Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live

CRDB YAKABIDHI MCHANGO WAKE KWA UBALOZI WA TANZANIA NCHI MAREKANI

0
0

 Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Dr. Charles Kimei (kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bwn. Martin Mmari kwenye kikao cha makabidhiano ya mchango wa CRDB kwa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani kwa ajili ya sherehe ya miaka 50 ya Muungano itakazoadhimishwa kitaifa Washington, DC April 26, 2014 CRDB kupitia kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ilimkabidhi Mhe. Liberata Mulamula fedha taslimu za Kimarekani dola 5,000 siku ya Ijumaa April 11, 2014. Makabidhiano hayo yalifanyikia Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani.
 Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Bwn. Saugata Bandyopadhyay CRDB Deputy Managing Director (operations and customer services)
 Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Bwn. Alex Ngusaru Director of Treasery wa CRDB
 Mhe. Liberata Mulamula akisalimiana na Bi. Tully wenngine katika picha ni Anderson Mlabwa (wapili toka kulia) na Director of Credit wa CRDB Bank na Bwn. Saugata Bandyopadhyay CRDB Deputy Managing Director (operations and customer services)
 Kikako cha makabidhiano kikiendelea.
 Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bwn. Martin Mmari akimkabidhi Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula kitita cha dola 5,000 katika kikao cha makabidhiano kilichofanyika Ubalozi wa Tanzania siku ya ijumaa April 11, 2014.
 Picha ya pamoja
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya CRDB Bwn. Martin Mmari, Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe, Liberata Mulamula na Mkurugenzi Mkuu wa CRDB Bank DR. Charles Kimei katika picha ya pamoja.

Wakazi wa Dar mnatambua uwepo wa Ziwa Mwananyamala??

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LEO TAREHE 12.04.2014

DARAJA LAKATIKA ENEO LA MAPINGA,BAGAMOYO - KAMANDA WA POLISI MKOA WA PWANI ATHIBITISHA

0
0
Wakazi wa eneo la Mapingwa Mkoani Pwani wakiwa kwenye mshangao mkubwa baada ya kushindwa kuvuka Daraja la Mto unaokatisha kwenye eneo hilo baada ya kutokuwepo kwa mawasiliano ya barabara kwa kukatika kwa daraja hilo kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha hivi sasa katika maeneo mbali mbali hapa nchini.

Akithibitisha kutokea kwa hitilafu hiyo,Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani,ACP Ulrich Matei amesema ni kweli kumetokea kwa tatizo hilo na amewataka watumiaji wa barabara ya Bagamoyo kubadilisha njia na kuwanza kutumia barabara ya Morogoro mpaka hapo daraja hilo litakapofanyiwa matengenezo.

Globu ya Jamii itaendeleo kuwataarifu taarifa mbali mbali zitakazo kuwa zikitufikia kwenye chumba chetu cha habari.

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA ATEMBELEA MJI WA KIHISTORIA WA UJIJI,AKUTANA NA WAVUVI WADOGO WADOGO ZIWA TANGANYIKA

0
0
 
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akimsikiliza Mzee Masoud Mwinyi Chande kwenye mnara wa kumbukumbu ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Inaelezwa kuwa Nyumba hiyo Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadili na Bibi Titi Mohamed.Kulia ni Mbunge wa Kigoma Mjini,Mh Peter Serukamba,Katibu wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye,pamoja na Mwenyekiti wa CCM-Kigoma Ndugu Amani Kabouru. 
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akielekezwa sehemu ya Chumba na mlango ndani ya nyumba ya kwanza ambayo Mwalimu Julius Nyerere alifikia Ujiji wakati akifanya harakati za kutafuta Uhuru, Nyumba hiyo inasemekana Mwalimu Nyerere alifika akiongozana na Suleiman Takadili na Bibi Titi Mohamed.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi ndani ya Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la mji wa kihistoria,Ujiji mkoani Kigoma.
 Sehemu ya njia (route) kama ionekanavyo pichani ndani mji wa kihistoria Ujiji mkoani Kigoma,iliyotumika kusafirishia Watumwa kwenda sehemu mbalimbali,katika njia hiyo kuna miembe inayoelezwa ina umri zaidi ya miaka 150 tangu kupandwa kwake,na inaelezwa inapatikana sehemu ya Tabora na Bagamoyo. 
 Mmoja wa wakazi wa eneo la Kibiri,ambalo liko ufukweni kabisa mwa ziwa Tanganyika mkoani Kigoma,akibandika mabango yake yenye ujumbe wa kumpokea Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana,alipokwenda kutembelea eneo hilo na kusikiliza kero mbalimbali za wavuvi wadogo wadogo.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma bango lenye ujumbe wa kulalamikia kodi kubwa  wanazotozwa wavuvi wadogowadogo wa Kibirizi,Kigoma.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Kibirizi mkoani Kigoma ambao wanakilio cha kutozwa kodi kubwa, kuvamiwa na majambazi wakati wa shughuli zao za uvuvi.
Pichani Kati ni Mbunge wa Kigoma Mjini,Mh Peter Serukamba akieleza jambo kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana (shoto) wakati wakielekea kutazama Nyumba ya Makumbusho ya Dr Livingstone iliyopo katika eneo la Ujiji mkoani Kigoma,kulia ni a Katibu wa NEC,Siasa na Uenezi,Nape Nnauye.

MKURUGENZI MKUU WA TANZANIA WOMEN'S BANK MS MARGARETH CHACHA AKUTANA NA WAKINA MAMA WA DMV

0
0
Mama Anna Mukami akiwakaribisha wakina mama wa DMV na kumtambulisha mkurugenzi mkuu wa Tanzania Women's Bank wakati Ms Margareth Chacha alipokutana na wakina mama DMV na kuwaelezea sababu za kuanzishwa Benki ya akina mama.
Mchungaji Dr. Nicku Kyangu Mordi akianza kwa sala kabla ya mkutano kuanza.
Ms Margareth Chacha Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Women's Bank akiongea na akina mama DMV siku ya Ijumaa April 11, 2014 na kuwapa faida ya kufungua AC na Benk hiyo ikiwemo masharti nafuu ya mikopo na kuwaeleza Mabenki mengine inakuwa vigumu kwa wanawake kupata mikopo na akatolea mfano wa sharti moja wpo ni kuwa na nyumba kwa uzoefu wake nyumba nyingi Tanzania zinakuwa kwa majina na waume zao kitu ambacho ni vigumu kwa wanawake wengi kukidhi masharti ya mikopo. Kitu kingine alichoelezea ni kuamisha pesa kupitia benki yao ni kwa haraka zaidi ukilinganisha na Benki zingine.
Mkuu wa Utawala na Fedha Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani Mama Lily Munanka akifuatilia maelezo ya Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Women's Bank kulia ni D
Wanakina Mama DMV wakifuatilia maelezo kutoka kwa mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Women's Bank.
Asha na Mrs Mtalemwa wakifuatilia maelezo.
Mzee Safari ambaye alihudhuria mkutano huo kati ni Mama Kayani.
Wakina mama wa DMV wakiwa kwenye mkutano na Ms Margareth Chacha Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Women's Bank.
Wakina mama wa DMV wakiwa kwenye mkutano na Mkurugenzi wa Tanzania Women's Bank
Wakina mama wa DMV wakifuatilia maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Women's Bank.

shujaa wa mvua dar es salaam

RAIS KIKWETE AONGOZA MAADHIMISHO YA KUMBUKUMBU YA MIAKA 30 YA KIFO CHA HAYATI EDWARD MORINGE SOKOINE WILAYANI MONDULI

0
0
Rais wa Jamhuri wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameketi na wajane wa hayati Edward Moringe Sokoine pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa katika misa ya kumbukumbu ya miaka 30 ya kifo cha Sokoine.
Mhe. Rais akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Mhe. Benjamini William Mkapa akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Dkt. Salim Ahmed Salim nae akiweka shada la maua.
Waziri Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Lowasa nae akiweka shada.
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiweka shada la maua katika kaburi la aliyekuwa waziri Mkuu wa Tanzania hayati Edward Moringe Sokoine.


KINANA AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU TANO MKOANI KIGOMA,AHUTUBIA HUKU MVUA KUBWA IKINYESHA

0
0
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa wilaya ya Kigoma mjini bila kujali mvua,ambapo alisisitiza kuwa CCM itatekeleza kila walichoahidi.
Kila mtu alijikinga na mvua kwenye uwanja wa Mwanga Community Centre
Viti vikitumika kujikinga na mvua iliyokuwa inanyesha wakati wa mkutano wa CCM uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre wilaya ya Kigoma mjini.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye (wa kwanza kulia),Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kigoma Dk. Aman Walid Kaborou, Balozi Karume na Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Kanali Mstaafu Issa Machibya wakiwa wamesimama kwenye jukwaa kuu wakati wa mkutano wa hadhara bila kujali mvua kubwa iliyokuwa inanyesha.
Mbunge wa Kigoma mjini Mheshimiwa Peter Serukamba akiwahutubia wakazi wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre na kuwaambia kuwa Kigoma imebadilika na bado anapigania wananchi hao wapate maji salama na ya kutosha.
:
Mjumbe wa NEC Balozi Ali Abeid Karume akiwahutubia wakazi wa Kigoma mjini  na kuwaambia kuwa Muungano wa Serikali mbili ndio Muungano pekee utakaodumisha Umoja miongoni mwa wananchi.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia umati wa wakazi wa Kigoma mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre, ambapo aliwaambia kuwa vyama vya upinzani vinaelekea kutoweka mapema kabla hata havijakomaa kidemokrasia.
Upinde wa Mvua unaonekanika kabla mvua kubwa kunyesha kwenye viwanja vya Mwanga Community Centre ambapo mkutano mkubwa wa CCM ulikuwa unafanyika.

TASWIRA KUTOKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

0
0
Mhe. Mchungaji Peter Msigwa akiwasilisha maoni ya walio wachache katika Bunge la Katiba linaloendelea Mjini Dodoma.
Mhe. Andrew Chenge akisimama na kumfahamisha Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kuwa nakala anayosoma Mchungaji Peter Msigwa ni tofauti na nakala walizonazo wabunge.
Mchungaji Peter Msigwa akisisitiza kuwa anayosoma ni nakala halisi.
Muwakilishi wa Kamati namba nne Katika Bunge la Katiba,Dkt. Hamis Kigwangala akiwasilisha mapendekezpo ya kamati yake.
Mh. Agustino Mrema akijadiliana jambo na Mhe.Aggrey Mwanri.
Mh. Tundu Lissu akiwasilisha mapendekezo ya walio wachache kamati namba nne. 
Baadhi ya Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wakiwa wamesimama na kupiga kelele mara baada ya Dkt. Francis Michael kuanza kuwasilisha maoni katika kamati yake wakidai alikuwa anawasilisha ndivyo sivyo walivyoyatoa wao.Picha na Deusdedit Moshi.

Makamu Mwenyekiti TASWA alamba nondozz yake ya uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini

0
0
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Egbert Mkoko (katikati) akipongezwa na walimu wake, Profesa Larry sterilz (kushoto) na Profesa Lynnete sterilz, baada ya kutunukiwa shahada ya pili ya uandishi wa habari katika Chuo Kikuu cha Rhodes, Afrika Kusini juzi. (Picha kwa hisani ya TASWA).

170 Tourists from Israel arrives for National Parks expedition

0
0
A total of 170 tourists from Israel have arrived in the country today ready for a nine days visit in the country, which will take them through Arusha, Serengeti and Lake Manyara National Parks respectively. 

Speaking during the arrival of the tourists at Kilimanjaro International Airport, Ms. Ronit Hershkovitz who is the Managing Director of the Israel based Safari Company said that the Tanzanian tourist attractions are now becoming famous in Israel and hoping that the number of Israel tourists in the country will increase tremendously in the near future following intensive promotion campaign done by her Safari Company which is the main organizer of the tour.

Tourists visit by the Israelis in to Tanzania Tourist attractions is organized jointly by the Tanzania National Parks (TANAPA) and Menelik Safari Company of Israel following the agreement reached in 2012 whereby TANAPA will offer special incentive package to attract more tourists from Israel. 

While in the country, the Israel tourists will also spend time in the Ngorongoro Conservation Area as well as visiting the island of Zanzibar. Ms. Hershkovitz said that this is the second trip organized by her company the first one being held in November last year in the northern circuit tourist attractions. The tourists arrived directly at KIA from Tel Aviv through chartered Tel Aviv-based El Al Israel Airlines which will now be operating between the two countries on a monthly basis before engaging themselves into a regular flight schedules.

The Northern Tanzania tourist circuit is made up of Mount Kilimanjaro, Ngorongoro Crater, the famous Serengeti National Park, Tarangire National Park, Arusha National Park, and Lake Manyara National Park, famous for its rare tree-climbing lions.

Issued by Corporate Communications Department
Tanzania National Parks
12th April, 2014.
Israel National Airline Boeng 737-800 carrying 170 tourists arrive at Kilimanjaro International Airport.
Smiling tourists from Israel after landing at Kilimanjaro International Airport.

READ MORE PHOTOS HERE

ngoma azipendazo ankal

0
0

Leo tena Mtu mzima Santana anakuja tena na "Oye Como Va" spesho kwa wafuasi wa chacha

MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA KONGAMANO KWA WANAFUNZI WA KIKE WA VYUO VIKUU NA SEKONDARI HUKO DODOMA

0
0
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akipanda mti eneo la jengo la utawala wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakati alipotembelea chuoni hapo kwa ajili ya kufungua rasmi kongamano la Mustakabali wa mtoto wa kike katika mazingira ya sasa kwa wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu vilivyopo Dodoma na Morogoro. Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa Chimwaga tarehe 12.4.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikaribishwa ukumbini na wanafunzi wa kike waliojawa na furaha na hamasa kubwa.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akishiriki kucheza kwa nderemo na vifijo na wanafunzi wa kike wa vyuo vikuu mbalimbali vya Dodoma na Morogoro wimbo uitwao ..”wanawake na maendeleo..” mara baada kuingia ukumbini. Mama Salma alikuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa kongamano la mustakabali wa mtoto wa kike katika mazingira ya sasa.

NSSF yapongezwa kwa kuviunganisha Vyombo vya Habari nchini katika michezo

0
0
WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenella Mukangala amelipongeza Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) kwa kuviunganisha vyombo vya habari anuai nchini Tanzania kupitia tasnia ya michezo. 

Dk. Mukangala ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia kwa niaba ya waziri, alipokuwa akifunga rasmi Mashindani ya 11 ya NSSF yanayoshirikisha vyombo vya habari anuai katika mchezo wa mpira wa miguu na mpira wa pete kwa wasichana. 

 Dk. Mukangala alisema kwamba mashindano hayo yamekuwa yakivikutanisha vyombo anuai vya habari kutoka Tanzania Bara na Visiwani hivyo kujenga uhusiano mzuri kwa washiriki kupitia michezo, huku yakiimarisha uhusiano kati ya vyombo hivyo na shirika la NSSF ambalo hudhamini mashindano hayo kila mwaka kwa muda wa miaka 11 mfululizo hivi sasa. 

 "...Hakuna ubishi kwamba miaka 11 sio michache kwa kuendesha mashindano kama haya, lakini kwa sababu uongozi wa NSSF unaheshimu na kukubali nafasi ya vyombo vya habari katika kuelimisha jamii ni wazi kwamba mtaendelea kutenga bajeti ya mashindano haya kila mwaka," alisema Dk. Mukangala. 

 Aidha aliwapongeza washindi wa mwaka huu kwa jitihada na nidhamu ya mchezo waliozionesha hadi kufanikiwa kutwaa ushindi, hivyo kuwataka wanahabari wote kuendelea kuyatumia mashindano hayo kwa kujenga mahusiano mazuri na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii. 

 Mwaka huu timu ya Kampuni ya Bussnes Times Limited (BTL) imefanikiwa kutwaa kombe la mpira wa miguu na kuzawadiwa fedha shilingi milioni nne na nusu baada ya kuishindilia Changamoto mabao matatu kwa mtungi, nafasi ya pili ilichukuliwa na timu ya Changamoto na kujinyakulia kikombe pamoja na kitita cha shilingi milioni tatu na nusu. 

Mshindi wa tatu mpira wa miguu imeibuka timu ya wenyeji wa mashindano hayo NSSF baada ya kuifunga timu ya Mwananchi, hata hivyo NSSF walichukua kikombe na kusamehe kitita chao cha shilingi milioni 2 kilichokabidhiwa mshindi wa nne, yaani Timu ya Mwananchi. 

 Neema ya mashindano hayo mwaka huu iliiangukia kampuni ya BTL ambapo kwa upande wa mpira wa Pete pia timu ya wasichana ya kampuni hiyo ilifanikiwa kutwaa ubingwa na kukabidhiwa kombe na fedha shilingi milioni 4, nafasi ya mshindi wa pili imechukuliwa na timu ya Habari kutoka Zanzibar na kujinyakulia kiasi cha shilingi milioni tatu na nusu. 

Washindi wa tatu mpira wa pete imeibuka timu ya NSSF ambao walitwaa kombe bila fedha ambazo zilichukuliwa na mshindi wa nne (Mwananchi). Kikombe cha nidhamu kimenyakuliwa na timu ya Tumaini wamiliki wa Redio na TV Tumaini pamoja na gazeti la Tumaini Letu. 

Jumla ya timu 20 za mpira wa miguu na 18 za mpira wa pete zimeshiriki mashindano hayo kwa mwaka huu idadi ambayo inazidi kuongezeka kila mwaka tangu kuanza kwa mashindano hayo. 

 Hafla ya kufunga mashindano hayo iliyofanyika katika viwanja vya Sigara (TCC) jijini Dar es Salaam pia ilihudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NSSF, Abubakar Rajabu, Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Dk. Ramadhani Dau viongozi waandamizi wa shirika la NSSF pamoja na wageni mbalimbali waalikwa.
Nahodha wa timu ya mpira wa pete ya Business Times Limited akikabidhiwa kikombe mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa. 
Nahodha wa timu ya mpira wa pete ya Business Times Limited akikabidhiwa kikombe mara baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa.Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (mwenye traksuti nyeusi) akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa mpira wa miguu. Wengine ni viongozi wajuu wa NSSF wakishuhudia. 
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia (mwenye traksuti nyeusi) akikabidhi kikombe kwa nahodha wa timu ya mpira wa miguu ya Business Times Limited baada ya timu hiyo kuibuka mabingwa wa mpira wa miguu. Wengine ni viongozi wajuu wa NSSF wakishuhudia.


MATAYARISHO YA MATENGENEZO YA KUREJESHA MAWASILIANO YA BARABARA KATI YA DAR – BAGAMOYO YAENDELEA

0
0
Mawasiliano ya barabara kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo yamejifunga kutokana na barabara hiyo kubomolewa na maji katika Daraja la Mpiji mpakani mwa mikoa wa Dar es Salaam na Pwani.

Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alifanikiwa kufika katika eneo hilo mara tu baada ya kupokea taarifa za kukatika kwa barabara hiyo. Akiwa ameongozana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Mussa Iyombe pamoja na watendaji wengine kutoka TANROADS, Waziri Magufuli amewaagiza watendaji hao kuhakikisha kuwa wanafanyakazi mchana na usiku ili barabara hiyo muhimu na yeye kupitisha magari mengi ifunguliwe mapema iwezekanavyo.

Zaidi ya maelekezo hayo, Mhe. Magufuli pia ameagiza kuahirishwa hadi itakapopangwa baadaye kwa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa TANROADS ambalo lilikuwa limepangwa kufanyika kuanzia siku ya Jumanne ya tarehe 15 Aprili 2014 huko mkoani Tanga. Hatua hiyo imechukuliwa ili watendaji hao wabaki katika vituo vyao vya kazi hadi hali ya mvua zinazoendelea kutulia na taarifa nyingine kutolewa.

Akizungumzia hali katika eneo hilo la Mpiji, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Alhaj Mussa Iyombe kwa upande mwingine alibainisha kuwa kilichozolewa na maji ni sehemu ya barabara na siyo daraja lenyewe la Mpiji.

Mvua kubwa zinazoendelea kunyesha katika maeneo mbali mbali hapa nchini zimesababisha madhara kadhaa kwa upande wa miundombinu ya barabara. Waziri Magufuli ameendelea kutahadharisha kuhusu shughuli za uchimbaji wa mchanga zinazofanywa karibu au chini ya madaraja, kwamba kwa maeneo mengi ndicho chanzo cha mito kuhama kutoka katika njia yake ya asili na kubomoa barabara. “Kama manavyoona daraja lenyewe ni zima na linauwezo mkubwa wa kupitisha maji lakini mto umehama kutokana na uharibifu wa mazingira” alisistiza Mhe. Magufuli.

Daraja la Mpiji lilifunguliwa rasmi mwezi Julai 2005 na Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete wakati huo akiwa ni Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.

TANROADS kwa kushirikiana na kampuni za ujenzi za SKOL na Estim Construction Company Limited zote za Dar es Salaam tayari wameanza kazi za kurekebisha sehemu hiyo.
Sehemu ya barabara iliyoomole katika Daraja la Mpiji kwenye barabara ya Dar es Salaam Bagamoyo.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (katikati) akipokea maelezo kutoka kwa Katibu Mkuu wa Wiara ya Ujenzi Alhaj Mussa Iyombe (aliyenyoosha mkono). Kulia ni Mbunge Mteule wa Jimbo la Chalinze Mhe. Ridhiwani Kikwete.
Waziri wa Ujenzi Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli (mbele wa kwanza kulia) akiongozana na Viongozi wengine wakati walipotembelea kukagua sehemu ya barabara iliyobomoka katika barabara ya Dar – Bagamoyo. Wengine kutoka kushoto ni; (Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam) Suleiman Kova, (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam) Mhe. Said Mick saddik na (Mbunge Mteule wa Chalinze) Mhe. Ridhiwan Kikwete.
Sehemu ya barabara na daraja.

MRADI WA SECO WAZINDULIWA JIJINI ARUSHA

0
0
Mradi wa kuunganisha sekta za Wazalishaji matunda, mbogamboga na wenye hoteli (SECO) unaofadhiliwa na Serikali ya Switzerland umezinduliwa Jijini Arusha.

Mradi huo ambao lengo lake kuu ni kuboresha maisha ya watanzania wanaojihusisha na sekta hizo kwa kuongeza uzalishaji wao na uhakika wa masoko ya ndani nan je ya nchi, unaanza utekelezaji wake mara ,moja ukiwa na thamani ya jumla ya Dola za Ki marekani milioni tatu na nusu.

Uzinduzi wa Mradi huo umeshuhudiwa na Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dkt Mukhisa Kituyi, Balozi wa Uswizi nchini Tanzania BwOlivier Chave na Mkurugenzi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara katika Wizara ya Viwanda na Biashara Bw Lucas Saronga.
Katibu Mtendaji wa UNCTAD Dkt Mukhisa Kituyi (Kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Mtangamano wa Biashara wa Wizara ya Viwanda na Biashara Bw Lucas Saronga( Katikati) na Balozi wa Uswizi nchini Olivier Chave(Kulia) wakisaini hati za makubaliano ya utekelezaji mradi wa SECO.
Picha ya pamoja ya wafadhili na wawakilishi wa Serikali ya Tanzania walioshiriki uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika Jijini Arusha.
Picha ya pamoja ya Washiriki wote wa Mkutano na uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika mjini Arusha.
Baadhi ya Washiriki wa uzinduzi wa mradi wa SECO uliofanyika Jijini Arusha.

Ripoti Ya Kamati Namba 4 iliyowasilishwa Bungeni na Dkt. Hamis Kigwangalla

0
0
Mh. Dkt. Hamis Kigwangalla

Rai ya Mdau hukusu Katiba

HOFU YA KUTOKEA MAFURIKO,WAKAZI WA KATA YA MABOGINI-KILIMANJARO WAITANA MSARAGAMBO KUZIBA MAPITIO YA MAJI

0
0
Wakazi wa Kitongoji cha Bogini wakiwa wamejitikeza kwenye Msaragambo kwa ajili ya kuchimba na kufukia kwa vifusi maeneo ambayo ni mapitio ya maji kwenda kwenye makazi ya watu.
Wakazi wa kata ya Mabogini wakiwa katika Msaragambo.
Shughuli ya kuziba maeneo korofi iliendelea.
Hata wale wasio na vitendea kazi walilazimika kutumia mikono kufanya shughuli hiyo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA
Viewing all 109589 articles
Browse latest View live




Latest Images