Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 38 | 39 | (Page 40) | 41 | 42 | .... | 3285 | newer

  0 0

  Michuano ya kuwania Kombe la Mataifa ya Afrika kwa upande wa soka(AFCON 2013) inaelekea ukingoni. 

  Usiku wa jana ulikuwa ni usiku wa michezo ya nusu fainali ambapo Nigeria walikuwa wanaumana na Mali na kisha Ghana wakavaana na Burkina Faso. Katika mchezo wa kwanza Nigeria walifanikiwa kuingia katika fainali kwa kuichabanga vibaya timu ya Mali kwa jumla ya magoli 4-1 kabla ya baadae Ghana kutupwa nje ya mashindano ya mwaka huu kwa kuchapwa kwa mikwaju ya penati baada ya kwenda sare ya 1-1 katika dakika za kawaida na 30 za nyongeza. 

  Jijini Dar-es-salaam, mashabiki wa soka wameendelea kufurahia michuano ya AFCON 2013 sehemu mbalimbali kupitia SuperSport Channels ambazo zinapatikana Live na pia katika High Definition(HD) kupitia DStv. Mojawapo ya sehemu hizo ni viota vya Samaki Samaki jijini Dar-es-salaam.
  Baadhi ya wafanyakazi wa kitengo cha mauzo DStv wakiongozwa na Meneja Mauzo, Salum Salum(mwenye t-shirt ya Blue) walikuwepo tayari kabisa kufurahi pamoja na wateja na mashabiki wa soka na pia kujibu maswali mbalimbali kutoka kwa wateja na mashabiki hao.
  Ukimuuliza shabiki yeyote wa soka atakwambia kwamba soka ina raha yake unapotizama na marafiki. Lakini....soka ina raha ya kipekee unapoitazama kwenye kiwango cha High Definition(HD). Ni DStv pekee wanaokuwezesha kupata raha hiyo.
  Cartoonist wa siku nyingi,Fred Halla alikuwa na mengi ya kuuliza lakini pia kusifia na kufurahia michuano ya AFCON 2013 kupitia DStv.
  Soka, mijadala, kinywaji...AFCON 2013 ina mengi. Samaki Samaki-Mlimani City.
  Baada ya kazi, ni AFCON 2013 kupitia DStv pekee!
  Unapozungumzia michezo,unazungumzia SuperSport.Unapozungumzia SuperSport unazungumzia DStv.
  Meneja Mauzo wa DStv,Salum Salum, amenidokeza kwamba Jumapili ijayo(tarehe 10 Feb) siku ya Fainali ya AFCON 2013 patakuwa na shughuli maalumu ya kumaliza msimu wa AFCON 2013 katika viota vya Samaki Samaki na sehemu zinginezo. Mashabiki watashinda zawadi mbalimbali na watapata kujua mengi zaidi kuhusu DStv ambao ni wakongwe wa digitali. Usikose kutizama fainali ambayo itakuwa kati ya Nigeria(Super Eagles) na Burkina Faso.

  Ili kujua mengi zaidi yanayojiri kwenye luninga yako,Jiunge na ukurasa wa Facebook wa DStv Tanzania kwa kubonyeza hapa.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akionyeshwa jambo na Seneta, James Inhofe wa Jimbo la Oklahoma, wakati alipomtembelea Ofisini kwake baada ya mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Seneta huyo jana Feb 6, 2013. Makamu wa Rais yupo nchini Marekani katika jiji la Washngton Dc kwa ziara ya siku nne.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na Naibu Waziri wa Uchumi, Nishati na Mazingira, Seneta,Robert D. Hormats, wakati alipofika katika Ofisi yake iliyopo katika jingo la Ofisi za Maseneta wa Marekani, akiwa katika ziara yake ya siku nne katika jiji la Washngton Dc Marekani, jana Feb 6, 2013.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Balozi Johnnie Carson, wakati makamu alipofika Ofisini kwa Balozi huyo kwa mazungumzo leo, Feb 7, 2013. Balozi Carson ni msaidizi wa Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani anayeshughulikia masuala ya Afrika.
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Rais wa Mfuko wa MCC, Daniel Yohannes, baada ya kumalizika kwa mazungumzo yao kuhusu kuendelea kwa mradi wa MCC ii, nchini Tanznia. Mazungumzo hayo yalifanyika jana Feb 6, 2013 katika Hoteli ya Omni iliyopo Washngton Dc Marekani, ambapo Makamu yupo nchini humo kwa ziara ya siku nne. Picha na OMR 

  0 0


  Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akimshika kwa furaha mtoto aliyezaliwa tarehe 5.7.2013 katika hospitali ya Mkoa wa Lindi, Sokoine huku mama wa mtoto huyo Muksim Issa ,19, anayetoka katika kijiji cha Mumbu kilichoko katika wilaya ya Lindi vijijini aliyelala kitandani akitabasamu. Mtoto huyo alizaliwa akiwa na uzito wa kilo 3.9 Mama Salma alitembelea hospitalini hapo kukabidhi vifaa vya hospitali tarehe 6.2.2013. Aliyesimama kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi Dr. Nasoro Hamid.
  Kikundi cha utamaduni kikiwatumbuiza waalikwa kwa ngoma ya Tambiko inayochezwa na watu wa kabila la Wamakonde wakati wa sherehe ya kukabidhi vifaa vya tiba kwenye hospitali kuu ya mkoa wa Lindi, Sokoine, tarehe 6.2.2013.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwahutubia viongozi na wafanyakazi wa hospitali ya mkoa wa Lindi, Sokoine,na wananchi waliohudhuria sherehe ya kukabidhi rasmi vifaa vya tiba kwenye hospitali hiyo tarehe 6.2.2013 huko Lindi Mjini. Waliokaa kushoto kwa Mama Salma ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ambaye pia ni Meya wa Lindi Mjini Ndugu Frank Magali na wa mwisho ni Mwakilishi wa Project C.U.R.E. nchin Tanzania Bwana Makembe Kimario.
  Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akikata utepe kuashiria kukabidhi rasmi kwa vifaa vya hospitali ya mkoa wa Lindi,Sokoine, vilivyotolewa na Taasisi ya WAMA kwa kushirikiana na Shirika la Project C.U.R.E. la nchini Marekani. Vifaa hivyo vina thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia saba. Kulia kwa Mama Salma ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Lindi Dr. Nasoro Hamidi akifuatiwa na Katibu wa CCM WA Mkoa huo Ndugu Adelina Gefi na kushoto ni Kaimu Mganga Mfawidhi wa hospitali Dr. Nicolaus Munni. Sherehe hiyo ilifanyika tarehe 6.2.2013.


  0 0


  Kampuni ya bia ya Serengeti imezidi kukonga nyoyo za wapenzi wa bia jijini Dar Es Salaam  kupitia kinywaji  chake cha Tusker Lite . Kinywaji hicho cha ukweli  kilizinduliwa  mwezi Novemba mwaka jana . Tusker Lite ina wanga kidogo  na ladha halisi  ya kuburudisha. Kwa mujibu wa matukio yanayoendelea  katika baa mbalimbali jijini,  wapenzi wa bia wamepata fursa ya kuzungumza na mabalozi wa kinywaji hicho na  kukiri  kuwa Tusker Lite ina ladha murua na kukubali kuwa Tusker Lite ni Lite ya ukweli .

  0 0

  Hatimaye filamu mpya ya wrong lane kutoka rastemwi productions imeanza kusambazwa mtandaoni, pata copy yako kupitia https://www.createspace.com/360868 
   Usifiche uhondo, wahabarishe na wenzio. kwa mawasiliano piga +1 857 288 8686 au tutumie barua pepe info@rastemwi.com 
  Pia waweza kutufuatilia hapa www.rastemwi.com ama facebook www.facebook.com/rastemwiproduktions ama youtube www.youtube.com/rastemwi

  0 0


  Makamu wa Pili wa  Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitoka kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha { AICC } Baada ya kuufunga Mkutano wa Mafuta na Maonyesho wa Afrika Mashariki  kwa niaba ya Rais wa Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein. Kulia ya Balozi ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania Mh. George Simba Chawene, na kushoto yake ni Waziri wa Nishati wa Uganda Mh. Irin Muloni na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki Mheshimiwa Jesca Eriyo. 
  Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.

  Na Othman Khamis Ame
  Mataifa ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Mashariki { EAC } yametakiwa  kuwa makini katika mfumo na muundo mzima wa Sekta ya Mafuta na Gesi ambayo inatarajiwa kuwa muhimili wa Uchumi mpya katika ukanda huu wa Bara la Afrika.
  Wito huo umetolewa na Rais wa Zanzibar  na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dr. Ali Mohammed Shein wakati akiufunga Mkutano wa Sita wa siku tatu wa Mataifa ya Jumuiya ya Afrika Mashariki  kuhusu mafuta, Gesi na Maonyesho ya Taaluma ya Sekta hizo uliokuwa ukifanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Arusha {AICC }.
  Dr. Shein ambaye Hotuba yake ilisomwa kwa niaba yake na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema  Ukanda wa Afrika Mashariki hivi sasa unahitaji kuwa na sauti ya pamoja katika muundo huo utakaowezesha  Sekta hiyo kuyanufaisha Mataifa hayo  Wanachama katika Maendeleo ya Kiuchumi.
  Alisema  Wawekezaji pamoja na Makampuni ya Kimataifa yanayojihusisha na Sekta ya Mafuta na Gesi yanaweza kushajiika na mfumo mzima  wa ukanda huu kutegemea zaidi sera na juhudi za Miundo mbinu itakayowekwa na Walaamu wa Mataifa hayo.
  “ Ukanda wa Afrika Mashariki umeonyesha dalili za mapema za kuwepo kwa rasilmali ya Mafuta na Gesi miaka mingi iliyopita lakini kilichokosekana ndani ya muda huo ni utaalamu wa Kuendesha Miradi inayotokana na Sekta hiyo”. Alifafanua Dr. Shein.
  Alifahamisha kwamba idadi kubwa ya Wawekezaji tayari wameshaonyesha  nia ya kutaka fursa ya kuwekeza katika Sekta ya Mafuta na Gesi ndani ya Ukanda wa Afrika Mashariki baada ya Uganda na Kenya kugundulika kuwa na Mafuta  na Gesi kwa Tanzania.
  Aliwapongeza Viongozi na Wataalamu wa Mataifa hayo ya Afrika Mashariki kwa juhudi zao zilizosaidia kufanikisha Mikutano na vikao vilivyolenga kuimarisha Sekta hiyo mpya kwa maendeleo ya Uchumi wa Mataifa yao.
  Akimkaribisha Mgeni rasmi kuufunga Mkutano huo wa Mafuta na Maonyesho Waziri wa Nishati wa Uganda Mh. Irin Muloni alisema uendeshaji wa sekta ya Mafuta katika ukanda wa mataifa ya Afrika Mashariki utaimarishwa ipasavyo kwa maslahi ya Mataifa hayo.Mh.
  Mapema Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki { EAC } Mheshimiwa Jesca Erio amewahakikishia wawekezaji wote watakaoamua kuwekeza kwenye sekta hiyo watajengewa mazingira bora ya ushirikiano.
  Mheshimiwa Jesca alisema mazingira bora ya uwekezaji ndani ya sekta ya Mafuta katika Ukanda wa Afrika Mashariki  ni suala la msingi katika kufanikisha na kuendeleza uchumi wa Mataifa hayo.
  Akisoma maazimio ya Mkutano huo Mhandishi Gosper  alisema ipo haja kwa  Mataifa hayo kufanya juhudi za ziada katika kuhakikisha Sekta hiyo inalindwa kwa vile inategemewa kubadilisha Uchumi wa Mataifa Wanachama.
  Mhandisi Gosper alifahamisha pia kwamba suala la mazingira lazima litiliwe mkazo  kwa lengo la kulinda rasilmali zilizopo.
  Mkutano wa saba wa Mafuta na Maonyesho wa Mataifa ya Jumuiya ya Uchumi ya Afrika Mashariki unatarajiwa kufanyika mwaka 2015.  0 0
 • 02/08/13--08:53: habari njema kwa wadau wote. • 0 0

  Mamongoo aka Jambo Squad ndani ya www.noizmekah.com kwa defxtro wakirecord "Tukunyema" Pini lao litalokuwa hewani mwisho wa mwezi huu. Wanatarajia kushoot video kwanza kabla ya official Audio Release kwa Hisani ya VMG Africa na Hoodpixx watayarishaj wa Film & Music Videos.

  0 0

  MHESHIMIWA MIZENGO P. PINDA (MB), WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

  1.            Mheshimiwa Spika, tumekuwepo hapa Bungeni, Dodoma kwa takriban siku 11 ambapo leo tunahitimisha shughuli zilizopangwa katika Mkutano wa Kumi wa Bunge lako Tukufu. Nitumie nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu mwenye wingi wa Rehema kwa kutufikisha salama siku ya leo.

  2.            Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba nitumie nafasi hii kutoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki waliopoteza Wapendwa wao katika ajali mbalimbali zilizotokea hapa Nchini, ikiwemo ajali ya Jahazi la Sunriseiliyotokea Wangwi katika Bahari ya Hindi na Ajali ya Lori kule Mbarali ambapo Watu wamepoteza maisha na kupata majeraha. Aidha, tunawapa pole Majeruhi wote na Abiria waliopoteza mali katika ajali hizo. Kwa kipekee kabisa napenda kutoa pole kwa Ndugu, Jamaa na Marafiki wa Askofu Thomas Laiser wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini Kati - Arusha ambaye amefariki jana Mchana na Askofu Mstaafu Amedeus Msarikie wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Moshi ambaye  amefariki Usiku wa kuamkia leo huko Nairobi alikokuwa anapata matibabu. Wote tunawapa pole sana!  0 0
 • 02/08/13--09:30: taswira toka bungeni leo
 •  Mbunge wa  Moshi Mjini Mhe Phillemon Ndesamburo akiongea na Mhe Lucy Owenya  (viti maalumu - CHADEMA)  Bungeni leo.  
  Waziri Mkuu Mizengo Pinda (kushoto) akibadilishana mawazo na wabunge (katikati ) Mary Mwanjelwa(-Viti Maalumu)  na  James Lembeli (kulia) Kahama leo Bungeni. 
  Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO

  0 0

   Katibu Mkuu, Mbarak Abdulwakil akipokea shairi alilolisoma Mtunzi wa Mashairi katika Jeshi la Magereza, Rashid Mtimbe (kushoto).

   Baadhi ya wajumbe wa TPS Saccos wakifurahia jambo wakati Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil alipokuwa anatoa hotuba yake ya ufunguzi wa makutano huo.  

   Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali, John Minja akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil.

   Mwenyekiti wa TPS Saccos, Deonice Chamulesile akitoa hotuba fupi ya kumkaribisha Mlezi wa TPS Saccos ambaye pia ni Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali, John Minja.

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka wa pili wa TPS Saccos unaofanyika katika Hotel ya Edema, mjini Morogoro.  

  Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wanne waliokaa kutoka kushoto) akiwa na wajumbe mbalimbali wa Chama cha Akiba na Kukopa (TPS Saccos) katika picha ya pamoja.

  PICHA ZOTE NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI

  WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI.


  0 0


  Kampuni yetu ya BEYOND EVENT ORGANISERS  inatarajia kuanza kuaanda matukio nchini Tanzania hususan katika jiji la Dar-Es-Salaam. Kwa kuanzia tutaanza na tafrija ya chakula cha usiku chenye hadhi ya mahaba kwa wapendanao (ROMANTIC DINNER).
  Naomba upitie link hii  http://www.surveymonkey.com/s/GSF9NTG ili uweze kutusaidia kuchangia maoni yako.
  Madhumuni ya zoezi hili ni kujaribu kupata maoni yako ili tuweze kuboresha shughuli yetu na kuhakikisha kuwa tunakidhi matakwa ya wateja wetu.
  Swali la tisa (9) linakupa fursa wewe ya kutueleza kwa kina yale unayofikiria ni muhimu katika kufanikisha shughuli hiyo. Kumbuka kuandika jina lako, nambari yako ya simu na anuani yako ya barua pepe (e-mail).
  Kwa kufanya hivyo utapewa punguzo la Tshs 10,000/= wakati wa kununua tiketi yako pindi muda utakapowadia.
  Nitashukuru kama utatusambazia ujumbe huu kwa marafiki zako, ndugu na hata wafanyakazi wenzio ili siku itakapowadia tufurahie kwa pamoja.
  Regards,
  MfundaYasini M.I.

  0 0
 • 02/08/13--11:17: Article 16
 • Picha na  mdau Greyson Msigwa

  0 0
 • 02/08/13--11:20: isiwe taabu...
 • Paparazzi mpya Da' Asha Baraka, Mkurugenzi wa Twanga Pepeta, akiwa kazini...Sasa sie kina Ankal tukale wapi???

  0 0
 • 02/08/13--20:24: Article 14


 • 0 0


  Ambassador Mbelwa Kairuki (left), Director of the Department of Asia and Australasia in the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation, today met with H.E. Ambassador Lu Youqing, Ambassador of the People's Republic of China in the United Republic of Tanzania to discuss various areas of strengthening cooperation between the two countries.  Among the pertinent issues discussed, the Ambassadors also discussed the energy sector and its potential to Chinese investors. 

  Ambassador Kairuki and Ambassdor Youqing in discussion together with other officials from both Tanzania and Chinese Governments.  From left is Mr. Ouyang Zhibing, Senior Officer from Embassy of the Republic of China to Tanzania, Mr. Lin Zhiyon(2nd left), Officer in charge of Economic Affairs in the Chinese Embassy and Mr. Ren (3rd left), Interpreter.  Others are Ms. Haika(right) and Mr. Ngaiza (2nd right), Foreign Service Officers in the Ministry of Foreign Affairs.  

  Ambassador Kairuki and Ambassador Youqing share a light moment during their discussion. 

  Ambassador Kairuki and Ambassador Youqing in a photo after their discussion held today in the Ministry of Foreign Affairs in Dar es Salaam. 
  All photos by Tagie Daisy Mwakawago of the Ministry of Foreign Affairs and International Co-operation. 

  0 0


  MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA

  Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inapenda kuwatangazia Wateja na Watumiaji wote wa Bandari kwamba imeanzisha Kitengo Maalum cha Huduma kwa Wateja kitakachopokea malalamiko, kero, taarifa, maoni, ushauri juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mamlaka.

  Kuanzishwa kwa Kitengo hiki ni moja kati ya Mikakati ya Mamlaka ya kuboresha huduma zake na kuondoa kero kwa Wateja na Watumiaji wa Bandari.
  Kwa huduma ya haraka tafadhali piga namba zifuatazo;
  0754 292998
  0756 849868
  0788 888801
  0789 334398
  Namba hizi pia zinapatikana kwenye mtandao wa TPA www.tanzaniaports.com
  MENEJIMENTI

  0 0


  A two-day forum on the environmental challenges for Tanzania’s development and energy security will bring together key stakeholders to discuss practical short, medium and long-term solutions to the dual pressures of environmental concerns and growing energy demands this week.

  Recent gas discoveries and plans for power generation using natural gas stand to bring about significant economic benefits for Tanzania. According to the MKUKUTA Report 2011, power generation was approximately at 75% of potential electricity capacity in 2010, while the rate of consumption is steadily increasing.

  Addressing the current energy deficiencies plays a significant role in the achievement of the country’s development aspirations. At the same time, on the global stage, the consensus is that power generation based on coal, oil, and gas is the major contributor to climate change. For Tanzania, the potential adverse environmental consequences resulting from growth in the energy sector are an important consideration.

  The event, to be held from the 13th – 14th February in Dar es Salaam and Bagamoyo, has been organised as UONGOZI Institute’s second Green Growth Platform,  which combines plenary meetings and field-site visits in promoting greater understanding of particular issues in support of sustainable development.

  The Vice President of Tanzania and patron of the Green Growth Platform, H.E. Dr. Mohamed Gharib Bilal will open the event, which will be followed by plenary presentations and discussion on the opportunities and challenges Tanzania faces relating to balancing growth in the energy sector with environmental sustainability, and the influence of global perspectives on Tanzania’s development in terms of energy security and environmental concerns.


  Contact:

  Hanna Mtango, Communications Manager, UONGOZI Institute

  Tel: +255 22 2602917, 0767 220 883, Email: hmtango@uongozi.or.tz


  0 0

  Mkurugenzi wa Masoko wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB)Devota Mdachi kushoto na maafisa wengine wakiwa katika maonyesho ya Utalii ya FITUR ambayo ni ya tatu kwa Duniani yaliyofanyika kuanzia Januari 30 mpaka Februari 3 mwaka huu nchini Madrid nchini Hispania na kushirkisha Bodi ya Utalii (TTB), Mamlaka ya Hifadhi za Taifa ya Ngorongoro (NCAA) na makampuni zaidi ya sita ya utalii kutoka nchini Tanzania katikati ni Esther Solomon (Senior Tourist Information Officer,(TTB) , Israel Naman ({Principal Conservation Officer, (NCAA) na Maria Kirombo (Park Warden, Arusha National Park).
  Devota Mdach kushoto, Maria Kirombo and Esther Solomon wakiwa katika banda la Tanzania nchini Hispania kwenye maonyesho ya utalii ya FITUR.
  Ujumbe wa Tanzania ukiwa katika picha ya pamoja na Youssou Ndour Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini Senegal ambaye pia ni mwanamuziki maarufu duniani wakati alipotembelea banda la Tanzania katika maonyesho hayo , Youssou Ndour amewahi kufanya ziara ya kimuziki mara tatu nchini Tanzania kabla ya kuteuliwa kuwa Waziri wa Utalii na Utamaduni nchini mwake.

  0 0


older | 1 | .... | 38 | 39 | (Page 40) | 41 | 42 | .... | 3285 | newer