Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live

Mwelekeo wa Kimbunga cha “HELLEN” na hali ya Mvua


MAJANGILI 6 YAKAMATWA NA MENO YA TEMBO 53 YENYE JUMLA YA KILO 169.7

0
0
DSCF3201Waziri wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu akizungumza na wanahabari wa vyombo mbalimbali vya habari jijini Arusha juu ya kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7 na majangili sita
DSCF3202Meneja Uhusiano wa Tanapa,Pascal Sheluteteakifurahia jambo na wanahabari jijini Arusha
DSCF3199
DSCF3198Wanahabari wa vyombo mbalimbali wakifatilia jambo kutoka kwa Waziri wa maliasili na utalii

Na Pamela Mollel,Arusha
Wizara ya maliasili na utalii imetangaza kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7na silaha moja ya kivita aina ya SMG na magazine tatu pamoj na majangili sita katika wilaya ya manyoni mkoani singida
 
Akitangaza mbele ya waandishi wa habari mkoani Arusha jana Waziri wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu alisema tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha kiombo Wilaya ya manyoni ambapo tembo 26 wameuwawa na majangili katika maeneo ya hifadhi za Rungwa na Kizigo
 
Waziri Nyalandu alisema kuwa jumla ya majangili 6 wameshikiliwa chini ya ulinzi mkali katika kituo cha polisi cha Manyoni ambapo walikutwa na meno ya tembo 53,silaha ya kivita moja na magazine tatu
 
Nyalandu alisisitiza kuwa pamoja na changamoto kubwa iliyopo dhidi ya ujangili serikali imeazimia kuwasaka na kuwakamata majangili na washirika wao popote walipo huku akidai kuwa zoezi la kuwasaka ni la usiku na mchana
 
Aidha alisema kuwa msako unaendelea kuwasata wauwaji wa tembe 26,huku akiwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu uhalifu watoe ushirikiano wao kwa askari wa wanyama pori,jeshi la polisi na vyombo vya usalama
 
Pia alitoa pongezi zake kwa mkurugenzi wa wanyama pori na kikosi chake dhidi ya ujangili kanda ya kati Manyoni na kikosi kazi maalum(Task force)kwa weledi na kujituma kwao ambapo imefanikisha kukamatwa majangili hao na meno ya tembo
Wizara ya maliasili na utalii imetangaza kukamatwa kwa meno 53 ya tembo yenye jumla ya kilo 169.7na silaha moja ya kivita aina ya SMG na magazine tatu pamoj na majangili sita katika wilaya ya manyoni mkoani singida
 
Akitangaza mbele ya waandishi wa habari mkoani Arusha jana Waziri wa maliasili na utalii Mh.Lazaro Nyalandu alisema tukio hilo lilitokea jana katika kijiji cha kiombo Wilaya ya manyoni ambapo tembo 26 wameuwawa na majangili katika maeneo ya hifadhi za Rungwa na Kizigo
 
Waziri Nyalandu alisema kuwa jumla ya majangili 6 wameshikiliwa chini ya ulinzi mkali katika kituo cha polisi cha Manyoni ambapo walikutwa na meno ya tembo 53,silaha ya kivita moja na magazine tatu
 
Nyalandu alisisitiza kuwa pamoja na changamoto kubwa iliyopo dhidi ya ujangili serikali imeazimia kuwasaka na kuwakamata majangili na washirika wao popote walipo huku akidai kuwa zoezi la kuwasaka ni la usiku na mchana
 
Aidha alisema kuwa msako unaendelea kuwasata wauwaji wa tembe 26,huku akiwaomba wananchi wenye taarifa kuhusu uhalifu watoe ushirikiano wao kwa askari wa wanyama pori,jeshi la polisi na vyombo vya usalama
 
Pia alitoa pongezi zake kwa mkurugenzi wa wanyama pori na kikosi chake dhidi ya ujangili kanda ya kati Manyoni na kikosi kazi maalum(Task force)kwa weledi na kujituma kwao ambapo imefanikisha kukamatwa majangili hao na meno ya tembo

Airtel yasaidia Afya ya Uzazi kupitia kampeni ya Wazazi Nipendeni

0
0
 Airtel Tanzania imetangaza kuendelea kushirikiana na M-Heath Tanzania katika Kampeni ya Wazazi nipendeni baada ya kuwa na ushirikiano wa mwaka mmoja wenye mafanikio  makubwa  katika  kuwasaidia kina mama wajawazito na watoto wachanga
Akiongea kuhusu mpango huo Meneja huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema”  katika kutambua umuhimu na changamoto zinazoikumba sekta ya Afya ya uzazi, Airtel tumeonelea ni vyema tukashirikia na wenzetu wa M- Health katika kuwawezesha kina mama wajawazito kupata takarifa za afya ya uzazi kirahisi. Katika mwaka wa kwanza wa ushirikiano huu program hii imeweza kufanya vizuri kiasi cha kuchaguliwa kuwa huduma bora ya mobile heath katika kategori namba 1 ya Tuzo za Connected Life zinazotolewa na Global mobile Awards kila mwaka
Aliongeza kwa kusema wanawake nchini Tanzania wapo katika hatari ya vifo vya uzazi kwa uwiano wa 38:1 yaani kati ya wanawake 38 basi yuko  1 katika hiyo hatari na kila mwaka Tanzania inakumbwa na  vifo vya watoto wachanga vyenye idadi ya kiasi cha watoto 48,100 ikiwa ni ya 10 kwa ukubwa duniani. Huduma ya ujumbe mfupi wa simu inawapatia watanzania , kina mama wajawazito na wamama wenye watoto wachanga hadi umri wa wiki 16 taarifa za afya kwa lugha ya Kiswahili bure yaani bila makato yoyote.
Airtel tunaahidi kuendelea kusaidia kampaini hii kwa kuendelea kuwawezesha wateja wetu waweze kupata huduma hii bure wakati wote na kuhakikisha tunachangia kikamilifu katika kutoa elimu na hatimae kusaidia kuboresha afya ya uzazi nchini.
Akiongea kwa niaba ya M- Health Tanzaania Mkurugenzi wa Mradi Janita Ferentinos alisema” tunapenda kuwashukuru sana Airtel kwa msaada wao mkubwa katika kuiwezesha kampaini hii kufanya vizuri. Ushirikiano wetu umetuwezesha kuwafikia watu wengi  waliojiandikisha.  Kwa watanzania wengi wanatumia huduma ya ujumbe mfupi zaidi , kwa kuondoa gharama na kufanya bure kumewezesha zaidi ya watanzania milioni 8 Tanzania kuweza kupata taarifa za msingi za afya ambazo zinaokoa maisha yao. Na ushirikiano huu umekuwa wa mafanikio kiasi cha mradi huu wa wazazi nipendeni kupewa Tuzo kama moja kati ya mpango bora wa M- Health duniani.

MKUU wa Mkoa wa Geita azindua mchakato wa uanzishwaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi (TIKA)

0
0
 1.       Mkuu wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula akifungua mkutano wa wadau mkoani Geita unatakaojadili mchakato wa uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi (TIKA).
  Katibu Tawala wa Mkoa  Severine Kahitwa akieleza umuhimu wa kuwa na utaratibu wa TIKA ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita.
Wadau wa mkutano huo wakifuatilia kwa makini hotuba ya Mkuu wa Mkoa huo.
Sehemu ya wadau wakisikiliza maagizo kutoka kwa mgeni rasmi ya namna ya kujadiliana katika mkutano huo.
  Mkutano huo pia haukuwanyima fursa ya kuelewa kinachozungumzwa ndani ya kikao hicho walemavu wa kusikia, mbele ni mkalimani wa walemavu hao John Mukube.
  Mkuu wa Mkoa Magalula Said Magalula akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya kundi maalum ambalo nalo limeshiriki mkutano huo.
 Wadau wakiwa makini kusikiliza mada zilizowasilishwa kwa ajili ya uanzishwaji wa TIKA mjini Geita.
 Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimshukuru mgeni rasmi kwa hotuba nzuri.

NI HATARI LAKINI SALAMA.

Article 24

0
0
CALL FOR PROPOSALS.
Tanzania Financial Services for Underserved Settlements (TAFSUS) is a Local Finance Facility which provides credit enhancement to Community Driven Settlement Upgrading Projects in the form of Guarantee or bridge finance. 

TAFSUS is a not-for-profit organization registered on 27th January 2009 with registration No 69478 as a Company limited by guarantee, located within TAWLAT offices, NIC Life House, 5th Floor at the Sokoine Drive/Ohio Avenue.

The Objectives of TAFSUS are:
·         To bring together key players involved in cities and national level settlement upgrading strategies to address the challenge of financing;
·         To catalyze the integration of commercial finance into settlement upgrading;
·         To provide mechanisms to blend different forms of funding to maximize affordability for the poor;
·         To provide a financial mechanism to support the implementation of city-based settlement upgrading strategies; and
·         To advocate for sound policies, enforcement of laws and proactive planning to prevent further growth/generation of unplanned areas.
TAFSUS is looking at supporting community initiatives through development of Bankable projects to access funds from commercial financial institutions with leverage of community contribution and Government subsidy. TAFSUS also offers technical support for developing and upgrading projects which include low cost housing, accesses to portable water and titling of properties in informal settlements.

TAFSUS has currently entered into Agreement with Azania Bank Limited to provide Credit Guarantee Facility to finance upgrading of unplanned settlements.

TAFSUS  now invites Associations, NGOs, Registered Communities or Groups to submit brief Concept Notes of maximum of 3 pages indicating name of organisation, nature of project, location, problem to be solved, beneficiaries, estimation of revenue and expenditures, Project costs and any other aspects that they feel should be known to enhance the acceptability of the project (Technical and Financial).

Budget Limit
The value of the Project per applying Organization, Group, community or individual differs depending on type of Project according to the guideline below:
Ø  Access to improved water supply; TZs. 30-100 Million per Project
Ø  Access to improved sanitation; TZs. 30-100 Million per Project
Ø  Housing Improvement; TZs. 1,000,000-5,800,000 per individual
Ø  Formalization of ownership; TZs. 500,000-4,800,000 per individual
Submission of the Concept Note

Mode of submission should be in hard copy and soft copy to;
TAFSUS Manager,
Tanzania Financial Services for Underserved Settlements,
P O Box 79603
Dar es Salaam- Tanzania

Tel No.  +255 222120285



NHC Kilimanjaro yatoa msaada wa bati kwa wahanga wa mvua ya Upepo wilaya za Mwanga na Hai.

0
0
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akipokea msaada wa bati toka kwa meneja wa shirika la nyumba la taifa NHC mkoa wa Kilimanjaro Shehe Kombo kama msaada kwa wahanga wa mvua iliyoambatana na Upepo mkali katika wilaya za Hai na Mwanga.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkabidhi msaada wa bati zilizotolewa na shirika la nyumba la taifa NHC mkoa wa Kilimanjaro, mkuu wa wilaya ya Hai,Noavatus Makunga .
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimkabidhi msaada wa bati zilizotolewa na shirika la nyumba la taifa NHC mkoa wa Kilimanjaro, mkuu wa wilaya ya Mwanga,Shahib Ndemanga.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akimshukuru Meneja wa shirika la nyumba la taifa NHC mkoa wa Kilimanjaro mara baada ya kukabidhiwa msaada wa bati kwa ajili ya wahanga  wa mvua iliyoambatana na Upepo mkali katika wilaya za Hai na Mwanga.
Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa NHC mkoa wa Kilimanjaro pamoja na wakuu wa wilaya waliopatiwa msaada wa bati.Na Dixon Busagaga wa globu ya jamii kanda ya kaskazini.
PICHA ZAIDI BOFYA HAPA

MTOTO MWENYE KIPAJI ADHIMU

0
0

Mtoto huyo pichani umri wake hauzidi hata miaka mitano (5) lakini sarakasi alizoruka zilimsangaza kila mtu, wahusika wanatakiwa watembee mikoani kuangalia vipaji hivi, hawa ndio watakaotuletea medali za Olympic miaka ya baadae kama wakiendelezwa. Hii ilikuwa Wilayani Handeni mkoani Tanga wakati wa sherehe za ufunguzi wa Barabara ya Mkata-Handeni hadi Korogwe kwa kiwango cha lami.

BASI LA LINAPOPATA HITILAFU KATIKATI YA HIFADHI YA NGORONGORO

0
0
Basi la kampuni ya AM likiwa limepata hitilafu katikati ya hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.
Gari la mafuta likivuka moja ya daraja ndani ya hifadhi hiyo.
Eneo la mto ambalo linatajwa kuwa ni manywesheo ya wanyama katika hifadhi ya taifa ya Ngorongoro ambapo basi la kampuni ya AM lilipata hitilafu.
Kondakta wa basi la AM aliyefahamika kwa jina la Majogoro akichota maji kwenye mto kwa ajili ya kuweka kwenye rejeta baada ya injini kuchemsha.
Basi lilikunywa maji ,madumu ya kutosha
Wanyama mbalimbali ndani ya hifadhi ya taifa ya Ngorongoro.

Nape asema CCM itashinda kwa kishindo jimbo la Chalinze

0
0
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Bonnele,Chalinze mkoani Pwani,juu ya mwenendo wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze.Nape amesema kuwa mpaka sasa Kampeni za CCM zinakwenda vizuri na wanaimani watashinda kwa kishindo kwenye Uchaguzi huo unaotarajiwa kufanyika Jumapili hii ya April 6,2014.
Sehemu ya Waandishi wa habari wakimsikiliza Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi wa CCM,Nape Nnauye mapema leo.

RAIS SHEIN AZUNGUMZA NA WAZIRI MATHIAS CHIKAWE IKULU ZANZIBAR LEO

0
0
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimkaribisha ofisini kwake Ikulu mjini Zanzibar, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe. Waziri Chikawe alifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Katikati ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (kulia) akimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (katikati) alipokuwa akifafanua jambo wakati wa mazungumzo yao yaliyofanyika Ikulu ya Zanzibar leo. Waziri Chikawe alifika ofisini hapo kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais huyo baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (watatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe (watatu kushoto), Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima (wapili kulia), Mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (wapili kushoto). Kulia ni Mkurugenzi wa Vitambulisho vya Taifa, Ofisi ya Zanzibar, Vuai Suleiman. Kushoto ni Kamishna wa Jeshi la Polisi Zanzibar, Hamdan Omary Makame. Waziri Chikawe alifika Ikulu ya Zanzibar kwa lengo la kujitambulisha kwa Rais Shein baada ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi. Viongozi hao pia walijadiliana masuala mbalimbali ya kuimarisha ulinzi na usalama wa Tanzania Bara na Visiwani. Kushoto ni Naibu Waziri wa wizara hiyo, Pereira Ame Silima. (Picha zote na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi).

MKUU WA MKOA WA GEITA AZINDUA MCHAKATO WA UANZISHWAJI WA MFUKO WA AFYA YA JAMII WA TIBA KWA KADI (TIKA)

0
0
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Magalula Said Magalula akifungua mkutano wa wadau mkoani Geita unatakaojadili mchakato wa uanzishaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii ujulikanao kama Tiba kwa Kadi (TIKA).
Katibu Tawala wa Mkoa  Severine Kahitwa akieleza umuhimu wa kuwa na utaratibu wa TIKA ndani ya Halmashauri ya Mji wa Geita.
  Ofisa Masoko na Elimu kwa Umma kutoka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya akimshukuru mgeni rasmi kwa hotuba nzuri.
Wajumbe wakipitia mada zilizoandaliwa katika mkutano huo.

WORLD BANK SUPPORTS TANZANIA'S EFFORTS TO STRENGTHEN THE BUSINESS CLIMATE AND MAKE THE POWER SECTOR FINANCIALLY SUSTAINABLE

0
0
The World Bank’s Board of Executive Directors has approved two operations from the International Development Association (IDA*) to help Tanzania strengthen its capacity to manage public expenditures, its business environment, and the financial sustainability of the power sector. 

Both operations aim to accelerate inclusive economic growth and pave the way for shared prosperity and reduced poverty.

The IDA credit of US$85 million for the Eleventh Poverty Reduction Support Credit (PRSC 11) which was approved today is designed to further strengthen the management of public finance and improve investment climate in select strategic areas. 

This is the final operation in a series of three annual programmatic development policy operations (DPOs) in support of Tanzania’s implementation of its poverty reduction strategy, MKUKUTA II, complemented by the First Five Year Development Plan (FYDP I).

“The operation will help to create a better business climate to stimulate private investment and help mobilize larger domestic revenue,” said Emmanuel Mungunasi, the World Bank Task Team Leader for the operation. “Benefits from growth will be shared more broadly across the country by creating a sound public expenditure policy through which revenues will be distributed.”

SHUKRANI

0
0
MAREHEMU BALOZI FULGENCE MICHAEL KAZAURA

Familia ya Marehemu Balozi Fulgence Michael Kazaura, inapenda kutoa shukrani za dhati kwa ndugu, jamaa, marafiki na majirani wote ambao tumeshirikiana  katika kipindi chote cha kumuuguza Mpendwa wetu Marehemu Balozi Fulgence Michael Kazaura hadi kifo chake kilichotokea tarehe 22 Februari, 2014 huko Chennai, India. Hii imetupa faraja kubwa sana wana Familia katika kipindi hiki kigumu.

Kwa namna ya pekee, Familia inatoa shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dr. Mohammed Gharib Bilal, Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Pinda, Rais Mstaafu, Mheshimiwa Benjamin William Mkapa, Mawaziri Wakuu wastaafu, Mheshimiwa Jaji Joseph Sinde Warioba, Mheshimiwa Edward Lowassa na Mheshimiwa Frederick Sumaye. Shukrani pia ziwaendee Jaji Mkuu Mheshimiwa Mohamed Chande Othman .

Waheshimiwa Mawaziri, Katibu Mkuu Kiongozi Mheshimiwa Balozi Ombeni Sefue, Katibu Mkuu Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt Richard Sezibera, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mheshimiwa Said Mecky Sadick, Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe, Viongozi wa Serikali wastaafu, Viongozi wa vyama vya Siasa, Mabalozi na Wawakilishi wa Nchi mbalimbali hususan Balozi wa Tanzania nchini India.

Vilevile, Familia inapenda kuwashukuru Kaimu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Balozi Nicolas Kuhanga, Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Rwekaza Mukandala, Jumuiya ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Bodi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Taasisi zifuatazo: Benki ya Afrika (BOA), Shirika la Ugavi wa Umeme (TANESCO), Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Centre for Diseases Control (CDC), Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania, Benki ya Standard Chartered, Benki ya Barclays Tanzania na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE) ,
Tunazishukuru pia Taasisi zifuatazo:  Wakala wa Huduma za Ndege za Serikali Tanzania, Chama cha Mabalozi Wastaafu Tanzania, Chama cha Maskauti Tanzania, ,  na Wanachama wa British Legion.

Mahsusi, Familia inawashukuru sana Mhashamu Methodius Kilaini  Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, , Paroko wa Kanisa la Mtakatifu Petro, Paroko wa Mugana, Mapadre, Masista na Watawa, kwa kuendesha ibada za Misa, Dar es Salaam na Kijijini Bugandika.

Kwa namna ya pekee pia tunawashukuru Madaktari na wauguzi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasisi ya Kansa Ocean Road, Hospitali ya Misheni Mikocheni, Taasisi ya Kansa ya Apollo, India. Vile vile wana Jumuiya ya Mtakatifu Cecilia, Kwaya ya Jumuiya ya Mtakatifu Cecilia ya Kanisa la Mt Petro, Oysterbay Dar es salaam, na Kwaya ya Parokia ya Mugana, Bukoba.

Kwa vile si rahisi kuwataja wote walioshirikiana nasi katika kipindi hiki cha Msiba, kwa taarifa hii tunawaomba wote kupokea shukrani zetu za dhati kwa moyo wa upendo mkubwa mlioonyesha kwetu.

Tunapenda pia kuwataarifu kuwa kutakuwa na Ibada ya Shukrani itakayofanyika siku ya Jumamosi tarehe 5 April, 2014, katika Kanisa la Mt. Petro Oysterbay, saa nne kamili asubuhi ambayo itafuatiwa na chakula cha mchana nyumbani kwa Marehemu, Mtaa wa Guinea, Nyumba No. B.3-1, TIRDO Estate, Oysterbay, saa sita kamili mchana. Karibuni sana.

MUNGU AILAZE ROHO YA MAREHEMU MAHALI PEMA PEPONI, APUMZIKE KWA AMANI. AMINA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje atembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Zambia

0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,Bw. John Haule (kulia anayeangalia nyaraka) akipata taarifa kutoka kwa Bw. Gration Kamugisha, Afisa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Miradi Hazina (U.T.T) kuhusu mikakati ya kuboresha nyumba zinazomilikiwa na Ubalozi, Lusaka- Zambia kwa kuingia ubiya na UTT, kulia kwa Bw. Haule ni Katibu Mkuu wa Hazina, Bw. Servacius Likwelile wa kwanza kushoto akisikiliza. Kikao hiki kilifanyika Ofisini kwa Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Grace J. Mujuma (anayetazama kamera). Wengine katika picha ni Bibi Justa Nyange, Mkuu wa Utawala, Ubalozini aliye kushoto kwa Bw. Haule na Bw. Mihalale Mwakibinga, Msajili kutoka Hazina aliyeketi kulia kwa Bw. Likwelile.

NANE (8) MBARONI KWA MAKOSA MBALIMBALI YA UHALIFU MKOANI DODOMA

0
0
Na Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma

Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma linawashikilia watu nane kwa makosa mbalimbali ya uhalifu kufuatia msako uliofanyika tarehe 01/04/2014 maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Dodoma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME - SACP amesema tukio la kwanza alikamatwa SIMON S/O MTUNDU, miaka 51, Kabila Mhehe, mkulima na mkazi wa kijiji cha Kisisi Kata ya Kimagiyi Tarafa na Wilaya ya Mpwapwa, akimiliki silaha aina ya Gobore lenye Namba MP. 00202182 kinyume cha sheria za umiliki wa silaha.

Kamanda MISIME amesema tukio jingine alikamatwa CHISEMI S/O ROBERT, miaka 34, kabila Mgogo, mkazi wa kijiji cha Kiboriani Wilaya ya Mpwapwa na wenzake wawili wakimiliki shamba la bhangi ekari moja na nusu (1.5) kinyume cha sheria. Shamba hilo limefyekwa na kuteketezwa kwa moto.

Aidha katika Wilaya ya Chemba Mkoani humo alikamatwa MUSSA S/O ALLY MADEBE, mwenye miaka 20, mkulima wa Kijiji na Kata ya Songolo Tarafa ya Goima na wenzake watatu wakiwa na misokoto nane ya Bhangi,  watuhumiwa watafikishwa mahakamani mara upelelezi utakapokamilika na msako bado unaendelea.

Kamanda MISIME amewashukuru wananchi hawa wanaoshirikiana na Jeshi la Polisi kwa kutoa taarifa na kushirikiana na Polisi katika misako.

TAHADHARI YA UTAPELI

RAIS KIKWETE ATEMBELEA ABERDEEN, SCOTLAND, AONGEA NA KUNDI LA WABUNGE WA UINGEREZA WANACHAMA WA BRITAIN TANZANIA SOCIETY

0
0
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia kundi la Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa walio marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa Britain and Tanzania Society (All Party Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London April 1, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata picha ya kumbukumbu na baadhi ya Wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya Uingereza walio marafiki wa Tanzania pamoja na wanachama wa Britain and Tanzania Society (All Party Parliamentary Group on Tanzania, and Britain Tanzania Society) katika mchapalo walioandaa kwa heshima yake katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Nje na Jumuiya ya Madola katika jengo la Durbur jijini London April 1, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akijaribu kuendesha mfano wa mtambo wa kufundishia namna ya kuchimba mafuta katika visima vilivyo bahari kuu (KCA Deutag Dart Drilling Simulator and Well Enginering System) alipotembelea Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali ya siku tatu nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho kuanzia mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi. Nyuma yake ni ujumbe alioongozana nao ikiwa ni pamoja na Waziri wa Biashara, Viwanda na Masoko wa Zanzibar Mhe Nassor Ahmed Mazrui (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Mhongo (wa pili kulia) Wa pili kushoto ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe Peter Kallaghe, akifuatiwa na Mkurugenzi wa Idara ya Ulaya katika Wizara za mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa Balozi Dorah Msechu.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na ujumbe wake katika picha ya pamoja na uongozi wa Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospter Muhongo wakisindikizwa na Naibu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Robert Gordon mjini Aberdeen, Scotland, Jumanne April 1, 2014 alikotembelea akiwa katika siku ya mwisho ya ziara yake ya kiserikali nchini Uingereza kwa mwaliko wa Waziri Mkuu wa Uingereza Bw. David Cameron. Zaidi ya Watanzania 20 wamepata udhamini wa kusoma katika chuo hicho mwaka huu, ambapo watasomea fani mbalimbali za sekta za mafuta na gesi.PICHA NA IKULU.

MWENYEKITI WA KAMATI NAMBA 1 YA BUNGE LA KATIBA AKUTANA NA WAANDISHI WA HABARI MJINI DODOMA

0
0
Mwenyekiti wa Kamati Nambari 1 ya Bunge Maalum la katiba, Ummy Mwalimu (kulia) akizungumza na Waandishi wa habari baada ya kuongoza kikao cha Kamati hiyo kwenye Kituo cha Mikutano cha Saint Gaspar mjini Dodoma  leo Aprili 2, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YAFUNGA MAFUNZO YA ZOEZI LA UORODHESHAJI WA VIWANDA NCHINI

0
0
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera akiwahutubia Wasimamizi na Wadadisi (hawapo pichani) muda mchache kabla ya kufunga mafunzo ya Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini, mafunzo hayo yamefungwa jana Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi wa Utawala na Masoko kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Stanley Mahembe akiwatambulisha wageni walioketi meza kuu (hawapo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini, mafunzo hayo yamefungwa jana Mkoani Morogoro.
Baadhi ya Wasimamizi na Wadadisi wa Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini wakimsikiliza kwa makini Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (hayupo pichani) wakati wa kufunga mafunzo ya Zoezi hilo jana Mkoani Morogoro.
Mgeni Rasmi Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe. Joel Bendera (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa Serikali pamoja na Wasimamizi wa Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda nchini mara baada ya kufunga mafunzo ya zoezi hilo jana Mkoani Morogoro. (PICHA ZOTE NA VERONICA KAZIMOTO).
Viewing all 109595 articles
Browse latest View live




Latest Images