Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live

programu ya upimaji wa Afya kwa wananchi kwa magonjwa yasiyoambukiza

$
0
0
 Meneja Masoko  na Elimu kwa Umma  toka  Mfuko  wa Taifa wa Bima ya Afya ( NHIF) Bi Anjela Mziray akiwaeleza waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu programu ya upimaji wa Afya kwa wananchi kwa magonjwa yasiyoambukiza inayoendeshwa na mfuko huo hapa nchini.kulia ni Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja na kushoto ni Afisa habari ,Idara ya Habari Maelezo  Bi Fatma Salum.
 Meneja Uhakiki na Madai wa mfuko huo Dk.Clement Masanja  akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kufanya mazoezi ili kujikinga na magojwa yasiyoambukiza kama kisukari, msongo wa mawazo  na shinikizo la damu,kushoto ni Meneja Masoko na Elimu kwa Umma Bi Anjela Mziray
 Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia mkutano wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) uliofanyika leo jijini Dar es salaam uliolenga kuelimisha wananchi kuhusu mapambano dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza kama Kisukari,shinikizo la damu na Saratani.

Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia yatoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi ya tehama

$
0
0

 Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia bi Prisca Ulomi akitoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)  wakati wa mkutano  na waandishi wa habari leo jijini Dar es salam .
Kaimu Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia Bi Prisca Ulomi akiwaeleza waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu hatua iliyofikiwa na Serikali katika  Uandaaji wa Sheria ya Matumizi Salama ya Mtandao,kushoto ni Afisa habari wa Idara ya Habari Maelezo Bi Fatma Salum.

WAKAZI WA KIJIJI CHA KABWE WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA WAFAIDIKA NA UVUVI WA SAMAKI ZIWA TANGANYIKA

$
0
0
 Baadhi ya akina mama wanaojishughulisha na biashara ya samaki,wakiwa wametoka bandari ya Kabwe,Wilayani Nkasi mkoani Rukwa mapema leo,ambapo dishi moja kama uonavyo pichani huuzwa kati ya shilingi Elfu 30,000/=
 Akina mama wakiwa na madishi yao ya samaki,akina mama wengi eneo hilo wameeleza kuwa wanafaidika na biashara hiyo ya samaki kwa kujiingizia kipato na hatimaye kujikwamua na ugumu wa maisha,wameeleza kuwa changamoto yao kubwa ni mitaji ya kutosha ili kuendeleza biashara hiyo ambayo Wanawake wengi hujishughulisha nayo.
 Dishi lililobebwa samaki aina ya Migebuka huuzwa shili Elfu Thelathini
Wavuvi wakirejea baada shughuli yao ya uvuvi kufanyika katika bandari ya Kabwe,Wilayani Nkasi mkoani Rukwa mapema leo.
Picha na MichuziJr-MICHUZI MEDIA GROUP-NKASI RUKWA

KATIBU MKUU WA CCM,KINANA AANZA RASMI ZIARA YAKE WILAYANI NKASI MKOANI RUKWA LEO

$
0
0
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipata maelezo mafupi kutoka kwa wenyeji wake kuhusiana na ujenzi wa hatua za awali za bandari ya Kabwe,wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

 Katibu Mkuu wa CCM;ndugu Kinana akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Kirando,wilayani Nkasi mapema leo.Kinana alisema kuwa tahakikisha Barabara ya kutoka Sumbawanga mjini kwenda kijiji cha kabwe itatengenezwa kwa kiwango cha lami."Nitaenda na mbunge wenu kushinikisha suala la barabara hii ili ijengwe kwa kiwango cha lami na kuwarahisishia sughuli za  kibiashara"alisema.Alisema kuwa maendeleo hayawezi kuja ikiwa miundombinu ni mibovu hivyo atahakikisha analifikisha kwa waziri mwenye dhamana pamoja na mkuu wa nchi ili kazi hyo ifanyike mapema. 

 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwahutubia wananchi na wanachama wa CCM,mapema leo jioni katika kijiji cha Kabwe,Wilayani Nkasi.Kinana alisema kuwa, Serikali inatambua  matatizo ya wananchi wa kjijini hapo ikiwemo suala la pembe jeo, maji pamoja na uvamizi wa wavuvi. "Miradi yote inayotekelezwa nchi nzima kwa sasa ni utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya mwaka 2010, hatubagui kwakua wote ni watanzania"alisema.Alisema kuwa Serikali inatambua kuwa shughuli kubwa ya kijini hapo ni uvuvi hivyo itajitahidi kuwe na utaratibu wa kuwasaiidia kupata mikopo ili waweze kununua zana za uvuvi ili waweze kujiendeleza.
 Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana akiangalia samaki katika kiwanda kidogo cha kuhifadhia samaki na kuuza katika kijiji cha Kabwe,Wilayani Nkasi mkoa wa Rukwa  mapema leo,ambapo pamoja na mengine Ndugu kinana alifanya mkutano wa hadhara ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya siku 21 katika mikoa ya Rukwa,Katavi na Kigoma,ziara hiyo ikiwa na lengo la kuimarisha Uhai wa chama,kusikiliza kero mbalimbali za wananchi na kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata ilani ya CCM.
 Samaki aina ya Migebuka ikiwa imeandaliwa kwa ajili ya kukaushwa kabla ya kuhifadhiwa kwenye majokofu  na kusafirishwa maeneo mbalimbali,ndani na nje ya nchi.
 Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza jambo na  Mbunge wa Jimbo la Nkasi Kaskazini,Mh.Ally Keisy alipokwenda kukagua ujenzi wa bandari ya Kabwe katika hatua za awali  na kujionea shughuli mbalimbali za uvuvi zinazofanyika katika kijiji hicho kabwe.
 Ndugu Kinana akishiriki ujenzi wa Ofisi ya CCM katika kijiji cha Kabwe,wilayani Nkasi mkoani Rukwa mapema leo jioni.
PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

BARAZA LA MADIWANI LA MJI KOROGWE LAUPOKEA KWA MIKONO MIWILI MPANGO TIBA KWA KADI (TIKA)

$
0
0
Afisa Utumishi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe, Bw. Lewis Kalinjuna akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani katika kupitisha sheria ndogo ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) kwenda katika Mfumo wa Afya ya Jamii Mijini wa Tiba kwa Kadi (TIKA). Kikao hicho cha mwisho kimefanyika Machi 29, 2014 katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe. Pembeni ni Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera (kulia), Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba (kushoto).
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) – Mkoa wa Tanga, Bw. Ally Mwakababu akitoa maelezo machache juu ya TIKA. Pembeni ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji ambaye ni Diwani wa Kata ya Mtonga, Mheshimiwa Francis Komba na Mwenyekiti wa Hamashauri ya Mji Korogwe ambaye ni Diwani wa Kata ya Kilole, Mheshimiwa Angello Bendera.
Wajumbe wa Baraza la Madiwani wakifuatilia kwa makini.

Uingereza ndani ya Tamasha la Pasaka

$
0
0
  MUIMBAJI wa Kimataifa raia wa Uingereza Ayobami David  ni mmoja wa waimbaji watakaoshiriki katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kuanza Aprili 20 katika mikoa nane hapa nchini. Ayobami ni muimbaji ambaye anafanya vizuri katika muziki huo wa Kumtukuza Mungu kupitia nyimbo mbalimbali.

Awali Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Pasaka inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Alex Msama ilijipambanua kwamba tamasha la mwaka huu wanatoka kivingine ili kuendana na kasi ya Sayansi na Teknolojia kwa kuwashirikisha waimbaji wa ndani na nje ya Tanzania. Kwa mujibu wa Msama kwa kuwa wameamua kukuza muziki huo hapa nchini, dhana hiyo itafanyika kila kona ya dunia ili Tanzania ipige hatua zaidi katika tasnia ya muziki huo.

Msama alisema miaka iliyopita walikuwa wakiwatumia katika matamasha yake yaliyoasisiwa tangu mwaka 2000, waimbaji kutoka Kenya, Zambia, Afrika Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) na  kwingineko. “Niliyoeleza mwanzoni yanakamilika, kwa sababu nilidhamiria kuliboresha zaidi Tamasha la Pasaka kwa kuwashirikisha waimbaji wa Kimataifa, mashabiki wakae mkao wa kula kupata ladha tofauti katika tamasha la mwaka huu,” alisema Msama.  

Aidha Msama alisema mbali ya Ayobami, Kamati imemuongeza muimbaji wa injili raia wa Rwanda, Lilliane Kabaganza ingawa bado taratibu zinaendelea kuwapata waimbaji wengine wa kimataifa. Mbali ya waimbaji hao wa Kimataifa, wengine ni Rebecca Malope, Keke Phoofolo (Afrika Kusini), Ephraim Sekereti (Zambia), Faraja Ntaboba (DRC) na Sarah K, Paul Mwai (Kenya).Baadhi ya waimbaji wa Tanzania waliothibitishwa kushiriki katika tamasha hilo ni pamoja na John Lisu, Rose Muhando, Upendo Nkone na Upendo Kilahiro.

Japan yasaidia Tanzania kuinua kilimo.

$
0
0
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akitia saini hati ya makubaliano ya msaada wenye thamani ya ziadi ya bilioni 6 unaolenga kukuza sekta ya kilimo uliotolewa   na Serikali ya Japan  kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo jijini Dar es salaam. Kulia ni Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda.
 Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) akikabidilishana nakala ya makubaliano waliosainina na Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) ambayo yanahusu msaada uliotolewa na Serikali ya Japan  kupitia Shirika la Kimataifa la Japan (JAICA) leo jijini Dar es salaam. 
 Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi akikabidilishana nakala za mkataba uliosainiwa na Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia) na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) leo jijini Dar es salaam. 
Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda (kulia), akiteta jambo na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kushoto) baada ya Serikali ya Tanzania kusaini mkataba na Serikali ya Japan leo jijini Dar es salaam.  (Picha zote na Eleuteri Mangi).
========= ========= =========

Na Eleuteri Mangi- MAELEZO
Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa zaidi ya sh. bilioni sita (6) za Kitanzania ambazo ni sawa na Yen milioni 380 zilizotolewa na Serikali ya Japan kupitia Shirika lake la Kimataifa la Misaada (JAICA) . Kauli hiyo ilitolewa leo jijini Dar es salaam na Katibu Mkuu Wizara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa kupokea msaada huo  ambao utatumika kukuza sekta ya kilimo na kupunguza umasikini nchini. Katibu Mkuu Dkt. Likwelile alisema kuwa msaasa huo utatumika kununulia mbolea (UREA) ili kuongeza tija katika uzalishaji mazao na unalenga kuwafikia wakulima wadogo wadogo nchini ili kuwaongezea kipato chao.

Katibu Mkuu huyo alisema kuwa msaada huo umekuja muda muafaka ambapo serikali inachukua hutua za makusudi kuinua sekta ya kilimo ambayo inawaajiri watanzania takribani asilimia 74 nchini.  Aidha, Katibu Mkuu aliishukuru Serikali ya Japan kwa msaaada huo na kumhakikishia Balozi wa Japan nchini Mh. Masaki Okanda kuwa msaada uliotolewa na Japan kupitia JAICA utatumika kulinganana malengo yaliyokusudiwa.

Kwa upande wake  Balozi wa Japan nchini Masaki Okanda alisema kuwa msaada uliotolewa na Serikali yake kupitia JAICA unalenga zaidi sekta ya kilimo na kusaidia kuimarisha miundo mbinu ya barabara na masoko ambayo ndiyo kiini cha ufanisi katika sekta hiyo. Naye Mwakilishi wa Mkuu wa JAICA nchini Yasunori Onishi alisema kuwa mahusiano mazuri yaliyopo kati ya Tanzania na Japan ni wa kihistoria ulianzishwa tangu mwakqa 1974 ambapo mkoa wa Kilimanjaro ulikuwa unanufaika na misaada hiyo katika kuboresha kilimo.

Akimshukuru Katibu Mkuu Likwalile na Balozi wa Japan nchini  Okanda, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika Yamungu Kayandabila alisema kuwa amefurahi Wizara yake kupata masaada huo na ameahidi kuwa utatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuleta kilimo chenye tija nchini. Serikali ya Japan nchini kwa kushikiana na Tanzania katika kusimamaia kilimo inaongozwa na nguzo kuu tatu ambazo ni kilimo, miundombinu na utawala bora, hali ambayo itaihakikishia nchi kuwa na uhakika wa mazao bora na hivyo kupunguza umasikini nchini.

TAARIFA ZIARA YA RAIS KIKWETE NCHINI UINGEREZA

$
0
0
THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail:  ikulumawasiliano@yahoo.compress@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
       P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 
                                                                                      
TAARIFA KWA UMMA

Uingereza inajivunia kuwa nchi inayoongoza katika uwekezaji nchini Tanzania na itaendelea kuisaidia Tanzania katika jitihada zake za kiuchumi na kuleta maendeleo .

Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron amemuambia Rais Kikwete wakati wa mazungumzo yaliyofanyika 10 Downing Street,  Leo tarehe 31 March, 14, ambapo ndipo yalipo Makao Makuu ya Waziri Mkuu wa Uingereza.

"Tunafurahia sana uhusiano wetu na kujivunia kuwa tunaongoza katika
Uwekezaji nchini Tanzania" Bw. Cameron amesema na kumhakikishia Rais Kikwete kuwa Uingereza iko tayari kutoa misaada zaidi.

Rais Kikwete amewasili nchini Uingereza tarehe 30 Machi, 2014 kwa ajili ya ziara ya kikazi ya siku 3 kufuatia mualiko wa Bw. Cameroon ambaye pia amemuomba Rais Kikwete aendelee kutoa mchango wake wa mawazo katika masuala ya kimataifa hasa baada ya mwisho wa muda wa malengo ya millennium ya 2015.

"Tunakaribia mwisho wa muda wa malengo ya millennia Mwaka 2015, tutahitaji kuweka vipaumbele vingine baada ya hivyo kama kuondosha umaskini, Maji safi na salama, masuala ya ufisadi na utawala bora, natumaini utaendelea kutoa mchango wako baada ya malengo hayo kufikia tamati" Waziri Mkuu Cameron amemuambia Rais Kikwete ambapo Rais amekubali ombi hilo na kuahidi ushirikiano wake.

Mapema leo asubuhi Rais amekutana na mtoto wa Mfalme Prince Andrew katika makazi ya Malkia ya Buckingham ambapo wamebadilishana mawazo kuhusu mambo mbalimbali ya Kimataifa na Kijamii.

Kabla ya kwenda Buckingham Rais amefungua mkutano kuhusu uwekezaji na kuelezea fursa na nafasi zilizopo za uwekezaji nchini Tanzania na kuelezea kwanini wawekezaji watakuwa wanafanya uamuzi bora kwa kuwekeza Tanzania kuwa ni pamoja na;

"Fursa nyingi, amani, usalama, soko la kutosha na kubwa kwa vile Tanzania iko katika Umoja wa Afrika Mashariki, Ukanda wa Maziwa Makuu na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika,hivyo kuwa na uhakika wa soko kubwa na pana" amesema.

Katika ziara yake Rais pia amekutana na Mstahiki Meya  wa Jiji la London Mama Alderman Fiona Woolf na kukaribishwa rasmi Jijini London. Mstahiki Meya  anatarajia kutembelea Tanzania, Mwezi Septemba Mwaka huu.

Rais alipowasili London tarehe 30 Machi,2014, alikutana na Watanzania wanaoishi nchini Uingereza na kuwaeleza maendeleo yaliyopo nchini Tanzania.

Rais anaendelea na ziara yake nchini Uingereza

Mwisho.

Imetolewa na;
Premi Kibanga.
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
London Uingereza
31 Machi, 14

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Sikiliza "Masafa marefu" na Tancut Almasi Orchestra live!

TAARIFA YA MSIBA: MAMA MZAZI WA SAID MDOE WA SALUTI5 AFARIKI DUNIA

$
0
0
MAMA mzazi wa mmiliki wa mtandao wa Saluti5, Said Mode - Bi Desta Mohamed - amefariki ghafla Jumatatu ya tarehe 31/3/2014 saa 1 za jioni.

 Alipata homa kali Jumapili mchana, akapelekwa hospitali (IMTU) akapata matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani. Hali yake haikuwa mbaya wala ya kutia mashaka.

 Jumatatu akaamka vizuri na akashinda vizuri hadi saa 12 za jioni hali ipoanza kubadilika tena. Akafariki akiwa njiani kupelekwa hospitali. Msiba uko Dar es Salaam, Mbezi Beach Old Bagamoyo Road kituo cha Zena Kawawa.

Mazishi yatafanyika Jumanne 1/4/2014 saa 10 alasiri kwenye makaburi ya Mbezi Beach (New Bagamoyo Road) mbele kidogo ya  Masana Hospital.
INNA LILLAHI WAINNA ILAYHI RRAAJIUN.

SUPER D AMPIKA JUMA BIGLEE KUPAMBANA APRIL 15 CHALINZE

$
0
0
Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Juma Biglee wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala amana CCM Dar es salaam jana.

Kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' kulia akimwelekeza jinsi ya kutupa makonde bondia Juma Biglee wakati wa mazoezi yanayoendelea katika kambi ya Ilala amana CCM Dar es salaam jana Biglee anajiandaa na mpambano wake april 15 Chalinzo mkoa wa pwani picha na www.superdboxingcoach.blogspot.com

Ngeleja mgeni rasmi tamasha la Pasaka jijini Mwanza

$
0
0
ALIYEKUWA Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja anatarajia kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Pasaka linalotarajia kufanyika Mei 4 Jijini Mwanza.Kwa mujibu wa Makamu Mwenyekiti  wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Abihudi Mang’era kamati imejipanga  kufanya tamasha la kishindo jijini humo kwa sababu maandalizi yake ni ya hali ya juu.

Mang’era alisema tamasha hilo litakuwa ni la aina yake ambako alitoa wito kwa wakazi wa Kanda ya ziwa kujitokeza kwa wingi katika tamasha hilo. Mang’era alisema sambamba na Ngeleja, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Stephen Masele anatarajia kuwa mgeni rasmi mkoani Shinyanga Mei 3. Aidha Mang’era  alisema mipangilio ya kuelekea tamasha hilo inaendelea vizuri hivyo wakazi wa Kanda ya Ziwa wakae mkao wa kula kupata neno la Mungu kupitia waimbaji mbalimbali wa Tanzania na nje.

Alisema tamasha hilo jijini Mwanza linatarajia kukongwa na muimbaji raia wa Afrika Kusini, Rebecca Malope na wengineo watakaoteuliwa na kamati ya maandalizi.

news alert: ankal anunua ndege kuondokana na adha ya foleni jijini dar es salaam

$
0
0
Ankal akijiandaa kuingia ndani ya ndege yake ndogo inayoweza kutua popote aliyoinunua hivi karibuni kutoka katika visiwa vya Ushelisheli (Seychelles Islands) ili kuepukana na adha ya foleni jijini Dar es salaam. 
Ankal ameiambia Globu ya Jamii kwamba amekuwa akisomea urubani wa ndege hiyo kwa siri kwa mwaka mmoja na sasa ameshatimiza  masaa 450 hewani na tayari ameshapata leseni ya kupaa katika jiji la Dar (mchana tu, kati ya saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni) na kutua katika viwanja mbalimbali vikiwemo vya Gymkhana (kwa wilaya ya Ilala), Uwanja wa Taifa wa zamani (wilaya ya Temeke) na Biafra (wilaya ya Kinondoni) na Maisara (Unguja). 
Maombi yake ya kutua katika miji  mingine mikubwa kama vile Mbeya, Mwanza, Arusha, Rukwa, Katavi, Njombe, Dodoma na Morogoro yanashughulikiwa na huenda akafanikiwa mara baada ya sehemu za kutua katika mikoa hiyo zitapothibitishwa na mamlaka husika.
Ankal anakuwa blogger wa kwanza Mtanzania mwenye kumiliki ndege yake mwenyewe. Anasema hiyo ni hatua moja kubwa aliyokuwa akiiota miaka kadhaa wakati alipokuwa anafikiria si tu namna ya kupambana na foleni mijini, bali pia kufikia habari moto na kwa muda muafaka..

MASHINDANO YA NSSF MEDIA CUP YAANZA KUTIMUA MBIO

$
0
0
MASHINDANO ya Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii inayowahusisha waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari (NSSF Media Cup) yameanza kutimua vumbi katika uwanja wa TCC, Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Akifungua mashindano hayo, Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudencia Kabaka, amewataka wanahabari nchini kuhakikisha wanajiunga na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), ili kujihakikishia maisha ya amani na utulivu baada ya kustaafu.

Alisema kuwa, wanahabari wanapaswa kwenda mbali zaidi katika kulitumia shirika hilo, ili kunufaika na mafao mbalimbali yanayotolewa kwa wanachama.

Katika ufunguzi huo, timu ya soka ya New Habari (2006) Ltd iliumana na Habari Zanzibar katika Soka, ambako hadi  filimbi ya mwisho Habari Zanzibar iliibuka kidedea kwa magoli 4-1, magoli ya Zanzibar yaliwekwa wavuni na Amoor Suleiman aliyeweka wavuni goli moja na Yusuph Juma magoli matatu huku goli la New Habari likiwekwa wavuni na Florian Mwasinde.

Kwa upande wa netiboli, timu ya Jambo Leo iliichapa timu ya Wizara ya Habari Bara kwa jumla ya magoli 59-8, katika pambano la upande mmoja lilipoigwa kwenye viwanja hivyo.

Katika mechi ya pili ya netiboli, Azam Media iliumana na Tanzania Standards Newspaper (TSN), ambako Azam waliibuka washindi kwa magoli 18-13.

Kabaka aliwataka washiriki wa mashindano hayo ya 11 yanayoshirikisha wafanyakazi wa vyombo vya habari kuonesha ushindani, ufundi na nidhamu ili kuongeza hamasa ya michuani hiyo.

Alivitaka vyombo vya habari kuepuka kuingiza wachezaji wasio wanahabari (mamluki), kudumisha lengo la umoja na ushirikiano baina ya shirika hilo kongwe na vyombo vya habari, ikiwamo kuwapa mazoezi wafanyakazi wa vyombo hivyo.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo. Wa pili kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Chiku Matesa.
Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka (wa pili kulia), akipata maelezo kutoka kwa Ofisa Uhusiano wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Carolyne Newa wakati alipotemberlea banda la NSSF wakati wa uzinduzi wa mashindano ya NSSF Media Cup 2014 kwenye uwanja wa TCC Chang’ombe jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka akisalimiana na mshambuliaji wa timu ya New Habari 2006, Joh Dande wakati wa uzinduzi wa michuano ya NSSF Media Cup 2014 kwenye uwanja wa TCC Chang'ombe Dar es Salaam.

Jumuiya ya Watanzania nchini Malaysia yapata Uongozi wao

$
0
0
Jumamosi ya tarehe 29 March 2014, watanzania waishio na wasomao Malaysia walikutana katika Ubalozi wa Tanzania na kuunda Jumuiya mpya ya Watanzania wanaoishi South East Asia.

Uongozi wa Wana Jumuiya hiyo ambao kwa kuanzia ni Watanzania waliopo Malaysia wakiwa na Balozi Mpya wa Tanzania,Dr. Aziz Ponary Mlima (katikati) na maafisa wa Ubalozi. Viongozi waliochaguliwa ni Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo, Katibu Mkuu, Waziri wa Fedha, Waziri wa Elimu, Waziri wa Jamiii, Utamaduni na Starehe ikiwa pamoja na Wadhamini wawili.

Picha nyingine ni Watanzania wote kwa pamoja na wafanyakazi wa Ubalozi na Balozi Mpya wa Tanzania nchini Malaysia.

Jumuiya hiyo ilianzishwa Mwishoni mwa wiki,ambayo inajulikana kama " Tanzanian Diaspora in South East Asia" ambayo itakuwa inawashirikisha Watanzania wote katika nchi za Malaysia, Indonesia, Thailand, Philippines, Brunei, Laos na Cambodia.

Picha zaidi zinaweza kuonekana kwenye Ukurasa wa Facebook


Watanzania kutoka maeneo hayo wanaombwa kujiunga ili tuweze kutambuana na itakapokuwa lazima kusaidiana.

Kwa niaba ya Tanzanian Diaspora South East Asia.

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL APANDA MTI KUADHIMISHA SIKU YA KUPANDA MITI KITAIFA

$
0
0
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Bilal, akipanda mti wa Mwembe nje ya Ofisi yake mpya ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya kupanda miti.
 Baadhi ya wafanyakazi wa Ofisi ya Makamu wa Rais wakimsikiliza Makamu wakati akizungumza nao.

URAFIKI WA KWELI

$
0
0
 Kuku na vifaranga vyake wakisaidiana kufanya kazi ya kula wadudu waliokuwepo kwa Mbwa huyu kama kamera yetu ilivyofanikiwa kuinasa taswira hii.

WASHINDI WA PROMOSHENI YA WINDA SAFARI YA BRAZILI NA SERENGETI WAENDELEA KUKABIDHIWA ZAWADI ZAO

$
0
0
 Meneja Mauzo eneo la Moshi mjini Fredrick Chambega (kulia) akimkabidhi zawadi ya king’amuzi mmoja wa washindi wa wiki wa promosheni ya Winda Safari YA Brazili na Serengeti Pasian Shirima (kulia) katika hafla fupi iliyofanyika mkoani Kilimanjaro, promosheni hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Bia ya Serengeti.
 Meneja Mauzo wa Kampuni ya Bia ya Serengeti mkoa wa Kilimanjaro Orest Mmbaga (kushoto) akimkabidhi zawadi ya simu aina ya Samsung Galaxy tab mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili na Serengeti Elly Kisanga (kulia) wakati wa hafla ya makabidhiani mkoani Kilimanjaro

Benki ya FNB yakutana na wateja wake wa Tanzania

$
0
0
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya FNB,Dave Aitken akizungumza na wateja wa benki hiyo wakati wa mkutano kati ya wateja na benki hiyo kujadili kuhusiana na mwelekeo wa uchumi wa kimataifa wa hapa nchini.
Baadhi ya washiriki wakifuatilia maelezo yaliyokuwa yakitolewa na mtoa mada katika mjadala huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya FNB Dave Aitken (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Nakuroei Investement Company LTD, Engineer Samwel Mollel.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya FNB Dave Aitken (kushoto) akiwa na baadhi ya washiriki wa mjadala huo ambao wakiwa na zawazi zao walizoshinda katika bahati nasibu iliyochezeshwa baada ya mjadala huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya FNB wakifuatilia presentation iliyokuwa ikifanywa na Mchambuzi wa Tafiti Nema Ramkhelawan kutoka benki ya FNB, Afrika Kusini.

KAMPENI ZA CCM JIMBO LA CHALINZE ZAENDELEA KWA KASI KATIKA HATUA ZA LALA SALAMA

$
0
0
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na vijana wajasiriamali wa UVCCM,Mara baada ya kufungua Shina la vijana la mshikamano Visakazi,lililopo kwenye kata ya Ubena Zomozi leo April 1,2014.
Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akizungumza jambo na mmoja wa wafugaji wa Kimasai wa Tawi la Kivuga kata ya Ubena Zomozi wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM za Ubunge jimbo la Chalinze,leo April 1,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wakazi wa kijiji cha Tokamisasa,Kata ya Ubena Zomozi wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM zinazoendelea kufanyika katika Kata mbali mbali ndani ya Jimbo la Chalinze leo April 1,2014.
Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akishiriki kucheza muziki na wananchi wa kitongoji cha Mbuyu kijiji cha Tokamisasa,Kata ya Ubena Zomozi,Wakati wa muendelezo wa mikutano yake ya kampeni za ubunge jimbo la Chalinze uliofanyika leo April 1,2014.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI.
Viewing all 110160 articles
Browse latest View live




Latest Images

<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596347.js" async> </script>
<script src="https://jsc.adskeeper.com/r/s/rssing.com.1596344.js" async> </script>