Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 416 | 417 | (Page 418) | 419 | 420 | .... | 3285 | newer

  0 0  0 0
 • 04/10/14--15:20: KALI TV THIS WEEK
 • This week, Kali TV brings you the 20th commemoration of the genocide against the tutsi in Washington DC. The powerful and emotional event featured speakers from different parts of the world and the testimonies from survivors of the genocide. Enjoy!

  0 0
 • 04/10/14--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • Sikiliza na soma tafsiri ya ngoma ya "Mario2 ya Madilu System akiwa na Franco Luambo Lwanzo Makiadi

  0 0


  Sisi watanzania wa Washington DC, Maryland na Virginia pamoja na vizazi vyetu tunapenda kutoa pongezi kwa Serikali yetu ya Tanzania kwa Mchakato mzima wa Katiba mpya unaoendelea.


  Tunapenda Kutoa Tamko Rasmi kwa Bunge la Katiba na Serikali kutoa haki ya Uraia kwa Watanzania Wote popote walipo Duniani. Uraia Wa Mtanzania aliezaliwa Tanzania na Kizazi chake usijali hali na mahala alipo Mtanzania Huyo.


  Kutokubaguliwa kwetu kwenye swala hili la Haki ya Kuzaliwa na Kuruhusiwa kwa Uraia Pacha kwa Waliozaliwa Tanzania na Vizazi vyao ni muhimu katika kuimarisha nchi, kutoa haki kwa Watanzania wote waliozaliwa Tanzania pamoja na vizazi vyao. Haki ya kuzaliwa  kwa watanzania wote kutaimarisha Zaidi mahusiano kati ya watanzania tulio nje na serikali yetu tukufu.


  Watanzania Hapa Washington, DC na tulio nje tumekuwa mbele kuitangaza nchi yetu, kuiwakilisha nchi yetu na kuibeba Bendera ya Tanzaniahuku nje . Watanzania tumekuwa tukishirikiana na Viongozi wa nchi yetu wanapokuja huku nje kwenye mambo mbalimbali ya kimaendeleo, kijamii na kielimu ili kuhakikisha nchi yetu inasonga mbele.


  Watoto wetu waliozaliwa huku nje wamekuwa wakiimba nyimbo ya Taifa la Tanzania wanapokuja viongozi mbali mbali huku na kwenye shughuli mbali mbali za kitaifa na kimataifa ambazo huwa tunaiwakilisha nchi yetu huku ugenini. 


  Watanzania wenye uraia wa Tanzania na Wale waliochukua Urai wa Hapa , pamoja na watoto wao waliozaliwa hapa ambao ni Wamarekani kwa kuzaliwa tunajisikia na tunaipenda Tanzania kama wenzetu walioko Marangu au Kimanzichana. Tofauti iliyopo ni kwamba sisi tuko huku na wenzetu wako Biharamulo. Watoto wetu wamezaliwa hapa na Binamu zao wamezaliwa Chalinze.  Sisi sote na watoto wetu ni watanzania na tunataka tutambulike na kuwa na haki sawa.


  Watanzania wa Washington DC, tumekuwa tukishirikiana kwa hali na mali na Ubalozi wa Hapa  kuitanganza nchi yetu na kuitetea na kuiletea sifa nzuri Tanzania. Hivi Sasa Ubalozi wetu hapa Unaandaa sherehe za Miaka 50 ya Muungano na Ni sisi Watanzania wa Ughaibuni tutashiriki kwa Moyo Mmoja na nguvu zote kuipeperusha bendera ya Tanzania kwa niaba ya nchi nzima. Watato wetu wataonyesha utamu wa nyimbo ya Taifa la Tanzania. Viongozi wa Taifa watazungumza na watanzania wa hapa na kujadili maendelea na muelekeo wanchi.     Sisi Ni Watanzania.  TanzaniaItajengwa Na Watanzania. Sisi Na Vizazi Vyetu Huku Ughaibuni ni Watanzania.


  Iddi Sandaly,


  Rais Wa Jumuiya Ya Watanzania , 
  WashingtonDC, Marylandna Virginia.


  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM,Kinana akiwa na viongozi wengene wakiangalia jinsi watanzania wanavyopata taabu na kunusurika kifo kwa kuvuka kwenye Mto Malagalasi wakitokea kuuza bidhaa zao na kununua mahitaji mengine katika Soko Buhinja, Kijiji cha Mrambi, Mkoa wa Makamba nchini Burundi. Wananchi hao kutoka Kijiji cha Kibande na vijiji viongine wilayani Buhigwe, Kigoma Tanzania, huenda Burundi kufanya biashara kutokana na upande wa Tanzania kutokuwepo na soko kunakosababishwa na kodi nyingi.
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akiangalia mto Malagalasi ambao ni mpaka wa Tanzania na Burundi, alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma,Kinana yupo katika ziara ya siku 5 mkoani humo ya kuimarisha uhai wa chama na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM.
   Hizi ni baadhi ya picha zinazoonesha jinsi wananchi wa Tanzania wakivuka mto huo na wengine kuvushwa kwa malipo, wakirudi Tanzania baada ya kufanya biashara upande wa Burundi. 
   Watu wote hao wakisubiri kuvushwa kwenye mto huo Malagalasi,kwa kimtumbwi kimoja ama kubebwa kama baadhi ya picha zinavyoonyesha
  Baadhi ya Wanahabari pichani Kulia Bakari Kimwanga kutoka gazeti la Mtanzania na Bwana Jongo kutoka gazeti la Uhuru wakionja joto ya kuvushwa kwenye mto wa Malagalasi ambao ndio sehemu ya mpaka kati ya Burundi na Tanzania.Kuonja adha hiyo hulipia kiasi cha fedha shilingi 500 mpaka 1000 kama nauli.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo kwa msisitizo na Mkurugenzi wa Maendeleo wa Halmashauri ya Buhigwe,Kaondo Julius walipokwenda kukagua  mpaka wa Tanzania na Burundi alipokuwa katika ziara wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.
  Msanii wa kikundi cha ngoma za utamaduni kutoka Burundi wakitumbuiza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Uwanja wa Kibande, Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.
  Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa chama cha CNDD-FDD,Mkoa wa Makamba nchini  Burundi,Bwa.Nishimwe Zen,kabla ya mkutano wa hadhara kufanyika katika kijiji cha Kibande,wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.

  0 0
 • 04/10/14--23:44: Article 22


 • 0 0

  Diwani wa Kata ya Endiamtu, Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Zacharia akiwahamasisha wakazi wa kitongoji cha Kilimahewa kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF) baada ya diwani huyo kuwachangia sh 500,000 za kaya 50 za kata hiyo.

  Ili kuwahamasisha wananchi wajiunge na mfuko wa afya ya jamii (CHF) Diwani wa Kata ya Endiamtu Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Lucas Zacharia amelipia sh500,000 za gharama za matibabu, kwa kaya 50 za watu 300 wa kata hiyo.

  Akizungumza jana kwenye mkutano wa kitongoji cha Kilimahewa kilichopo katika kata hiyo, Zacharia alisema wananchi wengi wakijiunga na CHF, dawa na vifaa tiba vitapatikana kwa wingi kwenye kituo cha afya Mirerani.

  Alisema kaya moja yenye baba, mama na watoto wanne wakichangia sh10,000 wanatibiwa kwa mwaka mmoja katika zahanati, kituo cha afya na hospitali kwenye wilaya husika hivyo jamii inatakiwa ichangamkie fursa hiyo.

  “Ndugu zangu, maendeleo yetu Endiamtu kwa pamoja tunaweza, hivyo tujiunge kwa wingi kwenye mfuko huu ambapo watu wengi tukijiunga Serikali inatuunga mkono nusu kwa nusu na kuboresha kituo chetu cha afya,” alisema Zacharia.

  Alisema endapo wananchi wakiweza kuchangia sh5 milioni kwenye mfuko huo, Serikali nayo inachangia sh5 milioni na wakichangia sh10 milioni, Serikali pia itachangia kiasi kama hicho hivyo mpango huo unamanufaa makubwa.

  Hata hivyo, ili kumuunga mkono Diwani huyo, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kilimahewa, Joseph Masasi naye alijitolea sh100,000 kwa kaya 10 zenye baba, mama na watoto wanne wa kitongoji hicho, watakaotibiwa na mfuko wa CHF.

  “Tunashukuru sana na tunampongeza diwani wetu Zacharia, ambaye ni mtu watu kwani kwa roho moja amejitolea sh500,000 kwa ajili ya kuwalipia watu wasio na uwezo wakiwemo wajane na yatima,” alisema Masasi.

  0 0

  KARIBUNI WOTE

  Kama mnavyofahamu kuwa siku ya tarehe 26 Aprili, 2014 Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatimiza miaka hamsini (50), kwa lugha nyingine ni “Golden Jubilee”.

  Katika kuadhimisha sherehe hii kubwa na muhimu, Ubalozi umeamua kuandaa Kongamano la Biashara (Investment Forum) kwa siku ya tarehe 25 Aprili, 2014 pamoja na siku ya terehe 26 Aprili, 2014 kuwa siku ya mdahalo (Scholars' day) mjini Berlin, Ujerumani. 

  Madhumuni makubwa ya Kongamano hili ni kuwatangazia na kuwaonyesha umma wa Wajerumani mafanikio mbalimbali yaliopatikana ndani ya muungano wetu kwa kuwaonyesha fursa tulizonazo za biashara katika nyanja za kilimo, utalii, nishati na madani, viwanda, elimu n.k.

  Hivyo, Mhe. Philip S. Marmo, Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani ana wakaribisha Watanzania wote wanaoishi nchini Ujerumani na wale wanaoishi kwenye maeneo ya uwakilishi ya Ubalozi kuja kushiriki kwenye Kongamano la Biashara siku ya tarehe 25 Aprili, 2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi hadi saa 11:00 jioni kwenye ukumbi wa Logenhaus, Emser Str.12-13, 10719 Berlin, Ujerumani.

  Aidha, Mhe. Balozi ana wakaribisha pia kwenye mdahalo siku ya tarehe 26 Aprili, 2014 kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana kwenye ukumbi wa Deutsche Bank, Unter den Linden 13-15, 10117 Berlin, Ujerumani.

  Kwa maeleozo zaidi piga simu:

  +49303030800

  ASANTENI SANA!

  0 0

  Afisa Uhusiano wa Airtel Jane Matinde akionyesha simu ya Aina ya Samsung S5 mara baada ya kuzindua ofa itakayowawezesha wateja wake kununua simu hityo na kujipatia vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.

  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel leo imetangaza ofa kabambe inayowawezesha wateja wake kununua simu ya kisasa ya aina Samsung S5 na kupata vifurushi vya muda wa maongezi, sms pamoja na data bure.

  Akiongea wakati wa kutangaza ofa hiyo Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema” leo tunayofuraha kuwatangazia wateja wetu ofa kabambe ambayo inawawezesha kununua simu ya Samsung S5 na kupata dakika 1500 bure , SMS 5000 kutuma mitandao yote pamoja na kifurushi cha internet cha 3GB kitakachomwenzesha wateja wetu kuperuzi katika mitandao kama vile facebook na twitter kupitia huduma yetu ya internet ya 3.75G yenye kasi zaidi. 

  Vifurushi hizi vitadumu kwa muda wa mwenzi mmoja kuanzia tarehe ambayo mteja atafanya manunuzi ya simu ya Samsaung S5”.

  Simu hii ya Samsung S5 inapatikana katika maduka ya Airtel yaliyopo Moroco, Mlimanicity, Jmall pamoja na maduka yote ya Samsung pamoja na maduka yanayouza simu za smart phones yaliyoko nchi nzima.

  Tunachukua nafasi hii kuwahimiza watanzania kuwa wakwanza kuchangamkia ofa hii” aliongeza Jane Matinde

  0 0


  0 0

  Mwenyekiti mwenza wa Kamati Kuu ya Taifa ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikiendesha Kikao cha Kamati hiyo kilichokutana katika Ukumbi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa { TAMISEMI } Mjini Dodoma.
  Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambao ni Wajumbe wa KamatiI Kuu ya Taifa ya Sensa Tanzania wakiendelea na Kikao chao Mjini Dodoma. Kutoka Kulia ni Waziri wa Habari M,h. Said Ali Mbarouk, Waziri wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Mh. Zainab Mohd, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omar KLheir pamoja na Waziri wa Nchi Ofiisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Mwinyihaji Makame.
  Baadhi ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Sensa kutoka Kushoto ni Kamishna wa Sensa Tanzania Bara Hajat Amina Mrisho Naibu Waziri wa Fedha wa Serikali ya Muungano wa Tanzania Mh. Muigulu Nchemba na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Dr. Florens Turuka.
  Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu Tanzania Dr. Alina Chua akitoa Taarifa fupi juu ya uhakiki wa mipaka kwa baadhi ya Wilaya Nchini Tanzania. Kulia ya Dr. Alibina Chua ni Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Nd. Mohd Hafidh. Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  0 0

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipata maelezo kutoka kwa watoto wa Marehemu Edward Sokoine aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania, Namelok Sokoine (MB) na Joseph Sokoine ambaye ni Afisa katika Ubalozi wa Tanzania nchini Canada, kuhusiana na maandalizi ya maadhimisho ya miaka 30 ya kifo cha aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli,Marehemu Edward Moringe Sokoine, yatakayoadhimishwa kesho April 12. Rais Jakaya Kikwete ataongoza maadhimisho hayo pamoja na marais na mawaziri wakuu wastaafu.
  Kaburi la aliyekuwa Waziri Mkuu na Mbunge wa Monduli,Marehemu Edward Moringe Sokoine.

  0 0


  0 0

  Mwandishi wa kitabu kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji ya hapa Tanzania yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa.Bi. Neema Lugangilra Apson akielezea maudhui ya Kitabu chake kwa wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kitabu chake jana usiku jijini Dar es Salaam. 
  Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kitabu kinachoeleza namna watanzania na makampuni ya usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa. Kulia ni mwandishi wa kitabu hicho Bi. Neema Lugangilra Apson.
  Bi. Neema Lugangilra Apson akionesha kitabu chake kinachoitwa “Local Content in Supplier Development” kinachoelezea namna watanzania na makampuni ya usambazaji yanavyoweza kushiriki, kuwezeshwa na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa.
  Mgeni Rasmi Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu kinachoelezea namna watanzania wanavyoweza kushiriki na kunufaika na sekta ya nishati ya gesi asilia hapa nchini. Kulia ni mwandishi wa kitabu hicho Bi. Neema Lugangilra Apson.


  0 0

  Meneja wa kanda ya Dar es salaam NMB, Bw. Salie Mlay akikabidhi kompyuta kwa Afisa elimu manispaa ya Temeke Bi. Honorina Mumba kwa ajili ya kituo cha walimu wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam. Msaada huu wa kompyuta mbili pamoja na mashine ya kuchapisha karatasi (Printer) vimetolewa na benki ya NMB kwa ajili ya mafunzo yanayotolewa kwa walimu katika wilaya hii.Hafla ya makabidhiano ilifanyika juzi jijini Dar es salaam. Akishuhudia makabidhiano hayo ni Mkuu wa kituo hicho cha walimu Temeke Bw.Daniel Matembele.
  Meneja wa tawi la NMB Temeke Bw.Harold Lambileki akimkabidhi sehemu ya Kompyuta Mkuu wa kituo cha walimu Temeke Bw.Daniel Matembele. Msaada huu wa kompyuta mbili Pamoja na mashine ya kuchapisha karatasi (Printer) vimetolewa na benki ya NMB kwa ajili ya mafunzo yanayotolewa kwa walimu katika wilaya hii.

  0 0

  Gavana wa Shirika la Lions Club nchini Bwana Wilson Ndesanjo akimvika Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete medali maalum ya Uongozi Bora na mahusiano mema wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Bwana Ndesanjo alisema klabu hiyo imeamua kumtunuku Rais Kikwete medali hiyo kwa kutambua mafanikio makubwa yaliyopatikana nchini katika Nyanja mbalimbali kutokana na uongozi wake mahiri.
  Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mkono na Gavana wa Shirika la Lions Club nchini Bwana Wilson Ndesanjo mara baada ya kuvalishwa medali maalum ya Uongozi Bora na mahusiano mema wakati wa hafla fupi iliyofanyika ikulu jijini Dar es Salaam leo
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa klabu ya Lions waliofika ikulu jijini Dar es Salaam leo kushiriki hafla ya kumtunuku Rais Kikwete medali maalumu ya Uongozi Bora na Mahusiano mema.(picha na Freddy Maro)

  0 0

  Mwenyekiti wa Kamati namba 1,Mh. Ummy Ally Mwalimu akiwasilisha mapendekezo ya kamati yake leo wakati wa muendelezo wa vikao vya Bunge la Katiba vinavyoendelea mjini Dodoma.
  Baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba wakiwa wamesimama kwa nyakati tofauti tofauti wakimkatiza Mwenyekiti wa Kamati namba 1,Mh. Ummy Mwalimu wakimtaka Mwenyekiti wa Bunge amtake Ummy Mwalim kusoma mapendekezo ya kamati badala ya kuwasilisha kwa mfumo wa kutosoma.


  0 0

  Katika siku za hivi karibuni, huko mkoani Mara wilaya ya Butiama kumejitokeza matukio ya mauaji yanayowalenga hasa akina mama wawapo katika shughuli zao mbalimbali. 

  Kufuatia matukio hayo, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu ametuma timu maalum ya wataamu itakayoongozwa na  Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai nchini, DCI Issaya Mngulu kwenda mkoani humo kuongeza nguvu kwa kushirikiana na wataalam wa mkoa huo, ili kuhakikisha kwamba wote wanaojihusisha na vitendo hivyo wanakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria haraka. 

  Jeshi la Polisi linawashukuru wananchi wanaoendelea kutoa  ushirikiano utakaosaidia watuhumiwa hao kuendelea kukamatwa na linatoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mara na maeneo ya jirani kuwa watulivu wakati upelelezi ukiendelea. 

  Aidha, Jeshi la Polisi nchini linawaomba wananchi wenye taarifa  za wahalifu hao kutoa taarifa hizo kupitia namba za simu zifuatayo; 0715 009930,  0754 785557 au katika kituo chochote cha Polisi.
  Imetolewa na:
  Advera Senso -SSP
  Msemaji wa jeshi la Polisi.

  0 0

  Balozi wa Tanzania Ubelgiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiwa katika picha ya pamoja na Mwakilishi wa Wadau wa Sekta ya Reli Ubelgiji Bwana. Jacques Delaunoit baada ya kumaliza kikao cha kuandaa Kongamano la Uwekezaji katika katika sekta ya Reli Tanzania. Kongamano hilo litafanyika Ubelgiji mwezi Mei, 2014.

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha Balozi wa Canada nchini,Mh. Alexandre Leveque ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika mazungumzo na Balozi wa Canada nchini,Mh.Alexandre Leveque ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mwenyekiti wa SAGCOT Fund Balozi Ami Mpungwe baada ya kufanya naye mazungumzo ikulu jijini Dar es Salam leo.(picha na Freddy Maro).

older | 1 | .... | 416 | 417 | (Page 418) | 419 | 420 | .... | 3285 | newer