Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 400 | 401 | (Page 402) | 403 | 404 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Sehemu ya wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Mkoani Rukwa katika Wilaya ya Kalambo (NHIF) wakiwa katika Mkutano wa kujadili umuhimu wa wa huduma za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na kuangalia namna ya kuzindua rasmi mpango wa kuchangia kabla ya kuugua katika Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo.
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akifungua rasmi Mkutano wa wadau wa mfuko wa afya ya jamii (CHF) Wilaya ya Kalambo Mkoani Rukwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya jana Mjini Matai. Katika salamu zake za ufunguzi alizitaka halmashauri Mkoani Rukwa kuhakikisha kuwa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) unakuwa ni ajenda ya kudumu katika vikao vyake vyote vya maamuzi, Aidha alizitaka Halmashauri ziandae utaratibu wa kuzitambua familia zisizo na uwezo wa kuchangia na zitenge fedha kutoka katika vyanzo vyake ili kuzilipia familia hizo na kuhakikisha kuwa hakuna mkazi wa Halmashauri husika anapoteza maisha kwa kukosa fedha za kuchangia katika Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). Mwanachama wa mfuko huo anatakiwa kuchangia Tsh 10,000/= kwa mwaka ambao ni mchango wa kaya moja isiyozidi watu sita.
  Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo Ndugu Filbert Ngaponda (Mwana wa Magreth) akiwatambulisha washiriki wa Mkutano huo wakiwepo watendaji wa Serikali na madiwani wa halmashauri hiyo pamoja na wageni mbalimbali waalikwa ambao ni wadau wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (CHF).  
  Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakifuatilia mada mbalimbali.
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta akihutubia washiriki wa mkutano huo.
  Ofisa Habari na Mawasiliano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa Ndugu Hamza Temba wa pili kushoto akiwa na baadhi ya watumishi wa Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NHIF) Mkoa wa Rukwa mara baada ya Mkutano huo.
  Wadau wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoani Rukwa wakijadili jambo kuhusiana na huduma za mfuko huko. Kulia ni Ramadhan Juma Ofisa Habari Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo, Hamza Temba Ofisa Habari Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa na Ndugu Mussa Hajj Chewa Mkaguzi wa ndani Ofisi ya Mkurugenzi Kalambo
  Picha ya Pamoja ya Mgeni Rasmi Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, viongozi wa Serikali, Muwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Watumishi wa ofisi hiyo Mkoa wa Rukwa. (Picha na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @Rukwareview.blogspot.com)

  0 0

   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia chama cha AFP, Ramadhani Mgaya akinadiwa na  Mkurugenzi wa habari na uenezi wa AFP kitaifa, Mwalami Uwesu wakati wa kampeni za mgombea huyo katika ebneo la sokoni Chalinze mjini Kata ya Bwilingu Chalinze.
   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kupitia chama cha AFP, Ramadhani Mgayaakijinadi kwa wananchi wa jimbo la Chalinze wakati wa kampeni zake za kuwania Ubunge jimboni humo.

  0 0

  Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mhe. Bernard K. Membe (Mb) pamoja na Mgeni wake Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani Mhe. Steinmeier walipokuwa wakiongea na Waandishi wa Habari (hawapo pichani)  
  Waziri Membe (Mb) akifafanua jambo kwa Waandishi wa Habari (hawapo pichani)
  Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Lazaro Nyalandu akisalimiana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Mhe. Steinmeier. Wakati wa ziara hiyo Mhe Steinmeier alimkabidhi Waziri Nyalandu ndege ndogo kwa ajili ya kukabiliana na uwindaji haramu  wa wanyamapori.
  Waziri Membe akiagana na Waziri Steinmeier mara baada ya kumaliza ziara yake nchini. 
  Mhe. Steinmeier akiagana na Balozi Philip Marmo.
  Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   Meneja wa benki ya NIC Mbuche Mgawa  wa nne kulia akipokea maelezo kutoka kwa bibi Mary Robert Kaswende meneja wa kituo cha Dymphna Special school iliyopo sakina kwa idd mara baaada ya kuwasili shuleni hapo.

   Watoto wa shule maalum ya Dymphna wakiwasikiliza wageni ambao ni wafanyakazi wa benki ya NIC
   Watoto wa shule hiyo wakiwa wamebeba bango la kutoa shukrani kwa benki ya NIC
  Watoto wa shule hiyo wakiwa wamebeba bango la kutoa shukrani kwa benki ya NIC, na BENKI YA NIC wakiwa pamoja na misaada waliyobeba na watoto wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya ziara ya kuwatembelea kituo hichon ambvacho ni maaalum kwa ajili ya kutoa elimu kwa watoto wenye matatizo ya mtindio wa ubongo.

  0 0


   Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi wa CCM Nape Nnauye akizungumza na Mwenyekiti wa UWT Kata ya Ubena Jesca Daudi ambaye alivunjwa mkono na watu wanaodaiwa kuwa ni Viongozi wa CUF waliovamia ofisi ya kata kwenye kijiji cha Tokamisasa.
   Katibu wa Wilaya ya Makete Miraji Mtaturu akizungumzia tukio lililomkuta  Mwenyekiti wa UWT Kata ya Ubena Jesca Daudi ambaye alivunjwa mkono na wanaodaiwa kuwa Viongozi wa CUF waliovamia ofisi ya kata kwenye kijiji cha Tokamisasa kuwa ni kitendo cha kinyama na cha kupingwa kwa nguvu zote na kitendo hicho kimemvua sifa za kuwa mgombea ubunge  wa CUF.

  0 0

  Bondia Mussa Mchopanga kushoto akionesha ufandi wa kutupa makonde kwa Azizi Swalehe wakati wa michuano ya mashindano ya Klabu bingwa ya ngumi mkoa wa Dar es salaam. Mchopanga alishinda kwa K,O ya raundi ya kwanza 

  Bondia Azizi Swalehe akiwa chini baada ya kupigwa konde zito na Mussa Mchopanga aliyesimama Mchopanga alishinda kwa K,O ya raundi ya kwanza.

  Bondia Maulidi Athumani kushoto akioneshana umwamba wa kutupiana makonde na John Christia wakati wa mashindano ya klab bingwa ya mkoa wa Dar es salaam Christian alishinda kwa point. Picha na Super D.

  0 0

  Na Mwene Said wa Globu ya 
  Jamii, Mahakamani
  Mtu mmoja raia wa Kenya Nelson Onyango (43), mkazi wa Kariakoo, jijini Dar es Salaam, amefikishwa katika Mahakamani akikabiliwa na mashitaka saba ya udanganyifu, kutumia kadi zisizosajiliwa, kuingiza nchini na kutumia mitambo ya simu bila kibali, kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) na kuisabishia serikali na mamlaka hiyo hasara ya Sh. Milioni 6.8. 
   Onyango alisomewa mashitaka yake leo  mbele ya Hakimu Mkazi Devota Kisoka aliyepangiwa kusikiliza kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam. 
  Jamhuri imewakilishwa na Mawakili wa Serikali Mwandamizi, Tumaini Kweka, Mwanaamina Kombakono na Mwanasheria Mkuu wa TCRA, Joannes Karungura na Inspekta wa Polisi, Jackson Kinunda. 
  Mheshimiwa Kweka alidai shitaka la kwanza, kati ya Julai mwaka 2010 na Novemba mwaka 2013, eneo la Kariakoo wilaya ya Ilala, jijini, bila halali na kwa makusudi mshtakiwa akiwa na nia ya kukwepa malipo halali alitoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa bila leseni ya TCRA. 
  Katika shitaka la pili, ilidaiwa kuwa siku na tarehe za tukio la kwanza, mshtakiwa alitoa huduma za simu za kimataifa bila kuwa na leseni ya TCRA. 
  Upande huo wa Jamhuri uliendelea kudai kuwa, shitaka la tatu, kati ya Januari na Novemba mwaka 2013, eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam, kwa nia ovu na kwa makusudi, mshtakiwa alitumia kadi za simu zenye namba 23 tofauti zisizokuwakuwa na usajili. 
  Wakili huyo Mwandamizi alidai katika shitaka la nne kuwa, siku na mahali pasipofahamika jijini Dar es Salaam, mshtakiwa aliingiza nchini mitambo ya elektroniki bila leseni ya TCRA. 
   Katika shitaka la tano, kwamba siku isiyofahamika eneo la Kariakoo, jijini mshtakiwa alisimika mitambo minne ya electroniki bila leseni ya TCRA. 
  Ilidaiwa katika shitaka la sita, Novemba 22,mwaka 22013 eneo la Kariakoo wilaya Ilala, jijini mshtakiwa akiwa na nia ovu na kwa makusudi, alitumia mitambo ya elektroniki ambayo ilikuwa haijathibitishwa na TCRA kutoa huduma ya mawasiliano ya kimataifa. 
  Katika shitaka la saba ilidaiwa kuwa, kati ya Julai mwaka 2010 na Novemba 2013, jijini Dar es Salaam, mshtakiwa akiwa hana leseni ya kumruhusu kufanya huduma za mawasiliano alichepusha simu za kimataifa na kuisababishia serikali hasara ya Sh. 6,842,880 kwa TCRA na serikali. Mshtakiwa alikana mashitaka yote na upande wa Jamhuri ulidai kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika. 
   Hakimu Kisoka alisema mshtakiwa atakuwa nje kwa dhamana kwa kuwasilisha mahakamani fedha taslimu Sh. Milioni 3.4, wadhamini wawili wanaofanya kazi katika taasisi za kuaminika. 
   Mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti hayo na alipelekwa mahabusu hadi Aprili 8, mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa.
   mtuhumiwa Nelson Onyango akiwa amepozi mahakamani akisubiri kusomewa mashitaka yake saba ya kutoa na kuchepusha mawasiliano ya kimataifa bila kibali cha TCRA. Anadaiwa kuisabishia serikali hasara ya Sh. milioni 6.8
  Mtuhumiwa Onyango (mwenye tishet iliyoandikwa LEE) wakati akisindikizwa na askari. Picha na Mwene Said wa dawati la mahakamani la Globu ya Jamii

  0 0  0 0

  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mizengo Kayanza Peter Pinda akiongea na waandishi wa habari leo mjini Dodoma juu ya mambo mbalimbali ikiwemo kuwaomba wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kuepuka mivutano na badala yake wazingatie mambo muhimu yatakayosaidia Taifa na Watanzania kupata Katiba mpya .

  0 0

   Na Richard Bagolele 
  Mradi wa kutibiti gugumaji kanda ya ziwa chini ya ufadhili wa wa mradi wa hifadhi ya mazingira ya ziwa Viktoria awamu ya pili (LVEM II) umetambulishwa rasmi wilayani Chato.
   Akiongea wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwennye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mratibu wa mafunzo hayo Bw. Emanuel Kitabo amesema lengo la kutambulisha mradi huo kwa wadau mbalimbali wa Chato ni kuhifadhi na kutunza mazingira ya ziwa Victoria vikiwemo vyanzo vyake ardhi oevu na madakio yake. 
  Bw. Kitabo Amesema lengo la kuandaa mafunzo hayo ni pamoja kuweka mfumo rahisi wa kupeana habari za udhibiti na ufuatiliaji wa shughuli za gugumaji, kuweka mfumo endelevu wa utafutaji raslimali pesa kutekeleza sheria ya udhibiti wa gugumaji ya mwaka 1999 pamoja na kuimarisha jamii kudhibiti gugumaji kibiolojia na kwa kutumia mikono. 
  Amesema njia rahisi ambayo jamii inaweza kutumia katika kudhibiti gugumaji ni pamoja na kutumia wadudu aina ya Mbawakavu ambao hushambulia gugumaji, njia nyingine ni kuondoa gugumaji kwa njia ya mkono na kudhibiti shughuli za kilimo kandokando ya ziwa. 
  Akichangia katika kikao hicho Mkuu wa Wilaya ya Chato ambaye alikuwa ni mgeni rasmi kwenye mafunzo hayo alishauri kuundwa kwa klabu kwa kila kijiji cha kupambana na udhibiti wa gugumaji. Wajumbe waliohudhuria mafunzo hayo wamesema ni lazima jamii ipewe elimu ya uharibifu wa mazingira ikiwemo kilimo kandokando ya ziwa na vyanzo vya maji. 
  Diwani wa kata ya Bwongera Mhe. Batholomeo Manunga amesema kuna kila sababu ya kusimamia sheria za ujenzi holela kandokando ya ziwa Victoria na uthibiti wa uvuvi haramu kupitia kamati za udhibiti wa mialo (BMU).
  Naye diwani wa kata ya Muganza Bw.Marco Maduka amesema suala la udhibiti wa gugumaji linatakiwa kuwa ajenda ya kudumu kwenye vikao mbalimbali kuanzia ngazi ya kijiji, kata hadi Wilaya. 
  Mradi huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miezi 18 kuanzia Desemba2013 ambapo mikoa ya Mwanza, Geita, Mara, Simiyu na Kagera itahusika katika mradi huo.
  Mradi utaandaa dodoso la ukusanyaji wa takwimu za shughuli za udhibiti wa gugumaji, kufundisha wataalamu wa kutumia dodoso la ukusanyaji wa takwimu kukusanya takwimu, kubaini maeneo yaliyoathiriwa, vikundi kazi na kuvijengea uwezo wa kudhibiti gugumaji pamoja na kuhimiza Halmashauri kutenga bajeti na mfumo endelevu wa upatikanaji wa fedha kugharamia shuguli za udhibiti wa gugumaji. 
  Gugumaji ni mmea uotao kwa kuelea majini na ni mmea hatari kwa viumbe vya majini ambao hustawi kutokana na taka kutoka viwandani, majumbani na kilimo kandokando ya ziwa. 
  Mmea huu kwa mara ya kwanza nchini Tanzania ulionekana mto sigi mwaka 1955 na baadae mto Pangani mwaka 1959 na mto Kagera mwaka 1985,
   Mratibu wa mafunzo ya udhibiti wa gugumaji Bw.  Emmanuel Kitabo akieleza lengo la mradi kwa wadau mbalimbali wa Wailaya ya Chato
   Mtaalamu kutoka LVEMP Emanuel Kitabo akionesha kwa wajumbe mdudu aina ya Mbawakavu ambaye hushambulia gugumaji
   Mtoa mada wa LVEMP Bw.Fred Kanuti Akionesha kwa wadau wa mafunzo tofauti ya mumea ulioathiriwa na mdudu aina ya Mbawakavu ambaye hushambulia gugumaji na mmea ambao haujaathiriwa na Mbawakavu
  Wadau mbalimbali wakifuatilia mafunzo ya udhibiti wa gugumaji ziwa vivtoria

  0 0

  Mkurugenzi na muasisi wa taasisi ya Tanzania Street Children (TSC), Bw. Altaf  Hirani akimkabidhi vifaa vya jezi meneja msafara wa timu ya watoto wa mitaani ya Tanzania, Majuto Ismail,  jijini Mwanza kabla ya kuondoka nchini kuelekea nchini Brazil kushiriki michuano ya kombe la dunia la watoto wa mitaani. Picha na Moses Mashalla.

  0 0

  MKUU wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo leo jijini Dar es Salaam amefungua mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yaliyowashirikishwa washiriki kutoka katika mikoa ya Dar es Salaam, Lindi, Pwani na Morogoro. Akizungumza katika hotuba yake ya ufunguzi wa mafunzo hayo yanayofanyika katika Chuo cha Mafunzo ya Jinsia kilichopo eneo la Mabibo jijini Dar es Salaam, Bi. Zuki Mihyo alisema kutokuwepo na misingi imara ya kutetea, kulinda na kudumisha demokrasia iliyojengwa kwenye misingi ya usawa wa kijinsia inayo tambulika Kikatiba kumechangia uwepo wa tatizo la unyanyasaji wa kijinsia nchini. 
  Alisema tatizo la unyanyasaji wa kijinsia licha ya kuwapata watu wa jinsia zote, limekuwa likiwaathiri zaidi wanawake na watoto wa kike tofauti na ilivyo kwa wanaume na watoto wa kiume katika jamii, hivyo kushauri kuna kila sababu ya kupambana na mifumo kandamizi inayochangia hali hiyo. 
  "...Wanawake na watoto wa kike mara nyingi wamekuwa wakifanyiwa ukatili huu na wanaume au wavulana ambao wanaweza kuwa ndugu zao wa karibu, marafiki na hata wenzi wao," alisema Mkuu huyo wa chuo cha GTI kilichopo chini ya Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP).

  Alisema suala la ukekelezaji wa mila na desturi kama vile ukeketaji, kurithi wajane na mila nyingine nyingi zinazowagandamiza wanawake na makundi ya pembezoni na kuwafanya kutokuwa na sauti wala kushiriki katika kutoa uamuzi kuanzia ngazi ya familia hadi taifa vimekuwa vikichangia ukatili wa jinsia kwa wasichana, wanawake na makundi mengine ya pembezoni.
   "...Tunaelewa kuwa wakati wa zamani mila nyingi zilikuwa na maana lakini kwa wakati huu mila hizo zimepitwa na wakati hivyo ziachwe ili kukomesha dhuluma, manyanyaso, ukandamizaji n.k, ili kuwa na usawa kwa watu wote," alisema.
   Aidha alifafanua kuwa lengo kuu la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo wa washiriki kuweza kushiriki katika kuchambua masuala ya jinsia, demokrasia na katiba mpya ili waweze kuyasimamia na kuyatetea katika mikakati mbalimbali ya maendeleo.
  Aliongeza kuwa malengo mahususi ni pamoja na kukuza uelewa na utambuzi wa uhusiano baina ya dhana za jinsia, demokrasia na katiba, kuchochea ushiriki na uwajibikaji wa asasi za kiraia na makundi maalumu yaliopo pembezoni na mchakato wa kidemokrasia na kutambua changamoto na fursa zilozopo katika kuingiza masuala ya jinsia na demekrasia kwenye katiba mpya.
   Akifafanua zaidi juu ya mafunzo hayo, mmoja wa watoa mada, Geoffrey Chambua alisema washiriki wanatoka katika ngazi ya jamii; yaani katika asasi za kiraia, vikundi vya kijamii, asasi za kidini, wajasiliamali na makundi maalumu wote kutoka katika mikoa ya Morogoro, Lindi, Pwani pamoja na Dar es Salaam yenyewe.
  Chambua alisema mafunzo kama hayo pia yanaendelea katika kanda anuai.
  Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (kulia, aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI. Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (kulia, aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya.Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI. Mkuu wa Chuo cha Mafunzo ya Jinsia (GTI), Bi. Zuki Njalai Mihyo (aliyesimama) akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya yalioandaliwa na GTI.Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya. Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tatu juu ya masuala ya Jinsia, Demokrasia na Katiba Mpya.
  Mmoja wa watoa mada wa mafunzo hayo, Geoffrey Chambua (aliyesimama katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo. Mmoja wa watoa mada wa mafunzo hayo, Geoffrey Chambua (aliyesimama katikati) akizungumza na washiriki wa mafunzo.


  0 0

  image001
  EAST AFRICAN COMMUNITY

  Tanzania and Kenya’s delay to sign a Bilateral Agreement on One Stop Border Post (OSBP) has interrupted the operationalization of Holili (OSBP) on the Tanzania side.
   Construction of Holili OSBP on Tanzania side was completed in December last year but the $5.7 million State-of-the-Art structure has remained idle for three months as the two Partner States still work on the legal text of the Bilateral Agreement.
   The construction of Taveta OSBP on the Kenya side is expected to be completed within two months and according to the financiers, Trademark East Africa (TMEA), the operationalization of Holili could have continued without waiting for Taveta had the two countries signed the agreement.

  According to TMEA Director, Integrated Border Management and One Stop Border Posts, Mr Theo Lyimo, the East African Community (EAC) passed a law on OSBP in April 2013 but it has not been assented to by the EAC Heads of States. 
  “Even if it (the law) will be signed, Legislations will be needed. This could take longer and that’s why the two countries opted for a bilateral agreement,’ said Mr Lyimo during a tour organised by TMEA for regional Journalists this week. 
  Mr. Lyimo said the bilateral agreement would be used in place of OSBP law because it could have taken longer to amend series of EAC laws, including the Customs Union Managements Act, so as to provide for changes in the way people will be crossing the borders under OSBP concept. 

  He said Tanzania had already approved the Bilateral Agreement and forwarded it to Kenya but the Kenyan side were waiting for the approval of the Cabinet. 
  The construction of the two OSBP projects at Holili and Taveta are expected to reduce 30 per cent total average time to clear cargo at the borders, which will in turn contribute to reducing transport costs and increase in intra-regional and foreign trade in EAC. 
  According to TMEA, Holili border currently serves between 40 to 50 trucks a day but the volume of traffic is likely to significantly increase up to between 400 to 450 trucks once the Voi-Taveta part of the road is upgraded. 
  The increase in traffic is likely because the distance by road from Mombasa port to Himo junction in Tanzania is much shorter (about 472 kilometres) compared to the much longer distance from Dar es Salaam port to Himo junction (935).Journalists from Tanzania and Kenya who visited Holili and Taveta witnessed a handful of trucks from Mombasa port offloading goods, including the cars for clients from Northern Regions of Tanzania.   

  Traders and truck drivers complained about the delays in clearance of goods at Holili border basically due to what they called ‘volatility’ of network systems used by the Tanzania Revenue Authority (TRA) to valuate duties to be paid by importers. 
  Apparently, Holili TRA Customs office only assesses the goods then sends information to Dar es Salaam for evaluation and this according to the traders could take weeks depending on the stability of the network.“Sometimes I stay here for two weeks this makes my business difficult as I have to pay container demurrage charges”, said Emmanuel Justine (36) adding that the delays also restricts the number of trips he makes per month. 
  Under the new OSBP concept, TMEA provides Microwave System for data transmission and storage, which is faster and bigger, as opposed to the satellite system currently used by TRA.Also TMEA is working with JICA with the aim of installing another system which will enable documents to be lodged at the point of entry (Mombasa port) to enable faster clearance at Holili. 
  The EAC OSBP project focuses on setting up the institutional and legal framework necessary for increasing collaboration at Inter-agency and bilateral levels, reviewing and implementing OSBP procedures, training border agency officials, and installing ICT networks, hardware, furniture and equipment.  TMEA finances construction of 13 OSBP in the entire EAC region.

  0 0

  Timu nzima ya Golden Bush Veterans ambao ndio Mabingwa wa Veterani Tanzania (Bara na Visiwani) watahamishia makali yao Kilombero mkoani Morogoro. Tutakapokuwa Kilombero Golden Bush Veterans tutakuwa na mechi moja ya kirafiki siku ya Jumamosi uwanja wa Ruaha dhidi ya Wenyeji wetu Kilombero Veterans yenye wachezaji wazoefu waliowika katika soka la bongo wakiongozwa Mustafa Hoza.

  Golden Bush itaondoka Dar es salaam siku ya Jumamosi saa kumi na mbili asubuhi, na msafara utaongozwa na Waziri Mahadhi kama mkuu wa msafara akisaidiwa na Ali Othman Nucci mjumbe wa kamati ya utendaji na msemaji wetu upande wa Zanzibar.

  Kikosi kizima cha wachezaji 25 chini ya mwalim Madaraka Seleman na nahodha Wisdom Ndlovu a k a Mwakalinga kimejiandaa vya kutosha kufanya maangamizi yatakoweka historia huko Kilombero siku ya tarehe 29 March 2014.

  Kwakuzingatia umuhimu wa game hii, Golden bush tunaweka camp ya wiki nzima Bagamoyo ili kujiweka sawasawa kwa ajili ya game hiyo ya kukata na shoka.

  Asanteni kwa kunisikiliza.
   Onesmo Waziri “Ticotico” 
  Msemaji wa timu

  0 0


  0 0


  0 0

  On 31 March, our new commercial partner for UK visa services, Teleperformance Ltd., will take over the running of our Visa Application Centre in Tanzania. The Visa Application Centre will be moving from its current location at the British High Commission to different premises in Dar es Salaam as follows:

  New Teleperformance Application Centre Address

  Viva Towers,

  294-295 Ali Hassan Mwinyi Road,

  Upanga,

  Dar es Salaam,

  Tanzania.


   Date of Relocation
  31 March 2014.


   UK visa customers will continue to complete their applications and pay their visa fee online at Visa4UK before selecting an appointment at the Teleperformance application centre. Hours of operation at the new centre will be increased from 0830-1630hrs, offering a wider range of daily appointments. Our standard service levels will not change as a result of outsourcing to a commercial partner. Operating outsourced Visa Application Centre facilities allows us more flexibility to drive improvements in customer service with greater access to added value services such as priority visas and return courier options. We will work closely with our commercial partner to ensure continuity of service during the transition period.

  All UK visa applications will continue to be decided by UK Visas & Immigration staff.


  The UK remains open for business and these new arrangements will allow us to maintain a world class, competitive visa system to support Britain in the global race. We are listening to the needs of our customers and these changes will improve our service by increasing the number of visa application centres globally and expanding the number of locations and countries where premium services are available.   0 0

   Na Eleuteri Mangi- MAELEZO 
   Serikali imesema utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa bomba la kusafirishia gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es salaam unaenda vizuri kulingana na ratiba yake na utakamilika kwa wakati. 
   Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue alipotembelea kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia kinachojengwa Kinyerezi wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi jijini Dar es salaam. 
   Balozi Sefue alisema kuwa ni vema kufanyakazi kwa uadilifu na hakuna mchezo, kazi ikitolewa ikamilike kwa wakati. 
   "Tujenge uchumi wa nchi yetu kwa kutumia umeme wa uhakika, uhakika huo unatokana na gesi asilia tuliyonayo" alisisitiza Balozi Sefue.
    Akifafanua zaidi Balozi Sefue alisema kuwa kugunduliwa kwa gesi nchini kumeanza kuleta manufaa mengi ikiwamo wanafunzi kupata udhamini katika masomo yao katika ngazi mbalimbali za elimu, shule zimejengwa, wananchi wa mikoa ya Lindi na Mtwara wanapata maji safi na kupata ajira mbalimbali. 
    Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi alisema kuwa fedha za ujenzi wa kituo cha kinyerezi I na ujenzi wa vituo vingine vya kinyerezi II, III na IV, zinatolewa na Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na wahisani. 
   Fedha za ujenzi wa kituo cha Kinyerezi I zimetolewa na Serikali kupitia TANESCO na ujenzi wa kituo cha kinyerezi II fedha itatokana na ubia kati ya Serikali ya Tanzania na Japani , wakati ujenzi wa kinyerezi III na IV fedha zitatokana na kuingia ubia kati ya Serikali na kampuni ya Kichina. Alimhakikishia Balozi Sefue kuwa Wizara yake ipo tayari kupokea maelekezo na ushsuri kutoka ngazi za juu za Serikali katika kutekeleza mradi huo wa ujenzi wa bomba la gesi asilia na hatimaye kuongeza uzalishaji wa umeme ili kujenga uchumi wa kipato cha kati ifikapo mwaka 2025. 
    Mkurugenzi Mkazi wa Mradi huo Bw. Shaun Moore, alimweleza Katibu Mkuu Kiongozi na msafara wake kuwa maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho yanaendelea vizuri kutokana na kampuni hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano mzuri na kampuni za kitanzania zilizochukua kandarasi tofauti za ujenzi wa kituo hicho ambapo takribani asilimia 98 ya kandarasi na wafanyakazi ni kutoka kampuni za kitanzania. 
   Ziara hiyo ilianzia mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na kuhitimishwa Dar es salaam ambapo Katibu Mkuu Kiongozi aliambatana na Makatibu Wakuu 12 wa Wizara zinzotekeleza Mpango wa Mataokeo Makubwa Sasa (BRN).

    Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiwasili kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia kinachojengwa Kinyerezi wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi kutoka Mtwara hadi jijini Dar es salaam. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mkazi wa Mradi huo kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro Shaun Moore na wa kwanza ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi.
   Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (katikati) akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi wa Mradi huo kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro Shaun Moore (wa kwanza kushoto) na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi.

    Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akikagua maendeleo ya ujenzi wa mradi huo akiwa na Mkurugenzi Mkazi wa Mradi kutoka kampuni ya Jacobsen Elektro Shaun Moore (wa kwanza kushoto) na wa pili kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Eliakim Maswi na kulia ni Mkurugenzi Mkuu TANESCO Felchesmi Mramba
    Mkurugenzi Mkuu TANESCO Felchesmi Mramba akimweleza Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue na msafara wake hatua zilizofikiwa kwenye ujenzi wa kituo cha kufua umeme kwa kutumia gesi asilia kinachojengwa Kinyerezi wakati akihitimisha ziara yake ya siku mbili ya kukagua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi jijini Dar es salaam.
   Moja ya eneo la kituo cha Kenyerezi I ambapo inajengwa mitambo ya kufua umeme kwa kutumia gesi asilia. 
   Picha zote na Eleuteri Mangi- MAELEZO

   0 0

   Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Bernard K. Membe (Mb) akizungumza na Waandishi wa Habari, kuhusu Mafanikio ya Wizara kwa kipindi cha miaka 50 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wa mwaka 1964 katika nyanja mbalimbali ikiwemo utekelezaji wa Diplomasia ya Uchumi, ushiriki wa Tanzania kwenye harakati za ukombozi na utatuzi wa migogoro Barani Afrika na Diplomasia ya Michezo .
   Waandishi wa Habari waliokuwepo wakati wa mkutano kati yao na Waziri Membe (hayupo pichani).
   Mkurugenzi Idara ya Ushirikiano wa  wa Kimataifa, Balozi Celestine Mushy (wa kwanza kushoto), Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia, Balozi Mbelwa Kairuki (katikati) pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga wakifuatilia mazungumzo ya Waziri Membe  na Waandishi wa Habari.
   Waziri Membe (Mb) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) huku Naibu wake Dkt. Mahadhi Juma Maalim (Mb.) akisikiliza.
   Mazungumzo yakiendelea.(Picha na Reginald Kisaka)


   0 0


    MWILI WA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA WA MARA JOHN GABRIEL TUPA UKITOLEWA KWENYE NDANI YA MAKAZI YAKE


    WAOMBOLEZAJI WAKIWA NYUMBANI KWA ALIYEKUWA MKUU WA MKOA HUYO.

  older | 1 | .... | 400 | 401 | (Page 402) | 403 | 404 | .... | 3272 | newer