Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 391 | 392 | (Page 393) | 394 | 395 | .... | 3283 | newer

  0 0
 • 03/17/14--20:00: ngoma azipendazo ankal

 • Juwata Jazz Band ft. Nico Zengekala 'Solemba' (with lyrics)

  0 0

  Baada ya kutokea vurugugu zilizosababishwa na baadhi ya wajumbe wa Bunge Maalum kupelekea Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Warioba  (pichani juu, akiongozwa kutoka Bungeni baada ya zoezi la kuwasilisha rasimu ya katiba kuahirishwa) kutokuwasilisha rasimu ya pili ya Katiba kwa wajumbe hao, Mwenyekiti wa Bunge Maalum Mhe. Samuel Sitta aliitisha kikao cha maridhiano na baadhi ya wajumbe wanaowakilisha makundi mbalimbali yaliyopo katika Bunge hilo ili kupata muafaka wa hoja zilizokuwa zimejitokeza.
  Baada ya kikao hicho kilichodumu kwa takribani masaa manne na kumalizika saa nne za usiku, Mhe. Samuel Sitta amewaeleza waandishi wa Habari matokeo ya kikao hicho, ambapo wajumbe wa kamati hiyo wameafikiana yafuatayo:

  1. Kikao cha Bunge Maalum kitaendelea kesho tarehe 18 Machi, 2014 Saa tatu asubuhi kwa kuanza na shughuli za kuapisha baadhi ya wajumbe ambao hawakuapa awali kwa muda wa dakika 30
  2. Kuhusu muda wa kuwasilisha Rasimu ya Katiba, Wajumbe wameafikiana Mwenyekiti wa Tume ya Marekebisho ya Katiba Jaji Joseph Warioba kuwasilisha Rasimu ya pili ya Katiba kwa wajumbe hao kwa muda wa saa nne badala ya saa mbili alizokuwa ametengewa awali, ambapo uwasilishwaji wa rasimu huo utaanza rasmi saa tatu na nusu asubuhi baada ya shughuli ya viapo kumalizika.
  3. Saa kumi kamili jioni kutakuwa na semina ya kanuni itakayofanyika katika Ukumbi wa Bunge ambapo Mwenyekiti wa iliyokuwa kamati ya kanuni Mhe. Prof. Costa Mahalu na wenzeke watawawezesha wajumbe kupitia vifungu vya kanuni hizo za Bunge Maalum, ambapo semina hiyo itaendelea hadi jumatano tarehe 19 machi, 2014
  4. Siku ya Alhamisi tarehe 20 Machi, kutakuwa na semina itakayoendeshwa na maafisa wawili kutoka kenya ambao watatoa uzoefu wao katika maeneo haya.
  5. Aidha wajumbe wamekubaliana Mhe. Rais kulihutubia Bunge siku ya Ijumaa jioni kama ilivyokuwa imepangwa awali, ambapo asubuhi kutatanguliwa na shughuli za Mwenyekiti wa Bunge Maalumu kuunda kamati 14 za Bunge Maalum.
   News alert hii imeletwa na 
  Owen Mwandumbya Kutoka Sekretariet ya Bunge Maalum
  Kwa picha zaidi baada ya hapo BOFYA HAPA

  0 0

   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja akibadilishana Mkataba wa Uwekezaji katika shughuli za Kilimo na Ufugaji na Mwekezaji toka Nchini Uturuki ambaye pia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya TARBIM LTD. Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza limetiliana saini Mkataba huo ambao utatekelezwa katika Shamba la Magereza lililopo Bagamoyo, Mkoani Pwani.
   Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja( meza kuu mbele) akisaini Mkataba  wa Uwekezaji katika shughuli za Kilimo na Ufugaji na Mwekezaji toka nchini Uturuki, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TARBIM LTD, Bw. Baddal Calikusu(wa kwanza toka kulia). Hafla fupi ya  utilianaji saini Mkataba huo umefanyika Machi 17, 2014 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza, Jijini Dar es Salaam.

  Mkurugenzi wa Kampuni ya TARBIM LTD(kulia mbele meza kuu) akiagana rasmi na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto mbele meza kuu) mara baada ya hafla fupi ya utilianaji saini wa Mkataba wa Uwekezaji katika shughuli za Kilimo na Mifugo ambapo Jeshi la Magereza kupitia Shirika lake la Magereza litatekeleza miradi ya Uzalishaji ya Kilimo na Ufugaji katika Shamba la Magereza lililopo Bagamoyo, Mkoani Pwani kwa kushirikiana na Kampuni ya Mwekezaji ya TARBIM LTD(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza)
  Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza Nchini, John Casmir Minja(mbele meza kuu) akitoa utambulisho wa Makamishna wa Jeshi la Magereza(waliopo kushoto)kwa Mwekezaji wa shughuli za Kilimo na Ufugaji kabla ya kutiliana saini Mkataba wa Uwekezaji wa masuala ya Kilimo na Ufugaji katika Shamba la Magereza lililopo Bagamoyo, Mkoani Pwani.

  0 0

  Wachezaji 31 wameteuliwa kujiunga na timu ya Taifa ya vijana wenye umri chini ya miaka 20 (Ngorongoro Heroes) kwa ajili ya michuano ya Afrika ambayo fainali zake zitafanyika mwakani nchini Senegal.

  Ngorongoro Heroes itakayokuwa chini ya Kaimu Kocha John Simkoko akisaidiwa na Mohamed Ayoub inaingia kambini kesho (Machi 19 mwaka huu) jijini Dar es Salaam kujiandaa kwa mechi ya kwanza dhidi ya Kenya itakayochezwa kati ya Aprili 4-6 jijini Nairobi.

  Kikosi kinachounda timu hiyo ambayo itarudiana na Kenya kati ya Aprili 25-27 mwaka huu jijini Dar es Salaam kinajumuisha pia baadhi ya wachezaji walioonekana katika mpango wa ung’amuzi wa vipaji kwa ajili ya maboresho ya Taifa Stars.

  Wachezaji walioitwa ni makipa Aishi Manula (Azam), Hamad Juma Hamad (Scouting- Temeke), Manyika Peter Manyika (Scouting- Ilala) na Mwinyi Hassan Hamisi (Mtende, Zanzibar).

  Mabeki wa pembeni ni Ayoub Semtawa (Coastal Union), Edward Charles (JKT Ruvu), Frank Linus Makungu (Scouting- Rukwa), Gabriel Gadiel Michael (Azam), Hussein Mkongo (Ashanti United) na Ibrahim Said Mohamed (Chuoni, Zanzibar). Mabeki wa kati ni Bashiru Ismail (Tanzania Prisons), Faki Rashid Hakika (Ashanti United) na Pato Ngonyani (Majimaji).

  Viungo ni Ally Nassoro (Coastal Union), Bryson Raphael (Azam), Farid Musa (Azam), Hamid Mohamed (Mbeya City), Hassan Mbande (Mtibwa Sugar), Ibrahim Mohamed Ibrahim (Scouting- Ilala), Idd Seleman (Ashanti United), Mohamed Issa Juma (Acudu, Afrika Kusini), Muhsin Ally Muhsin (Scouting- Kinondoni), Seleman Magoma (Scouting- Ruvuma) na Tumaini John (Scouting- Mwanza).

  Washambuliaji ni Ally Salum Kabunda (Ashanti United), Ibrahim Hamad Hilika (Zimamoto, Zanzibar), Jafari Mwambusi (Mbeya City), Kelvin Friday (Azam), Ramadhan Bilal (Mlale JKT), Salum Abdilah Mineli (Ndanda) na Sibiank Lambard (Tanzania Prisons).

  YANGA, AZAM KUUMANA VPL TAIFA
  Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaendelea kesho (Machi 19 mwaka huu) kwa mechi kati ya Yanga na Azam itakayochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kuanzia saa 10.30 jioni.

  Tiketi kwa ajili ya mechi hiyo zitaanza kuuzwa saa 2 asubuhi katika magari maalumu kwenye vituo vya Shule ya Sekondari Benjamin Mkapa, Ubungo Terminal, mgahawa wa Steers uliopo Mtaa wa Samora/Ohio, OilCom Ubungo, Buguruni Shell, Dar Live- Mbagala, kituo cha daladala Mwenge na Uwanja wa Taifa.

  Baada ya saa 6 mchana mauzo yote yatahamia Uwanja wa Taifa ambapo milango kwa ajili ya mechi itakuwa wazi kuanzia saa 7.30 mchana.

  Viingilio katika mechi hiyo vitakuwa sh. 30,000 kwa VIP A, sh. 20,000 kwa VIP B na C wakati viti vya rangi ya chungwa, bluu na kijani kiingilio ni sh. 7,000.

  Mechi hiyo itachezeshwa na mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam ambapo atasaidiwa na Anold Bugado (Singida), Florentina Zablon (Dodoma) na Lulu Mushi (Dar es Salaam). Kamishna wa mechi hiyo Emmanuel Kavenga kutoka Mbeya wakati mtathimini wa waamuzi ni Alfred Rwiza wa Mwanza.


  Boniface Wambura Mgoyo
  Media and Communications Officer
  Tanzania Football Federation (TFF)

  0 0

   Mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili Omari Mikidadi (47) kutoka Mbagala jijini Dar es Salaam akipokea zawadi ya simu ya kisasa aina ya Samsung Gallaxy tablet kutoka kwa mwakilishi wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Erick Tafisa(kulia), wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam. 
   Meneja Promosheni wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Davis Kambi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili Alex Sylvester(34) kutoka Zanzibar, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam.
  Meneja Promosheni wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Davis Kambi (kushoto) akimkabidhi mmoja wa washindi wa promosheni ya Winda Safari ya Brazili  Rogers Isdory (29) kutoka Tabata, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika wiki hii jijini Dar es Salaam.

  0 0

   kushoto Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Fatma Ally, akiwa na Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe wakizindua kisima cha maji.

   Waziri wa Maji Profesa.Jumanne Maghembe, pamoja naMkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Fatma Ally wote kwa pamoja wakifungua bomba la maji kuashiria uzinduzi rasmi wa matumizi ya maji.
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe akimtwisha ndoo ya maji mkazi wa kijiji cha Mvumi makulu Mkoani Dodoma.
   Muonekano wa kisima kichozinduliwa.
   Kulia Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe (katikati),Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Fatma Ally, na kushoto Afisa Tarafa Chamwino Mvumi Mohamed Mfaki akielekea kuzindua bomba la maji.
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe, akipanda mti.
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe akisalimiana na Mkurugenzi ya Halmashauri Wilaya Chamwino Mkoani Dodoma Adrian Jungu.baada ya kuwasili kuzindua mradi mkubwa wa maji wenye uwezo wa kuwahudumia wakazi zaidi ya elfu 13 uliogharimu zaidi ya shilingi milioni 300.kilichopo katika kijiji cha Mvumi makulu Mkoani Dodoma
   Waziri wa Maji Maji Profesa.Jumanne Maghembe, akiongea na wana kijiji wa Mvumi makulu Mkoani Dodoma.PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE,DODOMA

  0 0

  MAHAKAMA Kuu Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, leo imefuta kwa mara ya pili maombi ya kufanya marejeo kuhusu kuliondoa shitaka la kukaidi amri halali iliyotolewa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, dhidi ya Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini, Sheikh Ponda Issa Ponda  (pichanibaada ya kufunguliwa kwa kukiuka sheria. 
   Kadhalika maombi hayo yamefutwa baada ya kukiuka kifungu cha 372 kidogo cha (2) cha Mwenendo wa Sheria za Makosa ya Jinai (CPA) ambacho hakiruhusu maombi hayo kupelekwa Mahakama Kuu. 
  Akitoa uamuzi wa mahakama, Jaji Augustino Mwarija alisema maombi hayo yamefunguliwa kwa kukiuka kifungu cha 372 kidogo cha (2) na kwamba amekubali pingamizi la Jamhuri na kuyafuta. Upande wa Jamhuri unaongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Bernad Kongola. 
  “Naona maombi haya yameletwa kwa kukiuka kifungu cha 372 kidogo cha (2) cha CPA, nakubaliana na pingamizi la Jamhuri … hatimaye mahakama imeona maombi yameletwa bila kuzingatia sheria nayafuta” Alisema wakati akisoma uamuzi uliyofuta maombi ya mshtakiwa huyo. Akifafanua zaidi alisema kifungu hicho siyo sahihi kwamba kinazuia uletaji wa maombi mahakamani dhidi ya amri ya awali na ya muda zinazofanya mahakama za chini isipokuwa amri ambazo zinahitimisha shauri lote la jinai. 
   “Kwa sababu hiyo hoja ya mleta maombi kwamba amri imetolewa kuhusu pingamizi la awali siyo sahihi na siyo tafsili ya kifungu hicho uamuzi huo haumalizi kesi… Sheikh Ponda ana mashtaka matano ya jinai na uamuzi wa Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate haukusu pingamizi la awali haukumaliza mashtaka “alisema Jaji Mwarija. 
   Mapema Desemba 11, mwaka 2013, kwa mara ya kwanza mahakama hiyo iliyoketi chini ya Jaji Rose Teemba iliyafuta maombi hayo baada ya upande wa Jamhuri kutoa pingamizi la awali kwamba kiapo kilichoambatana na maombi hayo kilikuwa na mapungufu ya kisheria ikiwemo kutokuwa na tarehe pamoja na jina la mtoa kiapo. 
   Jaji Teemba alisema mara alipopokea jalada la kesi hiyo aliona mapungufu hayo lakini siku Desemba 2, mwaka huu alishangaa kuona kiapo kimefanyiwa marekebisho. 
  Hata hivyo, Desemba 13, mwaka 2013, Sheikh Ponda kupitia mawakili wake Obadia Hamidu na Juma Nassoro alifungua maombi mengine ambayo jana yamefutwa baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kuwasilisha pingamizi la awali la kupinga maombi hayo. 
   DPP aliwasilisha pingamizi la awali dhidi ya Sheikh Ponda akidai maombi yake hayana mashiko ya kisheria na aliomba mahakama kuyafuta. 
   Katika pingamzi hilo, DPP aliomba kuwa maombi ya Sheikh Ponda hayaruhusiwi kusikilizwa mahakamani hapo chini ya kifungu cha 372 kidogo cha (2) cha Mwenendo wa Sheria ya Makosa ya Jinai (CPA), kilichofanyiwa marekebisho mwaka 2002. 
   Kifungu hicho kinaeleza kwamba mtu hataruhusiwa kuwasilisha maombi yoyote ya marejeo ambayo yanatokana na maamuzi au amri ya mahakama ya chini ambayo hayakumaliza kesi. 
  Akijibu hoja za DPP, wakili wa utetezi Juma alidai kuwa maombi hayo yana mashiko ya kisheria na kwamba mshtakiwa ana haki ya kusikilizwa na mahakama hiyo. 
   Katika kesi ya msingi, Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka ya kukaidi amri halali, kuharibu imani za dini, kushawishi na kutenda kosa. Kesi hiyo inasikilizwa mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Richard Kabate katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Morogoro. 
   Awali, Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP), aliwasilisha ombi la kuzuia dhamana dhidi ya mshtakiwa huyo kwa sababu ya maslahi ya nchi na usalama wake mwenyewe. 
  Baada ya Shekh Ponda kunyimwa dhamana wakili wake, Nassoro aliwasilisha ombi jingine mahakamani hapo la kufuta shitaka la kwanza ambalo ni kukaidi amri halali akidai kuwa mahakama hiyo haina uwezo kisheria kusikiliza vinginevyo lifunguliwe katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam. 
   Akitoa sababu za kutaka kufutwa ama kuhamishia shtaka hilo katika Mahakama ya Kisutu, Wakili Nassoro, alidai kuwa amri hiyo halali anayodaiwa kuivunja mteja wake ilitokana na hukumu iliyotolewa katika Mahakama ya Kisutu Mei, mwaka 2013 ambayo Ponda alihukumiwa kifungo cha nje cha mwaka mmoja na kutotakiwa kufanya kosa lolote la jinai katika kipindi cha mwaka mmoja. Hata hivyo, Hakimu Kabate alitupilia mbali maombi hayo na Sheik Ponda  ya kufanya marejeo Mahakama Kuu dhidi ya shitaka hilo.

  0 0

   Balozi Mdogo wa Tanzania Dubai,  Mhe. Omar Mjenga,  amefanya kikao cha maandalizi ya siku ya Taifa ( National Day) kusherehekea miaka 50 ya Muungano pamoja na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania waishio UAE makao yao yakiwa Dubai.  
  Kushoto ni ndugu Shabir Damji, katibu wa Jumuiya, kati ni Bi Shamira ambaye ni  mwenyeji wa sherehe hizo katika Le Meridien Hotel na Mhe Omar Mjenga, mjini Dubai leo. Chini wakipanga namna ya kufanikisha sherehe hizo


  0 0

   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa sambamba na Mwakilishi wa Hoteli ya Waride Resort  Bwana Massliano  Bramucci wakikata utepe kuashiria ufunguzi wa Kituo cha Huduma za akina Mama wajawazito katika Kijiji cha Pwani Mchangani Mkoa wa Kaskazini Unguja.
   Mfadhili wa ujenzi wa Kituo cha akina mama wajawazito cha Pwani Mchangani Bwana Massiliano Bramucci akitoa maelezo kwa  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif mara tu baada ya kukifungua Kituo hicho.
    Balozi Seif pamoja na wageni wengine waalikwa katika uzinduzi wa kituo cha huduma za akina mama wajawazito wakiangalia Gari la wagonjwa litakalotoa huduma kwenya Kituo hicho.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akisindikizwa wakati anaondoka hospitalini hapo. Kwa habari na  picha zaidi 
  BOFYA HAPA

  0 0

  Visit the forum at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar Es Salaam. This is a unique gathering of businesspersons, investors, policymakers and industry leaders to foster bottom-up, practitioner-driven, business to business and business to government solutions for economic development.

  0 0

  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akipokea moja ya kati ya mbili ya Kadi za Chadema kutoka kwa aliekuwa Mwanachama wa Chadema,Mrisho Issa mkazi wa Kijiji cha Msata,ndani ya Jimbo la Chalinze.Mwingine alierudisha kadi ni Kassim Msakamali (hayupo pichani).
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (katikati) akiwainua mikono Wanachama wapya wa Chama cha Mapinduzi,Kassim Msakamali (wa pili kushoto) na Mrisho Issa (wa pili kulia) ambao wote ni Wananchi wa Kijiji cha Msata,Chalinze.Kulia ni Meneja wa Kampeni za Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete aiwasalimia wananchi wa Lugoba,Chalinze.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akiambatana na Mwenyekiti wa Kampeni wa Chalinze (CCM),Saleh Mpwimbwi (kushoto) pamoja na Msafara wake wakielekea kuhani Msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete na ujumbe wake wakishiriki kwenye dua ya pamoja mara baada ya kufanyika kwa kisomo cha kumuombea Marehemu ambaye ni Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman (alieketi nyuma ya mgombe) mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (aliesimama kulia) akizungumza machache wakati alipofika kuhani msiba wa Mtoto wa Mzee Mashaka Athuman mkazi wa kijiji cha Rupungwi,Kata ya Mandela iliopo ndani ya Jimbo la Chalinze jana Machi 17,2014.

  BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

  0 0
  0 0

  Naibu Waziri wa Fedha Mhe Mwigulu Mchemba akifuatilia (kulia) kwa karibu kikao cha Bunge la Pamoja la Afrika, Karibiani, Pacific na Jumuiya ya Ulaya kinachoendelea Strasbourg Ufaransa. Mhe. Mchemba anawakilisha Baraza la Mawaziri la Afrika, Karibiani na Pacific katika kikao hiki. Pamoja na mambo mengine, kesho atalihutubia Bunge na kujibu maswali ya Wabunge. Kulia ni Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya Dr. Diodorus Buberwa Kamala.

  0 0

  With salams and Jambo from Bukoba

  Every year Rebeka was born with a lump and as she grew the lump also grew bigger, Dr. David pointed that it was originated from the spine and she can only be operated by a Neuron Surgeon

  We  now appeal to our generous donors to help the suffering humanity. 
  See below
  Mubaarak Abdullah

  0 0

   


  WASHIRIKI wa shindano la Maisha Plus ambayo kwa mwaka 2014 inatambulika kwa jina la Maisha Plus Rekebisha, kutoka nchini Kenya, Rwanda,Uganda na Burundi tayari wameshawasili nchini na jana wameelekea wako mkoani Morogoro kushiriki shughuli za kijamii.

  Mratibu wa onyesho hilo, Ally Masoud Kipanya amesema hili ni kundi la tatu kushiriki shughuli za kijamii, ambapo kundi la kwanza lilikuwa Iringa, kisha la pili likaenda Zanzibar na hili la tatu linaenda Morogoro kushiriki shughuli za kijamii, huku lengo kubwa likiwa ni kubadilisha maisha ya wanajamii wa huko.

  "Hii ndio sababu Maisha Plus ya mwaka huu inaitwa Maisha Plus Rekebisha, ambapo lengo kuu ni kuangalia matatizo ya eneo husika na kuangalia jinsi ya kutatua, na sio kulalamika, tunataka kurekebisha wananchi wenye fikra za kusubiri kufanyiwa, kuwa wepesi wa maamuzi na kutatua matatizo waliyonayo", alisema Masoud

  “Wananchi wengi hulalamikia serikali juu ya maswala mbalimbali ambayo hata wao wenyewe wanaweza kuyarekebisha bila kusubiri kufanyiwa”,alisema.

  Washiriki kutoka nchi jirani ni walio mkoani Morogoro kwa sasa ni Loveness Asantely ,Mary Sidi(kutoka Kenya), Borandanginye Aurore, Mvano Ciza, na Abdou Karim(kutoka Burundi), Aminata Siira(kutoka Uganda), Uwamahoro Fatima, Ngabozinza Khalid, na Ngabozinza Daniel (kutoka Rwanda)

  Kupitia Maisha Plus Rekebisha mwaka huu, wananchi watapata elimu juu ya kuepukana na mambo mbalimbali katika jamii ikiwemo magonjwa kama malaria, kipindupindu, homa ya manjano na mengineyo.

  Washiriki wote kwa ujumla kutoka nchi za jirani wanatakiwa kuwa 12 nambili,waliofika nchini ni 10 wawili wanaotambulika kwa majina Said Rashid (Uganda) na Caron Abisai (Kenya) bado hawajafika.

  0 0


  0 0

   Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Mawaziri wa  Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Madola na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe. Bernard Membe akiendesha kikao cha 43 cha chombo hicho cha utendaji cha Jumuiya ya Madola Jijini London Uingereza. 
   Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi 9 zinazounda Kikosi Kazi cha Jumuiya ya Madola chini ya Uenyekiti wa Tanzania wakishiriki kwenye Mazungumzo na waandishi wa Habari baada ya kumaliza kikao chake cha 43 jijini London Uingereza.

   Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Nchi 9 zinazounda Kikosi Kazi cha Jumuiya ya Madola chini ya Uenyekiti wa Tanzania wakishiriki kwenye Mazungumzo na waandishi wa Habari baada ya kumaliza kikao chake cha 43 jijini London Uingereza.

   Mhe. Bernard Membe, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania akiwa kwenye kikao na Mabalozi wa Nchi za Afrika Wanachama wa Jumuiya ya Madola jijini London, pembezoni mwa kikao cha Mawaziri wa Kikosi Kazi cha Jumuiya hiyo.
  Balozi wa Tanzania nchini Uingereza Mhe. Peter Kallaghe akimkaribisha Mhe. Bernard Membe, Mwenyekiti wa Kikosi Kazi cha Mawaziri wa Nchi za Jumuiya ya Madola kuzungumza na Mabalozi wa Nchi za Kiafrika  wanachama wa Jumuiya hiyo.
  ----------------------------------------
  Kikao cha 43 cha Kikosi Kazi cha Mawaziri wa Jumuiya ya Madola kimeipunguzia adhabu nchi ya Fiji na hivyo kuiruhusu kushiriki kwenye baadhi ya matukio ikiwemo michezo ya Jumuiya ya Madola ya mwaka 2014. 
   Kikao hicho kilichofanyika Jijini London Uingereza chini ya uenyekiti wa Mhe. Bernard Membe (Mb.), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania kilifikia uamuzi huo baada ya kupitia na kuridhishwa na hatua mbalimbali zilizochukuliwa na Fiji katika kujiandaa na uchaguzi mkuu ujao ikiwa ni jitihada za kutetea uanachama wake ndani ya jumuiya hiyo. 
   Akiongoza mjadala huo, Mhe. Membe alisifu hatua za makusudi zilizochukuliwa na nchi hiyo kama vile kushugulikia masuala ya haki za binadamu na utawala bora, kuanzisha daftari la kudumu la wapigakura, kuandaa mazingira ya uwazi kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Septemba 2014 ikiwemo kuandaa mazungumzo na wadau mbalimbali wa siasa na aliyekuwaWaziri Mkuu aliyeingia kijeshi kujiuzulu na kugombea kama raia. 
   Akiendesha kikao hicho cha kwanza kama mwenyekiti wa chombo hicho muhimu, Mhe. Membe alisisitiza umuhimu wa kikosi kazi hicho kutekeleza majukumu yake bila urasimu na ubaguzi bali kwa kutoa fursa sawa za ushiriki wa nchi wanachama na kuzingatia misingi ya haki kwa manufaa ya wanachama wote. 
   Mhe. Membe pia aliwasisitizia mawaziri wenzake wanao tumikia chombo hicho kuwa makini na kuheshimu mila na desturi za nchi wanachama hususan zile za Kiafrika na kuepuka kushinikiza ajenda ambazo zinagusa dini, tamaduni na mila za nchi nyingi za kiafrika, kama vile ndoa za jinsia moja. Alisema kwa kufanya hivyo Jumuiya ya Madola itahatarisha muungano na mshikamano uliopo sasa ndani ya jumuiya hiyo. 
   Aidha, Mhe. Membe alisema hazina kubwa ya Jumuiya ni wingi wa nchi wanachama na tamaduni na desturi mbalimbali zinazowakilishwa na wanajumuiya. Hivyo kuheshimu tamaduni zote ndio kutajenga heshima ya Jumuiya ya Madola kimataifa. 
   Akiwashukuru wajumbe wa kikosi kazi kama mwenyekiti, Mhe. Membe alisema jukumu la uenyekiti wa chombo hicho si dogo, lakini wajumbe wa chombo hicho wakiungana kwa pamoja na kwa msaada wa Sekretarieti yaJumuiyayaMadolaanahakikandaniyamiakamiwiliyauenyekiti wake Jumuiya hiyo itaendelea kusimamia misingi muhimu ya jumuiya hiyo bila kutetereka. 
   Mhe. Membe ameiwakilisha Tanzania kama Waziri mwenye dhamana kuanzia mwaka 2011 akiwa kama mjumbe, na mwaka 2013 Jijini Colombo Sri Lanka alichaguliwa bila kupingwa kuwa mwenyekiti kwa miaka miwili. Waziri wa Mambo ya Nje wa New Zealand Mhe. Murray McCully alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti. 
   Ukiacha Tanzania na New Zealand, wajumbe wengine ni mawaziri wa Mambo ya Nje kutoka nchi saba ambazo ni Cyprus, Guyana, India, Pakistan, Sierra Leone, Visiwa vya Solomon na Sri Lanka ambao wanaingia kwa nafasi yao ya uenyekiti wa Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali za Jumuiya ya Madola. 

   Imetolewa na: 
  Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali 
   Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa 
   18 Machi, 2014

  0 0

   Mbunge a Jimbo la Mchinga,Mh. Said Mtanda (kulia) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014,wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (wa pili kushoto walioketi).Picha na Othman Michuzi,Chalinze.

   Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014.Katika Mikutano yake kwenye Vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga ndani ya Jimbo hilo,Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo.
  Wananchi wa Kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze wakimsikiliwa kwa makini Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete.
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akilakiwa na wanakijiji wa Kijiji cha Msigi Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014.


  0 0

  Hi, 
   Leo ndio tumeachia rasmi audio ya wimbo wa BARAKAH Da PRINCE (msanii mpya kutoka Tetemesha Entertainment), baada ya kutoa video yake wiki iliyopita. Wimbo unaitwa Jichunge na umefanywa katika studio ya Tetemesha chini ya maproducer wawili KidBoy na producer mpya anaitwa Nusder. Tunaomba support yako kadri utakavyoweza. 
   ARTIST NAME: BARAKAH Da PRINCE 
  SONG TITLE: JICHUNGE 
  WRITTEN BY: BARAKAH & KIDBOY 
  PRODUCED BY KIDBOY & NUSDER
   MIXED BY: KIDBOY 
  MASTERED BY: MISJAH @24MASTERING - NETHERLANDS (www.24mastering.com)

  0 0

  kutoka kushoto Dkt. Grace Mallya kutoka Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Bi. Grace Mwangwa Mtaalamu wa masuala ya Jinsia, Wizara ya Fedha na aliyekaa nyuma ni Bi. Constacia Gabusa Kaimu Mkurugenzi -(Jinsia) Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, wakifuatilia hotuba ya Waziri.
  Mhe. Sophia Simba ( Mb) Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, akielezea uzoefu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia ( MDGs) ni katika Mkutano wa 58 wa Kamisheni kuhusu Hali ya Wanawake unaoendelea hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa. Waliokaa pamoja na Mhe. Waziri ni Muwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, Balozi Tuvako Manongi. Bibi. Anna Maembe, Katibu Mkuu, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Bibi. Asha Ali Abdulla, Katibu Mkuu, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
  Ujumbe wa Tanzania unavyoonekana katika ujumla wao, wa kwanza ni Katibu wa Waziri, Bi Teodosia Mbunda akijadiliana jambo na Mhe. Jaji Iman Aboud
  Bibi. Mwanaidi Saleh Abdulla, Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Bi. Fatma Mbarak Hashim Mtaalam masualaya Jinsia,( Zanzibar), Bw. Seif Shaaban Mwinyi, Kamishna na mratibu wa shughuli za Idadi ya Watu, Tume ya Mipango- (Zanzibar) na aliyekaa nyuma ni Bw. Adam Hans Kadege, Mtakwimu kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto. Tanzania imewakilishwa vizuri katika mkutano huu kwa kuwa na wajumbe kutoka pande zote za Muungano.
  Wajumbe wengine wakifuatilia hotuba ya Mhe. Waziri. Kutoka kushoto, ni Bi. Joyce Mlowe kutoka Wizara ya Katiba na Sheria, Bi Mhaza Gharibu Juma, Mkurugenzi wa Mipango, Sera na Utafiti, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto - Zanzibar na Bi. Halima Abdulrahman Omar, Mtaalamu wa Jinsia, Wizara ya Uwezeshaji, Ustawi wa Jamii, Vijana, Wanawake na Watoto- Zanzibar . pamoja na kuhudhuria majadiliano ya mada kuu kuhusu mafanikio na changamoto za utekelezaji wa MGDs, wajumbe wa Tanzania pia wamekuwa wakishiriki kikamilifu katika majadiliano ya mada nyingine nyingi zinazofanyika katika mikutano ya pembezoni ( side-events)

  Na Mwandishi Maalum
  Wakati Mkutano wa 58 wa Kamisheni  kuhusu Hali ya wanawake, ukiwa umeingia wiki yake ya pili,  Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  imeeleza kwamba imejitahidi na imefanikiwa  kufikia  baadhi ya   Malengo ya Maendeleo ya Millenia  hata kabla ya  mwaka 2015.
  Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto,  Mhe. Sophia Simba ( Mb) ameyasema hayo siku ya  jumatatu wakati Tanzania ilipopata fursa ya kuielezea jumuiya ya kimataifa uzoefu wake katika utekelezaji wa  MDGs na changamoto  ambazo bado inaendelea kukabilina nazo katika baadhi ya  malengo.
  Mhe. Sophia Simba,  amesema Tanzania  imefanya vizuri katika  malengo nane kati ya  nane ingawa bado inakabiliwa na changamoto katika baadhi ya maeneo ambayo alielezea pia namna serikali inavyojipanga kukabiliana nayo.
  Kwa wiki mbili sasa,   wawakilishi wa kutoka nchi mbalimbali duniani  zinazohudhuria mkutano huu hapa Umoja wa Mataifa,  wamekuwa  wakipashana habari na wakubadilishana  uzoefu  kuhusu masuala  yahusuyo haki za wanawake, za mtoto wa kike na ustawi wao na maendeleo yao.

  Aidha wawakilishi  hao  wamekuwa  pia  wakiijadili mada kuu ya mkutano huu ambayo ni mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya  Millennia,  ambapo kile nchi imekuwa ikitoka uzoefu wake.
  Baadhi ya malengo  aliyoeleza kwamba Tanzania imefanya vizuri ni pamoja na lengo   namba mbili linalohusu fursa ya elimu ya msingi kwa  watoto wote na kwa kuzingatia uwioano wa kijinsia.
  Aidha akabainisha pia kwamba   Tanzania  imefanya vizuri katika  lengo  la tatu kuhusu fursa sawa za  kijinsia na uwezeshwaji wa wanawake ambapo alitolea mfano ongezeko la wanawake katika vyombo vya utoaji  maamuzi kama vile  Bunge na Baraza la  Wawakilishi. 
  Na  katika  sekta ya elimu ya sekondari ingawa  uwiano huo unapungua   kuelekea elimu ya juu
  Waziri wa  Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto akielezea zaidi mafanikio ya  utekelezaji wa MDGs, ameeleza pia kwamba kumekuwa na mafanikio ya kuridhisha katika upunguzaji wa  vifo vya watoto wachanga chini ya miaka mitano kwa pande zote mbili za  Muungano.
  Hata hivyo licha ya mafanikio  ya kuridhisha katika eneo hilo, Waziri Simba anasema  bado watoto wanaendelea kupoteza maisha kwa maradhi yanazulikia kama vile  malaria na  kuharisha.
   Kuhusu lengo namba tano   kuhusu   upunguzaji wa  vifo vya wanawake wajawazito,  Waziri anasema, eneo hilo bado linachangamoto nyingi na kwamba kasi yake ni ndogo.
  Ametaja baadhi ya changamoto zinazolikabili eneo hili kuwa ni  uhaba wa  wataalamu, eneo ambalo anasema tayari serikali inalitafutia ufumbuzi,  ukosekanaji wa huduma za upasuaji wa dharura eneo ambalo amesema serikali pia inalifanyia kazi kwa kujaribu kuviwezesha vituo vya afya kuwavipatia vifaa na wataalam
   Kuhusu lengo la sita linalohusu  huduma za afya,  Tanzania, kwa mujibu wa Mhe, Waziri,  bado inachangamoto  nyingi katika  kukabiliana na maambukizi ya virusi vinavyosambabisha ugonjwa wa ukimwi, malaria na Kifua kikuu magonjwa ambayo yanagusa sehemu kubwa ya  jamii.
   Akasema  serikali imejitahadi sana katika kuyadhibiti magonjwa haya ,  kiasi kwamba kumekuwapo na   udhibiti wa maambukizo  miongoni mwa watu wazima.
  Kuhusu lengo  namba saba linalohusiana na  Mazingigira endelevu,  pamoja na  huduma za maji safi na salama,  Waziri anasema,  bado kuna tatizo kubwa la  upatikanaji wa maji safi na salama hasa maeneo ya vijijini.
  Mhe. Waziri Simba anabainisha kwamba   changamoto kubwa  kwa Tanzania iko katika utekelezaji wa lengo namba moja, linalohusu utokomezaji wa umaskini  uliokidhiri na  njaa.
  Pamoja na kuelezea mafanikio na changamoto za utekelezaji wa  MDGs,  Waziri Simba,  amesema Tanzania  inaunga mkono  msimamo wapamoja wa   Umoja wa Afrika,  unaosisitiza kwamba  usawa wa jinsia na uwezeshwaji wa wanawake,  uwe lengo linalojitegemea  katika  Malengo Mapya ya Maendeleo Endelevu baada ya  2015 ( SDGs).

older | 1 | .... | 391 | 392 | (Page 393) | 394 | 395 | .... | 3283 | newer