Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live

KIBONZO CHA LEO


WAZIRI WA NISHATI NA MADINI KUWA MGENI RASMI SIKU YA WANATAALUMA UJERUMANI

$
0
0
Waziri wa Nishati na Madini  Profesa Sospeter Muhongo atakuwa mgeni rasmi katika siku ya wanataaluma itakayofanyika Aprili 26, mwaka huu katika mji wa Berlin, Ujerumani ambapo atazungumzia fursa za uwekezaji Tanzania hususan katika sekta ya mafuta na gesi. 

Profesa Muhongo atatoa mada hiyo ya fursa za uwekezaji nchini ikiwa ni moja ya shughuli zilizopangwa kufanyika katika siku mbili za kongamano la uwekezaji litakalofanyika katika mji wa Berlin, nchini humo mnamo tarehe 25 na 26 Aprili mwaka huu.

Kongamano hilo la uwekezaji limeandaliwa na Ubalozi wa Tanzania  nchini Ujerumani ikiwa ni njia mojawapo ya kusheherekea  Jubilee ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo makampuni mbalimbali kutoka Tanzania yanatarajia kuonesha  shughuli zinazolenga katika kuonesha fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini.

Mada nyingine zitakazowasilishwa katika siku mbili za kongamano la Uwekezaji Ujerumani ni pamoja na mahusiano baina ya Ujerumani na Tanzania na hatma ya majengo ya kihistoria Tanzania.

Kongamano hilo la siku mbili litaenda sambamba na maonesho ambapo watendaji wa Wizara na Taasisi watapata fursa ya kuelezea fursa za uwekezaji zilizopo katika sekta sekta ya Nishati na Madini ikiwemo umeme, gesi asilia na mafuta, nishati jadidifu na kutoa maelezo kuhusu ramani zinazoonyesha madini yanayopatikana nchini.

Rais Kikwete afungua ofisi ya TRA KARATU

$
0
0
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, Mbumge wa Karatu mchungaji Israeli Nase(Watatu kushoto),Waziri wa Maji Profesa Jumanne Maghembe(Wapili kushoto),Mkuu wa Mkoa wa Arusha Magesa Mulongo(kushoto) na Mkurugenzi wa Utumishi na utawala wa TRA aliyemwakilisha Kamishna mkuua wa TRA Bwana Abubakari Kunenge(wapili kulia) na kulia ni mwakilishi wa ofisi ya TRA Mkoa Bi.Caroline Ntinku.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akifunu kitambaa katika jiwe la msingi kuashiria kufungua rasmi ofisi ya Mamlaka ya mapato Wilaya ya Karatu leo mjini Karatu.picha na Freddy Maro

VIINGILIO MECHI YA STARS NA BURUNDI VYATAJWA

KESI YA MRAMBA YAPIGWA KALENDA

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imepiga kalenda kesi ya kuisababishia serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7 kwa matumizi mabaya ya madaraka leo aprili 22, hadi hapo itakapotajwa tena kwa ajili ya kuangalia amri iliyotolewa Novemba 20, mwaka 2013 itakavyotekelezwa ya kutoa misamaha ya kodi, inayowakabili aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba na wenzake ya matumizi . 

 Mapema mwaka jana Jopo la mahakimu watatu linalosikiliza kesi hiyo, likiongozwa na Jaji John Utamwa, lizitaka pande zote mbili Jamhuri na utetezi katika kesi hiyo, kuwasilisha hoja za kisheria, baada ya kukataliwa kwa shahidi wa wa tatu wa utetezi, aliyekuwa Kamishna wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Felician Busigara. 

 Wengine katika jop hilo ni, Jaji Sam Rumanyika ambao walianza kusikiliza kesi hiyo kabla ya kupanda wadhifa na kuwa majaji na msajili Saul Kinemela. Busigara, alipokuwa akitoa ushahidi wa upande wa utetezi, alizua mvutano wa kisheria kuhusu ushahidi aliokuwa anatoa ulijikita kwenye utaalam badala ya kuhusika na kesi ya msingi na upande wa mashtaka uliwasilisha pingamizi la kumkataa shahidi huyo. 

 Kutokana na mvutano huo, jopo hilo liliamuru pande zote mbili kuwasilisha hoja zao za kisheria kuhusu ushahidi wa shahidi huyo. Mbali na Mramba washtakiwa wengine ni, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Gray Mgonja. 

 Akiahirisha kesi hiyo, Jaji Rumanyika alisema jopo halijakamilika na kwamba wajumbe wengine wana udhuru wa kikazi hadi leo itakapotajwa na kuangalia kuhusu amri iliyotolewa na mahakama hiyo itatekelezwa vipi. 

 Mramba na wenzake, wanakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya sh. bilioni 11.7 kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart.

TAARIFA YA MSIBA KILUVYA GOGONI NA KIBOSHO

$
0
0
Marehemu Mzee Aloyce Kirango
Familia ya Mzee Aloyce Kirango wa Gogoni, Kiluvya, Dar es salaam,  inasikitika kutangaza kifo cha Baba yao mpendwa kilichotokea tarehe 21 april 2014 asubuhi. Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwa marehemu  Gogoni  Kiluvya. Habari ziwafikie ndugu jamaa na marafiki wote wa familia.

SHEREHE ZA MUUNGANO KITUO CHA GENEVA, SWITZERLAND ZAFANA

$
0
0
Balozi wa Tanzania katika Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Geneva,  Mhe.  Modest Mero, akimkaribisha Balozi wa Jamhuri ya watu wa  China-Geneva, Liu Jieyi katika tafrija maalum ya maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa ILO hii leo na kuhudhuriwa na mabalozi wa nchi mbalimbali ikiwemo balozi huyo China UN mjini Geneva, Balozi wa Kenya, Balozi wa Afrika Kusini, Balozi wa Togo, Balozi wa Botswana, Balozi wa Cameroon, Balozi wa Rwanda, wawakilishi wa Mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa na Watanzania waishio Switzerland. Kushoto ni Mke wa balozi huyo Rose  Mero.
 Mke wa Balozi Mero, Rose  Mero akisalimiana na ujumbe wa Ubalozi wa Denmark. pamoja nao ni Balozi Modest Mero na Balozi wa Dernmark-UN.
 Balozi Mero alitoa hotuba ambayo ilielezea historia, maendeleo, na maendeleo ya mchakato wa Katiba mpya, Hotuba hiyo pia iliweza kubaiinisha wazi ni vipi Tanzania na Watanzania wameweza kumudu kurumu katika muungano huo kwa miaka 50 sasa.
Balozi Modest Mero akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Maofisa katika Ubalozi wa Tanzania UN mjini Geneva. 

WAZIRI WA ARDHI AFANYA MAZUNGUMZO NA KATIBU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE YA USHELISHELI

$
0
0
Wazirii wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na mgeni wake wa Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure(kulia) alipotebela Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Nchi wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ushelisheli, Barry Faure (Kulia) akizungumza na Wazirii wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Prof. Anna Tibaijuka (Kushoto) wakati alipotembelea Wizara hiyo jijini Dar es Salaam.Pembeni yao ni Maafisa kutoka Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi na Wizara ya Mambo ya Nje.

MHOLANZI AKABIDHIWA MIKOBA YA KUINOA TAIFA STARS

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limetangaza rasmi Mart Nooij kutoka Uholanzi kuwa kocha mkuu mpya wa timu ya Taifa (Taifa Stars).

Rais wa TFF, Jamal Malinzi amemtambulisha kocha huyo leo (Aprili 26 mwaka huu) kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Akiwa amefuatana na Makamu wake Wallace Karia, amesema anafurahi kumtangaza Nooij na ana matarajio kuwa Tanzania itanufaika na uzoefu wake mkubwa wa ukocha, hasa katika bara la Afrika.

“Nawaahidi Watanzania kuwa sitomuingilia kocha katika kazi yake. Kama mimi sitomuingilia kocha, basi hakuna mtu yeyote atakayemuingilia. Tumemwajiri yeye kwa vile ni mtaalamu, hivyo hakuna sababu ya kumuingilia,” amesema Rais Malinzi.

Naye Nooij ambaye amepewa mkataba wa miaka miwili amesema yeye ni mtu wa maneno mafupi, hawezi kuahidi kitu lakini ana matarajio ya kuifanya Taifa Stars ifanye vizuri katika mashindano mbalimbali.

Amesema kabla ya kukubalia kufundisha Taifa Stars alikuwa na klabu ya St. Georges ya Ethiopia, lakini vilevile amewahi kufundisha mpira wa miguu barani Afrika katika nchi za Burkina Faso, Mali na Msumbiji.

Wasifu wa Nooij umeambatanishwa hapo chini

SHEREHE ZA MIAKA 50 YA MUUNGANO ZAFANA UJERUMANI, PROFESA MUHONGO MGENI RASMI

$
0
0
 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb.) (kushoto) akiingia katika ukumbi wa Deustche Bank uliopo Berlin, Ujerumani kabla ya kuzindua rasmi sherehe za jubilee ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Kulia ni balozi wa Tanzania Ujerumani Mhe. Philip Marmo.

 Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo (Mb) akizungumza na  baadhi ya wajumbe waliohudhuria  sherehe hizo

 Kikundi cha ngoma za sanaa kutoka Jeshi la Wananchi Tanzania kikitumbuiza  kabla ya kuanza kwa sherehe hizo.

Mpiganaji maulid wa kitenge ndani ya old trafford

$
0
0
 Mtangazaji wa michezo wa Radio One na ITV Maulid Kitenge akiwa na wachezaji nyota wa zamani wa Manchester United Quintin Fortune (chini)  na Bryan Robinson (juu) kwenye uwanja wa Old Trafford muda mfupi kabla ya kuanza kwa mechi ya Manchester United na Norwich City

ANGER TAINER AIBUKA UPYA AACHIA SINGLE MATATA

wasanii 50 wakiimba "hello hello tanzania" katika sherehe za miaka 50 ya muungano

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Afro 70 Band  wanakupa "Week End"

Siku ya hakimiliki duniani: Msanii JB azungumzia hali ilivyo Tanzania

$
0
0
Wakati leo ni siku ya hakimiliki duniani, maudhui yakiangazia filamu na mustakhbali wake kwa wabunifu wa kazi hiyo na waigizaji, suala la hakimiliki bado linaonekana kuwa ni changamoto.
Hakimiliki bunifu inaelezwa kuwa ikieleweka na kutumiwa vyema ndiyo muarobaini wa sekta hiyo kunufaisha wabunifu wa kazi hiyo ya sanaa na waigizaji na hivyo kuwawezesha kuendelea kufanya kazi hiyo.
Je nchini Tanzania hakimiliki iko vipi? Joseph Msami wa Idhaa hii amezungumza na Jacob Steven al maarufa JB ambaye ni mmoja wa wasanii na watayarishaji mashuhuri wa filamu nchini humo. Kwanza anaanza kwa kueleza hali ya hakimiliki ilivyo.

(SAUTI MAHOJIANO)
KUSIKILIZA BOFYA HAPO CHINI:


TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 27.04.2014.

$
0
0
KATIKA TUKIO LA KWANZA:

 MTOTO ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA VANESA PATRICK NJOJO(03) MKAZI WA ISISI, WILAYANI MBARALI ALIUAWA KWA KUPIGWA NGUMI NA BABA YAKE MZAZI AITWAYE PATRICK  NJOJO(23) MKAZI WA ISISI.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 23:45USIKU HUKO KATIKA KIJIJI CHA ISISI, KATA NA TARAFA YA RUJEWA, WILAYA YA MBARALI, MKOA WA MBEYA. INADAIWA KUWA CHANZO CHA TUKIO HILI ULEVI WA POMBE ZA KIENYEJI WA BABA HUYO. MTUHUMIWA AMEKAMATWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA KATIKA HOSPITALI YA WILAYA MBARALI.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII KUEPUKA ULEVI KWANI NI HATARI KWA AFYA ZAO NA UNA MADHARA KATIKA JAMII. AIDHA ANATOA WITO KWA WAZAZI/WALEZI KUWAFUNDISHA WATOTO WAO KWA UTARATIBU MZURI ILI KUEPUKA MATATIZO.
  
KATIKA TUKIO LA PILI:

 MTOTO MWENYE UMRI WA MIAKA 4 – 5 ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA FESTO  MBIGA, MKAZI WA NSALAGA AMEFARIKI DUNIA PAPO HAPO BAADA YA KUGONGWA NA GARI LENYE NAMBA ZA USAJILI SM 9124 AINA YA FAW LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA RAMADHANI MWALYOYO (30) MKAZI WA ILOMBA JIJINI MBEYA.

TUKIO HILO LIMETOKEA MNAMO TAREHE 26.04.2014 MAJIRA YA SAA 14:45 MCHANA HUKO KATIKA KIJIJI CHA NSALAGA, KATA YA UYOLE, TARAFA YA IYUNGA, BARABARA KUU YA MBEYA/IRINGA, JIJI NA MKOA WA MBEYA. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA, MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA. MTUHUMIWA AMEKAMATWA.

KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO VYA MOTO KWA KUZINGATIA NA KUFUATA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOEPUKIKA.
  
                                                      Signed by:

                                      [AHMED Z. MSANGI – SACP]


KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.

VODACOM YAIPIGA JEKI SHULE YA BARAZANI MANYARA‏

$
0
0
Diwani wa Kata ya Maghay, wilayani Mbulu mkoani Manyara Bw.Nicodemus Michael (kulia) na Kaimu Meneja wa Vodacom Tanzania kanda ya Kaskazini, Michael Kabusi wakikata utepe kuashiria makabidhiano ya jengo la darasa la shule ya msingi Barazani iliyoko wilayani Mbulu mkoani Manyara, lililojengwa kwa msaada wa Vodacom Foundation.
Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Barazani iliyoko wilayani Mbulu mkoani Manyara wakishuhudia tukio la makabidhiano ya jengo la darasa lililojengwa kwa msaada naVodacom Foundation.
Wanafunzi wa shule ya msingi Barazani iliyoko wilayani Mbulu mkoani Manyara wakiimba kwaya wakati wa tukio la makabidhiano ya jengo la darasa lililojengwa kwa msaada na Vodacom Foundation.

WATANZANIA WAISHIO MJINI SHANGHAI WALIVYOSHEREHEKEA MAADHIMISHO YA MIAKA 50 YA MUUNGANO WA TANZANIA

$
0
0
Baadhi ya Watanzania waishio katika mji wa Shanghai nchini China wamesherehekea maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania kwa kukutana pamoja na kuzungumza mambo mbali mbali ya kimaendeleo. Licha ya sherehe hizo za Miaka 50 ya Muungano,pia ziliambatana na kuwaaga baadhi ya wahitimu kutoka vyuo mbalimbali wanaotarajia kumaliza mwaka huu.
Baadhi ya Watanzania waishio Shanghai wakipiga picha ya pamoja katika shamra shamra za Maadhimisho ya Miaka 50 Muungano wa Tanzania,yaliyofanyika jana.
Baadhi ya Watanzania wanaomaliza masomo yao mwaka huu wakipiga picha ya pamoja mbele ya keki ya Muungano.
Mmoja wa wahitimu Bi. Hellen Shayo akipokea cheti kutoka kwa Mwenyekiti wa Watanazania waishio Shanghai cha kuwa mwanachama hai kwa kipindi chote alichokuwa hapa.

Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar awasilisha agizo la Serikali yake kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

$
0
0
Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Bwana Xie Yunliang akiwasilisha agizo la Serikali yake kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi la kuridhia na kukubali kusaidia Ujenzi wa uwanja wa Michezo wa Mau Tse Tung uliopo Mtaa wa Mperani - Kikwajuni Mjini Zanzibar.
Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar Xie Yunliang akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake ndani ya Jewngo la Pius Msekwa Bungeni Mjini Dodoma. Pembeni yao upande wa kushoto ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibarf Mh. Mohamed Aboud Mohamed.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiishukuru Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China kupitia Balozi Wake Mdogo aliyepo Zanziobar Bw. Xie Yunliang kwa kukubali wazo la SMZ la kuiomba China kusaidia ujenzi wa Uwanja wa Michezo wa Mao Tse Tung Jina linalotokana na Muasisi wa Taifa hilo la China. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Serikali ya Jamuhuri ya Watu wa China imeridhia na kukubali kugharamia ujenzi wa Kiwanja cha michezo kilichopewa jina na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar la Mau Tse Tung kilichopo miperani Kikwajuni Mjini Zanzibar.

Kauli hiyo imetolewa na Balozi Mdogo wa Jamuhuri ya Watu wa China aliyepo Zanzibar Bw. Xie Yunliang wakati akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi hapo katika Ofisi yake iliyomo ndani ya Jengo la Msekwa  Bungeni Mjini Dodoma.

Balozi Xie Junliang alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba Timu ya wataalamu wa China inatarajiwa kukifanyia utafiti na uchunguzi kiwanja hicho baadaye mwaka huu sambamba na utiwaji saini Makubaliano ya ujenzi wa kiwanja hicho unaotarajiwa kufanyika mapema mwaka ujao.

Alisema ujenzi wa uwanja huo uliopewa heshima ya Jina la Kiongozi muasisi wa Taifa la China Marehemu Mao Tse Tung utajumuisha kiwanja cha mchezo wa soka pamoja na michezo mengine ya ndani mfano mchezo wa Table Tennis.

“ Tunatarajia ujeni wa kiwanja cha Mao utakapokamilika utakuwa na uwezo wa kuhudumia wanamichezo wa michezo tofauti ukiwemo ule unaopendwa zaidi wa soka “. Alisema Bwana Xie Junliang.

Balozi Mdogo wa China aliyepo Zanzibar alimueleza Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwamba uhusiano wa kidugu uliopo kati ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla pamoja na China unastahiki kuenziwa zaidi.
Alimuhakikishia Balozi Seif kwamba Jamuhuri ya Watu wa China itaendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika harakati zake za kujikwamua kiuchumi.

Alisema matengenezo makubwa ya ujenzi wa Hospitali ya Abdulla Mzee iliyopo Mkoani Kisiwani Pemba, ujenzi wa maegesho ya ndege katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar pamoja na matayarisho wa matengenezo ya chumba cha wagonjwa mahututi  { ICU } mwezi Juni mwaka huu katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja ni miongoni mwa uthibitisho wa uhusiano wa pande hizo mbili.

 Akitoa shukrani zake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameipongeza Jamuhuri ya Watu wa China kwa moyo wake wa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar na Tanzania kwa ujumla katika miradi ya Kiuchumi na Maendeleo.

Balozi Seif alisema mchango wa Serikali ya China kwa Zanzibar umesaidia kuiwawezesha asilimia kubwa ya Jamii Zanzibar kustawika Kijamii na hata kiuchumi kupitia miundo mbinu iliyowekwa na Serikali kwa msaada wa Nchi hiyo rafiki.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alitolea mfano msaada mkubwa uliotolewa na China katika ujenzi wa skuli za Wilaya za Sekondari katika Wilaya zote za Unguja na Pemba.

Alisema mradi huo mkubwa wa sekta ya Elimu umekuja kufuatia ongezeko kubwa la idadi wa wanafunzi wanaofanikiwa kujiunga na masomo ya Sekondari katika maeneo tofauti ya Zanzibar.

“ Kutokana na ongezeko kubwa la wanafunzi hasa eneo la Wilaya ya Magharibi katika Kisiwa cha Unguja tumelishuhudia hivi karibuni katika skuli ya Kijitoupele na Serikali kupitia Wizara ya Elimu tunaliangalia tatizo hilo kwa mtazamo wa kujenga skuli mpya katika Mtaa wa Pangawe “. Alisema Balozi Seif.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza China kupitia Balozi wake huyo kwa mchango wake mkubwa katika Nyanja ya Elimu mchango ambao tayari watoto wa Zanzibar wanaendelea kufaidika nao.

Othman Khamis Ame

Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

Zamoyoni mogella na Abeid Mziba watembelea kambi ya ARS

$
0
0
Shirikisho la mpira wa miguu nchi (TFF), imetakiwa kuhahakisha inawalea vijana waliopata nafasi ya kushiriki kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars ili waweze kulisadia taifa kwa hapo baadae.

Wachezaji wa zamani wa timu ya Taifa Abeid Musiba na Zamoyoni Mogella walitoa kauli hiyo kwenye uwanja wa Azam wa Complex jijini Dar es Salaam jana, alipokwenda kuwatembelea washiriki wa kliniki ambayo ina washiriki 72 kutoka nchi 12 Barani Afrika huku Tanzania ikiwakilishwa na washiriki 19.

‘Ninayo furaha kuona mwekezaji kama Airtel kwa kushirikiano na Klabu ya Manchester United ya Uingereza, zimejitokesa kusaidia maendeleo ya soka, hatuna budi kuhakikisha vipaji hivi vinaendelezwa pamoja na kukuzwa zaidi,’ alisema Mogella.

Mogella alisema kuwa hana uhakika serikali imeweza kutoa miundo mbinu inayowezesha michezo kufanyika, hivyo jukumu la kuhakikisha vipaji na elimu wanayoipata vijana hawa inabaki kwa TFF.

Kwa siku za karibuni serikali imekuwa ikitoa mazingira kwa wawekezaji kama hawa ili waweze kufanya kazi yao vizuri. Na kwa maana hiyo nayo watahamasika na kuwekeza zaidi kwenye sekta za michezo. Wakati sisi tunacheza mambo kama hayo hayakuwepo. Alisema Musiba.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa timu ya Yanga Africans alisema Tanzania na hata baadhi ya nchi za Afrika zilikuwa hazifanyi vizuri kwenye michuano ya kimataifa sio kwa sababu hazina vijana wenye vipaji vya soka, bali ni kutoka na ukosefu wa programu madhubuti za kuendeleza vijana ambao ndio muhimili wa maendeleo ya soka.
Wachezaji nyota wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars Zamoyoni Mogella na Abeid Mziba, wakisalimiana na washiriki wa kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars inayoendelea kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Mchezaji nyota wa zamani wa timu ya Taifa, Taifa Stars Zamoyoni Mogella, akiongea na washiriki wa kliniki ya soka ya kimataifa ya Airtel Rising Stars wakati walipowatembelea kwenye kliniki hiyo inayofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex.
Baadhi wa washiriki wa kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars wakifuatilia kwa umakini mafunzo ya darasani kwenye uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Viewing all 110133 articles
Browse latest View live




Latest Images