NAFASI ZA MAFUNZO YA UALIMU NGAZI YA STASHAHADA KWA MWAKA WA MASOMO 2014/2015
↧
↧
ankal ndani ya kijiwe cha ughaibuni
Ankal na Ze Fulanazzzz yake akiwa na wadau wakuu wa KIJIWE CHA UGHAIBUNI alipotembelea Maryland, Marekani hivi karibuni, na kutia ubani katika kipindi hicho ambacho kimejizolea umaarufu mkubwa duniani kote. Kulia kwake ni Producer DJ Luke Joe, akifuatiwa na nyota wa mchezo Ben Mwaipaja na Mwanangu Yasin 'Mtoto wa Salamander' bila kumsahau mwenyekiti wa kijiwe. Nyuma ya kochi ni wadau ambao bila wao kipindi hicho kisingekuwa hai. Hii ni baada ya kurekodi kipindi ambacho kitaruka hivi karibuni. Kaa mkao wa kula....
↧
ngoma azipendazo ankal
Slim ali na The Hodi Boys wakikupa "You can do it" ikiwa spesho request ya Balozi Cisco Mtiro
↧
CHEGE,YP WALIVYOPAGAWISHA WAKAZI WA JIJI LA DAR WALIOFURIKA KWA WINGI KWENYE FUKWE YA COCO BEACH
Msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya wa kundi la TMK Family Chege akiwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwenye Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka na kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika fukwe za bahari ya hindi coco beach.
Msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Msomi John a.k.a War killer akiwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam katika Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka na kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika fukwe za bahari ya hindi coco beach.
Msanii chipukizi wa muziki wa kizazi kipya Amir Jabir mkazi wa Namanga jijini Dar es Salaam akiwapagawisha wakazi wa jiji la Dar es Salaam kwenye Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka na kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika fukwe za bahari ya hindi.
Nyomi ya watu iliyofurika kwenye Tamasha la Cheka Bombastik lililoandaliwa na Vodacom Tanzania mahususi kwa ajili ya wateja wake katika msimu huu wa sikukuu ya pasaka na kufanyika kwa siku mbili mfululizo katika fukwe za bahari ya hindi jijini Dar es Salaam.
↧
SHIRIKISHO LA MCHEZO WA BAO TANZANIA LA LAANI VIKALI WANASIASA WANAO WAKASHFU WAASISI WA MUUNGANO
Na Sixmund J. Begashe wa Makumbusho ya Taifa.
Shirikisho la Mchezo wa Bao Tanzania limelaani vikali wanasiasa wanao simama na kutoa maneno ya kejeli zidi ya waasisi wa Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani kwani huko ni kutokuwa na maadili yenye sura alisi ya Utanzania.
Hayo yamesemwa na Raisi wa shirikisho hilo Bw Monday Likwepa kwenye Mashindano ya Mchezo maalum wa Bao wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya Muungano wa Tanzania Bara na Visiwani yanayo fanyika Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
‘’ Shirikisho kwa kupitia mchezo huu na wadau wake wote wamesikitishwa na kukerwa sana na tunalaani vikali vitendo vya baadhi ya Wajumbe wa Bunge maalum la Katiba na Wabunge wa Jamuuri ya Muungano kwa kutumia nafasi walizo pewa sasa wamegeuza na kuwatuhumu, zalilisha na kuwakashfu waasisi wa Muungano wetu Hayati Baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere na Mzee Abeid Amani Karume’’ Alisema Bw Likwepa.
Bw Likwepa aliongeza kuwa watanzania wakumbuke kuwa waasisi wa Muungano wetu walikuwa ni wanachama wa Mchezo wa Bao hivyo chama hakitokuwa tayari kuona walio kuwa wanachama wake ambao ndio wakombozi wa nchi hii wanadhalilishwa hivyo watafanya maandamano siku ya Tar 26 Aprili 2014 kuanzia Chang’ombe TCCT hadi uwanja wa Taifa mbele ya Rais wa Jamuhuri ya Muungano kwa lengo la kulaani vikali tabia hii mbaya.
Nae Mzee Jabiri Sultan Nyumba ambae alikuwa akiudhuria michezo ya Bao ya Mwl Nyerere huko kwa Mzee Shaban Kalolo Mtaa wa Jangwani amewashauri wanasiasa kuiga mfano wa waasisi wa Muungano wetu walivyo tumia muda wao mwingi kuliunganisha Taifa na si kulisambaratisha kama wanavyo taka kufanya wanasiasa wa chache hivi sasa.
‘’wanasiasa watumie Lugha nzuri zenye maelewano na kujenga kama tunavyo zitumia kwenye mchezo wa Bao, Lungha zetu uvunja itikadi za vyama, udini na Ukabila, si za ugomvi ni za kujenga, inashangaza sana kuona wanasiasa wanakosa busara, nivyema tukatatua matatizo yetu kwa busara’’ aliongeza Mzee Nyumba.
Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure amesema kuwa wataendelea kuuwenzi mchezo wa Bao kwa kuifadhili Shirikisho hili la Bao nchini kwa kulipatia mahali pa kufanyia shughuli zao, kwani wanatambua mchango wa Mchezo huu katika Ukombozi wa Taifa letu.
Michuano hii ya Mchezo wa Bao wa Maadhimisho ya miaka 50 ya Muungano wa Tanzania imeshirikisha Timu 13 za hapa jijini Dar es Salaam na itafungwa rasmi Tar 26 Aprili na Waziri wa Uchukuzi Mh Harrison Mwakwembe na Mshindi wa kwanza atajinyakulia Tsh 500,000/=, wapili Ths 300,0000/= na watatu Tsh 200,000/=.
Kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure (katikati) akimsikiliza kwa makini mmoja wa Makamisaa wa Mchezo wa Bao na kulia ni Mzee Jabiri Sulutan Nyumba.
kaimu Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Bw Achiles Bufure (katikati) akifuatilia kwa umakini mchuano mkali kati ya mchezaji wa Nyayo na Mzinga.
timu mbali mbali zikiumana vikali katika michuano ya Bao ya kuadhimisha miaka 50 ya Muungano wa Tanzania, inayo endelea katika ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
wachezazi wa Timu mbali mbali wakifuatilia matokeo ya awali ya mchezo huo wa Bao inayo endelea katika ukumbi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni Dar es Salaam.
↧
↧
TASWIRA YA MZEE WA FEVA AKIIPIGA CHABO BOBABODA ILIYOBEBA MSHIKAKI
↧
Wana Familia wa Kikundi cha ujirani mwema Ndachi, Dodoma walivyoisherehekea sikukuu ya Pasaka
Mtendaji Mkuu wa Photo Solutions Deusdedit Vallery Moshi (kushoto) na mkewe Silvia akifurahia jambo na familia yake,kutoka kulia Aika Deusdedit,Amani-Khan Deusdedit na Amini-Mchamungu Deusdedit wakati wakisheherekea Sikukuu ya Pasaka na kikundi cha Ujirani Mwema Ndachi Dodoma
Wana Familia wa Kikundi cha ujirani mwema Ndachi, Dodoma wakisheherekea Sikukuu ya pasaka Pamoja kuadhimisha zaidi ya miaka elfu mbili ya ufufuko wa Yesu Kristo.Kikundi hiki kinashirikiana katika shuhuli za kijamii.
Katibu wa kikundi Mwalimu Richard Msaky katikati akizungumza na wanakikundi pamoja na kutoa salamu za Pasaka.
↧
TAMASHA LA PASAKA LATIKISA UWANJA WA TAIFA, MEMBE ASEMA WANANCHI WATAAMUA SERIKALI IPI WANAITAKA
Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya nje na Ushirikiano wa kimataifa Mh. Bernard Membe aliyemuakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Tamasha la Pasaka lililofanyika jana kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama na katikati ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Angela Kairuki.
Akizungumza na mamia ya mashabiki waliojitokeza katika tamasha hilo Mhe Membe amewaomba Watanzania kuwa watulivu wakati huu wa mchakato wa katiba mpya
Amesema uamuzi wa ni serikali gani iwe moja, Tatu au Mbili Wananchi ndiyo waaamua na wao wabunge watakipitisha kile kitachoamliwa na wananchi.
Mwanamuiki wa muziki wa injili kutoka nchini Afrika Kusini Keke Letse Phoofolo akicheza na mashabiki wake wakati alipokuwa akifanya vitu vyake kwenye uwanja wa Taifa jana.
Mwimbaji wa muziki wa injili kutoka nchini Zambia Ephraim Sekereti akiimba jukwaani jana. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
↧
ziara ya wazee club ya arusha nchini Kenya
Baadhi ya wanachama wa wazee club arusha wakiwa na picha ya pamoja na watoto yatima jijini Nairobi nchini kenya walipowatembelea siku ya pasaka
Arusha Wazee Club wakiwa Nairobi kwa michezo ya pasaka na timu ya wazee ya Green Yard
Timu ya Arusha Wazee Club wakiwa Nairobi kwa michezo ya pasaka na timu ya wazee ya Green Yard. Picha kwa hisani ya Kipepeo Tours .
↧
↧
UTUMISHI YAANZA MASHINDANO YA MEI MOSI KWA KISHINDO
Timu ya mpira wa Pete ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma imeanza mashindano ya Mei Mosi 2014 kwa ushindi mnono kwa kuichapa timu ya Alliance One ya Morogoro magoli 46 kwa 7.
Mchezo huo ulifanyika katika Uwanja wa Jamhuri Siku ya Pasaka uliwachukua Utumishi takribani dakika 10 za mchezo kuwasoma wapinzani wao na kuanza kufunga ambapo hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Alliance One walishakubali magoli 23 dhidi ya 5.
Wachezaji waliofanikisha ushindi huo ni Fatuma Machenga (GS) kwa kushirikiana Mwadawa Twalibu (GA), ambao walifanikiwa kufunga magoli 34 na 12 katika goli la wapinzani wa Utumishi.
Mara baada ya mchezo huo nahodha wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Elizabeth Fusi alisema kuwa amefurahishwa na matokeo hayo na kuahidi kuendelea kuzitimulia vumbi timu pinzani katika michezo itakayofuata. “Tumepania kuwa mabingwa mwaka huu hivyo tutacheza kwa bidii ili kuhakikisha tunatimiza ndoto yetu” Fusi alisema.
Naye, Mwenyekiti wa timu ya Alliance One Bw. Charles J. Kung’aro alikiri kuwa timu yake ilizidiwa mbinu za kimchezo na Utumishi hivyo kuwaweka wachezaji wake katika wakati mgumu kimchezo hasa wanaposhambuliwa. “Tuliruhusu wautawale mchezo hivyo ikawa rahisi kwao kutufunga hivyo tumejipanga kurekebisha makosa yetu ili tufanye vizuri katika mechi zijazo” Bw. Kung’aro alisema.
Mashindano ya Mei Mosi 2014 kitaifa yanafanyika mjini Morogoro kwa kuhusisha michezo ya mpira wa miguu, netiboli, kuvuta kamba, riadha, mbio za baiskeli, karata, bao na drafti.
Mchezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Fatuma Machenga (GS) akigombea mpira hewani na mchezaji wa timu wa Alliance One (GK) katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayoendelea katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wachezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) na Alliance One wakiwa kwenye harakati za kugombea mpira katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi 2014 yanayofanyika katika Uwanja wa Jamhuri mjini mjini Morogoro.
Mchezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Fatuma Machenga (GS) akifunga goli dhidi ya timu ya Alliance One katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji wa timu ya Alliance One (GK) akitoa upinzani kwa Fatuma Machenga (GS) wa Ofisi ya Rais (Utumishi) katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Mchezaji wa timu ya Ofisi ya Rais (Utumishi) Mwadawa Twalibu (GA) akitoa pasi kwa Fatuma Machenga (GS) katika mechi ya mashindano ya Mei Mosi mwaka huu iliyofanyika jana Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
↧
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 21.04.2014.
↧
SALAMU ZA MWISHO WA MSIMU TOKA KWA WEKUNDU WA MSIMBAZI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UONGOZI wa Simba SC unapenda kuwashukuru wanachama na washabiki wake wote hapa nchini kutokana na mshikamano mkubwa waliounyesha wakati wa kuelekea kumalizika kwa Ligi Kuu ya Vodacom msimu huu.
Ingawa matokeo hayakuwa mazuri siku zote, lakini mapenzi ambayo washabiki walionyesha kwa klabu yao lilikuwa ni jambo la faraja kwa uongozi, benchi la ufundi pamoja na wachezaji.
Wachezaji wa Simba pia wameelezea kufurahishwa kwao na namna washabiki waliokwenda kwenye Uwanja wa Taifa kutazama pambano la Watani wa Jadi Jumamosi iliyopita, walivyowashangilia kwa dakika zote tisini.
Uongozi wa Simba unapenda kuwaahidi washabiki wake kwamba utafanya kila uwezalo kuhakikisha kwamba klabu inajiandaa vya kutosha kufanya vizuri msimu ujao.
Makosa ambayo yalisababisha timu isifanye vizuri msimu uliomazika yatatazamwa na kufanyiwa upembuzi yakinifu ili yasijirudie tena katika msimu unaokuja na mingine.
Simba SC inaamini kwamba wanachama wake watakuwa bega kwa bega na uongozi kuhakikisha kwamba mambo yanakwenda vizuri msimu ujao.
MAPATO
Msimu huu ulikuwa na changamoto kubwa sana za kimapato. Katika mechi baina ya Simba SC na Ashanti iliyochezwa jijini Dar es Salaam, mgawo kwa Simba SC ulikua ni zaidi kidogo ya shilingi laki tatu. Hii ni rekodi katika historia ya Simba.
Hili lilisababishwa zaidi na kutofanya vizuri kwa timu. Hata hivyo, uongozi ulijitahidi kwa kadri ilivyowezekana kupambana na changamoto hizi kwa kutumia vyanzo vyake vya ndani na ubunifu.
Pamoja na changamoto zote hizo, uongozi ulijitahidi kuisimamia timu na hata katika mechi ya Watani wa Jadi iliyofanyika Jumamosi iliyopita, timu iligharamiwa na viongozi waliopo pasipo kupata msaada wowote kutoka nje ya uongozi.
Kupitia uzoefu uliopatikana msimu huu kwenye eneo la mapato, uongozi sasa utabuni namna nyingine za kuongeza mapato ili kupambana na changamoto za kupungua kwa mapato ya milangoni.
TIMU
Mara baada ya kumalizika kwa Ligi Kuu, klabu imevunja kambi na wachezaji wote wamepewa ruhusa ya kupumzika hadi katika wiki ya kwanza ya mwezi Julai mwaka huu ambapo timu itaanza mazoezi kujiandaa na msimu ujao.
Na kama ilivyo katika vitabu vya Sayansi ya Michezo, Simba itafanya mazoezi ( Pre Season) kwa walau wiki sita kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu msimu ujao. Simba haitakuwa na mechi yoyote ya kirafiki na wala haitashiriki mashindano yoyote yatakayokuwa yameandaliwa katika kipindi cha kati ya mwezi Juni au Julai; labda kama benchi la ufundi litaona inafaa.
KOCHA LOGARUSIC
Uongozi wa Simba unaendelea na mazungumzo na kocha wake, Zdravko Logarusic, kuhusu kumuongezea mkataba wake na mazungumzo hayo yatafikia tamati mwishoni mwa wiki hii.
Klabu itatoa tamko rasmi kuhusu endapo itaendelea au haitaendelea na mkataba wake na kocha huyo baada ya kumalizika kwa mazungumzo hayo. Kwa sasa, haitazungumzia lolote kuhusu hilo hadi mwishoni mwa wiki hii.
Imetolewa na
Ezekiel Kamwaga
Katibu Mkuu
Simba SC
↧
Majibu ya Mh.Jerry Silaa kuhusiana na taarifa zinazosambazwa mitandaoni
Nimepokea kwa Masikitiko makubwa taarifa zinazosambazwa mitandaoni ikidaiwa ni mawasiliano baina yangu na Ridhiwani Kikwete, Mjumbe wa NEC na Mbunge mteule wa Jimbo la Chalinze.
Ingawa si tabia yangu kukanusha mambo yaliyotengenezwa kwa sababu anazojua muandaaji lakini kwa idadi ya simu nilizopokea kwa faida ya wengi ni bora niseme yafuatayo.
1.Kwa wanaofahamu matumizi ya whatsapp, screen shot hii ilipaswa kutoka kwenye simu yangu, kwa maana nyingine ni mimi mwenyewe ndiye chanzo cha jambo hili.
2. Wanaonifahamu whatsapp sio moja ya njia yangu ya mawasiliano, situmii simu aina ya samsung ambayo ndiyo inayoonekana ilikuwa inatumika katika mawasiliano hayo,na pia siifahamu na wala sijawahi kuwa na namba ya Airtel ya Ridhiwani.
3. Ukiiangalia Lugha na aina ya uchaguzi wa maneno uliotumika si aina yangu ya uandishi na maneno hata ambayo huwa nayatumia katika mazungumzo ya kawaida,mtu yoyote anayejua siasa atatambua mazungumzo hayo hayana mantiki yanaongelea mambo mengi na watu wengi kwa wakati mmoja.
4.Tarehe 5 April nilikuwa kwenye hall of fame Chuo kikuu Mzumbe na si Chalinze nilikokuwa tarehe 2,3 na 7. Muda wa ujumbe unatofautiana sana 5 am, 6.30am na 2.32pm.
Screenshots zinaonyesha kwamba majadiliano hayo yalifanyika tarehe 5 April ambayo mimi nilikuwa tayari Chuo Kikuu Mzumbe.
Mimi niliondoka Dar kwenda Chalinze rasmi siku ya tarehe 2 nikitokea katika shughuli za ugawaji wa madawati katika shule ya Sekondari Pugu ambapo nilikuwepo huko tangu asubuhi bila kupitia sehemu yoyote na niliongozana na MNEC Anthony Mavunde kwa kupitia njia ya kisarawe ili kukwepa foleni. Na tarehe 7 nilienda tena Chalinze kusherehekea ushindi.
5. Jambo hili ni rahisi sana kulitengeneza kwa simu mbili na kusave majina unayotaka na unawezo hata wa kutoa ya upande wa pili inayoonyesha jina langu.Matumizi haya ya teknolojia ni vyema yatumike katika mambo ya msingi badala ya kujaribu kuleta fitna zisizo na maana na kujaribu kuwapa watu tabia ambazo hawajawahi kuwa nazo.
6. Ushauri wangu ni kwa kila mmoja wetu hasa wanasiasa kuwa makini na kuepuka kufitinishwa kwa fitina nafuu kama hii. Kwa jambo lilozungumzwa kwanza wakati bado na pili wanasiasa wa ngazi yangu na Ridhwan si wakulijadili jambo kubwa namna hiyo kwa hoja dhaifu hivyo na tena kwenye whatsapp.
-JERRY SILAA.
Source ya majibu ni facebook page ya Jerry Silaa.
↧
↧
NEW ALERT: AJALI MWANZA WATU ZAIDI YA 20 WAFARIKI PAPO HAPO
Zaidi ya watu 20 wamefariki dunia papo hapo na wengine wengi kujeruhiwa, baada ya basi la LUWULE walilokuwa wakisafiria kutoka Musoma kwenda Mwanza kuacha njia, kugonga nyumba na kupinduka katika kijiji cha Itwimila wilaya ya Busega.
↧
TANZIA: MKUU WA WILAYA YA KALAMBO AFARIKI DUNIA
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo enzi za uhai wake Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae amefariki dunia jioni ya leo katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari.
Taratibu za mazishi zitatangazwa mapema mara baada ya kikao cha wanandugu. Tunatoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba huu. Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa,
Jina lake lihimidiwe.
AMIN
(Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
Taratibu za mazishi zitatangazwa mapema mara baada ya kikao cha wanandugu. Tunatoa pole kwa wale wote walioguswa na msiba huu. Sisi tulimpenda lakini Mungu kampenda zaidi.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa,
Jina lake lihimidiwe.
AMIN
(Na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa)
↧
Maendeleo ya Msiba wa Mhe. Moshi Mussa Chang'a,nyumbani kwa marehemu Mbagala jijini Dar leo
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya akiwa ni mwenye majonzi wakati akisaini kitabu cha Maombolezo ya Kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari.
Msiba upo nyumbani kwa Marehemu,eneo la Mbagala jijini Dar es Salaam ambapo taratibu zote zinafanyika hapo.
Taarifa za awali zinaeleza kwamba Shughuli ya kuaga mwili wa Marehemu,Mhe. Moshi Mussa Chang'a itafanyika kesho Aprili 22,2014 nyumbani kwake Mbagala na baadae mwili utasafirishwa kwenda kijijini kwao Mkoani Iringa kwa Mazishi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwassa wakati wakiwa kwenye Msiba wa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a,nyumbani kwa Marehemu Mbagala,jijini Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick (katikati) akijadiliana jambo na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa,Injinia Stella Manyanya (kulia) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Bahi,Mh. Betty Mkwassa wakati wakiwa kwenye Msiba wa Mkuu wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a,nyumbani kwa Marehemu Mbagala,jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya Waheshimiwa wakuu wa Wilaya mbali mbali hapa nchini wakiwa kwenye msiba wa Mkuu mwenzao wa Wilaya ya Kalambo, Mhe. Moshi Mussa Chang'a ambae alifariki dunia jana jioni katika Hospitali ya Muhimbili Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu ya ugojwa wa shinikizo la damu na Kisukari,nyumbani kwa Marehemu Mbagala jijini Dar es salaam.
↧
Moto wa wateketeza maduka matatu na mgahawa mjini Dodoma usiku wa kuamkia leo
Wananchi wa mji wa Dodoma wakiangalia sehemu ya madhara ya tukio la moto uliotokea usiku wa kuamkia leo katika baadhi ya maduka yaliopo kwenye Barabara ya Nyerere Karibu na Makao makuu ya CCM mjini Dodoma,moto huo umeteketeza maduka matatu na mgahawa wa New Chick Villa Reustaurant. Maduka yaliyoathirika na moto huo ni Gulio La Mahafa Duka lililokuwa linauza bidhaa mbali mbali kwa jumla na reja reja zikiwamo bidhaa za Bakhresa,Duka la Esheki Investment lililo kuwa likiuza bidhaa za maofisini,vitabu na huduma ya uchapaji pomoja na Duka la madawa la lijulikanalo kama Kavula Pharmacy.Picha na Deusdedit Moshi,Globu ya Jamii Dodoma.
Wakazi wa Mji wa Dodoma wakiendelea kuangalia maduka hayo huku wengi wao wakiwa hawaamini kilichotokea.
Kila aliekatiza katika eneo hilo akusita kusimama na kuangaria athari hiyo ya moto kwenye Maduka hayo.
Sehemu iliyokuwa na maduka ikiwa imeteketea kabisa kwa moto uliotokea leo Barabara ya Nyerere karibu na Ofisi za makao makuu ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Sehemu iliyokuwa na maduka ikiwa imeteketea kabisa kwa moto uliotokea leo Barabara ya Nyerere karibu na Ofisi za makao makuu ya Chama cha Mapinduzi CCM.
Waokoaji wakihesabu baadhi ya bidhaa walizookoa kutoka stoo ya Mahavaz Gumo.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 21/04/2014.
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA DODOMA KWA VYOMBO VYA HABARI TAREHE 21/04/2014.
Hali ya ulinzi na usalama ilikuwa ni shwari na wananchi walisherehekea kwa amani na utulivu isipokuwa kulikuwa na matukio mawili ya moto kuunguza nyumba.
Tukio la kwanza lilitokea tarehe 20/04/2014 majira ya 20:30 hrs usiku katika mtaa wa Barabara ya Nyerere “zamani kuu street” mkabala na CCM Makao Makuku Dodoma, nyumba ya biashara yenye maduka mbalimbali iliungua kwa moto na kuteketeza mali mbalimbali na mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Frank Pilla, miaka 45, mkazi wa Ipagala, alijeruhiwa kwa moto sehemu za mikononi na usoni na kulazwa Hospitali ya Mkoa Dodoma na kuruhusiwa saa 08:00hrs asubuhi tarehe 21/04/2014 baada ya kupatiwa matibabu.
Maduka matatu yaliteketea kwa moto huo ambayo ni:-
1. Mahavaz Gumo duka la bidhaa za chakula ambalo linamilikiwa na Frank Pilla, miaka 45, mfanyabiashara mkazi wa Ipagala,
2. Stationary na M-Pesa liamilikiwa na Esheki Elikana Moshi, miaka 54, mfanyabishara mkazi wa Miyuji,
3. Malaika Cosmetics, duka la vipodozi linalomilikiwa na Jamila Baduwel, miaka 30, mfanyabishara mkazi wa Area “D” na
4. Duka moja la Dawa baridi Kavula Pharmacy linalomilikiwa na Mariam Rashidi, miaka 40 mfanyabiashara mkazi wa Chamwino, liliokolewa na zima moto. Uharibifu uliosababishwa na moto huo ni kuungua kwa paa la duka hilo na kuta.
Moto ulianzia katika duka la Mahavaz Gumo na kusambaa kwa kasi katika maduka mengine ya jirani na kuteketeza mali zilizokuwemo. Thamani ya mali iliyoteketea haijafahamika na chanzo cha moto huo hakijafahamika, uchunguzi unaendelea.
Tukio la pili lilitokea majira ya 21:00hrs usiku huko Area “D” Bock R site two Manispaa ya Dodoma, nyumba anayoishi Mh. Amina Makilagi, Mbunge wa Viti Maalum kupitia CCM kutoka Mkoa wa Mwanza ambaye hakuwepo yupo safarini. Vitu mbalimbali viliteketea kwa moto na thamani yake bado haifahamika. Chanzo cha ajali hiyo ya moto bado hakijafahamika, uchunguzi zaidi unaendelea.
Aidha Polisi Mkoa wa Dodoma tunawashikilia wanawake 12 kwa kosa la kujihusisha na biashara ya kuuza miili (Ukahaba).
Imetolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
↧
↧
David Moyes: Manchester United 'no comment' on boss reports
National newspapers say the club will dispense with the Scot's services following a poor season.
However a United spokesperson would only confirm Moyes has not been sacked.
When pressed on whether the manager would leave before the end of the season, the spokesperson added, "we do not comment on speculation".
None of the newspapers are reporting that Moyes has been sacked yet. The Daily Mail writes that he will be dismissed before the end of the season, while the Daily Telegraph says he has lost the support of club owners the Glazer family and is facing the sack.
The Daily Mirror , meanwhile, reports that the United board will sack him, but report it is unclear whether that will happen before the weekend's game at home to Norwich.
Moyes was chosen by Sir Alex Ferguson to succeed him as United manager when he stepped down from the role after 26 years in charge last summer.
The 50 year-old was handed a six-year deal to leave Everton for the Premier League champions but his tenure could be nearing an end after just 10 months. For source and more CLICK HERE
↧
PASAKA YA KATIBA
↧
SITTA AMPA TAARIFA YA MWENENDO WA BUNGE MAALUM DKT. SHEIN
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Samuel Sitta akimpatia taarifa juu ya mwenendo wa Bunge Maalum la katiba na ulipofikia, Rais Wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mheshimiwa Dkt. Ali Mohammed Shein, alipomtembelea nyumbani Ikulu ya Migombani Zanzibar. Mhe Sitta alikuwa Visiwani Zanzibar kwa lengo la kuonana na Mhe. Shein kumpatia taarifa kamili ya shughuli za Bunge Maalum la Katiba. Picha na Owen Mwandumbya - Bunge Maalum
↧
More Pages to Explore .....