasa la mchakato wa kupata katiba mpya.
 
Aidha Guninita ameongeza kuwa wapo wanasiasa watako fanya mikutano na maandamano kwa kuwashirikisha vijana na kuwapatia pesa ili kuleta vurugu kitendo ambacho kinaweza kuhatarisha amani na maisha yao,hivyo wahakikishe kuwa hawajihusishi kwa namna yeyote katika vitendo hivyo.
 
Pia amewataka wazazi kushiriki kikamilifu katika kutoa michango mbalimbali ya maendeleo katika elimu,na kuacha kuchangia michango mingine isiyo na tija katika jamii zikiwemo harusi na vipaimara.
 
Katika mahafari hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa Guninita aliahidi kutoa vitanda 40 vyenye thamani ya shilingi milioni 4.8 ikiwemo ahadi yake ya shilingi laki mbili na elfu arobaini kwa ajili kununulia vitanda viwili.

Shule ya Sekondari  ya Mwembetogwa ni shule inayomilikiwa na wazazi ilianzishwa mwaka 1984 wakati huo ikiwa na wanafunzi wa kidato cha kwanza hadi cha nne pekee na wahitimu waliokabidhiwa vyeti walikuwa 122 kati ya 150 walitarajiwa kuhitimu kidato cha sita.

Rais Kikwete ahudhuria Mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Arusha

$
0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Arusha(AICC) kwenye mkutano wa 12 wa Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika mjini Arusha.Rais Kenyatta ndiye mwenyekiti wa jumuiya hiyo ya wnanachama watano.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda wakijadiliana jambo kabla ya ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Afrika Masharariki uliofanyika mjini Arusha leo(picha na Freddy Maro).

TANZANIA YAWASILISHA STADI JUU YA JINSI YA KUDHIBITI IDADI YA WAFUNGWA MAGEREZANI LEO JIJINI DAR

$
0
0
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji wa Magereza, Deonice Chamulesile akisoma risala ya ufunguzi katika Kikao cha uwasilishaji wa Stadi juu ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani iliyofanywa na Asasi ya Kiraia ya IRaWS - T. Kikao hicho kimefanyika leo Aprili 30, 2014 katika Ukumbi wa Luther House, Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza, Nicas Banzi(wa pili kushoto) ni Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Onel Malisa(wa kwanza kushoto) ni Katibu Mtendaji wa Asasi ya IRaWS - T, Naibu Kamishna Mstaafu wa Magereza, John Nyoka.
Baadhi ya Watoa Mada mbalimbali wakifuatilia kwa makini uwasilishaji wa Stadi juu ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani(kushoto) ni Afisa Mtafiti Mwandamizi toka Tume ya Kurekebisha Sheria, Prof. Sufian Bukurula.
Mhadhiri toka Kitivo cha Sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bw. James Jesey(aliyesimama) akiwasilisha rasmi Stadi ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani.
Kamishna wa Huduma za Urekebishaji, Deonice Chamulesile(wa pili kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbalimbali waliohudhuria Kikao hicho cha uwasilishaji wa Stadi juu ya jinsi ya kudhibiti idadi ya Wafungwa Magerezani. Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Luther House, leo Aprili 30, 2014 Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kulia) ni Makamu Mwenyekiti wa Asasi ya IRaWS - TANZANIA, Kamishna Mkuu Mstaafu Magereza Nicas Banzi(wa pili kushoto) ni Mwenyekiti wa Asasi ya IRaWS - Tanzania, Kamishna Mkuu Mstaafu wa Magereza Onel Malisa(wa kwanza kushoto) ni Afisa Mwandamizi Mstaafu wa Magereza, Bi Regina Thomas(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).

SALAM ZA HERI YA "MEI MOSI" KUTOKA NGOMA AFRICA BAND

WAZIRI SAMIA SULUHU HASSAN ABAINISHA UMUHIMU WA ZIWA TANGANYIKA

$
0
0
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais  (Muungano),Mhe. Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia) akihutubia Mkutano wa Mawaziri na Wadau wa Ziwa Tanganyika. Mhe Waziri Samia amezishauri nchi Wanachama zilizo katika Bonde la Ziwa Tanganyika kuunganisha nguvu zao kulinda Ziwa Tanganyika kwa manufaa ya kiuchumi na kiusalama ya nchi hizo. Kikao cha Wadau wa Ziwa Tanganyika kimefanyika leo Bujumbura katika Hoteli ya Ziwa Tanganyika.

UPITIAJI RASIMU YA KATIBA YA CLUB YA SIMBA WAMALIZIKA

$
0
0
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw. Leornad Thadeo akitoa ufafanuzi kwa Wanahabari hawapo pichani kuhusu Rasimu ya Katiba ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Simba baada ya wanahabari kutaka kupata ufafanuzi juu ya hatma ya Katiba na uchaguzi wa Klabu hiyo.

Na: Genofeva Matemu

Serikali kupitia Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imemaliza kupitia Rasimu ya Katiba ya Club ya Simba kwa ajili ya kuidhinisha katiba hiyo na kuifanya Club ya Simba kuendelea na taratibu za uchaguzi mkuu.

 Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Michezo Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Leonard Thadeo alipokutana na waandishi wa habari kujibu hoja mbalimbali za waandishi leo jijini Dar es Salaam.

 Akijibu moja ya hoja iliyomtaka kufafanua Wizara imefikia wapi katika upatikanaji wa Katiba ya Club ya Simba Bw. Thadeo amesema kuwa upitiaji wa Katiba umemelizika na kuonekana kuwa na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha katiba hiyo.

 “Mchakato wa upitiaji wa Katiba ya Club ya Simba umemalizika jana lakini kumekuwepo na mapungufu machache yanayohitaji kurekebishwa ili Wizara iweze kuidhinisha Katiba hiyo” amesema Bw. Thadeo.

 Akifafanua zaidi Bw. Thadeo amesema kuwa mapungufu hayo yanalenga zaidi upande wa kisheria ambapo mtu anaweza kutafsiri neno vibaya hivyo kupata maana tofauti na Katiba ilivyokusudia hivyo kuitaka Club hiyo kufanya marekebisho hayo mapema na kurejesha Katiba hiyo Wizarani kwa ajili ya kuidhinishwa.

 Aidha Bw. Thadeo amewataka waandishi wa habari pamoja na wanachama wa Club ya Simba kuwa na subira ili waweze kupata Katiba itakayokidhi malengo ya Club yao kwani mchakato wa upitiaji wa Katiba ulihitaji umakini.

MKUTANO WA KATIBU MKUU WA FIFA

$
0
0
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), Jerome Valcke anawasili nchini kesho (Mei 1 mwaka huu) ambapo atafungua semina ya mawasiliano kwa nchi wanachama wa Baraza la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Valcke ambaye atafuatana na maofisa wengine saba wa FIFA baadaye kesho hiyo hiyo (Mei 1 mwaka huu) atakuwa na mkutano na waandishi wa habari. Mkutano huo utafanyika saa 4 kamili asubuhi kwenye hoteli ya Double Tree by Hilton iliyopo Oysterbay, Dar es Salaam.

BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA MAWASILIANO

SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

DIAMOND AWAAHIDI MAKUBWA WAKAZI WA MTWARA

$
0
0
Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania,Kelvin Twissa (kulia)akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani)kuhusiana na udhamini wa Tamasha la Heels & Ties litakalofanyika makonde beach Mtwara na kutumbwizwa na Msanii mahiri Diamond Platinum na Wema Sepetu. Mteja anaweza kununua tiketi yake kwa njia ya M-pesa kwa kutuma pesa kwenda 0754 980 769 na kupata punguzo la asilimia 20%. Pamoja nae katika picha ni Nassib Abdul Maarufu Kama Daimond Platinum.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Nassib Abdul, Diamond Platinum akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusiana na Tamasha la Heels & Ties litakalofanyika makonde beach Mtwara na kudhaminiwa na Vodacom Tanzania, Wateja wanaweza kununua tiketi yake kwa njia ya M-pesa kwa kutuma pesa kwenda namba 0754 980 769. na kupata punguzo la asilimia 20%. Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa

Nyota wa muziki wa Bongo flava nchini anayepasua anga ya Afrika, Rais wa wasafi kama wengi wanavyomuita, Diamond Platnum, Dangote ameahidi makubwa kwa mashabiki wake wote wa Mkoa wa Mtwara kuhusu show ya aina yake inayotarajiwa kufanyika katika umbi wa  Makonde Club mjini Mtwara siku ya ijumaa tarehe 2 mwezi huu.

 Msanii huyo aliyeafanikiwa kujizolea mamilioni ya mashabiki wa muziki wa Bongo flava atasindikizwa na kipenzi chake, Malkia wa Bongo Movie nchini, Wema Sepetu - 'Beautiful Onyinye' au Madame kama mashabiki wake wanavyopenda kumwita.

 Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, katika ofisi za Vodacom Tanzania, ambao ndio wadhamini wa tamasha hilo amesema Mashabiki wakae mkao wa kula burudani ya nguvu ya muziki kutoka kwa kipenzi chao ambaye hafikirii kukosea wala kuwaangusha mashabiki wake katika show zake zote anazozifanya.

"Mashabiki wote waliopo Mtwara watashuhudia nikiimba live nyimbo yangu  mpya ya My number One remix niliyomshirikisha Davido kutoka nchini Nigeria. Kwa kawaida huwa sipendi kuwaangusha mashabiki zangu hivyo basi nawaahidi makubwa sana katika tamasha hilo na ningependa kuwaona wengi wakihudhuria show hiyo kwani kutakuwepo na mengi ambayo hawakutarajia kuyaona" Alisema Diamond.

Msanii Diamond ambaye kwa sasa ndiyo mwenye mafanikio makubwa ya kimuziki nchini amekuwa ni kivutio kikubwa kwa mashabaiki wa ndani na nje ya nchi kila mahali anapoalikwa kufanya shoo na hivyo kujizolea sifa lukuki na hata kuchaguliwa kuwania tuzo mbali mbali za muziki barani Afrika.

 Kwa upande wao wadhamini wa tamasha hilo Mkuu wa kitengo cha masoko na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania, Kelvin Twissa amesema mtandao wao unajivunia kudhamini tamasha kubwa kama hili kwani hakuna kitu ambacho wanakijali kama wateja wao haijalishi wapo kona gani ya Tanzania.

 "Tunajivunia kuwa sehemu ya Wadhamini wa Tamasha hili kubwa, Vodacom siku zote tumekuwa tukitoa kipaumbele kwa wateja wetu, Kipindi cha Pasaka tulifanya Tamasha pale coco beach na sasa ni zamu ya watu wa Mtwara" alisema Twissa na kuongeza.

 "Tutawafikia wateja wetu popote pale walipo na kuwapa burudani Vodacom imekuwepo nchini kwa zaidi ya miaka kumi sasa na kwa kipindi chote hicho watanzania wameonyesha kutuunga mkono na kutufanya tuwe mtandao unaaongoza siku zote Hivyo hatuna budi kuwafanyia yale ambayo wanaweza wakafurahi ikiwemo kuwaletea burudani kama hii".

"Ili kuwarahisishia wateja wetu na wananchi kwa ujumla, mteja anaweza kununua tiketi yake kwa njia ya M-pesa kwa kutuma pesa kwenda 0754 980 769. Na atapatiwa ufafanuzi wa jinsi ya kupata tiketi yake. Wateja watakaotumia njia hii watapata punguzo la asilimia 20 (20%). Wateja wa Vodacom na Mashabiki wote kwa ujumla wasiache kuhudhuria shoo hiyo ambayo itakuwa na kishindo kikubwa na kwa aina yake". Alisema.

 Aidha, "Vodacom tunaahidi kuenedelea kuwaunga mkono wasanii wetu wa Kitanzania na kujivunia kilicho chetu, wote ni mashahidi kwa namna ambavyo tumekuwa msitari wa mbele kuwaunga mkono wasanii wetu na tutaendelea na jitihada hizo na kufikia viwango vya wasanii wengine wa kimataifa," Alihitimisha Twissa.

KESI YA VIPIMO VYA HIV FEKI DHIDI YA VIGOGO MSD

$
0
0
Na Sultani Kipingo

UPANDE wa Jamhuri katika kesi ya inayowakabili watu wanne watano wakiwemo maofisa wa Bohari Kuu ya Dawa (MSD) ya matumizi mabaya ya madaraka na kuingiza nchini vipimo feki vya kupimia virusi vya ukimwi na kuisababishia serikali hasara ya Sh.bilioni 3, umeomba mahakama kuhamia nyumbani kwa mshtakiwa wa kwanza Sylvester Matandiko kwa ajili ya kumsomea mashtaka yake.


Maombi hayo yaliwasilishwa jana na Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Hellen Riwa.



Swai alidai kuwa washtakiwa wengine wameshasomewa mashitaka bila Matandiko kuwepo mahakamani kwa madai kuwa ni mgonjwa kutokana na sababu hiyo, upande wa Jamhuri unaomba Mahakama kuhamia nyumbani kwa mshtakiwa huyo.



"Mheshimiwa hakimu, niliongea na mke wa mshtakiwa kwa njia ya simu na akanijibu kwamba hali yake siyo mbaya sana na kwamba tatizo kubwa hana uwezo wa kutembea umbali mrefu... ni rai yetu Jamhuri kuhamishia mahakama nyumbani kwa mshtakiwa ili aweze kusomewa mashitaka yanayomkabili" alidai Swai.



Hata hivyo, upande wa utetezi uliomba mahakama kama ikiamua kufanya hivyo iwe kwa tahadhali kutokana na hali ya mshitakiwa kuwa bado kuimarika kwa sababu anasumbuliwa na maradhi ya kiharusi.



Hakimu Riwa alisema kesi hiyo itatajwa tena Mei 30, mwaka huu.



Mbali na Matandiko ambaye ni Mkurugenzi wa Oparesheni Kanda ya Kaskazini wa MSD, wengine ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa MSD, ambaye pia ni Meneja wa Viwango, Sadiki Materu, Wasajili kutoka Bodi ya Maabara za Afya ni Zainabu Mfaume na Joseph Nchimbi.



Katika kesi ya msingi, washtakiwa wote kwa pamoja, wanakabiliwa na mashtaka saba, ya kutumia madaraka vibaya, na hivyo kuisababishia hasara Serikali ya dola za Marekani 2,093,500, kwa kuruhusu uingizaji wa vitendanishi feki vya HIV nchini, na kuingizwa Bohari Kuu ya Dawa.



Swai alidai kuwa katika shitaka la kwanza, washtakiwa wote, kati ya Januari 20 na Julai 20, 2012, walikula njama ya kutenda kosa la kutumia madaraka yao vibaya kinyume cha sheria ya kuzuia na kupambana na rushwa.



Alidai katika shitaka la pili dhidi ya Matandiko ambaye hakuwepo mahakamani hapo, kwamba Februari 3, 2012, katika ofisi za MSD iliyopo wilayani Temeke, Dar es Salaam, alitumia madaraka yake vibaya kwa kuruhusu Bodi ya Maabara za Afya kupitia barua yenye kumb. MSD/003/2011/2012/390 ya Februari 3, 2012 kutoa kibali kwa Kampuni ya SD Africa, kuingiza vitendanishi vya HIV SD Bioline ½ 3.0 feki vilivyotengenezwa na Standrd Diagnostics ya Korea vilivyozuiliwa na Serikali kuingizwa nchini.



Aidha, ilidaiwa kwamba kwa kufanya hivyo, Kampuni ya SD Africa ilipata faida ya dola za Marekani 2,093,500, sawa na zaidi ya Sh.bilioni 3.



Swai alidai katika shitaka la tatu kwamba mshtakiwa Zaynabu na Sadiki, Januari 17, mwaka 2012, katika ofisi za Bohari Kuu ya Dawa, walitumia madaraka yao vibaya kwa kumshauri Naibu Mkurugenzi wa itifaki, kukubali Kampuni ya SD Africa kuingiza vipimo hivyo feki na kujipatia kiasi hicho cha fedha na kuvisambaza MSD.



Shitaka la nne linamhusu mshtakiwa Sadiki, ambaye anadaiwa kwamba Februari 29, mwaka 2012, katika ofisi za Bohari Kuu ya Dawa, aliidhinisha ubora wa vipimo hivyo vilivyozuiwa na Serikali kuingia nchini, na hivyo kusababisha Kampuni ya SD Africa kujipatia fedha hizo.



Shtaka la tano linamkabili Nchimbi, anayedaiwa kwamba Februari 7, mwaka 2012, akiwa Bodi ya Maabara za Afya, alitumia madaraka vibaya kwa kupitisha hati ya malipo namba SD111225-20 ya Desemba 25, mwaka 2012 na SD120109-3 ya Januari 9, mwaka 2012 kwa ajili ya kuingiza vipimo hivyo feki.



Katika shitaka la sita ilidaiwa kuwa Zaynabu kupitia cheo chake alitumia madaraka yake vibaya kwa kutoa cheti cha kuingiza na kusafirisha bidhaa mbalimbali za afya za maabara namba 00010131, cha Februari 7, mwaka  2012, ili kuingiza vipimo hivyo feki.



Swai aliendelea kudai kuwa shitaka la saba  linawakabili washtakiwa wote, katika vipindi hivyo, waliisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 3 kwa kuingiza vipimo hivyo feki vilivyozuiliwa na Serikali ya Tanzania.

Waziri Chikawe, IGP, DCI wala kiapo cha kuwa wajumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza

$
0
0
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe.Mathias Chikawe akila kiapo cha kuwa Mwenyekiti wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Njengafibili Mwaikugile jijini Dar es Salaam jana .Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Msajili wa Mahakama kuu Bw.Benedict Mwingiwa
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu akila kiapo cha kuwa mjumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza  mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Njengafibili Mwaikugile jijini Dar es Salaam jana .Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Msajili wa Mahakama kuu Bw.Benedict Mwingiw
 Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Nchini DCI Issaya Mngulu akila kiapo cha kuwa mjumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza  mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Njengafibili Mwaikugile jijini Dar es Salaam jana .Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Msajili wa Mahakama kuu Bw.Benedict Mwingiwa
 Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdani Omar Makame  akila kiapo cha kuwa mjumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza  mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Njengafibili Mwaikugile jijini Dar es Salaam jana .Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Msajili wa Mahakama kuu Bw.Benedict Mwingiwa
Kamishna wa Utawala na Utumishi wa Jeshi la Polisi, Thobias Andengenye akila kiapo cha kuwa mjumbe wa Tume ya utumishi ya Jeshi la Polisi na Magereza  mbele ya Jaji wa Mahakama kuu Mhe. Njengafibili Mwaikugile jijini Dar es Salaam jana .Tume hiyo inashughulikia masuala ya kiutumishi kwa askari polisi na Magereza.Katikati ni Msajili wa Mahakama kuu Bw.Benedict Mwingiwa Picha zote na Frank Geofray-Jeshi la Polisi

SERIKALI YAOMBWA KUJENGA VIWANJA VYA VOLLEBALL

$
0
0
Timu ya mpira wa wavu Mbozi akiwa katika picha kabla ya kupambana na wenzao MUst Mbeya. (picha zote na denis mlowe).

Na Denis Mlowe, Iringa

Makamu Mwenyekiti wa Idara ya michezo ya Halmashauri ya Manispaa Iringa, Kalulu Nsumba ameiomba Serekali pamoja na wadau wa Michezo kusaidia upatikanaji wa vifaa vya mchezo na viwanja bora  ili waweze kuuendeleza mchezo wa Volleball.
 
Nsumba ameyasema hayo katika Bonanza la Mchezo huo lililoandaliwa na na Iringa Manispaa Sport Club lilofanyika kwa siku mbili katika viwanja vya Shule ya sekondari Lugalo na kuzilikisha timu nane za mikoa ya Iringa,Njombe na Mbeya.
 
Amesema mchezo wa volleyball umesaulika na lengo la kuandaa ni kukuza mchezo huo utambulike kama mpira wa miguu na kujenga ushirikiano miongoni mwa vijana wa Nyanda za juu Kusini.
 
 Ameongeza kuwa Nyanda za Juu Kusini kuna vipaji lukuki vya mchezo huo lakini kinachokosekana ni vifaa na viwanja vya mchezo huo na kuwataka wadau kujitokeza kudhamini na kusaida ujenzi wa viwaja bora na kuwataka vijana kujiunga na mchezo huo.
 
Nsumba amedai kuwa kama kutakuwa na ushirikiano wa kutosha na kuwezeshwa kikamilifu mchezo huo kama ilivyo kwa mpira wa miguu anaamini kuwa Iringa na mikoa ya jirani inaweza kuwa na timu zinazoweza kufanya vizuri katika mashindano ya kitaifa na kimataifa.
 
Alizitaja timu zilizoshiriki bonanza hilo kuwa ni Iringa Manispaa (IMC), Chuo Kikuu cha Iringa (Tumaini), Chuo Kikuu Kishirikishi cha Mkwawa, Must Mbeya, Mbozi Vollebal Club, Tukuyu Volleball Club, Njombe, Ruco na kuwashirikisha vijana zaidi ya 100.
 
Aliwashukuru makampuni ya MT.Huwel, Assas, Meneja wa NBC mkoa wa Iringa na Mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa Iringa na shule ya sekondari Lugalo kwa msaada waliotoa kufanikisha bonanza hilo linalotarajiwa kufanyika kila mwaka kwa mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe.

MWENDELEZO WA TAMASHA LA PASAKA;MWANAMUZIKI REBECCA MALOPE KUTUMBUIZA MEI 4 JIJINI MWANZA

$
0
0
MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope anatarajiwa kutua kwenye jiji la Mwanza a.k.a ROCKY CITY  Mei 4,ikiwa ni sehemu ya muendelezo wa Tamasha la Pasaka 2014

Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama amesema kuwa Nyota huyo wa muziki wa nyimbo za Kiroho,ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha hilo,ameeleza kuwa msanii huyo alipata kura nyingi kutoka kwa mashabiki waliompendekeza kutumbuiza jijini humo.


“Tunashukuru kwamba baada ya mapendekezo ya mashabiki tuliwasiliana na Rebecca ambaye ameonesha uungwana wa hali ya juu na kutukubalia ombi letu. 



“Lakini pamoja na kukubali ana ratiba ya maonesho sehemu nyingine huko kwao, hivyo ametuambia hatatumbuiza katika mikoa yote ambayo tamasha litafanyika mwaka huu, hivyo tutaangalia wapi tumpangie kulingana na ratiba yake. 


“Lakini niwahakikishie mashabiki wetu kwamba msanii huyo tutakuwa naye na sasa ni suala la Kamati ya Maandalizi kuona ratiba yake ilivyo na kisha nasi tumuweke kwenye ratiba yetu ili mashabiki wafurahi,” alisema Msama. 



Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006).
Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao tayari wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro, Rose Muhando na waimbaji wengine ambao inaelezwa watatajwa hapo baadae.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images