Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110118 articles
Browse latest View live

TASWIRA KUTOKEA KWENYE MIWANI

$
0
0
 Taswira ya wadau wakiserebuka,iliyonaswa kutoka kwenye kioo cha Miwani.


kuna mtu kapigwa six o'clock leo, nani huyo??

JUST IN: MGENI AKWAMA KATIKA KILELE CHA MAWENZI MLIMA KILIMANJARO

$
0
0
Mtalii kutoka nchini Ujerumani anayefahamika kama Bi. Jeanne Traska (32) akiwa na muongoza wageni Athuman Juma leo majira ya saa mbili na nusu asubui wamekwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro kwa kamba iliyonasa na kuwafanya wasiweze kushuka chini wala kwenda juu.

Bi. Jeanne na Athuman Juma walianza kupanda mlima kupitia Kampuni ya Nordic Tours tarehe 18.3.2014 kwa kutumia njia ya Rongai - Kibo –Marangu safari ambayo ingewachukua siku tano. 
Hadi sasa taarifa za awali zinaonyesha kuwa Bi. Jeanne alitakiwa kwenda kileleni Kibo lakini katika mazingira yasiyofahamika alibadili uamuzi na kuelekea kilele cha Mawenzi ambacho huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.

Shirika la Hifadhi za Taifa kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours wanaendelea na jitihada za uokoaji kwa kutumia askari ambao wanaelekea eneo la tukio pamoja na helikopta itakayosaidia zoezi la uokoaji kwa kutegemea na hali ya hewa itakavyotulia ambapo hivi sasa kuna mawingu mazito katika eneo la mlima.

Umma utaendelea kufahamishwa maendeleo ya jitihada za uokoaji kadri zitakavyopatikana.


Imetolewa na Idara ya Mawasiliano

Hifadhi za Taifa Tanzania


22.03.2014

ngoma azipendazo ankal

$
0
0
Nu Shooz  na "Point of no return"

VYUO mbalimbali nchini Vyashauriwa kujenga mahusiano ya kirafiki ili kubadilishana uzoefu katika kufanya kazi zao.

$
0
0
  Mtembeza wageni wa Kanisa la Mkunazini akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Taifa cha Utalii kutoka Dar es salam walipokuwa wakitembelea Kanisa hilo.
 Wanafunzi wakipata maelezo kwa Mtembeza wageni juu sehemu walipokuwa wakihifadhiwa watumwa Kanisani hapo.
 Wanafunzi wakitoka nje kwa furaha mara baada ya kutembelea Kanisa la Mkunazini liliopo Mjini Unguja. 
 Hapa wanafunzi wakijichagulia katika moja ya maduka ya vinyago na nguo za Kiswahili yaliopo Ngome kongwe Mjini Unguja. 
 Wanafunzi wakionyeshana Spices. 
 Mtembeza wageni wa Kidishi Multi Spices Farm Bwana. Mur- tala Rashid akiwaonyesha mmoja wa mmea wa Spice na kuwafahamisha matumizi yake, mmea huo unaotambuliwa kwa jina la mchaichai katika chamba hilo.

MKUU WA MKOA WA NJOMBE AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA TENKI LA MAJI MWONGOLO MAKETE MJINI

$
0
0
 Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapeteni Mstaafu Aseri Msangi akiweka jiwe la msingi ujenzi wa tanki la maji lililopo Mwongolo Makete Mjini.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapt. Mstaafu Aseri Msangi akimsikiliza meneja wa maji Makete mjini akisoma taarifa, kushoto kwake ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro.
Meneja wa mamlaka ya maji makete mjini, Bw. Yonas Ndomba akimkabidhi taarifa ya ujenzi wa tanki la maji la Mwongolo Makete mjini Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi.
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi (katikati) akielekea kwenye ujenzi wa mradi wa maji Mwongolo Makete mjini kwa ajili ya kuweka jiwe la msingi, kulia ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro na kushoto ni katibu tawala msaidizi upande wa maji mkoa wa Njombe Bw. Christopha Nyandiga.
PICHA ZAIDI INGIA HAPA

PUNGUZENI GHARAMA YA KUCHIMBA VISIMA - WAZIRI MKUU

$
0
0

WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameitaka Wizara ya Maji itafute njia mbadala zitazosaidia kupunguza gharama za kuchimba visima ili wananchi waweze kupata maji safi na salama.
 
“Wizara ya Maji angalieni uwezekano wa kupunguza gharama za uchimbaji wa visima ili wananchi waweze kumudu kuchimba visima na wapate uhakika wa maji safi na salama,” alisema.
 
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo jana (Jumamosi, Machi 23, 2014), wakati akifunga Maadhimisho ya Wiki ya Maji Kitaifa yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma.
 
“Hivi sasa nimeambiwa gharama ya kuchimba kisima mita moja ni sh. 150,000/. Je kama mtu anataka kuchimba kisima chenye urefu wa mita 180 au 200 itakuwaje? Ni dhahiri kuwa watu hawataweza kumudu hizo gharama. Angalieni namna ya kuzipunguza,” alisisitiza.
 
Waziri Mkuu ambaye alikuwa akifunga maadhimisho hayo kwa niaba ya Rais Jakaya Kikwete aliwataka wakazi wa mkoa wa Dodoma waendelee kuthamini dhana ya uchangiaji ili waweze kumudu kuendeleza miradi hiyo.
 
Aliwataka pia watunze vyanzo vya maji na kutunza miundombinu pamoja na mitambo iliyonunuliwa kuendesha visima mbalimbali kwani maji yana gharama. “Ninawasihi sana muitunze mitambo iliyowekwa kuendeshea visima hivi kwani ni vifaa vya gharama sana,” aliongeza.
 
Mapema, Waziri Mkuu alizindua kisima cha maji kwenye kijiji cha Mkonze nje kidogo ya mji wa Dodoma ambacho ujenzi wake umegharimu sh. milioni 519.6/-. Kisima hicho chenye vichoteo 15, kitawanufaisha wakazi 5,887 kati ya 6,869 sawa na asilimia 85.7 ya wakazi wa kijiji hicho.
 
“Kabla ya kujengwa kisima hiki, ndoo ya maji ya lita 20 ilikuwa ikiuzwa sh. 500/- lakini sasa ndoo moja inauzwa kwa sh. 100/- tu,” alisema Mhandisi Mohammed Kali wakati akitoa taarifa ya mradi huo kwa Waziri Mkuu.
 
Waziri Mkuu pia aliweka jiwe la msingi kwenye tenki la maji katika Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) lenye uwezo wa kuhifadhi mita za ujazo 4,500. Ujenzi wake unatarajiwa kukamilika Novemba, 2014.
 
Akizungumza na wanajumuiya ya UDOM walioshiriki uzinduzi huo, Waziri Mkuu alisema mradi huo mkubwa unaenda sambamba na ujenzi wa mradi mwingine mkubwa wa maji taka (recycling plant). “Ninawasihi muangalie uwezekano wa kutumia maji machafu yatakayosafishwa ili yatumike kumwagilia miti na maua muweze kutunza mandhari ya UDOM,” alisema.
 
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa tenki hilo, Waziri wa Maji, Prof. Jumanne Maghembe alisema hadi kukamilika kwake, mradi huo utagharimu sh. bilioni 28. Alisema mradi huo unaojumuisha ujenzi wa miundombinu ya maji safi na maji taka katika Chuo hicho, umefanyika chini ya Mpango wa Kuendeleza Sekta ya Maji nchini (WSDP).
 
Naye Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia anayesimamia nchi za Tanzania, Burundi na Uganda, Bw. Phillippe Dongier alisema wao kama wadau wa maendeleo, wanaona fahari kushirikiana na Wizara ya Maji katika kuleta maendeleo ya sekta hiyo kwa Watanzania.
 
Uzinduzi wa miradi hiyo ya maji ni sehemu ya miradi 13 iliyopangwa kuzinduliwa mkoani Dodoma kwenye maadhimisho ya maji ya mwaka huu. Hata hivyo, mkoa huo una miradi 69 ya maji ambayo ujenzi wake unaendelea kwa awamu tofauti.
 

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMAPILI, MACHI 23, 2014

Tamasha la Bagamoyo Marathon lazinduliwa

$
0
0
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel (kushoto) akishikana mikono na Mkurugrenzi wa Kampuni ya 4Beli, Gilbert Herman baada ya kuzindua  Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo Wilayani  Bagamoyo, Pwani .  Anayeangalia ni,  Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali.
Katibu Tawala wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali alizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo iliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani .  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala, Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel na Mkurugenzi wa 4Beli, Giulbert Herman.
Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf  Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo katika uzinduzi wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel, Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya 4Beli, Deogratius Soka (kulia) akisoma hotuba wakati wa uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani mwishoni mwa wiki.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala,  Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel, Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman.
Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Elisante ole Gabriel akizungumza katika hafla ya uzinduzi  wa Tamasha la Kihistoria la Bagamoyo uliyofanyika Bagamoyo, Mkoani Pwani.  Wengine kutoka kushoto ni, Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Riadha Tanzania, Mama Ombeni Zavala,  Ofisa Elimu wa Mkoa  wa Pwani , Yusuf Kipengele aliyekuwa akimwakilisha mkuu wa mkoa huo,  Katibu Tawala  wa Wilaya ya Bagamoyo, John Mhali na Mkurugenzi wa 4Beli, Gilbert Herman.
Baadhi ya watu waliohudhuria uzinduzi huo wakimsikiliza mgeni rasmi.

MAADHIMISHO YA WIKI YA MAJI MKOA WA NJOMBE YAFANA KATIKA VIWANJA VYA MABEHEWANI

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Aseri Msangi akipata maelekezo kwenye banda la idara ya maji kuhusu bili za maji, katika wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
Mkuu wa mkoa Kapt. Msangi akisikiliza maelekezo toka kwa mtaalamu wa maji, katikati ni mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro.
Mkuu wa mkoa akipata maelekezo kuhusu mfumo mzima wa maji Makete mjini unavyofanya kazi.
 Kikundi cha sanaa cha SUMASESU kikitumbuiza kwenye maadhimisho hayo ya wiki ya maji.
 Kikundi cha sanaa kijulikanachoa kama Mchana Hasarani kikikonga nyoyo za washiriki wa maadhimisho hayo.
 Mkuu wa wilaya ya Makete Mh. Josephine Matiro akizungumza kwenye maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani Makete mjini.
 Mkuu wa mkoa wa Njombe kapteni Mstaafu Aseri Msangi akihutubia wananchi waliofika kumsikiliza katika maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa katika viwanja vya mabehewani makete mjini.
Mkuu wa mkoa akihutubia wananchi.Picha zote na Edwin Moshi, Makete

Naibu Waziri afunga mashindano ya Netball Afrika Mashariki

$
0
0
Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akitoa hotuba yake wakatiwa uzinduzi wa mashindano ya klabu bingwa ya mpira wa pete ya Afrika Mashariki.

 Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akicheza mpira wa Pete kuashiria ufunguzi wa Mchezo wa kwanza wa mashindano ya mpira wa Pete wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki kati ya Uganda Bima na Magereza Morogoro.

 Waziri wa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Abdulla Juma Abdulla Saadala akicheza mpira wa Pete kuashiria ufunguzi wa Mchezo wa kwanza wa mashindano ya mpira wa Pete wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki kati ya Uganda Bima na Magereza Morogoro
========  =====  ======



EAST AFRICAN NETBALL CHAMPIONSHIPS OPENS IN DAR ES SALAAM
ANTHONY ISHENGOMA

Dar es Salaam March 22-The Deputy Minister Ministry of East African Cooperation Dr. Juma Abdulla Juma Abdulla Saadala today officially opened East African Netball Competitions in Dar es Salaam. 

Addressing Netball Athletes from East African Countries the Deputy Minister pointed out that these competitions marks our long good relationship that has existed before the first defunct community of 1977 stressing that since the beginning of the competitions both defunct and the new community has enjoyed sports cooperation. 

Quoting article 19 of the Treaty for the establishment of the East African Community the jovial Minister said that it requires Partner States to strengthen and harmonize cultural and sports relationship and that is what we are implementing today. 

 He said the Competitions intend to strengthen the integration by bringing on board unit among East Africans, desire to win competitions, maintain health and the ability to win competitions and to develop friendship among athletes of East Africa. 

The East African Netball Association and Kenya Netball Association Secretary Lilian Anup  has urged referees to officiate games according to the rules of the game maintaining that  failure to adhere on rules may lead to punitive measures against them. 

She said that Tanzania has been missing in East African Netball Competitions for unknown reasons and failed to hide how glad she was after Tanzania returned adding that the lost glory is finally retained. He thanked Tanzania Netball Association Chairman Anna Kabila for succeeding the mission. Tanzania has been missing in the competition since the year 2006.  

She called for sponsors to join the Netball game to stop it from its demise adding that Uganda Netball female competitions are recording good status due to the sponsorship they enjoy calling them the best in East Africa. 

Marealle apewa tena Ukamanda wa Vijana wa CCM Moshi Mjini

$
0
0
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Kamanda wa vijana UVCCM Bw Agrey Marealle Akila kiapo cha utii kwa CCM wakati wa kusimkwa kuwa Kamanda wa vijana wa CCM wilayani humo mbele ya mgeni rasimi Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)
 Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Wilaya ya Moshi Mjini(MNEC) Bw Agrey Marealle akiwa amekalishwa kwenye kigoda huku akiwa na ngao na mkuki mara baada ya kusimikwa kuwa Kamanda wa vijana UVCCM wilayani humo na Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(hayuko pichani)
 Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(kushoto) akimvalisha kofia Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Moshi Mjini Bw Aggrey Marealle kuwa Kamanda wa Vijana wa CCM wilayani humo Mjini katika halya iliyofanyika viwanja vya CCM katab ya Njoro.
Mkamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Mboni Mhita(kushoto) akimkabidhi mkuki Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka wilaya ya Moshi Mjini Bw Aggrey Marealle katika hafla ya kumsimika kuwa Kamanda wa Vijana wa UVCCM wilayani humo katika sherehe ya kumsimika iliyofayika katika viwanja vya CCM kata ya njoromjini humo.
=======  =======  =======
Marealle apewa tena Ukamanda wa Vijana wa CCM Moshi Mjini
*Ahimiza mshikamano kwa wanaCCM

MJUMBE wa halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM), kupitia Moshi  Mjini, mkoani Kilimanjaro, Aggrey Marealle, amesema mshikamano   miongoni mwa wanachama wa chama hicho ndiyo pekee utakaopelekea chama    hicho kufanya vyema katika chaguzi zijazo.

Bw. Marealle aliyasema hayo juzi mjini Moshi, wakati wa hafla ya
kusimikwa kwake kama kamanda wa vijana wa umoja wa vijana wa CCM,
(UVCCM), wa wilaya ya Moshi Mjini  kwa kipindi cha pili cha miaka
mitano, hafla iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa tawi la wakereketwa
la Marealle lililopo Kata ya Bondeni, Moshi Mjini.

"Changamoto kubwa ambayo CCM imekuwa ikikumbana nayo nyakati za
kuelekea chaguzi mbali mbali ni kutokuwa na mshikamano jambo ambalo
mara nyingi hutokana na makundi ndani ya chama, ni vyema tukaepuka
hili na msamiati wetu mpya uwe ni mshikamano, hapa tutashinda",
alisema.

Aidha alitoa wito kwa wananchi hususan wanachama wa CCM kutokutumia 
changamoto za kimaisha walizonazo kama sehemu ya maamuzi katika 
kuchagua viongozi na mstakabali mwingine wa kisiasa.

Katika hafla ya uzinduzi wa tawi hilo la wakereketwa, Bw. Marealle
alisema kada ya vijana ni nguzo ya Taifa ambayo haina budi kulindwa
kwa kuhakikisha maswala yanayowahusu yanapewa kipaumbele ili wasikate 
tamaa.

Akihutubia katika hafla hiyo ambayo ilienda sanjari na kusimikwa
makamanda wapya wa UVCCM Kata zote za Moshi Mjini, Makamu Mwenyekiti    
wa UVCCM Taifa, Mboni Mhita, alisema kuwa kazi kubwa ya makamanda wa    
vijana wa CCM ni kuwaunganisha vijana, kubaini kero zao na  
kuzishughulikia kwa wakati.

Bi Mhita alielezea kazi zingine kuwa ni pamoja na kuwasaidia vijana
kupata ajira za zikiwemo zile za kujiajiri wenyewe pamoja na kutoa
ushauri kwa vijana unaohusiana na mwelekeo wa kisiasa na kimaisha kwa
ujumla.

"Kwa kufanya hivi mtakuwa mnaweka nguzo imara ya Taifa kwa ajili ya
miaka mingi ijayo", alisema na kutoa wito kwa vijana kuwa tayari
kupokea ushauri watakaopata kutoka kwa makamanda hao wapya wa vijana.

Aidha aliwaasa vijana kuiepusha na matumizi ya dawa za kulevya pamoja
na anasa zilizopitiliza ambapo alisema mambo hayo yanachangia kwa
kiasi kikubwa kupunguza ari na nguvu kazi ya Taifa.

MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR ATEMBELEA SHAMBA LA WAZIRI MKUU DODOMA

$
0
0
 Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wanachuo wa Chuo cha Nyuki cha Tabora waliotembelea shamba lake lililopo Zuzu, Dodoma kujifunza ufugaji bora wa nyuki  Machi 22, 2014.
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiongozana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd kukagua zao la zabibu  katika shamba lake  lililopo Zuzu , Dodoma
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitoa maelezo kuhusu  zao la migomba kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Idd ambaye alitembelea shamba lake lililopo Zuzu mjini Dodoma. Wa pili kulia ni Mbunge wa Simanjiro, Christopher ole Sendeka na kulia ni Majasiliamali wa Dar es salaam, Alphonce Buhatwa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

DMV YAFANYA MISA YA KUMBUKUMBU NA KUOMBOLEZA KIFO CAROLINE MWAISELAGE DMV

$
0
0
Misa ya kumbukumbu iliyofanyika siku ya Jumamosi March 22, 2014 College Parka Maryland kwa ajili ya maerehemu Caroline Mwaiselage aliyekuwa mfanyakazi wa Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani aliyekutwa na mauati alipokua amekwenda Tanzania march 7, 2014 mwaka huu.
Kushoto ni mume wa marehemu Chris Muhoka na kulia Martin Koroso aliyekuja toka Michigan 
Watoto wa marehemu. 

NEWZZZ ALERT: MTALII ALIYEKWAMA KILELE CHA MAWENZI MLIMA KILIMANJARO AOKOLEWA.

$
0
0
Mtalii Jeanne Traska kutoka Ujerumani
Bi.Jeanne Traska kutoka Ujerumani na Muongoza Wageni Athumani Juma wakiwa katika Lango la Marangu pamoja na vifaa mbalimbali walivyokwama navyo katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro mara baada ya kuokolewa.

Kikosi cha Uokoaji katika Hifadhi ya Taifa Kilimanjaro kimefanikiwa kumuokoa mtalii Bi. Jeanne Traska (32) kutoka Ujerumani pamoja na muongoza wageni Athuman Juma ambao jana walikwama katika kilele cha Mawenzi Mlimani Kilimanjaro. Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kufika eneo la kilele cha Mawenzi na kwa kutumia mbinu za uokoaji za kisasa kabisa kiliweza kuwanasua majira ya kumi na moja jioni.


Licha ya hali mbaya ya hewa iliyotokana na mawingu mazito katika eneo hilo, Kikosi cha Uokoaji cha TANAPA kiliweza kukabiliana na hali hiyo na kuweza kuwanasua na kisha kuwapeleka katika kituo cha Horombo majira ya saa mbili usiku ambapo walichukuliwa na gari kupitia njia maalum ya uokoaji na kufika katika Lango Kuu la Marangu saa nne na nusu usiku.


Hali ya hewa ilisababisha helikopta maalum iliyoletwa kwa ajili ya zoezi la uokoaji kushindwa kufanya kazi kwa kuwa mawingu mazito hayakuwezesha marubani kuliona eneo la kilele kwa urahisi.


Hivi sasa mtalii huyo pamoja na muongoza wageni wake bado wapo chini ya uangalizi wa hifadhi kwa kushirikiana na Kampuni ya Nordic Tours iliyomleta mgeni huyo.


Aidha, kwa kuwa ni tukio lisilo la kawaida, uongozi wa hifadhi unaendelea kuchunguza sababu zilizowafanya kuchepuka njia na kuelekea kilele cha Mawenzi badala ya Kibo. Kwa kawaida Kilele cha Mawenzi huwa hakitumiwi na watalii isipokuwa kwa kujaza fomu maalum inayoonyesha kuwa mgeni amekubali kwa hiyari yake kupanda kilele hicho.


Imetolewa na Idara ya Mawasiliano

Hifadhi za Taifa Tanzania

23.03.2014

newdeal afrika and ben TV sa thank you to diamond platinumz

$
0
0
 The  management  of  Newdeal  Africa  and  Ben television in  London want  to  the  thank  Tanzania's  greatest  hero,  singer  and song writer Diamond Platinumz. Our  producers  here say  that you  are  among  the  greatest in  the  modern Music  industry Tanzania  has  produced.Keep it  up.It  was  great  to  work  with  you.
Thank  you.


SIMBA YAPEPESUKA, YADUNGWA 1-0 NA COASTAL UNION

$
0
0
Wachezaji wa Simba wakiingia uwanjani wakati wa mchezo wao na Coastal Union ya Tanga.
Wachezaji wakisalimiana.
 Benchi la ufundi la Simba.
 Kikosi cha Coastal Union ya Tanga.
 Kikosi cha Simba.
 Mashabiki wa Simba wakishangilia timu yao.
Mashabiki wa Simba wakichagiza ushindi.
 Mshambuliaji wa Simba, Ramadhani Singano akimiliki mpira huku akizongwa na beki wa Coastal Union ya Tanga, Hamadi Juma katika mchezo wa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Coastal ilishinda 1-0. (Picha na Francis Dande)
Mshambuliaji wa Simba, Haruna Chanongo akimtoka beki wa Coastal Union ya Tanga, Mohamed Mtindi katika mchezo uliofanyika leo kwenye Uwanja wa taifa.
 Wachezaji wa coastal wakishangilia ushindi wa timu yao.
 Mashabiki wa simba wakiwa wameduwaa baada ya kumalizika kwa mchezo na kupata kipigo cha bao 1-0.
Wachezaji wa Coastal Union wakiomba duwa baada ya kumalizika kwa mchezo. Picha na Francis Dande

Article 7

IZAAS MEDICAL PROJECT IN BUKOBA HAVE A SPECIAL CASE

$
0
0
With salams and jambo from IZAAS 
 1. This is a special case, please help my sister 
 2. She was offered to choose between crunches and wheel chair and she happily choose crunches. Kindly read below

TIC yasaini mkataba wa ushirikiano wa pamoja na Kampuni ya Tanga Fresh Ltd

$
0
0
Kituo cha Uwekezaji Nchini (TIC) na Kampuni ya Tanga Fresh Ltd pamoja na wajasiriamali wapatao 60 kutoka katika vituo mbalimbali vya kupoozeshea maziwa katika mkoa wa Tanga wametiliana saini mkataba wa ushirikiano kwa ajili ya kuwajengea uwezo wajasiriamali hao ili waweze kukua kibiashara. 
 Utiaji saini huo umefanywa na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bi. Juliet Kairuki; Meneja Mkuu wa Tanga Fresh Ltd, Bw. Michael Karata na mwakilishi wa wajasiriamali hao, Bi. Asnat Mbwambo. Tukio hilo lililofanyika mwishoni mwa wiki mjini Tanga lilishuhudiwa na Mkuu wa mkoa huo, Bi. Chiku Gallawa. 
 Akizungumza wakati wa makubaliano hayo, Bi. Kairuki alisema pamoja na shughuli mama za kituo cha uwekezaji za kutangaza fursa za uwekezaji ndani na nje ya nchi, serikali inatambua umuhimu wa kuwajengea uwezo wajasiriamali wadogo. 
 “TIC kama moja ya taasisi za serikali tunatambua uwepo wa wajasiriamali wadogo na umuhimu wao kwa uchumi , tunatambua kuwa wanahitaji kukua kibiashara, hivyo kwa kufanya hivi tunatimiza azma ya serikali katika kuwainua watu wetu,” alisema mkurugenzi huyo. 
 Aliisifu kampuni ya Tanga Fresh Ltd kwa kukubali kugharamia asilimia 50 katika kuendesha mafunzo ya program hiyo pamoja na huduma nyingine katika kipindi chote kuanzia Machi 2014 hadi Machi 2015. 
 “Napenda kuchukua fursa hii kutoa wito kwa makampuni mengine kuiga mfano wa Tanga Fresh Ltd na kuwa na moyo wa kujitolea katika kusaidia wajasiriamali kupata elimu ambayo itasadia kuwajengea uwezo,” alisema. 
 Alisisitiza kuwa kituo hicho kitaendelea kushirikiana na serikali ya mkoa wa Tanga na wadau wengine katika kuhakikisha kuwa shughuli za uwekezaji zinaendelea kukua katika mkoa huo. “Mkoa wa Tanga una fursa nyingi, hivyo ni jukumu letu kushirikiana na taasisi nyingine pamoja na serikali ya mkoa katika kukuza uwekezaji,” alisema. 
 Kwa upande wake, Bi. Gallawa, alisema TIC pamoja na kampuni ya Tanga Fresh wamefungua milango kwa wajasiriamali wa mkoa wake, hivyo ni jukumu la wafanyabiashara hao kuzingatia kwa umakini kile watakachofundishwa. 
 “Tanga Fresh na TIC wamejitoa sana, nawaomba muwe makini katika kufuatilia na kuweka katika matendo kile mtakachofundishwa,” alisema. Aliongeza kuwa mkoa wake umefarijika sana na utiaji saini wa makubaliano hayo kwani ni njia mojawapo ya kuona wajasiriamali wanaanza safari ya kuelekea katika mafanikio ya kweli. 
 “Sasa njia inaanza kuonekana, si kwenu ninyi tu wajasiriamali bali hata sisi viangozi wenu, hii inatupa moyo kuwa yapo makampuni binafsi na taasisi za umma ambazo zipo mstari wa mbele kusaidia watu wa chini katika biashara,” aliongeza. 
 Awali, Bw. Karata alisema kampuni yake itaendelea kutoa ushirikiano pale serikali itakapokuwa tayari, hasa katika kusaidia watu walio katika sekta za kilimo na ufugaji. “Sisi tumekuwa tunafanya kazi moja kwa moja na wafugaji pamoja na wakulima wanaotuzunguka, hivyo ni jukumu letu kuwaangalia na kuwainua kiuchumi ili waweze kuboresha maisha yao,” alisema Bw. Karata. Aliongeza kuwa pamoja na kununua maziwa kutoka kwa wafugaji hao wadogo bado wamekuwa wakitoa elimu hasa ya ufugaji pamoja na kilimo ili waweze kufuga kisasa zaidi.
 Mbali na ofisi ya mkuu wa mkoa kushuhudia zoezi hilo la utiaji saini makubaliano hayo, wadau wengine waliofika katika sherehe hizo ni benki za NMB, CRDB, na EXIM pamoja na TCCIA.
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bi. Chiku Gallawa (katikati)  akikata utepe kuashiria kuzinduliwa rasmi kwa programu ya mwaka mmoja ya  kutoa elimu ya biashara kwa wajasiriamali wadogo wapatao 60 kutoka katika vituo mbalimbali vya kupoozeshea maziwa katika mkoa huo mwishoni mwa wiki mjini Tanga.  Programu hiyo itaendeshwa na Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) kwa kushirikiana na kampuni ya Tanga Fresh Ltd.  Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIC, Bi. Juliet Kairuki na Meneja Mkuu wa kampuni ya Tanga Fresh, Bw. Michael Karata (kulia).
 Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bi. Chiku Gallawa ( katikati )  akionyesha mikataba kwa waandishi wa habari mara baada ya  Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) na Kampuni ya Tanga Fresh ltd pamoja na wajasiriamali wapatao 60 kutoka katika vituo mbalimbali vya kupoozeshea maziwa katika mkoa wa Tanga kutiliana saini mkataba wa kuwajengea uwezo kibiashara wajasiriamali hao mwishoni mwa wiki mjini Tanga. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa TIC Bi. Juliet Kairuki na kulia ni Meneja Mkuu wa Tanga Fresh Bw. Michael Karata.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC) Bi. Juliet Kairuki akitia saini mkataba wa ushirikiano wa pamoja na Kampuni ya Tanga Fresh Ltd pamoja na wajasiriamali wapatao 60 kutoka katika vituo mbalimbali vya kupoozeshea maziwa  katika mkoa wa Tanga mwishoni mwa wiki iliyopita ili kuwajengea uwezo wajasiriamali hao. Wa pili kulia  ni Meneja Mkuu wa Tanga Fresh Ltd, Bw. Michael Karata, mwakilishi wa wajasiriamali hao, Bi. Asnat Mbwambo (kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Bi. Chiku Gallawa (kulia). 

MAMLAKA YA HALI YA HEWA ZANZIBAR YAADHIMISHA SIKU YA MAMLAKA HIYO DUNIANI

$
0
0
Na Miza Kona - Maelezo Zanzibar
 Wanafunzi wa vyuo na sekondari wameitaka jamii kuwa na mwamko wa kufuatilia taarifa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya Hewa pamoja na kutembelea vituo hivyo ili kuweza kujua na kupata taarifa za mwenendo wa hali ya hewa Nchini. 
Kauli hiyo wameitoa leo huko katika ofisi za Mamlaka hiyo ziliopo Uwanja wa Ndege Zanzibar katika Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani, wamesema jamii imekuwa haina mwamko mzuri katika kufuatilia taarifa za hali ya hewa nchini. 
Wamesema kuwa kila siku jamii inatakiwa kujua na kufuatilia taarifa hizo ili kuweza kufahamu hali ya hewa ilivyo ili kuepukana na majanga na matatizo yanaweza kutokea ambapo mamlaka hiyo hutoa taarifa. 
Aidha wanafunzi hao wamewataka wanafuzi wenzao kutembelea katika vituo vya Mamlaka hiyo kwenda kusoma kwa vitendo na kuona shughuli hizo zinavyotolewa. Wanafunzi hao wametembelea sehemu mbali mbali na kuona jinsi shuguli za kituo hicho zinavyofanyika ikiwepo sehemu ya usalama wa Anga, kipima joto, kipima mvua, kipima upepo, pamoja utabiri wa hali ya hewa. 
Wakitoa maelezo kwa wanafunzi maafisa mbali mbali wa Mamlaka hiyo wamesema kuwa huduma nyingi zinazoendeshwa nchini huwa zinashirikiana na Mamlaka ya Hali ya Hewa kwa taarifa za hali ya hewa ili kuendesha kazi zake. 
Wamefahamisha Mamlaka ya Hali ya Hewa hushirkiana na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege jinsi ya kuingia kutoka kwa ndege nchini na namna ya kuwasiliana katika uendeshaji shughuli wa zake. Aidha wamefahamisha kuwa Mamlaka hutoa taarifa zake kwa kutumia vipimo mbali mbali viliopo nchini vikiwemo kipima ju, kipima upepo pamoja na kipima mvua na kutoa taarifa jamii jinsi ya hali ya hewa ilivo na itakavyokuwa nchini. 
 Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Mohammed Khamis Ngwali , amesema vijana wanatakiwa kubadilika na kuchukua tahadhari za kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa ili kizazi kijacho kiweze kufaidi dunia yenye mazingira bora. 
Hata hivyo Shirika la Hali ya Hewa linawahamasisha vijana katika kujihisha na masuala ya hali ya hewa ili kupata maarifa na uelewa na hatua za kuchukua katika kipindi cha hiki cha mabadiliko ya hali ya hewa duniani. 
Amesema hatua hii muhimu ikichukuliwa na vijana italeta ustawi wa kizazi cha sasa na kijacho kwa kujenga jamii iliyo imara baadae pamoja na kuokoa dunia kwenye majanga yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini. Maadhimisho ya Siku ya Hali ya Hewa Duniani hufanyika kila ifikapo tarehe 23 Machi, kauli mbiu ya mwaka huu ni ushirikishwaji wa vijana katika Masuala ya Hali ya Hewa.
 Mtaalamu wa Hali ya Hewa Bw. Hassan Khatib Ame akitoa ufafanuzi wa kitu kwa wanafunzi wa Skuli ya Kombeni walipotembelea Ofisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa iliopo ndani ya Uwanja wa ndege wa Zanzibar ikiwa ni pamoja na kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyo adhimishwa leo.
 Afisa Usalama wa Anga Bw. Rashid Omar Mselem akiwafahamisha kitu wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani kuhusiana na usalama wa Anga na Hali ya Hewa pindi inapokuwa mbaya, katika kuadhimisha siku ya Hali ya Hewa Duniani.
 Wanafunzi wakipata maelezo juu ya upimaji wa Hali ya Hewa kwa Mtaalamu wa Hali ya Hewa Bw. Khamis A. Salum.
 Wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani wakisikiliza kwa makini maelezo ya Mtabiri wa Hali ya Hewa (hayupo pichani) Bw. Hafidhi Juma Bakari walipofika ofisini kwake Uwanja wa Ndege wa Zanzibar 
 Mtabiri wa Hali ya Hewa Bw. Hafidhi Juma Bakari akifafanua kitu kwa wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani walipofika ofisini kwake kwa ziara ya kimasomo na kusherehekea siku ya Hali ya Hewa Duniani iliyoadhimishwa leo Duniani kote.
 Mkurugenzi Mamlaka ya Hali ya Hewa Zanzibar Bw. Muhammed Khamis Ngwali (wakatikati) waliosimama akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa Chuo cha Uwalimu Chukwani.
Mkurugenzi Mamlaka ya Hali ya Hewa Zanzibar Bw. Muhammed Khamis akiwa na baadhi ya wafanyakazi wa Mamlaka hiyo kwenye picha ya pamoja katika kusherehekea siku ya Hali ya Hewa Duniani. Picha na Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar
Viewing all 110118 articles
Browse latest View live




Latest Images