Quantcast
Are you the publisher? Claim or contact us about this channel


Embed this content in your HTML

Search

Report adult content:

click to rate:

Account: (login)

More Channels


Showcase


Channel CatalogChannel Description:

Most read Swahili blog on earth

older | 1 | .... | 380 | 381 | (Page 382) | 383 | 384 | .... | 3270 | newer

  0 0  0 0

  Kikao cha semina ya wajumbe wa Bunge maalum la Katiba kilichokuwa kiendelee leo saa nne asubuhi baada ya Mwenyekiti wake wa Muda Mhe. Pandu Amir Kificho Kuaarisha jana mchana sasa kitaendelea leo tarehe 8 machi 2014 saa tisa alasiri. 

  Hii ni kutokana a kamati ya maridhiano inayopitia vifungu ilivyokuwa inafanyia kazi kuomba mda zaidi.Hivyo wajumbe wote wa Bunge maalum wanaombwa kufika Bungeni kuendelea na semina hiyo saa tisa alasiri badala ya saa nnne asubuhi.

  Imetolewa na: 
  Katibu wa Baraza la wawakiliashi 
  na 
  Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
   Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Askofu Mstaafu Donald Mtetemela akiongoza sala ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.
  Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba Sheikh Thabit Noman Jongo akiongoza  dua ndani ya ukumbi wa Bunge leo Mjini Dodoma.


  0 0
 • 03/08/14--06:49: TAWOPHA wanawake day
 •  
  Chama cha Wanawake katika Fani ya Wafamasia (TAWOPHA) kinapenda kuwatakia wanawake wote Tanzania na Duniani kote sikukuu njema ya wanawake. Wanawake tunaweza kama tukifanya kazi kwa bidii na kupeana  mawazo chanya  ili kujiletea maendeleo.

  “Chochea Mabadiliko Kuleta Usawa wa Kijinsia”.


  0 0

  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Waziri wa Maendeleo ya jamii jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba kufuatia kifo cha mwanaye Marehemu Leeford Simba huko Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa mkono wa pole na kumfariji Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba kufuatia kifo cha Mwanaye Leeford Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leedford anatarajiwa kuzikwa leo katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Neema Mathew(kulia) na waombolezaji wengine kufuatia kifo cha Mumewe Leeford Simba kilichotokea juzi. Marehemu Leeford Simba ni mtoto wa Waziri wa Maendeleo ya Jamii jinsia na Watoto Mhe.Sophia Simba.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,Mh. Benjamin Mkapa akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Leeford Simba ambaye ni Mtoto wa Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu,Mh. Benjamin Mkapa akimfariji mtoto wa Marehemu Leeford Simba ambaye ni Mtoto wa Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Mke wa Makamu wa Rais,Mama Zakhia Bilal akitoa heshima za mwisho kwa mwili wa Marehemu Leeford Simba ambaye ni Mtoto wa Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  Waziri Mkuu Mstaafu,Mh. Edward Lowassa akitoa heshima za mwisho kwa Marehemu Leeford Simba ambaye ni Mtoto wa Waziri Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto Mhe. Sophia Simba wakati wa ibada ya kumuombea marehemu iliyofanyika nyumbani kwake Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.

  Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiweka saini kwenye kitabu cha maombolezo nyumbani kwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto,Mhe. Sophia Simba kufuatia kifo cha mwanaye,Marehemu Leeford Simba,Masaki jijini Dar es Salaam leo.Marehemu Leeford Simba amezikwa jioni ya leo kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.


  0 0

  Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wameungana na Wanawake wengine kote duniani katika kusheherekea Siku ya Wanawake Duniani, iliyofanyika katika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke, jijini Dar es Salaam. Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alikuwa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Hawa Ghasia (Mb.). Kauli mbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni "CHOCHEA MABADILIKO KULETA USAWA WA KIJINSIA"
  Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa na nyuso za furaha wakati wa maadhimisho hayo.
  Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika maandamano.
   Mhe. Ghasia (wa tatu kutoka kushoto) akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Said Mecky Sadick pamoja na wageni waalikwa katika jukwaa wakiwashangilia Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa (hawapo pichani) walipokuwa wakipita mbele yao .
  Wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakipita mbele ya mgeni rasmi (hayupo pichani) wakiwa wamejawa na furaha.
  Wanawake  kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa wakiwa katika Picha ya Pamoja
  Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu, Bibi Amisa Mwakawago akiwaongoza wanawake wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirkiano wa Kimataifa kutoka uwanjani mara baada ya maadhimisho.Picha na Reginald Kisaka

  0 0
 • 03/08/14--07:49: Taarifa ya Msiba
 • Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) anasikitika kutangaza kifo cha Mfanyakazi wa Wakala Mhandisi Charles M. Madinda kilichotokea ghafla leo jumamosi tarehe 8/3/2014 katika hospitali ya Amana – Ilala Dar es Salaam. Habari ziwafikie Wafanyakazi wote wa TANROADS, Wizara ya Ujenzi na Taasisi zake zote pamoja na ndugu, jamaa na marafiki popote pale walipo.

  Marehemu anatarajiwa kuzikwa nyumbani kwake Morogoro siku ya Jumanne tarehe 11/3/2014. Marehemu ataagwa kesho Jumapili saa tano asubuhi kwenye hospitali ya Amana – Ilala Dar es Salaam. Tunatoa pole zetu za dhati kwa watoto wa marehemu, ndugu, majirani na marafiki.

  Bwana alitoa, Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. 
  AMINA

  0 0
 • 03/08/14--09:30: Article 0


 • 0 0


  0 0


  0 0

  Si mwengine ila ni yule yule Mkali wa Dance Tanzania kutoka THT kwa jina la Question ambaye ametoa nyimbo yake mpya na kuonyesha kipaji chake kingine cha kuimba na nyimbo iitwayo 'Nakupenda' 
  Vilevile atakuja na movie yake ambayo ipo kwenye mapishi na Action kali ambazo hazijawahi kutokea in Bongo Movies.
  Sponsors wa movie hio wanatafutwa 
  wasiliananae simu 0717792876.

  0 0

  Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal akiambatana na Mwenyeji wake,Shamim Mwasha wakati akikagua kazi mbalimbali za wanawake kwenye hafla ya Siku ya Wanawake,iliyofanyika jioni ya leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam..
  Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Asha Bilal na Mwenyeji wake,Shamim Mwasha wakipitia moja ya vitabu vya watoto vilivyotungwa na mmoja wa wanawake wa Tanzania.
  Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya 8020 Fashions ambao ndio waratibu wa Hafla ya Siku ya Wanawake,Shamim Mwasha akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni Rasmi kuja kutoa hotuba yake.Hafla hiyo imefanyika jioni ya leo kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee,jijini Dar es Salaam.

  Mgeni Rasmi katika Hafla ya siku ya Wanawake,Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mama Asha Bilal akihutubia mamia ya kinamama waliohudhulia hafla hiyo.


  0 0

  Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraimu Kwesigabo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam kuhusu mfumuko wa bei nchini.
  Na. Aron Msigwa – MAELEZO.

  Ofisi ya Taifa ya Takwimu imesema kuwa hali ya mfumuko wa bei nchini imeendelea kuwa katika kiwango kisichobadilika katika kipindi cha mwezi Januari na Februari mwaka huu kutokana na kupungua kwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali.

  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraimu Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa Taifa kwa mwezi Februari 2014 umeendelea kubaki katika kiwango cha asilimia 6.0 kama ilivyokuwa mwezi Januari mwaka huu.

  Amesema kuwa kasi ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma kwa mwezi Februari 2014 imebakia kuwa sawa na ile iliyokuwepo mwezi Januari huku kukiwa na ongezeko dogo la upandaji wa bei kwenye baadhi ya bidhaa na huduma mwezi kwa mwezi Februari 2014 ikilinganishwa na bei za mwezi Februari mwaka jana.

  Ameeleza kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na migahawa kwa mwezi Februari umeongezeka hadi asilimia 6.9 kutoka asilimia 6.6 za mwezi Januari mwaka huu huku bidhaa zisizo za vyakula kasi ya ongezeko la bei ikipungua hadi asilimia 6.3 mwezi Februari 2014 kutoka asilimia 6.7 za mwezi Januari mwaka jana.

  Amefafanua kuwa mwenendo wa bei za bidhaa za vyakula kama samaki, mbogamboga, ulezi na matunda zimeonyesha kuongezeka kwa kiwanga kikubwa kwa mwezi Februar ikilinganishwa na bei za bidhaa hizo kwa mwaka uliopita huku bei za bidhaa zisizo za vyakula za vitambaa vya suti za wanaume, kodi za pango la kuishi, mkaa, na nauli za bajaji zikionyesha ongezeko.

  Kwa upande wa mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi,ameeleza kuwa kumekuwa na ongezeko kwa asilimia 1.4 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 1.8 kwa Januari mwaka huu, huku fahirisi za bei za taifa zikiongezeka hadi kufikia 148.62 kati ya Februari mwaka uliopita na Februari mwaka huu.

  Amezitaja bidhaa zilizochangia ongezeko la fahirisi za bei nchini kuwa ni pamoja na dagaa,samaki wakavu, mbogamboga na viazi mviringo huku bidha zisizo za vyakula zikiwa pombe za kienyeji, vitambaavya suruali, viatu vya wazi vya plastic, mafuta ya dizeli na Petroli pamoja na huduma za unyoaji na usafi wa nywele.

  Aidha kufuatia hali hiyo ya mfumuko wa bei Bw. Kwesigabo ameeleza kuwa uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma za jamii kwa mwezi Februari umeonyesha kupungua na kufikia shilingi 67 na senti 29.

  “Kupungua kwa thamani ya Shilingi kunamaanisha kwamba, kama mtu alikuwa na uwezo wa kununua bidhaa kwa Shilingi 100 mwaka jana, basi kwa mwaka huu itampasa aongeze zaidi ili aweze kununua kitu kama kile kile, kwa mfano badala ya shilingi 100 inabidi atumie Shilingi 132”

  Kuhusu ulinganifu mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei nchini Kenya umepungua kidogo na kufikia asilimia 6.86 kwa mwezi Februari kutoka asilimia 7.21 za mwezi Januari , huku Uganda ikiwa na asilimia 6.7 kwa mwezi uliopita kutoka asilimia 6.9 za mwezi Januari.

  0 0

  Carol Mbilinyi enzi ya uhai wake

  KWA WENZANGU WANA PAZI,
   DADA YETU CARO MWAISELAGE MBILINYI ANAZIKWA KESHO TAREHE 9 MARCH 2014  SAATISA MCHANA KWENYE MAKABURI YA KINONDONI JIJINI DAR ES SALAAM. KABLA YA HAPO SHUGHULI ZA MISA ZITAFANYIKA KANISA LA KILUTHERIL  UKONGA.

   TUJITAHIDI KUMSINDIKIZA DADA 
  YETU KWENYE SAFARI YAKE YA MWISHO.

  KWA TAARIFA ZAIDI TUNAWEZA KUMPIGIA SIMU KAKA YAKE DR. JULIUS MWAISELAGE KWENYE NO. 255754764412
  ,
  MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI
  AMINA

  0 0
 • 03/08/14--19:00: ngoma azipendazo ankal
 • KOFFI OLOMIDE  

  0 0
 • 03/08/14--23:35: KIBONZO CHA NATHAN MPANGALA


 • 0 0

  Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) lilifikia makubaliano na kampuni ya Adidas kupitia msaada wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kupatiwa vifaa vya michezo.

  Kufuatia makubaliano hayo TFF tulipatiwa vifaa kadhaa vya adiads kwa ajili ya timu ya Taifa ya wakubwa (Taifa Stars). Vifaa hivyo zikiwemo jezi tulianza kuvitumia kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Namibia iliyochezwa Machi 5 mwaka huu jijini Windhoek kama inavyoonekana pichani.

  Vifaa hivyo zikiwemo jezi vitaendelea kutumiwa na Taifa Stars hadi hapo utaratibu mpya wa jezi za timu ya Taifa utakapokamilika.

  TFF tunaishukuru kampuni ya Adidas ambao ni washirika wa CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) kwa miaka mingi kwa mchango wao huu wa kuendeleza mpira wa miguu nchini.

  Boniface Wambura Mgoyo
  Media and Communications Officer
  Tanzania Football Federation (TFF)

  0 0


  0 0


  0 0

  Pichani shoto ni Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu,Jerry Silaa wakishangilia jambo kwa pamoja na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Ndugu Godfrey William Mgimwa,katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi Katenge katika kijiji cha Mgama,kata ya Mgama,Iringa Vijijini.
  Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu,Jerry Silaa pichani kulia akizungumza mbele ya wanachama wa CCM na wananchi kwa ujumla waliofika kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jana kwenye uwanja wa shule ya msingi Katenge katika kijiji cha Mgama,kata ya Mgama,Iringa Vijijini.Jerry Silaha amewataka wananchi na wakazi wa kijiji hicho kumpigia kura ya ndio ifikapo machi 16,Ndugu Godfrey Mgimwa ili aweze kuliongoza jimbo la Kalenga na kuyaendeleza mambo yote yaliyoachwa na Mbunge aliyepita.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza mbele ya Wanachama wa chama hicho na Wanachi kwa ujumla kwenye mkutano wa kampeni wa uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama,Iringa Vijijni akimpigia debe mgombea ubunge wa jimbo hilo,Ndugu Godfrey Mgimwa.
  Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu,Jerry Silaa pichani kulia akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya chama cha CCM,Ndugu Godfrey William Mgimwa,katika mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika kwenye kijiji cha Ibumila kata ya Mgama,halmashauri ya Iringa vijijini mkoani Iringa.Jerry Silaa amewaomba wana Ibumila na wana Kalenga kwa ujumla wake kumchagua Godfrey Mgimwa ili kukamilisha mipango mbalimbali aliyoiacha na aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo Marehemu Dk.William Mgimwa.
  Kada wa CCM,Ndugu Fredrick Mwakalebela akimpigia debe mgombea Ubunge wa jimbo la Kalenga,kupitia chama hicho,Ndugu Godfrey Mgimwa katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama,wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini humo.
  Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilala na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,Ndugu,Jerry Silaa akipeana mkono na Mwenyekiti wa CCM mkoa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu mara baada ya kumaliza kumuombea kura mhombea Ubunge wa jimbo la Kalenga kupitia CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa.
  Mwenyekiti wa CCM mkoa Iringa,Bi.Jesca Msavatavangu akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa uchaguzi mdogo Jimbo la Kalenga, katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama,Iringa Vijijni akimpigia debe mgombea ubunge wa jimbo hilo,Ndugu Godfrey Mgimwa.
  Mgombea Ubunge Jimbo la Kalenga,kupitia CCM,Ndugu Godfrey Mgimwa akiwa emakalishwa kwenye kigoda mara baada ya kuvalishwa mgorole wa kimila kwama ishara ya heshima na kumtakia ushindi wa kishindo,mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Mgama kata ya Mgama wakati wa mkutano wa kampeni uliofanyika kijijini hapo jana.PICHA NA MICHUZIJR-MICHUZI MEDIA-KALENGA,IRINGA.

  0 0


older | 1 | .... | 380 | 381 | (Page 382) | 383 | 384 | .... | 3270 | newer