Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | 2 | 3 | (Page 4) | 5 | 6 | .... | 3272 | newer

  0 0

  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda amewataka Watanzania kuwa na utamaduni wa kucheki afya zao mara kwa mara wakati akiwahutubia wananchi walio hudhuria sherehe ya Krismas aliyoianda katika kijiji cha Kibaoni,Mkoani Katavi.
  Waziri Mkuu,Mizengo Pinda na Mkewe Tunu Pinda wakifungua muziki wa dansi katika sherehe ya Krismasi ambayo alianda kwa wananchi waliokuja kusherehekea sikukuu hiyo katika kijiji cha Kibaoni Katavi.Waziri Mkuu yupo kijijini kwao Kibaoni kwa mapumziko ya krismasi na mwaka mpya.
  Wananchi walio hudhuria sherehe ya Krismasi ambayo iliandaliwa na Mh Waziri Mkuu,Mizengo Pinda katika kijiji cha kibaoni wanaonekana wakiserebuka muziki wa dansi.
  Badhi ya wakina mama wakiwa na msaidizi wa Waziri Mkuu Mama Kapaya wakiwa wamejipumzisha kwenye kivuli wakibadilishana mawazo kutokana na sherehe ya Krismasi ilivyo fana katika kijiji cha Kibaoni.

  0 0


   Mgeni rasmi katika kampeni ya Mradi wa Upandaji Miti jijini Mwanza, Henry Mongi, akipanda mti  wakati wa kampeni hiyo katika moja ya mitaa ya jiji hilo.Anayeshudia kulia ni Afisa Ubora wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), Caroline Muhonoli na wa pili kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Fasheni Lugo. Mradi huo umefadhiliwa na Kampuni ya Bia Tanzania.
   Mkurugenzi wa Uhusiano na Sheria wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Steven Kilindo, akifukia udongo kwenye shimo alilopanda mti wakati wa kampeni ya upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki..Wanaoshuhudia katikati ni Meneja Ubora wa kampuni hiyo, Caroline Muhonoli na nyuma ya Kilindo ni Diwani wa Kata ya Mkuyunim, Lugo Fashen.TBL imetumia zaidi ya milioni 30 kupanda miti 7000 katika mikoa ya Mwanza,Kilimanjaro na Mbeya. Kwa Mkoa wa Mwanza pekee imetumia sh. mil. 10 kupanda miti 2600.
   Meneja wa TBL Mwanza, Richmondx Raymond akipanda mti katika uzinduzi wa mradi wa upandaji miti jijini Mwanza mwishoni mwa wiki, uliofanywa na kampuni hiyo kwa kupanda miti 2600 kando kando ya barabara za Balewa, Kenyatta, machemba na shule za sekondari Nyamaganana na Nyegezi na Kiwanda cha Bia cha kampuni hiyo. 

  0 0


  0 0

  Dah! Hata sijui niseme nini. Kuhama sihami (kwangu Bwawa ni kama kabila, sio dini ama utaifa)  lakini hamu sina kwa jinsi gundu linavyotuelemea Bwawa la Maini, kiasi hata kuangalia mechi siku hizi ni kwa nadra sana, achilia mbali kuzungumzia, kwani tukishinda gemu moja leo ujue mechi tatu zijazo kama sio droo basi kichapo. Nani katuroga wajameni??? Yaani katika gemu 19 tumeshinda 6 na droo 7, hii kweli ni haki jamani??? Halafu kwenye nafasi tuko wa 10 hadi dakika hii. Sijui nijitungike...Ah, nshachoka mie!


  0 0

  Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka (katikati), akitembelea moja ya miradi mikubwa ya ujenzi wa shule inayotekelezwa na mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi wa ABG wa Mahusiano na Serikali, Bw. Emmanuel ole Naiko.
  Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka (katikati), akitembelea moja ya miradi mikubwa ya ujenzi wa shule inayotekelezwa na mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara hivi karibuni. Kulia ni Mkurugenzi wa ABG wa Mahusiano na Serikali, Bw. Emmanuel ole Naiko.
  Waziri wa Ajira na Kazi, Gaudensia Kabaka (kushoto), akitembelea moja ya miradi mikubwa ya ujenzi wa shule inayotekelezwa na mgodi wa North Mara unaomilikiwa na kampuni ya African Barrick Gold (ABG) wakati wa ziara yake kwenye mgodi huo uliopo wilaya ya Tarime mkoa wa Mara hivi karibuni. Kushoto kwa waziri ni Mkurugenzi wa ABG wa Mahusiano na Serikali, Bw. Emmanuel ole Naiko.

  0 0

   Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Haruna Masebu (kushoto), Haruna Masebu akielezea utendaji wa mamlaka hiyo wakati wa mkutano wa pamoja na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) wa kubadilishana mawazo, Dar es Salaam . Kulia ni Mwenyekiti wa TEF, Absalom Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari. (PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG)

  Mhariri wa habari wa gazeti la Daily News, Leonald Mwakalebela akiuliza swali wakati wa mkutano wa wahariri wa vyombo vya habari wa kubadilishana mawazo na uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dar es Salaam
  Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu (kulia) akijadiliana jambo na maofisa wake muda mfupi kabla ya mkutano na Jukwaa la Wahariri kuanza katika Hoteli ya JB Belmonte Dar es Salaam.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri (TEF), ABsalom Kibanda akizungumza na  Haruna Masebu Bosi wa Ewura.
  Mkurugenzi Mkuu wa EWQURA, Haruna Masebu akiwakaribishwa wahariri kwenye mkutano huo
  Mhariri Mkuu wa gazeti la Habari Leo, Joseph Kulangwa akiuliza swali kuhusu tatizo la maji wakati wa mkutano wa pamoja kati ya Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) na Jukwaa la Wahariri Tanzania,  jijini Dar es Salaam. Kulia ni Tumiani Abdalah wa Daily News.
  Mkurugenzi wa Maji na Maji Taka wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (Ewura), Mhandisi Mutaekulwa Mutegeki (kushoto) akielezea kuhusu mfumo wa maji safi na taka wakati wa mkutano na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri (TEF), wa kubadilisha na mawazo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Umeme wa mamlaka hiyo, Mhandisi Anastas Mbawala na Mkurugenzi wa Uchumi wa Ewura, Felix Ngamlagosi.
  Meneja Ufundi wa Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA, Gerald Maganga akifafanua jambo kuhusu masuala ya mafuta wakati wa mkutano na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri (TEF), wa kubadilisha na mawazo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi wa Gesi Asilia wa mamlka hiyo, Mhandisi Charles Omujuni.
  Mkurugenzi wa Uchumi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA, Felix Ngamlagosi akifafanua jambo kuhusu utendaji wa mamlaka hiyo wakati wa mkutano na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri (TEF), wa kubadilisha na mawazo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi wa Maji na Maji Taka wa EWURA, Mhandisi Mutaekulwa Mutegeki.
  Mkurugenzi wa Sheria wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA, Miriam Mahanyu (kushoto) akifafanua jambo kuhusu utendaji wa mamlaka hiyo wakati wa mkutano na wajumbe wa Jukwaa la Wahariri (TEF), wa kubadilisha na mawazo hivi karibuni jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu.
  Mhariri wa Habari wa gazeti la Habari Leo, Mgaya Kingoba akichangia hoja wakati wa mkutano huo. Kutoka kulia ni Joyce Shebe wa ITV na Mhariri wa Redio Uhuru, Godfrey Chongolo.
  Mtangazaji wa Star Tv, Tom Chilala akiuliza swali kwa uongozi wa Ewura. Kushoto ni Mhariri wa gazeti la Dira ya Mtanzania, Abraham Ojuku.
  Mhariri wa Redio Uhuru, Godfrey Chongolo akiomba muongozo katika mkutano huo. Kulia ni Joyce Shebe wa ITV.
  Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano wa Ewura, Titus Kaguo akifafanua jambo wakati wa mkutano huo
  Katibu Mkuu wa Jukwaa la Wahariri, Nevile Meena akizungumza katika mkutano huo. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Ewura, Haruna Masebu.
  Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Absalom Kibanda (kulia) akiongoza mkutano wa wahariri wa kubadilishana mawazo na uongozi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa EWURA, Haruna Masebu.

  0 0


  H.E. Jakaya Mrisho Kikwete, President of the United Republic of Tanzania has sent a congratulatory message to H.E. Shinzo Abe, the new Prime Minister of Japan. The message reads as follows:

  “His Excellency Shinzo Abe,
  Prime Minister of Japan,
  Tokyo,
  JAPAN.

  Your Excellency,

  “Let me express my warmest congratulations on your deserved election as the new Prime Minister of Japan on election held on 16th December, 2012. Your election to the Premiership speaks volume on the confidence the people of Japan bestowed upon you at this period of economic difficulty facing Japan and the world at large.

  I look forward to working closely with you in bringing our bilateral relations to greater heights and achieving its full potential. I am particularly optimistic that under your stewardship, the forthcoming TICAD V Summit to be held on June 2013 in Yokohama will be a great success.

  I take this opportunity to reaffirm my country’s commitment and desire to continue working with you and your Government in further strengthening the existing ties of friendship and cooperation between our two countries and peoples.

  I wish you every success in streering the affairs of your great nation and looking forward to meet you during that time to discuss issues of mutual interest to our two countries.

  Please accept, your Excelency, my best wishes for your continued good health, progress and prosperity of the people of the Japan”.

  ISSUED BY: MINISTRY OF FOREIGN AFFAIRS AND INTERNATIONAL COOPERATION, DAR ES SALAAM.

  27TH DECEMBER, 2012.

  0 0


  0 0
 • 12/27/12--02:51: vigogo barabarani
 • Globu ya Jamii leo imepita mitaa ya Kinondoni Mkwajuni karibu na ile Bar ya Masai na kukuta vigogo vimewekwa katikati ya barabara kwa madai ya kuzuia magari yanayokwenda kasi.sasa sijui utaratibu huu katika sheria za usama barabarani upo katika kifungu gani??

  0 0

  MAANDALIZI ya Mkutano Mkuu wa Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) yanaenda vizuri na wajumbe wanatarajiwa kufika Bagamoyo Ijumaa Desemba 28, 2012 mchana kwenye hoteli ya Kiromo View Resort watakapolala na kufanyia mkutano.

  Ijumaa hiyo washiriki watatembelea maeneo mbalimbali ya kihistoria Bagamoyo na jioni kutakuwa na mechi ya kirafiki kati ya timu ya soka ya TASWA FC na Bagamoyo Veterani itakayofanyika Uwanja wa Mwanakalenge na usiku wajumbe watakuwa na chakula cha pamoja na kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali yahusiyo michezo na taaluma ya habari.
  Mkutano Mkuu utafunguliwa Jumamosi Desemba 29, saa tatu asubuhi na mgeni rasmi atakuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Kusaidia timu za Taifa za Vijana, Ridhiwani Kikwete.TASWA imechukua jukumu la kumualika kutokana na kuwa mdau mkubwa na rafiki wa chama chetu.

  Mkutano utafungwa jioni ya siku hiyo na Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene ambaye hiyo pia itakuwa nafasi nzuri kwake kuweza kuzungumza na wana habari kuhusiana na masuala mbalimbali ya kitaaluma.


  Katika mkutano huo wanachama wa TASWA watapata fursa ya kupokea na kujadili Ripoti ya Utendaji ya chama, Mapato na Matumizi, maendeleo ya chama na masuala mbalimbali yanayohusu waandishi wa habari za michezo na maendeleo ya michezo kwa ujumla.


  Pia kutakuwa na semina maalum itakayoendeshwa kwa washiriki wa mkutano huo, ili wawe na uelewa kuhusiana na ajenda ya kuinua kipato kwa wanachama ambayo nayo itajadiliwa kwenye mkutano huo.

  Kamati ya Utendaji ya TASWA imekubaliana iwasaidie wanachama wake waweze kujitegemea kwa kuanzisha Chama cha Akiba na Mikopo (SACCO’S), lakini imeamua kwanza iwaite wataalamu wa vyama vya ushirika watoe elimu juu ya jambo hilo na kukishakuwa na uelewa wa kutosha suala hilo litakuwa kama ajenda kamili ya kuanzisha chama hicho kwenye mkutano wetu.

  0 0


  Dar es Salaam December 27, 2012.

  NBC Tanzania wishes to confirm that after serving the bank as Managing Director since 1 June 2010, Lawrence Mafuru has with effect from 31 December 2012 decided to leave the bank to pursue other interests.

  Upon the receipt of regulatory approval, we will make an announcement on Lawrence’s replacement.
  The Board of NBC Tanzania wishes to take this opportunity to thank Mr. Mafuru for the contribution he made to NBC Tanzania since joining as Head of Treasury in August 2007 and in his role as Managing Director and at the same time wish him the best for the future.

  NBC is one of the most represented retail bank in the country with 45 years experience in providing financial services. Apart from offering traditional banking services, NBC also prides itself with an expanded branch network and footprint. NBC has 52 branches, 302 Visa enabled ATMs, and over 264 Points of Sales strategically located throughout the country. NBC has employed over 1200 staff.

  Conveniently everywhere.

  0 0

  Ofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Hadija Komba (kulia), akigawa zawadi ya madaftari kwa washindi wa shindano la kuvuta kamba kwa niaba ya watoto waliokuwepo kwenye Bonanza la michezo lililofanyika kwenye ufukwe Cine Club jijini Dar hivi karibuni.
  Wadau wa NSSF wakishindana kuvuta kamba.
  Washindi wa shindano la kuvuta kamba timu ya Wazazi wakiwa katika picha ya pamoja na Ofisa wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Hadija Komba (wa nne kulia), baada ya kuwakabidhi zawadi ya madaftari ishirini kila mmoja.

  0 0


  Kutokana na mgomo wa madaktari uliotokea kati ya tarehe 23 na 29 mwezi juni 2012.Wizara iliwasilisha malalamiko kwenye Baraza la madaktari Tanganyika ili lifanye uchunguzi kuhusu madaktari hao .
  Idadi ya madaktari wote waliogoma walikuwa 394, kati yao madaktari 376 walikuwa ni madaktari walio katika mafunzo kwa vitendo (Interns) kutoka hospitali za Muhimbili, K.C.M.C. Bugando, Mbeya Rufaa, St.Francis - Ifakara, Dodoma, Temeke, Mwananyamala, Amana, Haydom na Sekou Toure. Aidha, Madaktari waajiriwa(Registrar) 18 walishiriki katika mgomo huo kutoka hospitali ya Rufaa ya Mbeya.

  Baraza lilipitia malalamiko yote na limetoa adhabu stahiki kwa kila daktari aliyethibitishwa kushiriki katika mgomo huo.  Adhabu hizo zilikuwa katika makundi yafuatayo; onyo, onyo kali na kusimamishwa udaktari kwa muda wa kati ya mwezi mmoja na miezi sita.Vile vile kuna Madaktari ambao hawakuwa na hatia ya kushiriki katika mgomo na hivyo walifutiwa mashtaka.  0 0


  Mara nyingi ukisikia nyimbo kutoka Arusha huwa inakuwa ni Hip Hop.Vijana kutoka katika jiji hilo lililopo kaskazini mwa Tanzania na ambalo mara nyingi limekuwa likiitwa “Geneva Of Africa”, wamekuwa wakiegemea zaidi katika upande wa Hip Hop.

  Well…that is about to change kwani kuna kundi ambalo lenyewe limeanza kwa RnB. Linaitwa Dady Dadyz na linaundwa na Solomon Mwaigwisya {rapper wa kikundi}, Atufigwege Mwailunga{singer wa kundi} na Emanuel Mghase { huyu anadeal na vitu vingine vya kundi kama kusambaza nyimbo na kusimamia stage perfomance}

  Kupata wimbo wao unaokwenda kwa jina 'Mzuri' ambao umerekodiwa pale FishCrab Studios chini ya Producer,Lamar sogea bongocelebrity BOFYA HAPA

  0 0

  Mgombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM kata ya Kawe Amani Nkurlu (kulia) akirudisha fomu ya kugombea nafasi hiyo kwa Katibu wa UVCCM kata ya Kawe Bi. Aisha Katundu.
  Katibu wa UVCCM kata ya Kawe Bi. Aisha Katundu (kushoto) akipokea fomu aliyoijaza Bw. Amani Nkurlu kwa nafasi ya kugombea Uenyekiti UVCCM kata ya Kawe alipofika ofisini hapo leo saa 7 mchana.
  Mgombea wa Uenyikiti wa UVCCM kata ya Kawe, Amani Nkurlu, akizungumza machache na Katibu wa CCM Kawe Bi. Aisha Katundu katika ofisi za CCM Kawe.
  Amani Nkurlu akijaza fomu ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa UVCCM kata ya Kawe.
  Baadhi ya wakereketwa wa CCM katika picha ya pamoja nje ya ofisi ya CCM Kawe. Kutoka kushoto ni Katibu Mwenezi wa tawi la Umbwelani Kawe- Ramadhani Malenge, Katibu wa Wazazi Kawe- mama Katenda, mgombea nafasi ya ukatibu UVCCM kata ya Kawe – Sambili Tegemeo na mgombea nafasi ya Uenyekiti UVCCM kata ya Kawe - Amani Nkurlu.
  Picha na Josephat Lukaza

  Baada ya uchaguzi wa UVCCM katika kata la Kawe kuvurugika mapema mwaka huu, uchaguzi huo unaorudiwa sasa umefika patamu ikibakia siku moja tu kuchukua fomu huku vijana wengi wakijitokeza kuwania nafasi mbali mbali katika jumuiya hiyo ya vijana illiyopo wilayani Kinondoni.
  Akizungumza na waandishi wa habari, mmoja wa wagombea wa Uenyekiti wa UVCCM katika kata hiyo, Amani Nkurlu (23) alisema “Siku zote nimekuwa nikitafakari ni kwa namna gani nitaweza kutoa mchango wangu katika chama na kuchangia mustakabali wa taifa letu Tanzania kwa ujumla.”
  “Ninaamini CCM bado inahitaji vijana makini na wengi zaidi wakukisemea, kuishauri na kuleta chachu ya maendeleo katika utendaji wake wa kazi wa kila siku kichama na kiserikali. Hii ndio dira yangu kwa CCM, nina imani na chama changu na nimejikita katika kuchangia mabadiliko hayo kupitia Umoja wa Vjiana,” Nkurlu alisema. 
  Nkurlu ambaye ana Shahada ya Mawasiliano kutoka Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (SAUT) ameshawahi kushika nyadhifa mbali mbali za uongozi ukiwemo; Mjumbe wa Halmashauri Kuu CCM – Tawi maalum la Kambarage SAUT, Waziri wa Mambo ya Nje, Mbunge katika serikali ya wanafunzi, na Rais wa AIESEC akiwa hapo hapo chuoni. Mwaka 2010 Nkurlu pia alipata kugombea nafasi ya Umakamu wa Rais katika serikali ya wanafunzi chuoni hapo lakini hakufanikiwa kwa kupata kura 1278 kati ya kura 2995 zilizopigwa na 54 kuharibika.
  Hivi sasa Nkurlu anamalizia Stashahada ya juu kutoka Chuo cha Diplomasia na pia ni mwajiriwa katika moja ya makampuni ya mawasiliano na matangazo jijini Dar es Salaam kama Mshauri wa Mawasiliano.

  0 0
 • 12/27/12--11:26: Article 21


 • 0 0


  Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) limepongeza bingwa mpya wa uzito wa Super Middle katika bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki yaa Kati, Mtanzania Francis Cheka, pichani juu.

  Katika barua yake aliyomtumia Francis Cheka Mwenyekiti wa kamati ya Ubingwa wa IBF/USBA Lindsey Tucker alisema "Tunachukua fursa hii kukutakia maisha na mafanikio mazuri kama bingwa wa IBF na kumhimiza kuishi kama bingwa". 

  Cheka atatakiwa kutetea taji lake katika kipindi cha miezi sita kufikia mwezi wa 6 mwakani dhidi ya mpinzani ambaye ana rekodi ya mapambano yasiyopungua 15 na mengi awe ameyashinda hususan mapambano mawili ya mwisho.

  Aidha IBF inampongeza bondia Chiotcha Chimwemwe kutoka Malawi kwa ushupavu wake na ushindani mzuri katika pambano hilo lililofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid katika jiji la Arusha tarehe 26 Desemba, 2012.

  Imetolewa na:
   Onesmo A.M. Ngowi
  Rais
  IBF/USBA Afrka, Ghuba ya Uajemi an Mashariki ya Kati

  0 0
 • 12/27/12--13:34: E24 NEW YEAR’S EVE PARTY
 • Banana Zorro and the Flamboyant B Band to set off the 2013 fire works @ East 24 Bar. Free Champaigne & snacks on the house at 12m, access to roof-top for the best view of all fireworks in the city. Also entertainment from DJ Juniour & the Noise Makers spinnin’ non-stop, new Sheesha area and billiards competition. Welcome to our beer house.

  0 0
 • 12/27/12--19:00: kumbukumbu

 • LENDA SILAS MABECHE
  03/06/1970  -  28/12/2008
  siku ,wiki,miezi na sasa ni miaka 4 tangia ututoke 28-12-2008,unakumbukwa sana na baba yako Silas Mabeche, Mama yako Grace Sambay,wadogo zako Eric,Irene,Sarah ,Evah na wanao Shawn na Baraka,kwa ucheshi,na upendo wako uliyokua nao,pia unakumbukwa na ndugu jamaa na marafiki na familia ya mabeche kwa ujumla
  Bwana alitoa na bwana ametwaa ,jina lake lihimidiwe
  AMEN

  0 0

  Gloria Gaynor na ngoma yake ya 'I Will Survive' 
  anakumbukwa  vichwani mwetu hadi leo  kwa ukali wake...

older | 1 | 2 | 3 | (Page 4) | 5 | 6 | .... | 3272 | newer