Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 389 | 390 | (Page 391) | 392 | 393 | .... | 3278 | newer

  0 0

   Baadhi ya Wanakijiji cha Kalenga A,kata ya Kalenga Iringa Vijijini mkoani Iringa wakiwa wamejitokeza mapema leo asubuhi kupiga kura kumchagua Mbunge wamtakae wa jimbo hilo la Kalenga.Uchaguzi Mdogo wa Jimbo hilo unafanyika leo,ambapo vyama Vitatu;CCM,CHADEMA na CHAUSTA vikiwa vimesimamisha wagombea wake katika uchaguzi huo unaotokana na kifo cha aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo,pia Waziri wa Fedha,Dk William Mgimwa.Aidha Wagombea wa Chadema Grace Tendega na wa CCM,Godfrey Mgimwa ndio wanaopewa nafasi kubwa ya kuchuana na hatimaye mmoja wao kuibuka kinara kwa kupigiwa kura na Wananchi,huku mgombea wa CHAUSTA,Richard Minja akipewa nafasi ndogo kutokana na maandalizi hafifu ya ushiriki wake.
   Baadhi ya akina Mama waliojitokeza kupiga kura mapema leo asubuhi katika kijiji cha Kalenga A,kata ya Kalenga Iringa Vijijini wakitazama majina yao kwenye ukuta tayari kwa kutumia haki yao ya msingi ya kumchagua kiongozi wamtakae kwa kupiga kura
   Mmoja wakazi wa kijiji cha Mangalali,kata ya Ulanda akiwa ndani ya chumba cha kupigia kura akisubiri kupiga kura mapema leo asubui.
  Wakazi wa kijiji cha Mangalali,kata ya Ulanda jimbo la Kalenga,wakiwa wamejipanga nje ya chumba cha kupigia kura mapema leo asubuhi.Kwa ujumla katika kata kadhaa ambako Globu ya Jamii imepita imeshuhudia kuwepo na utulivu mkubwa,wapiga kura wamejitokeza kadiri ya uwezo wao bila kubugudhiwa na hali ya namna yoyote,huku Jeshi la Polisi Mkoa wa Iringa likiwa limejipanga vyema kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa katika uchaguzi huo Mdogo wa Ubunge jimbo la Kalenga.PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA GROUP-KALENGA,IRINGA.

  0 0

   Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka akiwa katika picha ya pamoja na watoto yatima wa kituo Nyumbani kilichoko Ismani.
   Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka akipanda mti katika shule ya msingi Igula katika Tarafa ya ismani
   Wafanyakazi wa shirika la Restless Tanzania, Mwadawa na Amne wakitoa maelekezo kwa Mkurugenzi bg wa  Halmashauri ya wilaya ya Iringa Pudenciana Kisaka juu ya shughuli za shirika hilo.


  0 0

  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akiwa katika zoezi la ukaguzi wa mabanda mbalimbali yaliyoandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu na huduma za mama wajawazito na watoto wachanga katika maadhimisho ya siku ya Utepe Mweupe Tanzania yaliyofanyika kitaifa Mkoani Rukwa katika Tarafa ya Mtowisa. Dkt. Seif Rashid alimuwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda ambae awali alikubali kushiriki maadhimisho hayo ambapo amekabiliwa na majukumu mengine ya kitaifa. Kushoto kwa Dkt. Seif Rashid ni Mratibu wa Taifa wa Utepe mweupe Mama Rose Mlay. Kauli Mbiu ya maadhimisho hayo ikiwa ni "WAJIBIKA MAMA AISHI"
  Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid akihutubia katika maadhimisho hayo ambapo aliwapongeza wadau wote wanaopigania na kusaidia afya ya mama na watoto na kuahidi kutoa kipaombele katika bajeti kwa ajili ya kusaidia kuokoa maisha ya mama wajawazito na watoto nchini. Aidha amezitaka Halmashauri nchini kutoa kipaombele kwa kuongeza bajeti zao katika kuhudumia afya ya mama wajawazito na watoto wachanga.
  Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Smythies Pangisa akitoa salamu za Mkoa wa Rukwa kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa huo Injinia Stella Manyanya katika Maadhimisho hayo ya kitaifa. Katika Salamu hizo alisema zipo changamoto nyingi  katika sekta ya afya zinazohitaji ufumbuzi wa haraka ikiwemo upungufu wa watoa huduma, vifaa tiba, dawa, magari ya kubebea wagonjwa, vituo vya kutolea huduma za afya na vingine kuwa mbali na maeneo ya wananchi kwa baadhi ya maeneo.
  Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa Daktari John Gurisha akifafanua baadhi ya mambo katika sekta ya afya Mkoani Rukwa.
  Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Kimanta akikabidhi kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Seif Rashid maoni na maombi ya wakazi wa Wilaya yake katika kuimarisha sekta ya afya katika Wilaya yao na Taifa kwa ujumla.
  Maadhimisho hayo yalitawaliwa na hali ya hewa ya mvua ambayo hata hivyo haikuathiri mwenendo mzima wa ratiba iliyopangwa, baadhi ya wananchi walilazimika kutumia miamvuli na wengine kuonyesha uzalendo mkubwa na kuamua kunyeshewa hadi kukamilisha maadhimisho hayo, hata hivyo mvua hiyo ilikatika karibu na kufikia mwishoni mwa maadhimisho hayo.
  Bi Adrianne Strong ambae nae ni mdau wa afya ya mama wajawazito na watoto wachanga akitoa salam zake na kujitambulisha. Hivi karibuni Bi Adriane Stong kwa kushirikiana na waumini wenzake wa Kanisa la University United Methodist Church la Washington DC Marekani walitoa msaada wa boti na life jacket kwa ajili ya kusaidia huduma za afya ya mama wajawazito na wagonjwa mwambao wa Ziwa Rukwa.
  Balozi wa Utepe Mweupe Tanzania ambae pia ni mwanamuziki Sara Thomas akijumuika na wanawake wengine kuimba wimbo wa kuihimiza Serikali na wananchi kutimiza wajibu wao katika kuhakikisha wanaokoa maisha ya mama wajawazito na watoto wachanga.
  Zoezi la uchangiaji wa damu salama lilikua likifanyika katika kila Wilaya za Mkoa wa Rukwa katika wiki ya maadhimisho hayo ya utepe mweupe ambapo chupa za damu zaidi ya alfu moja zilichangiwa na wananchi wa Mkoa wa Rukwa. (Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa @rukwareview.blogspot.com)

  0 0  Nyumba za Askari wa jeshi la polisi zilizopo eneo la Chumbageni nyuma ya kituo cha polisi kikuu cha Chumbageni jijini Tanga zikiungua moto. Hahdi sasa chanzo cha moto huo pamoja na athari zake havijajulikana


  Askari wa kikosi cha Zimamoto wakiwa kazini
  Mkuu wa wilaya ya Tanga Mh.Halima Dendegu akiwasili katika eneo la tukio
  Mh.Halima Dendegu akishuhudia ajali ya moto huo katika nyumba za polisi Chumbageni,jijini Tanga hapo jana 
  Wananchi wakishuhudia na kusaidia vikosi vya zimamoto katika uzimaji moto huo.
  Baadhi ya vitu vilivyookolewa katika ajali ya moto.

  Picha kwa hisani ya Tanga kunani(TK)

  0 0

  Mrembo Sarah Paul aliposhiriki furaha yake ya siku ya kuzaliwa na watoto wa kituo cha TZ 820 FPTC NG'AMBO STUDENT CENTER - Kilichopo Tabora.
  Kila mmoja alipata nafasi ya kufurahia keki iliyoandaliwa maalumu kwa watoto hao.
  Baadhi ya vitu alivyowaandalia watoto hao na kuvikabidhi kwenye shirika hilo.
  Sarah Paul, mshindi wa shindano la urembo la Redds Miss Tabora 2012, ambaye pia mwaka jana alishiriki katika shindano hilo hadi kufikia fainali za Miss Tanzania.
  ****
  Leo katika kusherehekea siku yake ya kuzaliwa amefanikiwa kuwatembelea watoto wanakusanywa na kanisa la FPCT NG'AMBO wanaopewa msaada na Shirika la Compassion International Tanzania na kuwasaidia watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Watoto hawa wanakusanywa kwa lengo la kuwatoa na kuwakomboa umaskini wa kiuchumi, kijamii, kimwili na kiroho na kuwawezesha waje wawe watu wazima wanaojua wajibu wao na kujitegemea.

  Pia huwalipia ada, huwauguza na kuwapeleka hosipitali wanapoumwa, huwafundisha ujasiriamali n.k Aliyasema  Suleiman H. Halletu mkurugenzi wa kituo kinachoitwa TZ 820 FPCT NG'AMBO STUDENT CENTER na kuongeza kuwa wana watoto 254 katika kituo chao.  0 0

   Waziri wa Maji  Profesa Jumanne Maghembe akipata maelezo kutoka kwa mtalamu kutoka nchini Australia Eng Johann Fabach kuhusu bomba lililotengenezwa kwa teknolojia ya kisasa nchini Australia ambalo haliharibiki kwa urahisi wala kupata kutu. Kushoto  ni mkurugenzi msaidizi  Prima Business ya nchini Australia Bibi Annastella Baradyana. Maonesho hayo yanafanyika katika uwanja wa Jamuhuri Mjini Dodoma Picha na Chris Mfinanga

  Ofisa Habari wa Dawasa Bi. Neli Msuya akitoa maelezo kwa waziri wa Maji  Profesa Jumanne Maghembe kuhusu shughuli zinazofanywa na Dawasa 


  0 0

  Maafisa na Askari Polisi hapa nchini  wametakiwa badili tabia zao kwa kujiepusha na vitendo vya kudai na kupokea rushwa kutoka kwa watu wenye Matatizo yanayohitaji huduma za kipolisi. 
   Hayo yameelezwa na Mkuu wa Kitengo Ufuatiliaji na Tathimini cha Jeshi la Polisi nchini, Naibu Kamishna (DCP) Mpinga Gyumi, wakati akitoa mada kwa washiriki wa Mafunzo ya kuimarisha Miundombinu ya Maadili na mapambano dhidi ya Rushwa yanayotolewa kwa Wakuu wa Polisi wa Tarafa na Majimbo yanayofanyika mjini Dodoma. 
   DCP Gyumi, ameonya kuwa Jeshi la Polisi halitamvumilia Afisa ama Askari yeyotw atakayekwenda kinyume na maadili ya Jeshi hilo jambo ambalo amesema limekuwa likipakwa matope. Akikariri baadhi ya vifungu vilivyomo kwenye kitabu cha miongozo ya Jeshi la Polisi nchini Police General Order (PGO), amesema kitabu hicho kimetoa makatazo kwa Askari Polisi wa vyeo mbalimbali na kutoa maelekezo mazuri yanayofaa kufuatwa na kila Askari Polisi. 
   DCP Gyumi pia amewakumbusha Maispekta hao pamoja na Maafisa wa ngazi ya juu wa Jeshi hilo kujiepusha na vitendo vya kupokea zawadi kwani kwa kufanya hivyo ni sawa na kuhalalisha rushwa. 
   Amesema rushwa imekua ikipunguza heshma na uadilifu kwa mtumishi na hivyo kumfanya kushindwa kuheshimu sheria, kanuni, taratibu na kuwafanya baadhi ya watumishi kujilimbikizia mali kwa njia zisizo halali, wizi na ubadhirifu wa mali ya umma. 
   Amewaonya wale wote wanaojihusisha na matumizi mabaya ya mali za umma kama vile magari, kompyuta, mashine na vitendeakazi vingine kuacha kufanya hivyo kwani matokeo yake ni kuitia serikali hasara. 
   Amewataka Maafisa na Askari wa ngazi zote kuwa wasafi mbele ya Jamii hali itakayilifanya Jeshi la Polisi kuwa kimbilio la wanyonge na sio kukimbiwa.
  “ Nawaombeni kila mmoja wenu kutimiza wajibu wake na kuzaliwa upya hata kama anadhani ameshindikana”. Alisema DCP Byatao. 
   Naye Kamishna wa Polisi Jamii nchini CP Mussa Ali Mussa, amewataka Mainspekta hao kuhakikisha kuwa wanaondokana na vitendo vya kudai na kupokea rushwa ili wawe mfano bora kwa jamii na Askari waliochini yao. 
   Awali Mkuu wa Kitengo cha Maadili na Nidhamu cha Jeshi la Polisi nchini SACP Patrick Byatao, alisema hadi sasa, zaidi ya Polisi 1,100 wakiwemo Maafisa Wanadhimu wa Polisi wa mikoa, Wakuu wa Upelelezi wa wilaya na wa Usalama Barabarani hapa nchini, wameshanufaika na mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Shirika la Misaada la Maendeleo la nchini Uingereza (DFID).
   Kamishna wa Polisi Jamii nchini,  CP Mussa Ali Mussa, akitoa maagizo kwa Wakaguzi wa Polisi wanaoshiriki katika mafunzo ya Miundombinu ya Maadili na mikakati ya kudhibiti rushwa yanayofanyika mjini Dodoma.
   Afisa Habari Mkuu wa Jeshi la Polisi Zanzibar Inspekta Mohammed Mhina (katikati) akiwaelekeza jambo waandishi wa Habari wa Jeshi la Polisi walioshiriki katika mafunzo ya Miundombinu ya Maadili na mikakati ya kupambana na rushwa. kushoto ni Inspekta . Dickson Gibeshi na kulia ni Sajini Shabani Msangi,
  Wakaguzi wa Polisi kutoka mikoa mbalimbali nchini wanaoshiriki  mafunzo ya miundombinu ya maadili na mikakati ya kupambana na vitendo vya rushwa wakimsikiliza Kamishna wa Polisi Jamii nchini CP. Mussa Ali Mussa, wakati akitoa mada juu ya umuhim wa Polisi Jamii. 

  0 0

  With salams and jambo from Bukoba,
    Now the question is where do the roots start? If it starts in the skin we can remove it at Mugana but if it originates from spine then only a Neuron Surgeon can do it. Read more below...  0 0

  Na Othman Khamis Ame wa OMPR
  Jamii Nchini imetahadharishwa kuwa makini katika kipindi hichi kilichoanza cha msimu wa mvua za masika ambacho kimezoeleka kuwa na matukio mbali mbali ya maafa yanayoleta athari kwa wananachi. 
  Tahadhari hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Maafa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wakati akiwafariji wananchi waliokumbwa na maafa kufuatia Upepo Mkali ulioambatana na mvua jana jioni katika maeneo ya Kwaalamsha, Makadara na Mkele ndani ya Wilaya ya Mjini. Balozi Seif ambae pia ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alisema mbali ya mvua na upepo lakini kipindi hichi cha masika pia hukumbwa na miripuko ya maradhi tofauti ya kuambukiza jambo ambalo jamii inapaswa kujihadhari nayo. 
  Aliwahakikishia wananchi hao kwamba Serikali Kuu kupitia Idara yake ya Maafa ambayo iko chini ya Ofisi yake inaendelea kufanya tathmini na hasara iliyowakumbwa wananchi hao na baadaye iangalie namna ya kusaidia nguvu zitakazowawezesha kurejea katika mazingira yao ya awali. 
  “ Nimekuja na Timu yangu Katibu Mkuu, Mkurugenzi Maafa na timu yake kuanza tathmini na maafa haya na baadaye kuandika ripoti itakayotusaidia sisi Serikalini namna ya kuchukuwa hatua za kukabiliana na maafa hayo yaliyojitokeza “. Alisisitiza Balozi Seif. 
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliwapongeza Wananchi mbali mbali waliojitolea nguvu, maarifa na hata hifadhi ya dharura kwa wenzao waliopatwa na maafa hayo kufuatia upepo huo wa ghafla. 
  Alisema kitendo hicho mbali ya kuleta faraja kwa waathirika hao pamoja na Serikali kwa jumla lakini pia kimeongeza upendo na kuimarisha ushirikiano na mshikamano miongoni mwa Wananchi hao. 
  “ Ukweli nimefarajika sana kusikia kwamba majirani zenu walikuwa pamoja na nyinyi muda wote wa tukio hili. Huu hasa ndio ujirani mwema unaotakiwa kuwemo ndani ya nyoyo za wanaadamu wakati wote “. Alifafanua Balozi Seif. 
  Wakitoa shukrani zao kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi baadhi ya wananchi hao walioathirika na upepo huo walielezea kufarajika kwao na hatua zilizochukuliwa na majirani zao katika kuwasaidia kukabiliana na maafa hayo. 
  Nyumba zipatazo Tatu katika Shehia ya Kwaalamsha, Tano Sheria ya Mkele na nyengine kadhaa ambazo bado idadi yake hajijajuilikana katika Shehia ya Makadara zimeathirika kutokana na upepo huo.
   Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwapa pole baadhi ya Wananchi ambao nyumba zao zilikumbwa na upepo mkali katika Shehia za Kwaalamsha, Makadara na Mkele Wilaya ya Mjini. 
   Moja ya kati ya Nyumba  tatu zilizoathirika na upepo mkali uliovuma na kuathiri nyumba mbali mbali katika Mtaa wa Kwaalamsha Mjini Zanzibar.
   Moja ya kati ya Nyumba  tatu zilizoathirika na upepo mkali uliovuma na kuathiri nyumba mbali mbali katika Mtaa wa Kwaalamsha Mjini Zanzibar.
  Baadhi ya nyumba zilizoathirika kutokana na upepo Mkali uliovuma  na kusababisha hasara kubwa katika Shehia ya Makadara Mjini Zanzibar.
  Picha na Hassan Issa wa OMPR , ZNZ

  0 0

  Walimu wa sekondari wakiwa duka la Kwetu Net (Internet Cafe) mjini Iringa leo wakiangalia kwenye mtandao halmashauri walizopangiwa  kwenda ambako watapangiwa shule za kufanyia kazi leo.

  0 0

  Na Saidi Mkabakuli 
  Tathmini iliyokuwa ikifanyika katika kutimiza ndoto ya kuwa na Bandari mpya ya Mbegani kufikia mwaka 2017 na kutekeleza Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16) imekamilika kwa takribani asilimia 90 ya eneo zima la mradi huo. 
   Hayo yamedhihirishwa na Mthamini Mkuu wa Ardhi ya Mradi huo, Mhandisi Emmanuel Mrema wakati akizungumza wakati wa mkutano wa pamoja na Timu ya Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipofanya ziara ya ukaguzi wa maendeleo ya mradi huo. Mhandisi Mrema alisema kuwa mpaka sasa jumla ya kaya 1100 kutoka vitongoji vya Bisibisi, Mji Mpya, Mlingotini na Pande vimeshafanyiwa tathmini, ambapo makadirio ya awali yanaonesha jumla ya shilingi bilioni 23 zinatarajiwa kulipwa kupisha mradi. 
  “Mpaka sasa takribani asilimia 90 ya eneo la mradi ambalo ni sawa na hekta 2000 limeshakamilika, ambapo kwa mujibu wa mapendekezo ya tathmini tunatarajia malipo kufanyika kufikia mwezi Juni mwaka huu,” alisema Mhandisi Mrema. 
  Akizungumza katika mkutano huo, mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri alisema kuwa kuna haja ya kuhakikisha fidia kwa wanavijiji hao inalipwa kwa wakati ili kuondoa usumbufu wa kusubiri malipo ya kwa muda mrefu hali itakayochochea kuchelewa kwa utekelezaji wa mradi. 
  “Nawaomba muhakikishe malipo yanafanywa kwa wakati ili kuwaondoshea usumbufu wananchi ili kulinda heshima ya Serikali na kuondosha kero ya kusubiri ya kusubiri kwa muda mrefu,” alisema Bibi Mwanri ambaye ni Naibu Katibu Mtendaji anayeshughulikia Huduma za Jamii na Maendeleo ya Idadi ya Watu. 
  Akijibu hoja ya ushirikishwaji wakati wa zoezi hilo, Mwenyekiti wa Kijiji cha Pande, Bw. Ubezi Kondo alisema kuwa kwa kiasi kikubwa wamekuwa wakishirikishwa katika kila hatua ya uthamini huo. 
  Aliongeza kuwa hali hii imewaongezea hamasa ya kuupisha mradi huo ili kutimiza ndoto ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete ya kujenga Bandari hiyo pamoja na ahadi aliyoitoa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1968. 
  “Kwa hakika tunaukubali mradi huu kwa mikono miwili ili kutimiza ndoto na ahadi za Rais Kikwete na ya Mwalimu Nyerere aliyoitoa mwaka 1968 wakati akifungua Chuo cha Mbegani ambapo aliahidi kuwa atahakikisha kunajengwa Bandari ya kisasa Mbegani,” alisema Bw. Kondo. 
  Kwa mujibu wa Naibu Katibu Mtendaji (Uchumi Jumla), Prof. Longinus Rutasitara ambaye ni kiongozi mwenza wa ukaguzi huo, uwekezaji katika Bandari mpya ya Mbegani unatoa fursa za kimkakati katika kufikia malengo ya Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16). 
   “Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka Mitano (2011/12 - 2015/16) unaweka bayana kuwa uwekezaji wa Bandari ni mojawapo ya maeneo ya kipaumbele na kimkakati ambapo kukamilika kwa ujenzi wa bandari mpya ya Mbegani Bagamoyo kunatarajiwa kupunguza msongamano wa meli katika bandari ya Dar es Salaam,” alisema Prof. Rutasitara. 
   Serikali imeaandaa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano ukiwa na lengo la kuwa na mfumo madhubuti wa kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025. 
  Lengo la Dira ni kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025.
   Meneja Miradi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Alexander Ndibalema (Kulia aliyesimama) akizungumza katika kikao cha pamoja kati ya Timu yaUkaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, wawakilishi wa wanavijiji vya Mradi wa Bandari Mpya ya Mbegani na Timu ya Uthamini wa Ardhi wa eneo la mradi. Waliokaa viti vya mbele ni viongozi wa Timu ya ukaguzi, Bibi Florence Mwanri (Wapili Kulia) na Prof. Longinus Rutasitara (Watatu Kulia). Kushoto ni Mratibu wa ziara hiyo, Bibi Salome Kingdom.
   Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Kulia) akizungumza katika mkutano huo.
   Mthamini Mkuu wa Ardhi ya Mradi huo, Mhandisi Emmanuel Mrema (Kulia) akizungumza katika mkutano huo.
   Mwenyekiti wa Kijiji cha Pande, Bw. Ubezi Kondo (Kulia aliyesimama) akizungumza wakati Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango ilipopita kijijini hapo kujua hali ya zoezi la tathmini ya ardhi kwa ajili ya mradi wa Bandari Mpya ya Mbegani. Kulia kwake ni Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri na Mthamini Mkuu wa Ardhi ya Mradi huo, Mhandisi Emmanuel Mrema.
   Mwenyekiti wa Kijiji cha Pande, Bw. Ubezi Kondo (Kushoto) akionesha eneo itakapokuwepo Bandari Mpya ya Mbegani. Wanaotazama ni Meneja Miradi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Alexander Ndibalema (Kulia), Mthamini Mkuu wa Ardhi ya Mradi huo, Mhandisi Emmanuel Mrema (Wapili Kulia) na Mmoja wa viongozi wa Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango, Bibi Florence Mwanri (Watatu Kulia).
   Meneja Miradi wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Bw. Alexander Ndibalema (Kulia) akitoa maelezo juu ya maendeleo ya Mradi wa Bandari Mpya ya Mbegani katika eneo itakapokuwepo bandari hiyo. Wanaomsilikiliza ni Timu Ukaguzi wa Miradi ya Maendeleo kutoka Ofisi ya Rais, Tume ya Mipango. Picha na Saidi Mkabakuli


  0 0

   Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipeana mikono  na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Mjumbe Maalum wa Rais wa Afrika Kusini Mhe. Maite Nkoana-Mashabane, ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje wa nvhi hiyo Ikulu jijini Dar es salaam leo.
  Picha na Ikulu
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumapili, Machi 16, 2014, amepokea ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini.

  Ujumbe huo wa Rais Zuma umewasilishwa kwa Rais Kikwete na Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Mheshimiwa Maite Nkoana-Mashabane wakati mama huyo alipokutana na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete, Ikulu, Dar Es Salaam.

  Mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo, viongozi hao wamejadili masuala yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Afrika Kusini na masuala ya kikanda ambako nchi zote mbili ni wanachama wa Jumuia ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

  Mheshimiwa Nkoana-Mashabane amendoka nchini mara baada ya kuwasilisha ujumbe huo kwa Rais Kikwete. 


  Imetolewa na;

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu,

  DAR ES SALAAM.


  16 Machi,2013


  0 0
 • 03/16/14--12:30: Bwawa la maini oyeeeee!
 •  Liverpool leo wameheza  kandanda safi ingine kwa miaka kibao kwa kuichabanga  Manchester United 3-0 katka uwanja wao wa nyumbani wa  Trafford on Sunday,  huku mkongwe asiyezeeka  Steven Gerrard akitikisa nyavu mara mbili kwa njia ya penati na kulihamasisha Bwawa la Maini kwa mara ingine tena.
  Kiungo huyo alipiga penati mbili za kufa mtu kuhakikisha vijana wa Brendan Rodgers wakiondoka na pointi tatu zote.
  Luis Suarez aliongeza maumivi kwa Man U baada ya ‘chumba’ cha uhakika cha  Daniel Sturridge  kilipoguswa na kudondoka mbele yake,  ambapo raia huyo wa Uruguay hakufanya makosa alipochomeka kitu nyavuni mbele ya kipa wa Man U  David De Gea kumaliza kazi ya siku.

  Ndio kusema Bwawa la Maini limechukua tena nafasi yake  pili (kuelekea ya kwanza) baada ya kuikopesha Manchester City kwa masaa kadhaa. Hadi sasa, kwa mujibu wa wataalamu wa soka,  hakuna sababu ya kulifanya Bwawa la Maini likose kunyakua ubingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza kwa mara ya 20!

  0 0

  Ofisi ya Katibu wa Bunge Maalum inawatangazia Wajumbe wa Bunge Maalum na umma kwa ujumla kuwa Mkutano wa Bunge Maalum utaendelea mjini Dododma kesho kwa ratiba ifuatayo:

  Tarehe 17/3/201 kuanzia saa 3:00 asubuhi kutakuwa na  kiapo kwa Wajumbe wa Bunge Maalum ambao bado hawajaapishwa. Hivyo Wajumbe wote ambao hawajaapa  kiapo cha ujumbe wa Bunge Maalum wanatangaziwa kufika Idara ya Shughuli za Bunge Maalum kesho saa 2:00  asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kutambuliwa.


  Saa 11:00 jioni Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba Jaji Joseph Sinde Warioba atawasilisha  Rasimu ya Katiba kwenye Bunge Maalum.


  Tarehe 18/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi Wajumbe wote wa Bunge Maalum watapewa semina kuhusu ufahamu mpana zaidi wa Kanuni za Bunge Maalum.

  Tarehe 19 na 20/3/2014 kuanzia saa 3:00 asubuhi wajumbe wote watapewa semina kuhusu Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  Tarehe 21/3/2014 saa 3:00 asubuhi kutakuwa na uteuzi wa Wajumbe wa Kamati za Bunge Maalum  na saa 10:00 jioni Mgeni Rasmi ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atalihutubia Bunge kuashiria ufunguzi rasmi wa Bunge Maalum.

  Atakayeipata taarifa hii amjulishe mwenzake. 

  Imetolewa na Ofisi ya

  KATIBU WA BUNGE MAALUM

  0 0

   
  Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akiwa amebebwa juu na wafuasi wa chama hicho usiku huu,kwenye Ofisi za CCM mkoa,huku wakisubiri matokeo rasmi kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi muda wowote kuanzia sasa.
  TOSA no.1 
  CCM 98 ,Chadema 20, CHAUSTA 0
  Ipamba no2. CCM 104, Chadema 10,CHAUSTA 0
  Isakulilo CCM 83,Chadema 8,CHAUSTA 0

  Kilindi A CCM 69 ,Chadema 23, CHAUSTA 0
  Ofisi ya Kijiji(Kilindi) CCM 117, Chadema 53, CHAUSTA0
  Zahanati  CCM 117,Chadema 67, CHAUSTA 1
  Ifunda
  Kivalali A CCM 99 Chadema 19 CHAUSTA 0
  Kivalali B CCM 109 Chadema 14, CHAUSTA 1
  Muwimbi CCM164, Chadema 22 CHAUSTA 0

  Mahanzi CCM 130 Chadema 46 CHAUSTA 0
  Ikungwe A CCM 131 Chadema 23 CHAUSTA 0
  Ikungwe B CCM 216 Chadema 13 CHAUSTA 0
  Magunga CCM 184 ,Chadema 4 CHAUSTA1
  Wasa CCM 149,Chadema 15 CHAUSTA 0
  Usengelidete CCM 260,Chadema 46,CHAUSTA O
   KAMANDA WA UVCC MKOA WA IRINGA  SALIM ASAS AKICHEZA  KWA SHANGWE  VIWANJA  VYA CCM MKOA KUSHEREKEA  USHINDO  WA  CCM KALENGA

  Matokeo ya Awali yasiyo rasmi baadhi ya vituo  inaongoza kwa mbali.


  0 0


  Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi akimnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete kwa Wananchi wa Kijiji cha Kibindu,Kata ya Mbwewe,Bagamoyo leo Machi 16,2014.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI,CHALINZE.
   Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Ridhiwani Jakaya Kikwete akisalimiana na wanakijiji wa kijiji cha Kwamsanja,wakati alipofika kwa ajili ya kuzungumza nao na kuwaomba kura katika Uchaguzi huo.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Kwaruhombo,leo Machi 16,2014.Ridhiwani Kikwete ameahidi kuyashughulikia Matatizo mbali mbali wanayokabiliana nayo Wananchi wote wa Jimbo la Chalinze,yakiwemo ya Barabara,Maji,Elimu,Matibabu na mengine mengi ambapo amesema atayafanyia kazi atakapopewa ridhaa ya kuwa kiongozi wa Wanachalinze.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kulia) akimsikiliza kwa makini Mlemavu wa miguu,Hamis Ibrahim Mkazi wa Kijiji cha Kwarihombo,ambaye alikuwa akimuomba Mgombea huyo msaada wa kupatiwa Baiskeli ya kulembelea kutokana na kwamba aliyonayo imechoka sana.Ridhiwani ameahidi kumpelekea Baiskeli mpya ya kutembelea Mlemavu huyo.
  Mgombea Ubunge kwa tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) na Meneja wa Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze (CCM),Steven Kazidi wakiangalia maendeleo ya ujenzi wa Daraja dogo katika Kijiji cha Chang'ombe,linalounganisha Barabara inayotoka Kwarihombo kupitia Kwamsanja mpaka Kibindu,Kata ya Kibindu,ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 16,2014.


  0 0


  0 0

  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akitizama sehemu ya mbele ya kiwanda cha kutengenezea Konyagi feki ambapo muonekano wake ni maduka na saloon.
  Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akitembelea sehemu ya nyuma ya kiwanda cha kutengeneza Konyagi feki katika eneo la kambi ya raha Bomang'ombe wilayani Hai.
  Sehemu ya bidhaa zilizokamatwa katika kiwanda hicho zikiwa kituo cha polisi Bomang'ombe.
  Kamanda wa Polisi mkoa wa Kilimanjaro Robert Boaz akionesha Pombe feki ya Konyagi  iliyokamatwa hivi karibuni wilayani Hai
  Kamanda Boaz akiwa ameshikilia sehemu ya malighafi zinazotumika kutengezea Konyagi Feki.
  Kamanda Boaz akionesha mihuri ambayo imekuwa ikitumika kuonesha tarehe ya kuanza na kumalizika kwa tarehe ya matumizi ya kinywaji hicho.
  Kamanda Boaz akitizama Ndoo kubwa maarufu kama Diaba ambayo yamekuwa yakitumika kuchuja pombe hiyo kabla ya kuwekwa katika karatasi maalum.
  Hivi ndivyo inavyoonekana pombe hiyo ikiwa na alama ya TRA.
  Baadhi ya watuhumiwa waliokamatwa baada ya kukutwa wakifanya shughuli ya utengenezaji wa bidhaa hiyo feki.
  ------------------------------
  Na Dixon Busagaga wa
   Globu ya Jamii, Moshi
  JESHI la polisi mkoani Kilimanjaro limefanikiwa kunasa kiwanda cha
  kutengeneza Pombe "Feki" aina ya Konyagi huku likiwashikilia watu nane
  waliokutwa ndani ya kiwanda hicho wakifanya shughuli ya utengenezaji
  wa pombe hiyo.

  Mbali na kiwanda na watuhumiwa hao pia Polisi imefanikiwa kunasa
  mitambo mbalimbali iliyokuwa ikitumika kiwandani hapo zikiwemo
  malighafi zilizokuwa zikitumika kufunga bidhaa hizo kabla ya kuuzwa
  katika maduka ya jumla ya kuuzia Pombe.

  Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro,kamishana mwandamizi msaidizi wa polisi,Robert Boaz alithibitisha kukamatwa kwa watuhumiwa hao Machi 14 mwaka huu majira ya saa 7:00 Mchana katika eneo la Kambi ya raha nje kidogo ya mji wa Bomang'ombe.

   "Askari polisi walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hawa baada ya
  wananchi kutoa taarifa za kuwepo kwa utengezaji wa Pombe ambayo
  haijaruhusiwa kisheria ikiwa na nembo ya Konyagi ndipo askari walianza
  uchunguzi na kufanikiwa kuwakamata watu hao katika nyumba
  inayomilikiwa na Elias Samson  mwenye umri wa miaka 31"alisema Boaz.

  Kamanda Boaz alisema watuhummiwa hao pia walikutwa na lita 400 za
  pombe ikiwa imehifadhiwa katika mapipa tayari kwa ajili ya kujazwa
  katika vifungashio pamoja na Katoni 46 za pombe hiyo zote zikiwa na
  nembo ya Konyagi.

  Mbali na vitu hivyo Boaz pia alisema watu hao walikutwa na Makasha
  tupu 178 ya kuhifadhi Konyagi yakiwa na nembo ,Pipa tupu 10
  zinazoaminika kuhifadhia pombe hiyo wakati wa utengenezaji na Mihuri
  miwili inayoonesha tarehe ya kutengezea na taraehe ya mwisho wa
  matumizi ya bidhaa .

  "Katika vitu vingine tulivyo wakuta navyo ni pamoja na majiko ya
  mafuta "Ya Mchina"zaidi ya matano,vifaa vingine ambavyo ni kama Pasi
  vilivyokuwa vikitumika kwa ajili ya kuchomea karatasi za nailoni baada
  ya kujaza hiyo Pombe"alisema Boaz.

  Kamanda Boaz aliyetembelea eneo kilipokuwepo kiwanda hicho aliwataja
  waliokamatwa kuwa ni pamoja na George Kisivani (28), Yusuf George
  (33), Preygod Urassa (27) na Richard Leonard (35) Hagai Nelson (38),
  Jackson Shayo (29), Greyson Jonathan (27) wote wakazi wa Arusha pamoja na Mohamed Rashidi (44) mkazi wa Dar es Salaam.

  Makasha na vifungashio
  vyakutwa na alama ya TBS na TRA.

  Katika hali isiyo ya kawaida Makasha ya bidhaa hiyo Feki yamekutwa
  yakiwa na alama ya Ubora itolewayo na shirika la viwango Tanzania
  ,(TBS) huku karatasi zenye Pombe zikiwa zimebandikwa karatasi
  inayotumiwa na mamlaka ya mapato nchini (TRA).

  Kamanda Boaz alisema uwepo wa alama hizo mbili ni kutaka kumuaminisha mnunuzi pamoja na mtumiaji wa bidhaa hiyo kuwa ni halali na imethibitishwa na taasisi hizo mbili muhimu zinazosimamia Ubora wa bidhaa pamoja na mapato.

  Alisema uchunguzi wa kina unafanyika ili kubaini watengezaji wa
  Makasha hayo,pamoja upatikanaji wa alama hizo za TRA huku akiongeza
  kuwa mbali na kosa hilo la kutengeneza bidhaa bandia pia watu hao
  wanashiriki katika kuhujumu Uchumi wa nchi.

   "Huu ni uhujumu Uchumi kwa sababu wametengeneza bidhaa feki ,harafu
  wanaziuza madukani bila ya kulipia kodi,wakiwaaminisha wauzaji wengine na watumiaji kuwa bidhaa yao imethibitishwa na TBS na wanalipa kodi kwa kuweka alama ya TRA"alisema Boaz.

  Kutokana na hali hiyo kamanda Boaz alisema tayari amefanya mawasliano na Uongozi wa shirika la viwango Tanzania (TBS) pamoja na mamlaka ya mapato nchni (TRA) ili kuondoa utata uliopo hku akiongeza haja ya kutolewa kwa elimu ili kuzuia athari za matumizi ya bidhaa zisizokuwa na ubora.

  0 0  0 0

   Na Abdulaziz Video, Kilwa
  Moto umeteketeza nyumba anayoishi mkuu wa wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, Mhe. Abdallah Ulega na kusababisha hasara kubwa ambayo idadi yake haijaweza kufahamika mara moja. 
   Habari kutoka wilayani humo na kuthibitishwa na Katibu tawala wa mkoa wa Lindi  Bw. Abdala Chikota alisema kwamba moto huo umeteketeza vifaa mbalimbali  ndani ya nyumba ya kiongozi huyo. 
   Bw. Chikota alisema moto huo umesababisha hasara kubwa. 
   Alisema kufuatia tukio hilo ofisi ya mkuu wa mkoa imetoa fedha Shilingi laki tano 500.000 pamoja na chakula kama mchele, unga sukari, mafuta ya kula pamoja na maharage ili kumsaidia DC huyo  katika kipindi hiki cha majonzi wakati  utaratibu mwingine wa kutatua tatizo la makazi yake ukifanyiwa kazi.
  Mkuu wa wilaya huyo, Mhe. Ulega, alisema kuwa vitu vichache tu ndiyo vimeweza kuokolewa, ambavyo vilikuwa rahisi kuchukuliwa ikiweno begi la nguo na nyaraka zake, na kwamba kwa sasa atalazimika kuishi katika jengo la Hostel. 
   Mhe. Ulega ameshukuru  juhudi za wananchi ambazo zimesaidia kuokoa vitu vichache, vikiwemo seti ya makochi, magodolo matatu na kitanda kimoja cha mbao
  Amesema wakati nyumba yake ilipokuwa ikiungua, familia yake akiwemo mke alikuwa safarini na amerejea leo mchana.
    Kwa upande wake kamanda wa polisi Regnal Mzinga amethibitiasha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa uchunguzi unafanyika ili kubaini chanzo cha moto huyo
  mkuu wa wilaya ya Kilwa, mkoani Lindi, Mhe. Abdallah Ulega (mwenye tracksuit ya bluu) na majirani wakiwa nje ya nyumba yake iliyoteketea kwa moto asubuhi ya leo
  Sehemu ya uani mwa nyumba hiyo
  Sehemu ya ndani
  Nyumba hiyo kwa mbele
  Sehemu ya ndani ya nyumba hiyo

older | 1 | .... | 389 | 390 | (Page 391) | 392 | 393 | .... | 3278 | newer