Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 431 | 432 | (Page 433) | 434 | 435 | .... | 3283 | newer

  0 0

  Mh Jenista Mhagama (Kushoto) akiongea na baadhi ya wabunge kutoka Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii na baadhi ya wafanyakazi wa VETA kutoka Makao Makuu na VETA Kanda ya Kusini wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA   Kwaajili ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii juu ya mradi wa Kuongeza sifa za kuajiliwa - EEVT iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki wa Kuu ya Tanzania, Jijini Dar Es Salaam. Katikati ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mh Magreth Sitta na Kulia ni Steven Ngonyani.
  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mh Magreth Sitta (Katikati) akiongea wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati hiyo iliyofanyika katika Ukumbi wa Benki kuu ya Tanzania leo Jijini Dar Es Salaam.
   Mkurugenzi Mkuu wa VETA Tanzania, Mh Mhandisi Zebadiah Moshi(kulia) akifungua semina iliyoandaliwa na VETA kwaajili ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Kijamii loe katika Ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
  Mkurugenzi wa Soko la Ajira, Mipango na Maendeleo Kutoka VETA, Bw Enock Kibendela akitoa mada juu ya mchango mkubwa unaotolewa na VETA Katika kukuza sekta ya ajira kwa vijana wanaopata mafunzo ya ufundi stadi wakati wa semina iliyoandaliwa na VETA kwa wabunge wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii leo katika ukumbi wa Benki Kuu ya Tanzania.
  Baadhi ya wabunge wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii pamoja na wafanyakazi wa VETA waliohudhuria semina iliyoandaliwa na VETA Kwaajili ya wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii juu ya mradi wa Kuongeza sifa za kuajiliwa - EEVT.

  0 0

  Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi wa pili kutoka kulia pamoja na Babu wa Kijiji cha Maisha Plus akiwasalimia akina mama Shujaa wa Chakula ambao wameingia Rasmi Kijiji cha Maisha Plus Jana usiku.
  Akina Mama Shujaa wa Chakula Wakiwa wanamuimbia wimbo maalum Profesa Anna Tibaijuka Waziri wa Nyumba Ardhi na  maendeleo ya Makazi mara baada ya kuwasili Kijijini hapo.
  Hawa ndio Mama Shujaa wa Chakula ambao jana usiku wameingia Rasmi katika Kijiji Cha Maisha Plus. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi limekutana Dar es Salaam chini ya Uenyekiti wa Eng. Alhaj Mussa Iyombe ambaye pia ni Katibu Mkuu wa wizara hiyo ambaye wakati wa ufunguzi wa Baraza hilo, Eng. Iyombe aliwajulisha wajumbe waliohudhuria kikao hicho kuwa, madhumuni makubwa ya kuwepo kwa mabaraza ya aina hii ni kushirikisha wafanyakazi katika utekelezaji wa shughuli za wizara ikiwa ni pamoja na kuwaweka wafanyakazi hao karibu na uongozi wao. 
   Baraza hilo ambalo linaundwa na wajumbe kutoka katika taasisi zote zinazosimamiwa na Wizara ya Ujenzi, ndilo pia chombo cha kutoa ushauri kwa uongozi na ufuatiliaji wake hasa kwa masuala yanayohusu maslahi ya wafanyakazi.
  Alisema kuwa Baraza hilo ndilo vile vile chombo kinachotoa fursa kwa viongozi kuwasilisha taarifa za utekelezaji kwa wafanyakazi wanaowaongoza. 
   “Hapa tutatathmini pia upandishwaji vyeo kwa wafanyakazi pamoja na taratibu za mafunzo” alisisitiza Eng. Iyombe na kuongeza kuwa katika kikao hicho ajenda kuu itakuwa ni kupokea na kujadili mipango na makisio ya bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha wa 2014/15. Hata hivyo.
  Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo aliwasilisha salamu za Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ambaye amelitaka Baraza hilo kujadili vile vile namna ya kuboresha mahusiano ya kati ya taasisi zinazosimamiwa na Wizara ya Ujenzi kwani kwa sasa mahusiano kati ya taasisi hizo si ya kuridhisha. 
  “Zipo huduma ambazo taasisi moja inaweza kupata kutoka taasisi nyingine iliyo chini ya wizara hii lakini inashangaza kuona huduma hizo zinatafutwa kutoka sehemu nyingine na tena kwa gharama kubwa” alihoji Waziri Magufuli. Aidha, Waziri Magufuli amewataka watendaji wote kuwa na utayari wa kutekeleza majukumu yao wakati wowote wanapohitajika. “
  Nyinyi watendaji mbali na utayari huo lakini pia ndio mnaotakiwa kusimamia mali za Serikali katika maeneo mnayoyasimamia” ilimalizia taarifa hiyo ya Waziri.
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Alhaj Mussa Iyombe (katikati) akiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Wizara ya Ujenzi,  Samuel Mticco (kushoto) pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Eng. Joseph Nyamhanga (kulia).
   Mkurugenzi wa Uatawala na Rasilimali watu Bi. Juliana Mwakitosi akichangia mada.
  Baadhi ya Wajumbe wakifuatilia mada
   Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Alhaj Mussa Iyombe (katikati waliokaa) akiwa na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka katika Idara na Vitengo vya Wizara ya Ujenzi
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Eng. Alhaj Mussa Iyombe (katikati waliokaa) akiwa na wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi kutoka katika Taasisi

  0 0  0 0

  Mkurugenzi wa kampuni ya Frontline Porter Novelli Bi. Irene Kiwia akimkaribisha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk.Seif Suleiman Rashid kwenye maonyesho ya siku ya malaria yaliyofanyika jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Suleiman Rashid alipotembelea banda la malaria safe lililokuwa linasimamiwa na wafanyakazi wa Johnhopkins University kwenye maonyesho ya siku ya malaria.
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Seif Suleiman Rashid alipotembelea banda la NMCP kwenye maonyesho ya siku ya malaria jijini mwishoni mwa wiki.
  Wafanyakazi wa Tanzania Breweries Limited (TBL) wakiwa kwenye banda lao kuhamasisha kupambana na ugonjwa wa malaria nchini.
  Wafanyakazi wa kampuni ya simu za mkononi Zantel wakiwa kwenye banda lao.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es salaam leo April 28-2014, kwa ajili ya kuhutubia wananchi kwenye maadhimisho ya siku ya usalama na Afya Duniani.
  Afisa mkuu mwandamizi wa mazingira katika mamlaka ya Bandari Thobias Sonda akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, juu ya utumiaji wa vifaa vya kupimia hewa, wakati alipotembelea Banda la maabara ya mkemia mkuu wa Serikali kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
  Mtaalam wa uchunguzi wa vyakula katika maabara ya mkemia mkuu wa Serikali Edith Wilbald akimpa maelezo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipotembelea Banda la maabara ya uchunguzi wa vyakula kwenye Maonesho ya maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.
  Mtaalam wa uchimbaji wa madini katika mgodi wa Noth Mara Gold Mine Paul Kagodi akimuonesha Makamu wa Rais vifaa vinavyotumika katika kazi ya uchimbaji wa madini wakati alipotembelea mabanda ya Maonesho kwenye maadhimisho ya siku ya Usalama na Afya Duniani yaliyoadhimishwa leo April 28-2014, Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam.


  0 0

  Benki ya NMB imezindua rasmi tawi lake jipya mjini Kigoma. Uzinduzi wa tawi hilo lililoko katika jengo la Bima barabara ya Lumumba katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ulifanyika mwishoni mwa wiki. Aidha, tawi hilo lililo mkabala na Soko Kuu la Kigoma, limelenga kutoa huduma kwa watu binafsi na wakazi wengi wa maeneo hayo hususan wafanya biashara ndogo ndogo.

  Akizungumza katika uzinduzi huo, Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw.Ramadhani Maneno alisema tawi hilo litasaidia kusogeza karibu huduma za kifedha kwa wakazi wa Kigoma kutokana na mkoa huo sasa kupata maendeleo ya kiuchumu na kijamii.“Binafsi naishukuru NMB kwa juhudi zake za kuboresha huduma zake kwa lengo la kukidhi matakwa ya wateja na kuwafikia katika maeneo mbalimbali chini”. alisema Maneno.

  Kwa upande wake, Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi, Bw. Abraham Augustine alisema “Tumekuwa tukifanya jitihada za kuhakikishia kwamba benki hii inatoa huduma bora kwa wateja wetu wengi. Katika juhudi hizi, tumekuwa tukipanua mtandao wa matawi kuhakikisha kwamba tupo katika maeneo jirani na wateja wetu”.

  Tawi hili la Kigoma litakua likitoa huduma zote kuanzia kuweka na kutoa fedha, mikopo, malipo kwa taasisi kubwa zikiwemo za serikali na nyinginezo.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani Maneno akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la NMB Kigoma .Hafla hii ya uzinduzi ilifanyika katika viwanja vya tawi la NMB Kigoma.Wakishuhudia ni Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Bw. Abraham Augustino (kushoto) pamoja na Meneja wa tawi la NMB Kigoma, Bw. Rogers Malang’u.
  Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani Maneno akipata maelezo kuhusu huduma za ‘NMB Fast Track’ kutoka na Meneja wa NMB Kanda ya Magharibi Bw. Abraham Augustino (kushoto) pamoja na Meneja wa tawi la NMB Kigoma, Bw. Rogers Malang’u.
  Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe, Bw. Charles Gichilu (kulia) akipata huduma kutoka benki ya NMB. Pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw. Ramadhani Maneno.
  Sehemu ya wageni waalikwa waliohudhuria uzinduzi huo.

  0 0

  Katika kilele cha kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Timu ya  Zanzibar Heroes kupokea Jezi kutoa kwa wadhaminini wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambazo jezi hizo zilitolewa na wageni rasmi waliohudhuria katika sherehe hizo akiwemo Mh. Mwigulu Nchemba  ambae ni Mbunge na naibu waziri wa fedha na Uchumi Tanzania bara na upande wa Zanzibar pamoja na Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame mwakilishi na waziri wa nchi ofisi ya rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar. 
  Naibu Mwakilishi Balozi wa kudumu wa Tanzania Umoja wa mataifa New York, Ramadhani Muombwa Mwinyi (kulia) akiwa pamoja na Viwe Juma, ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya BENKI ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambao ni wadhamin wa timu hiyo wakimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein Siku ya Jumamosi April 26, ndani ya Ubalozi wa Tanzania jiji Washington DC nchini Marekani, ili kujianda kupambana na timu ya Kilimanjaro Stars kwa mchezo wa kuwania Kombe la Muungano. 
  Viongozi: Wageni rasmi wa sherehe za Muungano  Mhe: Mwigulu Nchemba (wapili kulia) akifuatiwa na Balozi Mulamula, pamoja na Balozi wa Waziri wa Nchi Zanzibar, Ofisi ya Rais na MBM Dr. Mwinyihaji Makame, (wakwanza kulia) Viwe Juma,wapili kulia  ambae ni Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) wakimkabidhi jezi nahodha wa timu ya Zanzibar Heroes Abuu Qullatein katika Sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kwenye ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC.
  Wasimamizi wa timu ya Zanzibar Heroes Seif Ameir na Dedie Rouba wakionyesha jezi walizodhaminiwa na (PBZ) Benki ya Watu wa Zanzibar.
  Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe  Juma akipata picha ya pamoja na Miss Tanzania USA
  Mkurugenzi wa Masoko na Maendeleo ya Biashara ya Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) Viwe  Juma akipata picha ya pamoja na wanamitindo wa Mitindo Night.
  Mwenyekiti wa Zanzibar Diaspora Asociation Bwana Omari Ali akipata picha ya pamoja na mgeni ndani ya Ubalozi wa Tanzania uliopo Jijini Washington DC Nchini Marekani
    
  Miss Tanzania USA  akipata picha ya 
  pamoja na  wanamitindo wa Mitindo Night

  Kawaida Katika kilele cha kusherehekea Miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Timu ya Zanzibar Heroes kupokea Jezi kutoa kwa wadhaminini wa Benki ya Watu wa Zanzibar (PBZ) ambazo jezi hizo zilitolewa na wageni rasmi waliohudhuria katika sherehe hizo akiwemo Mh. Mwigulu Nchemba ambae ni Mbunge na naibu waziri wa fedha na Uchumi Tanzania bara na upande wa Zanzibar pamoja na Mhe. Dr. Mwinyihaji Makame mwakilishi na waziri wa nchi ofisi ya rais ambaye pia ni Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar.

  0 0

  After collecting the PFA Players' Player of the Year honour on Sunday evening, Liverpool forward Luis Suarez revealed his depth of gratitude to his teammates, family and the club's supporters.
  A phenomenal season in which the Uruguayan has registered 30 goals in 31 appearances in the Barclays Premier League was rewarded with the individual accolade at a ceremony in London.
  The Reds' No.7 saw off competition from colleagues Steven Gerrard and Daniel Sturridge, plus Eden Hazard, Adam Lallana and Yaya Toure, to scoop an award he was runner-up for 12 months ago.
  To mark the achievement, Suarez posted a special video on his personal YouTube channel, highlighting the important support he has received at Anfield and at home along the way. 
  "We've just arrived from the Player of the Year awards," beamed the 27-year-old with the trophy clutched in his hands.
  "I'm very happy with this award - thanks to all of the players who voted for me.
  "Congratulations to all of my teammates too; I couldn't have won this award without them.
  "Special thanks to Sofia, my wife, who is here to enjoy it with me, and to my two children, who I love with all my soul.
  "And thanks to all of the supporters who have helped me too.

  0 0

  Na Adam Kinguti
  Ubalozi wa Tanzania nchini Msumbiji ukishirikiana na baadha ya Wawekezaji kutoka Tanzania, Bakhresa, Magodoro Dodoma, Macktech, Kampuni ya usafiri -Maning Nice pamoja na Jumuiya za Watanzania Msumbiji  na Swaziland walifanikisha sherehe za miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwishoni mwa juma jijini Maputo.
   Wageni waalikwa kutoka balozi mbalimbali nchini Msumbiji  walihudhuria sherehe hizo za miaka 50 ya Muungano  katika ubalozi wa Tanzania jijini Maputo
  Nguli wa Taarab Bi Shakila  (wa tatu kushoto) 
  akiwa na kundi la J.K.T. wanaimba wimbo wa Viva FRELIMO.
  Mhe. Balozi Shamim Nyanduga akitoa hotuba 
  kwenye Sherehe za Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania.Nyuma yake ni 
  Mgeni Rasmi Nhe.Carmelita Rita Namashulua, Waziri a Nchi, Utawala wa
   Mozambique akitoa hotuba yake na mumewe Bw. Nyanduga.

  Mgeni Rasmi Nhe.Carmelita Rita Namashulua, 
  Waziri wa Nchi, Utawala wa Mozambique akitoa hotuba yake.

  Mhe. Balozi Shamim Nyanduga akisaidiana kukata keki na Waziri wa Nchi, Utawala wa 
  Msumbiji Mhe. Carmelita Rita Namashulua aliyekuwa mgeni rasmi. Wengine ni Kanal Lwimbo, Mshauri wa Jeshi,  Bw. Frank Mwega, Mchumi na Ofisa Utawala wa Ubaloz, na mume wa balozi Bw. Nyanduga
  Mhe. Balozi Shamim Nyanduga akiingia kwenye ukumbi wa Kaya Kwanga pamoja na mgeni rasmi Mhe. Carmelita Rita Namashulua, mumewe Bw. Nyanduga (kati) pamoja na maafisa wa ubalozi.
  Toka kulia ni Kanal Lwimbo, Mshauri wa Jeshi, Mhe. Balozi Shamim Nyanduga na Bw. Frank Mwega, Mchumi na Ofisa Utawala wa Ubaloz
  Mhe. Balozi Shamim Nyanduga akipiga 
  makofi baada ya kukabidhi zawadi kwenye kituo cha kulea watoto yatima
  Mhe. Balozi Shamim Nyanduga akimkaribisha Mhe. Carmelita Rita Namshulua, Waziri wa Nchi, Utawala 

  0 0

   Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Samuel Sitta akiangalia vitabu katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kushuhudia uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba hiyo.
   Naibu Waziri Wizara ya Fedha Mhe. Adam Malima akiangalia vitabu katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kushuhudia uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba hiyo.
    Mawaziri kutoka Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wanaoshughulikia masuala ya Jumuiya wakiwa wakipitia machapisho mbalimbali katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kabla ya kushuhudia uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba hiyo.
   Waziri Sitta akioneshwa mkataba wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki iliyovunjika mwaka 1977.
  Waziri Sitta akiongea na vyombo vya habari mara baada ya uzinduzi wa kituo cha taarifa katika maktaba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

  0 0

  Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia Mhe Naimi Aziz na Mwambata Jeshi Brig. Gen. Bishoge wakiwa wamesimama  kwa heshima wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa na kwaya ya Kamisheni ya Umoja wa Afrika jijini Addis Ababa.  Aliyesimama kwenye podium ni Bw. Samwel Shelukindo, Afisa Mambo ya Nje Mkuu ambaye alikuwa MC katika sherehe hizo.
    Mhe. Balozi Naimi Aziz akitoa hotuba katika sherehe hizo.
   Mhe. Balozi Naimi Aziz akikata keki ya Miaka 50 na wageni waalikwa. Kutoka kushoto ni Balozi wa Equatorial Guinea, Balozi wa Uganda, Balozi wa DRC, Balozi wa Gambia,  Balozi wa Brazil, Balozi wa Mauritania na Balozi wa Misri.
   Baadhi ya Wageni waalikwa waliohudhuria sherehe hiyo.
   Siku ya sherehe ya Muungano, Ubalozi uliamua pia kutoa somo la historia ya muungano kwa watoto wa Tanzania waishio nchini Ethiopia. Pichani Bw. Nsavike Ndatta, Afisa Mambo Nje Mkuu wa Ubalozi akitoa somo hilo maalum kwa watoto hao

  0 0

  Wimbo huu maalumu wa Muungano umeimbwa na wasanii 50, kutoka katika mahadhi tofauti tofauti ya muziki kama Bongo Flava, Taarab, Dansi, Hiphop na muziki wa injili. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu, wasanii 50 tofauti kuimba wimbo kwa pamoja, na kwa ushirikiano mkubwa, wasanii hawa wanatukumbusha umuhimu wa Muungano ambao ndio utanzania wetu. Wasanii waliohusika Amini Kadjanito Mwasiti Linah Christina Shusho Khadija Kopa Frola Mbasha Ommy Dimpoz Diamond Josse Mara Kalala Jr Ali Kiba Peter Msechu Mrisho Mpoto Abdul Kiba Mzee Yusuph Angel Mwana Fa Nikki Wa pili G Nako God Zilla Madee Asley Shaa Mandojo Domokaya Shilole

  0 0

  Vikao vya Kamati za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (sio la Katiba) vimepangwa kuanza leo na vitaendelea hadi Mei 5, 2014 katika kumbi mbalimbali jijini Dar es salaam, kwa mujibu wa ofisi za Bunge. Kuona ratiba ya kila kamati na mahali watakofanyia vikao 

  0 0

  Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo katika Ikulu ya Dar es Salaam amekabidhi vitabu 2,181 kwa Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kwa ajili ya vyuo vya Jeshi ili kuongeza taaluma. 
   Rais amekabidhi vitabu hivyo kwa Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na kuahidi kuendelea kutafuta vitabu zaidi kwa ajili ya kuboresha Maktaba ya Jeshi iliyopo katika Chuo Cha Kijeshi kilichopo Monduli, Mkoani Arusha. 
   Maktaba hiyo ilianzishwa na Mheshimiwa Rais wakati alipokuwa mkufunzi katika chuo hicho miaka iliyopita. 
   "Lazima mtenge bajeti kwa ajili ya vitabu lakini na mimi nitaendelea kutafuta vitabu niwaletee ili kuijengea uwezo Library yetu ya Monduli”. 
   Akipokea vitabu hivyo kwa niaba ya Jeshi, Jenerali Davis Mwamunyange amemshukuru Rais kwa juhudi zake za kuboresha Jeshi la Wananchi Tanzania kwa ujumla na kulifanya kuwa la kisasa zaidi. 
   “Juhudi zako za kuliendeleza Jeshi letu imetuongezea uwezo na kujiamini zaidi. Bila juhudi zako tusingefika hapa tulipo na tunajivunia sana mafanikio haya” amesema Jenerali Mwamunyange .
  -Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikabidhi vitabu 2069  kwa uongozi  wa Jeshi(JWTZ) kwa matumizi katika maktaba mablimbali za jeshi nchini.Wapili kushoto ni Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange na Watatu kushoto ni Mnadhimu Mkuu Jeshini Luteni Jenerali Samuel Ndomba.

  -Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi na makamanda waandamizi wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania wakati wa hafla ya kukabidhi vitabu 2069 kwa ajili ya matumizi katika maktaba za jeshi.Vitabu hivyo ni mchango binafsi wa Rais Katika kuboresha mafunzo ya kisasa jeshini(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Katika mazingira ya yasiyoelweka, natangaza KUPOTEA kwa vyeti vya kuzaliwa vyenye majina ya Marianne Mwiki na Even Mwiki.


  *ACSE from Lutheran Junior Seminary mwaka 2001

                    *CSE from Mpwapwa Secondary School mwaka 1997

  Mara ya mwisho vilitumwa Arusha Tanzania 2005.

  Mwenye taarifa ya mtu yeyote kujiita Marianne Mwiki katika nafasi yeyote ya kazi, shule ama chuo  sehemu yeyote, tafadhali tujulishe haraka iwezekanavyo, zawadi kubwa itatolewa kwa Mwenye taarifa yeyote itakayoweza kusaidia kupatikana kwa vyeti hivyo.


  Tupigie simu kwenye number: +447939736412 ama +255756160237

  Email: mwikigm@yahoo.com

  Police ref:MPWE/RB/920/2013
  0 0

  Na Ripota wa Globu ya Jamii.

  OFISI ya mkurugenzi wa Mashtaka Nchini imemfutia mashtaka ya mauaji,mmoja  kati ya watuhumiwa nane wa mauaji ya kukusudia dhidi ya
  mfanyabiashara wa madini ya Tanzanite bilionea , Erasto Msuya (43).

  Hati ambayo imetumika kumwachia huru Joseph Damas (Chusa) ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu wa madini hayo  imetolewa na kusainiwa na
  mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) Elieza Feleshi na kisha Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuiwasilisha kwa Hakimu anayesikiliza kesi hiyo, Munga Sabuni .

  Hati hiyo ambayo hufahamika kama “Nolle Prosecution “ilitolewa mbele ya mahakama hiyo April 16 mwaka huu kwa ajili ya kuingiza rasmi katika kumbukumbu za Mahakama.

   “Mheshimiwa hakimu, upelelezi wa kesi hii, umekamilika na ikikupendeza, upande wa mashitaka tunaomba tarehe nyingine kwa ajili ya kuwasomea washitakiwa maelezo ya mashahidi kabla ya kulipeleka jalada lenye mashitaka haya, Mahakama Kuu kwa ajili ya kuanza kusikilizwa kwa kesi ya mauaji ya kukusudia namba 06 ya mwaka 2013.”alieleza Julius Semali wakili wa serikali.

  “Tumepokea hati ya kuachiwa huru kwa mshitakiwa namba 07, Joseph Damas,”alisema Wakili  Semali.

  Baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo, Hakimu Munga aliahirisha kesi hiyo hadi Mei 06 mwaka huu na kuamuru washitakiwa saba, waliosalia katika kesi hiyo kurejea rumande hadi hapo, shauri hilo litakapotajwa
  tena mahakamani hapo ikiwa ni kwa ajili ya kusoma maelezo ya mashahidi.

  Bilionea Msuya aliuawa mwezi Agosti mwaka jana kwa kupigwa, majira ya saa 6:30 mchana kando ya barabara kuu ya Arusha-Moshi, eneo la Mijohoroni, Wilaya ya Hai, Karibu na Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) na kufa papo hapo.

  Washitakiwa wanaokabiliwa na kesi hiyo ya mauaji ya kukusudia ni Sharif Mohamed Athuman (31), Mchimbaji mdogo wa madini na mkazi wa Kimandolu mkoani Arusha, Shaibu Jumanne Saidi maarufu kama Mredii (38), mkazi wa Songambele Wilaya ya Simanjiro na Mussa Juma Mangu (30), mkazi wa Shangarai kwa Mrefu mkoani Arusha.

  Wengine ni Jalila Zuberi Said (28), mkazi wa Babati, Sadiki Mohammed Jabir a.k.a “Msudani” au “Mnubi”(32), mkazi wa Dar es salaam na Lang’ata Wilayani Hai, Karim Kihundwa (33), mkazi wa Kijiji cha
  Lawate, Wilaya ya Siha na Alli Musa Majeshi, mkazi wa Babati mkoa wa Manyara.


  0 0

  The Court’s quarter sessions started today, with the Taxation ruling of Alcon International Limited (Appellant) versus the Standard Chartered Bank Uganda and Others (Respondents). 

  In the Ruling, the Court taxed a bill of costs Total to $22,884 to be paid by the Respondents to the Appellant as it was awarded in the Judgement of the case as the costs incurred by the Appellant during the hearing process of the Appeal.  

  The Ruling was delivered by the Deputy Registrar East African Court Of Justice, Her Worship Ms. Geraldine Umugwaneza. 

  During this quarter a total of 25 matters will be handled of which 6 are in the Appellate Division and 19 in the First Instance Division. The Appellate Division will have 1 Taxation, 1 hearing, 2 scheduling conferences, and 2 Judgements and the First Instance Division will have 14 hearings, 4 scheduling conferences and 1 Judgement. All matters will be in open Court. 

  All the matters will come before the Honourable Judges of both the Appellate and First Instance Divisions.

  About the EACJ
  The East African Court of Justice (EACJ or ‘the Court’), is one of the organs of the East African Community established under Article 9 of the Treaty for the Establishment of the East African Community. Established in November 2001, the Court’s major responsibility is to ensure the adherence to law in the interpretation and application of and compliance with the EAC Treaty.

  Arusha is the temporary seat of the Court until the Summit determines its permanent seat. The High Courts of the Partner States serve as sub-registries.

  0 0

   Prof Japhet Killewo, a medical doctor and Epidemiologist from Muhimbili University, speaks to experts who convened in Dar es Salaam to share research findings and discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania. The third year dissemination workshop was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Tunajali.
   Assistant director, Reproductive and Child Division in the ministry of Health and Social Welfare, Dr Neema Rusibamayila specks during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro (year three) by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences and the Johns Hopkins University in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare and Junajali, whose target is to reduce maternal and infant mortality.
   Mainen Moshi, Director of research and publications at Muhimbili University of Health and Allied Sciences specks during a two days workshop on evaluation of the integrated maternal and newborn healthcare programme in Morogoro (year three) by the Muhimbili University of Health and Allied Sciences, the Johns Hopkins University and Tunajali in partnership with the Ministry of Health and Social Welfare, whose target is to reduce maternal and infant mortality.
  A section of experts who convened in Dar es Salaam for a two days seminar to share research findings and to discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania, shares a light moment as they follow the proceedings. The meeting was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Tunajali.
  Assistant director, Reproductive and Child Division in the ministry of Health and Social Welfare, Dr Neema Rusibamayila (seated center) in a group photo with experts who convened in Dar es Salaam for a two days seminar to share research findings and to discuss meaningful policies to address maternal and newborn health in Tanzania. The meeting was sponsored by the United States Agency for International Development (USAID) and organized by partners within the Ministry of Health and Social Welfare, Muhimbili University, Johns Hopkins University and Tunajali.
  ======  =====  ======
  Community Health Workers boosts maternal health services in Tanzania 


  Evidence is showing that Maternal and Newborn Child Health Community Health Workers (MNCH CHWs) in the country are playing key roles in bridging the gaping gaps of improving maternal services.  During a presentation yesterday at the evaluation of integrated maternal and newborn health care programme in Morogoro region, the Tunajali Technical Director, Mr Protas Ndayanga said that in the five regions they operate, between July last year and March this year, they helped track 20,000 HIV/AIDS patients.  "Of these that they tracked, there were 5,500 for three days didn't show up for their appointments and the community health worker tracked them down and recorded the results. The biggest challenge they face is when the patients don't provide the correct address," he explained.  Results from the third year of the Morogoro Evaluation Project indicate that 99 per cent of all CHWs are happy working and that 90 per cent felt their work to be valued by both the health facility workers and the community.  High levels of satisfaction was reported for the availability of job aids (90 per cent) and registers (91 per cent); level and quality of training received (90 per cent) and quality of their own work (88 per cent).  "Almost all (93 per cent) were unsatsified with the availability of transport used for care provision and for travel to the health facility and 80 per cent of CHWs were dissatisfied with financial incentives provided," the interim report read in part.  During the opening of the two day dissemination workshop of the report, the Ministry of Health and Social Welfare Director of Preventive Services, Dr Neema Rusibamayila said that the findings of the evaluation would allow key adjustments for optimal performance of the project and inform the policy.  Dr Rusibamayila said that the workshop was a follow up of two workshops held in January 2012 and March 2013 which also aimed at sharing findings from the first and second year of the activities implemented by the project.  "The reports of these dissemination workshops showed that, there was critical information provided which was used to adjust programme strategies. In addition, the workshops fostered closer collaboration among stakeholders," she said.  In her keynote speech, the USAID Country Representative, Dr Raz Stevenson said that in this evaluation, the project activities aimed at assess the role of CHWs and the CHW support systems in delivering an integrated package of interventions.  Dr Stevenson said the research aimed to both assess the functionality of the recurrent integrated CHW programme, as well as to generate information to feed into planning for a national scale-up of the facility and community based intervention package.

  0 0


older | 1 | .... | 431 | 432 | (Page 433) | 434 | 435 | .... | 3283 | newer