Quantcast
Channel: MICHUZI BLOG
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live

KAMATI ZA TROIKA ZA MABALOZI WA AFRIKA, KARIBIANI, PACIFIC NA JUMUIYA YA ULAYA ZAKUTANA

$
0
0
 Balozi wa Tanzania Jumuiya ya Ulaya na Mwenyekiti wa Kamati ya Mabalozi wa Afrika, Karibiani na Pacific (ACP) Dr. Diodorus Buberwa Kamala ( mwenye tai yenye rangi za bendera ya taifa) akiwa katika picha ya pamoja na  Wajumbe wa   kamati za Troika za Mabalozi wa ACP na Jumuiya ya Ulaya. Kamati hizo zimekutana leo Brussels kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha ushirikiano wa ACP na Jumuiya ya Ulaya. Kulia kwa Balozi Kamala, ni Balozi Mhe. Dimitrious Touloupas Mwenyekiti wa Mabalozi wa Jumuiya ya Ulaya na Mwakilishi wa Ugiriki  katika Kamati ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Ulaya.

WAZAZI MKOANI RUVUMA WATAKIWA KUTOWAFICHA WATOTO VIZIWI.

$
0
0
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Said Thabit Mwambungu amewataka wazazi wenye watoto walemavu wa kusikia (Viziwi) kutowaficha ndani badala yake watoe taarifa kwa viongozi wa serikali za vijiji na mitaa ili wasaidiwe kupatiwa huduma muhimu ya elimu. 
Ametoa wito huo leo wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha Viziwi mkoa (CHAVITA) ambapo amewahakikishia kuwa serikali inathamini na kuwatambua viziwi kuwa ni kundi maalum katika jamii linalohitaji elimu maalum Ameongeza kusema kuwa huduma zote anazohitaji binadamu pia zinahitajiwa na watu wenye ulemavu wa kusikia na kusema kwani hayakuwa matashi yao kutaka ulemavu huo.
“Ulemavu wa kutokusikia au kutokuzungumza si laana kwani tatizo hili linaweza kumpata mtu yeyote yule” alisema Mwambungu.
Amewasihi wazazi na walezi wote mkoani Ruvuma kuwapeleka shule watoto viziwi kwani elimu husika kwa wasiosikia au kuzungumza ipo na inatolewa bure katika shule maalum za umma. Ameitaja shule maalum kwa viziwi ya Ruhuwiko iliyopo Songea Manispaa kama mfano wa shule zinazotoa elimu wa watoto wasioosikia na kuzungumza hivyo ni vema sasa wananchi wakawapeleka watoto kupata ujuzi na maarifa yatakayowasaidia kujikimu na maisha. Mwambungu ameziagiza halmashauri zote mkoani Ruvuma kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa walimu wenye taaluma za kufundisha watu wenye ulemavu ili kusaidia kufundisha katika shule zenye watoto viziwi au wasioona ili walemavu hawa wapate mawasiliano stahiki. 
Katika kusaidia jitihada za CHAVITA kujitangaza na kuunda umoja wao Mkuu wa Mkoa Mwambungu amewachangia shilingi laki nne (400,000/=) ili kutunisha mfuko wa viziwi mkoa wa Ruvuma na kuwasihi watu wenye mapenzi mema kuwasaidia walemavu wa aina zote. 
Katika risala ya CHAVITA kwa mgeni rasmi iliyosomwa na Grevas Komba wameomba suala la elimu lipewe kipaumbele kwa viziwi kwani hakuna vituo vya kutosha kwa mafunzo kwa viziwi. Pia wameomba serikali kudhamini walimu watakaosaidia kutatua tatizo la wasiosikia ili wapate wakalimani wenye ujuzi na utaalam wa mawasiliano. 
 Mkoa wa Ruvuma kwa mujibu wa takwimu za CHAVITA unao viziwi 256 waliotambulika kwa wilaya zote tano ambapo wengine hawajahesabiwa kutokana na kufichwa na wazazi na walezi wao.
 Grevas Komba na Bahati Nyoni ambaye ni Katibu wa Viziwi mkoa wa Ruvuma wakisoma risala ya viziwi kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiongea wakati alipofungua mkutano  mkuu wa mwaka wa chama cha viziwi mkoa wa Ruvuma (CHAVITA) leo katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa.Kushoto ni mwalimu Rehema Nyagawa ambaye ni mkalimani wa kujitolea 
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwa katika picha ya pamoja na wananchama wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa chama hicho hivi leo mjini Songea. Picha na habari  na  Revocatus Kassimba

msako wa nondozzzzzzz......

Lipumba, Mbatia, Mbowe na Vuai wakichangia mjadala Bungeni jioni hii

$
0
0
Busara za viongozi wa kisiasa katika  semina ya kujadili kanuni zimeokoa jahazi na kikao kuendelea salama leo jioni. 
 Mwenyekiti wa chama cha CUF na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Prof. Ibrahimu Lipumba akichangia.
 Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi na Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe.James Mbatia akichangia .
 Mwenyekiti wa chama cha CHADEMA na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe. Freeman Mbowe akichangia.
Naibu katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Tanzania Visiwani  na mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Mhe.,Vuai Ali Vuai akichangia upatikanajoi wa mwafaka wakati wa kujadili rasimu ya kanuni leo jioni. Picha na Deusdedit Moshi wa Globu ya Jamii.

Kombe la dunia lazinduliwa Paris

raha ya vijijini...

$
0
0
 Raha ya vijijini ni chakula fresh kutoka shambani. Hapo juu Ankal akiwa Kiwira akiburudika na 'mabifu', na chini  akitoka shambani  kuchuma miwa huko Tukuyu, mkoani Mbeya

Ubongo Kids Webisode 5 - Umoja ni Nguvu

Watanzania Waaswa Kujihadhari na Ugonjwa wa Figo

$
0
0
Na Lorietha Laurence-Maelezo

Asilimia 1.03 ya vifo hutokana na ugonjwa wa figo, hayo yalisemwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii  Seif Rashidi alipokuwa akitoa tamko kwa waandishi wa habari  leo jijini Dar es salaam,kuhusu siku ya afya ya figo itakayoadhimishwa  tarehe 13 Machi,mwaka huu mjini Dodoma.

 Kauli mbiu ya maadhimisho hayo “Figo huzeeka, kadiri mtu anavyozeeka. Jali Afya ya Figo zako”. Lengo ni  kuelimisha  jamii ili iweze kuelewa umuhimu wa  figo katika   mwili, watu kubadili staili za maisha, kuhamasisha  watoa huduma kuhusu wajibu wao katika kugundua magonjwa ya figo na kupunguza hali hatarishi za ugonjwa sugu wa figo na kuandaa mikakati madhubuti ya kukinga na kuthibiti magonjwa ya figo.

“ Nawasihi watu wawe na taratibu za kufanya vipimo mara kwa mara, pia kujali afya zao kwa kuwekeza katika maendeleo ya afya zao ili kujikinga na ugonjwa wa figo” alisema Mhe.Rashidi .


Serikali yawaasa watanzania kuthamini na kutunza viwanja vya michezo

$
0
0
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Leonard Thadeo akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uharibifu wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Bw. Leonard Thadeo(hayupo pichani) leo jijini Dar es Salaam alipokutana nao kuzungumzia uharibifu wa miundombinu katika Uwanja wa Taifa. Picha na Frank Shija - WHVUM

wadau sereki na zainab wameremeta

$
0
0
 Wadau Sereki na Zainab wakila pozi baada ya kumeremeta hivi karibuni
 Sereki na Zainab wakifurahia siku yao ya kwanza pamoja 
Mmmmmmmwwwwwwwaaaaaaaa....

SIJAJA KUFANYA KAMPENI JIMBO LA KALENGA,NIMEKUJA KUTOA TAHADHARI TU-MAKAMU MWENYEKITI CCM, PHILIP MANGULA.

$
0
0
Makamu Mwenyekiti (BARA) wa CCM,Ndugu Philip Mangula akihutubia kwenye kumtano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Kalenga,mapema leo jioni kwenye Kata ya Kalenga-Iringa vijijini.

kama ulikosa kuona tuzo za oscars mwaka huu wa 2014 hii hapa

IN TANZANIA DUAL CITIZESHIP OPPONENTS LACK DECENT ARGUMENTS.

$
0
0
                      
                                 BY MOHAMED MATOPE             
As I closely follow the debate over the constitution amendment in Dodoma, I find myself more prideful of my politicians than ever before. Though prideful, the question still remains: Why did it take so long?
Well, earlier last month, constituent assembly ware granted a power to reshape the constitution draft as well as adding issues that were left out in the previous draft.
Though the extent of that authority lacks specification, this does serve as a propellant into the right direction, given it provides a possibility of inclusion of a dual citizenship clause.
My stance on this issue should not be mistaken, winning the political battle over dual citizenship is immensely important to me. As a Diaspora’s member and a person who believes in progressive values, this debate attests that our country is slowly, but assuredly, advancing toward equal human rights.I would much rather have the referendum passed in 2014 than never have it passed at all. 
I also understand that it has faced a pretty staunch political fight up until this point, but I don’t really understand why.
If one person could articulate to me a coherent reason why Tanzania should not have dual citizenship, I would surely listen to what they had to say out of pure curiosity. 
The problem is, though, that none of them have remotely convinced me of the rationality of their opposition. The first, and most common, argument I hear against dual citizenship derives its basis on the value of loyalty. That is, dual citizenship implies split loyalty and one can never be truly loyal to two countries.
This argument is always something of a convenient fiction. To begin, there are numerous benefits to our country, such as in the realm of global competitiveness, when dual citizenship is embraced. It is not an accident that many countries including, our neighbors Kenya, Uganda, Burundi and Rwanda have adopted dual citizenship laws.
In response to those claiming it is unpatriotic (uzalendo) to have more than one passport; it is, after all, unrealistic to approach a debate over the dual citizenship through the lens of nationalism. Dual citizenship should be viewed as an opportunity to take advantage of the vast talents, ualifications, skills, expertise and experiences of our unrecognized nationals in Diaspora. 
Other, more logical, arguments against dual citizenship exist, but nonetheless, are not without fault. For example, many opponents of dual citizenship claim it will lead to an influx of Tanzanians coming home to take jobs (kula huku na kule).
This argument is unfair, considering that the Tanzanians in the Diaspora have also made homes in their new countries. Some have housing payments, debts, school age children or college age children that they are still obligated to. 
Dual citizenship will mostly provide the opportunity for some Tanzanians in the Diaspora to travel home without harassment, to own home, to start a project, conduct research and above all, be able to participate in the growth of our country. 
One of the absolute worst, and irrational arguments on this issue, is that dual citizenship gives leeway for nationals in the Diaspora to take over political positions. I am astonished that this is actually being considered a pragmatic argument.  
First and foremost, these individuals need to understand that, under the dual citizenship laws Tanzania’s government will reserve its right to decide what type of restrictions it wants to impose on dual citizens.
Furthermore, many countries restrict dual citizens from running for specified offices such as the office of President and Vice-President. 
And, in some instances, other countries have established a residential requirement. 
In Nigeria, for instance, the law requires a person to live in the country for 3-10 years before he/she can qualify to run for any office. Ideologically, some people may never wish to acknowledge and accept the realities of the changing world, even in the height of fact -based evidences.
But by denying Tanzanians in the Diaspora the right to have dual citizenship, we are not only denying them a  constitution right, but also specific rights that would otherwise be guaranteed to all Tanzanians, whether it is permission to enter or leave a country, as often as they wish, or  be it purchasing a home and business.
To withhold these rights, on the basis of unsubstantiated arguments, is an affront to humanity. I commend Tanzania’s Constitution Assembly, for realizing a problem and making efforts to mend it, but why is it taking so long for the 77 percent of Tanzanians, who are in favor of dual citizenship (according to the polls) to bring the matter onto the ballots?   

 MOHAMED MATOPE IS A CONTRIBUTOR BLOGGER AND SYNDICATED COLOMNIST FOR VARIOUS AFRICA’S MAGAZINES.

NEWS FLASH: UHARIBIFU UWANJA WA TAIFA - TFF YAIOMBA RADHI SERIKALI, KULIPA HASARA ILIYOPATIKANA, YASEMA WANAOFANYA FUJO NA UHARIBIFU VIWANJANI KUKIONA

$
0
0
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) tunalaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.

Tunaiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
Uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo. 
Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Kwa mujibu wa Serikali, viti kumi viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao. 
Tumebeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa vile TFF ndiyo wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa, na ndiyo tulioomba idhidi ya kutumia uwanja huo. 
Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu.

Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi.

Boniface Wambura Mgoyo
Media and Communications Officer

Tanzania Football Federation (TFF)

NINA UCHUNGU WA KULIENDELEZA JIMBO LA KALENGA,NIPENI NAFASI TUIJENGE KALENGA YETU-GODFREY MGIMWA


KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI APOKEA MAGARI MAWILI KUTOKA KAMPUNI YA TRANSAID YA NCHINI UINGEREZA KWA AJILI YA MAFUNZO KWA VITENDO KWA WANAFUNZI WANAOSOMA KOZI YA UDEREVA KATIKA CHUO CHA TAIFA CHA USARIFISHAJI (NIT)

$
0
0
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa ofisini kwake kabla ya kupokea magari mawili ambayo yamekabidhiwa kwa chuo hicho na Shirika la Transaid la nchini Uingereza, hafla ya kukabidhi magari hayo imefanyika leo asubuhi katika viwanja vya NIT.
Taswira ya tanker trailer la futi 40 na Folk Lift ambayo yamekabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) na Kampuni ya Transaid leo asubuhi katika viwanja vya chuo hicho. Magari hayo yatasaidia wanafunzi wanaosoma kozi za udereva chuoni hapo.
Sehemu ya Wafanyakazi wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakimsikiliza Mgeni Rasmi (hayupo pichani), wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari mawili kwa ajili ya kufundishia mafunzo ya udereva chuoni hapo, magari hayo yalimekabidhiwa leo asubuhi na Shirika la Transaid la nchini Uingereza.
Mkurugenzi wa Mradi ya Usalama Barabarani wa Shirika la Transaid la Nchini Uingereza, Mr. Neil Rettie (mwenye tai ya blue) akimkabidhi funguo za gari aina ya Iveco kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka kwa ajili ya mafunzo ya Udereva yanayotolewa na Chuo Cha Taifa Cha Usafirhsaji (NIT), Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya chuo hicho leo Asubuhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt. Shaaban Mwinjaka akiwasha gari ya kuinulia mizigo focal lift kama ishara ya kupokea moja ya magari mawili yaliyokabidhiwa na Shirika la Transaid la nchini Uingereza kwa Chuo cha Taifa cha Usafirshaji (NIT), leo asubuhi. Anayeshuhudia ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Dkt. Zakaria Mganilwa
Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Dkt Shaaban Mwinjaka, akiwasha gari aina ya Folk Lift lililokabidhiwa kwa Chuo Cha Taifa Cha Usarifshaji (NIT), kwa ajili ya wanafunzi wataochukua mafunzo ya udereva chuoni hapo. Magari hayo yamekabidhiwa leo asubuhi katika viwanja vya Chuo hicho. (Picha na kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Uchukuzi)

Wimbo wa Hongera wanawake na Erica Lulakwa Gleenn

$
0
0
Muimbaji Erica Lulakwa na wimbo wa Hongera Wanawake aliyoimba kwenye sherehe za Kilele cha maadhimisho ya mwanamke Duniani, iliyoandaliwa na kundi zima la Tano Ladies siku ya Jumamosi March 8, 2014 ndani ya Ukumbi wa Hampton Inn Jijini Maryland nchini Marekani.
(Picha na Swahilivilla.blogspot.com)

WAZAZI MKOANI RUVUMA WATAKIWA KUTOWAFICHA WATOTO VIZIWI

$
0
0
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiongea wakati alipofungua mkutano  mkuu wa mwaka wa chama cha viziwi mkoa wa Ruvuma (CHAVITA) leo katika ukumbi wa Maktaba ya mkoa.Kushoto ni mwalimu Rehema Nyagawa ambaye ni mkalimani wa kujitolea.
Grevas Komba na Bahati Nyoni ambaye ni Katibu wa Viziwi mkoa wa Ruvuma wakisoma risala ya viziwi kwa mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Said Mwambungu akiwa katika picha ya pamoja na wananchama wa Chama cha Viziwi Mkoa wa Ruvuma mara baada ya kufungua mkutano wa mwaka wa chama hicho hivi leo mjini Songea.

Mkuu wa mkoa wa Ruvuma,Mh. Said Thabit Mwambungu amewataka wazazi wenye watoto walemavu wakusikia (Viziwi) kutowaficha ndani badala yake  watoe taarifa kwa viongozi wa serikali za vijiji na mitaa ili wasaidiwe kupatiwa huduma muhimu ya elimu.

Ametoa wito huo leo wakati akifungua mkutano mkuu wa mwaka wa chama cha Viziwi mkoa wa Ruvuma (CHAVITA) ambapo amewahakikishia kuwa serikali inathamini na kuwatambua viziwi kuwa ni kundi maalum katika jamii linalohitaji elimu maalum

Ameongeza kusema kuwa huduma zote anazo hitaji binadamu pia zinahitajiwa na watu wenye ulemavu wa kusikia nakusema kwani hayakuwa matash iyao kutaka ulemavu huo.

“Ulemavu wa kutokusikia au kutokuzungumza si laana kwani tatizo hili linaweza kumpata mtu yeyote yule” alisema Mwambungu

Amewasihi wazazi na walezi wote mkoani Ruvuma kuwapeleka shule watoto viziwi kwani elimu husika kwa wasio sikia au kuzungumza ipo na inatolewa bure katika shule maalum za umma.

Ameitaja shule maalum kwa viziwi ya Ruhuwiko iliyopo Songea Manispaa kama mfano wa shule zinazotoa elimu kwa watoto wasio sikia na kuzungumza hivyo ni vema sasa wananchi wakawapeleka watoto kupata ujuzi na maarifa ya takayo wasaidia kujikimu na maisha.

Mwambungu ameziagiza halmashauri zote mkoani Ruvuma kuhakikisha zinatoa kipaumbele kwa walimu wenye taaluma za kufundisha watu wenye ulemavu ili kusaidia kufundisha katika shule zenye watoto viziwi au wasioona ili walemavu hawa wapate mawasiliano stahiki.

Katika kusaidia jitihada za CHAVITA kujitangaza na kuunda umoja wao Mkuu wa Mkoa,Mh. Mwambungu amewachangia shilingi laki nne (400,000/=) ili kutunisha mfuko wa viziwi mkoa wa Ruvuma na kuwasihi watu wenye mapenzi mema kuwasaidia walemavu wa aina zote.

Katika risala ya CHAVITA kwa mgeni rasmi iliyosomwa na Grevas Komba wameomba suala la elimu lipewe kipaumbele kwa viziwi kwani hakuna vituo vya kutosha kwa mafunzo kwa viziwi.

Pia wameomba serikali kudhamini walimu watakao saidia kutatua tatizo la wasio sikia ili wapate wakalimani wenye ujuzi na utaalam wa mawasiliano.

Mkoa wa Ruvuma kwa mujibu wa takwimu za CHAVITA unao viziwi 256 walio tambulika kwa wilaya zote tano ambapo wengine hawajahesabiwa kutokana na kufichwa na wazazi na walezi wao.

MSIMAMO WA LIGI KUU YA VODACOM TANZANIA BARA 2013/2014

Tanzania-Israel Business & Investment Forum (TIBIF) 2014

$
0
0
Book your place now at the 1st Tanzania-Israel Business & Investment Forum on 17th-20th March 2014 at Julius Nyerere International Convention Centre in Dar Es Salaam. This is a unique gathering of businesspersons, investors, policymakers and industry leaders to foster bottom-up, practitioner-driven, business to business and business to government solutions for economic development.

Call +255784262001 or +255768014698 today or email us on info@kingdomleadership.ne.tz
Viewing all 110000 articles
Browse latest View live


Latest Images