Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 390 | 391 | (Page 392) | 393 | 394 | .... | 3278 | newer

  0 0


  UTAMADUNI huu ulioanza wa waamini licha ya kusali, pia wakaenda kusherehekea sikukuu hizi za kiroho ni mgeni na mzuri kwa kuwa unawajenga watu kiroho, na kuwaepushia uwezekano wa kutumbukia katika matatizo kwa kwenda katika maeneo mbalimbali ya sterehe; Amesema Askofu Method Kilaini.

  Mhashamu Kilaini ambaye ni Askofu Msaidizi wa Jimbo Katoliki la Bukoba, ameyasema hayo alipozungumza na Gazeti hili kuhusu Tamasha la Pasaka linalotarajiwa kufanyika katika jiji la Dar es Salaam, Aprili 20 mwaka huu ambayo ni Sikukuu ya Pasaka.

  Mwaka huu Sikukuu ya Pasaka inaangukia Jumapili ya Aprili 20, Tamasha la Pasaka linatarajiwa kufanyika katika mikoa mbalimbali nchini kwa siku tofauti  kuanzia Siku hiyo ya Pasaka. Akifafanua faida za Tamasha la Pasaka na mengine ya kidini kama Tamasha la Krismasi, Mhashamu Kilaini amesema yanasaidia kuifanya dini isiishie kanisani pekee kwa siku za sikukuu mfano Pasaka na Krismasi, badala yake kuifanya iende hata katika maeneo ya starehe yanayozingatia usafi wa kimwili na kiroho.

  “…Wakienda kwenye matamasha kama hili la Krismasi, watu waanze kwa sala, maombi na hata mahubiri kidogo ili waendeleze moyo wa kumpenda Bwana (Yesu Kristo) maana katika matamasha kama haya, hakuna ulevi, uzinzi wala ufuska,” amesema Mhashamu Kilaini.Akaongeza, “Utamaduni huu wa kusherehekea siku za Sikukuu katika Jina la Bwana katika matamasha ni mpya, lakini pia ni mzuri maana unawaondoa watu katika vishawishi vya kuhangaikia katika mambo yanayowatia hatarini kimwili na kiroho na kulazimisha matumizi ya pesa yasiyo ya lazima….”

  Amesema ili kushirikishana neema na baraka katika matamasha kama hilo la Pasaka, ni vema waamini wakajitokeza na kwenda kwa pamoja kama familia ili wafurahie kwa kufahamiana vema zaidi na Wakristo wenzao. Hata hivyo amesema katika sikukuu kama hizi, ni vema pia kuzingatia suala la usalama wa familia kwa kuhakikisha kuna ulinzi ili kuepusha uwezekano wa kufanyika vitendo vya kihalifu. “…Kwa yule anayependa kukaa na familia yake nyumbani, akae nyumbani, badala ya kwenda katika baa na sehemu nyingine zinazohatarisha imani, amani na usalama wake,” amesema. Tamasha hilo linatarajiwa kuwashirikisha wadau mbalimbali wakiwamo waimbaji maarufu wa muziki wa Injili toka ndani na nje ya nchi.

  Kampuni ya Msama Promotions inayoandaa Tamasha la Pasaka mwaka 2014 imekuwa ikiendesha upigaji kura kwa njia ya ujumbe mfupi za maandishi za simu za mkononi (sms) ili waumini na wapenzi wa Tamasha la Pasaka wamchague mgeni rasmi, waimbaji wanaotaka watumbize katika tamasha hilo pamoja na mikoa wanayoitaka. Zoezi la upigaji kura linaendelea.

  Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo, Alex Msama amenukuliwa na vyombo vya habari akiutaarifu umma kuwa, kupitia upigaji kura huo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete anaendelea kuongoza kwa kura za kuwa mgeni rasmi katika Tamasha hilo zilizofikia milioni 6.9 idadi ambayo haijafikiwa na kiongozi mwingine yeyote.

  Habari zinasema katika kura hizo, Rais Kikwete anafuatiwa na aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe na Waziri wa Afrika Mashariki, Samwel Sitta, Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe, Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Regnald Mengi na Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ufunuo na Uzima, Josephat Gwajima. Kwa upande wa muziki wa Injili, waimbaji kadhaa wamekwishachomoza miongoni mwao wakiwa ni Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Voice Acapela na Sarah Kiare kutoka Kenya.

  Hivi karibuni, waimbaji Rose Muhando na John Lisu wamewashukuru mashabiki wa Tamasha la Pasaka kwa kuwapigia kura nyingi zilizowahakikishia kushiriki katika Tamasha hilo. Mchuano mkali kumpata mgeni rasmi kwa upigaji kura huo ulikuwa hasa baina ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda, Regnald Mengi, Mwangalizi Mkuu wa WAPO Mission International Askofu Mkuu Sylvester Gamanywa na Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekolo maarufu kama “Mzee wa Upako”.

  0 0

  Kamanda wa polisi mkoa wa
  Njombe SACP Fulgence Ngonyani
  Na Edwin Moshi, Njombe
  Jeshi la polisi mkoani Njombe linamshikilia Bw. Yusufu Sadick Mkalile (33) kwa tuhuma za kumuua mtoto wake wa kumzaaa mwenyewe kwa kumziba pua na mdomo.
  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa waandishi wa habari na Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe SACP Fulgence Ngonyani  imesema kuwa mtuhumiwa alitenda mauaji hayo Machi 16 mwaka huu majira ya saa 03:20 asubuhi, ambapo alimziba pua na mdomo mwanaye huyo aitwaye Udai Yusufu (8) hali iliyosababisha kukosa hewa na kufariki.

  Tukio hilo limetokea chumbani, nyumbani kwao mtaa wa Nazareth, kata ya Mjimwema tarafa ya Njombe Mjini wilaya ya Njombe, na hadi anafariki marehemu alikuwa akisoma darasa la pili katika shule ya Msingi Meta mkoani Mbeya
  Mtuhumiwa wa mauaji hayo ambaye ni mkulima mkazi wa Stereo mkoani Mbeya amekamatwa na polisi na anaendelea kuhojiwa kuhusiana na mauaji hayo. Chanzo bado hakijafahamika.

  0 0


  0 0

  WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameagiza wananchi wa mji wa Kibaigwa kutunza vyanzo vya maji vinavyopatikana katika Wilaya ya Kongwa ili kuendelea kupata huduma ya maji safi na salama ambayo ni huduma muhimu kwa mahitaji ya wananchi wa Wilaya hiyo. 
   Amesema hayo leo mchana (Jumatatu, Machi 17, 2014), wakati akizindua rasmi Mradi wa Maji uliojengwa na Kampuni ya China Hunan uliochimba Visima viwili vya maji Safi na Salama vyenye urefu wa mita 101 katika Mji Mdogo wa Kibaigwa ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya wiki ya Maji ambayo hufanyika kila mwaka, na mwaka huu maadhimisho hayo kitaifa yanafanyika mkoani Dodoma. 
  Waziri Mkuu aliwaeleza wananchi waliohudhuria kwamba chanzo hicho cha maji ni muhimu na ni utajiri wa mji wa Kibaigwa ambao wananchi wa mji huo wameombwa kutunza vyema chanzo hicho kwa ajili ya matumizi yao ya kila siku. 
   ‘‘Nimeelezwa kuwa visima hivi vinauwezo wa kutoa maji lita 62 kwa saa“, Ni lazima mtafute njia ya kuwaeleimisha wananchi ili muweza kuhifadhi upatikanaji wa maji safi na salama katika mji wa Kibaigwa kwa kuangalia namna ya kujenga mazingira bora ya kutunza chanzo kile, alisema Waziri Mkuu. 
   ‘‘Mradi huu ulianza kujengwa mwezi Machi 2011 na umekamilika mwezi Septemba, 2013 kabla ya mradi kuanza Mji mdogo wa Kibaigwa ulikuwa na wakazi wapatao 18,550 kati ya hao Wakazi 8,904 tu, sawa na asilimia 48 ndio walipata huduma ya maji, kwa mradi huu wa sasa asilimia 90 ya wananchi wa Kibaigwa wanauhakika wa kupata maji safi na salama na zaidi ya wananchi elfu 13,000 wanauwezo wa kupata huduma ya maji hayo“, alisema Waziri Mkuu.
  Hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika Wilaya ya Kongwa ni asilimia 68 ukiondoa mji mdogo wa Kibaigwa na sasa kuna miradi kumi katika vijiji kumi ambavyo ni Mkoka, Chigwengweli, Songambele, Malanje, Igangwa, Mseta, Mlali Iyengu, Mlali Bondeni, Ngumbi na Pembamoto, miradi hii ikikamilika itaongeza idadi ya watu wanaopata huduma ya maji Safi na Salama na kufikia asilimia 75 katika Wilaya ya Kongwa.
  Waziri Mkuu alisema, Miradi hii ni kiashiria kuwa Serikali kupitia Ilani yake ya Chama Cha Mapinduzi inatambua umuhimu wa sekta ya Maji kwa maendeleo ya Kiuchumi, Kijamii na hifadhi za mazingira, hivyo Serikali itahakikisha upatikanaji wa maji safi na salama kufikia asilimia 75 Vijijini na asilimia 95 Mijini ifikapo 2015. Waziri Mkuu alisema, ‘‘nimesikia kuwa ndoo ya lita 20 ni sh 20, ndoo ya lita 10 ni sh 10 na pipa ni sh 250
  “Kwa utaratibu huo ni vema uongozi wa Mji wa Kibaigwa kuangalia utaratibu wa kutunza fedha hizo kwani kutakuwa na matengezo na marekebisho ya mashine pale zitakapo haribika, pia aliwaomba kuanzisha utaratibu wa kutoa taarifa walau kila baada ya miezi mitatu ili wananchi kupafamau mapato na matumizi ya huduma ya maji inayotolewa. 
   Vilevile, Waziri Mkuu alisema Sera ya Maji ya mwaka 2002 inalenga katika kuhakikisha kuwa Wananchi Vijijini wanapata huduma ya maji safi na salama kwa umbali usiozidi Mita 400 kutoka kwenye makazi yao. 
  IIi kufikia lengo hilo, Serikali kwa kushirikiana na Washirika wa Maendeleo, Serikali za Mitaa, Wananchi na wadau wengine itaendelea kuboresha huduma za maji vijijini kwa kujenga miradi mipya, kupanua na kukarabati miundombinu ya maji. Maadhimisho ya Wiki ya Maji yalianza mwaka 1992 ambapo iliamuliwa kuwe na kauli moja kuanzisha Wiki ya Maji Duniani. Mwaka huu Kimataifa yanafanyika Tokyo, Nchini Japan.
     Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Mradi wa Maji wa Mji Mdogo  wa Kibaigwa wilayani Kongwa ikiwa ni moja ya shughuli za Wiki ya  Maji nchini Machi 17, 2014.. Kulia kwake ni Waziri wa Maji, Profesa Jumanne Maghemb
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua bomba la maji kuashira uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Mji Mdogo wa Kibaigwa wilayani Kongwa ikiwa ni Moja ua Shiguli za wikiya Maji. Kulia Kwake ni Waziri wa Maji na kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Rehema Nchimbi.(Picha na Ofisi ya Waziri  Mkuu)
    Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Maji wa Mji Mdogo  wa Kibaigwa wilayani Kongwa ikiwa ni Moja ya Shuguli za wiki ya Maji Machi
   Waziri Mkuu, Mizengo Pinda  akimtwika ndoo ya maji, bibi Emaculata Mazengo wakati alipozindua  mradi wa maji wa Mji mdogo wa Kibaigwa wilayani Kongwaikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya Maji  Machi 
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia baada ya kuzindua mradi wa maji wa mji mdogo wa Kibaigwa wilayani Kongwa ikiwa ni moja ya shughuli za wiki ya maji  Aprili 17, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

  0 0

  Na Nafisa M. Ali 
  Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 leo imekabidhi rasmi Ripoti ya ajali hiyo baada ya kumaliza kazi hiyo kwa Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar. 
  Akikabidhi Ripoti hiyo Mwenyekiti wa Bodi hiyo Khamis Ramadhan Abdallah amesema kazi hiyo waliyopewa wameweza kuimaliza kwa mujibu wa siku walizopewa na walikuwa huru bila ya kuingiliwa na mkono wa Serikali wala Taasisi yoyote. 
  Aidha alisema Bodi ilifanya kazi katika mazingira magumu lakini walichukulia kazi hiyo niyanyumbani na niwajibu wao kufanya kwa Maslahi ya wananchi wa Zanzibar. Hata hivyo alisema hapo awali kazi hiyo walipangiwa kuifanya kwa kipindi cha mwezi mmoja lakini kutokana na uzito wa kazi hiyo na majukumu mengine walilazimika kuomba mwezi mmoja ambapo kazi hiyo walitakiwa kuikabidhi kesho na badala yake wameweza kuikabidhi leo.
  Mwenyekiti huyo alitoa shukran zake za dhati kwa niaba ya bodi hiyo kwa mamlaka ya Usafiri Baharini kwa ushirikiano mzuri waliouonesha kwa bodi hiyo kwa kipindi chote cha kazi hiyo. 
  Kwa upande wake Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman ameipongeza Bodi hiyo kwa kufanya kazi bila ya upendeleo na zaidi walizingatia uhalisia wa kazi yao na siyo kubabaishwa na Mtu. 
  Alisema chombo hicho hakikuundwa kwa kutafutwa nani mbaya wala mkosa wa ajali hiyo bali kimeundwa kwa ajili ya kuangalia mapungufu yaliyopo na kuweza kurekebishwa ili Wazanzibari wasizidi kuumia. Hata hivyo alisema dalili nzuri ipo katika Ripoti hiyo na kazi iliyobaki ni kuisoma kwa kina na kisha kukabidhi katika Mikono ya Serikali kuu kwa mujibu wa taratibu zilizopo. 
  Aliishukuru sana bodi hiyo kwa vile ilikuwa huru na kuweza kufanya kazi kwa kina bila kizuizi cha mtu wala Serikali. Naye Naibu Katibu mkuu wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Tahir A.K Abdullah amesema Wananchi hivi sasa wanasubiri kuona Serikali imefanya nini tokea ajali hiyo imetokea ambapo aliwatoa wasiwasi kuwa haki itatendeka kwa mujibu wa uchunguzi uliofanyika. 
  Bodi hiyo ya Wajumbe watano ambayo iliyoundwa chini ya Sheria ya Usafiri wa Baharini kifungu no. 4552 na 4551 ya mwaka 2006 imeundwa kufuatia ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2 iliyotokea Miezi miwili iliyopita katika Mkondo wa Nungwi ilipokuwa ikitokea Pemba kuja Unguja. IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR
   Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis Ramadhan Abdallah (kushoto) akikabidhi Ripoti ya Bodi hiyo baada ya kukamilika kwa Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Rashid Seif Suleiman Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
  Mwenyekiti wa Bodi ya kuchunguza ajali ya Meli ya MV. Kilimanjaro 2, Khamis Ramadhan Abdallah (katikati) akisoma baadhi ya vipengele vya Ripoti hiyo wakati wa kumkabidhi  Waziri wa Miundo mbinu na Mawasiliano Zanzibar Rashid Seif Suleiman (Mwenye Kanzu)Ofisini kwake Kisauni nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
  Picha na Nafisa M. Ali-WMM

  0 0


  Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam limewafukuza kazi askari wake wanne waliodhibitika kujihusisha na matukio ya uhalifu, kwa mujibu wa  Kamanda wa kanda hiyo Kamishna Suleiman Kova (pichani).

  Kamanda Kova    amesema leo jijini kuwa hatua hiyo imekuja baada ya uchunguzi wa awali kubaini kuwa askari hao wamekuwa wakijihusisha na vitendo vya uhalifu. 
  Ameseme vitendo hivyo ni pamoja na tukio la Machi 9, 2014 ambalo lilitokea eneo la Mbezi beachi A jijini Dar es salaam ambapo majambazi wapato 15 walifika katika ofisi za kampuni ya Kichina ijulikanayo kwa jina la Hongyang na kupora vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na fedha taslimu  na simu na kisha kutoweka. 
  Kamishina Kova amesema kuwa askari hao wanaotoka katika vikosi mbalimbali ni pamoja na aliyekuwa koplo Rajabu Mkwenda mwenye namba E6396 aliyekuwa askari wa makao makuu Polisi, F9412 PC Saimon wa kituo cha polisi kati, F9414 PC Albanus Poosa wa kikosi cha bendi ya polisi Dar es salaam, na F9512 PC Selemani wa kituo cha polisi kigamboni. 
  Aliseme watu hwao wanastahili adhabu hiyo na hatua zingine zinazofuata kutokana na vitendo hivyo, na kwamba wao kwa sasa sio polisi tena na wanakosa haki zao zote.
  Kamanda Kova aliongeza kuwa katika kuhakikisha haki inatendeka katika suala hilo, watuhumiwa wote hao wametambuliwa na mashahidi na kwamba  taratibu za kipelelezi zilidhibitisha kujihusisha kwao na majambazi ambao ni raia. 
   Kamishina Kova amesema jeshi hilo lipo katika hatua za kujisafisha ili  lionekane ni jeshi bora na zuri mbele ya wananchi.

  0 0


  Na Andrew Chale

  KAMPUNI ya uuzaji wa bidhaa za majumbani na ofisini ya Home Shopping Centre (HSC) imemzawadia mshindi wake wa kwanza wa ‘pendezesha nyumba na HSC’, Rehane Jaffer zawadi ya sh 500,000.  Shindano hilo linaendeshwa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook kwa  jina la ‘Give a Way’. 
  Mshindi alikabidhiwa hundi ya kiasi hicho cha pesa jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Meneja Mauzo na Masoko wa HSC, Nadhir Mubarak Bahayan ambaye aliwataka watanzania kushiriki shindano hilo ambalo kila Ijumaa watakuwa wakijishindia sh. 500,000. 
   “Wateja wetu wa HSC, wanatakiwa kujiunga kwenye mtandao wetu wa facebook na kisha kututumia picha walizopamba ndani ya nyumba zao zitokanazo na bidhaa zetu,” alisema Nadhir. Alisema shindano hilo litaendeshwa kwa mwezi mzima wa Machi 2014
   . 
  Mshindi huyo aliipongeza HSC kwa shindano hio na kusema ni faraja kwake na familia yake. Aidha zoezi hilo ambalo litaendeshwa kwa muda wa mwezi mzima wa Machi huku kila Ijumaa ikitarajiwa kutangaza washindi na kukabidhiwa hundi siku inayofuata. 
   Nadhir aliwataka wateja wao kuwa na tabia ya kutembea kwenye mtandao wa HSC, na kushiriki kupitia https://www.facebook.com/hsctz

  0 0


  0 0

  Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na
  Kozi fupi, 
  Bwana, Juma M. Kanuwa
    
  CHUO CHA DIPLOMASIA DAR ES SALAAM, katika kuendeleza wito na wajibu wa kutoa mafunzo ya muda mfupi na mrefu, mnamo tarehe 31stMarch - 4th Aprili 2014 kitafanya kozi fupi ya ITIFAKI NA MAHUSIANO YA UMMA (PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS) Chuoni Kurasini, Dar es salaam,

  Wawezeshaji wa Mafunzo haya ya muda mfupi kawaida huwa ni mabalozi na wakufunzi waliobobea sana katika mambo ya Diplomasia hivyo kuwapa washiriki uzoefu na kesi halisi zilizowahi kutokea katika eneo husika la mafunzo ili kuwajengea uwezo na waweze kwenda kufanyia kazi moja kwa moja mafunzo na utaalam walioupata.


  Akiongea na waandishi wa habari, Mkuu wa Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi, Bwana, Juma M. Kanuwa akilisisitiza kwamba kutokana na umuhimu wa utaalam wa mambo ya ITIFAKI NA MAHUSIANO YA UMMA (PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS) katika sehemu za kazi, mafunzo hayo yatarudiwa tena tarehe 31st March - 4thAprili 2014, alisema;
   “CHUO CHA DIPLOMASIA kilifanya mafunzo haya mnamo tarehe 3rd– 7 Februali 2014, lakini kutokana na maombi ya wengi na kwakuwa mafunzo haya ya PROTOCOL AND PUBLIC RELATIONS ni muhimu sana hasa eneo la ‘PROTOCOL’,  yatarudiwa tena mnamo tarehe 31st March - 4th Aprili 2014 hapa hapa Chuo cha Diplomasia ili wale wote walioshindwa kuhudhulia hapo awali waweze kuja kwa wingi chuoni na kupata mafunzo hayo toka kwa mabalozi na wataalam waliobobea na wenye uzoefu wa miaka mingi…” 
  Akaongeza kuwa  “..nafasi zimebaki chache hivyo nawashauri wale wote wanaotaka kushiriki mafunzo haya waje Chuo cha Diplomasia au wawasiliane na mratibu kwa namba +255713667303na pia watembelee tovuti ya chuo cha Diplomasia www.cfr.ac.tz kwa maelezo na tangazo la kozi hii…”                                                                                                 

  Mafunzo haya ni muedelezo wa mafunzo ya muda mfupi yaani ‘kozi fupi’ zinazofanywa na CHUO CHA DIPLOMASIA – DAR ES SALAAM, kila mwezi ambapo kozi mbali mbali zimekuwa zikifanyika, kama Utatuzi wa Migogoro “CONFLICT RESOLUTION AND MEDIATION” na Usalama wa taarifa ( INFORMATION SECURITY) iliyofanyika mapema hivi karibuni.

  Pia CHUO CHA DIPLOMASIA kinaweza kufanya kozi kulingana na mahitaji ya taasisi/ wateja na kinakaribisha wadau wote

  Kwa maelezo zaidi wasiliana na Idara ya Utafiti, Uchapishaji, Ushauri na Kozi fupi,

  Mobile: +255713229722, +255713667303                                  
  Website:  www.cfr.ac.tz    
  E-mail:  lucassoona@yahoo.com
  0 0

  Meneja Uhusiano na Mawasiliano  wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Bw. Abel Ngapemba akifanunua kwa waandishi umuhimu wa mradi wa uchimbaji magadi soda  katika mkutano na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO. Kushoto kwake ni Mhandisi wa mradi Godfrey Mahundi na mkuu wa kitengo cha viwanda vya Kemikali Mhandisi Abdallah Mandwanga.
  ----------------------------------------  
  Na Frank Mvungi-MAELEZO

   Tanzania ni miongoni  mwa wazalishaji wakubwa wa magadi soda yatakayoingizia taifa Shilingi Bilioni  480 kwa mwaka, imefahamika.

   Meneja Uhusiano na Mawsiliano wa Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC), Bw. Abel Ngapemba  alisema leo kuwa hatua hiyo inatokana na kugunduliwa kwa kwa kiasi kikubwa cha madini hayo katika Bonde la Engaruka  Wilayani Monduli mkoani Arusha.
  Alizitaja faida za kugundulika kwa madini ya magadi soda kuwa ni ajira zaidi ya 500 na fedha za kigeni kutokana  na mauzo ya madini hayo nje ya nchi.

  Alisema kuwa viwanda vinavyotegemea magadi soda kama malighafi ya uzalishaji hali itakayochochea kukua kwa sekta ya viwanda hapa nchini.

  Bw. Ngapemba  alibainisha kuwa madini ya magadi soda yanatumika viwandani  katika utengenezaji wa bidhaa kama vioo, sabuni, dawa za meno, dawa za hosipitali, uoakaji mikate, kutengeneza  karatasi, nguo, na usafishaji wa maji.

  Alifafanua kuwa utafiti uliofanywa na wataalamu wazalendo kuanzia mwaka 2010 hadi 2013 na ulifanyika kwa awamu  tatu yakwanza ikiwa ni uchunguzi wa awali na kutafuta maeneo ya kufanyia uchorongaji ili kubaini wingi na ubora wa magadi soda.

  Alisema kuwa kazi ilifanywa na kampuni ya OC, na kwamba awamu iliyofuata ni kuangalia njia ya uvunaji wa magadi soda hayo iliyofanywa na JSC Service.

  “Matokeo ya utafiti huo yameonyesha kuwapo kwa magadi soda kiasi cha mita za ujazo bilioni 4.7 na inakadiriwa kila mwaka wastani wa mita za ujazo milioni 1.9 zinaongezeka katika eneo hilo”, alisema Ngapemba.

  Alisema kuwa NDC itahakikisha kuwa katika utekelezaji wa miradi hii mazingira hayataathiriwa na tunu za taifa zitalindwa ambapo mtazamo wa shirika hilo ni kuwapo kwa mradi wa uvunaji magadi, utalii, na ufugaji.
  0 0

  Jopo la wang’amuzi vipaji vya soka limetangaza majina ya wachezaji 36 waliopataikana katika mchakato wa maboresho ya Taifa Stars ulioshirikisha mechi za mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar.

  Kaimu Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Salum Madadi amesema jopo hilo liling’amua vipaji 143 katika mchakato, lakini waliochukuliwa kwa sasa ni hao 36 tu.

  Amewataja wachezaji waliochaguliwa katika mchakato huo kwa upande wa makipa ni Abdulaziz Khatib Haji (Mjini Magharibi), Abubakar Abbas Ibrahim (Tanga), Benedicto Tinoko Mlekwa (Mara) na Mtindi Kheri Ali (Kaskazini Unguja).

  Kwa upande wa mabeki wa pembeni waliochaguliwa katika mchakato huo ambao upo chini ya udhamini wa Kilimanjaro Premium Lager ni Edward Peter Mayunga (Kaskazini Pemba), Hussein Moshi (Tabora), Omari Kindamba (Temeke) na Shiraz Abdallah (Ilala).

  Mabeki wa kati ni Abbas Ali Haji (Kaskazini Unguja), Ancy Abdon (Kagera), Emma Namwamba (Temeke), Hussein Juma Akilimali (Njombe), Joram Nasson (Iringa), Kayombo Silvanus Henrico (Ilala), Miraji Maka (Mwanza),  Ramadhan Ame Ramadhan (Kusini Unguja) na Said Juma Ali (Mjini Magharibi).

  Viungo wapo Abubakar Mohamed Ally (Kusini Unguja), Hashim Ramadhan Magoma (Shinyanga), Juma Said Jega (Lindi), Mtenje Alban Juma (Tanga), Ryna Mgonyike (Temeke) na Yusuf Mpilipili (Temeke).

  Washambuliaji ni Abdallah Kagumbwa (Temeke), Abrahman Othman Ally (Mjini Magharibi), Athanas Fabian Bayagala (Mbeya), Athanas Mdamu (Mwanza), Ayubu Hashim Lipati (Ilala), Chunga Said (Manyara), Mbwana Mshindo Mussa (Tanga), Michael David Mlekwa (Lindi), Mohamed Seif Said (Kusini Pemba), Omar Athuman Nyenje (Mtwara), Paul Michael Bundala (Ilala), Ramadhan Kapalamoto (Kinondoni) na Roman Nyapunda (Temeke).

  Amesema wastani wa umri wa wachezaji hao ambao watafanyiwa vipimo vya afya Machi 19 na 20 mwaka huu kabla ya kambini Machi 21 mwaka huu, Tukuyu mkoani Mbeya ni miaka 21.

  Timu hiyo itakuwa chini ya Madadi akisaidiwa na makocha Hafidh Badru, Salum Mayanga na Patrick Mwangata. Aprili 13 mwaka huu utafanyika mchujo ili kupata wachezaji wa mwisho watakaoungana na wale wa Taifa Stars watakaoingia kambini Aprili 22 mwaka huu.

  Taifa Stars inatarajiwa kucheza mechi ya kirafiki mapema mwezi Mei mwaka huu ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mechi za mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika (AFCON) zitakazofanyika mwakani nchini Morocco.


  Boniface Wambura Mgoyo
  Media and Communications Officer

  Tanzania Football Federation (TFF)

  0 0

   mshindi wa jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa akiwa na mke wake Robby Mgimwa wakifurahia hati aliyokabidhiwa ya kuwa mbunge.
   Godfrey Mgimwa akiwa anafurahia ushindi katikati Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Iringa vijiji mama Mtavilalo.

  0 0

  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifungua mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014
  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe kuzindua Kampuni ya Balton Tanzania, baada ya kufungua rasmi mkutano wa Wafanyabiashara na Wawekezaji kati ya Israel na Tanzania, katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, leo Machi 17, 2014. Kushoto ni Mtaalamu wa Kilimo, Maximillian Sarakikya (kulia) ni Mkuu wa Maendeleo ya Biasara na Habari, Linda Byaba.
  Baadhi ya washiriki wa mkutano huo wakimsikiliza kwa makini Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akiwahutubia ukumbini humo. Kwa picha zaidi BOFYA HAPA

  0 0

   

  Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kushoto) akimkabithi mfano wa hundimwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo wakati wa halfa ya Tuzo za Mwanamakuka 2014 ambapo Airtel Tanzania ni moja kati ya Wadhamini wa tuzo hizo,  Bi Leil Mwambungu aliibuka na kutangazwa mshindi wa mwanamakuka 2014. Akishuhudia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Bank ya Wanawake  Tanzania Bi Margreth Chacha (wakwanza kulia), Hafla ya mwanamakuka ilifanyika jana katika ukumbi wa Escape 1 mikocheni Dar es salaam. 

   Afisa uhusiano wa Airtel Bi Jane Matinde (kulia) akimpongeza mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika halfa ya Tuzo za mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam
  mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu mara baada ya kutangazwa katika hafla ya Tuzo za mwanamakuka iliyofanyika Escape 1 jijini Dar esaalam, pichani kushoto ni Mkurugenzi  Mkuu wa Bank ya Wanawake  Tanzania Bi Margreth Chacha

  ========  ========  =========
  Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel  imekabithi waandaaji wa Tuzo za mwanamakuka The Unity of Women Friends kiasi cha million tano pesa taslimu wakati wa halfa ya  tuzo za mwanamakuka 2014 zilizofanyika jijini Dar es saalam mwisho wa wiki
  Tuzo hizi za mwanamakuka 2014 ziliwashirikiasha washindi 10 wa mwaka 2012 na mwaka 2013 ambapo washindi hawa walifatiliwa biashara zao na kuchaguliwa mshindi mmoja aliyefanya vizuri na kutumia vyema zawadi aliyoshinda katika kuendeleza biashara zao ambapo bi Leila Mwambungu aliyekuwa mshindi wa pili mwaka Jana kuibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014
  Akiongea wakati wa kukabithi zawadi hiyo, Afisa Uhusiano wa Airtel bi Jane Matinde alisema”  Tunayofuraha kuwa  wadhamini  wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa miaka mitatu mfululizo kwa sasa na kuwa sehemu ya kuleta mabadiliko kwa wanawake kupitia tuzo hizi. tunafurahi kuona jinsi kina mama hawa wajasiriamali walioshinda miaka iliyopita wakifanya vizuri katika biashara zao.
  Na sisi Airtel leo tunakabithi kiasi cha kiasi cha shilingi milioni tano kama mchango wetu kwa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka 2014. Tunaamini kiasi hichi cha fedha kitaweza kuwawezesha waaandawaji wa tuzo hizi kufanikisha halfa hii na kuwafikia wanawake na kuwawezesha  kutanua mitaji yao na hatimae kuongeza kipato na faida zaidi na kujikwamua kiuchumi”.
  “Tutaendelea kushirikiana na The unity of Women Friends ili kuhakikisha tunaweza kuwafikia wanawake wengi zaidi nchini” aliongeza Matinde.
  Kwa upande wake mshindi wa mwanamakuka 2014 bi Leila Mwambungu Alisema “naona fahari na furaha kuwa mshindi wa tuzo hizi za mwanamakuka kwa mwaka huu, napenda kuwashukuru sana waandaaji wa tuzo hizi kwa kuniona kupitia juhudi ninazoziweka katika kazi zangu na biashara zangu. Mpaka sasa nimeweza kuajiri watanzania kupitia biashara zangu na  Kiasi hii nilichozawadiwa leo kitanisaidia sana kukuza mtaji. Cha msingi wanawake tupendane na kushirikiana napenda kuwahasa wanawake wenzangu kutokata tamaa na kuongeza  katika biashara zao,  haijalishi kama mtaji mdogo bali wajipange na kujikita katika uzalishaji na hatimae kuinua mtaji na kuweza kufanya biasha kwa mtaji mkubwa, hakuna siri nyingine ya mafanikio zaidi ya jitihada , hari na kujiwekea malengo na kuhakikisha yanafikiwa kwa wakati uliopagwa.
  Naye mwenyekiti na Mratibu wa Mradi wa The Unity of Women friends Maryam Shamo alisema Tuzo hizi za Mwanamakuka zinaendelea kukua na kuziboresha zaidi,   kwa mwaka huu lengo letu lilikuwa ni kuwawezesha wachache kwa kuwafatilia washindi wetu 10 wamiaka iliyopita na kuona jinsi gani biashara zao zinavyoenda na kumzawadia anayefanya vizuri zaidi. Lengo ni kuendelea kuwahamasisha na kufatilia mafanikio yao kwa karibu.
  vilevule tukiangalia miaka iliyopita tuliweza kuwashirikisha wanawake tu katika sherehe za tuzo hizi lakini kwa mwaka huu tumeamua kushirikisha familia kwa kuandaa bonanza ambapo wakinababa na watoto kwa pamoja tunasherehekea mafanikio haya, na kusherehekea siku ya wanawake duaniani huku tukienzi juhudi za wanawake jasiri nchini na kuwazawadia
  Tunashukuru sana Airtel kwa kushirikiana nasi miaka mitatu kwa sasa na tunaamini kuwa bado wataendelea kutoa mchango wao na kushirikiana nasi na kutuunga mkono kwa miaka mengine ijayo na kuhakikisha lengo letu la kumwinua mwanamke wa kitanzania linafikiwa. Alisema Shamo
  Kwa mwaka huu Tuzo hizi zilishirikisha washindi waliopatikana miaka iliyopita ambapo kati yao pamoja na Tatu  Ngao, Mwananne Msekalile, Sikudhani Daudi, Nasra, Aziz, Khalid, Leila Mwambungu, Selestina Renatus, Maajab Yusufu na Agnes Daudi  ambapo Bi Leila Mwambungu Ameibuka kuwa mshindi wa mwanamakuka 2014

  0 0

   Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akiwa na Makamu wake Jaji Augustino Ramadhani baada ya kuwasili bungeni mjini Dodoma na muda mfupi kabla ya kuanza  kuwasilisha rasimu ya Katiba Mpya. 
   Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba  wakiwa wamesimama kupinga Jaji Joseph Warioba asiwasilishe rasimu ya katiba huku wakipiga kelele na kugomga meza.
   Baadhi ya wajumbe wa Bunge la Katiba  wakiwa wamesimama kupinga Jaji Joseph Warioba asiwasilishe rasimu ya katiba 

  Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Warioba akijiandaa kuwasilisha rasimu ya Katiba Mpya. Hata hivyo zoezi hilo liliahirishwa hadi kesho wakati baadhi ya wajumbe waliposimama na kutaka  baadhi ya kanuni walizojiwekea zifuatwe, baada ya kuonekana hazikufuatwa. 
   Muafaka ulifikiwa baadaye na rasimu hiyo itawasilishwa kesho kwa Jaji Warioba kufanya hivyo kwa masaa manne badala ya moja ama mawili yaliyopendekezwa awali.  Habari kamili  zitawajia muda mfupi ujao...

  Picha na Deusdedit Moshi 
  wa Globu ya Jamii, Dodoma

  0 0

   Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Baraza la Watumishi Bw. George D. Yambesi, katikati, akiendesha mkutano wa Baraza, kulia ni Naibu Katibu Mkuu Bw. HAB Mkwizu na kushoto ni Katibu Bi. Lilian Denis.
   Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri Kazi Bw. Mick Kiliba akitoa mchango wake wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma
   Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi Rasilimaliwatu Bw. Emmanuel Mlaya akitoa mchano wake wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Ofisi ya Rais, Utumishi.
  Wajumbe wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
   Wajumbe wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi.
  Wajumbe wakiimba wimbo wa mshikamano wakati wa mkutano wa Baraza la Wafanyakazi. Picha na Happy Shayo

  0 0

  Leo ni Hepi Besdei ya kuzaliwa 
  mdau Ronnie  Mtawali. 

  Globu ya Jamii inamtakia afya nyema na maisha ya furaha kwa siku hii.
  Ankal ana furaha na fahari kubwa kuwa mmoja wa marafiki wa karibu wa Ronnie ambaye miaka takriban 20 iliyopita alimpigia picha zake za harusi. 

  0 0

  Mhe. Mutaza Mangungu mbunge wa Kilwa kwa tiketi ya CCM akiongea na Vijimambo mchana wa Jumamtatu March 17, 2014 kutoka Dodoma na kuelezea faida ya Uraia pacha. Msikilize hapo chini

  0 0

  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akiwa ameambatana na mkuu wa wilaya ya Moshi,Ibrahim Msengi wakiwa na mwenyeji wao mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi,(MUWSA)mhandisi Cyprian Luhemeja wakati akitembelea chanzo cha maji cha Cofee Curing.
  Chanzo cha Maji cha Cofee Curing.
  Jengo dogo ambalo linatumika kuhifadhi dawa maalumu ya kuweka kwenye maji kwa ajili ya Chlorination.
  Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro Leonidas Gama akipata maelezo kutoka kwa mmoja wa maofisa wa MUWSA.
  Mkurugenzi wa mamlaka ya maji safi na maji taka mjini Moshi(MUWSA)Injinia Cyprian Luhemeja akifafanua jambo kwa mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro ,Leonidas Gama wakati alipotembelea Tanki la maji la Kil.(Kulia)ni mkuu wa wilaya ya Moshi Ibrahim Msengi.
  Kwa picha zaidi na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii BOFYA HAPA

  0 0

  We offer a choice of comfortable rooms and great rates. More than 20 well appointed and spacious rooms with double-gazed windows. 
  Conference room are available for various functions such as seminars, cocktail parties, product launches etc. Garden Bar Located at the Garden side of the Hotel. 
  We are located at the Mbezi – Salasala Area. 
   We are the latest addition to Dar es Salaams mid-market hotel portfolio. 
   In order to suit your budget we have decided to offer you subsidized rates while maintaining service excellence and efficiency. Restaurant –Garden Bar – Conference Room – Outside Catering – Business Centre & Laundry Services
  Seduta hotel by night
  Garden facilities
  Luxurious bedroom
  Restaurant
  Hotel Seduta by day

       BED / BREAKFAST
            Single Room Tsh.60,000/- or USD 40.
            Standard Room Tsh,70,000/- or  USD45.
            Delux Room   Tsh,90,000/- or USD 60.
            Suite Room    Tsh,100,000/- or USD 77.
            Executive Room T,sh,120,000/- or USD 80.
            Executive Suite Room. Tshs.150.ooo/- or USD 95.

               CONFERENCE
            TSH,54,000.PER PERSON FULL DAY.
            TSH,45,000.PER PERSON HALF DAY.older | 1 | .... | 390 | 391 | (Page 392) | 393 | 394 | .... | 3278 | newer