Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live

WEMA SEPETU ASHINDA TUZO YA IJUMAA SEXIEST GIRL, WEUSI, WANAUME FAMILY WAFUNIKA SHOO YA PASAKA DAR LIVE

$
0
0
Mrembo Wema Isaac Sepetu 'Beautiful Onyinye' akiwa na tuzo yake baada ya kuibuka Ijumaa Sexiest Girl 2013/14 ndani ya Dar Live usiku wa kuamkia leo.
Wema akiwashukuru mashabiki wake waliompigia kura na hatimaye kuibuka mshindi.
...Akiwapa tano mashabiki waliofurika Dar Live katika Sikukuu ya Pasaka. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

Article 24

Mazungumzo na Dr Patrick Nhigula kuhusu Bunge maalum la Katiba

$
0
0
Karibu katika mazungumzo na Dr Patrick Nhigula kuhusu mwenendo wa Bunge Maalum la Katiba na mwenendo mzima wa nchi ya Tanzania.
Huu ni mfululizo wa mazungumzo na watu mbalimbali kuhusu suala hili muhimu kwa mustakabali wa nchi ya Tanzania.
Karibu
Kwa maoni, tafadhali wasiliana nasi kwa barua pepe kwanzaproduction at gmail dot com

Rais Kikwete atuma salamu za rambirambi kwa Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,kufuatia vifo vya watu 11 katika ajali ya basi

$
0
0
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za rambirambi Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mheshimiwa Paschal Mabiti,kuomboleza vifo vya watu 11 ambao wamepoteza maisha yao katika ajali ya basi iliyotokea mkoani humo Jumatatu, Aprili 21, 2014.

Katika salamu hizo, Rais Kikwete amesema kuwa ni jambo la kusikitisha  kuwa ajali zabarabarani zinaendelea kuchukua maisha ya watu wasiokuwa na hatia.

“Nimepokea kwa huzuni nyingi taarifa ya ajali hiyo ambayo nimejulishwa kuwa imetokea katika Kijiji cha Itwimila katika Wilaya ya Busega katika Mkoa wako wa Simiyu wakati basi lililokuwa linasafiri kutoka Tarime, Mkoa wa Mara kwenda Mwanza kupitia Simiyu lilipoacha njia na kugonga nyumba kabla ya kupinduka.”

Amesema Rais Kikwete: “Nakutumia salamu zangu za rambirambi na najiunga nanyi katika kuomboleza msiba huu mkubwa katika nchi yetu. Aidha, kupitia kwako, natuma salamu za dhati ya moyo wangu kwa familia zote ambazo zimepoteza wapendwa wao katika ajali hiyo. Naungana nao katika kuomboleza wapendwa wao. Napenda wajue kuwa msiba wao ni msiba wangu. Pia, naungana nao katika kumwomba Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema aziweke peponi roho za marehemu.”

Rais Kikwete vile vile ametoa pole kwa wote ambao wameumia katika ajali hiyo, akiwaombea wapone haraka na kurejea kwenye shughuli zao za kujiletea maendeleo.

Imetolewa na;

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.
21 Aprili,2014

2ND ROUND SCHOLARSHIPS FOR TANZANIAN WOMEN

$
0
0
Background
Most of managers and leaders in Tanzania formal and informal business sectors are men. In order to address this gap, Evin School of Management is providing opportunities for Tanzanian women who are in junior office positions, such as Office Assistants, Receptionists, Store-keepers, and others, to study General Management at Certificate and Diploma level to enable them to take advantage of available internal promotions or job vacancies within and outside their organisations. In year 2013 Evin School of Management gave out scholarships to 20 women to study for a General Management Programme at Certificate and Diploma level. The General Management Course is an approved and validated programme by NACTE.
Eligibility
Applicants must meet the following eligibility criteria:
1. Must be employed for 3 or more years

2. For Diploma, applicants must hold A-Level qualifications. For Certificate programme, O-Level qualification is required.

3. Those without the aforementioned formal qualifications but are fluent in both written and spoken English will be considered.

Application Process
Interested applicants are invited to send their Letters of Expression of Interest for the Scholarship and CVs through info@evinschools.com so as to reach us before 25th April 2014.

Decision Criteria: First Come basis
Scholarship Value:
Evin School of Management will offer partial scholarship of 50% of tuition fees for the first twenty (20) successful applicants for each programme.

For Enquiries, Contact Evin School of Management through:

Admissions Office, Evin School of Management

327 Garden Rd, Mikoncheni, P.O. Box 34780, Dar Es Salaam

Washiriki wa kliniki ya Airtel Rising Stars kutoka nchini Sierra Leone wawasili nchini

$
0
0
Meneja Uhusiano Airtel Tanzania Jackson Mmbando akiongea kwenye Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius mara ya kupokea timu ya Airtel Rising Stars kutoka Sierra Leone ambao watahudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Mchezaji Fatmata Mansaray wa timu ya Airtel Rising Stars chini ya miaka 17 kutoka Sierra Leone, akiongea na waandishi wa habari baada ya kufika Dar es Salaam kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.
Wachezaji wa Airel Rising Stars kutoka Sierra Leone wakiwasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Julius Nyerere kuhudhuria kliniki ya soka ya kimataifa ya Manchester United itayoanza Jumatano, 23-27 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Wachezaji sita na kiongozi mmoja kutoka Sierra Leone waliwasili jijini Dar es Salaam jana asubuhi tayari kushiriki kliniki ya soka ya kimataifa ya siku tano itakayofanyika kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia kesho, Jumatano 23 Aprili, 2014. Washiriki kutoka Madagascar walitajiwa kutua jijini jana usiku.

Kwa mujibu wa kuwasili kwa wachezaji, wengi wao wanatarajia kufika leo mchana na baadaye usiku kuhudhuria mafunzo hayo yanayoshirikisha zaidi ya wachezaji 72 kutoka nchi za Kenya, Uganda, Malawi, Sierra Leone, Burkina Faso, Chad, Congo Brazzaville, DRC, Niger, Madagascar, Gabon, Seychelles na mwenyeji – Tanzania.

Wachezaji hao chipukizi, wasichana na wavulana, walijipatia tiketi ya kushiriki kliniki baada ya kufanya vizuri katika mashindano ya Airtel Rising Stars kwenye nchi zao pamoja na timu zilizotwaa uchampioni wa mashindano ya kimataifa yaliyofanyika nchini Nigeria mwaka jana.

Kliniki hii itaendeshwa na wakufunzi kutoka klabu maarufu duniani ya Manchester United ikiwa na lengo la kutoa mafunzo ya kuwawezesha wachezaji na kuwajengea uwezo wa kutandaza kabumbu ya kusisimua hasa katika idara ya ushambuliaji.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe atakuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi inayotarajiwa kuhudhuriwa na wageni mbalimbali kutoka wizara inayohusika na michezo, shirikisho la mpira wa miguu nchini, Airtel Tanzania na wadau wengine wa soka.

Hii ni fursa nyingine muhimu kwa wachezaji hao chipukizi chini ya umri wa miaka 17 kuonyesha vipaji vyao na kujiendeleza kisoka. 

Program ya Airtel Rising Stars ni mpango wa maendeleo ya soka kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 barani Afrika ukidhaminiwa na kampuni ya simu za kiganjaji ya Airtel na kuungwa mkono na Manchester United. Lengo lake ni kusaidia kuibua vipaji vya soka kutoka ngazi ya chini (grassroots) hadi Taifa.

Rais Kikwete akizungumzia kuhusu uchumi na mafuta alipokutana na Watanzania waishio nchini Uingereza

TAARIFA RASMI KWA UMMA YA KIFO CHA MKUU WA WILAYA YA KALAMBO MHE. MOSHI CHANG'A, KUZIKWA JUMATANO MKOANI IRINGA

$
0
0
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA WAZIRI MKUU

TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA


MKOA WA RUKWA

Anuani ya simu:”REGCOM”                          Simu Na:(025)-2802138/2802144

Fax Na. (025) 2802217



             OFISI YA MKUU WA MKOA,

     S.L.P. 128,

     SUMBAWANGA.




Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella M. Manyanya (Mb) kwa masikitiko makubwa anapenda kuwajulisha juu msiba mkubwa ulioukumba Mkoa wetu wa Rukwa wa kuondokewa na Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Mhe. Moshi Mussa Chang’a (62) aliyefariki jana jioni terehe 20 April, 2014 katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugonjwa wa Shinikizo la Damu na Kisukari.


Mwili wa Marehemu Mhe. Chang’a unategemewa kusafirishwa kesho jioni kutoka Jijini Dar es Saam hadi nyumbani kwao Mkoani Iringa ambapo mazishi yake yatafanyika keshokutwa siku ya Jumatano tarehe 23 April, 2014.


Marehemu Mhe. Chang’a alizaliwa Mkoani Iringa Januari Mwaka 1952 na amewahi kushika nafasi mbalimbali Serikalini na katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Katika nafasi ya Ukuu wa Wilaya amewahi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bukoba, Mbeya, Tabora, Mkalama na Kalambo Mkoani Rukwa ambapo mauti yake yamemfika.


Katika Ngazi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) amewahi kuwa Katibu wa CCM Wilaya ya Njombe na Iringa Vijijini na Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Iringa.


Marehemu Mhe. Chang’a ameacha watoto watano (5) na Mjukuu Mmoja (1).Watoto wa kiume 3 na Wakike 2.

Kwa niaba ya Wananchi wa Mkoa wa Rukwa tunatoa pole kwa ndugu, jamaa, marafiki, na wote walioguswa na msiba huu mkubwa. Tunawaombea kwa Mwenyezi Mungu awape nguvu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.


Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi.


Mungu ailaze roho ya Marehemu mahala pema peponi “AAAMIN”



Imetolewa na:


OFISI YA MKUU WA MKOA

RUKWA

Tarehe 21 April, 2014.

UJUMBE WA LEO

KUMBUKUMBU

$
0
0
Marehemu Mwl. Ernestina Kahabuka

Dakika, saa, siku, miezi na sasa miaka mitano toka ulipotuaga tarehe 15/04/2009 na kuzikwa nyumbani kijiji cha Buhangaruti, Mugana Parish Bukoba.

Unakumbukwa daima na mme wako Dr. F.C. Kahabuka, wanao – Anny, Oliva, Mary, Primus, Pelagia, na wakwe zako, wajukuu, zako wote, ndugu zako wote, majirani, ndugu na jamaa na wanafunzi wako wote tunazidi kukuombea upumzike mahali pema huko peponi

Amina

Tulikupenda sana mama lakini Mungu alikupenda zaidi

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 22.0 4.2014

The Avenue wiki hii

Chief Woodward delivers news to failed Man United boss in early morning Carrington meeting with Ryan Giggs to take charge until end of season

$
0
0
David Moyes has been sacked by Manchester United with immediate effect.
Chief executive Ed Woodward arrived at Carrington at 8am on Tuesday morning to inform the Scot face-to-face of the news.

Moyes had already been informed of his fate and thanked club staff at the training complex in anticipation of his departure. The players were not present at the time.

A tweet on the club's official Twitter account read: 'BREAKING: Manchester United announces that David Moyes has left the club. The club would like to place on record its thanks for the hard work, honesty and integrity he brought to the role.'

Ryan Giggs will take temporary charge for the rest of the season as interim manager.
It emerged on Monday that United's owners, the Glazer family, had lost patience with Moyes after a dismal season that has seen the reigning Barclays Premier League champions slump to seventh in the table.

The final straw was Sunday's 2-0 defeat at Everton, their 11th in the Barclays Premier League this season, and a result that left the title holders 13 points off the Champions League places.
Saying goodbye: United's owners, the Glazer family, lost patience with Moyes after a string of bad results
David Moyes has been sacked by Manchester United with immediate effect

TASWIRA KUTOKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akiwasili kwenye ukumbi wa Bunge kwa ajili kuendesha na kusimamia mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.leo mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akiongoza dua ya kuliombea Bunge na Taifa kabla ya kuanza mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.leo mjini Dodoma kabla ya kuanza kwa kikao cha asubuhi.
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Samuel Sitta akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Bunge hilo leo mjini Dodoma wakati wa mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakishiriki dua ya kuliombea Bunge hilo leo mjini Dodoma kabla ya kuanza mjadala kuhusu maboresho ya Sura ya Kwanza na Sita ya Rasimu ya Katiba mpya.

Mwenezi wa Chadema Wilaya ya Meatu arudi CCM pamoja na viongozi wengine wa Chadema

$
0
0
 Aliyekuwa Katibu Mwenezi wa Chadema wilaya ya Meatu Kimwaga Jackson Ndibo akirudisha vitu vya Chadema zikiwemo kadi, bendera na katiba kwa viongozi wa CCM baada ya kurudi rasmi.
 Mwenyekiti wa Vijana  mkoa wa Simiyu na MNEC wa Itilima Ndugu Njalu Silanga akikabdihi kadi ya CCM kwa  moja ya viongozi wa Chadema Meatu waliorudi CCM.
 Mwenyekiti wa Vijana  mkoa wa Simiyu na MNEC wa Itilima Ndugu Njalu Silanga akihutubia wakazi wa wilaya ya Meatu na kuwahakikishia wananchi hao CCM imejipanga kuendelea kuleta maendeleo ya nchini.
Mwenyekiti wa Vijana Mkoa wa Simiyu na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wilaya ya Itilima Ndugu Njalu Silanga (wa katikati) akiwa pamoja na viongozi wa Chama wilaya ya Meatu.

KIJIWE CHA UGHAIBUNI

Vyoo vipya 18 vya Skuli ya Kijitoupele Zanzibar vyafunguliwa rasmi

$
0
0
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akivizindua rasmi vyoo vya Skuli ya Kijitoupele A, B na Sekondari pamoja na Mifereji na Tangi la Maji vilivyojengwa na ufadhili ya Shirika la Umoja wa Mtaifa la Kuhudumia Watoto { UNECEF }.
Mifereji Maalum iliyozunguukwa na wanafunzi kwenye sherehe ya kuzinduliwa rasmi ambayo imejengwa kwa ajili ya kuhudumia wanafunzi wa Skuli ya Kijitoupele A,B na Sekondari.
Moja kati ya madarasa ya skuli ya msingi ya Kijitoupele yanaonekana kuwa na msongamano mkubwa wa wanafunzi wasiopunguwa idadi ya 240.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akibadilishana mawazo na Mwenyekiti wa Kamati ya Skuli ya Kijitoupele Nd. Manafi Said Mwinyi mara baada ya hafla ya kuzinduliwa kwa vyoo vya skuli hiyo.Kushoto ya Nd. Manafi ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mh. Ali Juma Shamhuna nanyuma yao ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi Mwanaid Saleh.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akimpongeza mwakilishi wa UNICEF hapa Zanzibar Bibi Francesca Morandini kwa uamuzi wa shirika lake kusaidia ufadhili wa ujenzi wa vyoo vya skuli ya Kijitoupele iliyopo Wilaya ya Magharibi. Nyuma ya Bibi Francesca ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Abdulla Mzee Abdulla. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

Michauno ya Heineken foosball yazidi kunoga

$
0
0
Mwakilishi wa kampuni ya Heineken Tanzania, Amon Theonest (kulia) akiteta na kapteni wa timu Boko stars Elifuraha Salimu pamoja na Rafael Masanga kuhusu ushindi wao mkubwa baada yakushinda michuano ya foosball pale Hisaje boko Dar es salaam. Washindi hao pia wameingia robo finali ya kuwania nafasi ya kwenda Ibiza Spain kuburudika na kutazama fainali za ligi ya mabigwa ulaya UEFA champions league.
Timu ya Boko Stars kushoto ikiongozwa na capteni Elifuraha Salimu pamoja na mwenzake Rafael Masanga wakichuana na timu ya Bongo stars (kulia)vilivyo pale Hisaje Park iliyopo Boko Dar es salaam. Timu ya Boko stars ilibuka kidedea kwa magoli 9 na imepata nafasi yakushiriki robo fainali za Michuano ya Heineken foosball itakayao fanyika Club 777 tarehe 26 Aprili.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ashuhudia makampuni ya simu yakiweka saini mkataba wa makabaliano ya usambazaji huduma za mawasiliano vijijini

$
0
0
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof. Makame Mbarawa (kushoto) akimsikiliza kwa makini Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Georgia Mutagahywa (kulia) muda mfupi kabla ya kuanza kwa hafla ya utiaji saini mikataba ya usambazaji huduma za mawasiliano ya simu za mkononi maeneo ya vijijini kati ya makampuni ya simu na Mfuko wa Wamasiliano kwa Wote - (UCSAF) jijini Dar es salaam. Katikati ni Mkurugenzi wa Mawasilano wa Airtel Beatrice Bandawe.
Mkuu wa Idara ya Sheria wa Vodacom Ngayama Matongo akimuongoza Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa kampuni hiyo Georgia Mutagahywa (aliyeketi) kutia saini mkataba wa makabaliano ya usambazaji huduma za mawasiliano vijijini kupitia ruzuku ya Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam. Wa pili kulia aliyesimama ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa akishuhudia. Vodacom kupitia mfuko huo itafikisha huduma kwenye kata 37 za pembezoni mwa miji na yenywe ikiahidi kufikisha huduma kwenye kata 36 za pembezoni kwa gharama zake ili kuwawezesha watanzania wasihia vijijini kuunganishwa kwenye mtandao wa huduma za simu za mkononi.
Kutoka kulia Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia Mutagahywa, Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) Peter Ulanga wakitia saini makubaliano yanayayawezesha makampuni ya simu kupokea ruzuku kwa ajili ya kufikisha huduma kwenye maeneo yaliyo pemebezoni na miji kadiri walivyoomba. Vodacom imeahidi kufikisha huduma hiyo kwenye kata 73 kati ya hizo 37 kupitia ruzuku YA UCSAF.
Ofisa Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Georgia Mutagahywa kulia akibadilishana nyaraka za mkataba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Kamugisha Kazaura zinazohusiha upokeaji wa ruzuku kwa ajili ya kufikisha huduma za mawasiliano vijijini inayotolewa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF).Wa kwanza kushoto ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko huo Peter Ulanga akisainia makubaliano hayo. Vodacom imeahidi kufikisha huduma kwenye kata 73 zilizopo vijijini kati ya hizo 37 kupitia ruzuku hiyo. Wa pili kulia waliosimama ni Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Prof Makame Mbarawa.

MTOTO AFUNGWA KAMBA KUZUIA ASITOROKE

$
0
0
Mtoto Samir mkazi wa mtaa wa Langoni kata ya Miembeni,akiwa amefungwa kamba katika mguu wake wa kushoto huku upande mwingine ukiwa umefungwa katika chuma kizito kilichopo jirani na mlango.

Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.

MTOTO Samir anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka minne hadi mitano mkazi wa mtaa wa Langoni katika manispaa ya Moshi,amejikuta katika wakati mgumu kutokana na tabia ya bibi yake kumfunga kamba katika mguu wake kwa lengo la kumzuia asiende kucheza mbali na nyumbani kwao.

Tukio hilo limetokea hivi karibuni katika eneo hilo ambapo bibi huyo ambaye jina lake halikufahamika mara moja alikutwa akiwa amemfunga kamba ya kudu mjukuu wake huyo katika mguu wa kushoto huku sehemu nyingine ikiwa imefungwa katika chuma kizito.

Kwa mujibu wa majirani walisema bibi huyo amekuwa akimfunga mtoto huyo mara kwa mara kwa zaidi ya nusu saa hasa nyakati ambazo bibi huyo amekuwa akifanya shughuli zake za usafi wa ndani pamoja na kufua.

Wakizungumza kwa sharti la kutotajwa majina,majirani hao wamesema imekuwa ni kawaida kwa bibi huyo ambaye anaishi na wajukuu zake kumfanyia kitendo hicho mtoto huyo huku akimzuia kucheza na wenzake wa nyumba za jirani.

“Sisi hiyo hali mbona tumeizoea mara kwa mara Samir akienda kucheza na wenzake huko mtaani,bibi yake akimkuta huko anamkamata na kisha kumfunga kwenye hilo chuma lililoko hapo mlangoni kwa zaidi hata ya nusu saa”alisema mmoja wa majirani.

Akizungumza tukio hilo Bibi huyo ambaye anakadiriwa kuwa na miaka zaidi ya 60 alikiri kumfunga mtotot huyo kwa madai kuwa amekuwa mtundu kupita kiasi na kwamba ametumia mbinu hiyo ili kumdhibiti asitoroke nyumbani.

“Hapa nyumbani naishi na wajukuu zangu ,wengine wako mashuleni na wengine wako kazini ambao ni wazazi wa huyu Samir,mmoja anafanya kazi Arusha,mwingine yuko hapo mjini(Moshi)sasa sina mtu wa kunisadia kumwangalia huyu mtoto”alisema Bibi huyo.

Alisema analazimika kumfunga kamba mtoto Samir kutokana na kuwa na tabia ya kwenda kuzurura katika nyumba za watu huku wakati mwingine huenda kucheza mbali na nyumbani jambo ambalo humpa shida kumpata kwa urahisi.

“Wakati mwingine nashikwa na hasira kumpiga siwezi hivyo naamua kumfunga kamba hapa mlangoni…watu wote si wazuri kumruhusu kuingia kila nyumba huko atafundishwa mambo mabaya ndio sababu nafanya hivi.”alisema Bibi huyo.

Mmoja wa wazazi walioshuhudia tukio hilo walisema wazazi wengi wamekuwa wakikosea kuwaacha watoto wao walelewe na bibi zao hali inayochangia kuwepo kwa vitendo vya ukiukaji wa hali ya watoto na kibinadamu kama ilivyotokea kwa mtoto huyo.

“Wazazi tumekuwa bize sana na shughuli za utafutaji ,hali hii inapelekea majukumu ya kulea watoto kuiacha kwa wasichana wa kazi na hata mama zetu kama ilivyo kwa familia hii ,sasa suala hili pia wakati mwingine linachangia makuzi mabovu kwa watoto”alisema Juma Nzota.
Viewing all 110088 articles
Browse latest View live




Latest Images