Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live

KUTOKA SHIRIKISHO LA SOKA NCHINI (TFF) LEO


LUGUMI ENTERPRISES LTD YAKABIDHI PAMPU YA MAJI NA SHILINGI MILIONI 10 KUKAMILISHA UJENZI WA NYUMBA YA WALIMU MAGU SEKONDARI MAGU.

$
0
0
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kushoto) ambaye alimwakilisha Mkurugenzi wake Bw. Said Lugumi, kukabidhi msaada wa Pump ya maji inayotumia umeme na fedha taslimu shilingi milioni kumi kwa Afisa Elimu Takwimu (W) Sekondari bw. John M. Mangu  katika makabidhiano yaliyofanyika viwanja vya shule ya Sekondari ya Magu.
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe akizungumza na wanafunzi wa Shule ya sekondari Magu wakati wa makabidhiano ya msaada wa pumpu ya maji inayotumia umeme pamoja na fedha taslimu shilingi  milioni kumi kwaajili ya kukamilisha nyumba ya walimu.
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kulia) akiwaongoza wanafunzi wa Magu Secondary kushusha vifaa vya pump ya maji inayotumia umeme ikiwa ni sehemu ya msaada alioukabidhi jana kwa shule hiyo.
Meneja wa Kanda ya Ziwa Kampuni ya Lugumi Enterprises LTD inayomiliki makampui ya Ran IT Solutions (EA) LTD na KZ Securty, Eligod Justine Sangawe (kulia) akiwaongoza wanafunzi wa Magu Secondary kushusha pump ya maji inayotumia umeme ikiwa ni sehemu ya msaada alioukabidhi jana kwa shule hiyo kutimiza ahadi iliyowekwa mwaka jana kwenye maafali ya 24 ya wahitimu wa kidato cha nne na Mkurugenzi wake Bw. Said Lugumi.
Hili ni sehemu ya kusanyiko la baadhi ya wanafunzi wa Shule ya sekondari Magu waliohudhuria makabidhiano hayo. 

TASWIRA MBALI MBALI KUTOKA BUNGE LA KATIBA MJINI DODOMA LEO

$
0
0
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, William Lukuvi (kulia) akizungumza , Anna Abdallah (katikati) na Tundu Lisu wakizungumza , Bungeni Mjini Dodoma Machi 11, 2014.
Wabunge wa Bunge Maalum la Katiba Kabwe Zitto na Ibrahim Lipumba wakiteta Bungeni Mjini Dodoma Machi 12, 2014.
Mwenyekiti wa Muda wa Bunge Maalum la Katiba, Pandu Kificho akiongozwa kutoka kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma Machi 12, 2014 bada ya kuahirisha Bunge hilo.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Mjumbe wa Bunge maalum la katiba na naibu Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuzi, Kaika Telele, Bungeni Mjini Dodoma Machi 12, 2014.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Mahakama yawarusu kwenda kutibiwa nje ya nchi Mawaziri Waandamizi wa zamani,Basil Mramba na Daniel Yona

$
0
0
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, imewaruhusu kwenda kutibiwa nje ya nchi  Mawaziri Waandamizi wa zamani,  Basil Mramba na Daniel Yona wanaokabiliwa na tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh. bilioni 11.7  kwa kutoa msamaha wa kodi baada ya kusikiliza maombi yao leo.

Uamuzi huo umetolewa leo mahakamani hapo na Jaji John Utamwa baada ya washtakiwa hao kuwasilisha maombi ya kwenda kutibiwa nje ya nchi.

Upande wa Jamhuri ulidai kuwa hauna pingamizi na maombi hayo.

Jaji Utamwa alisema baada ya kusikiliza maombi hayo mahakama inawaruhusu washtakiwa kusafiri kwenda nje ya nchi kutibiwa na kwamba pamoja na ruhusa hiyo Mramba na Yona siku ya kusikiliza kesi Aprili 22, mwaka huu wahudhurie mahakamani.

Mbali na Mramba na Yona, mshtakiwa mwingine ni, Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.

Kesi hiyo imepangwa kusikilizwa Aprili 22 hadi 25, mwaka huu.

Katika kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.

Ilidaiwa kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation  waliingia mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha Sheria ya Manunuzi ya Umma.

TATHIMINI YA HALI YA UHALIFU MKOA WA MBEYA KWA KIPINDI CHA FEB- 2014 IKILINGANISHWA NA KIPINDI CHA MWEZI JAN- 2014

$
0
0
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,SACP Ahmed Z. Msangi

taswa fc, taswa queens kupimana ubavu na Chuo cha Dacico

$
0
0
 TIMU ya soka na netiboli ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na Taswa Queens kesho zitacheza mechi maalum za kirafiki dhidi ya Chuo Cha Uandishi wa Habari, Mawasiliano ya Umma na Utawala kijulikanacho kwa jina la Dar es Salaam City College (Dacico).

Mechi hiyo imepangwa kufanyika Kibamba, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam na maandalizi yake yamekwisha kamilika kwa mujibu wa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary.

Majuto alisema kuwa  mechi hizo zimepangwa kuanza saan 9.00 alasiri na zimeandaliwa ili kuendeleza uhusiano baina yao na chuo hicho maarufu na bora nchini.
Alisema kuwa wanatarajia kuondoka jijini saa 5.00 asubuhi na kabla ya kucheza mechi hizo, watapata fursa ya kutembelea mazingira ya chuo hicho na baadaye kuzungumza na wanafunzi na walimu.

“Tumepokea mwaliko na naamini watataka kujifunza kutoka kwetu, sisi ni waandishi wa habari ambao tupo tayari kazini na pale kuna wanafunzi ambao wanataka kuja kufanya kazi tunayofanya sisi, hivyo hii ni ziara muhimu sana mbali ya kucheza michezo,” alisema Majuto.

Alisema kuwa kocha mkuu wa timu ya soka, Ali Mkongwe na msimamizi wa timu ya netiboli, Sharifa Mustapha waliendesha mafunzo mazuri kwa wachezaji kwenye mazoezi na lengo kubwa ni kupata ushindi.

Mkurugenzi wa Dacico, Idrisa Mziray alisema kuwa wamejiandaa vyema kwa ajili ya mechi hizo na lengo kubwa ni kuongeza mtandao wa chuo chao ambacho kina matawi handi mikoani. Mziray alisema kuwa wanafunzi wao wa tawi la Mbeya nao wamefika kwa ajili ya ziara hiyo na kuonyesha uwezo wao katika michezo.

“Tupo tayari kwa ajili ya mechi hizo, tunajua Taswa FC na Taswa Queens ni timu nzuri nah ii imetokana na kufanya vyema katika mechi zao mbali mbali, tupo tayari kwa changamoto,” alisema Mziray.

Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe Angellah Kairuki na mmiliki wa Bongo5 wachaguliwa kuwa miongoni mwa viongozi vijana duniani ‘Young Global Leaders 2014

$
0
0
 Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Mhe.Angellah Kairuki  (kushoto) pamoja na Mwanzilishi na Mwenyekiti Mtendaji (CEO) wa Bongo5 Media Group na Jefag Logistics Tanzania Ltd, Luca Neghesti (chini) wameteuliwa kuwa miongoni mwa viongozi vijana duniani, ‘Young Global Leaders 2014’ 
 Watanzania hao wawili wameingia kwenye jopo hilo ambalo mwaka huu linaundwa na vijana 214 kutoka nchi 66 duniani kutoka serikalini na makampuni binafsi. 
Mwaka huu Afrika ina wawakilishi 19 peke yake. 
 Idadi hiyo imepatikana kufuatia maombi kutoka kwa watu zaidi ya 5,000 waliopendekezwa kutoka duniani kote na hatimaye kuchaguliwa baada ya mchujo mkali na kamati maalumu iliyo chini ya uenyekiti wa Malkia wa Jordan, Rania Al Abdullah. 
 Young global leaders ni vijana chini ya miaka 40 wanaosifika kwa michango yao katika jamii na pia ni viongozi wadogo kwenye maeneo yao ya kazi na wameweza kufikia uongozi ndani ya muda mfupi na pia kutokana na Ustawi wao wa kijasiriamali. 
Neghesti amepata nafasi hiyo kutokana na mafanikio ya kiujasiriamali kupitia Bongo5 Media Group, KINU na JEFAG logistics na DICD (Dar es salaam Inland Container Depot). 
 Watanzania wengine waliowahi kuchaguliwa kwenye jopo hilo ni pamoja na January Makamba, Mohammed Dewji, Elsie Kanza, Lawrence Masha na Susan Mashibe.

CHANZO: http://www.weforum.org/news/19-young-global-leaders-africa-recognized-world-economic-forum

elimu kwa umma juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi ili kulinda tabaka la Ozoni.

$
0
0
 Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete akitoa hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Mafunzo ya wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi Nchini katika Hotel ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete (Katikati) na Mkurugenzi wa mazingira Dkt. Julius Ningu (Kulia) wakimsilikiza Bw. Julio Esterban Mshauri Mwelekezi kutoka UNIDO akitoa ufananuzi kwa wakufunzi kutoka Vyuo vya ufundi nchini.
 Sehemu ya washiriki wa warsha wakifatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa mgeni rasmi.
Washiriki wa Mafunzo wakiwa katika picha ya Pamoja na Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais Eng. Angelina Madete watatu kutoka kulia mara baada ya ufunguzi wa warsha.
--
 Na Lulu Mussa na Rashda Swedi,
Ofisi ya Makamu wa Rais

Serikali inaendelea na jitihada za kutoa elimu kwa umma juu ya njia bora za kuhudumia majokofu na viyoyozi ili kulinda tabaka la Ozoni.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es Salaam na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Eng. Angelina Madete wakati wa ufunguzi wa Warsha ya Mafunzo kwa Wakufunzi kutoka Vyuo mbalimbali vya Ufundi nchini.


Katika Hotuba yake Bi Madete amesema kuwa kemikali haribifu zinauwezo mkubwa kuharibu tabaka la Ozoni na kuongeza joto angani. Kutokana na sababu hizo, Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na jamii za kimataifa zimekubaliana kufanya jitihada za kuondoa kemikali  hizo hatarishi.

Bi Madete ameainisha baadhi ya kemikali hizo kuwa ni methyl bromide,halons na chloroflorocarborns ambazo hutumika kama vipozi katika majokofu, viyoyozi, vifaa vya  kuzima moto, usafishaji chuma, ufukizaji wa mazao katika maghala na utengenezaji wa magodoro ambazo huleta madhara kwa tabaka la ozoni na adhari zake hutokea kwa binadamu, mimea na viumbe hai.

Katika awamu ya kwanza, Tanzania imefanikiwa kuondoka tani  296 za kemikali hizo haribifu ikiwa ni utekelezaji wa Mkataba wa Montreal na Vienna ambayo Tanzania iliridhia mwaka 1993.
Aidha, Bi Madete ameyataja madhara yatokanayo na uharibifu wa Tabaka la Ozoni kuwa ni kuongezeka kwa magonjwa ya saratani ya ngozi,uharibifu wa macho maarufu mtoto wa jicho, na upungufu wa uwezo wa mwili kujikinga na maradhi.  Athari hizi kwa kiasi kikubwa zinatokana na shughuli za kibinadamu kama vile matumizi ya kemikali haribifu na zisizo rafiki kwa mazingira. 
Warsha hii ya siku mbili imeratibiwa na Ofisi ya Makamu wa Rais na inajumuisha wakufunzi kutoka Vyuo vya Ufundi vya Zanzibar na Mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Kigoma, Mbeya na Mwanza. 

Mh. Stephen Wasira na Mh. Augustino Lytonga Mrema wazungumzia Umuhimu wa Muungano

Taarifa Kutoka Maisha Plus Mama shujaa

$
0
0


Tunawaomba RADHI kutokana na kutoonekana kwa vipindi vyetu hewani kuanzi Jumamosi tarehe 8. Hii imetokana na sisi Kama waandaaji kuwaomba TBC KUSITISHA kurusha vipindi.


Kipindi cha kwanza kilirushwa saa 4.20 usiku, cha pili kikarushwa saa 4.50 usiku, cha tatu kikarushwa saa 3 usiku na cha nne (cha jumamosi) HAKIKURUSHWA KABISA!

Kwa kuwa jambo hili linahusisha makubaliano, tunaomba muwe na subira wakati tukirekebisha mambo ili muweze kuitazama Maisha Plus SEHEMU na muda UNAOELEWEKA ndani ya siku chache zijazo.

Tunawaomba RADHI kwa usumbufu wowote uliojitokeza.
 


Imetolewa na Uongozi
dMb Co. Ltd

Taarifa ya Maendeleo ya Msiba, New York

$
0
0
Kama mlivyofahamishwa awali Mtanzania mwenzetu Mama Lulu John Maro Mwaluko (pichani) amefariki dunia asubuhi ya siku ya Ijumaa tarehe 7 Machi 2014. 
Mama Mwaluko alikuwa akikaa Queens, New York,  na alishawahi kuwa mwalimu na alifundisha high school hapa New York.  
Mama Mwaluko alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani yaani kansa. Alikuwa akitibiwa huko katika hospitali ya Calvary huko Bronx, New York.
Michango yenu kwa ajili ya kufanikisha shughuli za msiba huu itumwe kwenye akaunti ifuatayo:
Bank: Citibank
Routing Number: 021000089
Account Number: 02472079
Bank Address: Citibank, Jamaica 89-50 164th St, Jamaica, NY 11432.
Jina la Account: Nanna Mwaluko na Helen Mwaluko.
Mama Mwaluko alishawahi kukaa na Marehemu mumewe China na Marekani kama Wanadiplomasia na alishastaafu kufundisha mwaka 2012 na kabla ya kufariki alikuwa mbioni kurejea Tanzania. 
Mama Mwaluko atakumbukwa na familia yake kama mama, dada, shangazi, mwalimu, mcha Mungu na mama mwenye busara. Katika kuomboleza msiba wa Mama Mwaluko, Watanzania wote tunaombwa kuifariji familia yake na ndugu zake kwa kujumuika nao katika sala na michango katika wakati huu mgumu wa maombolezo. 
Mnaweza kuwasiliana na Emma Kasiga kwa simu namba 612-229-4050 na Nanna Mwaluko kwa simu namba 347-693-6129 na Camelot Funeral Home kwa simu namba 914-664-8500. Taarifa zaidi za msiba huu zitafuata baadae.
 Siku ya Jumatano itakuwa ni siku ya kuaga mwili wa Marehemu kuanzia saa tisa na nusu hadi saa mbili za usiku pale Camelot Funeral Home. Anwani ni: 
Camelot Funeral Home, 
174 Stephens Avenue, 
Mount Vernon, 
New York, 10550. 
Wote mnaombwa kufika kumuaga 
Mama  Lulu John Maro Mwaluko na kuifajiri familia yake.
Imetolewa na Uongozi -  Jumuiya ya Watanzania New York.
Mwenyezi Mungu aiweke roho ya 
Marehemu mahali pema peponi. 
Amina.

MGAHAWA WA KISASA KUFUNGULIWA HIVI KARIBUNI WASHINGTON DC

$
0
0
NAFASI ZA KAZI KUTANGAZWA SOON, TEGA SIKIO
COOKS
SERVERS
BUSBOYS
MANAGER
GET YOUR RESUME READY
THE BEST EAST AFRICAN CUISINE IN NORTH AMERICA

BENDI PENDWA TWANGA PEPETA ZIARANI NYANDA ZA JUU.

$
0
0
 Bendi pendwa ya African Stars “Twanga Pepeta” mwishoni mwa mwezi huu itafanya ziara ndefu ya maonyesho katika mikoa ya nyanda za juu kusini. 
 Twanga Pepeta itaanzia ziara yake NJOMBE siku ya Jumatano tarehe 26-03-2014 katika ukumbi wa Turbo.
 Siku inayofuata tarehe 27-03-2014 siku ya Alhamisi kwa mara ya kwanza kabisa watakuwa Wilaya mpya ya MBABABAY katika ukumbi wa BAY LIVE SOCIAL HALL. 
 Ziara ya Twanga Pepeta siku ya Ijumaa tarehe 28-03-2014 itahamia Songea mjini katika ukumbi wa Serengeti. 
Siku ya Jumamosi tarehe 29-03-2014 itakuwa ni zamu ya Jiji la Mbeya katika ukumbi wa City Pub. Maandalizi ya ziara yanaendelea vizuri na Twanga Pepeta imejitayarisha vilivyo kukonga nyoyo za mashabiki watakaojitokeza katika maonyesho yake. 
 Twanga Pepeta itatumia ziara hii kuitangaza albamu yake mpya ya Nyumbani ni Nyumbani pamoja na kupiga nyimbo zilizopo kwenye albamu zake 12.

To Fellows, Associates, Graduates and Students in Tanzania

Mfumo wa E-Warranty wawasaidia wateja wa Samsung kishinda zawadi mabalimali

$
0
0
Mhasibu mkuu wa Samsung Tanzania Bw. Ibrahim Kombo (Kulia) akikabidi zawadi kwa mshindi wa mwezi Januari wa huduma ya e-warranty Bw. Sherali Faril wakati wa hafla fupi yya makabidhiano ya zawadi mbalimbali kwa wateja waliojishindia bidhaa za Samsung kwa droo ya mwezi Januari baada ya kununua simu halisi ya Samsung.
Baadhi ya washindi wa Samsung e-warranty katika picha ya pamoja na Mhasibu Mkuu wa Samsung Tanzania Bw. Ibrahim Kombo (wa pili toka kulia) mara baada ya tukio la kukabidhi zawadi kwa washindi hao waliojinyakulia bidhaa mbalimbali toka Samsung baada ya kununua simu halisi za Samsung na Kuzisajili katika mfumo wa e-warranty ikiwa ni njia yya kupambana na bidhaa feki.

WALIOKWAMISHA UJENZI WA MIUNDOMBINU MLOGANZILA SASA WARUHUSU UJENZI KUENDELEA

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Mecki Sadiki (kushoto) akizungumza na mkazi wa eneo la Mloganzila Bw. Fredy Justine Masondole (kulia) ambaye aliweka pingamizi kuzuia miundombinu ya maji, umeme na barabara kupita katika eneo lake , Hata hivyo mkazi huyo aliruhusu ujenzi kuendelea baada ya mazungumzo ya kupatikana kwa muafaka kufikiwa. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Mhandisi Felchian Mramba.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mh. Saidi Mecki Sadiki (katikati) akizungumza jambo wakati alipotembelea eneo la ujenzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS) lililo kwenye mpaka wa wilaya ya Kisarawe na mkoa wa Pwani leo.Wengine kutoka kushoto ni Katibu Tawala wa mkoa wa Dar es salaam Bi.Therezia Mmbando,Mkurugenzi Mkuu wa DAWASA Bw. Archard Mutalemwa na Meneja wa Tanroad mkoa wa Dar es salaam Bw. Ndyamukana Julius.
Mkazi wa eneo la Mloganzila Bw. Fredy Justine Masondole (Katikati) akiwapeleka katika eneo la nyumba yake lenye mgogoro viongozi wa mkoa wa Dar es salaam wakiongozwa na Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Saidi Mceki Sadiki (upande wa nyuma katikati), mkuu wa wilaya ya Kinondoni Jordan Lugimbana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es salaam Bi. Theresia Mmbando.
Mafudi wakiendelea na ujenzi wa awali wa ofisi za muda katika eneo itakapojengwa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi cha Muhimbili(MUHAS) lililo kwenye mpaka wa wilaya ya Kisarawe na mkoa wa Pwani leo Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.

mshkaki

JK APOKEA MSAADA WA MAGARI 11 YA KUKABILIANA NA UJANGILI LEO

$
0
0

Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake kushukuru msaada magari 11 ulioyatolewa na Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti, Selous na Maswa.
Rais Jakaya Kikwete wa pili kushoto akipata maelezo kuhusu msaada wa magari 11 kutoka kwa Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir (katikati)na kulia ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti Selous na Maswa.Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir(katikati) akitoa hotuba yake kuhusu msaada magari 11 waliyoyatoa kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti ,Selous na Maswa,kushoto wa pili ni Rais Jakaya Kikwete na wa kwanza ni Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel na kulia wa pili Waziri wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu.Rais Jakaya Kikwete wa pili kushoto akionesha moja ya ufunguo wa msaada wa magari 11 mara baada ya kukabidhiwa na Mkurugenzi wa Frankfurt Zoological Society (FZS) kanda ya Afrika, Robert Muir ( kulia wanne) katika hafla iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Msaada huo umetolewa na FZS kwa ajili ya kupambana na vitendo vya ujangili katika hifadhi za Serengeti ,Selous na Maswa.Balozi wa Ujerumani nchini Hans Koeppel akizungumza jamabo wakati wa hafla hiyo iliyofanyika leo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na Magreth Kinabo -MAELEZO

polisi mkoani katavi wakamata mtu akiwa na meno ya tembo na gobole

$
0
0
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Katiavi Afande Dhahiri Kidavashari akionesha meno ya tembo vipande 2 yenye thamani ya shilingi 22  aliyokamatwa nayo mtuhumiwa Bathoromeo Mtongwa Machi 8, 2014 katika kijiji cha Kilida, tarafa ya Mamba wilaya ya Mlele ambapo pia mtuhumiwa huyo alikamatwa na gobole 1 na risasi 14.
Mkaazi wa kijiji cha Kilida tarafa ya mamba wilaya ya mlele Bathoromeo Mtongwa (58) akiwa katika kituo cha polisi cha mkoa wa Katavi baada ya kukamatwa na meno mawili ya tembo yenye uzito wa kilo 15 yenye thamani ya shilingi milioni 22 na gobole moja pamoja na risasi 14. 
-------------------------
Na Walter Mguluchuma, 
Mpanda, Katavi
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Bathoromeo James Mtongwa mkaazi  wa Kijiji cha Kilinda Tarafa ya Mamba Wilaya ya Mlele Mkoa wa Katavi amekamatwa akiwa na vipande viwili vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 15 vyenye thamani ya shilingi milioni 22 pamoja na bunduki moja aina ya Gobore na Risasi 14
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Mkoa wa Katavi Kamishna mwandamizi msaidizi  Dhahiri Kidavashari.  mtuhumiwa huyo alikamatwa Machi 7, mwaka huu majira ya saa mbili na nusu usiku.
Alisema mtuhumiwa alikamatwa kufuatia taarifa toka kwa raia wema ambazo ambazo zililifikia jeshi la polisi pamoja na askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi kuwa mtuhumiwa anamiliki nyara za Serikali kinyume cha sheria.
Alifafanua  siku hiyo ya tukio majira ya saa mbili usiku polisi wakiwa na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi walifika kwenye kijiji hicho cha Kilinda nyumbani kwa mtuhumiwa Bathoromeo na kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa na kufanikiwa kukamata risasi 14.
Kamanda Kidavashari alieleza wakati askari hao wakiendelea na upekuzi kwa kushirikiana na uongozi wa kijiji walilitilia shaka eneo moja la nyumba hiyo ya mtuhumiwa kutokana na eneo hilo kuonekana kuwa limechimbwa hivi karibuni.
Alisema  askari walipoamua kuchimba eneo hilo na baada ya kufukua kwa kitambo kidogo walifanikiwa kukuta meno ya Tembo vipande hivyo vya meno ya tembo vikiwa vimefukiwa ardhini hapo.
Baada ya kukamatwa kwa maneno hayo ya Tembo polisi walianza kumhoji mshitakiwa kwa kumtaka awaelekeze sehemu ambayo amekuwa akihifadhi Silaha ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya ujangili
Kamanda Kidavashari alieleza baada ya mahojiano mtuhumiwa aliweza kueleza kuwa bunduki ambayo amekuwa akiitumia kwenye matukio ya ujangili ameificha eneo linaloitwa King’anda lililopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Katavi.
Alisema mnamo Mnamo Machi 8, 2014 majira ya saa nane mchana mtuhumiwa aliwaongoza Askari Polisi na Askari wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi hadi eneo la King’anda  na kuwaonyesha silaha hiyo  kwenye kichaka.
Mtuhumiwa anatarajiwa kufikishwa Mahakamani wakati wowote mara baada ya upelelezi wa tukio hili utakapokamilika mapema iwezekanavyo.
Pia jeshi la polisi Mkoa wa Katavi lanatowa wito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi kwa kutowa taarifa za watu wanaojihusisha na uwindaji haramu wa rasilimali za Taifa ili kulinda na kuhifadhi rasilimali zetu kwa manufaa ya vizazi vijavyo.

watano wachukua fomu kugombea ubunge jimbo la chalinze

$
0
0

Jumla ya wagombea watano wamechukua fomu za kuwania Kiti cha Ubunge katika Jimbo la Chalinze, Bagamoyo, 
Zoezi  litafungwa rasmi tarehe 12 Machi 2014 saa kumi kamili alasiri, kwa mujibu wa taarifa ya Afisa Uchaguzi wa Jimbo la Bagamoyo, David Shija.

Wagombea hao ni:-

  1. Mathayo Torongey (CHADEMA)
  2. Phabian Skauki wa (CUF)
  3. Vuniru Hussein (NRA) 
  4. Ramadhan Mgaya (ASP) 
  5. Ridhiwani Kikwete (CCM)
Viewing all 110017 articles
Browse latest View live




Latest Images