Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 415 | 416 | (Page 417) | 418 | 419 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Rais Paul Kagame wa Rwanda akimkaribisha Katibu Mkuu wa CCM, Ndugu Abdulrahman Kinana katika mazungumzo yaliyofanyika katika Hoteli ya Serena, Mjini Kigali Rwanda, juzi. 
  Picha na Edward J. Mpogolo, 
  wa ofisi ya Katibu Mkuu wa CCM

  0 0
 • 04/10/14--02:17: KUMBUKUMBU
 • BERNARD THOMAS NDERUMAKI

  Ni mwaka mmoja umepita tangu mungu alipokuchukua mnamo tarehe 10 Aprili, 2013. Si rahisi kumpata mbadala wako, kwani ulikuwa Mume, Baba, Babu, Mwalimu, Rafiki na zaidi ya yote mtu mwenye upendo wa kweli kwa jamii. Kumbukumbu zako hazitakaa zitutoke kirahisi, na tutakua tukikukumbuka milele. Pumzika kwa amani.

  Misa ya kumbukumbu itafanyika Kilema Moshi siku ya Jumamosi tarehe 26 Aprili, 2014, saa 7 Mchana.

  Wote mnakaribishwa.

  0 0

  Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel Wakwanza kutoka kushoto akitoa mada katika Kongamano la Sita la Kigoda cha Mwalimu Nyerere linaloendelea kwenye Ukumbi wa Nkurumah wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

  0 0

  Oparesheni Nzito ya kuzuia Bodaboda na Bajaji zisifanye safari zake  kutoka Mwenge na maeneo mengine kuelekea mjini Posta imechukua sura mpya leo baada ya Askari wa Usalama wa Barabarani kuanza kukamata Bodaboda na Bajaji zote zinazovuka Mwenge kuelekea Posta, Zoezi hilo ambalo limefanyika Mwenge Mataa Jijini Dar limeendelea kufanyika na kufamikiwa kuwanasa wengi.

  Kwa mujibu wa Msemaji na Muongozaji wa Oparesheni hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina lake alisema kwamba wameamua kufanya hivyo ili kuzuia Msongamano wa Magari pamoja na bodaboda pia Bajaji kuelekea Mjini Posta, Aliongeza kuwa kumekuwa na uhalifu sana wa Silaha unaotumiwa na bodaboda hasa maeneo ya mjini hivyo ndio maana wameamua kuzuia.

  "Tumefanya hivi ili kuepusha msongamano kuelekea Posta, lakini pia kumekuwa na uhalifu sana unaotumiwa kwa njia ya Bodaboda hivyo tunafanya oparesheni hii ili kupunguza tatizo hili. Tulicho kifanya tumewaruhusu kufanya safari pembezoni mwa mji tuu hivyo Eneo la Mwenge kwa sasa Limeingia katika zone ya eneo la Mjini,Kama tuliweza kuzuia Daladala ndogo"Hiace" pia na hawa watakuja kuelewa ingawa ni zoezi gumu na linalo hitaji elimu ya ziada ambayo tumesha anza kuwapa na tunaendelea kuwapa"  alimalizia kwa kusema "Pia hii ni Oparesheni ya kawaida tuu ya kukamata wale ambao hawana Leseni za kuendesha vyombo hivi pamoja na makosa mbalimbali" alisema Polisi huyo.

  Kwa mujibu wa madereva wa Bodaboda na Bajaji wamesema kwamba huo ni uonevu kuwakataza wao wasiweze kwenda Mjini kwani na wao wanatafuta ridhiki yao na wameomba Serikali iwasaidie wapatiwe njia mbadala ya wao kwenda maeneo hayo. 

  Wanao ruhusiwa kwenda Posta na Bajaji au Bodaboda ni wale ambao ni wamiliki binafsi na wanatakiwa wapite njia hizo wakiwa Bila abiria yoyote.

   Oparesheni Kamata Bodaboda na Bajaji ikiwa inaendelea upande wa Mwenge mataa ambapo Bajaji nyingi zimekamatwa
   Askari wa Usalama wa Barabarani akiwa anawaandikisha Baadhi ya Bodaboda na Bajaji wenye makosa mbalimbali ili waweze kulipia tozo pamoja na kupelekwa kituo cha Polisi.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0

  Wajumbe wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) wakiendelea na Mkutano huo leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.Mkutnao huo umefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Peter Ilomo (katikati mwenye tai nyekundu).
  Katibu Mkuu Ofisi ya Rais,Peter Ilomo akizungumza wakati wa kufungua Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA),Irene Isaka (kushoto) akizungumza kwenye Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

  Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko,Mitaji na Dhamana (CMSA),Nasama Masinda akieleza jambo wakati Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA) unaofanyika leo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

  Mwenyekiti wa Mkutano wa 32 wa Sekta ya Fedha, Soko la Mitaji na Mifuko ya Jamii kwa nchi wanachama wa SADC (CISNA),Oaitse Ramasedi (wa tatu kushoto) akiongoma Mkutano huo unaoendelea kufanyika hivi sasa kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya White Sands jijini Dar es Salaam.

  BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI

  0 0

  Mhe.Sada Salum(Mb.) (katikati) Waziri wa Fedha na Uchumi awasili Washington DC kuongoza ujumbe wa Tanzania katika mikutano ya Benki ya Dunia na Shirika la Fedha Duniani (IMF) Pichani ni Bw.Paul Mwafongo (kulia)na Bw.Suleiman Saleh (kulia)Maofisa wa Ubalozi wa Tanzania Washington DC

  0 0

   AMREF, the leading international African organisation in health today rebranded to Amref Health Africa after 57 years as the African Medical and Research Foundation. 

  A key reason for the rebrand is to ensure that our name more accurately reflects the nature and scope of our work, which has grown beyond research and provision of basic medical services to strengthening of health systems through training and capacity building and strategic programming in areas such as maternal and child health, HIV, Water and Sanitation, TB and Malaria, and clinical and diagnostics services. 

   “Our new name exemplifies our commitment to improving health in Africa through a wide a range of critical programmes and services so that we can achieve lasting health change for the people of Kenya and Africa in general,” said Director General Dr Teguest Guerma.

  Although we are rebranding, our focus remains the same:  communities continue to be the primary beneficiaries of our work. Our rebrand will in effect put us in a more strategic position to continue working with our partners and aligning ourselves as an African-led and Africa-based health organisation seeking to meet the needs of the most vulnerable populations on the continent.

  Since 1957, Amref Health Africa has been providing health services to the most vulnerable communities, working in partnership with a cross-section of stakeholders including governments. With seven offices in Africa and 10 in Europe and North America, Amref Health Africa reaches over 30 countries with its work and has impacted the lives of millions of people living in hard-to-reach parts of Africa.


  0 0

  Mwenyekiti wa chama cha mpira wa Miguu Mkoa wa Kagera (KRFA) Jamal Emil Malinzi amewasili leo Alhamis tarehe 10-4-2014 saa nne asubuhi katika Uwanja wa ndege wa Bukoba Mjini na kupokelewa na Wadau wengi, Huku ikiwa ni mara ya kwanza tangu achaguliwe Rais wa TFF. 
  Bw. Jamal Malinzi baada ya kutua amezungumza na Viongozi wa Soka Mkoani hapa Kagera na baadae kuhudhulia Kikao cha kamati Tendaji ya KRFA na siku inayofuata utakuwepo mkutano mkuu wa KRFA.
  Kulia ni Bw. Pelegrinius .A. Rutayuga, Mjumbe wa kamati Tendaji ya KRFA , Mjumbe wa mkutano mkuu wa TFF na Mshauri Mkuu wa Kiufundi TFF makao makuu, nae alikuwepo Uwanja wa Ndege Bukoba kwa mapokezi ya Rais wa TFF Ndugu Jamal Malinzi. Na hapa wakiteta jambo kwa kushirikishana na wadau pamoja na Viongozi.
  Rais wa shirikisho la Mpira wa miguu nchini TFF Ndugu Jamal Malinzi (kulia) akizungungumza na baadhi ya Viongozi wa Soka na wadau waliojitokeza kumpokea leo kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo. Kushoto ni Bw. Salum Chama Katibu wa KRFA Kagera, Anayefuata ni Bw. Ndg Ruge Masabala
  Kushoto ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) Jamal Emil Malinzi kwenye picha na Mwandishi wa Mtandao wa Jamii Bukobasports.com leo muda mchache alipotua kwenye Uwanja wa Ndege mjini Bukoba leo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Mwakilishi wa walio wachache  katika kamati namba tano, Mhe.David Kafulila akiwasilisha mapendekezo ya walio wachache katika kamati yake
  na Deusdedit Moshi
   Mwakilishi wa walio wachache  katika kamati namba tano,Mhe.David Kafulila katikati akishangiliwa na baadhi ya wajumbe baada ya kuwasilisha mapendekezo ya walio wachache katika kamati yake Picha na na Deusdedit Moshi
   Mwakilishi wa waliowachache  katika kamati namba tano,Mhe.David Kafulila katikati akishangiliwa na baadhi ya wajumbe baada ya kuwasilisha mapendekezo yao  


  0 0

  Baadhi ya mitandao ya habari ya kijamii zimekuwepo habari zilizonukuliwa zikitoa taarifa kuwa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limetangaza nafasi za ajira kwa Wahifadhi Wanyamapori madaraja ya pili na tatu.

  Shirika la Hifadhi za Taifa linapenda kutoa ufafanuzi kuwa nafasi hizo zilizotangazwa sio za Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) bali ni ajira zilizotangazwa na Serikali Kuu kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma – Ofisi ya Rais na ambako kimsingi maombi ya nafasi hizo ndiko yanakopaswa kupelekwa.


  Imetolewa na Idara ya Mawasiliano

  Hifadhi za Taifa Tanzania


  10.04.2014


  0 0

   Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe.Juma Nkamia akiongea na baadaye kupiga picha ya pamoja na warembo washiriki wa shindano la kumtafuta REDD'S MISS UDOM 2014 Yatakayo fanyika mjini Dodoma katika Ukumbi wa Kilimani Landmark Tarehe 11/04/2014 na kusindikizwa na burudani kutoka Bendi ya Twanga Pepeta
  Na Deusdedit moshi


  0 0
 • 04/10/14--08:15: Article 12


 • 0 0

  Na Mohammed Mhina, 
  wa Jeshi la Polisi- Zanzibar
  Makachero wa Jeshi la Polisi Zanzibar, wamefanikiwa kuzikamata silaha mbili na risasi 40 za Kivita zinazosadikiwa kutumika katika matukio mbalimbali ya kihalifu likiwemo la mauaji ya Askari Polisi mmoja lililotokea Machi 2, mwaka huu huko kwenye Hoteli ya Kitalii ya Pongwe Bay mkoa wa Kusini Unguja Zanzibar. 
  Katika tukio hilo Askari Polisi mmoja mwenye namba F.5607 Koplo Mohammed Mjombo(44) aliuawa huku mwenzake mwingine mwenye namba F.6198 Konstebo Ibrahim Juma Mohammed(35) akijeruhiwa vibaya kwa risasi kabla ya kuporwa silaha aliyokuwa nayo. Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake, Mkurugenzi wa Upelelezi Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, amesema kuwa pamoja na kukamatwa kwa silaha hizo pia Makachero hao wamewatia nguvuni majambazi watatu kati ya wanne waliohusika katika tukio hilo la mauaji ya Askari Polisi. 
  Alisema silaha hizo zilikamatwa nyumbani kwa mmoja wa watuhumiwa anayeishi eneo la Mkokotoni katika mkoa wa Kaskazini Unguja zikiwa zimefungwa na vipande vya plastiki na vitambaa na kuviringishwa katika waya mpya wa kupigilia madirisha. 
  Bila ya kuwataja majina yao kwa sababu za kiupelelezi, DCI Ilembo ameainisha wazi kuwa baadhi ya watuhumiwa hao ni wenyeji wa Pangani mkoani Tanga na wengine ni wenyeji wa Kisiwa cha Pemba Zanzibar. 
  Amesema katika mahojiano na makachero wa Polisi, Majambazi hayo pia yalikiri kuhusika na matukio mbalimbali katika mikoa ya Viisiwani na Mikoa ya Tanzania Bara matukio ambayo yangali yakichunguzwa katika Vituo mbalimbali vya Polisi. 
  Watuhumiwa hao pia walipatikana na vitu mbalimbali zikiwemo fedha taslimu shilingi 490,000 za Kitanzania, dolla 75 za Kimarekani, Euro na fedha kadhaa za Kichina pamoja na vitu mbalimbali zikiwemo simu za mkononi. 
  Amesema bado Jeshi la Polisi linaendelea kuwahoji watuhumiwa hao ili kuweza kuipata silaha ya Polisi aina ya SMG ambayo waliiporwa kutoka kwa Askari wakati walipowavamia na kuwashambuliwa kwa risasi. 
   SACP Ilembo ameshukuru kuwa kukamatwa kwa silaha hizo pamoja na watuhumiwa, kumetokana na taarifa za siri za Raia wema zilizotolewa Polisi na kupelekea kufanyiwa kazi na kuleta mafanikio hayo. 
  Amewaomba wananchi katika maeneo mbalimbali kuendelea kushirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa za siri zitakazowafichua watuhumiwa wakiwemo waliofanya na wanaotarajia kufanya makosa ili waweze kufuatiliwa na kukamtwa na kufikishwa mahakamani kwa hatua zaidi.
   Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, akizungumza na Waandishiwa Habari juu ya kukamatwa kwa majambazi wakiwa na silaha mbili ikiwemo SMG moja na Bastola moja zikiwa na jumla ya risasi 40.
   Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, akionyesha silaha zilizokamatwa na Makachero wa Jeshi la Polisi Zanzibar kutoka kwa watuhumiwa wa Ujambazi wa kutumia silaha.
   Baadhi ya Waandishi wa Habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, wakati akitoa taarifa za kukamatwa kwa watuhumiwa pamoja na silaha.
   Silaha na baadhi ya vifaa vilivyokamatwa kutoka kwa watuhumiwa hao wa ujambazi 
  Baadhi ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai Zanzibar SACP Yusufu Ilembo, wakati akitoa taarifa za kukamatwa kwa silaha pamoja na Watuhumiwa wa Ujambazi

  0 0

   Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba akiongea na Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia. Twissa na Mworia walitembeela vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group katika ziara ya akwaida ya kuimarisha uhusiano.
   Muongoza Matangazo wa kituo cha Radio Clouds na Clouds TV Barnabas Madili akionyesha namna kazi ya kuongoza matangazo inavyofanyika wakati Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa(wa kwanza kushoto) na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia walipotembelea vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group. Wa tatu kushoto ni  Mkurugenzi wa Uzalishaji na Vipindi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.
   Waendeshaji wa kipindi cha Morning Choice kinachorushwa na kituo cha Radio cha Choice FM Baby Kabai (kulia) na Evans Bukuku wakionesha manjonjo kwa Mkuu wa Masoko wa Vodacom Kelvin Twissa na Mkuu wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Rosalynn Mworia (hawapo pichani) walipotembelea vyombo vya habari vilivyo chini ya Clouds Media Group. 
   
   Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Corporation Hussein Bashe(kulia)akiwaonesha Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia(katikati) na Meneja Uhusiano  kwa Umma wa Kampuni hiyo Matina Nkurlu moja ya magazeti yanayochapishwa na kampuni yake wakati maofisa hao walipotembelea ofisi za Magzeti ya Mtanzania zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kukuza uhusiano miongoni mwa kampuni hizo.Wa kwanza kulia ni Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Mtanzania  Dennis Msacky.
  Mkuu wa Idara ya Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania Rosalynn Mworia  (katikati) na Meneja Uhusiano  kwa Umma wa kampuni hiyo Matina Nkurlu  wakimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi  Mtendaji wa New Habari Corporation Hussein Bashe( kulia) akiwalezea mfumo wa uchapaji magazeti. Maofisa hao wa Vodacom walitembelea ofisi za New Habari Corporation zilizopo Sinza jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kukuza uhusiano kati ya kampuni hizo.

  0 0  0 0  0 0

   Mchungaji Peter Msigwa kushoto akijadiliana Jambo na Naibu waziri wa Sheria na Katiba Mhe Angellah Jasmine Kairuki.
  Wajumbe Profesa Ibrahim Lipumba na Mheshimiwa Ismail Jusa Ladhu wakijadiliana jambo.
  M/kiti wa kamati namba mbili Mhe.Shamsi Vuai Nahodha akiwasilisha  taarifa za kamati namba mbili leo katika bunge maalum

   Mheshimiwa Ismail Jusa Ladhu akimwonyesha Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Frederick Werema  
  Mhe Profesa Mark Mwandosya kushoto akitafakari jambo na Mhe.Paul Makonda wakati wa uwasilishaji wa maoni ya kamati mbalimbali katika kikao cha Bunge maalum leo. 
  Wabunge wakigawiwa mapendekezo ya kamati mbali mbali kati yakumi nambili wakati wakikao leo cha Bunge maalum leo.
  Picha na Deusdedit  Moshi wa Globu ya Jamii.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb.) akisalimiana na Gavana wa Jimbo la Maryland la nchini Marekani, Mhe. Martin O'Malley walipokutana jijini Washington D.C kwa mazungumzo kuhusu namna ya kuimarisha ushirikiano kati ya Jimbo hilo na Tanzania katika masuala ya uchumi, jamii na siasa. Mhe. Membe alipata fursa ya kukutana na Gavana huyo alipokuwa mjini humo kwa ajili ya kumwakilisha Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye upokeaji Tuzo ya Kiongozi mwenye Mchango Mkubwa zaidi katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa Mwaka 2013.
  Mhe. Gavana O'Malley akisalimiana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani, Mhe. Liberata Mulamula
  Mhe. Waziri Membe akitoa salamu maalum kwa wajumbe kabla ya mkutano kuanza. Pembeni ni Mhe. Gavana O'Malley.
  Mhe. Membe akizungumza huku Gavana O'Malley akimsikiliza.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adufye, akimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa  Jumatano, Aprili 9, 2014. Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe Job Ndugai ambaye yuko katika ziara ya kikazi ambapo naye alialikwa kuhudhuria hafla hii
   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe akifurahia baada ya kupokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.Kushoto ni Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Mhe Job Ndugai ambaye yuko katika ziara ya kikazi ambapo naye alialikwa kuhudhuria hafla hii

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe akimshukuru Balozi wa Nigeria nchini Marekani Profesa Adebowele Adefuye baada ya kupokea Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 anayopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
  Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Liberata Mulamula akifurahia Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe akimpa Naibu Spika Mhe Job Ndugai  Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.

   Naibu Spika Mhe Job Ndugai ambaye yuko Washington kwa zaiara ya kikazi akifurahia Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopewa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
  Kiongozi wa kwaya iliyotumbuiza katika hafla hiyo akiimba atika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa , Jumatano, Aprili 9, 2014.
  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mheshimiwa Bernard Membe, akiwa na Balozi Liberata Mulamula (kushoto)  baada ya sherehe  ya  kupokea  Tuzo la Kiongozi Mwenye Mchango Mkubwa Zaidi Katika Maendeleo ya Bara la Afrika kwa mwaka 2013 aliyopokea kwa niaba ya  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika  sherehe ya kutunuku Tuzo hiyo kwenye Hoteli ya St. Regis mjini Washington, D.C., usiku wa Jumatano, Aprili 9, 2014. Picha na IkuluT

  0 0

  Hatimaye kikosi kazi cha Proin Promotions Limited kimeshawasili mkoani Dodoma tayari kwa Kazi ya Kusaka vipaji vya kuigiza Katika Kanda ya Kati ambayo inawakilishwa na Mkoa wa Dodoma. 
  Shindano hili linaendelea ambapo awali lilianzia Kanda ya Ziwa Mkoani Mwanza na hatimaye kupatikana kwa washindi watatu wa kanda ya Ziwa huku wakisubiri washindi wa Kanda nyingine kupatikana Kwaajili ya fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na mshindi mmoja kuibuka na Kitita Cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania.
  Timu nzima ya Proin Promotions Limited ambao ndio waratibu na waendeshaji wa Shindano hili tayari wapo sawa kwa shughuli hiyo katika kanda ya kati. Zoezi la kusaka Vipaji vya Kuigiza katika Kanda ya Kati itafanyika Mkoani Dodoma ambapo litaanza tarehe 12 Aprili 2014 katika Ukumbi wa African Dreamz uliopo Area C Mjini Dodoma.
  Mpaka Sasa kanda zilizobakia ni Kanda ya Juu Kusini  ambapo Mkoa utakaowakilisha ni Mbeya, Kanda ya Kusini  usaili utafanyika Mkoani Mtwara, Kanda Pwani usaili utafanyika Mkoa Dar Es Salaam na Kanda ya Kaskazini usaili utafanyika katika Mkoa wa Arusha huku Mkoa wa Kigoma ukipewa upendeleo wa kuiwakilisha Kanda ya Ziwa tena ambapo tayari zoezi hilo ndipo lilipoanzia Mkoani Mwanza.
  Kabla ya Usaili wa kusaka Vipaji vya Kuigiza Kuanza Siku ya Ijumaa kutakuwa na Promotion Party itakayofanyika Katika Ukumbi wa Disco wa 84 kuanzia saa tatu usiku na kuendelea
  Wakazi wa Kanda ya Kati wanashauriwa kujitokeza kwa wingi kwaajili ya kuonyesha Vipaji vyao na kuitumia fursa hii katika kukuza vipaji vyao

older | 1 | .... | 415 | 416 | (Page 417) | 418 | 419 | .... | 3270 | newer