Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live

News Alert: Helkopta ya yaanguka wakati wa Kuruka kwenye Uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere jijini Dar leo

$
0
0
Helkopta ya Jeshi la Polisi Tanzania ikiwa imepiga mweleka mapema leo katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K. Nyerere mara baada ya kupatwa na hitilafu ya kiufundi wakati wa ikitaka kuruka.Taarifa za uhakika kabisa zilizoifikia Globu ya Jamii,zinaeleza kuwa Helkopta hiyo ilishindwa kuruka kwa kwenda mbele na badala yake iiliruka kwa kurudi nyuma,hali iliyopelekea Panga la Helkopta hiyo kujipigiza kwenye moja ya Paa la Karakana la Uwanjani hapo na kupiga mweleka.Hakuna aliedhulika katika ajali hiyo.

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA YA KUKAGUA ATHALI ZA MAFURIKO DAR NA MAENDELEO YA UJENZI WA DARAJA LA MPIJI

$
0
0
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Eng. Mussa Iombe, sehemu ya Daraja la Mpiji linalounganisha Bagamoyo na Dar es Salaam, lililokatika kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini, wakati Makamu alipofanya ziara hiyo ya kujionea maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo leo Aprili 13, 2014.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya viongozi wanaosimamia shughuli ya daraja hilo, baada ya kuwasili eneo hilo leo.
Sehemu ya daraja hilo, linavyoonekana baada ya kuongezeka upana kwa kulika kutoka mita 25 na sasa kufikia mita 75, ambapo tayari Malori yameanza kumwaga vifusi vya mawe ili kuziba eneo hilo na kuweza kuunganisha njia hiyo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiongozana na baadhi ya viongozi kuelekea eneo la tukio kukagua maendeleo ya ujenzi wa Daraja la Mpiji lililokatika kutokana na Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini.
Nguzo za umeme zikiwa zimeinama baada ya kuzidiwa nguvu na maji hayo yaliyobomoa daraja.

bwawa la maini oyeeee!

$
0
0
 Ankal akifurahia ushindi wa 3-2 dhidi ya Man City leo huko Anfield. 
 Baadhi ya Bongo Kops wakiserebuka kwa ushindi leo
 Nahodha Steven Gerald na wenzie wakifurahia ushindi
Wadau wa Bongo Kops na mwenyekiti wao Musley (kati) wakiwa na furaha baada ya gemu

HOJA YA HAJA: "Tubadili Jiji la Dar es Salaam: Kuna Zaidi ya Mafuriko"

NGOMA AFRICA BAND YA UJERUMANI YAOMBOLEZA KIFO CHA MWANA MUZIKI MKONGWE MUHIDIN GURUMO (RIP)

$
0
0
 Tumepokea kwa huzuni tele na majonzi makubwa taarifa ya kifo cha mkongwe wa muziki wa dansi nchini Tanzania na Africa ya mashariki marehemu mzee Muhidin Maalimu Gurumo Kilichotokea leo 13.04.2014 huko nyumbani Tanzania.
Pamoja na kuwa mbali na nyumbani bendi ya muziki wa dansi Ngoma Africa Band yenye makao yake nchini Ujerumani  inaungana na watanzania wote popote pale katika kuomboleza msiba huu.
Tunatoa pole zetu kwa bendi ya Msondo Ngoma pamoja na familia ya marehemu,mwenyezi mungu
amlaze mahala pema peponi marehemu Mzee Muhidin Maalim
Gurumo (RIP)

Amin

Marehemu Muhidin Maalim Gurumo enzi za uhai wake

Umoja wa waTanzania Ujerumani (UTU) kufanya mkutato mkuu wa Uchaguzi 26.April 2014 Berlin

$
0
0
Berlin,Ujerumani,
Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatarajia kufanya mkutano wake mkuu  wa uchaguzi siku ya kilele cha sherehe za muunganno wa Tanzania mjini Berlin, Ujerumani. siku ya tarehe 26.April.2014 kuanzia saa 7 mchana katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.

Watanzania wote wanaoishi Ujerumani wanaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huu muhimu wa chombo chao UTU ambao kinawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani bila kujali itikadi zao za kidini, jinsia, wala kabila.

Umoja wa watanzania ujerumani unafuraha kubwa ya kuwafungilia milango wale wote ambao wanataka kujiunga na umoja huo. Pia milango ipo wazi kwa wadau na wale wote wanaohitaji ushauri juu ya kuwekeza au kuchangia maendeleo ya jamii nyumbani Tanzania.

Pia pata kuwepo na vyakula vya kitanzania

KUFIKA KWENU KATIKA MKUTANO HUU NDIO MAFANIKIO YA WATANZANIA WOTE

UMOJA NI NGUVU , UTENGANO NI UDHAIFU

UMOJA WA KITAIFA NDIO MSINGI IMARA KWA WATANZANIA
MUNGU IBARIKI TANZANIA

Kwa maelezo zaidi wasiliana simu :    +491737363422
Email. kamati.utu@googlemail.com

MKUTANO WA KRFA WAFANA MJINI BUKOBA, JAMAL EMIL MALINZI KUENDELEA KUWA MWENYEKITI KRFA

$
0
0
Na Faustine Ruta, Bukoba

Chama cha mpira wa miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) kimefanya mkutano mkuu wa kawaida kwenye ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera na Mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Missenye Kanal Issa Njiku. 

Awali akisoma taarifa yake mwenyekiti wa KRFA ambae pia ni Rais wa TFF Jamal Emil Malinzi aliwashukuru wajumbe wote wa mkutano mkuu kwa namna walivyoshiriki kwa namna tofauti katika kuendeleza michezo katika wilaya zote za Mkoa wa Kagera,Hotuba iliyosheheni mipango kedekede ya kuinua soka kwa ujumla nchini Tanzania na Kagera ikiwemo. 

Katika mambo mengi aliyoeleza ameweza kueleza changamoto nyingi zinazoikabiri KRFA na kuwataka viongozi kuhakikisha wanawasiliana na Halimashauri za wilaya zao kutenga maeneo ya viwanja vya michezo,akiongelea uwanja wa Kaitaba amesema anayofuraha kuwajulisha wajumbe kuwa sasa uwanja huo unawekewa nyasi bandia kwa ufadhili wa FIFA kwa asilimia mia moja, Lakini pia amehaidi kuitisha Harambee ya wadau mbalimbali jijini Dar es salam kwa ajili ya kupata pesa ya kujenga jukwaa moja katika uwanja wa Kaitaba Bukoba. 

Pia aliweza kuelezea kuhusiana na nafasi ya Uenyekiti wa KRFA, Amesema tangu amepata nafasi ya Rais TFF amekuwa akikutana na maswali mengi ya waandishi wa habari na wadau kuhusiana na kujiudhuru nafasi hiyo, (Wakati nakuja Bukoba nilikuwa na wazo ili la kujiudhuru, Lakini kila mjumbe aliesimama hapa ameniomba nisijiudhuru mpaka wengine kutamka kuwa iwapo nitajiuzuru basi nao watajiudhuru nafasi hii, lakini kuna mjumbe kasema wapo watu wakati wa kampeni walikuwa wakisema natafuta nafasi hii ili niweze kugombea urais, kwahiyo basi naomba nitamke kuwa sitojiudhuru nitaendelea kuwa mwenyekiti wa KRFA.)
Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA)Jamal Emil Malinzi akizungumza na Wajumbe waliojitokeza katika mkutano huo wa Utekelezaji wa Chama cha Mpira wa Miguu (KRFA) Mkoa wa Kagera, Ambapo pia alizungumzia swala zima la kuendelea kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Mkutano uliofanyika  kwenye Ukumbi wa Mkuu wa mkoa wa Kagera
Mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi mkoani Kagera, Kanali Mstaafu Issa Njiku akizungumza na wajumbe.

SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS LAINGIA SIKU YA PILI MKOANI DODOMA, MCHUJO KUANZA KESHO

$
0
0
Mmoja wa washiriki wa Shindano la kusaka Vipaji vya Uigizaji Tanzania, lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) Bw  akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kumaliza kwa zoezi la usaili katika shindano la TMT.
Baadhi ya washiriki waliojitokeza kwa ajili ya Kushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya uigizaji wakiwa katika mstari tayari kwa kupewa fomu ya usaili ili kuweza kushiriki kwenye shindano la TMT.
 Baadhi ya washiriki waliofika katika ukumbi wa African Dream kwaajili ya usaili wa shindano la kusaka vipaji vya kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakijaza fomu kwaajili ya shindano hilo ambalo kwasasa linaendelea Katika Kanda ya Kati Mkoani Dodoma.
Kundi la kwanza likiwa tayari kwaajili ya kupewa namba za ushiriki mara baada ya kumaliza zoezi zima la kujaza fomu za ushiriki katika shindano la kusaka vipaji vya Kuigiza lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents linaloendelea kufanyika Mkoani Dodoma leo ikiwa inawakilisha Kanda ya Kati.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma.
Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma.
Shindano la Tanzania Movie Talents leo limeingia siku ya pili ya usaili mkoani Dodoma, Kanda ya Kati ikiwa na washiriki waliojitokeza zaidi ya 600. Shindano hili limeibua hisia za Watu wengi kutokana na Umahiri wake na kuwa shindano la kwanza kutokea Afrika Mashariki na Kati huku maandalizi yake yakiwa yamefanyika kwa umakini wa hali ya juu huku Majaji wa Shindano hilo wakitokea kuwa Vivutio vikubwa kwa washiriki hao kutokana na jinsi wanavyotoa Uamuzi.
Washiriki zaidi ya 600 wameweza kujitokeza kushiriki shindano hili ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na mpaka sasa zoezi hili limeingia siku ya pili ambapo timu ya TMT imeendelea kusaili vijana waliojitokeza.
Safari ya Mchujo wa shindano hili kwa kanda ya kati ambapo shindano hili linafanyika mkoani Dodoma utaanza kufanyika kesho Jumatatu ili kuweza kupata washindi watatu bora ambao kila mmoja atajiondokea na Kitita cha Shilingi laki tano (500,000) kwa kila mshindi na baadae kujiunga na washindi wengine wa kanda zilizobakia Kwaajili ya fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na kupelekea Mshindi kujinyakulia zawadi kubwa kabisa ya Kitita cha pesa za Kitanzania Milioni 50 (50,000,000/=) na vilevile washindi kumi bora katika fainali hiyo watakuwa chini ya Uangalizi wa Kampuni ya Proin Promotions na watafanya kazi ya pamoja na hatimaye kazi yao kuweza kuuzwa nchini nzima na wao kunufaika na kazi hiyo.
Shindano hili linaloendelea kufanyika mkoani Dodoma linatarajiwa kumalizika mnamo Jumanne ya 15 April 2014 na siku hiyohiyo Washindi watatu watatangazwa.
Baada ya shindano hili kumalizika Kanda ya Kati Mkoani Dodoma, shindano litaelekea Kanda ya Nyanda za Juu Kusini Mkoani Mbeya kwaajili ya vijana kuweza kuitumia fursa hii kwaajili ya kuonyesha Uwezo na vipaji vyao katika Kuigiza.
Katika Shindano hili vijana wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuitumia fursa hii na hatimaye kuweza kuonyesha vipaji vyao kwa maana huu ndio muda wao.
Hakuna viingilio katika shindano hili na fomu zinapatikana bila gharama yoyote ile.

Umoja wa waTanzania Ujerumani (UTU) kufanya mkutato mkuu wa Uchaguzi .April 26, 2014 mjini Berlin

$
0
0
Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) unatarajia kufanya mkutano wake mkuu  wa uchaguzi siku ya kilele cha sherehe za muunganno wa Tanzania mjini Berlin, Ujerumani. siku ya tarehe 26.April.2014 kuanzia saa 7 mchana katika ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.
Watanzania wote wanaoishi Ujerumani wanaombwa kuhudhuria kwa wingi katika mkutano huu muhimu wa chombo chao UTU ambao kinawaunganisha watanzania wote waishio ujerumani bila kujali itikadi zao za kidini, jinsia, wala kabila.
Umoja wa watanzania ujerumani unafuraha kubwa ya kuwafungilia milango wale wote ambao wanataka kujiunga na umoja huo. Pia milango ipo wazi kwa wadau na wale wote wanaohitaji ushauri juu ya kuwekeza au kuchangia maendeleo ya jamii nyumbani Tanzania.
Pia pata kuwepo na vyakula vya kitanzania

KUFIKA KWENU KATIKA MKUTANO HUU NDIO MAFANIKIO YA WATANZANIA WOTE. UMOJA NI NGUVU , UTENGANO NI UDHAIFU
 UMOJA WA KITAIFA NDIO MSINGI IMARA KWA WATANZANIA
MUNGU IBARIKI TANZANIA

Kwa maelezo zaidi wasiliana simu :    +491737363422

KARIBUNI WOTE KATIKA KONGAMANO LA BIASHARA MJINI BERLIN, UJERUMANI

$
0
0
Mhe. Philip S. Marmo, Balozi wa
Tanzania nchini Ujerumani 
 Kama mnavyofahamu kuwa siku ya tarehe 26 Aprili, 2014 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza miaka hamsini (50), kwa lugha nyingine ni “Golden Jubilee”.
 Katika kuadhimisha sherehe hii kubwa na muhimu, Ubalozi umeamua kuandaa Kongamano la Biashara (Investment Forum) kwa siku ya tarehe 25 Aprili, 2014 pamoja na siku ya terehe 26 Aprili, 2014 kuwa siku ya mdahalo (Scholars' day) mjini Berlin, Ujerumani.
 Madhumuni makubwa ya Kongamano hili ni kuwatangazia na kuwaonyesha umma wa Wajerumani mafanikio mbalimbali yaliopatikana ndani ya muungano wetu kwa kuwaonyesha fursa tulizonazo za biashara katika nyanja za kilimo, utalii, nishati na madani, viwanda, elimu n.k.
 Hivyo, Mhe. Philip S. Marmo, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani anawakaribisha Watanzania wote wanaoishi nchini Ujerumani na wale wanaoishi kwenye maeneo ya uwakilishi ya Ubalozi kuja kushiriki kwenye Kongamano la Biashara siku ya tarehe 25 Aprili, 2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni kwenye ukumbi wa Logenhaus, Emser Str.12-13, 10719 Berlin, Ujerumani.
Aidha, Mhe. Balozi anawakaribisha pia kwenye mdahalo siku ya tarehe 26 Aprili, 2014 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana kwenye ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.
 Kwa maeleozo zaidi piga simu:
 +49303030800
 ASANTENI SANA!

Business Development Manager wanted at Gemini Tours & Safaris

RAY C: NEW SONG TEASER: LEGENDARY MUSIC-STUDIO

$
0
0
Ray C akiwa ndani ya Legendary Music Studio akirekodi moja kati ya nyimbo zake Mpya. It was a good experience working with such a Big Tanzanian and East African Female Artist. Stay tuned for more good music from Legendary Music-Tanzania stay tuned kwa Ujio Mpya wa Ray C.

SIKILIZA KIPINDI ' KUTOKA SOKO LA HABARI KARIAKOO' KILA ASUBUHI.

NEWS ALERT: MUHIDIN MAALIM GURUMO AFARIKI DUNIA

$
0
0
MAALIM MUHIDIN GURUMO ENZI ZA UHAI WAKE.

NGULI WA MUZIKI WA DANSI HAPA NCHINI NA ALIEKUWA KIONGOZI WA BENDI YA MSONDO NGOMA,MAALIM MUHIDIN GURUMO AMEFARIKI DUNIA MCHANA WA LEO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA YA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA KWA MATIBABU.

MAALIM GURUMO AMEFIKWA NA MAUTI HAYO BAADA YA KUSUMBULIWA NA MARADHI KWA KIPINDI KIREFU, HALI ILIYOMPELEKEA KUAMUA KUSTAAFU MUZIKI.

MSIBA UPO NYUMBANI KWA MAREHEMU TABATA MAKUBURI NA MIPANGO YOTE ITAFANYIKA HAPO.

GLOBU YA JAMII KWA MASIKITIKO MAKUBWA,INATOA POLE KWA WAFIWA WOTE PAMOJA NA WAPENZI WOTE WA BENDI YA MSONDO NGOMA MAHALA POPOTE PALE WALIPO.

TUNAMUOMBEA KWA MWENYEZI MUNGU AIWEKE ROHO YA MAREHEMU MAALIM GURUMO MAHALA PEMA PEPONI.

- AMIN.

JK atembelea maeneo yaliyokumbwa na mafuriko Mkoa wa Pwan

$
0
0

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mmoja wa baadhi ya abiria waliokwama baada ya barabara ya Chalinze-Dar es Salaam kuharibiwa vibaya na mafuriko

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkewe Mama Salma Kikwete na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza wakikagua athari za mafuriko zilizoharibu vibaya barabara ya Chalinze- Dar es Salaam eneo la Ruvu Darajani leo.Mamia ya abiria walikuwa wamekwama kutokana na mafuriko hayo



i Rais akisalimiana na kuzungumza na wanafunzi na mtoto aliyemfuata na kumsalimia.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete,Mke wa Rais Mama Salma Kikwete,Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mwantumu Mahiza na Mbunge wa Chalinze Ridhiwani Kikwete wakikagua athari za mafuriko maeneo ya Ruvu Darajani na Visiga
Picha na Freddy Maro

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AWASILI SALAMA MKOA WA KATAVI USIKU HUU AKITOKEA KIGOMA.

$
0
0
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia kwa ufupi wakazi wa mji wa Karema mkoani Katavi usiku huu mara baada ya kuwasili akitokea mkoani Kigoma kwa boti na kusafiri nayo ndani ya ziwa Tanganyika takribani kwa masaa kumi na manne.Kutokana na safari hiyo kuwa ndefu ya majini,inaelezwa kuwa kuna baadhi ya Watu wamedai msafara wa Katibu Mkuu huyo,Kinana umepotea ziwa Tanganyika,jambo ambalo si la kweli na la kizushi.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwapungia wenyeji wake (hawapo pichani) waliofika kumpokea usiku huu kwa boti akitokea mkoani Kigoma  katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne
 Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanal Mstaaf Issa Machibya akishuka kwenye boti usiku huu kwenye bandari ya Karema mkoani Katavi akiwa ameambatana na Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,na Viongozi wengine wa Taifa,Mkoa na Wilaya tayari kwa kuanza ziara ya siku nne mkoani Katavi. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishuka kwenye boti wakati wenyeji wake (hawapo pichani) walipokuwa wakimsubiri kumpokea usiku huu akitokea mkoani Kigoma  katika bandari ya Karema mkoani Katavi,ambako amemaliza ziara yake ya siku tano na kuhamia mkoani Katavi ambako pia atakuwa na ziara ya siku nne.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Viongozi mbalimbali wa mkoa na Wilaya ndani ya Mkoa wa Katavi usiku huu,alipokuwa akiwasili kwenye bandari ya Karema mkoani humo usiku huu.Kinana ameongoza na Katibu Wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,Mjumbe wa NEC,Balozi Ali Karume,Mkuu wa mkoa wa Kigoma,Kanal Issa Machibya,Mwenyekiti wa CCM,Mkoa wa Kigoma ndugu Kabouru na wengineo.
 Kinana akipokelewa na Gwaride la chipukizi usiku huu ndani ya mkoa wa Katavi.

ngoma azipendazo ankal

KUMBUKUMBU YA MUHIDIN MAALIM GURUMO (RIP)

Kufikia kikomo kwa Windows XP, nini athari zake kwa mtumiaji?

$
0
0

Mnamo tarehe 8/4/2014 kampuni ya utengenezaji wa mitambo endeshi ya kompyuta (Operating Systems) ya Microsoft ilisitisha utoaji wa huduma za muda mrefu kwa mitambo ya XP, ni moja ya mitambo endeshi inayotumika na watu wengi sana.Tangu kutoka kwa taarifa hizo, kumekuwa na maneno na mikanganyiko mingi mno kwa wateja hususan hapa Tanzania.

Kwakuwa ni mitambo inayotumika kwa weingi kwenye kompyuta nyingi zinazotumika kwenye mabenki na maofisini, hivyo watu walifika mbali hata kusema eti pesa zetu hazipo salama tena. Hivyo, ili kuondoa hofu hizi zinazoizunguka jamii, ungana nasi Dudumizi kwenye kujua nini maana ya kikomo hiki cha huduma na jinsi gani kinaweza kuathiri biashara yako?

 Kwanini XP imefikia kikomo?

XP iliingia sokoni miaka 12 iliyopita, tangu kuingia kwake, imekuwa ni mtambo endeshi unaotumika kwa wingi na makampuni mengi duniani kote. Na pia ni moja ya mtambo endeshi kutoka Microsoft uliokaa kwa muda mrefu sokoni. Ingawa katika uhai wa Windows XP, kumekuwa na matoleo mengine mengi kama Windows Vista, Windows 7 na ya sasa ambayo ni Windows 8, lakini kampuni ya Microfost imeendelea kutoka msaada wa kiufundi na kimatumizi kwa wateja wake wote, hivyo kwa maneno mengine tunaweza kusema,muda wake wa maisha umefika na ni mzigo kiutendaji na hata kibiashara kwa Microsoft kuendelea kuhudumia Windows XP ndiyo maana wameamua kusitisha huduma kwa Windows XP.

Je nini maana ya usisitshwaji wa Huduma?

Hapa ndipo palitokea mkanganyiko miongoni mwa watu wengi, kusitishwa kwa huduma hakumaanishi kuwa kompyuta zote zinazotumia XP hazitotumika tena kama wengine walivyoifananaisha na uhamaji wa mitambo ya analog kwenda Digital. 

MH. SITTA AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI YA BUNGE MAALUM LEO

$
0
0
Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. samuel Sitta akiongoza kikao cha kamati ya uongozi ikiwa ni pamoja na kupitia ratiba ya Bunge hilo leo. Kushoto ni Katibu wa Bunge Maalum la Katiba Ndg. Yahya Khamis Hamad.
Mwanasheria Mkuu wa serikali Mhe. Fredrick Werema akifafanua jambo wakati wa kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum leo. Kamati hiyo ilikaa kupitia ratiba nzima ya Bunge Maalum na jinsi litakavyoendelea na sura za rasimu ya katiba.
Wajumbe wa kamati ya Uongozi ya Bunge Maalum wakimsikilija Jaji Fredrick Werema akifafanua baadhi ya vipengele vilivyomo katika kanuni za Bunge Maalum. Picha na Owen Mwandumbya.
Viewing all 110167 articles
Browse latest View live




Latest Images