Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 401 | 402 | (Page 403) | 404 | 405 | .... | 3270 | newer

  0 0

  Meneja Mkuu wa kampuni ya Global Publishers Ltd, Abdallah Mrisho, akielezea mchakato wa kumpata 'Mwanamke wa Mwaka' utakavyokuwa. Kushoto ni Mratibu wa Matukio wa Global Publishers, Luqman Maloto.
  Wanahabari wakiwa kazini.
  Luqman Maloto akisistiza jambo kwenye mkutano huo.

  KAMPUNI ya Global Publishers Ltd ambao ni waandaaji wa shindano la kumtafuta mwanamke bora wa mwaka ambaye mchango wake wa maendeleo kwa jamii umewazidi wenzake, imethibitisha fainali hizo kufanyika keshokutwa Jumamosi.
  Akizungumza na wanahabari kwenye Hoteli ya Atriums, Jijini Dar es Salaam, Meneja Mkuu wa kampuni hiyo, Abdallah Mrisho, amesema fainali hiyo itafanyika mjini Dodoma ambapo mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye atawakabidhi tuzo washiriki wanne walioingia fainali na kumkabidhi tuzo maalum mmoja kati yao aliyewazidi wenzake alioingia nao fainali.
  Washiriki walioingia fainali ni Prof. Anna Tibaijuka, Dk. Asha-Rose Migiro, Anna Kilango Malecela na Dk. Maria Kamm.
  (PICHA : RICHARD BUKOS / GPL )

  0 0
 • 03/27/14--05:53: MWANZA ARE YOU READY?

 • 0 0  0 0

   Na Saidi Mkabakuli 
  Maendeleo ya ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Julai mwaka huu kufuatia kuendelea vyema kasi ya kundaza bomba hilo. 
  Wakizungumza na wakaguzi wa miradi ya maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Wahandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela na Mhandisi Omary Kitiku wamesema kuwa kasi ya sasa ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo kijiji cha Madimba, mkoani Mtwara inatia moyo na hivyo kuashiria kukamilika kwa mchakato huo kwa wakati. 
  “Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 za bomba la gesi kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam zimeshatandazwa hali inayokwenda sambamba na mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiki,” alisema Mhandisi Yagela. 
  Kwa mujibu wa Mpangokazi wa ujenzi wa kiwanda hiko hadi kufikia mwisho wa Julai kiwanda kinatakiwa kukamilika, na mpaka sasa, makazi ya wafanyakazi imekamilika. 
  Akizungumza wakati wa ukaguzi huo, Mmoja wa viongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alisema kwamba kukamilika kwa bomba hilo kunatoa mwanya wa kukamilika kwa wakati uzalishaji wa umeme katika vituo vya Kinyerezi, jijini Dar es Salaam. 
  “Kukamilika kwa bomba hili kunatoa fursa ya kwa Mradi wa kuzalisha umeme kiasi cha Megawati 150 na Megawati 240 kwa kutumia gesi asilia vilivyopo Kinyerezi, jijini Dar es Salaam,” alisema Bibi Mwanri. 
  Kwa mujibu wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16), Miundombinu ni kipaumbele cha kwanza, hasa uwekezaji mkubwa katika miundombinu ya nishati ambapo nguvu kubwa imewekwa katika uwekezaji wa miundombinu ya nishati ambapo utekelezaji wa ujenzi wa bomba la gesi Mtwara hadi Dar es Salaam unafanywa sambamba na ujenzi wa mitambo miwili ya kuzalisha umeme kwa kutumia gesi katika eneo la Kinyerezi Dar es Salaam. Serikali imeandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 -2015/16) wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. 
  Lengo kuu la Mpango huu ni kufungulia fursa za ukuaji uchumi wa nchi ili kuweka misingi ya ukuaji mpana wa uchumi na unaolenga watu walio masikini zaidi. 
  Mpango wa Kwanza wa Maendeleo wa Miaka Mitano unawianisha katika mfumo mmoja wa mipango mbalimbali ya maendeleo ya kitaifa ili kutoa mwongozo wa utekelezaji na kuipa Serikali fursa na mfumo rasmi wa ufuatiliaji na tathmini wa miradi ya maendeleo kitaifa. Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
   Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha michoro ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea eneo la ujenzi huo, Madimba, mkoani Mtwara. Wanaotazama ni wakaguzi hao, kutoka kushoto ni Prof. Longinus Rutasitara, Bibi Salome Kingdom, Bibi Florence Mwanri na Bw. Jordan Matonya.
   Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais ikijionea maendeleo ya ujenzi wa kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara.


    Vongozi wa Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Prof. Longinus Rutasitara (Kushoto) na Bibi Florence Mwanri (Kulia) wakiangalia moja ya bomba la kusafirishia gesi. Bomba moja lina uzito wa tani tano na urefu wa mita 11. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 zimeshatandazwa.
  Mhandisi wa Ujenzi kutoka Shirika la Mafuta Tanzania (TPDC), Mhandisi Mwita Yagela (Kulia) akiwaonesha mabomba ya kusafirishia gesi Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipotembelea baadhi ya maeneo yanakopita mabomba hayo. Mpaka sasa jumla ya kilomita 350 kati ya kilomita 492 zimeshatandazwa.  

  Mafundi wakiendelea na ujenzi wa makazi ya wafanyakazi katika kiwanda cha kuchakata gesi kilichopo Madimba, mkoani Mtwara. 


  0 0

  Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, ameelezea kuridhishwa kwake na hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miradi mitatu inayoendelea kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume. 
  Miradi hiyo inahusisha ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege, ujenzi wa uzio wa eneo la uwanja wa ndege, pamoja na ujenzi wa jingo jipya la abiria (Terminal 2). 
  Akizungumza katika ziara ya kutembelea miradi hiyo huko uwanja wa ndege wa Zanzibar, Maalim Seif amesema hatua iliyofikiwa inatia moyo, na kuwataka wakandarasi na wasimamizi wa miradi hiyo kuhakikisha kuwa inakamilika kwa wakati. 
  Amesema Serikali kwa upande wake itaweka mkakati wa makusudi ili iweze kumaliza kuwalipa fidia wananchi ambao bado hawajalipwa, na kuruhusu ujenzi wa uzio uweze kukamilika kwa akati. 
  Mapema meneja wa mradi wa ujenzi wa uzio huo Bw. Frederick Nkya, alimueleza Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar kwamba hadi sasa tayari asilimia 73 ya ujenzi huo imeshakamilika. 
  Hata hivyo amesema changamoto kubwa inayowakabili ni eneo la mita elfu tatu na mia moja ambapo sehemu kubwa ya eneo hilo bado wananchi hawajalipwa fidia. 
  Amefahamisha kuwa hadi sasa eneo la mita elfu mbili na mia saba ndilo ambalo halijafanyiwa tathmini kuweza kuwalipa wananchi walioko katika maeneo ya mradi huo. 
  Miradi ya ukarabati na ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka (Taxiway) pamoja na sehemu ya maegesho ya ndege (Apron) katika uwanja huo inafadhiliwa na Benki ya Dunia pamoja na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo mradi wa ujenzi wa uzio wenye urefu wa mita 11,690 katika uwanja huo, unatekelezwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pekee, ambapo zaidi ya shilingi bilioni sita zitatumika hadi kukamilika kwa mradi huo. 
  Kuhusu mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria ambao awali ulikumbwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa eneo la mradi, meneja wa mradi huo Bw. Ibrahim Zhang, amesema kazi hiyo sasa inaendelea vizuri. 
  Mradi wa ujenzi wa jingo jipya la abiria awali ulitiwa saini mwezi wa Septemba 2009 baina ya Wizara ya Miundo mbinu na Mawasiliano na Kampuni ya ujenzi ya Beijing Construction Engineering Group ya China, lakini baadae serikali iligundua kuwa ukubwa wa jengo uliopendekezwa mwanzo haukidhi haja. 
  Hivyo Serikali ilikubaliana na mkandarasi kuongezwa ukubwa wa jengo kutoka mita 15,600 hadi mita 17,800 kwa ongezeko la fedha dola za kimarekani milioni 11 nukta 8, na kufanya gharama za mradi huo kufikia dola la kimarekani milioni 82.2
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiangalia ramani ya ujenzi wa miradi mitatu ya uwanja wa ndege wa Zanzibar, alipofanya ziara ya kutembelea miradi hiyo.
    Mtathmini wa viwango vya ujenzi wa miradi hiyo Bw. Mohd Juma, akitoa maelezo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais kuhusiana na ujenzi huo.
   Meneja wa Mradi wa ujenzi wa njia za kupitia ndege wakati wa kuruka Frederick Nkya akionyesha ramani ya ujenzi huo.
  4.  Meneja wa mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria bw. Ibrahim Zhang, akimueleza Maalim Seif hatua zinazoendelea za ujenzi huo.
   Meneja wa mradi wa ujenzi wa jengo jipya la abiria bw. Ibrahim Zhang, akimueleza Maalim Seif hatua zinazoendelea za ujenzi huo.
   Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Mhe. Maalim Seif Sharif Hamad, akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Wizara ya Miundo mbinu na mawasiliano, viongozi wa uwanja wa ndege wa Zanzibar pamoja na wakandarasi wa miradi ya ujenzi katika uwanja wa ndege wa Zanzibar. Picha na Salmin Said, OMKR.

  0 0
 • 03/27/14--06:13: Article 17


 • 0 0

  Ni swali ambalo kila mtu huwa anajiuliza hasa ukizingatia kuwa takwimu zinaonesha kwamba wanawake ni wengi zaidi ya wanaume katika jamii. Kama ni hivyo, kwa nini wagombea wengi wa nafasi mbali mbali za uongozi ambao ni wanawake hushindwa katika chaguzi? 
  Je, ni kwamba wanawake hawapendi kuwapigia kura wanawake wenzao? Na kwa nini wanawake hawachaguani? Sikiliza maoni ya wadau wengi hapa kwa kutazama video hii:

  0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeanza mchakato wa kuendeleza uwanja wake uliopo eneo la Mnyanjani jijini Tanga.

  Shughuli inayoendelea kwa sasa ni kupima udongo (soil test) na kuandaa michoro kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha michezo (Sports Complex) ukiwemo uwanja wa mpira wa miguu na majukwaa yake.

  TFF imetuma maombi rasmi kwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro kuomba eneo la kujenga kituo cha michezo ikiwemo uwanja wa mipira wa miguu na majukwaa yake.

  Pia Mkuu wa mkoa ameombwa kuingilia kati kuwaondoa wafanyabiashara waliovamia uwanja wa mpira wa miguu wa Jamhuri (King George Memorial ground) mjini Moshi.

  TFF inawakumbusha viongozi wa vyama vya mikoa ambao hawajaomba maeneo ya kujenga vituo vya michezo vikiwemo viwanja vya mpira wa miguu, waongeze jitihada za kufanya hivyo, TFF itawaunga mkono.

  TFF inachukua fursa hii kuvipongeza vyama vya mpira wa miguu ambavyo ama tayari vimeshachukua hatua au viko mbioni kuchukua hatua kutafuta na kuendeleza maeneo kwa ajili ya matumizi ya mpira wa miguu.

  TFF inaahidi kuunga mkono juhudi hizi na pale itakapohitajika kuongeza nguvu haitasita kufanya hivyo.

  Wakati huo huo, TFF inalishukuru Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa kugharamia uwekaji nyasi za bandia kwenye Uwanja wa Kaitaba, na pia kusaidia uendelezaji wa uwanja wa TFF wa Tanga.

  JAMAL MALINZI
  RAIS
  SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)

  0 0

  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika jana, Machi 26, mwaka huu, katika eneo la Kigamboni, wilayani Temeke akiwa katika ziara yake mkoani Dar es Salaam, kusikiliza kero za wananchi na kujadiliana nao njia ya kuzitatua na kukagua utekelezaji wa ilani ya Chama. 


     Akizungumza na wananchi wa Kigamboni, Ndugu Kinana ameahidi kulichukua suala linaloonekana kuzua mgogoro mkubwa baina ya wananchi na serikali la ujenzi wa mji wa kisasa wa Kigamboni,  na ameahidi kulifikisha kwenye vikao vya ngazi ya juu kabisa vya CCM kwa uamuzi wa uhakika na wa kudumu.
    Kinana amesema, baada ya kulifikisha kwenye vikao vya juu ya CCM atarejea tena Kigamboni kuzungumza na wananchi ili kuwapa majibu sahihi.
     "Hapa ni lazima tujue, wazo la kubuniwa mradi huu lilianzishwa na nani, kwa lengo na maslahi gani, na wananchi ninyi mnaoishi hapa mlihusishwa kwa kiwango gani kuhakikisha mchakato mzima unakuwa halali kwa mujibu wa sheria za nchi", alisema Kinana.

   
  Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Kinana alipoowahurubia katia mkutano huo
   Kassim Abdallah mkazi wa Vijibweni Kigamboni akitoa hoja zake mbele ya Kinana kuhusu mradi huo

  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia Mkutano wa hadhara mjini Muheza jana jioni. Rais Kikwete anatarajia kuhitimisha ziara yake ya kikazi mkoani Tanga leo. Picha na Freddy Maro.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na mtoto Hassan Mustafa(13) mwenye tatizo la kudumaa muda mfupi baada ya Rais Kikwete kukagua na kuzindua maabara katika shule ya sekondari ya Potwe, wilayani Muheza 

  0 0

  Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza wakati swa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki mashindano ya NSSF Media Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Machi 29. 
   Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akizungumza wakati swa hafla ya kukabidhi vifaa kwa timu zinazoshiriki mashindano ya NSSF Media Cup yanayotarajiwa kuanza rasmi Machi 29.
   Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume akimkabidhi vifaa vya michezo, mwakilishi wa timu ya Star Tv, Tom chilala kwa ajili ya mashindano ya NSSF CUP yanayotarajiwa kuanza Machi 29.
   Meneja Kiongozi Idara ya Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Eunice Chiume (kushoto), akimkabidhi vifaa vya michezo, mwakilishi wa Kampuni ya Free Media Ltd, wachapishaji wa magazeti ya Tanzania Daima na Sayari, Francis Dande kwa ajili ya mashindano ya NSSF MEDIA CUP yanayotarajiwa kuanza Machi 29, 2014. Kwa habari kamili na picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

  Mheshimiwa michuzi tunashukulu sana kwa kazi yako ya kutujulisha yanayoendelea TANZANIA leo naomba unipe nafasi niweke ya moyoni mwangu na maoni yangu kuhusu huu mstakabali wa kupata katiba ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
  Mengi yamekuwa yakisemwa sana kuhusu hii katiba au ni muundo ghani wa muungano tunaoutaka,watu wengi na wana siasa wamesahu kwamba muungano huu na katiba hii ya zamani ndio umetufanya tuwe na undungu  na pia tuwe na amani mpaka hapa tulipo.
  Watu wengine wameandika katiba baada ya kumwaga damu na nitatowa mfano Kenya,Rwanda,Uganda,Burundi na majirani zetu wa Congo je hawa wana siasa wa CCM,CUF,CHADEMA haya yote mnaonekana kwenye macho yenu na kwenye masikio yenu hamkuyaona au kuyasikia??

  Wazee wetu waliotangulia walikuwa na nia nzuri sana lakini leo inaonekana ndoto zao zitakufa na Muungano wetu  ambao umetupa amani na maendeleo yetu tuliyonayo mpaka leo yako mashakani, kutokana na watu wanaosema wanawalilia waTanzania kumbe  ni watu walio na agenda ambazo ni za kutumikia vibaraka wa nje.
  Ndugu WaTanzania tume ya Mzee Warioba ilifanya kazi imekusanya maoni yaliyotolewa na watu na hii aiweze kuwa ndio katiba ya watanzania bali ni maoni ya wananchi na mwongozo wa kuweza kuandika katiba ya waTanzania,na baadhi ya mambo yaliyowekwa mule ndani mengine ni mazuri na mengine nilazima yafanyiwe mabadiriko tupende au tusipende kwa mfano sijawahi kuona MP anakuwa na kikomo,ili nasema  USA,UK,ambao tunawaona ni kama mababa wa demokrasia hawana kikomo,pili Tanzania ina watu milioni 44 au tano itakuwaje bunge liwe na wabunge 75 ,kuna mambo mengi ya kujadili na siyo jambo la Muungano  pekee. Katiba ina mambo mengi jamani!
  Ndugu Wa Tanzania Raisi ametowa maoni yake mazuri na kasoro zilizomo katika hiyo rasimu hakuja kuwafundisha hao wabunge au kuwaambia nini cha kufanya bali alikwenda kufungua bunge na kutowa maoni yake na kuwaachia nyinyi wabunge kazi ya kufanya  lakini leo nashangaa wabunge wa upinzani wameanza kusema maneno ya kuropoka ropoka mbunge aliye onysha amekoma na kutowa maneno ya busara ni Mheshimiwa Zito. Hongera ndugu Zito.
  Ndugu Watanznia napenda kuwaomba hawa wabunge tumewatuma kutupatia katiba na siyo maneno tunataka katiba ya watanzania siyo ya maoni ya CHADEMA au CCM au CUF au ya Warioba au Kikwete muache maneno wakati wa meneno umekwisha tunataka mkae na kazi ianze mwongozo upo na kilicho baki ni nyinyi sasa mkae hapo dodoma muanze kazi rasimu mko nayo na katiba ya zamani ipo tunataka mtuandike katiba ya  Watanzania ambayo itamlinda na kumpa haki yake MTanzania wa Bara na Visiwani awe kilema,mtoto,mzee,wa makamu,au kijana,katiba ambayo ina samini utamaduni wetu na kulinda mila zetu pamoja na kulinda mali zetu na ambayo itakuwa  mwongozo  wa uongozi wa kisiasa,kiuchumi,sheria,demokrasia,na accountability na responsibility na mwongozo elimu na health ,katiba itakayo mtowa au kumpa mwongozo wa kumtowa mtanzania kwenye umasikini.

  NINGEPENDA KUMNUKUHU BABA WA TAIFA KIPENZI CHA WATANZANIA THE GREAT BLACK WA KARNE YA ISHIRINI ALIVYOSEMA PALE DODOMA WAPIGA KURA TUPATIHENI RAISI ANAYE FAA.  

  NA MIMI NASEMA NYINYI WABUNGE WA CCM, WA CHADEMA,CUF,DP NA HAO WABUNGE WA VYAMA VINGINE NA VIONGOZI WENU TUNATAKA KATIBA YA WATANZANIA SIYO YA MAONI ,

  WAKATI NI HUU NA MUDA NI HUU MTUPE KATIBA YA WATANZANIA NA SIYO YENU NYINYI MNAYOTAKA TUNATAKA KATIBA YA WATANZANIA, MWONGOZO MKO NAO.

   IT IS TIME, WE ARE  TIRED OF YOUR NOISE. 
  IT'S  TIME YOU  WENT TO WORK .
  Bwana michuzi asante  kwa kunipa 
  nafasi ya kutowa maoni yangu

  Yusef Israel

  0 0

  Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba wana wajibu wa kutekeleza kazi zao kwa mujibu wa Kanuni walizojiwekea za kuendesha Bunge hilo ili kiuwa mfano mwema wa matendo mazuri mbele ya jamii ya Watanzani kutokana na dhima waliyokabidhiwa. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati akizungumza na wana Habari mbali mbali wanaoripoti matukio ya Bunge la Katiba hapo katika Ukumbi wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mjini Dodoma. 
  Balozi Seif alisema vitendo vya uvunjifu wa amani kila siku ili Bunge Maalum la Katiba liahirishwe kwa sababu za Kisiasa na msimamo ya kisiasa inayofanywa na baadhi ya wajumbe wa Bunge hilo si jambo jema. 
  Alisema mchakato huo wa Bunge Maalum la Katiba umekuwa ukishuhudiwa na Wananachi walio wengi Nchini kutawaliwa na wanasiasa wanaoonyesha dhahiri nia zao za kutaka kuvunja Muungano kutokana na kauli zao. 
  Alieleza kwamba kaulio nyingi zinazotolewa na kushuhudiwa na Wananchi kupitia vyombo vya Habari zimekuwa na muelekeo wwenye kuchionganisha Wananchi wa pande mbili za Muungano. 
  “ Inasikitisha sana kuona baadhi ya wabunge wa Bunge la Katiba wanaendeleza ushabiki wa Kisiasa ndani ya Vikao vya Bunge hilo kwa kutengeneza mbinu za kuongeza muda wa Vikao wakisahau kwamba kodi za Wananchi zinapotea bila ya kufanya kazi zilizokusudiwa kufanywa na Waheshimiwa sisi Wajumbe “. Alisema Balozi Seif. 
  Balozi Seif alifahamisha kwamba pamoja na hatua nzuri iliyofikiwa na Wajumbe wa Bunge hilo ya kujadili Rasimu ya Katiba na kuweza kubadilisha, kuboresha, kuongeza au kupunguza lakini bado zipo changamoto zinazolikabili Bunge hilo. 
  Alizitaja baadhi ya changamoto hizo kuwa ni pamoja na kukosekana kwa uvumilivu miongoni mwa Wajumbne wa Bunge Maalum, Bunge kutawaliwa na hisia za kisiasa zaidi badala ya kuweka maslahi ya Taifa mbele pamoja na kuwepo kwa vikundi vya watu wachache wasiotaka mchakato huo wa Katiba Mpya kuendelea kutokana na utashi wa kisiasa. 
  Akizungumzia suala la Mikutano ya hadhara inayoanza kuchukuwa sura mpya ya kutaka kugawanywa Wananchi ndani ya kipindi hichi cha mchakato wa Bunge la Katiba Balozi Seif aliwatahadharisha Wananchi kuwa macho na tabia hizi zinazoonekana kutaka kuleta mgawanyiko wa Jamii kati ya Tanzania Bara na Zanzibar. 
  Alisema kauli za Baadhi ya Viongozi wa Kisiasa kuwataka Wananchi wa Upande mmoja wa Muungano kuacha shughuli zao za Kimaisha na kurudi katika makazi yao waliyozaliwa ni kuashiria jinsi viongozi hao walivyo na nia mbaya katika kuvunja Umoja wa Nchi na Muungano uliopo hivi sasa. Balozi Seif alieleza matumaini yake kwamba Muungano uliopo hivi sasa wa Tanzania itaendelea kudumu, kuwepo na kuendelea kwa kipindi kirefu kijacho kwa vile bado unaridhiwa na kukubalika na jamii ya wananchi walio wengi ndani ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Tume ya Mabadiliko ya Katiba na Uongozi wake kwa kazi waliyoifanya ya kukusanya maoni ya Wananchi pamoja na kumshukuru Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete na Rais wa Zanzibar Dr Ali Mohd Shein kwa muongozo wao wa muelekeo wa mchakato huo. 
  Alisema dhamira ya Viongozi hao iko wazi na dhati katika kuhakikisha Taifa hili la Tanzania linapata katiba Bora ya Wananchi kupitia Bunge Maalum la Katiba lililoundwa kwa mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Sura ya 83, toleo la Mwaka 2012. 
  “ Kazi iliyopo mbele yetu ni Bunge Maalum kukaa kama Kamati ambazo ni 12 ili kujadili kwa kina rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ili kupata Rasimu nzuri itakayoleta faida kwa Wananchi “. Alifafanua Balozi Seif. Balozi Seif Ali Iddi.
  Aliwashukuru watendaji wa vyombo mbali mbali vya Habari kwa kazi nzito wanayoendelea kuifanya katika kuwapatia Taaluma na Habari Wananchi juu ya masuala tofauti ikiwemo mchakato wa Katiba unaoendelea Mjini Dodoma. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwaasa Wanahabari hao kwamba ni vyema wakaelewa kuwa bado wanakabiliwa na dhima ya kuielimisha Jamii umuhimu wa kuichunga amani iliyopo hapa Nchini. 
  “ Napenda muelewe kwamba bado mna dhima ya kuielimisha jamii umuhimu wa kuichunga amani iliyopo Nchini “. Alisisitiza Balozi Seif. 
  Akijibu baadhi ya maswali ya wana Habari hao likiwemo lile linalodaiwa kwamba Zanzibar imevunja Katiba kwa kubadilisha baadhi ya vifungu vya sheria na ikiwemo Zanzibar kuitwa Nchi, Balozi Seif aliwatoa hofu wana habari hao kwamba Zanzibar kamwe haijavunja katiba kwa vile haina Utaifa. 
  Alisema Utaifa uliopo na unaoendelea kutumiwa na kujuilikana ni ule wa Utanzania akatolea mfano masuala ya Kimataifa yanashughulikiwa na Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania. 
  “ Hebu nikuulizeni Nyinyi Waandishi mna kumbu kumbu yoyote mnayoijua au kuikumbuka kwamba kuna Balozi yeyote wa Zanzibar katika Mataifa ya Kigeni ? “. Aliuliza Balozi Seif.
    Balozi Seif akizungumza na Wana Habari waliojumuika na Baadhi ya Mawaziri wa SMZ katika Ukumbi wa TAMISEMI Mjini Dodoma. Picha na Hassan Issa – OMPR – ZNZ.


  0 0

  2face has dominated the music industry for years and continues to push creative boundaries at home and abroad. His most recent album birthed some of his biggest songs to date including the soulful hit, 'Dance In The Rain'.

  The Hypertek Digital/960 Music Group megastar has just released a brand new video for ‘Dance in the Rain’. This visually stunning video is unlike anything that audiences have seen from 2face before.

  ‘Dance in the Rain’ is one of his most popular songs off his AWAY AND BEYOND PLUS album. This album features remixes of some of his songs with artists such as T-Pain and Cabo Snoop among others.


  0 0

  Askari wakiwa wamebeba mwili wa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, John Tupa baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege Dodoma leo Machi 27, 2014. Marehemu ataagwa kwenye viwanja vya Nyerere Dodoma Machi 28, 2014 kabla ya kusafirishwa  kwenda kilosa kwa mazishi. 
  Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu.

  0 0

   Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA cha Angola Comrade Julio Mateus Paulo akipokelewa na Ndg. Phares Magesa Mjumbe wa NEC kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alipowasili leo. Katibu Mkuu huyo wa Chama kinachoongoza Angola amewasili Dar es Salaam  kuhudhuria Mkutano wa vyama vya Kisoshalisti ulimwenguni unaoanza kesho katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere.
   Ndg.Magesa (MNEC) akiwa katika mazungumzo mafupi na Comrade Paulo katika ukumbi wa VIP uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere
  Katibu Mkuu wa Chama cha MPLA cha Angola Ccomrade Julio Mateus Paulo akiongozana na  Ndg. Phares Magesa Mjumbe wa NEC kwa niaba ya Katibu Mkuu wa CCM  uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere baada ya kuwasili leo

  0 0


  0 0

   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akilakiwa na Wananchi wakazi wa Kijiji cha Chahua,Kata ya Bwilingu leo Machi 27, 2014 wakati wa Muendelezo wa Kampeni zake za kuomba ridhaa kwa Wananchi hao ya kuwa kiongozi wao kwa Maendeleo ya Jimbo la Chalinze.Picha zote na Othman Michuzi.
   Meneja wa Kampeni za CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Steven Kazidi akiwasisitiza Wananchi wa Kijiji cha Chahua kuzitunza vyema Shahada zao za kupigia kura,ili siku ikifika ya kupiga kura wasipate shida na waweze kupiga kura Mtu anaefaa kuwa Kiongoizi wa Jimbo la Chalinze. 
   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia na kutoa Sera zake kwa wananchi wa Kijiji cha Chahua,Kata ya Bwilingu leo Machi 27, 2014 .
   Mwenyekiti wa Kijiji cha Chahua,Christina Kejeli (kulia) akitoa maelezo ya Maendeleo ya Kijiji kwa Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) wakati wa muendelezo wa Mikutano ya Kampeni iliyofanyika leo Machi 27, 2014 katika vijiji vya Chahua na Matuli,Kata ya Bwilingu.
   Diwani wa Kata ya Bwilingu,Ahmed Kalama akisisitiza jambo wakati wa kuzungumzia mafanikio ya Kata yake pamoja na Changamoto ambazo bado hazijafanyiwa kazi ndani ya Kata hiyo,mbele ya Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze.
   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwasalimia wakina Mama wa jamii ya watu Wafugaji (Wamasai) wakati alipowasili kwenye Kijiji cha Matuli kwa ajili ya kuendelea na Mikutano ya Kampeni zake za kuomba ridhaa ya kuwa Mbunge wa Jimbo la Chalinze.  0 0

  Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pasifiki (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiongoza kikao cha Kamati ya Mabalozi wa ACP leo Brussels. Kikao hicho kimeidhinisha Euro 350 milioni za kusaidia utekelezaji wa shughuli za kulinda amani Afrika zitakazotelewa na Jumuiya ya Ulaya kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Ulaya (EDF).

  0 0

  Since 2010 various Vendors and about to be married couples have benefited being part of HARUSI TRADE FAIR.

  This year, 2014, we shall celebrate 5 years of its existence since the Wedding fair inception in year 2010, with more than 6,000 persons who have visited the fair over the years specifically dedicated to the Bride and Groom to be, and their friend and family and wedding industry stakeholders.

   
  CELEBRATING FIFTH ANNIVERSARY
  CONTACT US:
  SMS/WHATSAPP: +255715303880
  EMAIL: info@harusitradefair.com

  Your A-Z guide to everything WEDDING
  Participate at this year Wedding Expo by securing a Full Tent, Half tent space or simply just booking a table.

  To DOWNLOAD the form NOW, Kindly CONTACT US

  To Contribute an article towards the HARUSI MAGAZINE, kindly contact us before 2 April 2014

  To Partner/Sponsor theWedding Fair Call Mr Omary on +255787747918

  If you NO LONGER want to receive email Updates, KINDLY UNSUBSCRIBEbelow. We Value you as our customer and apologies for any inconvenience caused.

  HARUSI TRADE FAIR is organized by 361 DEGREES


  Copyright © 2014 Harusi Trade Fair, All rights reserved.

  as part of our commitment to compliance with our dissemination of information, your email will NOT be given to any third Party

  Our mailing address is:
  Harusi Trade Fair
  48B, Drive Inn, Namanga
  P.O. Box 10684
  Dar Es Salaam
  Tanzania

  Add us to your address book

older | 1 | .... | 401 | 402 | (Page 403) | 404 | 405 | .... | 3270 | newer